Translate

Jumamosi, 3 Oktoba 2020

Sickle Cell Ni Ugonjwa Gani?

 

 

Sickle cell disease (SCD) ni kundi la maradhi ya kurithi ya chembechembe nyekundu za damu. Chembechembe nyekundu za damu zenye afya huwa za mviringo, na hutembea ndani ya mishipa midogo ya damu kusambaza oksijeni kwenye sehemu zote za mwili. Ndani ya mwili wa mtu mwenye ugonjwa wa sickle cell, chembechembe nyekundu za damu hugeuka kuwa ngumu na zinazonatanata na huwa na umbo la C, umbo linalofanana na kifaa cha shambani kiitwacho “sickle”. Seli hizi hufa mapema, hali ambayo husababisha mtu awe na upungufu wa damu kila wakati. Na, wakati seli hizi zikisafiri ndani ya mishipa midogo ya damu, hukwama na kuuziba mtiririko wa damu. Hali hii huweza kuleta maumivu makali na matatizo mengine makubwa kama maambukizi, acute chest syndrome na stroke.

Aina Za Sickle Cell Disease

Aina za ugonjwa wa sickle cell ambazo huonekana kwa wingi ni zifuatazo:

Alhamisi, 1 Oktoba 2020

16-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Kuweka Nadhiri Kwa Asiyekuwa Allaah

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

 

16- Kuweka Nadhiri Kwa Asiyekuwa Allaah

 

Alhidaaya.com

 

 

Kuweka nadhiri ni mtu kuilazimisha nafsi yake kwa kitu ambacho hajalazimishwa na Shariy’ah.  Amesema Al-Isfhaan (Rahimahu Allaah) katika Mufradaat Alfaadhw Al-Qur-aan (uk. 797): “Nadhiri ni unapojishurutisha kutenda jambo lisilokuwa wajibu kwa sababu ya kutaka jambo fulani likutokee. Anasema Allaah:

 

إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَـٰنِ صَوْمًا 

Hakika mimi nimeweka nadhiri ya swawm kwa Ar-Rahmaan [Maryam: 26]

 

Baadhi ya ‘Ulamaa wameharamisha kwa dalili ya Hadiyth ifuatayo:

 

عن النبيَّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ ؛ أنه نهى عن النذر  وقال:  إنه لا يأتي بخير. وإنما يستخرج من البخيل

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza nadhiri akasema: ((Haileti khayr bali inatolewa kutoka kwa bakhili)) [Muslim (1639)]

 

Na katika riwaayah nyingine:

 

  نَهَى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ النَّذْرِ وَقَالَ:  إِنَّهُ لَا يَرُدُّ شَيْئًا وَلَكِنَّهُ يُسْتَخْرَجُ بِهِ مِنْ الْبَخِيلِ

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza nadhiri akasema: ((Hakika hairudishi chochote, bali inatolewa kutoka kwa bakhili)) [Al-Bukhaariy (6693)]   

 

Na Hadiyth ya Mama wa Waumini ‘Aaishah  (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba  amesema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

 من نذر أن يُطِيعَ اللهَ فلْيُطِعْهُ ، ومن نذرَ أن يعصِيَه فلا يَعْصِه

((Aliyeweka nadhiri kumtii Allaah amtii, na aliyeweka nadhiri kumuasi Allaah, basi asimuasi))[Al-Bukhaariy (6696)]

 

 

Kutokana na Hadiyth hii, inadhihirisha kukubaliwa kwake nadhiri pindi mtu akiazimia, kwa dalili pia za Qur-aan:

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ

Na chochote mtoacho au mkiwekacho nadhiri, basi Allaah Anakijua. [Al-Baqarah: 270]

 

Na pia kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا﴿٧﴾

Wanatimiza nadhiri na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea kwa upana. [Al-Insaan: 7]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

ثُمَّ لْيَقْضُوا تَفَثَهُمْ وَلْيُوفُوا نُذُورَهُمْ

Kisha wamalize ‘ibaadah zao; wajisafishe taka zao na watimize nadhiri zao, [Al-Hajj: 29]  

 

 

Na kwa vile nadhiri ni aina ya ‘Ibaadah, haifai kuielekeza kwa asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) mfano kuifanya kwa ajili ya Nabiy, au Walii, au Shaykh, au kaburi na kadhaalika. Kufanya hivyo ni shirki kubwa inayomtoa mtu nje ya Uislamu.

