Translate
Jumapili, 30 Desemba 2018
Kuelekea Qibla wakati wa Kuchinja
Je, ni lazima kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja...?
Jibu
Kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja sio wajibu.
Mtu anaweza kuchinja kichinjwa chake ijapokuwa hakuelekea Qiblah. Lakini wanachuoni (Rahimahumu Allaah) wamesema kuwa bora zaidi ni mtu aelekee Qiblah. Kwa sababu ni ´ibaadah.
Lakini hata hivyo hawakusema kuwa ni sharti. Iwapo mtu atachinja kwa kuelekea upande usiokuwa Qiblah ni halali. Sio jambo limechukizwa. Hapana neno.
Tofauti na wanavosema watu wasiokuwa na elimu. Baadhi yao wanasema kwamba ni lazima kuelekea Qiblah, jambo ambalo si sahihi.
Rejea : Al-Liqaa' ash-Shahriy (42)
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2SvU024
via IFTTT
Hukumu ya Kufunga Mikono katika Swalah
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
"Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema;
"Sisi Manabii tumeamrishwa kuharakisha kula futari zetu na kuchelewesha kula daku letu, na kuweka mikono yetu ya kulia juu ya kushoto ndani ya Swalaah." [At-Twabaraaniy na Ibn Hibbaan]
"Nikamtazama! akatoa takbiyr, kisha akanyanyua mikono yake mpaka ikakaribia masikio yake, kisha akauweka wa kulia juu ya upande wa nyuma wa mkono wa kushoto." [Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake na An-Nasaaiy na Abu Daawuwd katika Sunan yake na Ahmad katika Musnad yake 4/318 na Ibn Maajah katika Sunan yake 1/266 na Ad-Daarimiy katika Sunan yake 1/314 na Ibnul Jaruud katika Al-Muntaqaa Hadiyth nambari 208 na katika vitabu vingi vingine"].
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2Sofhe8
via IFTTT
Uharamu wa Mwaka Mpya
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
Naam,Ndugu zangu katika Imaani, na leo tena nachukua fursa hii kuwahusia Nafsi zenu pamoja na kuihusia Nafsi yangu juu ya Kumcha Allaah(Subhaana wa Taala) na Salamu zimfikie Kipenzi cha Ummah huu na Maswahaba zake, Amabad.
Ndugu zangu katika Imaani, Leo ni Tarehe 31/12/2018 katika Tarehe za Kikafiri na ni Ada zao katika Tarehe kama ya leo ikifika kuanzia jioni huwa wanajiandaa katika kuukaribisha Mwaka Mpya wao wa Kikafiri ambao umetengenezwa tu watu.
Kwahiyo Muislamu anatakiwa ajitenge na wala asishiriki nao katika sherehe hizi za Kikafiri maana wengi huwa wanakesha kwa kuukaribisha na kupiga mabaruti na wengine kucheza miziki nakadhalika.
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2Su60kP
via IFTTT
74. Matamshi ya Tashahhud – Tamko la Ibn ´Umar
3- Tashahhud ya Ibn ´Umar. Ibn ´Umar amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
التحيات لله، [و]الصلوات [و]الطيبات، السلام عليك أيها النبي و رحمة الله، السلام علينا و على عباد الله الصالحين، أشهد أن لا إله إلا الله و أشهد أن محمداً عبده و رسوله
“Maadhimisho, swalah na mazuri yote yanamstahikia Allaah. Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume[1]! Amani ishuke juu yetu na juu ya waja wema wa Allaah. Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah[2] na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.”[3]
[1] Ibn ´Umar amesema:
“Niliongeza:
و بركاته
“… na baraka Zake… “
[2] Ibn ´Umar amesema:
“Niliongeza juu yake:
وحده لا شريك له
“… hali ya kuwa yupekee, hana mshirika… “
Nyongeza mbili hizi katika Tashahhud zimethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ibn ´Umar hakuziongeza kutoka kwake mwenyewe. Asingeweza kamwe kufanya kitu kama hicho. Nyongeza mbili hizo alijifunza nazo kutoka kwa Maswahabah wengine waliozisikia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akaziongeza katika Tashahhud yake aliyoisikia moja kwa moja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[3] Abu Daawuuud na ad-Daaraqutwniy ambaye ameisahihisha.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2EWreDJ
via IFTTT
73. Matamshi ya Tashahhud – Tamko la Ibn ´Abbaas
2- Tashahhud ya Ibn ´Abbaas. Ibn ´Abbaas amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitufunza Tashahhud kama anavyotufunza [Suurah katika] Qur-aan: Alikuwa akisema:
التحيات المباركات الصلوات الطيبات لله، [ال]سلام عليك أيها النبي و رحمة الله و بركاته، [ال]سلام علينا و على عباد الله الصالحين، أشهد أن لا إله إلا الله و [أشهد]أن محمداً رسول الله
“Maadhimisho, baraka, swalah na mazuri yote yanamstahikia Allaah[1]. Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume! Amani ishuke juu yetu na juu ya waja wema wa Allaah. Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na [nashuhudia] ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah.”
Katika upokezi mwingine imekuja:
و أن محمداً عبده و رسوله
“… na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.”[2]
[1] an-Nawawiy amesema: ”Hadiyth inafahamisha kwamba maadhimisho na yote yaliyo baada yake yanamstahikia Allaah (Ta´ala) pekee na si mwengine.”
[2] Muslim, Abu ´Awaanah, ash-Shaafi´iy na an-Nasaa’iy.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2EXMud1
via IFTTT
72. Matamshi ya Tashahhud – Tamko la Ibn Mas´uud
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwafunza Maswahabah sampuli mbalimbali za Tashahhud:
1- Tashahhud ya Ibn Mas´uud. Ibn Mas´uud amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinishika mkono wangu kwa mikono yake miwili na akanifunza Tashahhud kama anavyonifunza Suurah katika Qur-aan:
التحيات لله، و الصلوات و الطيبات، السلام عليك أيها النبي و رحمة الله و بركاته، السلام علينا و على عباد الله الصالحين، أشهد أن لا إله إلا الله و أشهد أن محمداً عبده و رسوله
“Maadhimisho, swalah na mazuri yote yanamstahikia Allaah. Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume! Amani ishuke juu yetu na juu ya waja wema wa Allaah [pindi anaposema hivo basi inamgusa kila mja mwema mbinguni na ardhini]. Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.”
Tulikuwa tukisema hivo wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bado yupamoja nasi. Alipofariki tukawa tunasema:
السلام على النبي
“Amani iwe juu ya Mtume.”[1]
[1] al-Bukhariy, Muslim, Ibn Abiy Shaybah (2/90/1), as-Sarraaj na Abu Ya´laa katika ”al-Musnad” (2/258). Imetajwa katika ”al-Irwaa’” (321). Maneno ya Ibn Mas´uud “Tulikuwa tukisema hivo wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bado yupamoja nasi. Alipofariki tukawa tunasema:
السلام على النبي
“Amani iwe juu ya Mtume.”
ni dalili inayoonyesha kuwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa wakisema katika Tashahhud ya kwanza wakati wa uhai wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
السلام عليك أيها النبي و رحمة الله و بركاته
“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume!”
Baada ya kufa kwake wakabadilisha matamshi na kusema:
السلام على النبي
“Amani iwe juu ya Mtume.”
Hilo pasi na shaka ni lazima liwe limetokana na kuridhia kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nadharia hiyo inaungwa mkono vilevile na ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) na jambo la hakika ni kuwa naye alifunza Tasahhhud kama ifuatavyo:
السلام على النبي
“Amani iwe juu ya Mtume.” (as-Sarraaj katika ”al-Musnad” (2/1/9) na al-Mukhallas katika ”al-Fawaa-id” (1/54/11) kwa cheni mbili za wapokezi kupitia kwake)
Haafidhw Ibn Hajar (Rahimahu Allaah) amesema:
“Nyongeza hii udhahiri wake ni kwamba walikuwa wakisema:
السلام عليك أيها النبي و رحمة الله و بركاته
“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume!”
wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa bado yuko hai. Alipofariki (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndipo wakaacha aina ya kumlenga na wakawa wanasema:
السلام على النبي
“Amani iwe juu ya Mtume.””
