Translate

Jumamosi, 27 Aprili 2019

Hiwsnul-Muslim: Utangulizi Wa Muislamu blog

Hiwsnul Muslim (Toleo Lilohaririwa)
Utangulizi Wa Muislamu Blog


بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمن الرَّحيم

Himdi Anastahiki Allaah (سبحانه وتعالى ) Rabb  wa walimwengu, Rahmah na amani zimshukie kipenzi chetu Nabiy Muhammad (صلى الله عليه  وآله وسلم ) na ahli zake, na Swahaba zake (رضي الله عنهم)  na wote waliotangulia kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.


Tunamshukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kutuwezesha kukifanyia kazi upya kitabu cha Hiswnul-Muslim ili kizidi kuleta manufaa kwa jamii yetu. Tumeonelea kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kukifanyia kazi upya kwa kufanya yafuatayo:


1.  Kuweka Aayah na Suwrah zote kamilifu ili  imtosheleze msomaji  kutimiza nyiradi zake zote. Mfano Suwrah ya Aliyf Miym As-Sajdah, Al-Mulk, Al-Ikhlaasw, Al-Mu’awwidhataan n.k., ambazo anatakiwa Muislamu azisome kabla ya kulala.


2.  Kutaja Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وسلم) kwa ukamilifu katika baadhi ya nyiradi au du’aa yenyewe na pia katika marejeo chini ya ukurasa pamoja na kuweka tarjama yake.


3.  Kuweka marejeo bayana ya Hadiyth; Raawiy (msimulizi) na Muhaddithuwna (wakusanyaji wa Hadiyth) kwa kunukuu marejeo yao. Tumebainisha marejeo ya mjalada na ukurasa katika mabano ya (   ) na tumebainisha nambari ya Hadiyth katika mabano ya [   ]. Baadhi ya sehemu tumeweza kuongezea marejeo zaidi ya yale yaliyotajwa katika kitabu cha asili.


4.   Kuweka sauti za Adhkaar na Du’aa hizo pamoja na matamshi yake ili msomaji aliye na udhaifu wa kusoma Kiarabu aweze kusikiliza na kuweza kufuatilia kutamka vizuri Adhkaar na Du’aa hizo.


5.  Kubainisha Ahaadiyth na Adhkaar ambazo baadhi ya ‘Ulamaa wameona kuwa hazijathibiti hivyo ni dhaifu, na badala yake kutaja ambazo zilizo Swahiyh.


6.   Kubainisha nyiradi au du’aa ambazo si za Nabiy (صلى الله عليه وسلم) bali ni Athar (za Salafus-Swaalih).   


7.  Kuzitaja Adhkaar au Du’aa  (khasa zile ambazo aghlabu hutumika kusomwa), kwa kubadilisha sarufi mfano; inapokuwa ni mwanamke au hali ya wingi, mfano Du’aa ya maiti, au Du’aa Ukiwa Na Wahka Na Huzuni  (namba 120), ambayo mwanamke anapaswa aseme:

أللَّهُمَّ إنِّي أَمَتُك، بِنْتُ عَبْدِك، بنتُ أَمَتِك
Allaahumma inniy amatuka, bintu ’abdika, bintu amatika ... 

Ee Allaah, hakika mimi mja Wako mwanamke, binti wa mja wako, binti wa mja Wako mwanamke...

Pia mfano wa du’aa namba (79) ya Sayyidul-Istighfaar iliyopo katika Nyiradi za Asubuhi Na Jioni ambayo inataja kwa kumkusudia mwanamume, hivyo mwanamke aseme:

اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ، خَلَقْتَنـي وَأَنا أَمَتُكَ
Allaahumma Anta Rabbiy laa ilaaha illaa Anta Khalaqtaniy wa ana amatuka...

Ee Allaah, Wewe ni Rabb wangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja Wako mwanamke...

Na kadhaalika .


8. Kumwekea msomaji asiyefahamu lugha ya Kiarabu kwa kutaja du’aa au nyiradi kamilifu kutokana na kubadilika wakati mfano du’aa namba  (80) katika  Nyiradi za Asubuhi Na Jioni pale inapotakiwa kubadilisha neno la
أَصْبَحْنا
Aswbahnaa (Tumeingia asubuhi)

Liwe badala yake:     
أَمْسَيْنا
Amsaynaa (Tumeingia jioni)


9. Kuipa maana sahihi baadhi ya misamiati khasa ambazo zinahusiana na mas-ala ya ‘Aqiydah.


10. Kufanya ulinganifu wa misamiati na kufafanua zaidi baadhi ya maana.


11.  Kutanabahisha makosa yanayotendwa na baadhi ya watu katika kutamka yasiyopasa ilhali yapasayo kutamkwa yamo katika kitabu hiki. Pia, kuongezea faida na fafanuzi ya baadhi ya maneno na kuweka tanbihi kadhaa.
           

