Translate
Ijumaa, 1 Machi 2019
Sababu ya kutungwa kitabu “Kashf-ush-Shubuhaat”
Swali: Ni mambo gani yaliyomfanya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) kutunga kitabu hiki?
Jibu: Kuweka wazi shubuha walizoleta waabudu makaburi na wakataka kuwapaka kwazo mchanga wa machoni waislamu.
from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2GQUNZf
via IFTTT
Hawa ndio wanamtahadharisha ar-Raajihiy
Muulizaji: Baadhi ya ndugu wanatahadharisha juu ya vitabu na darsa tunazozifanyia tarjama za Shaykh ´Abdul-´Aziyz ar-Raajihiy…
al-´Abbaad: Ni nani anayetahadharisha naye?
Muulizaji: Baadhi ya ndugu walioko al-Madiynah. Wanamfanyia Tabdiy´ na wanatahadharisha naye bali wanatahadharisha juu ya wale ndugu wanaochuma faida kutoka kwake na kufanyia tarjama vitabu vyake.
al-´Abbaad: Hawa wanaotahadharisha naye ni waovu.
Muulizaji: Kwa hiyo unapendekeza waendelee?
Jibu: Endeleeni, endeleeni, endeleeni.
from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2NDk1ux
via IFTTT
Ametaka kuzidisha masiku juu ya masiku aliyojiwekea kufanya I´tikaaf
Swali: Kuna mtu amenuia kufanya I´tikaaf siku saba kisha baada ya hapo akanuia kuendelea. Je, akate I´tikaaf yake na aanze I´tikaaf kwa nia mpya? Kwa msemo mwingine ni kwamba abaki katika ile nia yake ya kwanza?
Jibu: Akinuia kufanya I´tikaaf siku saba basi anatakiwa kufanya I´tikaaf siku saba kisha aikate I´tikaaf yake. Kwani anatakiwa kupambanua I´tikaaf ya wajibu na isiyokuwa ya wajibu. Kwa hivyo anapaswa kutoka nje ya I´tikaaf baada ya siku saba. Baada ya hapo hakuna neno akitaka kufanya I´tikaaf. Katika jambo hili kuna kujichokesha. Mtu anatakiwa asiichokeshe nafsi yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakika dini hii ni nyepesi.”
Midhali ameweka nadhiri ya kufanya I´tikaaf siku saba basi analazimika kutoka baadaye na astarehe. Baada ya kustarehe akitaka kufanya I´tikaaf iliyopendekezwa, basi hakuna neno.
from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2EhbitK
via IFTTT
Kwenda msikitini na nguo za kulalia 02
Swali: Mtu ambaye anakuja kuswali msikitini akiwa na nguo za kulalia (pyamas) anatakiwa kukemewa na khaswakhaswa ikiwa ni msikiti Mtakatifu? Watu wengi wanafanya hivo.
Jibu: Swalah ni sahihi. Lakini bora ni yeye kuja na nguo nzuri. Kunaweza kusemwa kwamba ni kwenda kinyume na muruwa ikiwa kitendo hicho kinaenda kinyume na desturi za watu. Haitakiwi kwa mtu kuja na nguo zinazokwenda kinyume na desturi za watu. Kwa sababu ni kwenda kinyume na muruwa. Ama kuhusu swalah yenyewe ni sahihi endapo nguo hiyo itakuwa ni safi na ni yenye kusitiri vile viungo visivyotakiwa kuonekana.
from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2T94cBR
via IFTTT
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri ...