Translate

Jumanne, 22 Septemba 2020

Faida 39 zitakazokushangaza za mafuta ya Nazi kiafya

FAIDA 39 ZITAKAZOKUSHANGAZA ZA MAFUTA YA NAZI KIAFYA

Zaidi ya tafiti 1500 zimethibitisha kuwa mafuta ya nazi ndiyo mafuta bora zaidi chini ya jua.

Hili halishangazi sababu karibu kila mtu anajua mafuta ya nazi ni dhahabu kwa afya ya mwili na ngozi kwa ujumla.

Bidhaa nyingi za vipodozi ukizichunguza utagundua huongezwa pia mafuta ya nazi ndani yake.

Ili upate faida hasa za mafuta haya ni lazima yawe ni ya asili na hayajachanganywa na kingine au kemikali yoyote, hayajapita kwenye moto wakati wa kuyatengeneza na yakiwa hivyo hujulikana kama mafuta bikra ya nazi (Virgin Coconut Oil).

Nyingi ya faida za mafuta ya nazi ni matokeo ya kuwa na asidi mafuta mhimu sana ijulikanayo kama ‘lauric’.

Lauric ni asidi mafuta mhimu ambayo ni mdhibiti mzuri dhidi ya bakteria, fangasi, sumu, vijidudu nyemelezi na maambukizi.

Ili kupata faida hizi nyingi za mafuta ya nazi unaweza kuyanywa au kupakaa juu ya ngozi.

Mafuta ya nazi ni moja ya chanzo cha viinilishe mhimu sana mhimu na hivyo kufanya moja ya dawa mbadala mhimu kuwa nayo.

Mafuta ya nazi yanaweza kutumika kuongeza kinga ya mwili, kuzuia matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji, kuponya matatizo katika figo, kutibu shinikizo la chini la damu, kupunguza hatari ya kisukari nk

Matumizi ya mara kwa mara ya mafuta ya nazi yanaweza kuongeza umeng’enywaji wa asidi amino, madini, vitamini mhimu na hivyo matumizi yake yanaweza kuboresha muonekano wako kwa ujumla.

Ndiyo maana siyo jambo la kushangaza kuona bidhaa nyingi kama vipodozi, sabuni na zile dawa za nywele ndani yake zikiongezwa mafuta ya nazi pia.

Kuna faida nyingi za kushangaza katika mafuta ya nazi kwa ajili ya afya na urembo ambazo ninapenda kukuonyesha kupitia makala hii.

Faida 39 zitakazokushangaza za mafuta ya Nazi kiafya

1. Huzuia na kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu

Wakati mafuta ya nazi yakiwa yamemeng’enywa na mwili huhamasisha uundwaji wa nguvu mpya za ubongo zijulikanazo kama ‘ketones’.

Ketones zina uwezo wa kusambaza nguvu katika ubongo hata kama insulin itakuwa chini ya kiwango kama matokeo ya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Insulin kazi yake kubwa ni kuishughulikia sukari (glucose) na hivyo kuzipa nguvu seli za ubongo.

Kwa bahati mbaya ubongo wa mtu mwenye ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu hauwezi kujitengenezea insulin yake kwa usahihi na vya kutosha.

Watu wanaosumbuliwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu wanatakiwa waongeze matumizi ya mafuta ya nazi kwenye vyakula vyao kila siku.

Kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu ni moja ya kazi za mafuta ya nazi ambayo ninapenda kukufahamisha kupitia makala hii.

2. Huzuia uwezekano wa kupata kansa

Mafuta ya nazi yanao uwezo wa kupigana na seli za kansa.

Tafiti za karibuni zinasema kitu chochote chenye uwezo wa kuuongezea nguvu ubongo husaidia pia kuzuia kusambaa kwa seli za kansa katika mwili.

Zaidi ni kuwa mafuta haya yana uwezo wa kumdhibiti bakteria ajulikanaye kama “helicobacter pylori” ambaye husababisha vidonda vya tumbo.

3. Yanaongeza kinga ya mwili mara dufu

Kinga imara ya mwili ina umhimu mkubwa katika kupigana na aina mbalimbali za magonjwa.

Kuongeza kinga ya mwili ni moja ya faida za mafuta ya nazi sababu ni mafuta ambayo hupigana dhidi ya bakteria, fangasi na virusi mbalimbali.

Unaweza kupakaa moja kwa moja juu ya ngozi au kuyanywa pia kuchanganya kwenye vyakula mbalimbali kwa ajili ya kuongeza kinga yako ya mwili.

4. Yanaongeza nguvu za ubongo

Utafiti mmoja uliofanywa mwaka 2004 unaonyesha mafuta ya nazi yana uwezo wa kuongeza nguvu za ubongo hata kwa watu wenye umri mkubwa na wazee.

Mafuta ya nazi yana asidi mafuta nzuri zenye uwezo wa kusaidia na kuzilinda seli za ubongo na kuziwezesha kufanya kazi kwa ufasaha zaidi.

5. Yanaongeza nguvu na uvumilivu

Mafuta ya nazi yana uwezo wa kukupa nguvu na kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, moja ya kazi mhimu zaidi ya mafuta haya.

Mafuta ya nazi yanajulikana vizuri kwa uwezo wake wa kukuongezea uvumilivu.

Hii ndiyo sababu wakimbia mbio wengi hupendelea kutumia mafuta ya nazi.

Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya nazi na kijiko kidogo kingine cha asali mbichi na unywe pamoja mchanganyiko huu kila siku kutwa mara 1 kabla ya kwenda kwenye mazoezi au kwenye kazi yoyote ngumu.

6. Dawa nzuri kwa matatizo ya mifupa

Ugonjwa wa mifupa husababishwa na vijidudu nyemelezi na mfadhaiko wa mwili wa muda mrefu.

Mafuta ya nazi yana viondoa sumu vyenye nguvu zaidi ambavyo vinaweza kuulinda mwili wako dhidi ya vijidudu nyemelezi.

Zaidi, matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kurahisisha umeng’enywaji wa madini ya kalsiamu tumboni mwako.

Upungufu wa madini ya kalsiamu mwilini husababisha mifupa kuwa hafifu jambo linaloishia kuleta ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).

Kuzuia ugonjwa wa mifupa unahitaji kuongeza mafuta ya nazi kuwa sehemu ya chakula chako.

Hii ndiyo faida ya mafuta ya nazi ambayo niliona si vema kama sitakuambia.

7. Husaidia kushusha uzito

Watu wengi wanaamini kwamba ili kupungua uzito basi hutakiwi kabisa kutumia mafuta.

Hata hivyo hili si jambo la kweli.

Kupunguza uzito ni moja ya kazi nyingine nzuri sana ya mafuta ya nazi.

Matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kusaidia mafuta kuchomwa zaidi mwilini huku kiasi chako cha njaa kikishuka.

Watu wenye vitambi au unene uliozidi wanatakiwa kuongeza mafuta ya nazi kwenye milo yao na miili yao itakaa sawa yenyewe.

8. Huondoa mfadhaiko (Stress)

Mifadhaiko ni jambo lisiloweza kuepukika katika maisha yetu.

Kazi ya mfadhaiko au stress ni kukufanya uwe imara zaidi, mpole na unayejiamini zaidi.

Unapofadhaishwa mwili wako huwa unajiongeza na kuwa na shauku ya kufanikiwa zaidi.

Hata hivyo mfadhaiko unapodumu kwa muda mrefu unaweza kuleta madhara makubwa kwa mhusika kihisia na hata kimwili pia.

Mfadhaiko wa muda mrefu unaweza kupelekea huzuni mbaya na hatimaye kuathiri muonekano wako.

Watu wenye mifadhaiko (stress) ya muda mrefu huonekana ni wenye umri mkubwa hata kama umri wao bado ni mdogo.

Tafiti za karibuni zimeonyesha uhusiano wa karibu uliopo kati ya matumizi ya mafuta ya nazi na kupungua kwa mfadhaiko wa akili.

Tunaweza kusema kuwa, kitendo hiki cha kuondoa mfadhaiko au stress ni moja ya kazi ya kustajaabisha kabisa ya mafuta ya nazi.

Asidi mafuta zilizomo ndani ya mafuta haya ndizo zinazohusika na kazi hii mhimu.

9. Huimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Ili mwili wako ubaki ni wenye afya na kuzuia usipatwe na magonjwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula na wakati huo huo mfumo imara wa uchukuwaji wa viinilishe, madini na vitamini mbalimbali kutoka kwenye chakula unachokula.

Kwa bahati nzuri, kuuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula ni kazi nyingine ambayo mafuta ya nazi yanaweza kukusaidia bila madhara mengine mabaya.

Matumizi ya mafuta ya nazi yatakuwezesha kuongeza uchukuwaji wa viinilishe mhimu kutoka kwenye chakula sababu mafuta haya yana madini ambayo huweza kuyeyuka kwenye mafuta kama kalsiamu na magnesiamu.

Zaidi, mafuta haya yanaweza kusaidia umeng’enywaji wa mafuta mengine magumu ndani ya mwili kama matokeo ya kuimarishwa kwa vimeng’enya vinavyohusiana na mmeng’enyo wa chakula.

10. Jitibu matatizo katika Kongosho na Kibofu cha mkojo

Kama unapata maumivu au matatizo yoyote katika kongosho au kibofu cha mkojo unahitaji kuongeza matumizi ya mafuta ya nazi.

Ukiendelea kutumia mafuta ya nazi kila mara utaweza kujitibu pia tatizo la mawe katika kibofu cha mkojo na kuondoa hali ya kutojisikia vizuri kutokana na magonjwa katika kongosho au kibofu cha mkojo.

11. Yanatengeneza Misuli ya mwili

Faida kubwa ya mafuta ya nazi haiishii katika uwezo wake wa kuchoma mafuta, bali yana kazi nyingine ya kushangaza zaidi nayo ni kutengeneza misuli ya mwili.

Kwenye bidhaa nyingi zinazouzwa zaidi duniani za kutengeneza virutubishi vya kutengeneza misuli ya mwili mafuta ya nazi lazima yawemo.

Kama unataka kuongeza misuli mingi mwilini kirahisi zaidi changanya tui zito la nazi kikombe kimoja (robo lita), ongeza vanilla vijiko vikubwa vitatu, ongeza maji maji ya chungwa vijiko vikuwa viwili na ndizi zilizoiva mbili.

Saga na mashine ya kusagia matunda jikoni (blender) mchanganyiko huu kwa pamoja na ule wote kutwa mara 1 kila siku.

12. Zuia jino kuoza na magonjwa ya kwenye fizi

Kuzuia kuoza kwa jino na magonjwa ya fizi ni moja ya kazi nyingine nzuri ya kushangaza ya mafuta ya nazi ambayo nimependa kukufahamisha kupitia makala hii.

Mafuta ya nazi ni dawa inayoweza kudhibiti bakteria wabaya na hivyo kuzuia kuoza kwa jino na maumivu mengine katika fizi.

Ili kuzuia haya unahitaji tu kutumia mafuta yako ya nazi kama dawa yako ya mswaki kila siku.

Unaweza pia kuongeza kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto ili kutengeneza dawa ya kusafisha mdomo (mouthwash).

13. Ongeza ufanisi wa Ini na Figo

Kwa mjibu wa madaktari wengi, kuna uhusiano wa karibu kati ya madhara ya figo na kushindwa kufanya kazi kwa ogani hii mhimu.

Kama tatizo la kufeli kwa figo halitapatiwa ufumbuzi linaweza kupelekea kifo. Figo na Ini ni ogani mhimu zaidi katika mwili ambazo zinatakiwa kupewa uangalizi wa karibu kila mara zisipatwe na madhara yoyote.

Kwa bahati nzuri, mafuta ya nazi yanayo uwezo wa kulinda figo na Ini visipatwe na madhara yoyote mabaya moja ya kazi ya mafuta ya nazi mwilini ulikuwa huijuwi bado.

Wanasayansi wameviona viinilishe katika mafuta ya nazi ambavyo ni mhimu sana kwa afya ya Ini na figo katika mwili wa binadamu.

14. Yanaondoa mawe katika figo na kibofu cha mkojo

Nazi pamoja na mafuta ya nazi huwa na asidi mafuta mhimu sana ambazo huhamasisha uundwaji wa ‘Monooctanoin’ ambayo hufanya kazi ya kuyeyusha mawe katika kibofu cha mkojo na figo.

Wagonjwa ambao hawawezi kumudu gharama za upasuwaji kuondoa mawe katika figo na katika kibofu cha mkojo wanaweza kujitibu hilo kwa kutumia mafuta ya nazi kama dawa mbadala.

Unachohitaji kufanya ni kunywa tu kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi kila siku kutwa mara 1 mpaka utakapokuwa umepona.

15. Yanatibu baridi yabisi

Mafuta ya nazi hudhibiti uvimbe na kuondoa sumu mwilini, kazi hizi mbili zinayafanya kuwa dawa bora ya kutibu ugonjwa wa baridi yabisi.

Unahitaji kijiko kidogo kimoja cha mafuta haya kila siku ili kujitibu na ugonjwa wa baridi yabisi.

16. Husaidia kazi za tezi koromeo (Thyroid gland)

Faida za mafuta ya nazi zinahusu pia kurekebisha kazi za ogani za mwili kama kuweka sawa mapigo ya moyo, kupumua na kuzalisha homoni mhimu.

Tezi koromeo huzalisha homoni mbili ambazo huwa na msaada mkubwa katika kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Ufanisi mzuri wa tezi hii huweza kuhakikisha mapigo ya moyo ni sawa, uzito sawa wa mwili, na usawa ulio sawa wa homoni.

17. Yanatibu kisukari aina ya kwanza

Kutibu kisukari aina ya kwanza ni moja ya kazi nyingine nzuri za mafuta ya nazi sababu mafuta haya yanao uwezo wa kuiweka sawa damu sukari (blood glucose) ndani ya mwili.

Mafuta ya nazi yamethibitika siyo katika kushusha kisukari aina ya kwanza tu bali pia katika kuweka sawa aina mbalimbali za homoni mwilini.

Kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi kwa siku kinatosha kwa kazi hii.

18. Hutibu maambukizi ya fangasi

Mafuta ya nazi ni moja ya dawa nyingine nzuri kwa ajili ya kutibu maambukizi ya fangasi kwa sababu moja kuu kwamba ni mafuta yanayoweza kuua bakteria na virusi mbalimbali.

Hii ni kazi ya mafuta haya ambayo isingekuwa vema kama nisingekujulisha kupitia makala hii.

Hii ni matokeo ya kuwa na ‘lauric acid’ na ‘capric acid’.

Tafiti mbalimbali zimeonyesha uhusiano uliopo baina ya matumizi ya mafuta yenye afya na kushuka kwa maambukizi ya fangasi.

Kwa fangasi yoyote juu ya ngozi unaweza kutumia mafuta haya kama mafuta yako ya kupakaa kila siku pia unaweza kunywa kijiko kidogo kimoja kila siku kuongeza kinga zaidi ya mwili.

19. Yanaweka sawa homoni zako.

Maradhi mengi mwilini huja kama sababu ya homoni zako kutokuwa sawa.

Ni bahati kufahamu kuwa mafuta ya nazi ni moja ya dawa za asili nzuri katika kuziweka sawa homoni zako.

Hii ni kwa sababu mafuta ya nazi yana mafuta mazuri yajulikanayo kama ‘lauric acid’.

Mafuta ya nazi huiweka sawa homoni mhimu sana kwa upande wa uzazi kwa mwanamke homoni ijulikanayo kama ‘estrogen’.

Chanzo kingine kizuri cha homoni hii ni pamoja na tunda la parachichi.

20. Yatakufanya usizeeke mapema

Kuzeeka mapema ni jambo lisilopendwa karibu na watu wote.

Kuzeeka mapema hakuathiri muonekano wako tu bali huathiri pia afya yako.

Tunapozungumzia juu ya faida za kushangaza zilizomo katika mafuta ya nazi lazima ujuwe kuwa mojawapo ni hili la kukufanya usizeeke mapema.

Viuajivijasumu vilivyomo kwenye mafuta ya nazi hufanya kazi mhimu katika kupunguza vijidudu nyemelezi na matatizo mengine katika ini.

21. Hupunguza maradhi ya ubongo

Kuzuia magonjwa ya ubongo ni faida nyingine ya mafuta ya nazi ambayo unapaswa kuijua.Asidi mafuta zilizomo kwenye mafuta ya nazi hubadilishwa na kuwa ‘ketones’ ambazo huzuia kutokea tatizo la kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Kupoteza kumbukumbu ni matokeo ya kuongezeka kwa kemikali ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘amyloid beta peptides’.

Kwenye mafuta ya nazi kuna kitu mhimu sana kijulikanacho kama ‘Phenolic compounds’ ambacho hudhibiti ile kemikali ya ‘amyloid beta peptides’ na hivyo kukuondolea tatizo la kupoteza kumbukumbu kirahisi zaidi.

22. Hupunguza njaa

Mafuta ya nazi yanaweza kukupunguzia hitaji lako la kutaka kula chakula kila mara kwa kuwa hufanya kazi ya kupunguza njaa ndani ya mwili.

Kutumia mafuta ya nazi kutakufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu na kama matokeo yake kutakusaidia kupunguza kiasi cha nishati unaingiza ndani ya mwili wako kila siku.

Kuna uhusiano wa karibu kati ya mafuta safi kwa afya na kuwa na njaa ya wastani.

23. Yanapunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa moyo

Tafiti mbalimbali Zimeonyesha kwamba Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto (high-density lipoproteins -HDL) unao uwezo wa kulinda moyo wako.

Hivyo mafuta ya nazi yanaweza kupunguza hatari kwako ya kupatwa na ugonjwa wa moyo moja ya kazi nyingine mhimu sana ya mafuta haya.

Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla.

Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.

24. Yanauongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Tafiti zimeendelea kuonyesha uhusiano uliopo kati ya matumizi ya mafuta ya nazi na kuimarika kwa mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula.

Mafuta ya nazi yanapokuwa yamemeng’enywa ndani ya mwili wako hutumika kama nguvu yako moja kwa moja.

Watu wanaotumia mara kwa mara mafuta ya nazi kwenye vyakula vyao kila siku wanakuwa na mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula jambo ambalo ni mhimu katika kuchoma mafuta na nishati ndani ya mwili.

25. Yanapigana kuondoa vijidudu nyemelezi

Maisha yetu ya kila siku yanapelekea kuundwa kwa vijidudu nyemelezi ndani ya mwili bila sisi kupenda.

Kuzidi kujitokeza kwa vijidudu nyemelezi ndani ya mwili ndiyo kunakopelekea mwili kuwa ni wa kuchokachoka kila mara na ni chanzo cha magonjwa mengine mengi.

