Translate

Alhamisi, 4 Juni 2020

04-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Shirki Inabatilisha ‘Amali

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

 

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno

 

04- Shirki Inabatilisha ‘Amali

 

Alhidaaya.com

 

 

‘Amali za Muislamu bila ya kuwa na niyyah safi kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) au ikhlaasw, huwa hazina thamani mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa dalili zifuatazo:

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا ﴿٢٣﴾

Na Tutayaendea yale waliyoyatenda ya ‘amali yoyote ile, Tutayafanya   chembechembe za vumbi zinazoelea hewani zinazotawanyika. [Al-Furqaan: 23]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴿٦٥﴾

Kwa yakini umefunuliwa Wahy na kwa wale walio kabla yako kwamba: “Ukifanya shirki bila shaka zitaporomoka ‘amali zako na bila shaka utakuwa miongoni mwa waliokhasirika.” [Az-Zumar: 65]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾

Na kama wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda. [Al-An’aam: 88]

 

 

 

Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametaja katika Hadiyth Al-Qudsiy:

 

 

عنْ ابي هريرة رضي الله عنه أنَّه صلَّى الله عليه وسلَّم قال: ((قال الله تعالى: أنا أغْنى الشُّركاء عن الشِّرْك، فمَن عمل عملاً أشْرَك فيه معي غيري تركتُه وشِرْكه))    

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Allaah Ta’aalaa Anasema: ‘‘Mimi ni mwenye kujitosheleza kabisa, sihitaji msaada wala mshirika. Kwa hiyo, yule afanyaye ‘amali kwa kunishirikisha na mtu, nitaikanusha pamoja na mshirika wake.”)) Yaani: hatopata ujira wowote kwa ‘amali hiyo. [Muslim (2985), Ibn Maajah (4202)]

 

 

Mfano bayana wa kubatilika ‘amali za mtu kwa anayetoa swadaqah kwa riyaa ni kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّمَّا كَسَبُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٢٦٤﴾

 Enyi walioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali yake kwa kujionyesha kwa watu wala hamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama jabali juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa ikaliacha tupu. Hawana uwezo juu ya lolote katika waliyoyachuma. Na Allaah Haongoi watu makafiri.  [Al-Baqarah: 264]

 

 



42-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Kigezo Kizuri Kwa Anayetaka Kufaulu Aakhirah

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

42-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Kigezo Kizuri Kwa Anayetaka Kufaulu Aakhirah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Amemjaalia Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa na tabia njema zilokamilika nazo ni kigezo kwa yeyote yule anayetaka kufuzu Aakhirah kwa kuingizwa Jannah (Peponi) na kuepushwa na Moto. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ  

Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Rasuli wa Allaah kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho  [Al-Ahzaab: 21]

 

Imaam As-Sa’dy (رحمه الله) amesema kuhusu kauli hiyo ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

“Mwenye kufuata kigezo chake amefuata njia ya kumfikisha katika Utukufu wa Allaah na hiyo ndio Njia Iliyonyooka. Na kigezo hicho kizuri hukifuata  na kupata tawfiyq kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho, kwa sababu ya kuwa kwake na iymaan, khofu ya Allaah, kutaraji thawabu na khofu ya adhabu Yake, basi hujihimiza kufuata kigezo cha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).” [Tafsiyr As-Sa’dy]

 

 

 

 



42-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake Katika Ibaadah: Hakujitukuza Kwa Kujitanguliza Yeye Katika Jamaraat (Kurusha Vijiwe Minaa)

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

46-Unyenyekevu Wake Katika Ibaadah Hakujitukuza Kwa  Kujitanguliza Yeye

Katika Jamaraat (Kurusha Vijiwe Minaa)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Ingawa kawaida ya viongozi hutangulia kutekeleza jambo, na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa ni kiongozi wa Swahaba katika kutekeleza taratibu za Hajj, lakini hakujipa umbele kama kiongozi, bali alifanya nao pamoja bila ya kujitukuza.  

