Translate

Jumatatu, 16 Desemba 2019

007-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kutoka Chooni


[11]
غُفْـرانَك
Ghufraanak

Nakuomba maghfira[1] (Ee Allaah).





[1]Hadiyth ya ‘Aaishah bint Abi Bakr As-Swiddiyq (رضي الله عنهما) - Aswhaab As-Sunan isipokuwa an-Nasaaiy ameitoa katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah. Taz takhriyj Zaad al-Ma’aad (2/386).


Dalili na magonjwa yanayohusiana na ujauzito

Undani wa mimba mapacha

Mimba au ujauzito mapacha ni hali ya kuwepo zaidi ya mtoto mmoja katika mfuko wa uzazi wa mwanamke mjamzito. Ingawa ujauzito wa namna hii huambatana na changamoto zaidi ya kawaida, kwa upande mwingine imekuwa ni fahari kwa mwanamama kuwa na ujauzito wa namna hii.
Kwa kawaida mimba pacha huwa ni watoto wawili, lakini pia mapacha wanaweza kuwa watatu, wanne, watano au hata sita.

Dalili za mimba mapacha

Ujauzito wa mapacha huambatana na changamoto nyingi kuliko ujauzito wa mtoto mmoja. Kuongezeka kwa baadhi ya changamoto hizi huweza kuwa dalili ya mimba mapacha.
Dalili hizi zinahusisha kupata kichefuchefu na kutapika sana kiasi cha kushindwa kufanya kazi, moyo kuenda mbio, kukosa pumzi, kuvimba miguu, kupata bawasili, tumbo kuwa kubwa kuliko kawaida pamoja na mama kuhisi mtoto kucheza sana kuliko kawaida.

Aina za mapacha

Mimba mapacha zipo za aina kuu mbili ambazo ni pacha wa kufanana na pacha wasiofanana. Pacha wa kufanana, wao hufanana mwili mzima kuanzia jinsia, sura, akili, vipaji na hata namna ya kuongea. Kwa upande wa pacha wasiofanana, hawa huweza kuwa jinsia moja au tofauti na pia huweza kuwa na tofauti kama zile za watoto wa familia moja waliozaliwa katika mimba tofauti.

Pacha wanavyotokea

Kumekuwepo na mkanganyiko wa kwa namna gani pacha hawa hutokea. Kwa mapacha wanaofanana, hawa hutokea ikiwa yai moja la mama litarutubishwa na mbegu moja ya baba kisha kujigawanya na kufanya viini tete viwili vilivyotokana na mbegu moja kutoka kila mzazi. Viini tete hivi hufanana kila kitu, kisha hukua na kutengeneza Watoto wawili. Kwa upande wa mapacha wasiofanana, mayai mawili ya mama hurutubishwa na mbegu mbili tofauti za baba na kutengeneza viini tete viwili ambavyo kila kimoja kinatokana na ya mbegu tofauti kutoka kila mzazi. Kutegemeana na mbegu zilizorutubisha mayai haya, watoto hawa wanaweza kuwa na jinsia tofauti na kutofautiana katika nyanja mbalimbali.

Nani anapata mimba ya pacha?

Kwa upande wa mapacha wanaofanana, mwanamke yeyote anaweza kupata pacha wa namna hii. Hii ni kwa sababu, mpaka sasa haijabainika ni kwa sababu zipi kiinitete kimoja kinaweza kujigawanya na kutengeneza watoto wawili. Kwa upande wa pacha wasiofanana, zipo sababu mbalimbali zinazopelekea mwanamke kupevusha mayai mawili kwa pamoja. (Ijulikane kuwa, kwa kawaida yai moja hupevushwa kila mwezi).
Wanawake wanaoweza kupevusha mayai mawili kirahisi ni wale waliotokea kwenye familia zenye mapacha (upande wa mama tu), wanaotumia madawa yakusisimua uzazi, wenye miaka 35 au zaidi, waliozaa watoto watano au zaidi, wenye asili ya Afrika (weusi) pamoja na baadhi ya vyakula (ikiwemo vya Kinaijeria) huweza kusababisha kupevusha yai zaidi ya moja.

Mapacha wa baba tofauti

Ndugu msomaji, pengine umewahi kusikia kisa cha watoto mapacha wenye baba tofauti. Mapacha wa namna hii hutokea baada ya yai la mama kurutubishwa na mbegu ya kiume na kupevusha yai jengine (kwa kawaida upevushaji husitishwa baada ya urutubishaji) ambalo litarutubishwa na mbegu za mwanaume mwengine. Hivyo, kwa lugha rahisi tunaweza kusema kuwa mimba imetunga juu ya mimba nyingine.

Mapacha walioungana

Mapacha walioungana hutokea ikiwa kiinitete cha mapacha wa kufanana hakitajigawanya kikamilifu. Mapacha wa namna hii ni adimu sana kwani hutokea mara moja kwenye mimba elfu hamsini. Mapacha hawa huweza kuungana viungo mbalimbali vya mwili kama vile vichwa, vifua, tumbo, makalio, migongo na muda mwingine huweza kutokea vichwa viwili kwenye mwili mmoja.


Hadiyth: Allaah Ndiye Mpangaji Bei (Faida Na Sharh)



Hadiyth: Allaah Ndiye Mpangaji Bei
(Faida Na  Sharh)

Imeandaliwa Na:   'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)





Imepokelewa na Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba kulitokea mfumuko wa bei ya bidhaa enzi ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).  Watu wakasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Tupangie bei.” Akasema:

((إِنَّ اللَّهَ هُوَ الْمُسَعِّرُ الْقَابِضُ الْبَاسِطُ الرَّزَّاقُ، وَإِنِّي لَأَرْجُو أَنْ أَلْقَى رَبِّي وَلَيْسَ أَحَدٌ مِنْكُمْ يَطْلُبُنِي بِمَظْلِمَةٍ فِي دَمٍ وَلَا مَالٍ))
((Hakika Allaah Ndiye Mpangaji bei, Mwenye Kubana, Mwenye Kukunjua na Mwingi wa Kuruzuku. Na hakika mimi, bila shaka, ninataraji kukutana na Rabb wangu, na ilhali hakuna yeyote kati yenu anayenitafuta kwa dhulma katika damu wala mali)) [Imaam  Ahmad na wengineo]


Faida Na Sharh:


Katika Hadiyth hii tukufu, kuna faida kadhaa:

Kwanza:
Mfumuko wa bei na ughali wa vitu, ni jambo ambalo liko Mkononi mwa Allaah ('Azza wa Jalla). Yeye Ndiye Akunjuaye na Abanae, na Ndiye Mwenye Kuongeza na Kupunguza. Anazikunjua riziki bei ya vitu ikashuka, na Anazibana na kuwa chache, na bei ya vitu ikapanda. Mvua zinapokosekana na mavuno kupungua, bei ya mazao hupanda, lakini zikinyesha katika wakati na kwa vipimo mwafaka, mazao huvunwa kwa wingi na bei hupungua. Na haya yote yako Mkononi Mwake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

Na ikiwa mambo haya yako chini ya udhibiti wa Allaah ('Azza wa Jalla), basi ni juu ya waja kutegemeza nyoyo zao kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kumwomba daima Awakunjuulie riziki zao, bei ya vitu ishuke na maisha yawe nafuu zaidi. Na ili kukubaliwa hili, ni lazima waja hawa wamridhishe Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kumtii, kuzishukuru neema Zake na kujiepusha na maasia. Wakifanya hivi, Allaah ('Azza wa Jalla)  Atawafungulia milango ya Baraka za mbinguni na ardhini. Anatuambia:

 وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَكِنْ كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُون
 Na lau watu wa kijiji wangeliamini na kucha, Tungeliwafungulia barakah toka mbinguni na ardhini, lakini walikadhibisha, Tukawaadhibu kwa sababu ya waliyokuwa wakiyachuma)). [Al-A’raaf: 96]



Pili:
Enzi bora kabisa na iliyotakasika zaidi ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba wake, haikusalimika na tatizo la mfumuko wa bei. Hiki ni kiashirio kuwa jamii au nchi yoyote inaweza kukabiliwa na tatizo hili na misukosuko mingineyo hata kama watu wake ni wachaji, wema na waadilifu. Majaribio mara yanakuwa adhabu na wakati mwingine yanakuwa kwa ajili ya kufuta mabaya na kunyanyua daraja.


Tatu:
Unapotokea mfumuko wa bei, Muislamu anatakiwa asipaparike, bali atulize roho yake na kuwa na yakini kuwa Alichopangiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  ni lazima atakipata na ambacho hakupangiwa hatokipata vyovyote aendavyo mbio. Riziki yake imeandikwa tokea yuko tumboni mwa mama yake.


Nne:
Unapotokea mfumuko wa bei, haijuzu kuwatupia lawama viongozi wa nchi, kwani suala hili liko Mkononi mwa Allaah ('Azza wa Jalla)  Peke Yake.


Tano:
المسعر ni moja kati ya Sifa za Sifa za Matendo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama alivyosema Imaam Ibn ‘Uthaymiyn alipoulizwa   [Liqaaul-Baab Al-Mafutwh]   



Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata Mawaidha, habari za kiislamu na waislamu, matukio yote yanayoigusa jamii ya kiislamu, mapishi, nashid , tafsiri za vitabu n.k  kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Bonyeza hapa Muislamu blog


Ummu 'Atwiyyah (Nusaybah Bint Al-Haarith Al-Answaariyyah)

Ummu ‘Atwiyyah Nusaybah Bint Al-Haarith Al-Answaariyyah   (رضي الله عنها)





Ummu ‘Atwiyyah ni mmoja katika wanawake wa kiislaamu ambao historia haitowasahau kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika Jihaad, elimu ya Fiq-h na pia kupokea Hadiyth. Mara nyingi jina lake huchanganywa na la Nusaybah bint Ka’ab ambaye alikuwa kinga ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika vita vya Uhud.
Ummu ‘Atwiyyah alitokea Madiynah na alisilimu mapema ulipofika Uislaam katika mji wa Madiynah pale Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomtuma Mus’ab ibn ‘Umayr kwenda kuwafundisha na kuwalingania dini.
Hatuna haja ya kuutaja wasifu wake lakini tuutathmini mchango hasa katika vita vya Jihaad kama anavyosimulia mwenyewe.


عن أم عطية رضي الله عنها قالت: غزوت مع النبي صلى الله عليه وسلم سبع غزوات أخلفهم في رحالهم، فأصنع لهم الطعام، وأداوي الجرحى، وأقوم على المرضى

Kutoka kwa Ummu ‘Atwiyyah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa): Nilikuwa nikipigana vita pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika vita saba nikibaki nyuma kwenye mizigo yao nikiwapikia chakula na kuwatibu majeruhi na kuwahudumia wagonjwa.

Haya ndiyo yalikuwa majukumu ya mwanamama shujaa aliyediriki kushiriki takriban vita vyote alivyopigana Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwani katika vita vya Khaybar, Ummu ‘Atwiyyah pia alikuwa ni miongoni mwa wanawake ishirini walioshiriki kwa ajili ya kupata ujira wa Jihaad.

Ama katika majala ya Fiq-h, Ummu Atwiyyah alikuwa ndiye mkoshaji mkubwa wa maiti za akinamama katika mji wa Madiynah enzi za Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ni yeye aliemuosha Zaynab bint Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipofariki kama anavyosimulia katika moja ya hadiyth zake:
Kutoka kwa Ummu ‘Atwiyyah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa):

لما ماتت زينب بنت رسول الله صلى الله عليه قال: (اغسلنها وتراً ، ثلاثاً أو خمساً ، واجعلن في الآخرة كافوراً أو شيئاً من كافور ، فإذا غسلتنها فأعلمنني) فلما غسلناها أعطانا حقوه ، فقال: (أشعرنها إياه)

Alipokufa Zaynab bint wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akasema: “Mkosheni witr – mara tatu au mara tano na jaalieni katika josho la mwisho Kaafur au kitu kidogo katika Kaafuur na mkishamaliza niiteni”. Tulipomaliza tulimuita na akaturushia shuka yake anayovaa kiunoni na kusema iwekeni jirani yake.

Ni kutokana na maneno ya Ummu ‘Atwiyyah ndivyo tulivyojua kwamba tunapoanza kuosha mayyit wetu tuanze upande wake wa kulia na katika sehemu tunazoziosha wakati wa kutia wudhuu kama ilivyosimuliwa na Al-Bukhaary na Muslim.
Ni kutokana na hadiyth ya Ummu ‘Atwiyyah ndivyo tulivyojuwa kwamba akinamama wamekatazwa kusindikiza jeneza kama anavyosimulia:

نهينا عن اتباع الجنازة ، ولم يعزم علينا

Tulikatazwa kulifuata Jeneza ingawa haikuwajibishwa juu yetu.

