Translate

Jumapili, 15 Machi 2020

Madhara zaidi ya Kisukari katika mwili

Kupenda vitu vitamu hususani jamii ya sukari huwa ni tamu sana kwenye ulimi lakini changamoto inakuja kule inakoelekea kwa ajili ya kutunzwa na kutumika, hapo ndo husababisha changamoto mbalimbali mwilini hasa kwenye baadhi ya viungo vya mwili.

Madhara ya muda mrefu ya ugonjwa wa kisukari huanza taratibu, kadiri unavyo kuwa na sukari na unavyo shindwa kuchukua hatua juu ya sukari hiyo ndivyo hatari ya kupata madhara makubwa huongezeka.

Pia ikumbukwe madhara yatoka nayo na kisukari huweza kuhatarisha maisha ya mtu.

Yafuatayo ni madhara ya sukari inapozidi mwili na kiwango sahihi cha sukari inayotakiwa mwili pale unapokuwa umekula chakula:

1. Vidonda vya miguuni

Ugonjwa wa kisukari huathiri miguuni hasa pale unapopata ganzi inapelekea kushindwa kuhisi maumivu hivyo hata ukipata jeraha au mchubuko unakuwa huhisi maumivu ya aina yoyote.

Unakuwa hauna tofauti na aliechomwa sindano ya ganzi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

Vidonda vya mtu mwenye kisukari ni vigumu sana kupona kwa sababu damu inakuwa haifiki ya kutosha kwenye kidonda na asilimia kubwa bakteria wabaya huanza kukishambulia kwa kasi kwa sababu kinakuwa ni kitamu 

Kwa kuwa kidonda kina bakteria na kinaonekana kuwa na malengelenge ya mafuta na hao bakteria hushambulia kwa kasi hivyo kusababisha kuongezeka kwa kidonda na mwishowe kukatwa endapo hutawahi huduma mapema ya kujikinga. ·        

2. Kutokuona vizuri au mtoto wa jicho

Mishipa ya kwenye macho huwa ni midogo midogo sana na iko laini sana ukiliganisha na mishipa ya sehemu zingine za mwili hivyo inapoingiliwa na sukari damu hushidwa kupita ya kutosha sehemu za macho na kumfanya mtu awe anaona ukungu ukungu au kutokuona kabisa. ·        

3. Madhara ya figo

Figo inapokuwa imezidiwa na kiwago kingi cha sukari hulazimika kupunguza maji ya ziada na utengenezaji wa calcium kwa ajili ya kulinda mifupa hivyo sukari nyingi kukimbilia kwenye damu na baadaye huwa sumu mwilini. ·        

4. Kiharusi (stroke)

Kwa kuwa madhara ya sukari mojawapo ni kudhoofisha mishipa kwenye mwili hivyo mtu wa kisukari ana hatari kubwa ya kupata stroke kwa sababu baadhi ya mishipa kwenye ubongo huathiriwa na kukosa uwezo wa kupitisha damu ya kutosha na mwishoe kupasuka na kusababisha kiharusi. ·        

5. Maradhi ya moyo

Vyanzo vya mishipa huanzia kwenye moyo na kusambaa pande zingine za mwili, moyo huathiriwa na ugonjwa wa kisukari kwa sababu sukari hudhoofisha mishipa na kumfanya mtu kuwa dhaifu hivyo kama damu haipiti ya kutosha kwenye mishipa inakuwa ni kirahisi kupata magonjwa ya moyo kama vile moyo kupanuka, moyo kuwa na tundo pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo. ·        

6. Kwa wanaume kuishiwa nguvu za kiume

Hili ni tatizo kubwa kwa wanaume kwa sababu mfumo wa uzazi wa mwanaume umeundwa kwa mishipa na misuli, kama patakuwa hakupati ujazo mzuri wa damu inakuwa ni rahisi sana kushidwa kushiriki tendo ndoa na wengi wao wanapopatwa na hali kama hii huigiwa na presha au msongo wa mawazo na kuibua matatizo mengine tena.  

