Translate

Alhamisi, 8 Oktoba 2020

17-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Kutabarruk (Kutafuta Kupata Baraka)

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم

 

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

 

17 -Kutabarruk (Kutafuta Kupata Baraka)

Alhidaaya.com

 

 

 

Maana ya barakah ni wingi wa khayr na kuthibitika kwake. 

 

 

Tabarruk ni aina mbili; iliyothibiti ki-shariy’ah kwa kutajwa kitu fulani kina baraka kama Anavyosema Allaah (Subahaanahu wa Ta’aalaa) kuhusu Qur-aan:

 

كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٩﴾

Kitabu Tumekiteremsha kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) chenye Baraka, ili wapate kuzingatia kwa makini Aayaat zake, na ili wapate kukumbuka wenye akili. [Swaad: 29]

 

 

Mfano wa kutaka baraka za Kitabu hiki (Qur-aan) ni kama vile alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ الله عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ قَرَأَ حَرْفًا مِنْ كِتَابِ اللَّهِ فَلَهُ بِهِ حَسَنَةٌ وَالْحَسَنَةُ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا لَا أَقُولُ الم حَرْفٌ وَلَكِنْ أَلِفٌ حَرْفٌ وَلَامٌ حَرْفٌ وَمِيمٌ حَرْفٌ))

Imetoka kwa 'Abdullaahi bin Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, ((Atakayesoma herufi moja katika Kitabu cha Allaah atapata hasanah (jema) moja, na kila hasanah moja ni sawa na thawabu kumi, wala sisemi 'Alif-Laam-Miym' ni herufi moja, bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi moja na Miymni herufi moja)) [At-Tirmidhiy (2910) na ameisahihisha Shaykh Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (3327), Swahiyh Al-Jaami’ (6469)]

 

 

Tabarruk inagawanyika sehemu mbili:

 

 

1-Iliyothibiti katika Shariy’ah ambayo inatokana na Muislamu kufanya juhudi katika ‘amali fulani ili achume thawabu nyingi na apate khayr nyingi kabisa. Mifano ni michache ni:

 

i) Kusoma Qur-aan na kufuata hukumu na maamrisho yake kama ilivyothibiti katika Qur-aan na Sunnah (Aayah na Hadiyth zilizotangulia kutajwa juu). Na pia Anasema Allaah (Subhanaahu wa Ta’aalaa):

 

إنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّـهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ ﴿٢٩﴾

Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa kutokana na yale Tuliyowaruzuku kwa siri na dhahiri wanataraji tijara isiyoteketea.

 

 

لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٣٠﴾

Ili (Allaah) Awalipe ujira wao timilifu, na Awazidishie kutokana na fadhila Zake, hakika Yeye ni Mwingi wa kughufuria, Mwingi wa kupokea shukurani. [Faatwir: 29-30]

 

 

 

ii) Kuomba maghfirah kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ambayo matokeo yake ni kujipatia khayr nyingi kama ilivyo tajwa kuhusu kauli ya Nabiy Nuwh (عليه السلام) alipowalingania watu wake:

 

 

اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا﴿١٠﴾

Nikasema: “Ombeni maghfirah kwa Rabb wenu; hakika Yeye ni Mwingi mno wa kughufuria.

 

يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا﴿١١﴾

 “Atakutumieni mvua tele ya kuendelea.”

وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا﴿١٢﴾

 “Na Atakuongezeeni mali na wana, na Atakupeni mabustani na Atakupeni mito.” [Nuwh: 10-12]

 

 

 

Na mifano michache miongoni mwa mingineyo katika Sunnah:

 

 

i) Kuswali katika Masjid Al-Haraam, Makkah ambayo Swalaah humo thawabu zake ni maradufu.   

 

عَنْ جَابِرٍ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((صَلَاةٌ فِي مَسْجِدِي  أَفْضَلُ مِنْ أَلْفِ صَلَاةٍ فِيمَا سِوَاهُ إِلَّا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ، وَصَلَاةٌ فِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ أَفْضَلُ مِنْ مِائَةِ أَلْفِ صَلَاةٍ فِيمَا سِوَاهُ)) رواه أحمد وابن ماجه

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swalaah katika Msikiti wangu ni bora kuliko Swalaah elfu kwengineko isipokuwa Al-Masjid Al-Haraam. Na Swalaah katika Al-Masjid Al-Haraam ni bora kuliko Swalaah elfu mia (laki moja) kwengineko)) [Ahmad, Ibn Maajah na imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy; Swahiyh Ibn Maajah (1163), Swahiyh Al-Jaami’ (3838)]

 

Pia:

 

 عن أبي هريرة رضي الله عنه ان رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((من قال : لا إلهَ إلَّا اللهُ وحدَه لا شريكَ له، له المُلْكُ وله الحمْدُ، وهو على كلِّ شيءٍ قديرٌ . في يومٍ مائةَ مرَّةٍ ، كانت له عِدلُ عشرِ رِقابٍ ، وكُتِبت له مائةُ حسنةٍ، ومُحِيَتْ عنه مائةُ سيِّئةٍ ، وكانت له حِرزًا من الشَّيطانِ يومَه ذلك حتَّى يُمسيَ ، ولم يأتِ أحدٌ بأفضلَ ممَّا جاء به إلَّا رجلٌ عمِل أكثرَ منه))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ’anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  ((Atakayesema: Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr [Hapana muabudiwa wa haki ila ni Allaah  Peke Yake, hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza], mara mia kwa siku, basi atapata sawa na thawabu za kuwaacha huru watumwa kumi na ataandikiwa mema mia moja na atafutiwa makosa mia moja, na atakuwa na kinga ya shaytwaan kwa siku hiyo yote hadi jioni na hatakuwa mtu yeyote mbora kumshinda ila yule aliyefanya zaidi yake)) [Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h, (4/95) [3293], Muslim (4/2071) [2691].