Kwa ujumla tumejaribu kadiri Alivyotuwezesha Allaah (سبحانه وتعالى) kukifanyia kazi upya kwa kukiboresha ili kitoe faida kwa wingi kwa kila upande. 


Marekebisho yetu hayo, hatumaanishi kwamba tutakuwa kamilifu katika kukiweka sawa kitabu hiki, kwani ukamilifu pekee ni wa Allaah (سبحانه وتعالى).  Mwandishi wa Kitabu hiki amechukua juhudi kubwa kabisa kuaandaa kitabu kama hiki. Tunamuombea Allaah (سبحانه وتعالى) Amlipe malipo mazito kabisa katika Miyzaan yake ya hasanaat. Tunaomba vilevile thawabu ziwafikie pia kila atakayekifanyia kazi na kila atakayekitumia kitabu hiki.


Tunawaomba wasomaji pindi watakapoona kosa lolote lile watujulishe kupitia muislamublog@gmail.com


Tunamuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Atusamehe makosa yetu na Atutaqabalie hii kazi iwe kwa ajili ya kupata Radhi Zake Pekee na Atulipe malipo mema kwayo.

وبِالله التَّوْفيق  وَصَلَّى اللهُ وَسَلَّمَ وَبَارَكَ عَلى نَبِيِّنَا مُحَمَّدٍ وَعَلى آلِهِ وَأَصْحَابِهِ أَجْمَعِينَ



from Muislamu Blog http://bit.ly/2V15rUB
via IFTTT

Fadhila Za Swiyaam Za Fardhi Na Za Sunnah



Kila amali njema atendayo Muislamu inalipwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) mara kumi yake ikiwemo Swawm  kama ilivyothibiti katika Hadiyth zifuatazo:


عنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ يُضَاعَفُ الْحَسَنَةُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا إِلَى سَبْعمِائَة ضِعْفٍ قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ إِلَّا الصَّوْمَ فَإِنَّهُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ))  
Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu): ((Kila ‘amali njema ya mwana Aadam inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah (‘Azza wa Jalla) Anasema: Isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa]  [Muslim na Ahmad]

Na pia:

عَنْ أَبي ذَرٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ:((مَنْ صَامَ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ فَذَلِكَ صِيَامُ الدَّهْرِ)) فَأَنْزَلَ اللهُ تُصْدِيقَ ذَلِكَ في كِتَابِهِ الْكَرِيمِ: ((مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا))، الْيَوْمُ بِعَشَرَةِ أَيّامٍ. أخرجه أحمد والترمذي وقال حديث حسن ، والنسائي وابن ماجه وابن خزيمة
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote atakayefunga (Swawm) kila mwezi siku tatu, ni sawa na Swawm ya milele)) Kisha Allaah Akateremsha Aayah ithibitishayo hayo: “Atakayekuja kwa 'amali nzuri basi atapata (thawabu) kumi mfano wa hiyo.” Siku moja kwa malipo ya siku kumi. [Imepokewa na At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan, An Nasaaiy na Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Al-Irwaa (4/102)]. Aayah: Suwrat Al-An’aam (160)]

Miongoni mwa Swiyaam za Sunnah ni Swiyaam za Ayyaamul-Biydhw kwa dalili ya Hadiyth:

عَنْ جريرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَن النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((صِيَامُ ثَلاثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ صِيَامُ الدَّهْرِ، أَيَّامُ الْبِيضِ صَبِيحَةَ ثَلاثَ عَشَرَةَ وَأَرْبَعَ عَشَرَةَ وَخَمْسَ عشَرَةَ))   
Imepokelewa kutoka kwa Jariyr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swiyaam siku tatu kila mwezi ni sawa na swiyaam ya milele; na masiku meupe ni tarehe kumi na tatu, kumi na nne na kumi na tano [13, 14, 15])) [An-Nasaaiy (2420) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb(1040)]

Maana Ya Al-Biydhw:  Masiku hayo yameitwa ‘Al-Biydhw’ (meupe) sababu usiku wa siku hizo hung'aa kutokana na mwanga wa mwezi. Ayyaam Al-Biydhw (Masiku Meupe) tarehe zake ni 13, 14 na 15 katika kila mwezi wa kalenda ya Kiislamu.

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasisitiza kufunga Swiyaam siku tatu katika kila mwezi, ikiwa ni Ayyaamul-biydhw au Jamatatu na Alkhamiys au siku zozote zile katika mwezi:

عن أبي ذر رضي الله عنه: قال لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((يَا أَبَا ذَرٍّ، إِذَا صُمْتَ مِنَ الشَّهْرِ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ فَصُمْ ثَلاثَةَ عَشَرَ وَأَرْبَعَةَ عَشَرَ وَخَمْسَةَ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: ((Ee Abuu Dharr! Endapo utafunga (Swawm) siku tatu za kila mwezi, basi funga siku ya 13, ya 14, na ya 15)) [Imepokewa na At-Tirmidhiy na kasema Al-Albaaniy kuwa ni Swahiyh]

Na pia:

قال صلى الله عليه وسلم: ((أَلا أُخْبِرُكُمْ بِمَا يُذْهِبُ وَحَرَ الصَّدْرِ صَوْمُ ثَلاثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْر))
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Je, nikujulisheni jambo litakaloondosha uovu wa moyo? Ni kufunga (Swawm) siku tatu kila mwezi)) [An-Nasaaiy (2/2386) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh An-Nasaaiy(2249)]

Asw-Suyuutwiy (Rahimahu Allaah) amesema katika An-Nihaayah: Uovu wa moyo ni; udanganyifu, wasiwasi, na imesemwa pia ni uhasidi, chuki, na imesemwa pia uadui na imesemwa ghadhabu”


Fadhila Za  Swawm Jumatatu Na Alkhamiys:

عن أبي هريرة رضي الله عنه: تُعرَضُ الأعمالُ يومَ الاثنينِ والخميسِ فأحبُّ أن يُعرَضَ عملي وأنا صائمٌ
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Amali zinapandishwa siku ya Jumatatu na Alkhamiys, basi napenda kwamba zipandishwe 'amali zangu nikiwa mimi nina Swawm.” [Swahiyh At-Tirmidhiy 747, Swahiyh At-Targhiyb 1041]

Na kuhusu Swiyaam ya Jumatatu:

عَنْ أَبِي قَتَادَةَ الْأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سُئِلَ عَنْ صَوْمِ الِاثْنَيْنِ فَقَالَ: ((فِيهِ وُلِدْتُ وَفِيهِ أُنْزِلَ عَلَيَّ)).
Kutoka kwa Abuu Qataadah Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu Swawm ya Jumatatu akasema: “Nimezaliwa siku hiyo na siku hiyo nimeteremshiwa (Qur-aan).” [Muslim]


Baadhi ya fadhila nyinginezo za Swawm:

1. Kufunga (Swawm) ni kuepushwa na moto masafa ya miaka sabini.

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: مَنْ صَامَ يَوْماً فِي سَبِيلِ اللَّهِ بَعَّدَ اللَّهُ وَجْهَهُ عَنْ النَّارِ سَبْعِينَ خَرِيفًا .
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayefunga  Swawm siku moja kwa ajili ya Allaah, Allaah Atamweka mbali uso wake na moto masafa ya miaka sabini)) [Muslim 2/208]

Na katika Hadiyth nyingine pia:

عن جابر رضِي الله عنه عن النبيِّ  صلى الله عليه وسلم  قال: ((الصِّيام جُنَّة يَستَجِنُّ بها العبدُ من النار))   
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swiyaam ni kinga itamuokoa mja kutokana na moto [wa Siku ya Qiyaamah])) [Ahmad 2/402, Swahiyh At-Targhiyb 1/411 na Swahiyh Al-Jaami’ 3880]


2. Mwenye kufunga (Swawm) atafunguliwa mlango wa Rayyaan huko Jannah.

عَنْ سَهْلٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِنَّ فِي الْجَنَّةِ بَابًا يُقَالُ لَهُ الرَّيَّانُ يَدْخُلُ مِنْهُ الصَّائِمُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يَدْخُلُ مِنْهُ أَحَدٌ غَيْرُهُمْ يُقَالُ أَيْنَ الصَّائِمُونَ فَيَقُومُونَ لَا يَدْخُلُ مِنْهُ أَحَدٌ غَيْرُهُمْ فَإِذَا دَخَلُوا أُغْلِقَ فَلَمْ يَدْخُلْ مِنْهُ أَحَدٌ ))
Imepokelewa kutoka kwa Sahl (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika katika Jannah kuna mlango unaitwa Rayyaan, wataingia humo siku ya Qiyaamah wenye kufunga (Swawm), hatoingia yeyote mwingine. Itasemwa: “Wako wapi waliokuwa wakifunga? Watasimama kuingia hatoingia yeyote mwengine, watakapoingia, utafungwa, basi hatoingia mwengine)) [Al-Bukhaariy 1763, Muslim 1947]


3. Swawm ni kwa ajili ya Allaah Pekee na mwenye Swawm hupata furaha mbili; anapofuturu na atakapokutana na Rabb Wake. Na harufu ya mdomo wake ni nzuri mbele ya Allaah kuliko harufu ya misk.


عنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ يُضَاعَفُ الْحَسَنَةُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا إِلَى سَبْعمِائَة ضِعْفٍ قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ إِلَّا الصَّوْمَ فَإِنَّهُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ يَدَعُ شَهْوَتَهُ وَطَعَامَهُ مِنْ أَجْلِي لِلصَّائِمِ فَرْحَتَانِ فَرْحَةٌ عِنْدَ فِطْرِهِ وَفَرْحَةٌ عِنْدَ لِقَاءِ رَبِّهِ وَلَخُلُوفُ فِيهِ أَطْيَبُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ رِيحِ الْمِسْكِ))
Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu): ((Kila 'amali njema ya mwana Aadam inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah (‘Azza wa Jalla) Anasema: Isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa; ameacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili Yangu. Kwa anayefunga atapata furaha mbili; furaha anapofuturu na furaha atakapoonana na Rabb wake, harufu inayotoka kinywani mwa aliye na Swawm ni nzuri mbele ya Allaah kuliko harufu ya misk)) [Muslim na Ahmad]


4. Du’aa ya mwenye Swawm inakubaliwa.

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((ثَلاَثَةٌ لاَ تُرَدُّ دَعْوَتُهُمْ,  الإِمَامُ الْعَادِلُ, وَالصَّائِمُ حَتَّى يُفْطِرَ, وَدَعْوَةُ الْمَظْلُومِ ...))
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (([Watu] Watatu hazirudishwi du'aa zao; Imaam muadilifu, mwenye Swawm mpaka afuturu, na du'aa ya aliyedhulumiwa…)) [Ahmad na Ibn Maajah. Pia Al-Bayhaqiy 3/345 na As-Silsilah Asw-Swahiyhah 1797]


5. Swawm itakuombea shafaa-‘ah Siku ya Qiyaamah.

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((الصِّيَامُ وَالْقُرْآنُ يَشْفَعَانِ لِلْعَبْدِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، يَقُولُ الصِّيَامُ:  أَيْ رَبِّ مَنَعْتُهُ الطَّعَامَ وَالشَّهَوَاتِ بِالنَّهَارِ فَشَفِّعْنِي فِيهِ.  وَيَقُولُ الْقُرْآنُ: مَنَعْتُهُ النَّوْمَ بِاللَّيْلِ فَشَفِّعْنِي فِيهِ.  قَالَ : فَيُشَفَّعَانِ))
Imepokelewa kutoka  kwa 'Abdullaah bin ‘Amr  (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa)  kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swiyaam na Qur-aan zitamuombea shafaa’ah mja siku ya Qiyaamah. Swiyaam itasema: “Ee ee Rabb!  Nimemzuia chakula chake na matamanio wakati wa mchana, basi nnamuombea shafaa-‘ah.” Na Qur-aan itasema: “Nimemzuia usingizi wake wakati wa usiku basi nnamuombea shafaa-‘ah.” Akasema: ((Basi [viwili hivyo] vinaombea shafaa-‘ah na kukubaliwa]. [Ahmad (174/2) Al-Haakim (1/554), Al-Bayhaqiy (3/181) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaamiy’ 7329]


6. Swawm hakuna mfano wake.

عَنْ أَبِي أُمَامَةَ  قَالَ: أَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقُلْتُ: مُرْنِي بِأَمْرٍ آخُذُهُ عَنْكَ قَالَ: ((عَلَيْكَ بِالصَّوْمِ فَإِنَّهُ لَا مِثْلَ لَهُ))  
Kutoka kwa Abuu Umaamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nilimwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikasema: “Niamrishe jambo [litakalonifaa Aakhirah] nilichukue kwako.” Akasema: ((Shikilia Swawm kwani hakika hakuna mfano wake)) [An-Nasaaiy]


7. Ukifariki ukiwa katika Swawm utaingia Jannah nayo ni Husnul-Khaatimah.

عن حذيفة  رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قَال: ((مَن خُتِمَ له بصيام يومٍ دخل الجنة))
Imepokelewa kutoka kwa Hudhayfah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayekuwa 'amali yake ya mwisho kabla ya kufariki ni Swiyaam ataingia Jannah)) [Ahmad 5/391. Swahiyh At-Targhiyb 1/412, Swahiyh Al-Jaami’ 6224]


from Muislamu Blog http://bit.ly/2GS7IrF
via IFTTT

03-Zawadi Kwa Wanandoa: Mahari

Zawadi Kwa Wanandoa

03- Mahari

المهر



Ulipaji wa Mahari huwa unategemea jamii waliyopo waoaji na huwa haina kiwango maalum. Na huitwa hayo mahari صداقا kwa maana ya kuwa ni dalili ya ukweli wa mtu kutaka kuoa, na huitwa wakati mwingine kuwa ni نحلة kwa maana ya kipewacho mtu kisichokuwa na mbadala, na huitwa wakati mwingine kuwa ni حباء kwa maana ya anachopewa mtu katika mali ili kumkirimu sahibu yake, au huitwa kuwa ni علاقة yaani chenye kuunganisha baina ya wanandoa wawili.


Ndoa katika Uislam haiwi ila kwa Mahari, kwa dalili ya neno Lake Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) :
وآ توا النساء صدقاتهن نحلة
“Na wapeni wanawake mahari yao…” (An-Nisaa: 4)

Na Akasema tena Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  katika Surat Al-Ahzaab:

يا أيها النبي إنا أحللنا لك أزواجك اللاتي آتيت أجورهن
“Ewe Nabii! Tumekuhalalishia wake zako uliowapa mahari yao…” (Al-Ahzaab: 50)

Na Akasema vile vile katika Surat An-Nisaa:
فما استمتعتم به منهن فآتوهن أجورهن فريضة
“ … basi wale mnaowaoa miongoni mwao wapeni mahari yao yaliyolazimishwa…” (An-Nisaa: 24)

Uislam haukupanga malipo maalum ya mahari, cha kuzingatia hapa katika mahari ni maridhiano ya pande mbili husika, lakini kinachopendeza ni kuwa iwe hafifu na kinachowezekana bila ya taklifa kwa yule muoaji.

Imepokewa kutoka kwa Aamir bin Rabia kuwa mwanamke wa kabila la Banii fazara aliolewa kwa Ndara mbili, akasema Mtume (Swalla AAllaahu 'alayhi wa sallam):

أرضيت عن نفسك  ومالك بنعلين؟  فقالت : نعم , فأجازه
“Je, kwa Nafsi yako na kwa mali yako umeridhika kwa ndara mbili? yule mwanamke akajibu: ‘ndio’, akamkubalia.” (At-Tirmidhiy)

Kutoka kwa Sahl bin Saad kuwa Mtume (Swalla AAllaahu 'alayhi wa sallam)  alimjia mwanamke akamwambia:
Ee, Mtume wa Allaah mimi nimeitoa Nafsi yangu kwako, baada ya kusema hivyo ikawa taabu kubwa (kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ), akasimama mtu akasema, ‘Ee, Mtume wa Allah niozeshe mimi kama wewe huna haja nae’, akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ,  ‘Je, una chochote cha kutoa sadaka?’ akajibu mtu yule: ‘Sina isipokuwa ni hili shuka langu ninalojifungia,’ akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) , ‘Ukimpa hii shuka yako utakaa bila kuwa na shuka ya kutumia, tafuta kitu kingine,’ akasema mtu yule, ‘Sina kitu kingine.’ Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  kumwambia mtu yule, ‘Tafuta walau pete ya chuma’, mtu yule akatafuta na hakupata kitu, akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  kumwambia mtu yule, ‘Je, umehifadhi chochote katika Qur’an?’ Akasema mtu yule, ‘ndio, sura kadha na kadha, na akataja sura hizo.’ Hapo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akasema, ‘Nimekuozesha kwa hicho ulichokuwa nacho katika Qur-aan.’”
(Al-Bukhaariy na Muslim)

Imepokewa kutoka kwa Anas, kuwa Aba Twalhah alimposa Umu Sulaym, akasema Umu Sulaym kumwambia Aba Twalhah, Wa-Allaahi! mfano wako harejeshwi, lakini wewe ni kafiri na mimi ni Muislamu, na haiwi halali kwangu kuolewa nawe, ukisilimu hiyo ndio mahari yangu, na sitotaka kingine zaidi ya hilo. Na hiyo ndio ikawa mahari yake (baada ya kusilimu Aba Twalhah).

Hadithi zote hizi za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  zilizotangulia zinakubali mahari hata ikiwa ni ndogo kiasi gani.



from Muislamu Blog http://bit.ly/2V15OPa
via IFTTT

Njia 10 Za Kuukaribisha Vizuri Mwezi Mtukufu Wa Ramadhwaan

Inatupasa tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) kwa kutupa umri tukiwa katika Uislamu na Iymaan hadi kutufikisha tena kukaribia Mwezi mtukufu wa Ramadhwaan. Na hii ni fursa nyingine Anayotupa Allaah Ta’aala katika maisha yetu kushuhudia mwezi huu na kupata fadhila zake.  

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa):     

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ))  (( أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ...
((Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa Swawm, kama waliyofaradhishiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allaah)) (([Mfunge] siku maalumu za kuhisabika….  [Al-Baqarah: 183-184]

Hii ni neema ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Ambaye Ametujaalia kuwa na miezi iliyo bora kuliko miezi mingine au siku bora au masaa bora kuliko mengine, ambazo thawabu zake za mema yanayotendeka humo huwa ni zaidi ya nyakati nyingine. Mfano wake ni kama kunapokuwa na mauzo yaliyopunguzwa bei dukani (sale), ambayo kawaida yake huwekwa kwa muda mdogo tu maalum.  Na muda huu mtu huweza kununua vitu vingi kwa malipo kidogo tu. Hali kadhalika Ramadhwaan, ni mwezi mmoja tu, lakini malipo yake huwa ni mengi kuliko hata malipo ya miezi yote mingine.  Ikiwa mtu atatimiza Swawm yake inavyopaswa na kufanya mema mengi, na akawa katika Twaa'ah (utiifu) kamili na kuomba maghfira, basi hutoka katika mwezi huu akiwa ameghufuriwa madhambi yake.


Amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

  ((من صام رمضان إيماناً واحتساباً، غفر له ما تقدم من ذنبه)) أخرجه البخاري ومسلم  
((Atakayefunga Ramadhwaan kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy na Muslim] 

Ramadhwaan ni mwezi ambao tunatimiza fardhi mojawapo ya Kiislamu. Ni mwezi uliojaa baraka, kheri na Rahmah za Allaah (Subhaanahu wa Ta’alaa). Kila Muislamu inampasa aukaribishe mwezi huu kwa furaha na matumaini kamili.

Zifuatazo ni njia kumi za kujitayarisha kuukaribisha mwezi wa Ramadhwaan na kupata manufaa makubwa pindi utakapotimiza:


1- Du'aa
Anza kwa kuomba Du'aa kwamba mwezi huu ukufikie wakati umo katika hali ya siha nzuri na usalama hata uweze Swawm na kufanya ‘ibaadah zako kwa hamu kubwa na wepesi.  


2-Mazoezi katika mwezi wa Sha'baan  

Funga Sunnah nyingi katika mwezi wa Sha'baan, soma Qur-aan Juzuu moja kila siku au chini yake au zaidi yake, amka usiku uswali japo Rakaa mbili, kisha zidisha kidogo kidogo hadi inapoingia Ramadhwaan uwe tayari umeshapata mazoezi mazuri.



3- Shukurani Na Furaha

Mshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kukupa uhai na siha hata uifikie Ramadhwaan nyingine.  Imaam An-Nawawy alisema, kwamba shukurani inapasa kwa kila jambo jema unalojaaliwa kubwa au dogo na vile vile shukurani inapasa kwa kila jambo baya Analokuepusha nalo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).  Kwa hivyo fanya 'Sajdatush-Shukr' [Sajda ya kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)] kwa neema hii tukufu.  


Furahia kukufikia mwezi wa Ramadhwaan kama unavyomfurahikia mgeni mpenzi anapokuja kwako na kumuandalia mazuri yote.  Maswahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum),walikuwa wakiamkiana unapoingia mwezi wa Ramadhwaan na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema hivi anapowabashiria khabari nzuri za mwezi wa Ramadhwaan:

((جاءكم شهر مبارك افترض عليكم صيامه تفتح فيه أبواب الجنة وتغلق فيه أبواب  الجحيم وتغل فيه الشياطين  فيه ليلة خير من ألف شهر من حرم خيرها فقد حرم)) رواه أحمد 
((Umekujieni mwezi wa Ramadhwaan, ni mwezi wa Baraka.  Imefanywa Swawm kwenu kuwa ni fardh, milango ya Jannah hufunguliwa na milango ya moto hufungwa na mashaytaan hufungwa. Umo katika mwezi huu usiku ulio bora kuliko miezi alfu.  Atakayenyimwa kheri zake hakika kanyimwa [yote ya kheri])) [Ahmad]


4-Jipangie wakati na weka maazimio


Ni jambo la kusikitisha kuona watu wengi wanafurahia kuingia mwezi wa Ramadhwaan kwa kujiandaa kupanga mambo ya kidunia badala ya mambo ya Aakhirah.  Wengi hukimbilia kwenda sokoni kununua nguo za 'Iyd, na kufurahikia vipindi vya Ramadhwaan katika televisheni ambavyo sio vya dini kama 'misalsal' (vipindi vya televisheni vinavyoendelea), na pia kuanza kukusanya video za filamu, mipira, na mambo ya kupotezea muda usiku wa Ramadhwaan. Pia wengine kunua karata, dhumna, meza ya mchezo wa keram kwa maandalizi ya vipumbazo na vipoteza muda katika mchana wa Ramadhwaan ili wasiihisi Swawm au kuupeleka muda haraka kama wanavyoamini wao. Badala ya kufanya maandalizi ya kununua misahafu ya ziada, kanda za mawaidha, Qur-aan, kukusanya video za mawaidha na mafunzo mbalimbali ya Dini, vitabu vya Dini kwa lugha wanayoifahamu kwa wepesi na kadhalika.


