Translate

Alhamisi, 29 Agosti 2019

091-Aayah Na Mafunzo: Mtu Wa Motoni Atatamani Kufidia Dhahabu Ya Ujazo Wa Duniani

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Mtu Wa Motoni Atatamani Kufidia Dhahabu Ya Ujazo Wa Duniani

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Taa'alaa):

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٩١﴾

91. Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi haitakubaliwa kutoka kwa mmoja wao dhahabu ya ujazo wa dunia nzima lau wakitaka kujifidia nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata mwenye kuwanusuru.

 

 

Mafunzo:

 

Anas (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ataitwa mtu katika watu wa Jannah, kisha Allaah Atamuuliza: Ee mwana Aadam! Umeonaje makazi yako? Atasema: Yaa Rabb! Hakika ni makazi bora kabisa. Allaah Atasema: Omba na tamani (utakalo)! Atasema: Hakuna ninaloomba au kutamani isipokuwa Unirudishe duniani nipigane katika njia Yako mara kumi – kutokana fadhila anazoziona za waliokufa mashahidi. Kisha ataletwa mtu katika watu wa motoni Atasema: Ee mwana Aadam! Umeonaje makazi yako? Atasema: Yaa Rabb! Makazi maovu kabisa! Atasema: Je, unataka kufidia Kwangu dhahabu kwa ujazo wa dunia nzima? Atasema: Naam ee Rabbi! Atasema: Umeongopa! Kwani Nilikuomba la chini kuliko hilo na jepesi zaidi wala hukufanya! Atarudishwa motoni.” [Ahmad, As-Silsilah Asw-Swahiyhah (3008), Swahiyh Al-Jaami’ (7996)].

 

 



Asbaabun-Nuzuwl: Al-Qamar: 1- 2

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

054-Al-Qamar Aayah 1 -2

 

 

 

Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى):

اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿١﴾

Saa imekaribia na mwezi umepasuka. 

 

وَإِن يَرَوْا آيَةً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ ﴿٢﴾

Na wanapoona Aayah (ishara, dalili) hukengeuka na husema: Sihiri inayoendelea [Al-Qamar: 1-2]

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

 

عَنْ أَنَسٍ، قَالَ سَأَلَ أَهْلُ مَكَّةَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم آيَةً فَانْشَقَّ الْقَمَرُ بِمَكَّةَ مَرَّتَيْنِ فَنَزَلَت: ((‏اقتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانْشَقَّ الْقَمَرُ))  إِلَى قَوْلِهِ ‏:‏ ‏ ((‏سحْرٌ مُسْتَمِرٌّ))  يَقُولُ ذَاهِبٌ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ ‏.

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kwamba watu wa Makkah walimuomba  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) awaletee Aayah (Ishara, muujiza), basi mwezi ukapasuka Makkah mara mbili (Yaani sehemu mbili), kisha ikateremka:

 

اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿١﴾

Saa imekaribia na mwezi umepasuka

 

Mpaka kauli Yake:

  سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ  

Sihiri inayoendelea [Al-Qamar: 1-2]

 

Yaani Sihiri (Uchawi) inayootoweka.

[Amesema Abuu ‘Iysaa (at-Tirmidhiy) Hii ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 
 

Pia,

 

 عن ابن عباس رضي الله عنهما قال كسف القمر على عهد رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم فقالوا: سحر القمر، فنزلت ((اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانْشَقَّ الْقَمَرُ، وَإِنْ يَرَوْا آيَةً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْرٌ مُسْتَمِرٌّ))  

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba mwezi ulipatwa katika zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) basi (makafiri) wakasema: “Sihiri (uchawi) unaoendelea.”  Ikateremka:

 

اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿١﴾

Saa imekaribia na mwezi umepasuka. 

 

وَإِن يَرَوْا آيَةً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ ﴿٢﴾

Na wanapoona Aayah (ishara, dalili) hukengeuka na husema: Sihiri inayoendelea [Al-Qamar: 1-2]

 

[Atw-Twabaraniy na Al-Haafidhw Ibn Kathiyr amesema katika Al-Bidaayah Wan-Nihaayah:  Isnaad yake ni Jayyid]

 



029-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Aliyekamilika Iymaan Kwa Tabia Na Kumfanyia Wema Mke

 

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 29

 

Aliyekamilika Iymaan Kwa Tabia Na Kumfanyia Wema Mke

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا  وَخِيَارُكُمْ خِيَارُكُمْ لِنِسَائِهِمْ خُلُقًا)) الترمذي وقال: حديث حسن صحيح

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muumin aliyekamilika iymaan ni aliye na tabia njema kabisa, na wabora wenu ni walio bora kwa wake zao kwa tabia))  [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Swahiyh Hasan]

 

 

 

Mafunzo na Mwongozo:

 

 

1. Uislamu unasisitiza kuwa na tabia njema kwa kila mtu.

 

 

 

2. Mume anasisitizwa kumfanyia wema mkewe katika maisha ya ndoa, si kumfanyia uovu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

وَلَا تَنسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ   

  Na wala msisahau fadhila baina yenu.  [Al-Baqarah (2: 237)]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

  وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ  

Na kaeni nao kwa wema. [An-Nisaa (4: 19)]

 

 

Pia rejea kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): [Ar-Ruwm 30: 21]

 

 

3. Inapasa kuweko subira baina ya mume na mke katika mitihani inayowakabili ya maisha baina yao. [((Na mkisubiri ni kheri kwenu)) [An-Nisaa (4: 25)].

 

 

 

4. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kigezo bora kabisa katika kuamiliana na wake [Al-Ahzaab (33: 21)].

 

Pia Hadiyth zifuatazo:

 

 

 ((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa mke wake, na mimi ni mbora kwa watu wangu wa nyumbani [ahli])) [Ibn Maajah na Ad-Daarimiy].

 

 

((Mwanamke ameumbwa kwa ubavu, na sehemu iliyopinda ya ubavu ni juu yake, ukijaribu kuunyoosha utauvunja, na lau utauacha utaendelea kupinda, nakuusieni [kuwafanyia wema]) wake zenu)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

((Allaah, Allaah, kwa wanawake,  hao ni wasaidizi wenu walio kwenye mikono yenu, mmewachukuwa kama ni amana kutoka kwa Allaah, na imekuwa halali tupu zao kwenu kwa neno lake Allaah  [iyjaab na qubuwl])) [Muslim, Abu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad]

 

Rejea pia Hadiyth namba (28), (35), (40).

 

 



29-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Rasuli Pekee Atakayeruhusiwa Ash-Shafaa'ah Ummah Wake

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

29-Rasuli Pekee Atakayeruhusiwa Ash-Shafaa'ah (Uombezi) Kwa Ummah Wake

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atakuwa Rasuli pekee atakayekubaliwa ash-shafaa'ah yake (uombezi) Siku ya Qiyaamah.  Atakapokuwa amesujudu kisha ataamrishwa kuinuka na kuomba ash-shafaa'ah:

  

 