  

Na pia:

 

عن عقبة بن عامر رضي الله عنه أن خرج رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليهِ وسلَّمَ ونحنُ في الصُفَّةِ. فقال: ((أيكم يحبُّ أن يغدو كلَّ يومٍ إلى بطحانَ أو إلى العقيقِ فيأتي منهُ بناقتيْنِ كوماويْنِ، في غيرِ إثمٍ ولا قطعِ رحمٍ؟)) فقلنا: يا رسولَ اللهِ  نحبُّ ذلك. قال: ((أفلا يغدو أحدكم إلى المسجدِ فيُعَلِّمَ أو يقرأَ آيتيْنِ من كتابِ اللهِ عزَّ وجلَّ خيرٌ لهُ من ناقتيْنِ. وثلاثٌ خيرٌ لهُ من ثلاثٍ  وأربعٌ خيرٌ لهُ من أربعٍ. ومن أعدادهنَّ من الإبلِ))

 

Imetoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (Radhwiya Allahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alitujia wakati tulikuwa katika Swuffah akauliza, kuna yeyote miongoni mwenu anayependa kwenda soko la Butw-haan au Al-'Aqiyq na akapata humo ngamia wawili (wa thamani kabisa wa kike) bila ya kutenda dhambi au kukata undugu? Tukajibu: “Ee Rasuli wa Allaah! Tunapenda hivyo.” Akasema: ((Basi aende mmoja wenu Msikitini akajifunze au asome Aayah mbili katika Kitabu cha Allaah basi akifanya hivyo ni bora kuliko ngamia (wa thamani kabisa wa kike). Na Aayah tatu ni bora kuliko ngamia watatu, na Aayah nne ni bora kuliko ngamia wanne, na mfano wa hivyo hivyo wa Aayah kwa ngamia)) [Muslim]

 

 

2- Tabarruk iliyoharamishwa ambayo huwa shirki au bid’ah

 

Kuitakidi kwamba kiumbe fulani ana baraka na kumuomba kiumbe huyo khayr ambazo hana uwezo nazo isipokuwa Allaah, huwa ni shirki kwa sababu ni Allaah (Subhaanahu Ta’aalaa) Pekee Mwenye kutoka baraka kama alivyothibitisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

عن جابر بن عبد الله رضي الله عنه: رأيْتُني مع النبيِّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم وقدْ حَضَرَتِ العَصْرُ، وليس معَنا ماءٌ غيرَ فَضلَةٍ، فجُعِلَ في إناءٍ فأُتيَ النبيُّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم بهِ، فأدْخَلَ يدَهُ فيه وفَرَّجَ أصابِعَهُ، ثم قال: ((حيَّ علَى أهلِ الوضوءِ، البَرَكَةُ مِن اللَّهِ)) فلقدْ رأيتُ الماءَ يَتَفَجَّرُ مِن بينِ أصابعِهِ، فتَوَضَّأ الناسُ وشَرِبوا، فجَعَلْتُ لا آلُو ما جَعَلتُ في بطْني منه، فعَلِمتُ أنَّه بَرَكَةٌ . قلتُ لجابرٍ :كَم كُنتُم يومَئِذٍ ؟ قال: ألْفًا وأربَعمِائةٍ

Imepokewa kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah akisema: “Nilikuwa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na muda wa kuswali Swalaah ya Al-‘Aswr ukafika. Tulikuwa hatuna maji isipokuwa maji kidogo tu ambayo yalikuwa ndani ya chombo ambayo yaliletwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Basi aliweka mkono wake ndani ya maji hayo na kutandaza vidole vyake na huku akisema: ((Njooni Haraka watu wote ambao wanataka kutawadha Hii ni baraka kutoka kwa Allaah)). Nikaona maji yakibubujika kutoka katika vidole vyake. Hivyo watu walitawadha na wengine wakawa wanakunywa maji hayo na mie nilitaka kunywa maji mengi kupita kiasi (kwa sababu nilijua kuwa ilikuwa ni baraka). Mpokeaji wa Hadiyth hii kutoka kwa Jaabir alisema kuwa nilimuuliza Jaabir Je, mlikuwa watu wangapi wakati huo? Akajibu, “Tulikuwa watu elfu moja na mia nne.” [Swahiyh Al-Bukhaariy(7/543) Swahiyh Muslim (4/779)]

 

 

Aghlabu shirki na bid’ah zinazotendwa katika kutabarruk:

 

 

i-Kufanya ‘ibaadah kadhaa kama kuomba du’aa na kuswali kuelekea kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kuitakidi kuwa du’aa na Swalaah hiyo ni ya kutakabaliwa au inamridhisha Allaah (Subhanaahu wa Ta’aalaa):

 

Amesema Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: “‘Ulamaa wengi wamewafikiana kwamba huu ni munkar uliozushwa na ni haraam, wala ma-Imaam wa Dini hawakutofautiana kwa hili.” [Ar-Radd ‘Alal-Bakriy, uk. 56]

 

Na akasema kuhusu du’aa mbele ya kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Wala asisimame mtu kujiombea kwani hiyo ni bid’ah, wala hakutokea Swahaabah akisimama kaburini kujiombea bali walikuwa wakielekea Qiblah na wakiomba katika Masjid yake.” [Majmuw’ah Ar-Rasaail Al-Kubraa li Ibn Taymiyyah (2/408)], na Iqtidhwaa Swiraatw Al-Mustaqiym (2/681)]

 

 

ii- Kugusa kaburi na kuta za kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au Al-Ka’bah na kujipangusia mwilini, au kubusu kwa kutegemea kupata khayr na barakah.

Lililothibiti kubusiwa ni Al-Hajar Al-Aswad pekee lilioko katika Al-Ka’bah kwa dalili:

((إِنَّ مَسْحَ الْحَجَرِ الأَسْوَدِ ، والركنَ اليمانيِّ، يَحُطَّانِ الخطايا حطًّا))

((Kugusa Al-Hajar Al-As-wad na Ar-Rukn al-Yamaaniy ni kufutiwa madhambi))  [Hadiyth ya Ibn ‘Umar; Swahiyh Al-Jaami’ (2194)]

 

Na ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alipolibusu alisema:

 

 "إني أَعْلَمُ أَنَّكَ حَجَرٌ لا تَضُرُّ ولا تَنْفَعُ، وَلَوْلا أَنِّي رأيت النبي صلى الله عليه وسلم يُقَبِّلُكَ ما قَبَّلْتُكَ" - البخاري و مسلم

“Hakika mimi najua kwamba wewe ni jiwe usiloweza kudhuru wala kunufaisha, na ingelikuwa sikumuona Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anakubusu basi nami nisingelikubsu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

iii-Kutabarruk sehemu sehemu ambazo zimetajwa katika Siyrah ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Imedhihirika watu wengi kukosea wanapofika Makkah au Madiynah kutekeleza ‘Umrah kupendelea kutembelea sehemu hizo wakiitakidi kuwa zina baraka na wengine hufika kujikalifisha kupanda majabali kama Jabal Ath-Thawr, Ghaar Hiraa, Jabali la ‘Arafah na sehemu nyinginezo.