 

Fataawa za ‘Ulaama kuhusu kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 

Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Swali: 

 

Je, ikiwa mtu ameweka nadhiri mfano akasema: “Allaah Akinipa shifaa kwa magonjwa yangu, nitachinja kwa ajili ya Allaah katika kaburi la fulani ili kujikurubisha kwa Allaah. Je, inajuzu mfano wa ‘amali kama hii? Na je, kuna sehemu zilizoharamishwa kuchinja?

 

Jibu: 

 

Ikiwa ameweka nadhiri kuchinja kwa ajili ya Allaah katika kaburi, basi nadhiri hii ni ya maasi, haijuzu kuitimiza. Na kuchinja katika kaburi ikiwa imekusudiwa kujikurubisha kwa mwenye kaburi, hiyo ni shirki kubwa inayomtoa mtu katika Dini hata kama ataja Jina la Allaah wakati anachinja.

 

Na ikiwa kujikurubisha kwa Allaah basi hayo ni maasi makubwa na wasiylah (njia ya kujikurubisha) za shirki kwa sababu haijuzu kuswali kaburini wala kuomba wala kuchinja kaburini hata kama tunakusudia Allaah kwani hivyo ni kujifananisha na washirikina na wasiyla za shirki. 

 

Abuu Daawuwd amepokea kutoka kwa Thaabit bin Adhw-Dhwahaak (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba mtu mmoja aliweka nadhiri kuchinja ngamia katika Buwaanah. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akauliza: ((Je, kuliweko masanamu ya kijaahiliyyah (kabla Uislamu) yakiabudiwa?”

Wakasema: “Hapana” Akasema: ((Je, kuliweko sherehe za kijaahiliyyah zikifanywa hapo?)) Wakasema: “Hapana” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Timiza nadhiri yako, kwani hakuna kutimiza nadhiri katika kumuasi Allaah, wala katika ambayo hayamiliki bin Aadam)). [Abuu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy]

 

 

 

Imaam bin Baaz (Rahimahu Allaah)

 

Swali:

 

Imenitokea mushkila nikaweka nadhiri kwa ajili ya mmojawapo wa ma-Imaam, kisha nikaja kutambua kuwa haifai kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah. Tambua kuwa sehemu aliyoko huyo Imaam iko mbali, je, inajuzu nilipize nadhiri hii kwa mafakiri au niifanyie kafara?

 

Jibu: 

 

Nadhiri hiyo ni baatwil, kwa sababu ni ‘ibaadah kwa asiyekuwa Allaah.  Inakupasa utubie kwa Allaah kwayo na urudi Kwake kwa kutubia na kuomba maghfirah na kujuta kwani nadhiri ni ‘ibaadah, Anasema Allaah Ta’aalaa:  

 

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ

Na chochote mtoacho au mkiwekacho nadhiri, basi Allaah Anakijua. [Al-Baqarah: 270]

 

Yaani: Atakulipeni kwayo. Na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

من نذر أن يُطِيعَ اللهَ فلْيُطِعْهُ، ومن نذرَ أن يعصِيَه فلا يَعْصِه

((Aliyeweka nadhiri kumtii Allaah amtii, na aliyeweka nadhiri kumuasi Allaah, basi asimuasi))  

 

Kwa hiyo nadhiri hiyo ni baatwil, na ni kumshirikisha Allaah (‘Azza wa Jalla) kama vile nadhiri kwa ajili ya ma-Imaam na waliokufa ni nadhiri baatwil na ni kumshirkisha Allaah, basi nadhiri haijuzu isipokuwa kwa ajili ya Allaah Pekee, kwa sababu ni ‘ibaadah kama vile Swalaah, na kuchinja na nadhiri, na kufunga Swiyaam na du’aa zote ni kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kama Anavyosema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾

Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada. [Al-Faatihah: 5]

 

 

Na Anasema (Subhaanahu):

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ

Na Rabb wako Amehukumu kwamba: “Msiabudu isipokuwa Yeye Pekee [Al-Israa: 23]

 

 

Na Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

فَادْعُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ﴿١٤﴾

Basi mwombeni Allaah wenye kumtakasia Dini japokuwa wanachukia makafiri. [Ghaafir: 14]

 

 

 

Na Anasema (‘Azza wa Jalla):

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا﴿١٨﴾

Na kwamba Misikiti ni kwa ajili ya Allaah, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah. [Al-Jinn: 18]

 

 

Basi ‘ibaadah ni haki ya Allaah, na nadhiri ni ‘ibaadah, na Swawmi ni ‘ibaadah, na Swalaah ni ‘ibaadah, na du’aa ni ‘ibaadah basi inawajibika kuisafisha kwa ajili ya Allaah Pekee. Kwa hiyo nadhiri hiyo ni baatwil, na haikupasi kufanya chochote, si kwa mafukara wala wengineo, bali inakupasa utubie tu na huna haja ya kuilipizia nadhiri hiyo kwa vile ni baatwil na ni shirki, ila tu utubie tawbah ya kikweli na kufanya matendo mema, Allaah Akuwafikie na Akuongoze katika yanayomridhisha na Akujalie ufanye tawbah ya kikweli.

 

 

 

 



54-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Anaombewa Du’aa Na Kuswaliwa Katika Kila Aina Za Ibaadah Za Waumini

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

54-Anaombewa Du’aa Na Kuswaliwa Katika Kila Aina Za Ibaadah Za Waumini

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ ﴿٤﴾

Na Tukanyanyulia juu utajo wako (ukawa mwenye kusifika mno)?  [Ash-Sharh: 4]

 

Allaah (عز وجل) Amemjaalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) fadhila adhimu kabisa nayo ni fadhila za kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika hali mbalimbali ya maisha ya Muislamu; katika Swalaah zote za faradhi na za Sunnah, namo ni katika Adhana na Iqaamah na katika kikao cha Tashahhud, katika Swalaah ya Jeneza, anapotajwa katika vikao vya elimu, zinapotajwa Hadiyth zake, katika ‘ibaada za Hajj na ‘Umrah, katika kuomba du’aa, katika Adhkaar za asubuhi na jioni, baada ya kutawadha, watu wanapokhutubia katika Minbar, zinapofungwa Nikaah,  Siku ya Ijumaa imeamrishwa kukithirisha kumswalia, na katika,  hali nyenginezo. Juu ya hivyo  imeamrishwa kuwa pindi inapoadhiniwa aombewe du’aa na kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Kumswalia kote huko humrudia fadhila zake kwa Muislamu anayetekeleza amri hii:

 

 

1-Baada Ya Kutawadha:

 

أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ  

Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah, Wahdahu laa shariyka Lahu wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu

 

2-Katika Adhana:

 

 

اللهُ أكبَر اللهُ أكبر، الله أكبر اللهُ أكبر، أشهدُ أنْ لا إلهَ إلَّا الله، أشهدُ أنْ لا إلهَ إلَّا الله، أشهدُ أنَّ محمدًا رسولُ الله، أشهدُ أنَّ محمدًا رسولُ الله، حيَّ على الصَّلاة، حيَّ على الصَّلاة، حيَّ على الفلاح، حيَّ على الفلاح، اللهُ أكبر اللهُ أكبر، لا إلهَ إلَّا الله

 

Allaahu Akbar Allaahu Akbar, Allaahu Akbar Allaahu Akbar, Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah, Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah,   Ash-hadu anna Muhammadan Rasuwlu-Allaah, Ash-hadu anna Muhammadan Rasuwlu-Allaah, Hayya ‘alas-Swalaah, Hayya ‘alas-Swalaah, Hayya ‘alal-Falaah, Hayya ‘alal-Falaah,   Allaahu Akbar Allaahu Akbar, laa ilaaha illa-Allaah