Ummu ‘Atwiyyah hakuwa mpokezi wa hadiyth tu bali pia alikuwa ni mwenye kuuliza na kutaka ufafanuzi katika masaail mengi kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

Aliwahi kumuuliza Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pale alipowaamrisha akinamama na wanawake kutoka kwenda kuswali Swala ya ‘Iyd kwamba: Je, asiyekuwa na nguo ya kujistiri anaweza kuruhusiwa kubaki nyumbani asiende kuswali? Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Na amuazime mwenzake”
Na hapa tunapata maelekezo ya kielimu jinsi Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyowaamrisha wanawake kutoka kwenda kuswali hata watoto wadogo, wanawari na wenye hedhwi na walitakiwa kubaki nyuma na wanaoswali wakileta Takbiyr (za ‘Iyd) na wao huleta na wakiomba du’aah pia huitikia kama ilivyosimuliwa na A-Bukhaariy na Muslim.

Na katika upande wa hadiyth, Ummu ‘Atwiyyah ni miongoni mwa kinamama waliobahatika kusimulia hadiyth nyingi kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Inasemekana alikuwa na hadiyth zinazofika arubaini na sita kati ya hizo zimo kwenye Swahihi A-Bukhariy na Muslim. Pia hadiyth zake hupatikana katika vitabu vyengine vinavyotegemewa.

Miongoni mwa Maswahaba wakubwa kama Anas Ibn Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu) pia alipokea baadhi ya hadiyth kupitia kwake. Kama walivyopokea Taabi’iyn kama kina Muhammad ibn Siriyn na dada yake Hafswah bint Siriyn na wengineo.

Baadae alihamia Baswrah ambapo alisifika kwa ‘ilmu yake na waislaamu wengi walifaidika na kunufaika kupitia kwake. Baadhi ya Maswahaba na hata Taabi’iyn walidiriki kufanya safari kwenda Baswra kwenda kumsikiliza Ummu ‘Atwiyyah katika masaail mengi ya kifiq-h na uoshaji wa mayyit.

Alifariki Baswrah akiwa na takriban miaka 70 katika umri wake (Radhwiya Allaahu ‘anhu)


02-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Kutangamana Na Wake


بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam

كِتَابُ اَلنِّكَاحِ
Kitabu cha Nikaah (Ndoa)

بَابُ عِشْرَةِ اَلنِّسَاءِ
02-Mlango Wa Kutangamana Na Wake





865.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {مَلْعُونٌ مَنْ أَتَى اِمْرَأَةً فِي دُبُرِهَا} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ وَاللَّفْظُ لَهُ، وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ، وَلَكِنْ أُعِلَّ بِالْإِرْسَالِ
 Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Amelaaniwa mwenye kumjamii mkewe katika duburi yake.”[1] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy, matini ya Hadiyth ni yake. Wapokezi wake ni madhubuti lakini imedhoofishwa kwa kuwa ni Mursal]



866.
وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَا يَنْظُرُ اَللَّهُ إِلَى رَجُلٍ أَتَى رَجُلاً أَوْ اِمْرَأَةً فِي دُبُرِهَا} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَالنَّسَائِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ، وَأُعِلَّ بِالْوَقْفِ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah Hamtazami mwanamume aliyemjamii mwanamume au mwanamke katika uchi wake wa nyuma.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan na imedhoofishwa kwa kuwa ni Mawquwf]



867.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  عَنِ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاَللَّهِ وَالْيَوْمِ اَلْآخِرِ فَلَا يُؤْذِي جَارَهُ، وَاسْتَوْصُوا بِالنِّسَاءِ خَيْرًا، فَإِنَّهُنَّ خُلِقْنَ مِنْ ضِلَعٍ، وَإِنَّ أَعْوَجَ شَيْءٍ فِي اَلضِّلَعِ أَعْلَاهُ، فَإِنْ ذَهَبْتَ تُقِيمَهُ كَسَرْتَهُ، وَإِنْ تَرَكْتَهُ لَمْ يَزَلْ أَعْوَجَ، فَاسْتَوْصُوا بِالنِّسَاءِ خَيْرًا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ
وَلِمُسْلِمٍ: {فَإِنْ اِسْتَمْتَعْتَ بِهَا اِسْتَمْتَعْتَ وَبِهَا عِوَجٌ، وَإِنْ ذَهَبْتَ تُقِيمُهَا كَسَرْتَهَا، وَكَسْرُهَا طَلَاقُهَا} 
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anayemuamini Allaah na siku ya mwisho, asimuudhi jirani yake.[2] Wafanyieni kheri wanawake, hakika wao wameumbwa kwa ubavu, na hakika kitu kilichopotoka zaidi katika ubavu ni ule wa juu, ukitaka kuunyosha utauvunja[3] na ukiuwacha utaendelea kupotoka, kwa hivyo wafanyieni wema wanawake.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]
Na katika Riwaayah ya Muslim: “Ukistarehe naye utastarehe naye akiwa na upotofu. Na ukitaka kumnyoosha utamvunja na kumvunja kwake ni kumtaliki.”