Haikuthibiti kuwa Swahaabah (Radhwiya Allaahu ‘anhum) walitabarruk na chochote au popote alipopita au alipokaa kitako Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya kuwa wao walikuwa na mapenzi makubwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wenye kutilia hima zaidi ya kutekeleza Sunnah.

 

Shaykh Al-Islaam amesema: “Kina Abu Bakr na ‘Umar na ‘Uthmaan na wengineo miongoni mwa Al-Muhaajiriyn na Answaar walikuwa wakisafiri kutoka Madiynah mpaka Makkah kutekeleza Hajj na ‘Umrah wala haikupokelewa kutoka kwao kuwa mmoja wao alikuwa akitafuta sehemu alizokuwa akiswali Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salalm). Basi ni dhahiri kwamba ingekuwa ni jambo la kupendekezwa wangekuwa wao ni wa kwanza kutangulia kufanya, kwani wao ni wajuzi zaidi wa Sunnah zake na wenye kufuata mno kuliko wengineo.” [Iqtidhwaa Swiraatw Al-Mustaqiym (2/748)]

 

Katika moja ya msafara wake kwenda vitani Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Swahaba zake walipitia sehemu wakataka kutafuta baraka kwa kuweka silaha zao katika mti, lakini aliwakataza. Na hii ni dalili pia haipasi kutabarruk kwa miti na vitu kama hivyo.

      

عن أَبِي وَاقٍد اللَّيْثِيِّ (رضي الله عنه) قَالَ: خَرَجْنَا مَعَ النَّبِيِّ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ) إِلَى حُنَيْنٍ وَنَحْنُ حُدَثَاءُ عَهْدٍ بِكُفْرٍ، وَلِلِمُشْرِكِينَ سِدْرَةٌ، يَعْكُفُونَ عِنْدَهَا وَيُنَوِّطُونَ بِهَا أَسْلِحَتَهُمْ، يُقَالَ لَهَا ذَاتُ أَنْوَاطٍ، فَمَرَرْنَا بِسِدْرَةٍ فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللهِ اجْعَلْ لَنَا ذَاتَ أَنْوَاطٍ كَمَا لَهُمْ ذَاتُ أَنْوَاط. فَقَالَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم):َ((الله أكبر! هَذَا كَمَا قَالَ قَوْمُ مُوسَى "اجْعَلْ لَنَا إِلَهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ" وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَتَرْكَبُنَّ سُنَّةَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ))

Imepokewa kutoka kwa Abuu Waaqid Al-Laythiyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Tulitoka pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwenda (vitani) Hunayn nasi ndio kwanza tumetoka katika ukafiri, na washirikina walikuwa na mkunazi wanaufanyia ‘ibaadah na walikuwa wakitundika silaha zao (kupata baraka). Wakiuita ‘Dhaatu Anwaatw’. Tukapita mbele ya mkunazi tukasema: “Ee Rasuli wa Allaah, tufanyie nasi Dhaata Anwaatw kama walivyokuwa nao (makafiri) Dhaatu Anwaatw.” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Allaahu Akbar!  (Allaah ni Mkubwa!) Hivi ni kama walivyosema watu wa Muwsa “Tufanyie nasi muabudiwa kama walivyokuwa nao muabudiwa.” Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, mtafuata nyendo za walio kabla yenu [za ujahili na kufru].)) [At-Tirmidhiy; Swahiyh At-Tirmidhiy (2180)]

 

iv- Kutabarruk kwa Msahafu:

 

Shaykh Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amejibu Swali: “Kuweka Msahafu katika gari kwa ajili ya kujikinga na khatari au kujikinga na jicho ni bid’ah, kwani Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) hawakuwa wakibeba Misahafu walipokuwa wakipanda ngamia wao kwa ajili ya kujikinga na khatari au jicho baya.” [Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb (2/4)]

 

 

v-Kutabarruk kwa watu kama mashekhe na wanaoitwa masharifu, kwa kuwagusa au kupangusa nguo zao au kuvaa nguzo zao au kunywa kinywaji walichoanza kunywa, au maji waliyoyatemea mate n.k. kwa kutegemea au kuitakidi vitu hivyo vina baraka.

 

Haikuthibiti kutoka kwa Swahaba kwamba walitabarruk kwa Swahaabah watukufu, kama Abu Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) wala wengineo waliobashiriwa Jannah wala watu wa nyumba ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa hiyo kufanya hivyo si jambo lenye kukubalika katika Shariy’ah.

 

 

 

 

 



55-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Aliwaimamisha Manabii Wote Katika Swalaah Siku Ya Israa Wal Miaraaj

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

55-Aliwaimamisha Manabii Wote Katika Swalaah Siku Ya Israa Wal Miaraaj

 

Alhidaaya.com

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofika Masjid Al-Aqswaa aliwasalisha Manabii wote wengine nyuma yake. Hadiyth ndefu yenye maelezo yafuatayo:

 

فلمَّا أَتَى النبيُّ صلَّى اللهُ عليهِ وسلَّمَ المسجدَ الأَقْصَى قامَ يصلِّي ، فالتَفَتَ ثُمَّ التَفَتَ فإِذَا النبيُّونَ أجمعونَ يُصَلُّونَ مَعَهُ . فلمَّا انصرفَ جِيءَ بِقَدَحَيْنِ ، أحدُهُما عن اليَمِينِ والآخَرُ عَنِ الشِّمالِ ، في أَحَدِهما لَبَنٌ وفي الآخَرِ عَسَلٌ ، فأخذَ اللَّبَنَ فَشربَ مِنْهُ ، فقال الذي كان مَعَهُ القَدَحُ : أَصَبْتَ الفِطْرَةَ

Pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofika Masjid Al-Aqwswaa alisimama kuswali, akageuka kisha akageuka, tahamaki Manabii wote walikuweko kuswali naye.  Alipomaliza akaletewa vyombo viwili, kimoja kuliani na kingine kushotoni. Kimojawapo kina maziwa na kingine kina asali. Akachukua maziwa akanywa, basi aliyekuwa naye (Jibriyl) alimwamba “Umeongozwa katika fitwrah.”  [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abaaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ameikhariji Ahmad Isnaad yake ni Swahiyh, na Imaam Ibn Kathiyr katika Tafsiyr yake]

 

 



11-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Zuhd Yake: Amefariki Hakuacha Mali

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

11-Zuhd Yake: Amefariki Hakuacha Mali

 

Alhidaaya.com

 

 

وعن عمرو بن الحارث أخي جُوَيْرِيّة بنتِ الحارِث أُمِّ المُؤْمِنِينَ ، رضي الله عنهما ، قَالَ : مَا تَرَكَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم عِنْدَ مَوْتِهِ دِيناراً ، وَلاَ دِرْهَماً ، وَلاَ عَبْداً ، وَلاَ أَمَةً ، وَلاَ شَيْئاً إِلاَّ بَغْلَتَهُ الْبَيضَاءَ الَّتي كَانَ يَرْكَبُهَا ، وَسِلاَحَهُ ، وَأرْضاً جَعَلَهَا لاِبْنِ السَّبِيلِ صَدَقَةً . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa 'Amri bin Al-Haarith, kaka yake Juwayriyyah bint Al-Haarith, Mama wa Waumini ambaye amesema: "Hakuacha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati wa kufariki hata dinari moja wala dirhamu wala mjakazi wala kijakazi wala kitu kingine chochote isipokuwa nyumbu wake mweupe aliyekuwa akipanda na silaha zake na ardhi aliyoiacha kama sadaqah kwa wasafiri." [Al-Bukhaariy]

 

Na alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:

 

 لَا نُورَثُ، مَا تَرَكْنَاهُ صَدَقَةٌ

haturithiwi na tunachoacha ni sadaka. [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

وقال عمرو بن الحارث رضي الله عنه : "مَا تَرَكَ النَّبِىُّ صلى الله عليه وسلم إِلاَّ سِلاَحَهُ وَبَغْلَتَهُ الْبَيْضَاءَ ، وَأَرْضًا تَرَكَهَا صَدَقَةً" رواه البخاري  

‘Amr bin Al-Haarith (Radhwiya Allaahu 'anhu)  amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam hakuacha chochote (baada ya kifo chake) isipokuwa ngao yake, nyumbu wake mweupe, na kipande cha ardhi ambacho alikiacha kwa ajili ya  sadaka.” [Al-Bukhaariy]

 

 

 



Jumapili, 4 Oktoba 2020

Dawa mbadala 11 zinazotibu kufunga choo au choo kigumu

DAWA MBADALA 11 ZINAZOTIBU KUFUNGA CHOO AU CHOO KIGUMU

Tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu ni jambo tunalolikwepa kwenye mazungumzo yetu ya kila siku.

Hata hivyo ni tatizo kubwa katika jamii na mbaya zaidi wengi hawajuwi madhara yake ni nini ya kuendelea kulivumilia tatizo hili.

Kupata choo kigumu au kufunga choo ni ishara ya tatizo lingine baya zaidi mwilini.

Kama kuna jambo unapaswa uliepuke kwa nguvu zote basi ni hili. Kwa afya bora kabisa hakikisha unapata choo kila siku mara 2 hata mara 3.

Choo kilaini siyo kigumu na chenye maumivu.

Wakati mwingine utakapopata tatizo hili naomba usiwe na aibu kulisema wazi hata kwa boss wako ili upate matibabu kwa haraka.

Kufunga choo au kupata choo kigumu ndiyo CHANZO KIKUU CHA UGONJWA WA BAWASIRI kwa waTanzania wengi na hii inachangiwa kwa sehemu kubwa kwa kula ugali wa sembe na kutokunywa maji mengi kila siku.

Pamoja na hayo, hakuna ugonjwa rahisi kutibika kama huu ikiwa utaamua kushughulisha kichwa chako kidogo hasa kwa kuangalia unakula na kunywa nini kila siku.

Dawa mbadala 11 zinazotibu kufunga choo au choo kigumu:

1. Mafuta ya Zeituni

Mafuta ya zeituni (olive oil) yanatosha kutibu hili tatizo.

Yana radha nzuri mdomoni na ni dawa pia.

Kama unaweza yafanye pia kama mafuta yako ya kupikia vyakula vyako mbalimbali, mafuta haya huweza kuliwa pia bila kupitishwa kwenye moto na hivyo ni mafuta mazuri kuweka kwenye kachumbari au saladi mbalimabali.

Matumizi: Chukua kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya zeituni changanya na kijiko kidogo kimoja cha chai cha maji maji ya limau na unywe asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa bado tupu.

Fanya hivi kila siku mpaka utakapopona.

2. Juisi ya Limau

Juisi ya limau inatumika kutibu tatizo la kupata choo kigumu au kufunga choo.

Chukua maji maji ya limau kutoka katika limau kubwa 3 na uchanganye na juisi ya matunda kupata kikombe kimoja (ml 250) na unywe yote kutwa mara 1 kila siku kwa siku kadhaa mpaka umepona.

Ukiacha hilo la kutibu kufunga choo limau ina vitamini C nyingi na hivyo itakuongezea kinga yako ya mwili kwa haraka zaidi (usizidishe hata hivyo).

3. Mazoezi ya kutembea

Kama unataka kupata choo kilaini na cha kawaida basi jitahidi uwe mtu wa kutembeatembea na si kukaa tu kwenye kiti kutwa nzima.

Maisha yetu ya kisasa na kazi za ofisini zinatulazimisha kuwa watu wa kukaa kwenye kiti masaa mengi wengine huamua tu kukaa kwenye kiti sebureni akiangalia TV asubuhi mpaka jioni!.

Aina hii ya maisha ni hatari zaidi kwa afya zetu kuliko hata madawa ya kulevya.

Jitahidi kila siku uwe unapata muda wa kutembeatembea kwa miguu mpaka dakika 60 au zaidi.

Hii itakusaidia kuondoa tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.

4. Vyakula vya nyuzinyuzi (fiber)

Mara nyingi utasikia watu wakisisitiza juu ya umhimu wa kula vyakula vya asili na vyenye nyuzinyuzi.

Chakula cha asili kina nafasi kubwa katika kuimarisha afya yako kwa ujumla.

Kinachonishangaza ni kuona watu bado wanaendelea kula ugali wa sembe ilihali inajulikana wazi ugali mweupe ndiyo chanzo kikuu cha kupata choo kigumu ikiwemo ugonjwa wa bawasiri.

Ninakusihi sana uanze kula ugali wa dona kuanzia sasa na kuendelea.

Hakikisha pia asilimia 80 ya mlo wako kwa siku ni matunda na mboga za majani.

Matunda kama ndizi na parachichi ni mhimu ule kila siku kadharika tumia unga au mbegu za maboga.

5. Mshubiri (Aloe Vera)

Mshubiri unajulikana wazi kwa kutibu tatizo hili la kufunga choo au kupata choo kigumu.

Ni mhimu utumie mshubiri fresh kabisa kutoka kwenye mmea moja kwa moja kuliko kutumia za dukani au za kwenye makopo.

Usitumie zaidi ya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya shubiri kwa siku.

Matumizi: Changanya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya aloe vera ndani ya kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani (hasa juisi ya parachichi) na unywe yote kutwa mara 1 hasa nyakati za usiku unapokaribia kwenda kulala kwa siku kadhaa au mpaka umepona.

6. Baking soda

Baking soda ni dawa nyingine ya asili nzuri kwa tatizo hili. Inafanya kazi vizuri kwa zaidi ya asilimia 95.

Sababu ya bicarbonate iliyomo ndani yake itakusaidia kupumua nje vizuri gesi au hewa yoyote ilisongamana ndani ya tumbo pia inasaidia kupunguza asidi mwilini.

Baking soda ni ile wamama huitumia katika kupika maandazi au mikate inapatikana katika maduka ya kawaida hata hapo nje kwa Mangi ipo.

Matumizi:

-Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha baking soda ndani ya nusu kikombe cha maji ya uvuguvugu (ml 125) na unywe yote kwa haraka kutwa mara 1 kwa siku 7 hivi au unaweza kuacha siku yoyote kabla kama tatizo litakuwa limeisha.

7. Mtindi

Unahitaji bakteria wazuri zaidi wakati huu unapokabiliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu.

Utahitaji pia kuacha kula vyakula vya kwenye makopo (processed sugars and foods).

Namna rahisi kabisa ya kuhakikisha mwili wako unapata bakteria wazuri ni kwa kutumia mtindi.

Tumia mtindi wowote ule uliotengeneza mwenyewe nyumbani au hata wa dukani (ila wa dukani usiwe umeongezwa vitu vingine ndani yake – sweetened yogurt).

Matumizi: Kunywa kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi wakati wa chakula cha asubuhi na kikombe kingine usiku unapoenda kulala kwa wiki 1 hata 2.

8. Fanya mazoezi ya kusimama na kuchuchumaa (squat)

Fanya mazoezi ya kuchuchumaaa na kusimama (squatting).

Hili ni zoezi mhimu kwa mtu anayesumbuliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.

Fanya kuchuchumaa na kusimama mara 25 na upumzike dakika 1 kisha unaendelea tena unachuchumaa na kusimaa hivyo hivyo mara 25 kwa mizunguko mitano (5 rounds) huku ukipumzika dakika 1 kila baada ya mzunguko mmoja.

Fanya zoezi hili kila siku mara 1 na usizidishe sana, ni mara 25 kwa mizunguko mitano inatosha na uzuri ni kuwa unaweza kufanya zoezi hili mahali popote.

Wakati huo huo unashauriwa kutumia choo cha kuchuchumaa yaani vile vyoo vya zamani na siyo hivi vya kisasa vya kukaa kama vile upo ofisini.

Vyoo hivi vya kukaa ndiyo moja ya vitu vinavyochangia upate pia ugonjwa wa bawasiri (kuota kinyama sehemu ya haja kubwa na kupata maumivu wakati unajisaidia).

9. Matunda

Asilimia 80 ya chakula chacko kwa siku iwe ni matunda na mboga za majani.

Unapoumwa na hili tatizo pendelea zaidi parachichi, papai na juisi ya ukwaju.

Kula matunda siyo mpaka uumwe au ushauriwe na daktari, fanya kuwa ndiyo tabia yako kila siku na hutakawia kuona mabadiliko makubwa kwa afya yako kwa ujumla.

10. Maji ya Kunywa

Maji ni uhai. Asilimia 75 ya mwili wako ni maji. Asilimia 85 za ubongo wako ni maji.

Asilimia 94 ya damu yako ni maji. Hakuna maisha bila maji.

Inashangaza sana kuona mtu anamaliza siku nzima au hata siku 2 hajanywa maji!

Kama wewe si mpenzi wa kunywa maji ya kutosha kila siku SAHAU KUWA NA AFYA NZURI MAISHANI MWAKO.

Hakikisha unakunywa maji kila siku lita 2 mpaka 3, kidogo kidogo kutwa nzima bila kusubiri kiu na hutaugua tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu.

11. UKWAJU

Tunda la ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu.

Tunda hili huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana katika afya ya mwili wa mwanadamu.

NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA UKWAJU.

>Nunua ukwaju wako, ukwaju unapatikana kwa wingi sana masokoni na kwenye supermarkets

>Andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni uache uchemke kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu

>Ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe

>Weka asali kwa kiasi unachopendelea pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata radha nzuri zaidi weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa.

>Ukwaju unakusaidia kuyeyusha chakula tumboni na hivyo kukuepusha na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu

Mambo mhimu mengine ya kuzingatia:

-Acha vilevi VYOTE

-Acha vinywaji baridi na juisi zote za dukani

-Acha chai ya rangi na kahawa na vinywaji vingine vyote vyenye kaffeina

-Acha kula vyakula vilivyokobolewa

-Acha kula mkate mweupe

-Acha kula vyakula vigumu

Kama una swali zaidi liulize hapo chini kwenye comment nitakujibu hapa hapa

Mawasiliano yangu ni : WhatsApp +255714800175

Share post hii kwa ajili ya wengine uwapendao

Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 5

Let's block ads! (Why?)

Jumamosi, 3 Oktoba 2020

Sickle Cell Ni Ugonjwa Gani?

 

 

Sickle cell disease (SCD) ni kundi la maradhi ya kurithi ya chembechembe nyekundu za damu. Chembechembe nyekundu za damu zenye afya huwa za mviringo, na hutembea ndani ya mishipa midogo ya damu kusambaza oksijeni kwenye sehemu zote za mwili. Ndani ya mwili wa mtu mwenye ugonjwa wa sickle cell, chembechembe nyekundu za damu hugeuka kuwa ngumu na zinazonatanata na huwa na umbo la C, umbo linalofanana na kifaa cha shambani kiitwacho “sickle”. Seli hizi hufa mapema, hali ambayo husababisha mtu awe na upungufu wa damu kila wakati. Na, wakati seli hizi zikisafiri ndani ya mishipa midogo ya damu, hukwama na kuuziba mtiririko wa damu. Hali hii huweza kuleta maumivu makali na matatizo mengine makubwa kama maambukizi, acute chest syndrome na stroke.

Aina Za Sickle Cell Disease

Aina za ugonjwa wa sickle cell ambazo huonekana kwa wingi ni zifuatazo:

Alhamisi, 1 Oktoba 2020

16-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Kuweka Nadhiri Kwa Asiyekuwa Allaah

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

 

16- Kuweka Nadhiri Kwa Asiyekuwa Allaah

 

Alhidaaya.com

 

 

Kuweka nadhiri ni mtu kuilazimisha nafsi yake kwa kitu ambacho hajalazimishwa na Shariy’ah.  Amesema Al-Isfhaan (Rahimahu Allaah) katika Mufradaat Alfaadhw Al-Qur-aan (uk. 797): “Nadhiri ni unapojishurutisha kutenda jambo lisilokuwa wajibu kwa sababu ya kutaka jambo fulani likutokee. Anasema Allaah:

 

إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَـٰنِ صَوْمًا 

Hakika mimi nimeweka nadhiri ya swawm kwa Ar-Rahmaan [Maryam: 26]

 

Baadhi ya ‘Ulamaa wameharamisha kwa dalili ya Hadiyth ifuatayo:

 

عن النبيَّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ ؛ أنه نهى عن النذر  وقال:  إنه لا يأتي بخير. وإنما يستخرج من البخيل

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza nadhiri akasema: ((Haileti khayr bali inatolewa kutoka kwa bakhili)) [Muslim (1639)]

 

Na katika riwaayah nyingine:

 

  نَهَى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ النَّذْرِ وَقَالَ:  إِنَّهُ لَا يَرُدُّ شَيْئًا وَلَكِنَّهُ يُسْتَخْرَجُ بِهِ مِنْ الْبَخِيلِ

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza nadhiri akasema: ((Hakika hairudishi chochote, bali inatolewa kutoka kwa bakhili)) [Al-Bukhaariy (6693)]   

 

Na Hadiyth ya Mama wa Waumini ‘Aaishah  (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba  amesema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

 من نذر أن يُطِيعَ اللهَ فلْيُطِعْهُ ، ومن نذرَ أن يعصِيَه فلا يَعْصِه

((Aliyeweka nadhiri kumtii Allaah amtii, na aliyeweka nadhiri kumuasi Allaah, basi asimuasi))[Al-Bukhaariy (6696)]

 

 

Kutokana na Hadiyth hii, inadhihirisha kukubaliwa kwake nadhiri pindi mtu akiazimia, kwa dalili pia za Qur-aan:

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ

Na chochote mtoacho au mkiwekacho nadhiri, basi Allaah Anakijua. [Al-Baqarah: 270]

 

Na pia kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا﴿٧﴾

Wanatimiza nadhiri na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea kwa upana. [Al-Insaan: 7]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

ثُمَّ لْيَقْضُوا تَفَثَهُمْ وَلْيُوفُوا نُذُورَهُمْ

Kisha wamalize ‘ibaadah zao; wajisafishe taka zao na watimize nadhiri zao, [Al-Hajj: 29]  

 

 

Na kwa vile nadhiri ni aina ya ‘Ibaadah, haifai kuielekeza kwa asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) mfano kuifanya kwa ajili ya Nabiy, au Walii, au Shaykh, au kaburi na kadhaalika. Kufanya hivyo ni shirki kubwa inayomtoa mtu nje ya Uislamu.

 

Fataawa za ‘Ulaama kuhusu kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 

Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Swali: 

 

Je, ikiwa mtu ameweka nadhiri mfano akasema: “Allaah Akinipa shifaa kwa magonjwa yangu, nitachinja kwa ajili ya Allaah katika kaburi la fulani ili kujikurubisha kwa Allaah. Je, inajuzu mfano wa ‘amali kama hii? Na je, kuna sehemu zilizoharamishwa kuchinja?

 

Jibu: 

 

Ikiwa ameweka nadhiri kuchinja kwa ajili ya Allaah katika kaburi, basi nadhiri hii ni ya maasi, haijuzu kuitimiza. Na kuchinja katika kaburi ikiwa imekusudiwa kujikurubisha kwa mwenye kaburi, hiyo ni shirki kubwa inayomtoa mtu katika Dini hata kama ataja Jina la Allaah wakati anachinja.

 

Na ikiwa kujikurubisha kwa Allaah basi hayo ni maasi makubwa na wasiylah (njia ya kujikurubisha) za shirki kwa sababu haijuzu kuswali kaburini wala kuomba wala kuchinja kaburini hata kama tunakusudia Allaah kwani hivyo ni kujifananisha na washirikina na wasiyla za shirki. 

 

Abuu Daawuwd amepokea kutoka kwa Thaabit bin Adhw-Dhwahaak (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba mtu mmoja aliweka nadhiri kuchinja ngamia katika Buwaanah. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akauliza: ((Je, kuliweko masanamu ya kijaahiliyyah (kabla Uislamu) yakiabudiwa?”

Wakasema: “Hapana” Akasema: ((Je, kuliweko sherehe za kijaahiliyyah zikifanywa hapo?)) Wakasema: “Hapana” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Timiza nadhiri yako, kwani hakuna kutimiza nadhiri katika kumuasi Allaah, wala katika ambayo hayamiliki bin Aadam)). [Abuu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy]

 

 

 

Imaam bin Baaz (Rahimahu Allaah)

 

Swali:

 

Imenitokea mushkila nikaweka nadhiri kwa ajili ya mmojawapo wa ma-Imaam, kisha nikaja kutambua kuwa haifai kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah. Tambua kuwa sehemu aliyoko huyo Imaam iko mbali, je, inajuzu nilipize nadhiri hii kwa mafakiri au niifanyie kafara?