Kuendelea kutumia mafuta ya nazi kutasaidia kuimarisha kinga yako ya mwili kwani mafuta ya nazi yana kiasi cha kutosha cha viuajivijasumu (antioxidants) dhidi ya vijidudu mbalimbali nyemelezi.

26. Yanaotesha nywele

Faida za mafuta ya nazi haziishii ndani ya mwili tu, bali yana faida nyingine nyingi yanapotumika nje ya mwili.

Tafiti zimeonyesha kwamba matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kuwa msaada mkubwa katika kuotesha na kukuza nywele.

Tafiti zimeonyesha kwamba matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kuzuia aina yoyote ya upotevu wa nywele.

Kupungua kwa protini kunaweza kuwa ni sababu nyingine ya kupotea kwa nywele zako kama hakutadhibitiwa kwa haraka.

Unachohitaji ni kuyafanya kuwa mafuta yako ya nywele na hutachelewa kuwa na nywele nzuri zinazopendeza.

Mafuta ya nazi ni mlinzi mzuri wa nywele zako.

27. Yanaondoa mba kichwani

Unasumbuliwa na mba kichwani?

Pakaa mafuta ya nazi na mba utapotea bila kupenda wenyewe.

Mafuta ya nazi ni moja ya dawa mbadala zenye nguvu kutibu tatizo la mba.

Dawa nyingi na vipodozi vya kuondoa mba kichwani huongezwa mafuta ya nazi ndani yake.

Tuliona pia pale juu kuwa hutumika kuotesha nywele.

Unahohitaji ni kufanya ni kuamua mafuta ya nazi kuwa ndiyo mafuta yako ya kupakaa kichwani na mba utapotea wenyewe kadri unavyoendelea kuyatumia.

28. Mafuta bora zaidi kwa ngozi yako

Mafuta pekee mazuri kwa ngozi yako ni mafuta ya nazi.

Hii ndiyo sababu dawa nyingi na vipodozi vya ngozi ndani yake huwa na mafuta ya nazi pia.

Kama una ngozi kavu au yenye mikunjokunjo basi pakaa mafuta ya nazi na ngozi yako itakuwa nzuri, nyororo, yenye rangi yake ya asili na ya kupendeza sana.

Waulize watu wa ukanda wa pwani hili wanalifahamu vizuri sana.

Kama utaamua kutumia mafuta ya nazi kama mafuta yako ya kupakaa magonjwa mengi ya ngozi utayasikia tu kwa jirani.

29. Yanalinda ngozi yako dhidi ya miale ya jua

Viinilishe vya asili kwenye mafuta ya nazi vinawezesha ngozi yako isiathirike na miale ya jua moja kwa moja.

Moja ya kazi nyingine ya kushangaza ya mafuta haya.Mafuta ya nazi ni miwani ya jua ya asili.

Kwa mjibu wa utafiti, mafuta ya nazi yanaweza kuzuia mpaka asilimia 20 ya miale ya jua kushindwa kukufikia moja kwa moja kwenye ngozi yako kama utayafanya kuwa ndiyo mafuta yako ya kupakaa.

Tafiti nyingi zimeonyesha miale ya jua kuwa ina athari nyingi ikitua moja kwa moja juu ya ngozi yako ikiwemo kufanya ngozi kuwa na makunyanzi, magonjwa ya ngozi na kansa ya ngozi.

30. Dawa nzuri ya kusugulia mwili (Scrub)

Wengi mnapenda kufanya scrub hasa usoni (facial). Kwa lugha nyepesi ni kitendo cha kusugua ngozi kwa dawa maalumu ili kuondoa uchafu wote na kuifanya ionekane nyororo na yenye kupendeza.

Sasa huhitaji dawa zenye kemikali kwa ajili hiyo wakati mafuta ya nazi yanaweza kukusaidia hilo bila madhara yoyote mabaya.

Fanya hivi changanya nusu kikombe (mln125) cha mafuta ya nazi na sukari kikombe kimoja na ufanye dawa ya kusugua na kusafisha uso wako.

Unaweza pia kutumia nazi yenyewe moja kwa moja kabla hujapata mafuta yake.

Tumezoea kutumia nazi jikoni kwenye mapishi, lakini nazi pia inaweza kutumika kama scrub ya asili ya ngozi yako.

Fuata hatua hizi zifuatazo ili kufanya ngozi ya uso wako iwe laini, nyororo na kufanya uso wako uwe laini, nyororo na wenye mvuto.

Scrub hii unaweza pia kuitumia kwa mwili mzima, lakini hapa nitaelezea namna ya kutumia kwa uso wako.

* Andaa nazi yako kwa kuikuna vizuri na ili upate matokeo mazuri jitahidi kuikuna taratibu ili itoke laini.

*Safisha uso wako kwa maji safi na sabuni ya kawaida isiwe sabuni ya dawa (medicated)

* Kausha uso wako kwa taulo safi.

* Baada ya uso wako kuwa mkavu, ichukue ile nazi yako uliyoikuna tayari, taratibu anza kusugua usoni kwa dakika kama 3 mpaka 5.

*Ukishamaliza hapo, utakaa hivyo bila kuuosha uso wako kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.

* Baada ya muda huo, utaosha uso wako kwa sabuni ya kawaida.

* Kausha uso wako kwa taulo safi, kisha paka losheni yako unayotumia siku zote.

Ili kupata matokeo mazuri fanya hivi kwa muda wa siku 5 mfululizo bila kuacha, yaani mara moja kwa siku.

Amini nakuambia utapata matokeo mazuri mpaka mwenyewe utaifurahia ngozi yako na hata vocha utaninunulia kunipongeza.

31. Yanatibu vidonda vya homa mdomoni

Mafuta ya nazi ni moja ya dawa nzuri kabisa kutibu vidonda vya homa ambavyo hujitokeza mdomoni.

Unahitaji kupakaa tu sehemu yenye tatizo moja kwa moja huku ukinywa kijiko kidogo kimoja kila siku na hutakawia kupona hivyo vidonda.

Hili linawezekana kutokana na sifa ile ile ya mafuta haya katika kupigana dhidi ya bakteria na virusi na vijidudu nyemelezi.

32. Yanaimarisha kucha

Ukitumia mafuta ya nazi utakuwa na kucha nzuri na zenye kupendeza.

Wakati huo huo kunyunyiza mafuta ya nazi kwenye kucha zako kunaua wadudu wowote wanaoweza kuharibu kucha zako.

33. Hufukuza wadudu mbali

Yanaweza kutumika kama dawa ya asili ya kufukuza wadudu (insect repellent) wakiwemo mbu.

Unachohitaji ni kuchanganya pamoja na kiasi kidogo cha mafuta ya karafuu au ya mnanaa (mint) na ujipake juu ya ngozi yako na hakuna mdudu yoyote akiwemo mbu atakayekusogelea.

Pakaa mchanganyiko huu mara kadhaa katika siku kwa matokeo mazuri zaidi.

34. Mafuta mazuri kwa ajili ya Lips

Wasichana na wamama wengi ni watumiaji wa bidhaa nyingi za lipstiki zenye kemikali kwa ajili tu ya kulainisha midomo yao ya nje (lips).

Kile wengi hawajuwi ni kuwa bidhaa hizi si salama sana kwa afya zao.

Bahati nzuri kwa wewe unayesoma makala hii mafuta ya nazi yanaweza kutumika kama lipstiki yako ya asili isiyo na madhara mabaya hapo baadaye.

Kwahiyo kama una tatizo la midomo kukauka basi uwe unapakaa mafuta ya asili ya nazi kila mara..

35. Ni mafuta mubadala ya kupikia yenye afya

Tofauti na mafuta ya alizeti au hata mafuta ya zeituni, kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi ya afya.

Mafuta haya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto.

Hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!

36. Ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama

Siyo kupika tu na mafuta ya nazi ndiko huleta afya, bali pia ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama kama mubadala kwa siagi au vitu vingine mnavyopaka juu ya mikate mnapokula.

Hii nikwa sababu mafuta ya nazi hubaki katika hali yake hata katika joto la kawaida la chumba tofauti na mafuta mengine.

37. Mafuta mazuri kwa ajili ya masaji

Mafuta ya nazi ni mafuta mazuri kwa ajili ya masaji na kukupatia hali ya utulivu unaouhitaji kupitia masaji.

Unaweza kuchanganya na mafuta mengine kama ya karafuu na kupata mchanganyiko wa mafuta maalumu kwa ajili ya masaji na ukiyatumia utaweza ku-relax kwa uzuri kabisa huku yakituliza mishipa, misuli, ubongo na mwili wako kwa ujumla.

38. Hutumika kulainisha uke mkavu

Mafuta ya nazi yana matumizi mengi sana mwilini zaidi ya 100, kuna wanawake wana tatizo la kuwa na uke mkavu muda wote hata wakisisimuliwa vipi bado huwa wakavu.

Kuondokana na tatizo hilo pakaa mafuta ya nazi katika uke wako na utaona faida yake nyingine ikiwemo ya kutibu, fangasi na bakteria tena bila madhara yeyote mabaya.

39. Husaidia katika ugonjwa wa aleji

Tukisema tuelezee faida zote za mafuta ya nazi kwa hakika hatutaweza.

Moja ya faida zake zinazoshangaza wengi ni uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji.

Kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.

UNAHITAJI MAFUTA YA NAZI?