Hayo ni baadhi ya madhara anayopatwa mtu mwenye kisukari japo anaweza kupatwa na changamoto zingine nyingi kwenye mwili wake na kumpelekea kupata shida awe mtoto au mtu mzima, lakini kwa kukosa uelewa na umakini zaidi kundi la watu wengi huishia kukatwa baadhi ya viungo na mwishowe kifo.

7. Kuvurugika kwa vichocheo vya mwili

8. Hatari ya kupata maambukizi kutokana na kushindwa kufanya kazi vizuri kwa seli nyeupe za damu

9. Kwa wamama wenye kisukari kinacho tokana na ujauzito kupata  aina ya pili ya kisukari

10. Kifafa Cha mimba

11. Matatizo ya ganzi na kupooza endapo kisukari kitaathiri mishipa ya fahamu

Soma hii pia > Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili

Kama unahitaji dawa ya asili inayotibu kisukari aina ya pili, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.

Makala hii inaendelea kuboreshwa kwa kuongeza picha na maelezo zaidi, endelea kuja …

Tafadhali SHARE kwa ajili ya wengine uwapendao.

Imesomwa mara 6

Let's block ads! (Why?)

Ijumaa, 13 Machi 2020

Hadithi 8 za uongo kuhusu bawasiri

Hadithi 8 za uongo kuhusu bawasiri

Hadithi namba 1: Ukiugua bawasiri hata ukipona utarudia kuugua tena na tena.

Ukweli ni upi: Madai haya hayana ukweli wowote hasa kwa yule ambaye amepata ugonjwa huu kwa sababu za muda mfupi tu kama vile ujauzito.  Kwa kawaida ukitibiwa ugonjwa huu na ukapona kitakachosababisha upate tena ugonjwa huu ni kutokuzingatia masharti unayopewa juu ya vyakula na namna ya kuishi kwa ujumla ili kujikinga na tatizo lisijirudie tena. Hata baada ya kupona bado unatakiwa uendelee kula vizuri na kuishi vizuri wakati wote ili kwamba usipate tena ugonjwa huu. Ni ugonjwa wa tabia na hivyo kadri unavyojiepusha na tabia zinazopelekea ugonjwa huu ndivyo unavyojiweka mbali na kuugua tena.

Hadithi: Bawasiri inaweza kuleta saratani ya utumbo mpana

Ukweli ni upi: Bawasiri kama bawasiri haiwezi kukuletea saratani ya utumbo mpana. Hata hivyo dalili za bawasiri zinafanana sana na zile za ugonjwa wa saratani ya utumbo mpana (colon cancer). Kwahiyo ni mhimu sana kwamba unahangaika kwa vyovyote utakavyoweza kupata matibabu kwa ajili ya bawasiri mapema wakati inapojitokeza na siyo kusubiri mpaka hali iwe mbaya kiasi cha kufananishwa na saratani.

Hadithi: Ninakula vyakula vya nyuzinyuzi hivyo siwezi kuugua bawasiri

Ukweli ni huu: Wakati kula vizuri hasa kupendelea kula vyakula vyenye nyuzinyuzi ni hatu anzuri y akujikinga usipatwe na bawasiri bado hilo pekee halizuii wewe kuugua ugonjwa huu. Kuna sababu zingine kuu zinazoleta ugonjwa huu ikiwemo tabia ya kukaa tu chini au kwenye kiti masaa mengi, kula ugali wa sembe na kutokunywa maji mengi ya kutosha kila siku.

Hadithi: Kuendesha baiskeli muda mrefu kunaweza kusababisha bawasiri.

Ukweli: Miaka mingi mababu zetu wamekuwa wakitegemea baiskeli kama usafiri wao mkuu na hawakuugua bawasiri kama tunavyoteseka sisi miaka ya sasa. Kuendesha baiskeli kunaweza kusikuletee bawasiri moja kwa moja ila kunaweza kuwa ni sababu mojawapo ya kutokea kwa dalili au hatua za mwanzo za bawasiri. Kama unaendesha baiskeli lakini unakula vizuri na baadaye unakuwa unatumia muda mwingi kusimama au kutembeatembea na siyo kukaa tu kwenye kiti kuna uwezekano mdogo wa wewe kupatwa na bawasiri. Kinachosaidia ni kwamba baiskeli tofauti na pikipiki au gari baiskeli ni sehemu ya mazoezi pia kwa mwili hivyo kuna faida za kiafya unaweza kuzipata ambazo zitakusaidia usipate bawasiri kirahisi kama vile ungekuwa boda boda au dereva wa gari.

Hadithi: Ni watu wazima tu ndiyo hupata bawasiri

Ukweli: Ingawa ni kweli ugonjwa huu kwa sehemu kubwa umekuwa ukionekana mara nyingi ukiwatokea watu wazima bado haimaanishi kwamba ni watu wazima tu ndiyo wanaougua ugonjwa huu. Ukweli ni kuwa mtu wa umri wowote ambaye muda mwingi anatumia kukaa chini au kwenye kiti, hali vyakula vingi vya nyuzinyuzi (fiber) na kula zaidi vyakula feki anaweza kupata ugonjwa huu bila kujali umri wake. Kwahiyo watoto na hata watu wazima wazee sana pia wote wanaweza kupatwa na ugonjwa huu. Ugonjwa huu unaonekana kuwatesa zaidi ya wanawake kuliko wanaume sababu ya tabia yao ya kupenda kukaa muda mrefu kwenye kiti na wengine kwa sababu zinazotokana na ujauzito.

Hadithi: Mara zote bawasiri huambatana na kutoka damu

Ukweli unasemaje: Madai haya tena hayana ukweli. Dalili za bawasiri zinaweza kutokea bila kuhusisha kutoka damu wakati wa kujisaidia. Kuna bawasiri za aina mbili hasa ambazo ni bawasiri ya andani na bawasiri ya nje na zote mbili siyo lazima zipelekee kuvuja damu. Kwenye bawasiri ya nje uvimbe unaweza kusikika na kuonekana sehemu ya nje ya tundu la haja kubwa na inaweza kuleta maumivu wakati unajisaidia lakini siyo lazima iambatane na damu. Ikikutokea kwamba bawasiri yako inaambatana na kutokwa damu utahitaji matibabu ya haraka zaidi kwani unaweza kupatwa na madhara mengine mabaya zaidi kiafya yatokanayo na damu kupungua kwa kupotea hivyo pole pole kila siku.

Hadithi: Bawasiri haiponi mpaka ufanye upasuwaji.

Ukweli ni: Upasuwaji (operation) siyo njia pekee ya kutibu tatizo hili. Upasuaji ni njia ya haraka (quick fix) ya kuondoa uvimbe wa bawasiri ya nje. Hapa unakuwa umeondoa uvimbe uliotokana na bawasiri na siyo bawasiri yenyewe. Bawasiri ni ugonjwa unaoanzia ndani ya mwili tumboni kwenye mmeng’enyo wa chakula. Uonapo uvimbe kwenye sehemu ya tundu la haja kubwa hiyo siyo bawasiri, huo ni uvimbe kama matokeo ya bawasiri. Pamoja na upasuaji ili kuondoa uvimbe bado utahitaji kula vizuri na kutumia baadhi ya dawa za kunywa ili kwamba chanzo cha ugonjwa wenyewe kilichojiunda tumboni kiweze kupotea ili kwamba usiendelee tena kuugua ugonjwa huu. Utakuwa shuhuda hapa kwamba umeshawahi kufanya upasuaji na bado wiki kadhaa mbeleni uliona uvimbe ukijirudia tena na ukabaki unashangaa.