 

 

3-Anaombewa Du’aa Na Anaswaliwa Inapoadhiniwa:

 

 

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   قَالَ : {مَنْ قَالَ حِينَ يَسْمَعُ اَلنِّدَاءَ : اَللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ اَلدَّعْوَةِ اَلتَّامَّةِ،  وَالصَّلَاةِ اَلْقَائِمَةِ،  آتِ مُحَمَّدًا اَلْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ،  وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا اَلَّذِي وَعَدْتَهُ، حَلَّتْ لَهُ شَفَاعَتِي يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ}  أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ

 

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kusoma anaposikia Adhana:

 

 اَللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ اَلدَّعْوَةِ اَلتَّامَّةِ،  وَالصَّلَاةِ اَلْقَائِمَةِ،  آتِ مُحَمَّدًا اَلْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ،  وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا اَلَّذِي وَعَدْتَهُ

Allaahumma Rabba haadhihid-dda’watit-ttaamah, wasw-Swaalaatil qaaimah, aati Muhammada  al-wasiylata wal fadhwiylah, wab-‘ath-hu maqaaman mahmuwdan alladhiy wa’adtah.

 

(Ee Allaah, Rabb wa mwito huu uliotimia, na Swalaah iliyosimama, mpe (Nabiy) Muhammad al-Wasiylah (cheo, heshima maalumu, daraja), na fadhila, na mfikishe daraja yenye kuhimidiwa, ambayo Umemuahidi).

Ash-Shafaa’ah (Uombezi) wangu umehalalika kwake Siku ya Qiyaamah.” [Imetolewa na Al-Arba’ah]

 

 

Na pia,

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ، أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏ " إذَا سَمِعْتُمْ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوامِثْلَ مَا يَقُولُ ، ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ ، فَإِنَّهُ مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا . ثُمَّ سلُوا اللَّه لي الْوسِيلَةَ ، فَإِنَّهَا مَنزِلَةٌ في الجنَّةِ لا تَنْبَغِي إِلاَّ لعَبْدٍ منْ عِباد اللَّه وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَنَا هُو ، فَمنْ سَأَل ليَ الْوسِيلَة حَلَّتْ لَهُ الشَّفاعَةُ

‘Abdullaah bin ‘Amruw (رضي الله عنهما)  kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akisema: ((Mtakapomsikia muadhini basi semeni kama anavyosema, kisha niswalieni, kwani mwenye kuniswalia mara moja Allaah Atamswalia mara kumi, na kisha niombeeni (kupata) ‘wasiylah’ ambayo ni manzila (heshima maalum) huko Jannah. Haitomstahikia isipokua mja mmoja katika waja wa Allaah, nami ninatarajia kuwa mja huyo, na mwenye kuniombea “Al-Wasiylah” atapata uombezi (wangu Siku ya Qiyaamah)) [Muslim (1/288)

 

 

4-Katika Iqaamah:

 

اللهُ أكبر اللهُ أكبر، أشهدُ أنْ لا إلهَ إلَّا الله، أشهدُ أنَّ محمدًا رسولُ الله، حيَّ على الصَّلاة، حيَّ على الفلاح، قد قامتِ الصَّلاةُ، قد قامتِ الصَّلاة، اللهُ أكبر اللهُ أكبر، لا إلهَ إلَّا الله. 