Mafuta ya nazi nauza 10000 kwa robo lita, ni mafuta ya asili kwa 100% nayatengeneza mimi mwenyewe nyumbani na hayapiti kwenye moto hata dakika 1.

Kama unahitaji niachie ujumbe WhatsApp +255714800175, Kama upo Dar naweza pia kukuletea ulipo unanilipa nauli ya daladala na natuma pia mikoani.

Hakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100 na kama unataka ya kunywa hakikisha hayajapita kwenye moto wanayaita bikra (virgin coconut oil), ikiwa utanunua dukani kuna uwezekano mkubwa yakawa yamechanganywa na kemikali zingine au haidrogeni kitu kinachoyapunguzia thamani yake ile ya asili.

Kama unapikia kwenye chakula najuwa wengi mnapenda wali wa nazi au hata tui lake likiwekwa kwenye samaki au hata mboga yoyote lazima utajing’ata ulimi, basi nakushauri usichanganye na mafuta mengine kwenye hicho chakula.

Tafadhali SHARE kwa ajili ya uwapendao

Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 6

Let's block ads! (Why?)

Makosa makubwa kabisa 6 wafanyayo wanawake kitandani

Makosa makubwa kabisa 6 wafanyayo wanawake kitandani  

Nimewahi kuandika huko siku za nyuma makosa makubwa manne wafanyayo wanaume kitandani, ni makala ilipendwa sana na wote na ukienda kwenye blog yangu unaweza kuiona na kuisoma wakati wowote.

Baadhi ya watu walinitafuta na kunitaka niandike pia na makosa wafanyayo wanawake kitandani ili kupata balansi.

Na leo nimeona niwatolee uvivu na kuwaletea hii kwa ajili ya wanawake.

Naitwa Tabibu Fadhili Paulo, ikiwa wewe ni mwanamke na unakosa au unaishiwa kabisa hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa tuwasiliane WhatsApp +255714800175 ninayo dawa nzuri ya asili inayoweza kuamsha mudi yako na ukarudi kama zamani tena.

Inajulikana wazi na watu wote kuwa ni rahisi sana kumfikisha mwanaume kileleni kuliko kumfikisha mwanamke.

Kumwamsha mwanaume na kumfikisha kileleni ni rahisi sana kama kumsukuma mlevi.

Bali ni shida sana kumfikisha mwanamke kileleni hasa kama mwanamke anakuwa na makosa haya 6 awapo kitandani ninayoeleza kwenye hii makala.

Mapenzi ni Sanaa na hakuna mtu mmoja anaweza kukuambia anafahamu yote au anafahamu kila kitu kuhusu mapenzi au tendo la ndoa.

Soma hii pia > Aina 4 za wanawake ambao hawawezi kuolewa

Makosa makubwa kabisa 6 wafanyayo wanawake kitandani

1. Kudhani mme ni mganga wa kienyeji

Kila mwanamke ni tofauti hasa linapokuja suala la nini anahitaji ili aweze kufika kileleleni.

Hata kama mwanaume ni mtu mzima na pengine ana uzoefu kuhusu tendo la ndoa bado hawezi kufahamu kwa kuhisi tu ni nini hasa huwa kinakuamsha hata unafika kileleni pengine hata kufika kileleni mapema kirahisi zaidi ISIPOKUWA UMEMWAMBIA.

Ni jambo la mhimu kuwasiliana unapokuwa kitandani na mwenza wako. Mwambie mimi nikishikwa sehemu fulani au nikiwekwa hivi najisikia vizuri zaidi, mwambie ni mme wako na rafiki yako wa karibu kuliko mtu mwingine yeyote.

Wapo baadhi ya wanawake anaweza kuchepuka kwa sababu hii ndogo.

Anajuwa ni kwa jinsi gani na namna gani anahitaji tendo la ndoa ila hawezi kumwambia mmewe moja kwa moja bali atachepuka akalale na fulani ambaye anajuwa hivyo anavyopenda yeye huku akimwacha mme hajuwi anakosea wapi.

Wanaume siyo waganga wa kienyeji kwamba kwa kuhisi tu anaweza kufahamu wewe unapenda vipi na ni wewe ndiyo unawajibika kumwelekeza pole pole na kwa lugha ya upole na staha.

Kumbuka kumweleza kwa upole na kwa lugha ya staha kwani tofauti na hapo unaweza tena kuvunja ndoa bila kujuwa.

Kwa mfano umeolewa na mwanaume na kila ukilala naye dakika 3 au 4 tayari amefika kileleni na hawezi kurudia tena, usiamke tu kwa kejeli na pengine kama mtu usiyejitambua na kumwambia ‘wewe huwezi kitu yaani unazingua tu mimi ningependa uende dakika 20 bila kupumzika’!

Hapo unaweza kulipata ulilolitafuta – talaka ya haraka na unaweza kuonekana kumbe wewe ni kahaba mzoefu.

Ipo namna ya kudai haki yako bila kuonekana msumbufu na usiye na akili.

Mwambie mme wangu ahsante sana kwa huduma nimefurahia sana umetumia dakika 4 natumaini kesho utafikisha dakika 8 ili nione ikiwa nitafurahi zaidi ya leo. Kwa lugha ya upole na tabasamu.

Na pengine utaanza kumtafutia na kumpikia vyakula vizuri vinavyoongeza nguvu na kumhimiza kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara na kumuombea kwa Mungu.

Kwahiyo kama tayari unajijuwa ni staili ipi ukifanya unafurahia zaidi au inakufanya usisimke zaidi au ufike kileleni kirahisi zaidi usisite kumwambia mmeo lakini usisahau kutumia lugha nzuri ya upole na yenye staha yenye mwelekeo wa kujenga zaidi na siyo kubomowa.

Tofauti na wanawake wengi mnavyofikiri kuhusu wanaume linapokuja suala la tendo la ndoa ukweli ni kuwa wapo wanaume wengi sana wasiojuwa tendo la ndoa linafanyikaje na wengine wapo mpaka wanaoa hawajawahi kushiriki tendo la ndoa na mtu mwingine yoyote.

2. Kutokuanzisha kamwe hitaji la tendo la ndoa

Wanawake wengi na hata baadhi ya wanaume huwa wanadhani kwamba ni mwanaume pekee ndiye anawajibika kuanzisha kutaka hitaji la tendo la ndoa.

Yaani ipo hivi; kila mara mtakaposhiriki tendo la ndoa anayekuwa alianza kusema twende kitandani au nasikia hitaji la tendo la ndoa kwenye ndoa nyingi huwa ni mwanaume!

Hilo ni kosa kubwa na wanaume wengi hawapendi hii tabia ila wengi wao hawana ujasiri wa kukuambia.

Hakuna kitu mwanaume anapenda kama kuambiwa mme wangu twende kitandani au mme wangu leo najisikia hamu ya kutaka kushiriki na wewe.

Kila mwanaume anapenda kuambiwa hivi.

Kama wewe ni mwanamke na unajitambuwa usiwe mjinga.

Siku moja moja mara moja moja kuwa wa kwanza kuhitaji jambo hilo.

Wapo wanawake yaani anajiona wazi ana ny*ge na anahitaji kushiriki lakini anakaa tu kimya na pengine akikutana na boda boda huko nje akamtaka anaweza kumpa kisa tu anaogopa kumwambia mmewe anahitaji tendo la ndoa.

Wapo wanaume wapo bize sana na kazi kiasi kwamba anaweza kumaliza wiki mbili hajakumbuka majukumu yake kitandani hivyo kumkumbusha au kumtaka siyo jambo baya na wanaume wengi wangependa kuwa na wanawake wa namna hiyo.

Mwanaume unapomkumbusha wakati mwingine kwamba unahitaji mkwaju ni ishara inayomjia kichwani kwake kwamba kumbe na wewe ni binadamu na kwamba kumbe huwa anakufikisha na kumbe ni kweli unamhitaji yeye kama yeye na siyo nyumba yake au gari lake au mali zake tu.

Wanaume wengi wakiambiwa hivyo na wake zao hujisikia vizuri sana na unaweza kumuona ghafla ana nguvu nyingi kuliko hata siku zingine alipoanzisha yeye kutaka mechi.

Hii ndiyo sababu makahaba wengi au nyumba ndogo nyingi wakikamata mme wako inakuwa ngumu kumrudisha tena kwako sababu wanaume ujinga wao wote upo hapo kitandani na kama hujuwi kukitumia kitanda chako vizuri kuna mwingine yupo tayari kumwamsha na kumtaka.

Tangu akiwa njiani kurudi nyumbani toka kazini mtumie ujumbe mme wangu leo ninahitaji dozi tafadhali usisahau.

Hilo tu linaweza kumfanya apitie kwa fundi akombowe gauni lako ulilopeleka kushona hivi karibuni hata kama hujamwambia!

Kama kawaida mimi lazima nikushauri. Hata hapa patumie vizuri. Isiwe kila siku wewe ndiyo unaanza sababu tu nimekuambia wanaume wanapenda hivyo, hapana, fanya mara moja moja pengine mara 2 au 3 hivi kwa mwezi siyo kila siku baadhi ya wanaume wanaweza kukuona vibaya tena ukizidisha.

Wapo baadhi ya wanawake hutumia lugha ya ishara kwa mfano anaweza kuwasha taa ya rangi fulani chumbani au akaweka muziki fulani au akatandika kitanda kwa namna fulani au akavaa tu mavazi fulani na mmewe atajuwa leo anahitaji.