Hadithi: Bawasiri ni ugonjwa usiotibika

Ukweli upoje: Bawasiri siyo ukimwi. Ni ugonjwa wa kawaida na unatibika na kupotea. Inawezekana umeshatumia dawa za kila namna na huoni dalili zozote za kupona. Bado kuna watu wanapona bawasiri hasa wale wanaozingatia maelezo wanayopewa na matabibu juu ya vyakula na namna ya kusihi kwa ujumla. Ni wale tu wanaoweka matumaini yote kwenye dawa bila kujibidiisha kubadili vyakula na mifumo yao ya maisha inayopelekea ugonjwa wa bawasiri ndiyo hawaponi. Hata kwa upande wa vidonda vya tumbo kuna imani za namna hii kwamba ni ugonjwa usiotibika. Siyo kweli, wapo wanaopona na mimi ninazo shuhuda za watu wanaopona bawasiri hata vidonda vya tumbo. Usikae tu na kuishi na ugonjwa wowote, chukua hatua.

Hitimisho

Bawasiri ni ugonjwa wa kawaida na unatibika. Tofauti na unavyoweza kufikiri nap engine hata kuona aibu, ni kuwa ugonjwa huu wanaugua watu wengi sana na hauchagui maskini wala tajiri. Ni ugonjwa wa pili unaotesa watu wengi baada ya U.T.I na una una uhusiano wa karibu na vidonda vya tumbo.

Upatapo ugonjwa huu usione aibu, chukua hatua mapema ili kuweza kupona kirahisi kuliko ukisubiri hali iwe mbaya zaidi kiasi cha matibabu kukugharimu zaidi na kuchukuwa muda mrefu kuliko kawaida.

Kama unahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kutibu bawasiri niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Kama unapenda kujifunza mengi zaidi kuhusu ugonjwa wa bawasiri bonyeza HAPA.

SHARE post hii kwa ajili ya wengine.

Imesomwa mara 1

Let's block ads! (Why?)

Jumatatu, 17 Februari 2020

Dawa ya kutoa sumu mwilini

Dawa ya kutoa sumu mwilini

SUMU ni kitu chochote ambacho kinaweza kuingia mwilini na kusababisha mifumo ya mwili ishindwe kufanya kazi ipasavyo.

Unafikiria kuwa una afya njema, lakini haujisikii vyema. Unapuuza, unaona ni vitu vidogo vidogo.

Hivyo, haushughuliki kwenda hospitali au kwa wataalamu wa afya kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

Hatimaye tatizo linakuwa kubwa. Unafika hospitali unaambiwa una saratani, unapata mshtuko mkubwa! Unaambiwa chanzo cha ugonjwa hakifahamiki, ila unaelezwa chakula na mtindo wa maisha kwa ujumla ni sababu kubwa.

Hii ina maana kuna uwezekano umeingiza sumu nyingi mwilini. Kinga ni bora kuliko tiba. Kama ungeelewa mapema, ungejikinga na saratani.

Sizungumzii sumu za kung’atwa na nyoka, wala sizungumzii sumu zinazohitaji matibabu ya dharura.

Nazungumzia sumu ambazo zinatuua polepole na kimya kimya bila ya sisi kujua wala kutambua chochote. Nazungumzia sumu ambazo kila kuchapo tuko kwenye mlango wa daktari.

Kila kuchapo afya zetu hizidi kuzorota zaidi. Hizi ni sumu ambazo ziko kwenye vyakula vyetu.

Ni sumu tunazozivuta katika hewa kila siku kutokana na mioshi ya magari, viwanda n.k.

Sumu ambazo zinaweza kutokana na madawa mbalimbali tunayojitibia afya zetu, sumu zinazotokana na vipodozi mbalimbali tunavyotumia kila siku kwa ajili ya urembo na kupendeza.

Tunapata sumu mwilini kwa sababu lazima tuvute hewa, hata kwa sekunde kadhaa tusipopata hewa ya oksijeni tunakufa.

Lakini tunavuta hewa iliyochafuliwa na mioshi ya viwanda na magari ambayo imetamalaki kila kona.

Hivyo lazima tufe polepole na kimya kimya!

Tunapata sumu mwilini kwa sababu lazima tule na tunywe. Lakini kwa bahati mbaya, vyakula vingi tunavyokula siyo salama, vimesheheni kemikali.

Tunapata sumu kwa sababu lazima tujipodoe, lazima tujipambe tupambike, na lazima tung’are tupendeze.

Kwa bahati mbaya sana, vipodozi vingi vimekuwa siyo vipodozi, ni vipopozi. Vimejaa kemikali ambazo huleta madhara mengi ya kiafya.

Tunapongeza mamlaka ya chakula na dawa, TFDA, kwa kuviteketeza baadhi ya vipodozi na kutoa orodha ya vipodozi visivyofaa, lakini hata hivyo juhudi kubwa lazima ifanyike.

Ishara zitakazokuonyesha mwili wako una sumu nyingi:

-Uchovu sugu
-Maumivu ya maungio
-Msongamano puani
-Kuumwa kichwa kila mara
-Tumbo kujaa gesi
-Kufunga choo au kupata choo kigumu
-Kukosa utulivu
-Matatizo mbalimbali ya ngozi ikiwemo chunusi
-Pumzi mbaya
-Mzunguko wa hedhi usio sawa
-Kuishiwa nguvu
-Kushindwa kupungua uzito
-Kupenda kula kula kila mara

Kinachosababisha mwili kuwa na sumu au taka taka

Mwili unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na mwili kwa namna mbili, ama kupitia mazingira tunayoishi (viwanda, migodi nk) au kupitia vyakula na vinywaji ambavyo tunatumia kila siku.

Sumu au taka pia zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali hasa za kizungu tunazotumia kujitibia magonjwa mbalimbali.

Mwili huzalisha hizi sumu au takataka (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng’enyo wa chakula mwilini mwako.

1. Kutokula matunda na mboga za majani

Matunda na mboga za majani ni vitu viwili mhimu sana ili kusafisha mwili wako na kukukinga dhidi ya sumu na taka taka mbalimbali.

Kama huna tabia ya kula matunda na mboga za majani kila siku ni wazi mwili wako utatengeneza sumu za kutosha.

2. Kula vyakula vya viwandani

Kama unataka kuepuka sumu au takataka nyingine kirahisi kuingia katika mwili wako basi pendelea zaidi kula vyakula vya asili vinavyopikwa nyumbani kuliko kula vya kwenye makopo au vya dukani au vya kwenye migahawa (fast foods).

3. Kutokunywa maji mengi kila siku

Sababu kubwa ya watu wengi kutengeneza sumu au taka mwilini mwao ni kutokunywa maji mengi kila siku. Maji ni uhai, bila kunywa maji mengi kila siku ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.

Haijalishi upo mazingira gani kama ni ya baridi au ni ya joto ni LAZIMA UNYWE MAJI YA KUTOSHA KILA SIKU IENDAYO KWA MUNGU.

Unahitaji maji glasi 8 mpaka 10 kila siku. Watu wengi wanahangaika namna ya kuondoa sumu kusafisha miili yao bila kujua kuwa maji pekee ya kunywa yanatosha kwa kazi hiyo.

Kumbuka asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 za ubongo wako ni maji, hivyo kama huna mazoea ya kupenda kunywa maji kila siku ni rahisi mwili wako kutengeneza sumu. .

4. Vinywaji vyenye kaffeina

Kama tayari imethibitika una sumu au takataka nyingi mwilini nakushauri uache kunywa chai ya rangi na kahawa.