عَنْ أَنَسٍ ، رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى الله عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ، قَالَ يَجْتَمِعُ المُؤْمِنُونَ يَوْمَ القِيَامَةِ فَيَقُولُونَ : لَوِ اسْتَشْفَعْنَا إلى رَبِّنَا ، فَيَأْتُونَ ادَمَ ، فَيَقُولُونَ : أَنْتَ أَبو النَّاسِ ، خَلَقَكَ اللهُ بِيَدِهِ ، وَأَسْجَدَ لَكَ مَلائِكَتَهُ ، وَعَلَّمَكَ أَسْماءَ كُلِّ شَيْءٍ ، فاشْفَعْ لَنا عِنْدَ رَبِّكَ ، حَتَّى يُرِيحَنا مِنْ مَكَانِنا هَذا ، فَيَقُولُ : لَسْتُ هُنَاكُمْ ـ وَيَذْكُرُ ذَنْبَهُ ، فَيَسْتَحْيي ـ ائْتُوا نُوحاً ؛ فَإِنَّهُ أَوَّلُ رَسُولٍ بَعَثَهُ اللهُ إِلي أَهْلِ الأَرْض ، فَيَأْتُونَهُ ، فَيَقُولُ : لَسْتُ هُنَاكُمْ ـ ويَذْكُرُ سُؤالَهُ رَبَّهُ مَا لَيْسَ لَهُ بِهِ عِلْمٌ ، فَيَسْتَحْيي ـ فَيَقُولُ : اؤْتُوا خَلِيلَ الرَّحْمنِ ، فَيَأْتُونَهُ ، فَيَقُولُ : لَسْتُ هُنَاكُم ، اؤْتُوا موسى ، عَبْداً كَلَّمَهُ اللهُ ، و أَعْطَاهُ التَّوْرَاةَ . فَيَأْتُونَهُ ، فَيَقُولُ : لَسْتُ هُنَاكُمْ ـ وَيَذْكُرُ قَتْلَ النَّفْسِ بِغَيْرِ نَفْسٍ ، فَيَسْتَحْيي مِنْ رَبِّهِ ـ فَيَقُولُ : اؤْتُوا عِيسَى ، عَبْدَ اللهِ وَرَسُولَهُ ، وَكَلِمَةَ اللهِ وَرُوحَهُ . فَيَأْتُونَهُ ، فَيَقُولُ : لَسْتُ هُنَاكُمْ ، اؤْتُوا مُحَمَّداً ، ـ صَلَّى الله عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ـ عَبْداً غَفَرَ اللهُ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ وَمَا تَأَخَّرَ ، فَيَأْتُونَنِي ، فَأَنْطَلِقُ حَتَّي أَسْتَأْذِنَ عَلَي رَبِّي فَيُؤْذَنُ . فإذا رَأَيْتُ رَبِّي وَقَعْتُ سَاجداً ، فَيَدَعُني مَا شَاءَ اللهُ ، ثُمَّ يُقَالُ : ارْفَعْ رَأْسَكَ ، وسَلْ تُعْطَهُ ، وَقُلْ يُسْمَعْ ، واشْفَعْ تُشَفَّعْ . فَأَرْفَعُ رَأْسي ، فَأَحْمَدُهُ بِتَحْمِيدٍ يُعَلِّمُنِيهِ ، ثُمَّ أَشْفَعُ ، فَيحُدُّ لي حَدّاً ، فَأُدْخِلُهُمْ الجَنَّةَ . ثُمَّ أَعُودُ إِلَيْهِ ، فإِذا رَأَيْتُ رَبِّي ( فَأَقَعُ ساجداً ) مِثْلَهُ ، ثُمَّ أَشْفَعُ فَيَحُدُّ لِي حَدّاً ، فَأُدْخِلُهُمُ الجَنَّةَ . ثُمَّ أَعُودُ الثالِثةَ ، ثُمَّ أَعُودُ الرَّابعة ، فَأقُولُ : مَا بَقِي في النَّارِ إِلَّا مَنْ حَبَسَهُ القُرْانُ ، ووَجَبَ عَلَيْهِ الخُلُودُ

 

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Watakusanyika Waumini Siku ya Qiyaamah na Watasema: Lau tungetafuta kuombewa shafaa’ah kwa Rabb wetu! Watakwenda kwa Aadam na watasema: Wewe ndio baba wa watu, Amekuumba Allaah kwa Mikono Yake na Akaamrisha Malaika wakusujudie, na Akakufundisha majina ya vitu vyote, basi tuombee kwa Rabb wako ili Atupe faraja kutokana na sehemu yetu hii? Atasema: Mimi siwezi kufanya mnaloomba! Na atakumbuka makosa yake na ataona hayaa, atasema: Mfuateni Nuwh, hakika yeye ndiye Rasuli wa kwanza Aliyemtuma Allaah kwa watu ardhini. Watamfuata. Naye atasema: Siwezi kufanya mnaloomba! Na atakumbuka kumuomba kwake Allaah kwa jambo asilokuwa nalo ujuzi.  Naye ataona hayaa na atasema: Nendeni kwa Khaliylur-Rahmaan. Watakwenda kwa Ibraahiym. Naye atawaambia: Siwezi kufanya mnaloomba! Nendeni kwa Muwsaa mja ambaye Allaah Alizungumza naye na Akampa Tawraat. Muwsaa atasema: Siwezi kufanya mnaloomba!  Atakumbuka kuwa aliwahi kumuua mtu bila ya haki na ataona hayaa kwa Rabb wake.  Atasema: Nendeni kwa ‘Iysaa kwani ni mja wa Allaah na Rasuli Wake na neno Lake na Roho Yake. Naye atasema: Siwezi kufanya mnaloomba! Nendeni kwa Muhammad, ni mja aliyefutiwa makosa yaliyotangulia na yajayo. Watakuja kwangu na nitakwenda kwa Rabb wangu kumuomba idhini (ya maombi), nitapewa idhini. Nitakapomuona Rabb wangu nitasujudu na Ataniacha hivyo hivyo mpaka Atakavyo. Kisha itasemwa: Inua kichwa chako na omba utapewa! Na sema yatasikilizwa (uyasemayo)! Na omba shafaa‘ah (uombezi) utapewa! Nitainua kichwa changu na nitamhimidi kwa Himdi Zake Atakazonifundisha, kisha nitaomba na Atanikubalia idadi kubwa ya watu, nitawaingiza Jannah. Kisha nitarudi tena Kwake. Nitakapomuona Rabb wangu, nitafanya kama mara ya kwanza, kisha nitaomba na Atanikubalia idadi kubwa ya watu nitawaingiza Jannah. Kisha nitarejea mara ya tatu, kisha nitarudi mara ya nne kisha nitasema: Hakuna watu waliobakia motoni isipokuwa Qur-aan imewazuia na watawajibika kubakia humo.” [Al-Bukhaariy (4476)]