Si vibaya ukienda mbali zaidi ukamwambia moja kwa moja baba Amina eee mwenzio leo nahitaji haki yangu.

Soma hii pia > Namna wanawake wanavyochangia upungufu wa nguvu za kiume kwa waume zao

3. Kuleta matatizo ya maisha kitandani

Kuna baadhi ya wanawake kitandani ndiyo mahakamani kwao yaani kila tatizo linalomsibu atalileta kitandani.

Chakula kimeisha, mtoto anadaiwa ada, kuna hela ya vikoba anahitaji, kuna gauni fulani zuri ameliona yote haya atasubiri wakati mpo kitandani ndiyo aseme!

Poleni sana wanawake wa tabia hii

Hakuna mwanaume anataka hilo.

Kitandani ni sehemu ya kusahau shida kwa muda hata kama zipo, ni sehemu ya kutoa stress zako zote na siyo kuzileta stress zingine tena.

Ukiwa kitandani zungumza muda mwingi mambo yanayohusu kitandani. Kama una shida fulani nikumbushe mchana baada ya kumaliza kula chakula au asubuhi wakati naelekea kazini siyo kitandani.

Mara nyingi mwanaume anajuwa unahitaji kitu fulani au hela fulani bila hata kumuomba au kumwambia na mwanaume mwenye akili atakupa au kukusaidia bila hata kuombwa au kukumbushwa.

Sasa nyinyi ndugu zangu tupo kitandani mara ooh nadaiwa vikoba mara mama mdogo anaumwa mara sijuwi nahitaji laki mbili nikanunuwe viatu! Uume utanisimama vipi hapo?

Ndiyo hapo kuanza kesema mme wangu amepoteza nguvu za kiume au hana hamu ya tendo la ndoa na mimi kumbe ni wewe mwenyewe ndiyo umemloga bila kujuwa.

Wanaume wengi wakitoka kazini huchagua kupita bar walewe na watulie na rafiki zao mpaka saa tano ndiyo anarudi nyumbani akifika moja kwa moja usingizi maana anaogopa kuwahi kurudi nyumbani atakutana na msululu wa matatizo kutoka kwa mkewe.

Ni kweli una tatizo, ni kweli una shida fulani, ni kweli unahitahi shilingi fulani, lakini angalia ni wapi unaniambia siyo kitandani. Kitandani ni sehemu ya mimi kujificha na kusahau kwa dakika kadhaa shida za huko duniani.

4. Kukubali kila anachoambiwa na mme

Kila mtu anakemia yake na kila mtu kuna vitu anavipenda na kuvichukia.

Ikitokea kila unachoambiwa au kuombwa wewe unakubali tu ni hatari kwa afya yako ya ndoa.

Kama kuna kitu hupendi sema wazi bila kuficha wala kuogopa kuwa mimi staili hii mme wangu siipendi. Usiigize wala usiogope kuwa muwazi na mkweli kabisa mimi hicho ulichoniambia sikipendi na siwezi.

Kama unaona siku hiyo ni vizuri mmeo atumie c*nd*mu mwambie nataka uvae leo au kama hupendi avae mwambie leo nataka kavu kavu, kama mmeo anapenda mfanye jikoni na wewe hujisikii mwambie nataka chumbani nk

Hiyo ni mifano tu siwezi kuandika kila kitu mengine jiongeze na wewe.

Pointi yangu hapa ni kuwa usikubali lolote unaloambiwa au kuombwa na mmeo kitandani ikiwa wewe kwa nafsi yako hupendi.

Kama anafanya kwa fujo sana kuliko inavyohitajika mwambie nenda pole pole lasivyo unaweza kuumia au kuchanika bila sababu na mdomo wa kukataa unao.

Wanawake wengi utasikia nilipata ujauzito huu kwa bahati mbaya nilimwambia mwenzangu atumie kinga na akakataa na yeye mwanamke akakubali!

Huo ni utahila.

Usikubali kila kitu hata ambavyo hupendi. Ni mwili wako upo huru.

5. Kukaa tu kitandani kama gogo

Wapo baadhi ya wanawake yaani ni kama gogo au samaki aliyekufa

Hajuwi hata kukata kiuno

Yaani yeye avuliwe nguo, awekwe kitandani, achezewe, aandaliwe, aingiliwe yeye ni kimya tu haseguki wala kugunaguna japo kwa umbeya.

Amekaa tu anasubiri wewe mwanaume ufanye kila kitu mpaka umwambie tayari nimemaliza twende tukaoge!

Huna hata aibu yaani.

Kata kiuno japo kidogo na wakati mwingine mwambie nataka nije juu yako na wewe mwanaume uwe chini, onyesha namna fulani ya kwamba na wewe upo na unashiriki na siyo kumwachia mmeo majukumu yote

Mme atakuona wewe ni mshamba na hujuwi kitu.

Kama kawaida hapa tena lazima nikuonye.

Nenda pole pole, usijionyeshe kwamba wewe unajuwa kila kitu na vyote na kuwa unaweza hadi kumfundisha mmeo!

Nenda pole pole na kwa akili.

Usikutane tu siku ya kwanza na mmeo halafu akaona wazi kabisa umemaliza chuo kikuu, hapana anza kwa kumuonyesha shule ya msingi umemaliza na unajiandaa kwenda sekondari.

Hii inafanana na ile ya kusubiri kila siku mmeo ndiyo aanze kutaka mechi.

Onyesha namna fulani kwamba upo na unafurahia tendo lenyewe na upo tayari na unapenda kushiriki. Mtazame usoni mmeo na siyo kufumba tu macho wakati wote.

Usiwe gogo na usiwe kimya dakika zote za mechi.

Kama unaweza kulia lia, kama unaweza kutamka maneno yoyote machafu kuhusu tendo la ndoa tamka ila usikae kimya muda wote kwani inaweza kumuonyesha mmeo hufurahii tendo na pengine akaona kama vile hakufikishi popote.

Kumbuka kila jambo na wakati wake na sehemu yake.

Soma hii pia > Dawa ya asili ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke

makosa wafanyayo wanawake kitandani

6. Kudanganya kama umefika kileleni

Wanawake wengine ni wa ajabu sana yaani unaweza kubaki unashangaa tu

Unajuwa kabisa hujafika kileleni lakini unadanganya ili kumridhisha mmeo bila kujuwa unajidanganya mwenyewe.

Yaani dakika 3 tu tangu muanze mwanamke anaanza kupiga kelele na kulia akijidai wazi amefika kumbe ni uongo mtupu!

Kuwa mkweli na muwazi huku ukitumia lugha yenye staha mwambie kama unaweza tuendelee kidogo na siyo kuongopa umefika kumbe bado matokeo yake ukikutana na msukuma mkokoteni mwenye misuli yake akakukoleza vizuri kesho unaanza kuwa mchepukaji kumbe ni wewe tu hukuwa mkweli kwa mmeo.

Siyo wanawake wote wanaweza kufika kileleni kila mara wanaposhiriki tendo la ndoa lakini kudanganya ni hatari zaidi kwa furaha yako siku za usoni. Na wanawake karibu wote wanafurahi sana maandalizi kabla ya tendo la ndoa.

Wanaume ningependa nyinyi binafsi mjifunze ishara na dalili za kweli anazozionyesha mwanamke wakati anapofika kileleni na siyo mdanganywe. Kama unahitaji kuzifahamu dalili na ishara hizi nitafute WhatsApp +255714800175 kipo kitabu kwa ajili hiyo nakiuza kwa Tsh 10000.

Kwa kawaida wanawake wanaweza kufika kileleni dakika ya 8 mpaka ya 13 tangu muanze kushiriki tendo la ndoa (siyo wakati wa maandalizi). Wengine wanaweza kuchelewa mpaka dakika ya 15 wengine mpaka dakika ya 20.

Ukiona umetumia dakika 3 na mkeo akakuambia amefika ujuwe wazi anakudanganya.

Lingine la mwisho na ambalo sipendi kulielezea sana ni usafi duni wa mwili, mavazi na maeneo yako ya siri.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.

Tunajaribu kwa namna na njia zozote tunazoweza kuweza kufikisha ujumbe huu kwenu na pengine ikiwezekana tuwe tumeweza kubadili maisha ya watu hasa ya mahusiano hata hivyo kazi hii kubwa haiwezi kufanikiwa bila ushirikiano wako.

Ikiwa wewe ni mwanaume na unaona kuna makosa mengine wanawake wanafanya zaidi ya haya niliyoandika hapa tafadhali niandikie hapo chini kwenye comment.

Makosa makubwa kabisa 6 wafanyayo wanawake kitandani Click To Tweet

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao

Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 11

Let's block ads! (Why?)

Jumatatu, 21 Septemba 2020

Sababu 9 zinazosababisha ukose au uchelewe kuona siku zako

Sababu 9 zinazosababisha ukose au uchelewe kuona siku zako

Kwa mwanamke kuchelewa kupata hedhi huwa hakushitui iwapo mwanamke anajua ni nini tatizo au sababu iliyopelekea yeye kukosa hedhi.

Na majibu ya kuchelewa kwa hedhi hupatikana pindi hedhi hiyo inapochelewa.

Mfano kama ulikua unategemea kupata mimba, ikichelewa inakua ni dalili ya kwanza ya wewe kuanza kufikiria jambo ulilolitaka linaelekea kutimia na hata ukatabasamu na kuwaza hatua nyingine ya kujipima nyumbani au kuenda hospitali.

Na kama hukuwa umetarajia ndio hivyo tena mawazo ya kila aina yatakuja kichwa kutaka kujua kwanini hedhi yako imechelewa na pengine usipate majibu kabisa.

Naitwa Tabibu Fadhili Paulo, mawasiliano yangu ni WhatsApp +255714800175

Sababu 9 zinazosababisha ukose au uchelewe kuona siku zako 1

Sababu 9 zinazosababisha ukose au uchelewe kuona siku zako

1. Umeacha kutumia dawa za uzazi wa mpango

Kama umekuwa ukitumia aina yoyote ya dawa ya uzazi wa mpango za kizungu iwe ni vidonge, sindano, kijiti na kadharika mara tu utakaposimama kuzitumia dawa hizi linaweza kukutokea tatizo la kutoona siku zako.

Dawa hizi za uzazi wa mpango za kizungu kwa sehemu kubwa wakati unazitumia zinaweza kurekebisha mzunguko wako wa hedhi na hivyo unapoacha kuzitumia mwili wako unaweza kupatwa na mshituko.

Hakuna maelezo zaidi ya kwanini mwili wako unapatwa na mshituko huu baada ya wewe kuacha kuzitumia dawa hizi lakini kinachojulikana ni kuwa mwili wako utahitaji muda fulani au miezi kadhaa mpaka urudi kwenye hali yako ya kawaida kama zamani kabla hujaanza kutumia dawa za uzazi wa mpango.

Jambo moja la kuwa nalo makini hapa ni kwamba bado unaweza kupata ujauzito wakati huu hata kama huoni siku zako kama matokeo ya kuvurugika kwa siku zako yaliyotokana na kuacha kutumia dawa za uzazi wa mpango.

Kwa hiyo ikiwa hutaki kupata ujauzito unahitaji kuwa makini sana wakati huu kwani unaweza kupata ujauzito wakati wowote ikiwa utashiriki tendo la ndoa bila kinga.

2. Inawezekana umepata ujauzito

Hata kama umekuwa ukitumia dawa za uzazi wa mpango na umekuwa makini sana katika hilo bado kama unaona hupati siku zako ghafa kuna uwezekano umepata ujauzito.

Hili ndiyo linapaswa kuwa wazo lako la kwanza ikitokea siku zako zimeacha au unaona zinachelewa sana.

Hii inatokana na ukweli kuwa wakati mwingine dalili za mwanzo za ujauzito zinaweza kufanana sana na dalili za kutaka kuona siku zako na inaweza kuwa shida kutofautisha dalili za mimba na dalili za kutaka kuona siku zako.

Kwahiyo kama umekuwa ukishiriki tendo la ndoa mara kwa mara na ghafla unaona huoni tena siku zako ni vizuri kufanya kipimo kuona ikiwa ni mjamzito au la. Fanya kipimo kila baada ya wiki mbili.

3. Umepata ugonjwa fulani

Wakati mwingine ukitokewa ukaona hupati siku zako inaweza kuwa ni matokeo ya wewe kuumwa au kupatwa na ugonjwa fulani mkubwa.

Homa, mafua, aleji au ugonjwa wowote mkubwa unaoweza kuklazimisha kwenda hospitali vinaweza kuwa sababu ya wewe kukosa siku zako kama kawaida.

Magonjwa yanaweza kuwa chanzo cha kuleta mfadhaiko au msongo wa mawazo katika sehemu ya ubongo inayohusika na kuweka sawa homoni na hivyo kuvuruga mzunguko wako wa kawaida.

4. Inawezekana una uvimbe

Je chuchu zako zinatoa maji maji ya maziwa?

Wanawake wengi ukikutana nao wenye matatizo ya uzazi watakuambia wameacha kuona siku zao na wanatokewa na maji maji katika chuchu zao za maziwa na wanapata maumivu ya kichwa ya mara kwa mara.

Ikiwa umepata uvimbe hasa katika tezi ya pituitari (prolactinoma au benign tumor) uvimbe huu unaweza kusababisha kuzalishwa kwa wingi kwa homoni iitwayo prolactin.

Homoni ya prolactin inapozalishwa kwa wingi kuliko inavyohitajika na mwili inaweza kukuletea tatizo la kukosa siku zako sababu inaingiliana kimajukumu na kuzuia homoni ya estrogen kuzalishwa.

Wakati wowote homoni ya estrogen inapokuwa ndogo au chache mwili wako unapata wakati mgumu kuleta hedhi yako na kukufanya usione siku zako.

5. Unafanya SANA mazoezi ya viungo kupita kiasi

Unaenda gym au kufanya mazoezi hata kama unahisi umechoka sana na kazi za kutwa nzima? Au kwa kifupi unaishi kwenye mazoezi?

Kufanya sana mazoezi na huku unakula chakula kidogo na huku unatokewa na kupungua uzito kwa haraka vyote hivi vinaweza kuwa sababu yaw ewe kukosa siku zako hasa kama BMI yako inashuka chini ya 19 au 18.

Unachohitaji hapa ni kupunguza mazoezi na kuongeza uzito kidogo kama ulishuka sana kama matokeo ya mazoezi.

Kumbuka kama inakutokea unakosa kuona siku zako kwa muda mrefu pengine zaidi hata ya mwaka basi ni hatari kwa afya yako hasa afya ya mifupa kama inavyowatokea wamama wengi baada ya siku zako kukoma baada ya miaka 45.

6. Una mfadhaiko wa akili (stress)

Labda unakabiliwa na mzigo mkubwa wa kazi kazini kwako au una shida nyingine tu za kila siku zinazokufanya uwe na mawazo mawazo kila mara inaweza kuwa sababu kwanini huoni siku zako.

Mfadhaiko, msongo wa mawazo, mvurugiko wa akili au stress kwa kiingereza ni kitu ambacho kinaweza kuufanya mwili wako uamuwe sasa siyo wakati wa wewe kupata ujauzito na hivyo kukataa kukupa siku zako.

Mfadhaiko wa akili unaweza kukuletea tatizo la mayai yako kushindwa kupevuka vizuri.

Hii njia ya asili ya mwili ili kukulinda wewe.

Wakati wowote utakapoamua kuachana na stress mwili wako utakurudishia hedhi yako na mzunguko wako utarudi na kutulia kama mwanzo.

Kwanini mwili unapunguza kasi ya upevushaji wa mayai wakati wa msongo wa mawazo?

Mwili unatambua kwamba upo kwenye kipindi cha hatari na unatakiwa upambane ili uishi kutokana na hatari inayokuwa mbele kwa hivo maisha ni kitu cha kwanza ndipo swala na hedhi lifuate.

Mwili utatengeneza homoni za kudhibiti stress kwa wingi kama cotisoli na adrenalini ili kukuandaa kupambana, ama kukimbia hatari iliyopo mbele yako.

Fikiria pale unapotembea usiku na ukaona kitu kisicho cha kawaida mbele yako, tazama mwili unavyobadilika, sasa mabadiliko ya homoni pale unapokutana na kitu cha hatari ni sawa na vile unapopata msongo wa mawazo.

Kadiri mawazo yanavyokuathiri ndivyo uvyonaharibu mpangilio wako wa mwili na kukupelekea ukose hedhi.

Soma hii pia > Kama una stress ni vigumu kupata ujauzito

7. Homoni zako zimevurugika

Hii ndiyo sababu namba moja ya hedhi yako kuacha kutoka au kuvurugika.

Tezi ya thairodi ni kiungo chenye umbo la kipepeo.

Kiungo hiki kipo kwenye shingo chini ya koromeo la sauti.

Kazi kuu ya Tezi hii ni kuzalisha homoni za (T3) na (T4), ambazo kwa pamoja hufanya kazi ya kurekebisha mzunguko wa damu na kazi mbalimbali za mwili.

Matatizo kwenye tezi ya Thairodi kama kushuka kwa uzalishaji wa homoni ama tezi kufanya kazi kupita kiasi huweza kuleta mabadiliko pia kwenye kiwango cha homoni za estrogeni na cotisoli.

Kiwango cha cotisoli kwenye damu kinapokuwa kingi hupunguza uwezo wa tezi ya thairoidi ambapo matokeo yake ni kushuka kwa kazi za mwili kama upevushaji wa mayai na uzalishaji wa homoni za kike

Vile vile lishe mbaya yenye upungufu wa virutubisho ikiwemo vitamini na madini na yenye sukari na viambata vya kuongeza ladha kwa wingi hupelekea tezi za Adrenali na Thairodi kufaya kazi kupita kiasi.

Kitendo hiki hupelekea uzalishaji wa kichocheo cha cotisoli ambacho kinapunguza uzalishaji wa homoni za uzazi.

Cotisoli inapokuwa nyingi zaidi pia inaweza kuleta madhara mwilini kama udhaifu wa mifupa, ngozi kuharibika, tishu za ubongo  na misuli kudhoofika na kukupa wewe tatizo la kuvurugika au kukosa hedhi.

8. Umeongezeka uzito

Kama vile ukiwa na uzito pungufu kunaleta tatizo la kukosa siku zako kadharika uzito uliozidi au unene uliozidi pia unaweza kukusababishia ukapoteza kuona siku zako.

Wanawake wenye uzito wa juu au unene uliopitiliza wana uwezekano wa mara mbili zaidi wa kuwa na mzunguko wa hedhi usioeleweka tofauti na wenye uzito mzuri wa kawaida.