Badala yake hamia kutumia chai yenye tangawizi au mdalasini au mchaichai.

Chai ya rangi na kahawa vina kaffeina ambayo kwanza huyasukuma maji nje ya mwili kwa haraka na kuuacha mwili bila kuwa na maji ya kutosha kwa ajili ya kazi zake.

Kaffeina pia ni madawa ya kulevya kundi la madawa yanayosisimua mwili (stimulants drugs).

5. Kutopata usingizi wa kutosha kila siku

Moja ya vitu vinaweza kukupelekea kuwa na sumu mwilini au takataka nyingi ni pamoja na kutokulala muda wa kutosha kila siku. Usingizi haukopwi na huwezi kuwa na ufanisi katika kazi zako kama hupati usingizi wa kutosha kila siku.

Usingizi siyo jambo la starehe tu, ni sehemu mhimu sana katika afya yako ya kila siku.

Bila kupata usingizi wa kutosha unaweza kuwa karibu na matatizo kama kuongezeka uzito, kushuka kwa kinga ya mwili na nguvu zako za mwili kwa ujumla zinaweza kushuka.

Unapopata muda wa kutosha wa kulala masaa 7 mpaka 8 kwa siku unaupa mwili wako nafasi ya kutosha ya kupumzika na kujiripea upya na hivyo ndivyo sumu na takataka nyingine zinavyoweza kukutoka kirahisi.

Ingia kulala mapema walau saa tatu usiku ingia kulala siyo unakaa unaangalia tamthiliya au mpira mpaka saa sita za usiku!

6. Mazingira tunayoishi

Kuna mazingira yanajulikana wazi kuwa ni vyanzo vya sumu mwilini. Maeneo ya migodi ya madini, maeneo yenye viwanda vingi, maduka yanayouza dawa za kilimo nk

Maeneo haya yanafaa kukaa mbali na makazi ya binadamu kwa usalama wa afya zetu.

7. Vyakula vilivyokobolewa

Ili kuwa na mwili msafi kabisa epuka kula mkate mweupe, sukari na vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi kama vile chipsi, maandazi na vingine vyote vinavyochomwa katikati ya mafuta mengi.

Mkate upo mkate mweusi (brown bread), sukari ipo asali mbichi, vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi unaweza kuamua kuwa unavioka (bake) au uvichemshe (boiling). Uchaguzi ni wako.

8. Mfadhaiko (stress)

Kile tayari unajuwa ni kuwa mfadhaiko au stress ni jambo baya kwa afya yako. Kile unatakiwa kujua kuanzia sasa ni kuwa ili kubaki na afya bora kabisa yenye TBS basi ukae mbali na stress.

Kama utaruhusu stress kutawala maisha yako basi ujuwe mwili wako hauwezi kufanya kazi zake vizuri ikiwemo ya kuondoa taka au sumu mbalimbali mwilini.

Stress peke yake inaweza kupelekea magonjwa mbalimbali mwilini zaidi ya 50. Unapokuwa na mfadhaiko mwili wako hauwezi kutoa taka nje kirahisi na kinga yako ya mwili inashuka matokeo yake unakuwa karibu na magonjwa mengine mengi.

Watu wengine wenye uelewa mdogo wakiwa na stress hukimbilia kutumia vilevi wakidhani zitapungua kumbe ndiyo wanazidi kuongeza tatizo bila kujua.

9. Dawa za kizungu

Dawa nyingi za hospitali huwa zina matokeo chanya (positive) na matokeo hasi (negative) pia ambayo ndiyo matokeo mabaya.

Kama unalazimika kutumia antibiotic kila mara au unameza dawa za kuondoa maumivu kila mara unaweza kuwa unaongeza sumu na taka mwilini bila kujua na bila sababu yoyote ya lazima.

Kuepuka hilo jaribu kutumia mitishamba au mimea ya asili kwa baadhi ya magonjwa ambayo si lazima uende hospitali. Siyo mafua tu mtu ameenda kuchoma sindano!