Ibn Hajar amesema vilevile:
“as-Subkiy amesema katika “Sharh-ul-Minhaaj” baada ya kutaja nyongeza hii kwa Abu ´Awaanah: “Ikiwa haya yamesihi kutoka kwa Maswahabah basi inafahamisha kwamba sio wajibu kusema kwa aina ya kumlenga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kufa kwake. Kwa hiyo mtu anaweza kusema:
السلام على النبي
“Amani iwe juu ya Mtume.””
Haya yamesihi pasi na shaka na nimepata upokezi wenye nguvu mwingine unaotilia nguvu. ´Abdur-Razzaaq amesema: “Ibn Jurayj amenikhabarisha: ´Atwaa amenikhabarisha ya kwamba Maswahabah walikuwa wakisema wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bado yuhai:
السلام عليك أيها النبي و رحمة الله و بركاته
“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume!”
Alipofariki wakasema:
السلام على النبي
“Amani iwe juu ya Mtume.””
Mlolongo wa wapokezi ni Swahiyh. Hata hivyo Sa´iyd bin Mansuur amepokea kupitia kwa Abu ´Ubaydah bin ´Abdillaah bin Mas´uud kutoka kwa baba yake ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwafunza Tashahhud. Baada ya kutaja tamko Ibn ´Abbaas akasema: “Wakati bado Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yuko hai ndipo tulikuwa tukisema:
السلام عليك أيها النبي و رحمة الله و بركاته
“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume!”
Ndipo akasema Ibn Mas´uud: “Hivo ndivyo tulivyojifunza na hivo ndivyo tunavyofunza.”
Ni kama kwamba Ibn ´Abbaas alisema hivo kwa lengo la kuhakiki na kwamba Ibn Mas´uud hakurejea kwake. Lakini upokezi wa Abu Ma´mar [kwa al-Bukhaariy] ni Swahiyh zaidi kwa sababu Abu ´Ubaydah hakuwahi kusikia kutoka kwa baba yake. Pamoja na hivyo cheni ya wapokezi mpaka kwake ni dhaifu.”
Wanachuoni wengi wahakiki, akiwemo al-Qastwalaaniy, az-Zarqaaniy na al-Luknawiy, wameyanukuu maneno haya ya Haafidhw Ibn Hajar kwa kuyakubali bila kuyapinga. Rejea katika asili kuhusu zaida juu ya maudhui haya.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2EW0rrc
via IFTTT
71. Uwajibu wa ile Tashahhud ya kwanza na du´aa zake zilizowekwa katika Shari´ah
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisoma Tashahhud kila baada ya Rak´ah mbili[1]. Kitu cha kwanza anachosema punde tu baada ya kukaa chini:
التحيات لله
“Maadhimisho yote yanamstahiki Allaah.”[2]
Akisahau (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Tashahhud ya kwanza, basi huleta Sujuud-us-Sahuw[3]. Aliamrisha Tashahhud na akasema:
“Mnapokaa chini kila baada ya Rak´ah mbili basi semeni:
…التحيات لله
“Maadhimisho yote yanamstahiki Allaah… “
na chagueni du´aa inayokupendezeni na mumuombe Allaah (´Azza wa Jall).”[4]
Katika upokezi mwingine imekuja:
“Semeni katika kila kitako:
…التحيات لله
“Maadhimisho yote yanamstahiki Allaah… “[5]
Vivyo hivyo alimwamrisha yule mtu aliyeswali kimakosa, kama ilivyotangulia punde tu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwafunza Tashahhud kama anavyowafunza Suurah kutoka katika Qur-aan[6]. Sunnah ni kuisoma kimyakimya[7].
[1] Muslim na Abu ´Awaanah.
[2] al-Bayhaqiy kupitia kwa ´Aaishah kwa cheni ya wapokezi nzuri, amesema Ibn-ul-Mulaqqin (2/28).
[3] al-Bukhaariy na Muslim. Imetajwa katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (338).
[4] an-Nasaa’iy, Ahmad na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” (1/25/3) kwa cheni Swahiyh. Udhahiri ni kwamba imewekwa katika Shari´ah kuomba katika kila Tashahhud hata kama sio Rak´ah ya mwisho. Haya pia ndio maoni ya Ibn Hazm (Rahimahu Allaah).
[5] an-Nasaa’iy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
[6] al-Bukhaariy na Muslim.
[7] Abu Daawuud na al-Haakim ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2EYoAhJ
via IFTTT
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri ...