Translate

Jumamosi, 8 Februari 2020

Ugonjwa wa mshipa wa ngiri

UGONJWA WA MSHIPA WA NGIRI

Ngiri hujulikana pia kama “Hernia” kwa Kiingereza.

Ugonjwa wa mshipa wa ngiri ni matokeo anayopata mtu kutokana na misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi na kupelekea viungo hivyo kutoshikiliwa vizuri katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Tunaweza kuufahamu zaidi ugonjwa wa ngiri kama hali inayotokea katika mwili ambapo sehemu fulani ya nyama ya viungo mbalimbali vya mwili hujipenyeza kupitia sehemu iliyo dhaifu ya mwili na kutokeza upande wa pili.

Sehemu inayoathiriwa mara nyingi ni maeneo ya tumbo, kokwa, pumbu na kadhalika ambapo baadhi ya viungo vya mwili vilivyomo tumboni hujipenyeza kupitia vitundu vinavopitisha mishipa ya fahamu inayohudumia kokwa (Spesmatic Cord), hivyo baada ya kujipenyeza huteremka hadi ndani ya korodani hali ambayo hukamilisha kuwepo kwa ugonjwa wa mshipa wa ngiri.

Sehemu ambazo Ngiri inaweza kutokea ni pamoja na maeneo ya:
*Tumboni
*Eneo la kinena
*Eneo la paja kwa juu
*eneo ambalo mtu amewahi kufanyiwa upasuaji siku za nyuma
*Kifuani nk

Ugonjwa huu wa ngiri unawapata watu wa jinsia zote na wa umri wowote.

Aina za Ngiri:
Ugonjwa wa mshipa wa ngiri unaweza kujitokeza maeneo mbalimbali ya mwili na aina ya ngiri hutegemea na sehemu ngiri ilipojitokeza.

*Ngiri maji – Hii ni aina ya ngiri ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama (hydrocele)

*Ngiri kavu (Hernia) – hujulikana pia kama ‘fermoral hernia’ kwa wanawake na huitwa ‘scrotal hernia’ kwa wanaume

*Ngiri ya kwenye kifua – hujulikana pia kitaalamu kama ‘hiatus hernia’

*Ngiri ya tumbo – hujulikana pia kama ‘Abdominal Hernia’

*Ngiri ya kwenye kitovu – hujulikana pia kama ‘Umbilical Hernia”

*Ngiri ya sehemu ya haja kubwa – hujulikana pia kama ‘Anal Hernia’

Tutaangalia aina nyingine zaidi za ngiri na maelezo yake katika masomo yanayofuata.

Dalili za aina zote za ngiri hazitofautiani sana na ngiri hujitokeza bila maumivu yoyote ingawa kuna baadhi ya ngili hua na maumivu makali hutegemea ngiri ilivotokeza.

Somo litaendelea ….

Je unaumwa ugonjwa wa ngiri? unaweza kuniambia baadhi ya dalili au maumivu unayoyapata? je unaweza kuniambia dawa gani ulitumia kupona ugonjwa huu?

Tafadhari Share kwa ajili ya wengine

Imesomwa mara 5

Let's block ads! (Why?)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...