 

Allaahu Akbar Allaahu Akbar, Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah, Ash-hadu anna Muhammadan Rasuwlu-Allaah, Hayya ‘alas-Swalaah, Hayya ‘alal-Falaah, Qad Qaamatis-Swalaah  Qad Qaamatis-Swalaah, Allaahu Akbar Allaahu Akbar, laa ilaaha illa-Allaah

 

 

5-Katika Kikao Cha Tashahhud:

 

 

التَّحِيّـاتُ للهِ وَالصَّلَـواتُ والطَّيِّـبات، السَّلامُ عَلَيـكَ أَيُّهـا النَّبِـيُّ وَرَحْمَـةُ اللهِ وَبَرَكـاتُه، السَّلامُ عَلَيْـنا وَعَلـى عِبـادِكَ الصَّـالِحـين، أَشْـهَدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ الله، وَأَشْـهَدُ أَنَّ مُحَمّـداً عَبْـدُهُ وَرَسـولُه

At-tahiyyaatu liLLaahi, was-swalawaatu, wat-twayyibaatu, Assalaamu ‘alayka ayyuhan-Nnabiyyu warahmatu-Allaahi wa Barakaatuh, Assalaamu ‘alaynaa wa ’alaa ‘IbaadiLLaahis-swaalihiyn. Ash-hadu an-laa ilaaha illa-Allaah wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu

 

اللّهُـمَّ صَلِّ عَلـى مُحمَّـد وَعَلـى آلِ مُحمَّد كَمـا صَلَّيـتَ عَلـى إبْراهـيمَ وَعَلـى آلِ إبْراهـيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد، اللّهُـمَّ بارِكْ عَلـى مُحمَّـد وَعَلـى آلِ مُحمَّـد كَمـا بارِكْتَ عَلـى إبْراهـيمَ وَعَلـى آلِ إبْراهيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد .

Allaahumma Swalli ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Swallayta ‘alaa Ibraahiyma wa ‘alaa aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd. Allaahumma Baarik ‘alaa Muhammad, wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Baarakta ‘alaa  Ibraahiyma wa ‘alaa  aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd.

 

 

6-Du’aa Haipandi Mbinguni Bila Ya Kumswalia Mwanzo Na Mwisho Wa Du’aa:

 

 

عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ (رضي الله عنه)  قَالَ: "إِنَّ الدُّعَاءَ مَوْقُوفٌ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ لاَ يَصْعَدُ مِنْهُ شَيْءٌ حَتَّى تُصَلِّيَ عَلَى نَبِيِّكَ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)"

Imepokelewa kutoka kwa ‘Umar bin Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu): “Hakika du’aa inasimama baina ya mbingu na ardhi haipandi masafa yoyote mpaka umswalie Nabiy wako (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)." [Swahiyh At-Tirmidhiy (486), Swahiyh At-Targhiyb (1676)]

 

 

7-Kukithirisha Kumswalia Siku Ya Ijumaa:

 

عَنْ أَوْسِ بْنِ أَوْسٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ مِنْ أَفْضَلِ أَيَّامِكُمْ يَوْمَ الْجُمُعَةِ، فَأَكْثِرُوا عَلَيَّ مِنْ الصَّلاةِ فِيهِ، فَإِنَّ صَلاَتَكُمْ مَعْرُوضَةٌ عَلَيَّ)) قَالوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَكَيْفَ تُعْرَضُ صَلاتُنَا عَلَيْكَ وَقَدْ أَرَمْتَ؟  قَالَ: يَقُولُ:  بَلِيتَ  قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى حَرَّمَ عَلَى الأَرْضِ أَجْسَادَ الأَنْبِيَاءِ)) رواه ابو داوُود بِاِسنادٍ صحيح

Imepokelewa kutoka kwa Aws bin Aws (رضي الله عنه)  ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه  وآله وسلم ) amesema: ((Hakika siku zenu zilizo bora mno ni siku ya Ijumaa, basi kithirisheni kuniswalia siku hiyo, hakika Swalaah zenu huwa naletewa)). Maswahaba wakauliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Vipi Swalaah zetu kuwa unaletewa na ilihali wakati huo utakuwa umeshaoza?” Akajibu: ((Hakika Allaah Ameiharamisha ardhi kula viwiliwili vya Manabii)). [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Swahiiyh]

 

 



10-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Zuhd Yake: Godoro Na Mto Wake Ulikuwa Duni

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

10-Zuhd Yake Godoro Na Mto Wake Ulikuwa Duni

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth zifuatazo zinaelezea kuhusu godoro na mto aliokuwa akilalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): 