 

Na  Hadiyth ifuatayo kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atakuwa na du’aa makhsusi ya kuombea Ummah wake ash-shafaa’ah (uombezi): 

 

عن أبي هريرة رَضِيَ اللَّهُ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ لِكُلِّ نَبِيٍّ دَعْوَةٌ، فَأُرِيدُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ أَنْ أَخْتَبِيَ دَعْوَتِي شَفَاعَةً لأُمَّتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ ‏"‏‏.‏

Kutoka kwa Abuu Huraryah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kila Nabiy na du’aa inayotaqabailiwa, nami nataka In Shaa Allaah nihifadhi du'aa yangu kwa ajili ya kuwaonbea shafaa'ah (uombezi) Ummah wangu Siku ya Qiyaamah)) [Al-Bukhaariy]

 

 Na pia:

 

عَنْ آدَمَ بْنِ عَلِيٍّ، قَالَ سَمِعْتُ ابْنَ عُمَرَ، رضى الله عنهما يَقُولُ إِنَّ النَّاسَ يَصِيرُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ جُثًا، كُلُّ أُمَّةٍ تَتْبَعُ نَبِيَّهَا، يَقُولُونَ يَا فُلاَنُ اشْفَعْ، حَتَّى تَنْتَهِيَ الشَّفَاعَةُ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَذَلِكَ يَوْمَ يَبْعَثُهُ اللَّهُ الْمَقَامَ الْمَحْمُودَ‏.‏

 Kutoka kwa Aadam bin ‘Aliy ambaye amesema: Nilimsikia Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) akisema: “Siku ya Qiyaamah, watu wataangukia kupiga magoti na kila Ummah utafuata Nabiy wake wakisema: “Ee fulani tuombee ash-shafaa’ah (uombezi)!” Mpaka shafaa’ah (ya hakika) itafika kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na hiyo ndiyo siku ambayo Allaah Atakayompandisha cheo kitukufu cha kusifiwa (Al-Maqaamah Al-Mahmuwdah).” [Al-Bukhaariy] 

 



29-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake: Aliwafunza Maswahaba Wawe Unyenyekevu Ili Wasifanyiane Ufidhuli Au Kujifakharisha

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

29-Unyenyekevu Wake Aliwafunza Maswahaba Wawe Unyenyekevu

Ili Wasifanyiane Ufidhuli Au Kujifakharisha

   

www.alhidaaya.com

 

 

 

 وَعَنْ عِيَاضِ بْنِ حِمَارٍ ‏  رضى الله عنه ‏- قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ   صلى الله عليه وسلم ‏  إِنَّ اَللَّهَ أَوْحَى إِلَيَّ أَنْ تَوَاضَعُوا, حَتَّى لَا يَبْغِيَ أَحَدٌ عَلَى أَحَدٍ, وَلَا يَفْخَرَ أَحَدٌ عَلَى أَحَدٍ } أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ .‏

 

‘Iyaadhw bin Himaar amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Ameniteremshia Wahyi kwamba (Nyinyi) muwe wanyenyekevu ili  msifanyianeni ufidhuli, wala msijifakharishe baina yenu)). [Muslim na wengineo]

 

 

 

 

 



Ijumaa, 23 Agosti 2019

28-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake: Hakukataa Kuhudumiwa Na Watumwa

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

28-Unyenyekevu Wake: Hakukataa Kuhudumiwa Na Watumwa   

www.alhidaaya.com

 

 

  عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا صَلَّى الْغَدَاةَ جَاءَ خَدَمُ الْمَدِينَةِ بِآنِيَتِهِمْ فِيهَا الْمَاءُ فَمَا يُؤْتَى بِإِنَاءٍ إِلاَّ غَمَسَ يَدَهُ فِيهَا فَرُبَّمَا جَاءُوهُ فِي الْغَدَاةِ الْبَارِدَةِ فَيَغْمِسُ يَدَهُ فِيهَا ‏.‏

 

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomaliza kuswali Alfajiri, watumwa wa Madiynah walikuja na vyombo vyao vya maji, basi hakimfikii chombo (cha maji) ila alitumbukiza mikono yake. Na mara nyengine huja asubuhi ya ubaridi mno (hata hivyo hakukataa kwa kupuuza ombi lao ila) alitumbukiza mkono wake.” [Muslim]

 



056-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Waaqi’ah: Aayah: 75-82

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

056-Al-Waaqi’ah: Aayah: 75-82

 

 

Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

 

فَلَا أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ ﴿٧٥﴾

Basi Naapa kwa maangukio ya nyota.

 

 

وَإِنَّهُ لَقَسَمٌ لَّوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ ﴿٧٦﴾

Na hakika hicho ni kiapo adhimu lau mngelijua.

 

 

إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ ﴿٧٧﴾

Hakika hii bila shaka ni Qur-aan tukufu.

 

 

فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ ﴿٧٨﴾

Katika Kitabu kilichohifadhiwa.

 

 

لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ ﴿٧٩﴾

Haigusi isipokuwa waliotakaswa kabisa.

 

 

تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٨٠﴾

Ni uteremsho kutoka kwa Rabb wa walimwengu.

 

 

أَفَبِهَـٰذَا الْحَدِيثِ أَنتُم مُّدْهِنُونَ ﴿٨١﴾

Je, kwa maneno haya nyinyi ni wenye kuikanusha na kuibeza?

 

 

وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ ﴿٨٢﴾

Na mnafanya badala (shukurani za) riziki zenu kuwa nyinyi mnakadhibisha.

 

 

وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ ﴿٨٢﴾

Na mnafanya badala (shukurani za) riziki zenu kuwa nyinyi mnakadhibisha. [Al-Waaqi’ah: 75-82]

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

 

عن ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ مُطِرَ النَّاسُ عَلَى عَهْدِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ أَصْبَحَ مِنَ النَّاسِ شَاكِرٌ وَمِنْهُمْ كَافِرٌ قَالُوا هَذِهِ رَحْمَةُ اللَّهِ ‏.‏ وَقَالَ بَعْضُهُمْ لَقَدْ صَدَقَ نَوْءُ كَذَا وَكَذَا ‏"‏ ‏.‏ قَالَ فَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ: ((‏فَلاَ أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ‏))‏ حَتَّى بَلَغَ ‏ ((وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ‏))

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba kulitokea mvua zama za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ambapo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: “Baadhi ya watu wamepambukiwa asubuhi wakiwa wenye kushukuru, na wengineo wenye kukufuru (kukosa shukurani kwa Allaah).” Walioshukuru walisema: “Hii ni Rahmah ya Allaah.” Na wale waliokufuru walisema: “Nyota kadhaa na kadhaa zimesadikisha.” Hapo ikateremka Aayah hii:

فَلَا أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ ﴿٧٥﴾

Basi Naapa kwa maangukio ya nyota.

 

Mpaka kufikia:

 

وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ ﴿٨٢﴾

Na mnafanya badala (shukurani za) riziki zenu kuwa nyinyi mnakadhibisha. [Al-Waaqi’ah: 75-82]

 

[Muslim Kitaabul-Iymaan, Mlango wa Kubainisha Kufru Kwa Anayesema Tumenyeshewa Mvua Kutokana Na Nyota]

 

 



20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...