 

 

 عَنْ قُدَامَةَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَرْمِي جَمْرَةَ الْعَقَبَةِ يَوْمَ النَّحْرِ عَلَى نَاقَةٍ لَهُ صَهْبَاءَ لاَ ضَرْبَ وَلاَ طَرْدَ وَلاَ إِلَيْكَ إِلَيْكَ ‏.‏

 

Amehadithia Qudaamah bin ‘Abdillaah kwamba: “Nilimuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa juu ya ngamia aliyechanganyika rangi nyekundu na kahawia, akirusha vijiwe katika Jamarah ya Al-‘Aqabah (Minaa) Siku ya An-Nahr (Siku ya Iydul-Adhw-haa), bila kumpiga mtu yeyote au kumfukuza." [At-Tirmidhiy na amesema Abuu ‘Iysaa Hadiyth Hasan Swahiyh. Imekusanywa pia na An-Nasaaiy na Ibn Maajah]

 

 

 



Jumatano, 3 Juni 2020

Fangasi ukeni na tiba yake

Fangasi ukeni na tiba yake

fangasi ukeni na tiba yake

Kwa kawaida mwanamke hutokwa na majimaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano.

Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho, hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu kama ‘Vaginosis’.

Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanaume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla.

Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni:

• Kuwa na wapenzi wengi
• Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango
• Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali
• Uchafu
• Uvutaji sigara
• Pombe
• Maambukizi ya Bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni

Dalili:

• Kutokwa na uchafu usio wa kawaida
• Kutokwa na uchafu wenye harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza
• Kuwashwa sehemu za siri na ndani ya uke
• Uke unaweza kubadilika na kuwa na rangi nyekundu
• Maumivu sehemu za siri wakati wa kukojoa
• Maumivu makali chini ya kitovu
• Kutokwa uchafu uliochanganyika na damu

Fangasi ukeni na tiba yake

Matibabu

Dawa ya asili ya fangasi ukeni  > Palimaua
Ili kutibu aina yoyote ya maambukizi ya ndani ya mwili ambayo yanahusu bakteria, virusi au fangasi kunategemea sana na uimara na ubora wa kinga yako ya mwili.

Kinga yako ya mwili inajumuisha aina ya seli nyeupe maalumu ambazo hutafuta na kuua bakteria na vijidudu vingine nyemelezi ambavyo husababisha magonjwa.

Kinga yako ya mwili inapokuwa ni dhaifu bakteria wabaya wanaweza kuongezeka na kujirundika mwilini na kusambaa mpaka kwenye via vya uzazi kwa njia ya damu.

Kwahiyo ili kutibu na kukinga P.I.D unahitaji kuwa na dawa ya uhakika ya kuboresha kinga yako ya mwili ifanye kazi kwa kiwango chake cha juu kabisa.

  • Palimaua ni mchanganyiko wa dawa kadhaa za asili maalumu kwa kuimarisha kinga ya mwili nzuri kuliko dawa nyingine yoyote unaifahamu au uliyowahi kutumia.
  • Ni dawa nzuri ya asili inayondoa sumu mwilini.
  • Ina Vitamini C. Vitamini C ni mhimu katika kurejesha kinga ya mwili kwa sababu ni vitamini inayofanya kazi ya kuripea seli za mwili na kinga ya mwili.
  • Vitamini C huimarisha ngozi ya mwili, nywele, fizi, macho na kuongeza nguvu ya jumla ya mwili
  • Ina Vitamini A ambayo ni moja ya vitamini zinazotajwa kuwa mhimu sana katika kuimarisha kinga ya mwili.
  • Vitamini A ni mhimu kwa watu wanaosumbuliwa na matatizo kama ya kuharisha, upungufu wa kinga mwilini, surua na malaria.
  • Palimaua husafisha mwili wako wote, inasafisha ini, figo, moyo, macho, inaimarisha meno, ngozi na nywele.
  • Ni dawa bora ya asili yenye nguvu dhidi ya bakteria (anti-bacteria), ni dawa dhidi ya virusi (anti-virus) na ni dawa pia dhidi ya fangasi (anti-fungus).
  • Pia ni dawa nzuri kwa mtu mwenye tatizo la kukosa usingizi.
  • Usingizi ni kitu mhimu katika kuongeza, kutunza na kuimarisha kinga ya mwili.
  • Kama hupati usingizi mzuri na wa kutosha kila siku ni vigumu mwili wako kuwa na kinga nzuri ya mwili na hivyo utashambuliwa kirahisi na magonjwa ya bakteria, virusi na fangasi.
  • Ikiwa ni mjamzito usitumie dawa hii.
  • Inatibu pia vidonda vya tumbo
  • Mara zote pata ushauri toka kwa tabibu kabla ya kuanza kutumia dawa yoyote

Mara uonapo dalili hizo unashauriwa kwenda kumuona daktari haraka iwezekanavyo kwa vipimo zaidi na dawa zaweza kuwa ni za kunywa au za kupaka.

Mpaka hapo nimekupa hii Elimu BURE pia nimekuandikia maelezo namna ya kutumia BURE hujanilipa hata sh 100. Hela haitibu mtu ndiyo maana hata matajiri hufariki.

Je unahitaji dawa ya asili ya kutibu fangasi ukeni? Kama ndiyo niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

MAMBO MHIMU YA KUZINGATIA:

Zingatia dawa peke yake haitofaa kitu bila kuzingatia ushauri au masharti mhimu yafuatayo:

1. Kunywa maji mengi kila siku kuanzia glasi 8 hadi 10
2. Tumia zaidi vyakula vyenye vitamini B, C, D na E
3. Tumia sana matunda hasa machungwa, limau, ndizi na vitunguu
4. Punguza vyakula vyenye wanga
5. Acha kutumia vidonge vya uzazi wa mpango, hii ni kwa sababu vidonge hivi vinasemwa huwa vinasababisha kushuka kwa kinga ya mwili na kukufanya mrahisi kupata maambukizi ya fangasi.
6. Epuka mapenzi kinyume na maumbile
7. Acha kutumia sukari na badala yake tumia asali
8. Usitumie chokoleti na vitu vingine vya namna hiyo
9. Kuwa na mpenzi mmoja tu
10. Pendelea kujiweka msafi muda wote
11. Oga maji ya moto
12. Acha vinywaji baridi, acha pia chai ya rangi na kahawa
13. Acha vilevi
14. Acha matumizi ya pafyumu hasa maeneo ya huko

MHIMU: Kama unahitaji USHAURI TU niandikie hapo kwenye comment nitakujibu, nitafute WhatsApp ikiwa tu unahitaji dawa toka kwangu moja kwa moja.

Mjulishe pia rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Fangasi ukeni na tiba yake Click To Tweet

Tafadhali SHARE post hii na wengine uwapendao

Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 9

Let's block ads! (Why?)

Jumanne, 2 Juni 2020

Dawa ya asili ya kutibu saratani ya tezi dume

Dawa ya asili ya kutibu saratani ya tezi dume

MAFUTA YA HABBAT SODA NI DAWA BORA YA SARATANI YA TEZI DUME

Mafuta ya habbat soda yana sifa ya kudhibiti vivimbe na seli za kansa.

Dawa hii ya asili imeshafanyiwa majaribio mengi na kila mara matokeo yake yamethibitika wazi kwamba ni dawa bora kwa kansa karibu zote. Ni dawa pia kwa tatizo lingine la uvimbe wa tezi ya prostate au eneo jirani inayosababishwa na vimelea vya maambukizi lijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘prostatitis’.

Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda yanaweza kuziua seli za saratani kwa zaidi ya asilimia 50 mpaka 80.

Mtume Muhammad (S.A.W) amewahi kunukuliwa akisema ‘Mafuta ya habbat soda ni dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa kifo’.

Daktari maarufu duniani Dr Gary Null anasema: “Mafuta ya habbat soda pengine ndiyo dawa pekee mhimu zaidi unaweza kuiweka katika mfumo wako wa mwili.”

Kwa hiyo katika moja ya orodha ya dawa zako katika kujitibu saratani ya tezi dume basi mafuta ya habbat soda lazima yawemo.

Vitu viwili mhimu zaidi ambavyo mafuta haya yanavyo ni ‘thymoquinone’ na ‘thymohydroquinone’.