Mwanamke kuwa na uzito uliozidi unaweza kuwa sababu ya matatizo ya homoni zake na uzito kupita kiasi una uhusiano na tatizo linguine la uzazi kwa wanwake lijuliknalo kwa kitaalamu kama Polycystic Ovarian Sydrome (PCOS).

Kama unataka kupungua uzito wako kwa njia salama bonyeza hapa.

9. Umepata watu wengine wa kulala nao chumba kimoja

Hili linaweza lisiwe na uthibitisho wa kisayansi lakini tafiti mbalimbali zinasema ikiwa ulikuwa unalala peke yako kwa kipindi kirefu na mara ukapata wasichana wengine wa kulala na wewe chumba kimoja hili linaweza kusababisha kuanza kupata hedhi isiyoeleweka.

Hili ni rahisi kutokea hasa kama umetoka nyumbani na umehamia shule ya bweni au hosteli kitendo hiki cha kuanza kuwa pamoja na wengine na kuzoeana nao kinaweza kukuletea kuvurugika kwa siku zako kama sehemu ya kuzoeana na makundi ya watu wengine.

Wasichana wengi wa chuo wanaweza kukuambia hili limewahi kuwatokea kwenye maisha yao.

Vipimo vifuatavyo vinaweza kufanywa kuchunguza sababu za kukosa hedhi kwa mwanamke:

  • Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha homoni za FSH, LH, TSH na prolactin ambazo uzalishwaji wake unachochewa na tezi ya pituitary, na pia kupima kiwango cha homoni ya estrogen inayozalishwa na ovary.
  • Kipimo cha ultrasound ya nyonga kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo katika njia ya uzazi na pia kuchunguza hali ya ovary.
  • CT scan au MRI ya kichwa kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo kwenye tezi ya pituitary au hypothalamus.
  • Vipimo vya kufahamu ufanyaji kazi wa tezi ya thyroid
  • Kupima damu ili kufahamu kiwango cha homoni ya prolactin katika damu
  • Kuchunguza uterus kwa kutumia aina ya X-ray inayoitwa Hysterosalpingogram na kipimo kingine kiitwacho Hysteroscopy ambacho huchunguza chumba cha uterus.
Kama unatafuta dawa nzuri ya asili ili upate ujauzito niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175
SHARE POST HII NA WENGINE UWAPENDAO
Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 4

Let's block ads! (Why?)

Alhamisi, 17 Septemba 2020

14-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Kuvaa Kitu Kwa Ajili Ya Kinga

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

14 -Kuvaa Kitu Kwa Ajili Ya Kinga

Alhidaaya.com

 

 

Itikadi za watu kuvaa vitu au kujifunga navyo mwilini kwa kuepusha au kujikinga na kijicho, husda na madhara mengineyo. Jambo hili halijuzu kwa sababu hivyo vitu havina uwezo wa hayo wala hakuna atakayeweza kumuondoshea mtu madhara isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Anasema:

 

وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٧﴾

Na Allaah Akikugusisha kwa dhara, basi hakuna yeyote wa kukuondolea hiyo isipokuwa Yeye; na Akikugusisha khayr, basi Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. [Al-An’aam:  17]

 

 

Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameharamisha hayo  katika Hadiyth mbali mbali:

 

 عَنْ قَيْسِ بْنِ السَّكَنِ الأَسَدِيِّ قَالَ: دَخَلَ عَبْدُ اللهِ بْنُ مَسْعُودٍ رضي الله عنه عَلَى امْرَأَةٍ، فَرَأَى عَلَيْهَا خَرَزًا مِنَ الحُمْرَةِ، فَقَطَعَهُ قَطْعًا عَنِيفًا، ثُمَّ قَالَ: إِنَّ آلَ عَبْدِ اللهِ عَنِ الشِّرْكِ أَغْنِيَاءُ، كَانَ مِمَّا حَفِظْنَا عَنِ النَّبِيِّ صلّى الله عليه وسلّم: ((إِنَّ الرُّقَى وَالتَّمَائِمَ وَالتِّوَلَةَ شِرْكٌ)) رواه الحاكم وقال: " صحيح الإسناد "، ووافقه الذّهبي والألبانيّ في "الصّحيحة" (برقم 331).

Imepokelewa kutoka kwa Qays bin As-Sakan Al-Asadiyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Abdullaah bin Mas‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliingia kwa mwanamke ambaye alivaa shanga nyekundu, akazikatilia mbali kisha akasema: “Hakika ahli ya ‘Abdullaah hawahitaji shirki!”. Akasema pia: “Katika ambayo amehifadhi kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni: ((Hakika Ar-Ruqaa (zisizothibiti), At-Tamaaim, At-Tiwaalah ni shirki).)) [Al-Haakim amesema Isnaad Swahiyh na ameikubali Adh-Dhahabiy na Al-Albaaniy katika Asw-Swahiyhah (331)]

 

At-Tamaaim:  Wanachofungwa watoto (kama kitambaa cheusi au nyuzi n.k.) shingoni (au mkononi) kukinga jicho baya.

 

 

Ar-Ruqaa au Al-‘Azaaim: Ni tabano au azima inayosomwa. Imeruhusiwa tu inapokuwa haina shirki. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameiruhusu inapokuwa hali ya kudonelewa na mdudu sumu au anapopatwa mtu na jicho baya (au husda) au homa.

 

 

At-Tiwaalah (mvuto wa ndere): Kinachodaiwa kuwa kinasababisha mwanamke apendwe zaidi na mumeme au mume apendwe zaidi na mkewe.

 

 

Hadiyth nyenginezo zinazoharamisha kuvaa vitu kwa ajili ya kinga ni zifuatazo:

 

عَنْ أَبِي بَشِيرٍ الأَنْصَارِيِّ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) أَنَّهُ كَانَ مَعَ رَسُولِ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي بَعْضِ أَسْفَارِهِ، فَأَرْسَلَ رَسُولاً, أَنْ ((لاَ يَبْقَيَنَّ فِي رَقَبَةِ بَعِيرٍ قِلادَةٌ مِنْ وَتَرٍ أَوْ قِلادَةٌ إِلاَّ قُطِعَتْ)).

Imepokewa kutoka kwa Abu Bashiyr Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba alikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika safari mojawapo. Akamtuma mjumbe kuamrisha kwamba: ((Kusiachwe kidani cha uzi au kidani chochote katika shingo za ngamia isipokuwa kikatwe)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Pia:

 

 رَوَى أَحْمَدُ عَنْ رُوَيْفِعٍ قَالَ؛ قَالَ لِي رَسُولُ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((يَا رُوَيْفِعُ، لَعَلَّ الْحَيَاةَ سَتَطُولُ بِكَ؛ فَأَخْبِرِ النَّاسَ أَنَّ مَنْ عَقَدَ لِحْيَتَهُ، أَوْ تَقَلَّدَ وَتَرًا، أَوِ اسْتَنْجَى بِرَجِيعِ دَابَّةٍ أَوْ عَظْمٍ؛ فَإِنَّ مُحَمَّدًا بَرِيءٌ مِنْهُ))

Ahmad amepokea kutoka kwa Ruwayfi’ ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameniambia: ((Ee Ruwayfi’! Huenda ukaishi zaidi baada yangu. Kwa hiyo wajulishe watu kwamba: Yeyote atakayefunga fundo ndevu zake, au akaweka nyuzi au mshipi shingoni mwake [kuwa ni talasimu] au akastanji na mkojo wa mnyama au mfupa, basi Muhammad amejitenga naye)). [Ahmad, Abuu Daawuwd]

 

 

Vitu ambavyo aghlabu hutumiwa na watu kuvivaa au kujifunga wakiamini vinawakinga:

 

 

a) Hirizi za vitambaa vyenye maandishi ndani ikiwa ya Quraan au mengineyo.

 

 

                   

 

   

 

 

 

 

 

b) Mtoto mchanga kupakwa masinzi au wanja usoni au kuandikwa Jina la Allaah!

 

 

c) Kuwapaka watoto wachanga wanja usoni na nakshi za nyota na mwezi, kwa kuamini ule wanja unazuia 'ayn (kijicho).  

 

 

d) Anapolazwa mtoto mchanga kukiwa chini ya mto wake vitu kama kisu, ndimu n.k.

 

 

e) Kuvalishwa vyuma mkononi.

 

f) Kuvalishwa mtoto mchanga au hata wakubwa, kidani chenye lakti ya Aayatul-Kursiy au Jina la Allaah! Ni jambo linalotendwa na wengi! Hakika ni kosa kubwa kwani ni kudhihirisha kutokumadhimisha Allaah kwa sababu kidani hicho anaingia nacho mtu chooni. Juu ya hivyo ni kuitakidi kuwa kinamkinga mtu na shari, uhasidi, jicho n.k. Imeshatangulia Hadiyth mbali mbali na Fataawa za ‘Ulamaa kukataza haya, na rejea mlango wa “Kutundika vitu”. 

 

g) Kuvalishwa kitambaa cheusi mkononi wengine wanatia mvuje ndani yake yenye harufu mbaya kuepusha majini.

 

h) Mapambo yenye kuandikwa Aayah za Qur-aan:

 

 

 

 

i) Mapambo ya vijiwe vya rangi ya buluu, vinginevyo vina jicho.

 

   

             

    

 

   

            

 

 

 

           

 

 

           

 

 

 

 

j) Kuvaa pete au mapambo yenye vito rangi kadhaa kwa kuitakidi rangi hizo zina maana ya wanachoita ‘bahati nzuri’ au kuleta hali fulani njema kutokana na tarehe au miezi ya kuzaliwa:

 

           

 

 

 

 



52-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ametumwa Kubashiria Na Kuonya Walimwengu

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

52-Ametumwa Kubashiria Na Kuonya Walimwengu

 

www.alhidaaya.com

 

 

Kama ilivyotangulia fadhila ya kuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ametumwa kwa Walimwengu wote, basi kubashiria na kuonya kwake hali kadhalika ni kwa ajili ya ulimwengu mzima na si kaumu yake tu kama ilivyokuwa desturi ya Manabii wengineo kabla yake:

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):   

 

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا ﴿١﴾

Amebarikika Ambaye Ameteremsha kwa mja Wake pambanuo (la haki na batili) ili awe muonyaji kwa walimwengu. [Al-Furqaan: 1]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

أَكَانَ لِلنَّاسِ عَجَبًا أَنْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ رَجُلٍ مِّنْهُمْ أَنْ أَنذِرِ النَّاسَ وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا أَنَّ لَهُمْ قَدَمَ صِدْقٍ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ قَالَ الْكَافِرُونَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ مُّبِينٌ﴿٢﴾

Je, imekuwa ni ajabu kwa watu kwamba Tumemfunulia Wahy mtu miongoni mwao kwamba: Waonye watu na wabashirie wale walioamini kwamba watapata cheo kitukufu mbele ya Rabb wao. Makafiri wakasema: Hakika huyu bila shaka ni mchawi bayana. [Yuwnus: 2]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَأَرْسَلْنَاكَ لِلنَّاسِ رَسُولًا ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا ﴿٧٩﴾

Na Tumekutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa watu uwe Rasuli na inatosheleza Allaah kuwa ni Mwenye kushuhudia yote. [An-Nisaa: 79]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ ۚ

Na nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia.[Al-An’aam: 19]

 

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٤٥﴾

Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekutuma uwe shahidi, na mbashiriaji na mwonyaji.

 

وَدَاعِيًا إِلَى اللَّـهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجًا مُّنِيرًا ﴿٤٦﴾

Na mlinganiaji kwa Allaah kwa idhini Yake; na siraji kali yenye nuru.

 

وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ بِأَنَّ لَهُم مِّنَ اللَّـهِ فَضْلًا كَبِيرًا ﴿٤٧﴾

Na wabashirie Waumini kwamba watapata kutoka kwa Allaah fadhila kubwa.

 

وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ وَدَعْ أَذَاهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٤٨﴾

Na wala usiwatii makafiri na wanafiki, na achilia mbali maudhi yao, na tawakali kwa Allaah. Na Allaah Anatosheleza kuwa Mdhamini. [Al-Ahzaab: 45-48]

 

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٦٧﴾

Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha ujumbe Wake. Na Allaah Atakuhifadhi dhidi ya watu. Hakika Allaah Haongoi watu makafiri [Al-Maaidah: 67]

 

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida  inayohusiana na maudhui ya fadhila hii:

 

 

02-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ametumwa Kwa Walimwengu Wote

 

 

 

 



08-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Zuhd Yake: Njaa Ilimtoa Nje

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

08-Zuhd Yake: Njaa Ilimtoa Nje

 

Alhidaaya.com

 

 

Siku moja au usiku mmoja, pindi njaa ilipomzidi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka nje, akakutana na Swahaba zake ambao nao pia wametoka nje kwa sababu ya kubanwa na njaa:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَوْمٍ أَوْ لَيْلَةٍ فَإِذَا هُوَ بِأَبِي بَكْرٍ وَعُمَرَ فَقَالَ ‏"‏ مَا أَخْرَجَكُمَا مِنْ بُيُوتِكُمَا هَذِهِ السَّاعَةَ ‏"‏ ‏.‏ قَالاَ الْجُوعُ يَا رَسُولَ اللَّهِ ‏.‏ قَالَ ‏"‏ وَأَنَا وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لأَخْرَجَنِي الَّذِي أَخْرَجَكُمَا قُومُوا ‏"‏ ‏.‏ فَقَامُوا مَعَهُ فَأَتَى رَجُلاً مِنَ الأَنْصَارِ فَإِذَا هُوَ لَيْسَ فِي بَيْتِهِ فَلَمَّا رَأَتْهُ الْمَرْأَةُ قَالَتْ مَرْحَبًا وَأَهْلاً ‏.‏ فَقَالَ لَهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ أَيْنَ فُلاَنٌ ‏"‏ ‏.‏ قَالَتْ ذَهَبَ يَسْتَعْذِبُ لَنَا مِنَ الْمَاءِ ‏.‏ إِذْ جَاءَ الأَنْصَارِيُّ فَنَظَرَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَصَاحِبَيْهِ ثُمَّ قَالَ الْحَمْدُ لِلَّهِ مَا أَحَدٌ الْيَوْمَ أَكْرَمَ أَضْيَافًا مِنِّي  قَالَ - فَانْطَلَقَ فَجَاءَهُمْ بِعِذْقٍ فِيهِ بُسْرٌ وَتَمْرٌ وَرُطَبٌ فَقَالَ كُلُوا مِنْ هَذِهِ ‏.‏ وَأَخَذَ الْمُدْيَةَ فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ إِيَّاكَ وَالْحَلُوبَ ‏"‏ ‏.‏ فَذَبَحَ لَهُمْ فَأَكَلُوا مِنَ الشَّاةِ وَمِنْ ذَلِكَ الْعِذْقِ وَشَرِبُوا فَلَمَّا أَنْ شَبِعُوا وَرَوُوا قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لأَبِي بَكْرٍ وَعُمَرَ ‏"‏ وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَتُسْأَلُنَّ عَنْ هَذَا النَّعِيمِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَخْرَجَكُمْ مِنْ بُيُوتِكُمُ الْجُوعُ ثُمَّ لَمْ تَرْجِعُوا حَتَّى أَصَابَكُمْ هَذَا النَّعِيمُ ‏"‏ ‏.‏ مسلم

 

Amehadithia Abuu Hurayrayh (رضي الله عنه) kwamba: Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka mchana mmoja, au usiku, akakutana na Abuu Bakr na ‘Umar (رضي الله عنهما) akawauliza: “Jambo gani lililokutoeni majumbani mwenu wakati huu?”  Wakasema: “Ni njaa ee Rasuli wa Allaah!” Akasema: “Nami naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, nami pia lililonitoa ni kama lililowatoa nyinyi. Twendeni!”  Wakafuatana naye hadi nyumbani kwa mtu miongoni mwa Answaariy, lakini hawakumkuta nyumbani kwake. Mkewe alipomuona (Rasuli wa Allaah) alimwambia: “Marhaban wa Ahlan” (Karibu). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Yuko wapi fulani?” Akajibu: Amekwenda kututafutia maji matamu.” Mara yule Answaariy akaja akamtazama Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba zake akasema: “AlhamduliLLaah! Leo hakuna mwenye wageni watukufu kama mimi!” Akaondoka kisha akarudi na kichala cha tende tosa, tende kavu na tende mbivu, Akwaambia: “Kuleni!” Akachukua kisu lakini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Usichinje mbuzi wa maziwa.” Akawachinjia wakala mbuzi yule na wakala katika kile kichala cha tende na wakanywa. Waliposhiba na wakamaliza kiu chao, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akawaambia Abuu Bakar na ‘Umar (رضي الله عنهما): “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, mtaulizwa Siku ya Qiyaamah juu ya neema hii. Njaa imewatoa majumbani mwenu, kisha hamkurejea mpaka mkapata neema hii.” [Muslim]

 

Na alifundisha du’aa ya kumumobea mtu anayekupa chakula au kinywaji useme:

 

اللّهُـمَّ أَطْعِمْ مَن أَطْعَمَني، وَاسْقِ مَن سَقانِي

Allaahumma Atw-’im man atw-’amaniy Wasqi man saqaaniy

Ee Allaah Mlishe aliyenilisha na Mnywishe aliyeninyweisha  [Hadiyth ya Al-Miqdaad bin Al-Aswad  (رضي الله عنه) - Muslim (3/126) [2055], Ahmad]

 

 

 



010-Aayah Na Mafunzo: Kula Mali Ya Yatima Ni Miongoni Mwa Mambo Saba Yanayoangamiza

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Kula Mali Ya Yatima Ni Miongoni Mwa Mambo Saba Yanayoangamiza

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا ۖ وَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا ﴿١٠﴾

10. Hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhulma hapana shaka kwamba wanakula katika matumbo yao moto, na watauingia moto uliowashwa vikali mno”

 

Mafunzo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه عن النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ)) قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَمَا هُنَّ؟  قَالَ: ((الشِّرْكُ بِاللَّهِ وَالسِّحْرُ وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ وَأَكْلُ الرِّبَا وَأَكْلُ مَالِ الْيَتِيمِ وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ وَقَذْفُ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ الْغَافلاَتِ)) متفق عليه

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:((Jiepusheni na mambo saba yanayoangamiza!)) Wakauliza: Ni yepi hayo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: ((Ni kumshirikisha Allaah, sihri [uchawi], kuua nafsi Aliyoiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki, kula ribaa, kula mali ya yatima, kukimbia wakati wa kupambana na adui na kuwatuhumu uzinifu wanawake Waumini waliohifadhika walioghafilika)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 



20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...