10. Vilevi

Moja ya vitu vinavyoweza kuleta sumu au taka mwilini moja kwa moja ni vilevi. Vilevi kama pombe, madawa ya kulevya, sigara, bangi na vinginevyo ni vitu vinavyopelekea mwili kuwa na taka moja kwa moja.

Namna pekee ya kuondoa sumu kutokana na vilevi ni kuviacha hivyo vilevi, ndiyo kuviacha.

Usitegemee asubuhi utumie dawa kuondoa sumu mwilini halafu jioni ukanywe pombe au ukavute sigara utegemee tu ile dawa uliyotumia asubuhi kwamba itafanya kazi, hapana unajidanganya, dawa ni kuacha vilevi moja kwa moja.

Vingine vya kuacha kama tayari imegundulika una sumu nyingi mwilini ni pamoja na vinywaji baridi vyote, juisi zote za dukani, chai ya rangi na kahawa.

Dawa ya kutoa sumu mwilini > Unga wa majani ya Mlonge

jinsi ya kutoa sumu mwilini

Unga wa majani ya mlonge ndiyo dawa pekee ya asili ya uhakika ya kuondoa sumu mwilini.

Hii ni orodha ya viondoa sumu (antioxidants) 46 na zaidi vipatikanavyo katika mlonge:

Antioxidants (9, 11, 12, 13, 14, 15)

  1. β-carotene
  2. calcium
  3. potassium
  4. quercetin
  5. chlorogenic acid
  6. hydroxyanisole (BHA)
  7. butylated hydroxytoluene (BHT)
  8. tertiary-butylhydroquinones
  9. propyl gallate
  10. vitamin E (tocopherols)
  11. ascorbic acid (vitamin C)
  12. glucose oxidase
  13. reduced glutathione
  14. citric acid
  15. polyphospages
  16. aminopolycarboxylic acids
  17. vanillin
  18. moringine
  19. strophantidin
  20. 4-(α-l-rhamnosyloxy)
  21. benzyl isothiocyanate
  22. 4-(4’-O-acetyl-α-l-rhamnosyloxy)
  23. benzyl isothioyanate
  24. catechin
  25. 4-(β-d-glucopyranosyl-1→4-α-l-rhamnopyranosyloxy)
  26. benzyl thiocarboxamide
  27. epicatechin
  28. 4-O-(α-l-rhamnosyloxy)
  29. benzyl glucosinolate
  30. 4-(α-l-rhamnopyranosyloxy)-benzylglucosinolate
  31. Kaempferol
  32. Niazimicin
  33. 4-(α-l-rhamnosyloxy)
  34. benzyl acetonitrile (niazirin)
  35. O-ethyl-4-(α-l-rhamnosyloxy)
  36. benzyl carmate
  37. Gallic acid
  38. Glycerol-1-1-(9-octadecanoate)
  39. p-Coumaric acid
  40. 3-O-(6’-O-oleoyl-β-d-glucopyranosyl)-β-sitosterol
  41. Ferulic acid
  42. β-sitosterol-3-O-β-d-glucopyranoside
  43. Caffeic acid
  44. 3-Hydroxy-4-(α-l-rhamnopyranosyloxy)
  45. benzyl glucosinolate
  46. Protocatechuic acid
  47. 4-(2/3/4′-O-acetyl-α-l-rhamnopyranosyloxy)
  48. benzyl glucosinolate
  49. cinnamic acid
  50. glucosinalbin
  51. ellagic acid
  52. glucoraphanin
  53. glucoiber

Mlonge unasafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele.

Mlonge una Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe. Mlonge UNA MADINI YA CHUMA MARA 25 ZAIDI YA ILE ILIYOMO KWENYE SPINACHI

Changanya matunda yote na mboga za majani zote bado viinilishe vyake kwa pamoja haviwezi kuvifikia vile vilivyomo kwenye mlonge!

Ni kusema mtu aliyekula matunda na mboga za majani zote bado hatakuwa na afya bora kama yule atakayetumia mlonge tu.

*Usitumie dawa hii bila uangallizi wa karibu wa Tabibu.

Kama unahitaji unga wa majani ya mlonge kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Unga wangu wa majani ya mlonge ni mzuri na naweza kusema pasipo na hofu kuwa huwezi kupata sehemu nyingine wenye ubora unaokaribia na wangu. Ninauandaa kwa umakini mkubwa ili ubaki na viinilishe vyake na ni wa kijani kweli kweli

Imesomwa mara 8

Let's block ads! (Why?)

Jumamosi, 8 Februari 2020

Ugonjwa wa mshipa wa ngiri

UGONJWA WA MSHIPA WA NGIRI

Ngiri hujulikana pia kama “Hernia” kwa Kiingereza.

Ugonjwa wa mshipa wa ngiri ni matokeo anayopata mtu kutokana na misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi na kupelekea viungo hivyo kutoshikiliwa vizuri katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Tunaweza kuufahamu zaidi ugonjwa wa ngiri kama hali inayotokea katika mwili ambapo sehemu fulani ya nyama ya viungo mbalimbali vya mwili hujipenyeza kupitia sehemu iliyo dhaifu ya mwili na kutokeza upande wa pili.

Sehemu inayoathiriwa mara nyingi ni maeneo ya tumbo, kokwa, pumbu na kadhalika ambapo baadhi ya viungo vya mwili vilivyomo tumboni hujipenyeza kupitia vitundu vinavopitisha mishipa ya fahamu inayohudumia kokwa (Spesmatic Cord), hivyo baada ya kujipenyeza huteremka hadi ndani ya korodani hali ambayo hukamilisha kuwepo kwa ugonjwa wa mshipa wa ngiri.

Sehemu ambazo Ngiri inaweza kutokea ni pamoja na maeneo ya:
*Tumboni
*Eneo la kinena
*Eneo la paja kwa juu
*eneo ambalo mtu amewahi kufanyiwa upasuaji siku za nyuma
*Kifuani nk

Ugonjwa huu wa ngiri unawapata watu wa jinsia zote na wa umri wowote.

Aina za Ngiri:
Ugonjwa wa mshipa wa ngiri unaweza kujitokeza maeneo mbalimbali ya mwili na aina ya ngiri hutegemea na sehemu ngiri ilipojitokeza.

*Ngiri maji – Hii ni aina ya ngiri ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama (hydrocele)

*Ngiri kavu (Hernia) – hujulikana pia kama ‘fermoral hernia’ kwa wanawake na huitwa ‘scrotal hernia’ kwa wanaume

*Ngiri ya kwenye kifua – hujulikana pia kitaalamu kama ‘hiatus hernia’

*Ngiri ya tumbo – hujulikana pia kama ‘Abdominal Hernia’

*Ngiri ya kwenye kitovu – hujulikana pia kama ‘Umbilical Hernia”

*Ngiri ya sehemu ya haja kubwa – hujulikana pia kama ‘Anal Hernia’

Tutaangalia aina nyingine zaidi za ngiri na maelezo yake katika masomo yanayofuata.

Dalili za aina zote za ngiri hazitofautiani sana na ngiri hujitokeza bila maumivu yoyote ingawa kuna baadhi ya ngili hua na maumivu makali hutegemea ngiri ilivotokeza.

Somo litaendelea ….

Je unaumwa ugonjwa wa ngiri? unaweza kuniambia baadhi ya dalili au maumivu unayoyapata? je unaweza kuniambia dawa gani ulitumia kupona ugonjwa huu?

Tafadhari Share kwa ajili ya wengine

Imesomwa mara 5

Let's block ads! (Why?)

[unable to retrieve full-text content]

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...