Vimeng’enya hivi viwili ndivyo vinaweza kusemwa kuwa ndiyo sababu ya mafuta haya kuwa ni dawa kwa kila ugonjwa. Vinaimarisha moja kwa moja kinga yako ya mwili na kuifanya ipatikane wakati wowote itakapohitajika na mwili.

Vimeng’enya hivi viwili ndivyo inaaminika ndiyo sababu mfalme Tut alipatikana na chupa ya mafuta ya habbat soda kwenye kaburi lake zaidi ya miaka 3300 iliyopita akitumaini kuyachukua na kuyatumia atakapofufuka!

Dawa ya asili ya kutibu saratani ya tezi dume 1

Habbat soda ina sifa hizi:

  1. Huondoa bakteria mwilini
  2. Huondoa uvimbe
  3. Huondoa sumu mwilini
  4. Inaondoa fangasi
  5. Inatibu kansa
  6. Inatibu pumu
  7. Inadhibiti kazi za histamini
  8. Inaua virusi
  9. Inazuia damu kuganda

Umhimu wa dawa hii ulikuwa umesahaulika kiasi fulani mpaka mwanzoni mwa miaka ya 1960.

Kuanzia 1960 kumekuwa na tafiti baada ya tafiti kuhusu uwezo wa dawa hii kutibu magonjwa mbalimbali mwilini na watafiti wote wameweza kuthibitisha pasipo na shaka kwamba ni dawa nzuri sana kwa kutibu na kuzuia saratani karibu zote.

Tafiti za hivi karibuni kutoka Maabara ya Kituo cha Utafiti wa Saratani Carolina Kusini Marekani umethitika pasipo na shaka kwamba mafuta ya habbat soda huzidhibiti seli za kansa kwa haraka sana kwa zaidi ya asilimia 80 muda mchache tangu uanze kuyatumia.

Utafiti huo umesema mafuta ya habbat soda yanaongeza seli za kwenye uboho wa mifupa (bone marrow cells) kwa asilimia mpaka 250 na hii ndiyo sababu inayoyafanya mafuta haya kuwa dawa bora zaidi katika kuongeza kinga ya mwili na hivyo kuzuia kuongezeka kwa vivimbe mwilini kwa zaidi ya asilimia 50.

Na majibu mazuri juu ya tafiti hizi hayaishii hapo, maelefu ya taarifa na tafiti kuhusu dawa hii yanaednelea kutolewa kila mara.

Mwisho wa siku rafiki kama unasumbuliwa na saratani ya tezi dume basi usiache kutumia mafuta ya habbat soda.

Namna ya kutumia mafuta ya habbat soda kutibu saratani ya tezi dume:

Tumia kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 2 asubuhi saa kumi na mbili na usiku saa tatu wakati unakula chakula katikati ya mlo wakati unaendelea kula chakula au baada ya chakula unapokaribia kwenda kulala.

Unaweza pia kuchanganya ndani ya kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani au unaweza kuchanganya na asali kijiko kikubwa kimoja na utumie.

Kwa matokeo ya uhakika tumia mwezi mmoja mpaka miwili hivi.

Kama utahitaji mafuta ya asili ya habbat soda niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175. Kama upo Dar naweza kukuletea mpaka ulipo bila gharama ya ziada.

Elewa mafuta haya hayapatikani kirahisi na ni kitu kisichojulikana na watu wengi, usipokuwa makini utauziwa feki.

Mjulishe pia rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Dawa ya asili ya kutibu saratani ya tezi dume Click To Tweet

Tafadhali SHARE post hii na wengine Uwapendao

Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 9

Let's block ads! (Why?)

Jumatano, 27 Mei 2020

Dawa ya kisukari inashukiwa kusababisha saratani

Dawa ya kisukari inashukiwa kusababisha saratani

Dawa ya kisukari inashukiwa kusababisha saratani

Dawa maarufu ya kudhibiti kisukari aina ya pili ijulikanayo kama Metformin inachunguzwa na Mamlaka ya chakula na dawa ya Marekani FDA kama inaweza kuwa ina vitu vinavyoweza kusababisha saratani.

Ripoti ya WSB  ya tarehe 9 disemba 2019 inasema Metformin inaweza kuwa na kitu kinachosababisha saratani kijulikanacho kwa kitaalamu kama N-Nitrosodimethylamine kwa kifupi NDMA kwa watumiaji wa dawa hiyo.

