Translate

Jumamosi, 1 Desemba 2018

Msimamo kwa jamii zinazomuasi Allaah

Swali: Sisi tunaishi na watu ambao wanatumbukia katika mambo ambayo yanamkasirisha Allaah na Mtume wake. Kama kama ambao wanachukulia wepesi jambo la swalah, wananyoa ndevu zao, wanaume wanaovaa mavazi marefu yenye kuvuka kongo mbili za miguu na maasi mengine ya waziwazi. Tunatakiwa kuwa na msimamo gani kwao?

Jibu: Ambaye anachukulia wepesi jambo la swalah ni mbaya zaidi kuliko ambaye ananyoa ndevu zake. Kunyoa ndevu ni maasi na ni haramu. Hapana shaka juu ya hilo. Lakini kuchukulia wepesi jambo la swalah ni khatari zaidi. Huyu akiendelea kuchukulia wepesi jambo la swalah basi usitangamane naye na wala usikae naye baada ya kumnasihi. Jitenge naye mbali.

Kuhusu ambaye ananyoa ndevu zake mbainishie Hadiyth zilizopokelewa juu ya jambo hili na mnasihi. Pengine Allaah akamwongoza. Asipokubali jitenge naye mbali. Kwa sababu ukitangamana naye ni kama kwamba umeridhia yale anayofanya.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kuhusu wana wa israaiyl ya kwamba mmoja wao alikuwa akikutana na ndugu yake katika maasi ambapo anamnasihi, kisha anakutana naye kwa mara ya pili akamnasihi, kisha anakutana naye kwa mara ya tatu akamnyamazia na wala hilo halimzuii kula pamoja naye, kukaa naye na kunywa naye. Allaah alipoona hali hiyo akazikutanisha nyoyo zao na akawalaani kupitia ulimi wa Mitume wao. Amesema (Ta´ala):

لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ

“Wamelaaniwa wale waliokufuru katika wana wa israaiyl kwa ulimi wa Daawuud na ‘Iysaa mwana wa Maryam. Hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakivuka mipaka. Walikuwa hawakatazani maovu waliyofanya.” (05:77-78)

Mtenda maasi akiendelea juu ya maasi yake na asipokee nasaha kutoka kwako, basi usiikae naye. Bali jitenge naye mbali. Usiikae naye isipokuwa wakati wa dharurah na wakati huohuo uchukie yale anayofanya. Ama kukiwa hakuna dharurah yoyote jiepushe naye mbali.



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2E7RV95
via IFTTT

Anakufuru anayewachukia na kuwatukana Malaika?

Swali: Je, kuwatukana Malaika ni kufuru inayomtoa mtu nje ya Uislamu?

Jibu: Ndio. Anayemtukana mmoja katika Malaika au mmoja katika Mitume kunahesabika ni kuritadi kutoka katika Uislamu. Nguzo za imani ni kumuamini Allaah, Malaika wake, Vitabu vyake, Mitume wake, siku ya Mwisho na kuamini Qadaar kheri na shari yake. Hizi ndio nguzo za imani. Katika hayo kunaingia vilevile kuwaamini Malaika (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Anayewatukana anakuwa mwenye kuritadi. Amesema (Ta´ala):

قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ

“Sema: “Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha kwenye moyo wako kwa idhini ya Allaah inayosadikisha yaliyo kabla yake.” (02:97)

Mpaka alipofikia kusema:

مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ

“Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake na Mtume Wake na Jibriyl na Miykaala, basi hakika Allaah ni adui kwa makafiri.” (02:98)

Amewaita kuwa ni makafiri. Ni dalili inayofahamisha kwamba anayewachukia Malaika au baadhi yao ni kafiri. Mayahudi wanamchukia Jibriyl (´alayhis-Salaam) na wanasema kwamba Jibiriyl ndiye adui wao. Allaah akawajibu namna hii na anawahukumu ukafiri kwa sababu ya kumchukia kwao Jibriyl (´alayhis-Swalaatu was-Salaam).

Wapo pia wanaosema kuwa Jibiryl alifanya khiyana ya amana na kwamba utume ulikuwa unatakiwa kwenda kwa ´Aliy na kwamba eti Jibriyl alifanya khiyana na badala yake akampa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanasema kwamba mwaminifu alifanya khiyana. Huku ni kumkufuru Allaah (´Azza wa Jall).



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2zAygKT
via IFTTT

New video by GROUP FAIDIKA NA MAWAIDHA on YouTube

*SAMEHE😊 UPATE KUSAMEHEWA👍🏽 👆🏼*



View on YouTube

New video by GROUP FAIDIKA NA MAWAIDHA on YouTube

Ni ipi hukmu ya mwanamke aliyeolewa huku tayari ana ujauzito* *Wa huyo mume anaemuoa*❓
Ni ipi hukmu ya mwanamke aliyeolewa huku tayari ana ujauzito* *Wa huyo mume anaemuoa*❓


View on YouTube

New video by GROUP FAIDIKA NA MAWAIDHA on YouTube

Ikiwa umezni na mwanamke akapata mimba akakwambia kua mtoto ni wako na wew huna uhakika wa huyo mtot
Ikiwa umezni na mwanamke akapata mimba akakwambia kua mtoto ni wako na wew huna uhakika wa huyo mtoto kama kweli ni wako au la siwako jeee ukimuhudumia mtoto huyo utapata dhambi au ukiacha kumuhudumia utapata dhambi sababu kama ulienda kutafuta vpimo vya damu na vikasibitisha kua ni wa kwako jeee nafaa nimchukue nikae nae mwenyewe sitopata dhambi*❓


View on YouTube

New video by GROUP FAIDIKA NA MAWAIDHA on YouTube

Je nini hukumu ya wanandoa kutokukutana kindoa kwa muda zaidi ya miezi saba au zaidi bila sababu yey
Je nini hukumu ya wanandoa kutokukutana kindoa kwa muda zaidi ya miezi saba au zaidi bila sababu yeyote ya maana*❓.


View on YouTube

New video by GROUP FAIDIKA NA MAWAIDHA on YouTube

Mume ameowa siku ya ijumaa,na akadhamiria mkewe atamuingilia siku ya J/pili ,ila kwa qadri za allah
Mume ameowa siku ya ijumaa,na akadhamiria mkewe atamuingilia siku ya J/pili ,ila kwa qadri za allah yule mume akafariki siku ya jumamosi na hali ya kuwa mume hajamaliza mahari, Na wala hajamuingilia mkewe hata mara moja,.suali Je.?(1) Mke huyo IPO haja amaliziwe mahari yake,au yeye ndio anapaswa arejeshe mahari ya mwanaume.?* *(2) Je.? mke huyo atalazmika kukaa EDA.? Na ni EDA gan hiyo itakua.?(3) Je.? mke huyo atapata Urithi kwa marehem.?*


View on YouTube

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...