 

Jibu: 

 

Nadhiri hiyo ni baatwil, kwa sababu ni ‘ibaadah kwa asiyekuwa Allaah.  Inakupasa utubie kwa Allaah kwayo na urudi Kwake kwa kutubia na kuomba maghfirah na kujuta kwani nadhiri ni ‘ibaadah, Anasema Allaah Ta’aalaa:  

 

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ

Na chochote mtoacho au mkiwekacho nadhiri, basi Allaah Anakijua. [Al-Baqarah: 270]

 

Yaani: Atakulipeni kwayo. Na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

من نذر أن يُطِيعَ اللهَ فلْيُطِعْهُ، ومن نذرَ أن يعصِيَه فلا يَعْصِه

((Aliyeweka nadhiri kumtii Allaah amtii, na aliyeweka nadhiri kumuasi Allaah, basi asimuasi))  

 

Kwa hiyo nadhiri hiyo ni baatwil, na ni kumshirikisha Allaah (‘Azza wa Jalla) kama vile nadhiri kwa ajili ya ma-Imaam na waliokufa ni nadhiri baatwil na ni kumshirkisha Allaah, basi nadhiri haijuzu isipokuwa kwa ajili ya Allaah Pekee, kwa sababu ni ‘ibaadah kama vile Swalaah, na kuchinja na nadhiri, na kufunga Swiyaam na du’aa zote ni kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kama Anavyosema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾

Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada. [Al-Faatihah: 5]

 

 

Na Anasema (Subhaanahu):

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ

Na Rabb wako Amehukumu kwamba: “Msiabudu isipokuwa Yeye Pekee [Al-Israa: 23]

 

 

Na Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

فَادْعُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ﴿١٤﴾

Basi mwombeni Allaah wenye kumtakasia Dini japokuwa wanachukia makafiri. [Ghaafir: 14]

 

 

 

Na Anasema (‘Azza wa Jalla):

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا﴿١٨﴾

Na kwamba Misikiti ni kwa ajili ya Allaah, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah. [Al-Jinn: 18]

 

 

Basi ‘ibaadah ni haki ya Allaah, na nadhiri ni ‘ibaadah, na Swawmi ni ‘ibaadah, na Swalaah ni ‘ibaadah, na du’aa ni ‘ibaadah basi inawajibika kuisafisha kwa ajili ya Allaah Pekee. Kwa hiyo nadhiri hiyo ni baatwil, na haikupasi kufanya chochote, si kwa mafukara wala wengineo, bali inakupasa utubie tu na huna haja ya kuilipizia nadhiri hiyo kwa vile ni baatwil na ni shirki, ila tu utubie tawbah ya kikweli na kufanya matendo mema, Allaah Akuwafikie na Akuongoze katika yanayomridhisha na Akujalie ufanye tawbah ya kikweli.

 

 

 

 



54-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Anaombewa Du’aa Na Kuswaliwa Katika Kila Aina Za Ibaadah Za Waumini

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

54-Anaombewa Du’aa Na Kuswaliwa Katika Kila Aina Za Ibaadah Za Waumini

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ ﴿٤﴾

Na Tukanyanyulia juu utajo wako (ukawa mwenye kusifika mno)?  [Ash-Sharh: 4]

 

Allaah (عز وجل) Amemjaalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) fadhila adhimu kabisa nayo ni fadhila za kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika hali mbalimbali ya maisha ya Muislamu; katika Swalaah zote za faradhi na za Sunnah, namo ni katika Adhana na Iqaamah na katika kikao cha Tashahhud, katika Swalaah ya Jeneza, anapotajwa katika vikao vya elimu, zinapotajwa Hadiyth zake, katika ‘ibaada za Hajj na ‘Umrah, katika kuomba du’aa, katika Adhkaar za asubuhi na jioni, baada ya kutawadha, watu wanapokhutubia katika Minbar, zinapofungwa Nikaah,  Siku ya Ijumaa imeamrishwa kukithirisha kumswalia, na katika,  hali nyenginezo. Juu ya hivyo  imeamrishwa kuwa pindi inapoadhiniwa aombewe du’aa na kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Kumswalia kote huko humrudia fadhila zake kwa Muislamu anayetekeleza amri hii:

 

 

1-Baada Ya Kutawadha:

 

أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ  

Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah, Wahdahu laa shariyka Lahu wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu

 

2-Katika Adhana:

 

 

اللهُ أكبَر اللهُ أكبر، الله أكبر اللهُ أكبر، أشهدُ أنْ لا إلهَ إلَّا الله، أشهدُ أنْ لا إلهَ إلَّا الله، أشهدُ أنَّ محمدًا رسولُ الله، أشهدُ أنَّ محمدًا رسولُ الله، حيَّ على الصَّلاة، حيَّ على الصَّلاة، حيَّ على الفلاح، حيَّ على الفلاح، اللهُ أكبر اللهُ أكبر، لا إلهَ إلَّا الله

 

Allaahu Akbar Allaahu Akbar, Allaahu Akbar Allaahu Akbar, Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah, Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah,   Ash-hadu anna Muhammadan Rasuwlu-Allaah, Ash-hadu anna Muhammadan Rasuwlu-Allaah, Hayya ‘alas-Swalaah, Hayya ‘alas-Swalaah, Hayya ‘alal-Falaah, Hayya ‘alal-Falaah,   Allaahu Akbar Allaahu Akbar, laa ilaaha illa-Allaah

 

 

3-Anaombewa Du’aa Na Anaswaliwa Inapoadhiniwa:

 

 

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   قَالَ : {مَنْ قَالَ حِينَ يَسْمَعُ اَلنِّدَاءَ : اَللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ اَلدَّعْوَةِ اَلتَّامَّةِ،  وَالصَّلَاةِ اَلْقَائِمَةِ،  آتِ مُحَمَّدًا اَلْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ،  وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا اَلَّذِي وَعَدْتَهُ، حَلَّتْ لَهُ شَفَاعَتِي يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ}  أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ

 

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kusoma anaposikia Adhana:

 

 اَللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ اَلدَّعْوَةِ اَلتَّامَّةِ،  وَالصَّلَاةِ اَلْقَائِمَةِ،  آتِ مُحَمَّدًا اَلْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ،  وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا اَلَّذِي وَعَدْتَهُ

Allaahumma Rabba haadhihid-dda’watit-ttaamah, wasw-Swaalaatil qaaimah, aati Muhammada  al-wasiylata wal fadhwiylah, wab-‘ath-hu maqaaman mahmuwdan alladhiy wa’adtah.

 

(Ee Allaah, Rabb wa mwito huu uliotimia, na Swalaah iliyosimama, mpe (Nabiy) Muhammad al-Wasiylah (cheo, heshima maalumu, daraja), na fadhila, na mfikishe daraja yenye kuhimidiwa, ambayo Umemuahidi).

Ash-Shafaa’ah (Uombezi) wangu umehalalika kwake Siku ya Qiyaamah.” [Imetolewa na Al-Arba’ah]

 

 

Na pia,

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ، أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏ " إذَا سَمِعْتُمْ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوامِثْلَ مَا يَقُولُ ، ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ ، فَإِنَّهُ مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا . ثُمَّ سلُوا اللَّه لي الْوسِيلَةَ ، فَإِنَّهَا مَنزِلَةٌ في الجنَّةِ لا تَنْبَغِي إِلاَّ لعَبْدٍ منْ عِباد اللَّه وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَنَا هُو ، فَمنْ سَأَل ليَ الْوسِيلَة حَلَّتْ لَهُ الشَّفاعَةُ

‘Abdullaah bin ‘Amruw (رضي الله عنهما)  kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akisema: ((Mtakapomsikia muadhini basi semeni kama anavyosema, kisha niswalieni, kwani mwenye kuniswalia mara moja Allaah Atamswalia mara kumi, na kisha niombeeni (kupata) ‘wasiylah’ ambayo ni manzila (heshima maalum) huko Jannah. Haitomstahikia isipokua mja mmoja katika waja wa Allaah, nami ninatarajia kuwa mja huyo, na mwenye kuniombea “Al-Wasiylah” atapata uombezi (wangu Siku ya Qiyaamah)) [Muslim (1/288)

 

 

4-Katika Iqaamah:

 

اللهُ أكبر اللهُ أكبر، أشهدُ أنْ لا إلهَ إلَّا الله، أشهدُ أنَّ محمدًا رسولُ الله، حيَّ على الصَّلاة، حيَّ على الفلاح، قد قامتِ الصَّلاةُ، قد قامتِ الصَّلاة، اللهُ أكبر اللهُ أكبر، لا إلهَ إلَّا الله. 

 

Allaahu Akbar Allaahu Akbar, Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah, Ash-hadu anna Muhammadan Rasuwlu-Allaah, Hayya ‘alas-Swalaah, Hayya ‘alal-Falaah, Qad Qaamatis-Swalaah  Qad Qaamatis-Swalaah, Allaahu Akbar Allaahu Akbar, laa ilaaha illa-Allaah

 

 

5-Katika Kikao Cha Tashahhud:

 

 

التَّحِيّـاتُ للهِ وَالصَّلَـواتُ والطَّيِّـبات، السَّلامُ عَلَيـكَ أَيُّهـا النَّبِـيُّ وَرَحْمَـةُ اللهِ وَبَرَكـاتُه، السَّلامُ عَلَيْـنا وَعَلـى عِبـادِكَ الصَّـالِحـين، أَشْـهَدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ الله، وَأَشْـهَدُ أَنَّ مُحَمّـداً عَبْـدُهُ وَرَسـولُه

At-tahiyyaatu liLLaahi, was-swalawaatu, wat-twayyibaatu, Assalaamu ‘alayka ayyuhan-Nnabiyyu warahmatu-Allaahi wa Barakaatuh, Assalaamu ‘alaynaa wa ’alaa ‘IbaadiLLaahis-swaalihiyn. Ash-hadu an-laa ilaaha illa-Allaah wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu

 

اللّهُـمَّ صَلِّ عَلـى مُحمَّـد وَعَلـى آلِ مُحمَّد كَمـا صَلَّيـتَ عَلـى إبْراهـيمَ وَعَلـى آلِ إبْراهـيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد، اللّهُـمَّ بارِكْ عَلـى مُحمَّـد وَعَلـى آلِ مُحمَّـد كَمـا بارِكْتَ عَلـى إبْراهـيمَ وَعَلـى آلِ إبْراهيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد .

Allaahumma Swalli ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Swallayta ‘alaa Ibraahiyma wa ‘alaa aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd. Allaahumma Baarik ‘alaa Muhammad, wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Baarakta ‘alaa  Ibraahiyma wa ‘alaa  aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd.

 

 

6-Du’aa Haipandi Mbinguni Bila Ya Kumswalia Mwanzo Na Mwisho Wa Du’aa:

 

 

عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ (رضي الله عنه)  قَالَ: "إِنَّ الدُّعَاءَ مَوْقُوفٌ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ لاَ يَصْعَدُ مِنْهُ شَيْءٌ حَتَّى تُصَلِّيَ عَلَى نَبِيِّكَ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)"

Imepokelewa kutoka kwa ‘Umar bin Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu): “Hakika du’aa inasimama baina ya mbingu na ardhi haipandi masafa yoyote mpaka umswalie Nabiy wako (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)." [Swahiyh At-Tirmidhiy (486), Swahiyh At-Targhiyb (1676)]

 

 

7-Kukithirisha Kumswalia Siku Ya Ijumaa:

 

عَنْ أَوْسِ بْنِ أَوْسٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ مِنْ أَفْضَلِ أَيَّامِكُمْ يَوْمَ الْجُمُعَةِ، فَأَكْثِرُوا عَلَيَّ مِنْ الصَّلاةِ فِيهِ، فَإِنَّ صَلاَتَكُمْ مَعْرُوضَةٌ عَلَيَّ)) قَالوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَكَيْفَ تُعْرَضُ صَلاتُنَا عَلَيْكَ وَقَدْ أَرَمْتَ؟  قَالَ: يَقُولُ:  بَلِيتَ  قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى حَرَّمَ عَلَى الأَرْضِ أَجْسَادَ الأَنْبِيَاءِ)) رواه ابو داوُود بِاِسنادٍ صحيح

Imepokelewa kutoka kwa Aws bin Aws (رضي الله عنه)  ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه  وآله وسلم ) amesema: ((Hakika siku zenu zilizo bora mno ni siku ya Ijumaa, basi kithirisheni kuniswalia siku hiyo, hakika Swalaah zenu huwa naletewa)). Maswahaba wakauliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Vipi Swalaah zetu kuwa unaletewa na ilihali wakati huo utakuwa umeshaoza?” Akajibu: ((Hakika Allaah Ameiharamisha ardhi kula viwiliwili vya Manabii)). [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Swahiiyh]

 

 



20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...