Soma hii pia > Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili

Kwa mjibu wa taarifa hiyo Metformin hutumika kwa wagonjwa wa kisukari aina ya pili.

Karibu kila mtu ana hatari ya kupatwa na saratani inayotokana na NDMA kutokana na ukweli kwamba ni aina ya taka inayoweza kupatikana katika maji na vyakula tunavyokula kila siku na ikiwa unakunywa au kula vyakula vyenye taka ya aina hii kuna uwezekano ukapatwa na saratani siku za mbeleni kwa mjibu wa FDA.

Pamoja na dawa hii ya Metformin kufanyiwa utafiti huu kuona kama inaweza kuleta shida ya saratani kwa watumiaji wake, bado wagonjwa wanashauriwa kuendelea kuitumia ili kudhibiti ugonjwa wao wa kisukari.

“Itakuwa ni hatari kwa wagonjwa wa kisukari kuacha kuitumia dawa hii bila kuzungumza kwanza na madaktari wao wa karibu’’ anasema Dr. Janet Woodcock wa mamlaka ya dawa na chakula Marekani – FDA.

Kama unapenda kujuwa mamlaka hii imefikia wapi na uchunguzi huu wapigie simu kwenye namba yao 1-888-463-6332.

Soma hii pia > Usizidharau ishara hizi 8 za mwanzo za kisukari

Je unaumwa kisukari aina ya pili na unahitaji dawa ya asili kwa ajili hiyo? kama ndiyo niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Mjulishe pia rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Dawa ya kisukari inashukiwa kusababisha saratani Click To Tweet

Tafadhari SHARE post hii na wengine uwapendao

Imesomwa mara 6

Let's block ads! (Why?)

Mambo 9 ya kushangaza na usiyoyajuwa kuhusu mbegu za kiume

Mambo 9 ya kushangaza na usiyoyajuwa kuhusu mbegu za kiume

Una elimu au uelewa wa kiasi gani kuhusu mbegu za kiume yaani shahawa?

Kuna uwezekano mkubwa hujawahi kuwa na muda wowote wa kupeleleza au kujifunza mengi kuhusu mbegu zako.

Kama hujawahi kupata shida kutungisha mimba unaweza usiwaze lolote kuhusu mbegu zako na ukaendelea kuzichukulia poa kila siku.

Soma hii pia > Vidonda vya tumbo husababisha upungufu wa nguvu za kiume

Mambo 9 ya kushangaza na usiyoyajuwa kuhusu mbegu za kiume

Mambo 9 ya kushangaza na usiyoyajuwa kuhusu mbegu za kiume

1. Ni nyingi sana

Bao moja linakuwa na mbegu karibu milioni 200 na lina ujazo wa karibu nusu kijiko cha chai.

Kama utazipanga kwa kufuatana mbegu za mshindo mmoja (bao) zinaweza kuchukuwa umbali wa kilomita 9.

Kitu kingine cha kweli na cha kushangaza kuhusu wingi wa mbegu za kiume ni kuwa zimekuwa zikipunguwa kwa wanaume wa viazi vyote mwaka hadi mwaka.

Yaani kama mwanaume wa mwaka 1990 alikuwa na jumla ya mbegu milioni 500 kwa mfano basi kuna uwezekano mkubwa mwanaume wa mwaka 2020 akawa na jumla ya mbegu milioni 450.

Tafiti za hivi karibuni zinataja mambo ya mabadiliko ya mazingira na tabia ya mwanadamu ndiyo vinahusika na kushuka kwa karibu asilimia 50 ya ujazo, wingi na ubora wa mbegu za wanaume katika kipindi cha miongo minne iliyopita.

2. Zina safari ndefu zinapoingia kwa mwanamke

Mbegu za kiume zina safari ndefu sana zinapoingia katika via vya uzazi vya mwanamke.

Kwanza kabisa huingia kwenye mlango wa kizazi (cervix), kasha kwenye mji wa mimba (uterus), na kisha husafiri kupitia mirija ya mayai (fallopian tubes) mpaka kulifikia yai la mwanamke linalosubiri kurutubishwa.

Mbegu chache sana huendelea kuwa hai katika safari hiyo ndefu, nyingi hufa njiani na nyingine huamua kulala au kupumzika njiani na inahitajika mbegu 1 tu katika mbegu milioni 200 anazokojoa mwanaume ili kurutubisha yai na kutunga mimba.

Kuna wakati huwa nakutana na wanaume hata wanawake ninapochat nao WhatsApp huniambia mara tu wakikojoa huona mbegu zao zikitoka nje ya uke kwahiyo wana wasiwasi huenda ndiyo sababu hawapati mtoto!

Kwa faida ya wengi niseme hapa kuwa mbegu za mwanaume hazina sehemu ya kuhifadhiwa katika uke wa mwanamke.

Kama hazijatunga mimba ambapo ni mbegu 1 tu inahitajika katika hizo milioni 200 nyingine zote lazima zitoke

Ndiyo maana ukishiriki tendo la ndoa utaona mkimaliza mwanamke lazima ataenda bafuni kujisafisha sababu lazima zitolewe nje.

Hata kama hataenda bafuni maalumu kwa ajili hiyo, bado wakati wowote hizo mbegu lazima zimtoke anapooga na kujisafisha nk

3. Zinaweza kuendelea kuwa hai kipindi kirefu

Baada ya mbegu kutoka kwa mwanaume akishakuwa amefika kileleni yaani amepiga bao na kuingia katika via vya uzazi vya mwanamke zinaweza kuendelea kuwa hai kwa siku mbili mpaka tano bado zikiwa hai.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa mbegu za kiume zinaweza kuendelea kupata viinilishe vyote inavyovihitaji ili kuwa hai zikiwa katika via vya uzazi vya mwanamke.

4. Zina mbio vibaya mno

Wakati mbegu zinatoka katika uume wa mwanaume huwa na spidi kubwa ambayo haiwezi kuelezewa.

Kabla hata ya mwanaume hajafika kileleni yaani hajakojoa au kabla hajapiga bao kiasi fulani cha mbegu (maji maji) huanza kutoka kwenye tundu la uume wake na hili linaweza kutokea mapema tu wakati wa mazungumzo wawili wakiwa chumbani.

Wanaume hawana udhibiti wa hili na wengi hawajuwi muda gani linaweza kutokea.

Hali inaweza kuwa ya kuonekana zaidi hasa kama mwanaume huyo si mtu wa kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara.

Bado wataalamu hawana hitimisho moja kwamba maji maji hayo ya mwanzo yanaweza kuwa na mbegu zinazoweza kutungisha ujauzito.

Kazi kubwa ya maji maji hayo ni kusaidia kulainisha mbegu zitakazokuwa zinatoka wakati wa tendo na kupunguza hali ya uasidi katika mrija unaopitisha mbegu kwenye uume (urethra).

Hii ndiyo sababu mbinu ya kuzuia ujauzito kwa kumwaga nje ina walakini mkubwa na usiitegemee sana katika kuzuia ujauzito kwani kuna uwezekano mwanaume akakumwagia kiasi fulani cha mbegu hata kabla hajafika mshindo wenyewe.

5. Kwa kawaida lazima zitoke

Kuna jambo huwa naulizwa na vijana wa kiume hata baadhi ya wanaume watu wazima kwamba wanapokojoa mkojo wa kawaida au wanapopata choo kikubwa wanaona mbegu zao zikitoka pia na wengi wanashikwa na butwaa na kudhani ni ugonjwa.

Kutokwa na mbegu wakati unakojoa mkojo wa kawaida au unapojisaidia haja kubwa ni ishara unakaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa.

Basi ni hivyo tu siyo ugonjwa.

Bali ikiwa mbegu hizo zinapotoka zinaambatana na maumivu au damu au zina harufu mbaya muone daktari haraka kwa uchunguzi zaidi.

Mwanaume anaweza kutokwa pia na mbegu akiwa usingizini bila hata yeye kujuwa, anaweza kutokewa na ndoto akihisi yupo na mwanamke anashiriki tendo la ndoa na mbegu humtoka kisha lazima ashtuke usingizini na tayari ataona mbegu zimejaa kwenye nguo yake ya ndani.

Mwanaume anaweza pia kutokwa na mbegu akiangalia picha au video za X.

6. Hazipendi joto

Mbegu za kiume yaani shahawa hazipendi joto.

Zinapenda mazingira ya joto yasiyozidi sentigredi 13.

Mji wa Dar Es Salaam mara nyingi una joto la kati ya 20 mpaka 30.

Mwili wa mwanaume unao mfumo wake wa ndani unaosaidia hizi mbegu zisipatwe na joto jingi.

Mwili wa mwanaume una viyoyozi (AC) karibu na korodani ambavyo hutumika kuondoa joto kwenye mfuko wa mbegu za mwanaume.

Hivi viyoyozi (veins) hufanya kazi kama transfoma ya umeme. Joto linapokuwa juu sana hushusha na linapokuwa chini sana hulipandisha ili kubaki katika hali ya sentigredi 13.

Mwanaume pia unatakiwa kuepuka mazingira ya joto sana hasa kutovaa chupi zinazobana sana na ikiwezekana usivae chupi vaa tu suruali peke yake ili kuziwezesha mbegu zako zisiingiliwe na joto na kuziwezesha zibaki na afya.

Mwanaume pia unashauriwa ukikaa au kusimama usipende kubana miguu yako ili kuzipa mbegu zako hewa ya kutosha wakati wote.

7. Zinaweza kuhifadhiwa katika friza

Siyo ice cream tu ndiyo unaweza kuzihifadhi katika friza

Kama unaumwa au una ugonjwa fulani hasa saratani au unahisi miaka kadhaa ijayo mbegu zako zaweza kuwa hazina ubora tena kama ulizo nazo leo, unaweza kuzifadhi katika friza kwa muda upendao wewe na siku ukizihitaji unazichukuwa na kumwekea mwanamke

Sasa tuelewane zipo friza maalumu huko hospitalini au maabara zinazoweza kutunza mbegu hizo bila mwisho (indefinitely) zikihifadhiwa kwenye joto la nyuzi joto -196 hivyo usije ukapiga punyeto sasa na kuzihifadhi wewe kama wewe!

Soma hii pia > Jinsi ya kuacha punyeto

8. Huwa hazifi haraka

Ni uongo kuamini kwamba mbegu za kiume yaani shahawa au manii hufariki mara tu zinapokutana na oksijeni (yaani mara tu zikitoka nje ya mwili wa mwanaume).

Mbegu za mwanaume hufariki zinapokosa maji na haziwezi kurudi tena kuwa hai zinapokuwa hazina umajimaji tena yaani zikikauka.

Maji ni uhai ndugu.

9. Zinapenda kupetiwapetiwa

Mwanaume anao uwezo wa kuchukuwa baadhi ya hatua katika kuishi kwake ili kuziongezea afya mbegu zake.

Mbegu hizi zinapenda kupetiwapetiwa au zinapenda kujariwa, kwa lugha nyepesi ni kuwa zinapenda uwe unazijali.

Kuna vitu ukivifanya vinaweza kusaidia kuongeza ubora wa mbegu zako ikiwemo wingi wake na afya yake kwa ujumla, vitu hivyo ni pamoja na kuacha vilevi, kupunguza msongo wa mawazo (stress), kudhibiti uzito wako, kupata usingizi wa kutosha, kukaa mbali na joto jingi, kukaa mbali na viwanda, kula chakula sahihi, kufanya mazoezi ya viungo nk

Soma hii pia > Vyakula vitano vinavyoua nguvu zako za kiume bila wewe kujuwa

Ikiwa una tatizo lolote kuhusiana na mbegu zako labda zimekuwa chache, hazina afya na uwezo wa kutungisha mimba nk tuwasiliane WhatsApp +255714800175

Mjulishe pia rafiki yako kwenye Twitter naye asome post hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Mambo 9 ya kushangaza na usiyoyajuwa kuhusu mbegu za kiume Click To Tweet

Tafadhali SHARE post hii na wengine uwapendao

Imesomwa mara 61

Let's block ads! (Why?)

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...