Huu ni mwezi wa kufanya ‘ibaadah na fursa ya kujichumia mema mengi yamfaayo mtu Aakhirah. Kwa hiyo ndugu Waislamu, tujitahidi kuutumia wakati wetu wote bila ya kupoteza hata dakika moja, na muhimu sana kujipangia mapema wakati wako kama ifuatavyo:


  • Ni bora kujipangia nyakati zote za mwezi mzima vipi utatumia muda wako wa mchana na usiku. Weka maazimio ya dhati kuchukua fursa kamili ya wakati wote wa mwezi huu.

  • Weka mpango maalum wa kazi zako hata uweze kuswali kwa wakati kila kipindi, kusoma Qur-aan, kula daku na mengineyo kama tutakavyotaja hapa chini.

  • Kama ni mwanafunzi na kama ulikuwa ukisoma usiku, lala mapema, kisha uamke uswali Qiyaamul-Layl na usome masomo yako baada ya hapo.

  • Anza mpango wako kwa siku chache na kama unahitaji kurekebisha kuboresha nidhaam yako fanya hivyo uweze kujua nidhaam ipi itakayowafikiana na hali yako. 
  
5- Tawbah na Maghfirah      

Omba Tawbatun-Naswuwhaa (toba ya kikwelikweli) kwa Rabb wako na waombe msamaha wale uliowakosea. Kufanya hivi kutanufaisha zaidi Swawm na Swalaah zako na pia kukupa iymaan kuwa huna haki ya mtu.


6- Jifunze Fiqhi ya Swawm

Jifunze elimu ya mambo yanayohusu Swawm (Fiqhi ya Swawm), hiyo ni muhimu ili usije kufanya jambo la kuharibu Swawm yako.  Jifunze Swawm kama aliyokuwa akiifunga Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  ndio mfano bora kabisa wa kuufuata.

Swawm haifunguliwi kwa kula na kunywa tu, bali pia ni kujiepusha na maneno mabaya na kufanya mambo mabaya kama kusengenya, kutukana, kugombana. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 ((من لم يدع قول الزور والعمل به والجهل فليس لله حاجة في أن يدع  طعامه وشرابه)) البخاري   

((Yeyote asiyeacha kusema maneno mabaya? Na vitendo vibaya basi hana haja kuacha chakula chake na maji)) [Al-Bukhaariy]


7- Jitayarishe kuchuma mema mengi  


  • Mwezi wa Ramadhwaan ni mwezi wa ukarimu, huruma, rahma na mapenzi.

  • Panga kabisa na kuweka kiwango fulani cha kutoa swadaqah na kutoa kwa maskini, anzia kwanza kwa ndugu na jamaa.

  • Kama inakupasa kutoa Zakaah, na umependa iwe katika mwezi wa Ramadhwaan fanya hima uitimize fardhi hii pia.

  • Weka 'azma ya kufuturisha kwa kualika ndugu, jamaa, jirani na marafiki kwani kumfuturisha mtu ni thawabu.

                                
قال صلى الله عليه وسلم : (( من فطر صائماً كان له مثل أجره غير أنه لا ينقص من  أجر الصائم شيء)) أخرجه أحمد والنسائي وصححه الألباني
Amesema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alahyi wa aalihi wa sallam) ((Atakayemfutarisha aliyefunga, atapata ujira kama ujira wake bila ya kupungua chochote katika ujira wa yule aliyefunga)) [Ahmad, An-Nasaaiy na kasahihisha Imaam Al-Albaaniy]

  • Kama unaye jirani asiye Muislamu, mjulishe kuhusu Ramadhwaan, faida na fadhila zake. Hii ni njia na fursa mojawapo ya kufanya da'wah kwa jirani yako.


8- Hitimisha Qur-aan, Hifadhi Na Jifunze Tarjama Na Tafsiyr. 


Jipangie wakati uweze kuhitimisha Qur-aan kwani Ramadhwaan ndio mwezi ulioteremshwa Qur-aan na hivi ndivyo alivyokuwa akifanya Jibriyl (‘alayhis-salaam) kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  kusoma naye Qur-aan yote:

 عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: "كان رسول الله صلى الله عليه وسلم أجود الناس، وكان أجود ما يكون في رمضان حين يلقاه جبريل، وكان يلقاه في كل ليلة من رمضان فيدارسه القرآن؛    رواه البخاري

Kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya-Allaahu ‘anhumaa)  kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) alikuwa ni mbora (mwenye matendo mema) wa watu, lakini alikuwa mbora  zaidi katika Ramadhwaan kwa sababu Jibriyl alikuwa akimjia kila usiku wa Ramadhwaan akimfundisha Qur-aan))  [Al-Bukhaariy]


Hadiyth hii inatufundisha yafuatayo:


  • Kusoma Qur-aan katika Ramadhwaan;

  • Kukutana kwa ajili hiyo;

  • Kupima hifdh yako ya Qur-aan kwa kukaa na Mwalimu au mwenye elimu nzuri ya Qur-aan kwa kukusikiliza au kukufundisha;

  • Kuongeza juhudi za kusoma Qur-aan zaidi katika mwezi wa Ramadhwaan:


Katika muda wa masaa 24 weka saa moja au mbili iwe khaswa ya Qur-aan kusoma na kujifunza maana ya maneno ya Rabb wako uonje ladha ya Qur-aan. Vile vile jitahidi kujiwekea wakati wa kuhifadhi japo Suwrah ndogondogo ili ukitoka katika Ramadhwaan uwe una Suwrah zaidi za kusoma katika Swalaah zako. 



9-Mdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Kila Mara


Usiache ulimi wako na moyo wako kuwa mtupu bila ya kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  kila wakati kila mahali. Huku unafanya kazi zako za jikoni, fanya Adkhaar za Tasbiyh (Subhaana Allaah), Tahliyl (Laa ilaaha illa-Allaah), Tahmiyd (AlhamduliLLaah), Takbiyr (Allaahu Akbar) na Adhkaar nyenginezo zilizothibiti katika Sunnah. Kufanya hivi utajichumia thawabu maradufu, kwa kutimiza wajib wako na kuongezea kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na juu ya hivyo kuongeza baraka katika kazi zako:



10- Darsa

Hudhuria Darsa katika mwezi huu au soma vitabu vya Dini, au sikiliza mawaidha.  Jambo hili ni muhimu sana kwani kusikiliza mawaidha ni njia muhimu na bora kabisa katika kuzidisha iymaan na elimu ya Dini yako. 

Kwa hakika unahitaji saa tu kuweza kutimiza jambo hili muhimu kila siku.  Kama huwezi kuhudhuria msikitini, Alhamdulillah, MUISLAMU BLOG  imejaa  mawaidha ya kusikiliza.  Tumia muda wako hata wakati unafanya kazi zako za nyumba na za jikoni huku unasikiliza mawaidha. Kwa hiyo badala ya kutazama televisheni na kusikiliza muziki jambo ambalo ni haraam ni bora utazame na kusikiliza mawaidha ujipatie manufaa, thawabu na kuongeza elimu yako. Kumbuka kwamba kama vile mwili unavyohitajia chakula, hali kadhalika moyo na nafsi zinahitaji chakula chake nacho ni kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kila aina ya kumdhukuru, na mawaidha na darsa za Dini ni mojawapo ya chakula kizuri kabisa cha kutakasa moyo na nafsi kwa kuzijaza iymaan na mapenzi ya Allaah ('Azza wa Jalla).

Kwa kumalizia, tunasema: 


Fungua Ukurasa mpya katika maisha yako  

Baada ya kuweza kuyatimiza hayo yote, basi hali yako ya iymaan itakuwa ni bora kabisa na utakuwa umejibadilisha na kuwa mtu tofauti na ulivyo.  Kwa hivyo weka maazimio ya kuendelea hata baada ya Ramadhwaan kuwa katika twaa'ah (utiifu) na ‘ibaadah kwa wingi, na kuendeleza Qiyaamul-Layl (Kisimamo cha usiku), kusoma Qur-aan japo kidogo kila siku, na iwe umefungua ukursa mpya wa maisha yako na kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)  Akuendeleze katika hali hii.


Tunachukua Fursa hii ya kuwaombeeni Ramadhwaan yenye baraka na kheri nyingi, tutoke katika mwezi huu tukiwa tumesafishwa madhambi yetu yote, na wenye kubeba thawabu nyingi ziwe nzito katika Miyzaan ya Hasanaat (mizani ya 'amali njema) Siku ya Qiyaamah. 

اللَّهُمَّ تَقَبَّلْ مِنَّا وَ مِنْكُم  

Ee Allaah Tutaqabalie sisi na nyinyi.


from Muislamu Blog http://bit.ly/2GEba9a
via IFTTT

Tafsiyr kalimat-it-Tawhiyd 02



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2IWysK9
via IFTTT

al-Kahf 79-82



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2voZQIC
via IFTTT

Sharh-ush-Shamaa-il al-Muhammadiyyah 18



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2Py0xIU
via IFTTT

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...