Translate

Alhamisi, 12 Septemba 2019

31-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kumtii Yeye Ni Sawa Na Kumtii Allaah

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

31-Kumtii Yeye Ni Sawa Na Kumtii Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):  

 

مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ﴿٨٠﴾

Atakayemtii Rasuli basi kwa yakini amemtii Allaah. Na atakayekengeuka basi Hatukukutuma kuwa mlinzi juu yao. [An-Nisaa: 80]

 

Na katika Hadiyth:

عَنْ أبي هُرَيْرة رضى الله عنه  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ مَنْ أَطَاعَنِي فَقَدْ أَطَاعَ اللَّهَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ عَصَى اللَّهَ، وَمَنْ أَطَاعَ أَمِيرِي فَقَدْ أَطَاعَنِي، وَمَنْ عَصَى أَمِيرِي فَقَدْ عَصَانِي ‏"‏‏.‏

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  amehadithia kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayenitii basi atakuwa amemtii Allaah, na atakayeniasi atakuwa amemuasi Allaah, na atakayemtii Amiri wangu (kiongozi niliyemteua), atakuwa amenitii mimi na atakayemuasi atakuwa ameniasi mimi)) [Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy, Ibn Maajah]

 

 Na katika Hadiyth nyengine:

 

عن عبدالله بن عمر رضي الله عنه أنه كان يومًا من الأيامِ عندَ رسولِ اللهِ صلَّى اللهُ عليهِ وسلمَ وهو في نفرٍ من أصحابِه فقال: ((ألستم تعلمون أنِّي رسولُ اللهِ؟)) قالوا: "بلى يا رسولَ اللهِ نشهدُ أنك رسولُ اللهِ" قال: ((ألستم تعلمونَ أن اللهَ تعالَى أنزلَ في كتابِه أنَّ مَن أطاعَني فقد أطاع اللهَ؟)) قالوا: "بلى نشهدُ أن مَن أطاعَك فقد أطاع اللهَ" قال: ((فإنَّ مِن طاعتي أن تطيعوا أئمَّتَكم فإن صلُّوا قُعودًا فصلُّوا قُعودًا))

‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba siku moja alikuwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) pindi alipokuwa na baadhi ya Maswahaba akasema: ((Je si mnajua kuwa mimi ni Rasuli wa Allaah?)) Wakasema: “Bila shaka ee Rasuli wa Allaah tunashuhudia kuwa wewe ni Rasuli wa Allaah.”  Akasema: ((Je, si mnajua kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Ameteremsha katika Kitabu Chake kuwa “Atakayenitii mimi atakuwa amemtiia Allaah?” Wakasema: “Bila shaka tunashuhudia kuwa atakayekutii wewe atakuwa amemtii Allaah.” Akasema: ((Miongoni mwa kunitii ni Imaam wenu wanaposwali wakiwa wamekaa kitako, basi nanyi mswali kwa kukaa kitako)) [Musnad Ahmad ni Hadiyth Swahiyh taz Asw-Swahiyh Al-Musnad, (761), na riwaayah nyengine Taz Swahiyh Ibn Hibbaan (2109), Swiffatusw-Swalaah ya Al-Albaaniy (1/87)]

 

 

 



31-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake: Akiwahudumia Maswahaba Kama Kuwamiminia Maji Ya Kunywa

 

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

31-Unyenyekevu Wake: Akiwahudumia Maswahaba

Kama Kuwamiminia Maji Ya Kunywa

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Hadiyth ndefu ya Abuu Qataadah kuhusu kisa cha kupitiwa kwao na usingizi Alfajiri …..