868.
وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: {كُنَّا مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  فِي غَزَاةٍ، فَلَمَّا قَدِمْنَا اَلْمَدِينَةَ، ذَهَبْنَا لِنَدْخُلَ. فَقَالَ: " أَمْهِلُوا حَتَّى تَدْخُلُوا لَيْلًا  يَعْنِي: عِشَاءً  لِكَيْ تَمْتَشِطَ اَلشَّعِثَةُ، وَتَسْتَحِدَّ اَلْمَغِيبَةُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 
وَفِي رِوَايَةٍ لِلْبُخَارِيِّ:{إِذَا أَطَالَ أَحَدُكُمُ الْغَيْبَةَ، فَلَا يَطْرُقْ أَهْلَهُ لَيْلاً}  
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika vita, tuliporudi Madiynah tulitaka kuingia (majumbani mwetu) Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akatuambia: Subirini,[4] ili muingie usiku yaani wakati wa ‘Ishaa ili (mke) mwenye nywele timtim apate kujichana, na yule aliyempoteza mumewe apate kujinyoa.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Katika Riwaayah ya Bukhaariy imesema: “Mmoja wenu atakapokuwa safarini muda mrefu basi asiwagongee katu watu wake wakati wa usiku.”



869.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {إِنَّ شَرَّ اَلنَّاسِ مَنْزِلَةً عِنْدَ اَللَّهِ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ، اَلرَّجُلُ يُفْضِي إِلَى اِمْرَأَتِهِ وَتُفْضِي إِلَيْهِ، ثُمَّ يَنْشُرُ سِرَّهَا} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika uovu wa watu kwa daraja kubwa mbele ya Allaah siku ya Qiyamah ni mwanamume anamjamii mkewe kisha akaeneza siri yake, na mwanamke anamjamii mme wake kisha anaeneza siri yake.”[5] [Imetolewa na Muslim]



870.
وَعَنْ حَكِيمِ بْنِ مُعَاوِيَةَ، عَنْ أَبِيهِ قَالَ: {قُلْتُ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! مَا حَقُّ زَوْجِ أَحَدِنَا عَلَيْهِ ؟ قَالَ: " تُطْعِمُهَا إِذَا أَكَلْتَ، وَتَكْسُوهَا إِذَا اِكْتَسَيْتَ، وَلَا تَضْرِبِ الْوَجْهَ، وَلَا تُقَبِّحْ، وَلَا تَهْجُرْ إِلَّا فِي اَلْبَيْتِ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَعَلَّقَ اَلْبُخَارِيُّ بَعْضَهُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa Hakiym bin Mu’aawiyah kutoka kwa baba yake amesema: “Niliuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Ni nini wajibu wa mke kwa mumewe? Akasema: Ni umlishe unapokula, umvishe unapovaa, wala usimpige uso, wala usimkaripie wala usimgure ila nyumbani tu.” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah. Al-Bukhaariy ameifanya ni Mu’alaqqah baadhi yake. Akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]



871.
وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {كَانَتِ الْيَهُودُ تَقُولُ: إِذَا أَتَى اَلرَّجُلُ اِمْرَأَتَهُ مِنْ دُبُرِهَا فِي قُبُلِهَا، كَانَ اَلْوَلَدُ أَحْوَلَ. فَنَزَلَتْ: "نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوْا حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ" [اَلْبَقَرَة : 223]} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ 
Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Mayahudi walikuwa wakisema: Mwanamume akimjamii mkewe kinyume nyume kwa uchi wa mbele mtoto akizaliwa atakuwa makengeza. Ikateremka Aayah hii: “Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo” [Al-Baqarah: 223] [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]



872.
وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَوْ أَنَّ أَحَدَكُمْ إِذَا أَرَادَ أَنْ يَأْتِيَ أَهْلَهُ قَالَ: بِسْمِ اَللَّهِ. اَللَّهُمَّ جَنِّبْنَا اَلشَّيْطَانَ وَجَنِّبِ الشَّيْطَانَ مَا رَزَقْتَنَا، فَإِنَّهُ إِنْ يُقَدَّرْ بَيْنَهُمَا وَلَدٌ فِي ذَلِكَ، لَمْ يَضُرَّهُ اَلشَّيْطَانُ أَبَدًا"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Lau mmoja wenu anapomuendea mkewe (amjamii) aseme:

اَللَّهُمَّ جَنِّبْنَا اَلشَّيْطَانَ وَجَنِّبِ الشَّيْطَانَ مَا رَزَقْتَنَا

BismiLlaah, Allaahumma jannibnaa ash-shaytwaana wa jannibi ash-shaytwaana maa razaqtanaa (Kwa jina la Allaah, Ee Allaah Tuepushe na shaytwaan, na umuepushe shaytwaan katika Utakachoturuzuku).  Kisha wakajaaliwa kupata mtoto, shaytwaan hawezi kumdhuru (mtoto huyo) milele.” [Al-Bukhaariy, Muslim]



873.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {إِذَا دَعَا اَلرَّجُلُ اِمْرَأَتَهُ إِلَى فِرَاشِهِ فَأَبَتْ أَنْ تَجِيءَ، لَعَنَتْهَا اَلْمَلَائِكَةُ حَتَّى تُصْبِحَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ  
وَلِمُسْلِمٍ: {كَانَ اَلَّذِي فِي اَلسَّمَاءِ سَاخِطًا عَلَيْهَا حَتَّى يَرْضَى عَنْهَا}
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwanamume atakapomuita mkewe kitandani akakataa kumuendea, akalala, Malaika wanamlaani (mke huyo) mpaka apambazukiwe.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Bukhaariy]
Na katika Riwaayah ya Muslim imesema: “…Aliye mbinguni Atamkasirikia (mke huyo) mpaka mumewe amridhie.”



874.
وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَعَنَ اَلْوَاصِلَةَ وَالْمُسْتَوْصِلَةَ، وَالْوَاشِمَةَ وَالْمُسْتَوْشِمَةَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Amemlaani mwanamke[6] mwenye kuunga na mwenye kuungwa nywele na mwenye kuchanja na mwenye kuchanjwa.” [Al-Bukhaariy, Muslim]



875.
وَعَنْ جُذَامَةَ بِنْتِ وَهْبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ:{حَضَرْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  فِي أُنَاسٍ، وَهُوَ يَقُولُ: لَقَدْ هَمَمْتُ أَنْ أَنْهَى عَنِ الْغِيلَةِ، فَنَظَرْتُ فِي اَلرُّومِ وَفَارِسَ، فَإِذَا هُمْ يُغِيلُونَ أَوْلَادَهُمْ فَلَا يَضُرُّ ذَلِكَ أَوْلَادَهُمْ شَيْئًا" . ثُمَّ سَأَلُوهُ عَنِ الْعَزْلِ ؟ فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  "ذَلِكَ اَلْوَأْدُ اَلْخَفِيُّ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ 
Kutoka kwa Judhaamah bint Wahb[7] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nilikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipowaambia watu: Nilitamani kukataza Ghiylah,[8] Nikatazama Warumi na Wafursi nikawakuta wanawafanyia Ghiylah watoto wao wala hilo halidhuru chochote watoto wao. Kisha Maswahaba wakamuuliza kuhusu ‘Azli’[9] Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akawaambia Huko ndiko kuua kwa siri.” [Imetolewa na Muslim]



876.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ رَجُلاً قَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنَّ لِي جَارِيَةً، وَأَنَا أَعْزِلُ عَنْهَا، وَأَنَا أَكْرَهُ أَنْ تَحْمِلَ، وَأَنَا أُرِيدُ مَا يُرِيدُ اَلرِّجَالُ، وَإِنَّ اَلْيَهُودَ تُحَدِّثُ: أَنَّ اَلْعَزْلَ المَوْؤُدَةُ اَلصُّغْرَى. قَالَ: " كَذَبَتْ يَهُودُ، لَوْ أَرَادَ اَللَّهُ أَنْ يَخْلُقَهُ مَا اِسْتَطَعْتَ أَنْ تَصْرِفَهُ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ وَاللَّفْظُ لَهُ، وَالنَّسَائِيُّ، وَاَلطَّحَاوِيُّ، وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ 
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa “Mtu mmoja alimjia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Mimi nina mjakazi, nami namfanyia ‘azli nachukia kubeba kwake mimba, nami nataka wanayotaka wanaume (kujimai) na Mayahudi huwa wanasema kuwa kufanya ‘azli ni mauaji madogo. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Wayahudi wamedanganya, lau Allaah Angalitaka kumuumba mtoto wewe usingaliweza kumzuia.” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Atw-Twahaawiyy, na wapokezi wake ni madhubuti]



877.
وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: {كُنَّا نَعْزِلُ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  وَالْقُرْآنُ يَنْزِلُ، وَلَوْ كَانَ شَيْئًا يُنْهَى عَنْهُ لَنَهَانَا عَنْهُ اَلْقُرْآنُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ  
وَلِمُسْلِمٍ:{فَبَلَغَ ذَلِكَ نَبِيَّ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  فَلَمْ يَنْهَنَا}
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tulikuwa tukifanya ‘Azl katika zama za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na Qur-aan inateremka. Lau kama (‘azl) ingekuwa ni jambo analokataza basi Qur-aan ingelitukataza.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika Riwaayah ya Muslim inasema: “...habari hiyo ikamfikia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) wala hakutukataza.”



878.
وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  كَانَ يَطُوفُ عَلَى نِسَائِهِ بِغُسْلٍ وَاحِدٍ} أَخْرَجَاهُ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ 
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Alikuwa akiwazungukia wakeze kwa josho moja.”[10] [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]
 
[1] Wanazuoni wote wamekubaliana kuwa kumuingilia mwanamke nyuma ni haraam.
[2] Kumkera na kumuudhi Muislamu ni jambo lisilotakiwa, ama kumuudhi jirani ni katika madhambi makubwa.

[3] Hadiyth hii inatufundisha kuwa wanawake waamiliwe kwa wema. Tabia ya mwanamke ni tofauti na ya mwanamume. Kuna sababu nyingi za matatizo anayoyapata mwanamke. Mwanamke ni kama ubavu, ambao ukiunyoosha utauvunja. Tabia ya maumbile aliyoumbwa nayo mwanamke haiwezi kubadilika.
[4] Hii ina maana ikiwa mtu ametoka safari ya mbali, si vizuri kuenda nyumbani kwake moja kwa moja. Ni vizuri kutuma taarifa ya kufika kwako kwanza. Kuna sababu nyingi kuhusu jambo hili. Mume anapoondoka, mwanamke hajiangalii kwa kujiremba na kujiweka vizuri kama kunyoa sehemu zake na usafi mzima wa mwili wake. Suala hili linaweza kuonekana dogo lakini linaweza kumfanya mume akapunguza mapenzi kwa mke wake.
[5] Ina maana ya kuelezea lile tendo kwa watu wengine, kwa hakika kufanya jambo hili kunapelekea katika kufanya jambo la haraam.
[6] Katika Hadiyth hii wamelaaniwa wanawake aina nne: 1-Wenye kuunga nywele, 2-Wenye kuungwa nywele, 3-Wenye kuchanja (tattoo), 4- Wenye kuchanjwa (tattoo) katika miili yao.

[7] Judhaamah bint Wahb ni dada yake ‘Ukaashah bin Mihdhan kwa mama, jina lake lingine ni Jundal Al-Asadiyyah. Alikuwa ni Swahaba miongoni mwa Waislamu wa mwanzo. Alihajiri Madiynah. Alikuwa ni mke wa Anis bin Qataadah.

[8] Ghiylah ni mwanamume amjamii mkewe naye ananyonyesha au akiwa ni mjamzito.
[9] ‘Azl ni kumjamii mkewe na ukifika wakati wa kushusha manii akayamwaga nje kwa ajili ya kupanga kizazi. Suala la uhalaal na uharaam wa ‘Azl ni kuwa kuna Hadiyth kuhusiana na suala hili. Ikiwa imeamuliwa kuwa ‘Azl ni halaal na kwa wakati huo huo Shariy’ah haipendekezi. Kwa kadhia ya mwanamke ambaye afya yake ni mbaya hapa ‘Azl itakuwa lina lengo la kuokoa maisha.
[10] Lengo la Hadiyth hii kuwa ugawaji wa muda haukuwa wajibu kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Ingalikuwa ni wajibu kwake kama kwa watu wengine asingelazimika kuwazunguka wote kwa usiku mmoja.


20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...