 

 

قَالَ: فَانْتَهَيْنَا إِلَى النَّاسِ حِينَ امْتَدَّ النَّهَارُ وَحَمِيَ كُلُّ شَىْءٍ وَهُمْ يَقُولُونَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ: هَلَكْنَا عَطِشْنَا ‏.‏ فَقَالَ: ‏"‏لاَ هُلْكَ عَلَيْكُمْ"‏ ‏.‏ ثُمَّ قَالَ: ‏"‏أَطْلِقُوا لِي غُمَرِي"‏ .‏ قَالَ: وَدَعَا بِالْمِيضَأَةِ فَجَعَلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَصُبُّ وَأَبُو قَتَادَةَ يَسْقِيهِمْ فَلَمْ يَعْدُ أَنْ رَأَى النَّاسُ مَاءً فِي الْمِيضَأَةِ تَكَابُّوا عَلَيْهَا ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ‏"‏أَحْسِنُوا الْمَلأَ كُلُّكُمْ سَيَرْوَى‏"‏.‏ قَالَ: فَفَعَلُوا فَجَعَلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَصُبُّ وَأَسْقِيهِمْ حَتَّى مَا بَقِيَ غَيْرِي وَغَيْرُ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم – قَالَ: ثُمَّ صَبَّ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ لِي: "‏اشْرَبْ "‏‏.‏ فَقُلْتُ: لاَ أَشْرَبُ حَتَّى تَشْرَبَ يَا رَسُولَ اللَّهِ:  قَالَ: "‏إِنَّ سَاقِيَ الْقَوْمِ آخِرُهُمْ شُرْبًا‏"‏ ‏.‏ قَالَ: فَشَرِبْتُ وَشَرِبَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم  قَالَ: فَأَتَى النَّاسُ الْمَاءَ جَامِّينَ رِوَاءً

 

 …(Abuu Qaatadah) akasema:  “Basi tukaendelea mpaka tukawafikia watu (tulioawaacha nyuma), na mchana ukawa umetanda na kila kitu kilishika joto  nao (Maswahaba) wakasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Tumeangamia! Tumebanwa na kiu!” Akasema:  ((Hamtaangamia)) Kisha akasema: ((Nipeni kikombe kodogo changu)).  Kisha akaomba aletewe jagi la maji. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaanza kumimina maji (katika kikombe kidogo) na Abuu Qaatadah akawa anawanyeshwa maji.  Watu walipoona kuwa kuna maji (kidogo) katika jagi, wakalielemea. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Tulieni! Maji yatakutosheni!)). Kisha (Maswahaba) wakaanza kupata (mgao wao) wa maji kwa utulivu (bila ya kudhihirisha kutapatapa) na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaanza kujaza (kifuniko) nami nikaanza kuwamiminia (maji) mpaka ikawa hakuna aliyebakia isipokuwa mimi na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Kisha akajaza (kikombe) maji na akaniambia: ((Kunywa!)) Nikamwambia: “Sitokunywa mpaka unywe wewe Ee Rasuli wa Allaah.” Akasema: ((Anayewamiminia watu hanywi mpaka wa mwisho wao amalize kunywa)). Nikanywa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanywa pia na watu wakafikia mahali pa maji wakiwa wanafuraha na kuridhika...    [Muslim]



096-Aayah Na Mafunzo: Masjid Al-Haraam Ni Ya Kwanza Kuanzishwa Duniani

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Masjid Al-Haraam Ni Ya Kwanza Kuanzishwa Duniani

Alhidaaya.com

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩٦﴾ 

Hakika nyumba ya awali iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ‘ibaadah) ni ile ambayo iko Bakkah (Makkah), yenye barakah na mwongozo kwa walimwengu. [Aal-'Imraan: 96]

 

Mafunzo:

 

Abuu Dharr (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Masjid gani ilijengwa ardhini mwanzo?  Akasema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Masjid Al-Haraam (Makkah).” Kisha nikasema: Kishaupi? Akasema: “Masjid Al-Aqswaa (Palestina).” Nikasema: Kuna muda gani baina ya kuwepo Masjid mbili hizo? Akasema: “Miaka arubaini na popote itakapokudiriki Swalaah basi swali hapo pia ardhi ni mahala pa kuswali.” [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 



049-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Hujuraat: 1

 

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

049-Al-Hujuraat: 1

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١﴾

Enyi walioamini! Msikadimishe (lolote) mbele ya Allaah na Rasuli Wake. Na mcheni Allaah; hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote. [Al-Hujuraat: 1]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

عن عبد الله بن زبير رضي الله عنه: قَدِمَ رَكْبٌ مِنْ بَنِي تَمِيمٍ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ: أَمِّرِ الْقَعْقَاعَ بْنَ مَعْبَدٍ‏.‏ وَقَالَ عُمَرُ: بَلْ أَمِّرِ الأَقْرَعَ بْنَ حَابِسٍ‏.‏ فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ: مَا أَرَدْتَ إِلَى ـ أَوْ إِلاَّ ـ خِلاَفِي‏.‏ فَقَالَ عُمَرُ: مَا أَرَدْتُ خِلاَفَكَ‏.‏ فَتَمَارَيَا حَتَّى ارْتَفَعَتْ أَصْوَاتُهُمَا، فَنَزَلَ فِي ذَلِكَ: ((‏يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَىِ اللَّهِ وَرَسُولِهِ‏))‏ حَتَّى انْقَضَتِ الآيَةُ‏.‏

Kundi la watu katika Bani Tamiyim walimjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) (kumtaka awateulie gavana wao). Abuu Bakr akasema: “Mteue Al-Qa’qaa’ bin Ma’bad.”  ‘Umar akasema: “Mteue Al-Aqra’ bin Haabis.” Hapo Abuu Bakr akamwambia (‘Umar). “Hukukusudia isipokuwa kunipinga mimi.” ‘Umar akasema: “Sikukusudia kukupinga.” Basi wawili hao wakabishana hadi sauti zao zikapanda juu, ndipo ikateremka:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١﴾

 

[Al-Bukhaariy]

 

 



031-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Du’aa Ya Malaika Kila Siku Kwa Mtoaji Sadaka Na Mzuiaji

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 31

 

Du’aa Ya Malaika Kila Siku Kwa Mtoaji Sadaka Na Mzuiaji

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَا مِنْ يَوْمٍ يُصْبِحُ الْعِبَادُ فِيهِ إلاَّ مَلَكَانِ يَنْزِلاَنِ فَيَقُولُ أَحَدُهُمَا: اللَّهُمَّ أَعْطِ مُنْفِقًا خَلَفًا. وَيَقُولُ الأَخَرُ: اللَّهُمَّ أَعْطِ مُمْسِكًا تَلَفًا)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Kila siku inayowapambaukia watu kuna Malaika wawili wanateremka, mmoja wao akiomba: Ee Allaah! Mwenye kutoa [sadaka] mlipe zaidi. Na mwengine huomba: Ee Allaah! Mwenye kuzuia mpe hasara)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Inapendekezeka kutoa sadaka kila siku ili kupata du’aa ya Malaika na kukhofu kuombewa hasara. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ ﴿٥﴾

Basi yule anayetoa (mali) na akamcha Allaah.

 

وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٦﴾

Na akasadikisha Al-Husnaa.

 

فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٧﴾

“Basi Tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi”

 

وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ ﴿٨﴾

Ama yule afanyaye ubakhili na akajiona amejitosheleza.  

 

وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٩﴾

Na akakadhibisha Al-Husnaa.

 

فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ ﴿١٠﴾

Na Tutamuwepesishia kwa yaliyo magumu.

 

وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّىٰ ﴿١١﴾

Na itamsaidia nini mali yake atakapoporomoka kuangamia (motoni).  [Al-Layl (92: 5-11)]

 

 

 

2. Allaah (سبحانه وتعالى) Ametoa ahadi kumwongezea mwenye kutoa mali yake. Rejea: Al-Baqarah (2: 245, 261), Al-Hadiyd (57: 11), Sabaa (34: 39).

 

 

3. Inafaa kumuombea mtoaji sadaka, Allaah (سبحانه وتعالى) Amlipe zaidi kwa alichotoa, na du’aa kwa bakhili anayezuia kutoa katika Njia ya Allaah  (سبحانه وتعالى) hasara panapohitajika.

 

 

4. Sadaka ni katika ‘amali bora kabisa mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى), kwani Ameitaja sana katika Qur-aan na hata kwamba Ameitanguliza kabla ya nafsi katika Aayah za Jihaad.

 

Rejea: An-Nisaa (4: 95), At-Tawbah (9: 20, 41, 81), Al-Hujuraat (49: 15), As-Swaff (61: 11).

 

 

5. Fadhila tele za kutoka sadaka katika Qur-aan na Sunnah. Rejea Hadiyth namba (32), (62).



Alhamisi, 5 Septemba 2019

30-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ummah Wake Utakuwa Wa Kwanza Kuhukumiwa Siku Ya Qiyaamah

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

30-Ummah Wake Utakuwa Wa Kwanza Kuhukumiwa Siku Ya Qiyaamah

www.alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، وَعَنْ رِبْعِيِّ بْنِ حِرَاشٍ، عَنْ حُذَيْفَةَ، قَالاَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ أَضَلَّ اللَّهُ عَنِ الْجُمُعَةِ مَنْ كَانَ قَبْلَنَا فَكَانَ لِلْيَهُودِ يَوْمُ السَّبْتِ وَكَانَ لِلنَّصَارَى يَوْمُ الأَحَدِ فَجَاءَ اللَّهُ بِنَا فَهَدَانَا اللَّهُ لِيَوْمِ الْجُمُعَةِ فَجَعَلَ الْجُمُعَةَ وَالسَّبْتَ وَالأَحَدَ وَكَذَلِكَ هُمْ تَبَعٌ لَنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ نَحْنُ الآخِرُونَ مِنْ أَهْلِ الدُّنْيَا وَالأَوَّلُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ الْمَقْضِيُّ لَهُمْ قَبْلَ الْخَلاَئِقِ ‏"‏ ‏.‏ وَفِي رِوَايَةِ وَاصِلٍ الْمَقْضِيُّ بَيْنَهُمْ ‏.‏

  

Kutoka kwa Abuu Hurayrah na Abuu Rib-‘iyy bin Hiraash kutoka kwa Hudhayfah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ilikuwa ni Ijumaa ambayo Allaah Aliigeuza kutoka kwa walio kabla yetu. Mayahudi wakawa na Siku ya Jumamosi na Manaswara Siku ya Jumapili. Allaah Akatuletea na kutongoza sisi Siku ya Ijumaa (siku tukufu ya Swalaah ya jamaah) Akajaalia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili (kuwa ni siku tukufu). Kwa utaratibu huu wao (Mayahudi na Manaswara) watakuja baada yetu Siku ya Qiyaamah. Sisi (ni Ummah) wa mwisho katika watu wa dunia, lakini wa kwanza miongoni mwa viumbe kuhukumiwa Siku ya Qiyaamah)) na katika riwaayah nyengine:  ((Kuhukumiwa miongoni mwao)) [Al-Bukhaariy]

 



30-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):Unyenyekevu Wake: Akiwafundisha Maswahaba Fadhila Za Unyenyekevu Kuwa Unapandisha Daraja

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

30-Unyenyekevu Wake:

Akiwafundisha Maswahaba Fadhila Za Unyenyekevu Kuwa Unapandisha Daraja   

www.alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَا نَقَصَتْ صَدَقَةٌ مِنْ مَالٍ،  وَمَا زَادَ اللَّهُ عَبْدًا بِعَفْوٍ إلاَّ عِزًّا، وَمَا تَوَاضَعَ أَحَدٌ لِلَّهِ إِلاَّ رَفَعَهُ اللَّهُ عَزَّ وَ جَلَّ)) مسلم

                                                                                

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Kutoa sadaka hakupunguzi mali, Allaah Humzidishia mja ‘izzah (utukufu) kwa ajili ya kusamehe kwake.  Na   yeyote anayenyenyekea kwa ajili ya Allaah, Allaah Aliyetukuka Atampandisha Daraja [Atamtukuza].  [Muslim]

 



20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...