 

عن عَائِشَةَ، قَالَتْ كَانَ وِسَادَةُ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم الَّتِي يَتَّكِئُ عَلَيْهَا مِنْ أَدَمٍ حَشْوُهَا لِيفٌ ‏.‏

 

Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba “Mto wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  aliokuwa akiulalia ulitengenezwa kwa ngozi ya mnyama iliyojazwa magamba ya mtende.” [Muslim]

 

 Na Hadiyth ndefu ya ‘Umar bin Al-Khatwwaab (رضي الله عنه) pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipojitenga mbali na wakeze:

 

“…Mlangoni wa chumba chake kulikuwa na mtumwa, ambaye nilikwenda kwake, nikamwambia: “Niombee ruhusa kwake ili niweze kuingia”. Akaniruhusu na nikaingia ili kumuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akiwa amejinyoosha juu ya jamvi lililoacha alama ubavuni mwake. Chini ya kichwa chake kulikuwa na mto wa ngozi, ndani yake mna usumba na kulikuwa na ngozi zilizokuwa zimetundikwa na majani kwa ajili ya kutengeneza ngozi. [Al-Bukhaariy]

 

Na pia kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema: “Mto wake aliokuwa akilalia usiku, ulikuwa ni wa ngozi uliojazwa ufumwele.” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuwd (4146) na At-Tirmidhiy. Iko katika Swahiyhul Jaami’i (4714)].

 

Na kuhusu godoro lake:

 

عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ فِرَاشُ رسول الله صلى الله عليه وسلم مِنْ أُدْمٍ حَشْوُهُ لِيفٌ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amesema: "Godoro la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) lilikuwa limetengenezwa kwa ngozi iliyotiwa magamba ya mtende." [Al-Bukhaariy]

 

 

 



019-Aayah Na Mafunzo: Maamrisho Ya Kumtendea Wema Mke Na Kuvumiliana

 

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Maamrisho Ya Kumtendea Wema Mke Na Kuvumiliana

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَرِثُوا النِّسَاءَ كَرْهًا ۖ وَلَا تَعْضُلُوهُنَّ لِتَذْهَبُوا بِبَعْضِ مَا آتَيْتُمُوهُنَّ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللَّـهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا ﴿١٩﴾

Enyi walioamini! Si halali kwenu kurithi wanawake kwa kuwakirihisha. Na wala msiwazuie kwa inda ili mpokonye baadhi ya vile mlivyowapa isipokuwa wakiwa wamefanya uchafu bayana. Na kaeni nao kwa wema. Na mkiwachukia, basi asaa ikiwa mnachukia jambo na Allaah Akalijaalia kuwa lenye khayr nyingi. [An-Nisaa: 19]

 

Mafunzo:

 

Maamrisho ya kumtendea wema mke yametajwa katika Hadiyth kadhaa za  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) miongoni mwazo ni:

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنِ النَّبِيِّ ـ صلى الله عليه وسلم ـ قَالَ ‏ "‏ خَيْرُكُمْ خَيْرُكُمْ لأَهْلِهِ وَأَنَا خَيْرُكُمْ لأَهْلِي ‏"‏ ‏ رواه الترمذي

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:  ((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa mke wake, na mimi ni mbora kwa watu wangu wa nyumbani [ahli])) [Swahiyh Ibn Maajah (1621), Swahiyh At-Targhiyb (1925)].

 

 Na pia,

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا  وَخِيَارُكُمْ خِيَارُكُمْ لِنِسَائِهِمْ خُلُقًا)) الترمذي وقال: حديث حسن صحيح

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muumin aliyekamilika iymaan ni aliye na tabia njema kabisa, na wabora wenu ni walio bora kwa wake zao kwa tabia))  [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Swahiyh Hasan]

 

Na kutomchukia: “Muumini mwanaume asimchukue (mke ambaye) ni Muumini, akichukizwa tabia moja, bila shaka ataridhika naye kwa tabia yake nyingine.” [Muslim].

 

Pia Sababun-Nuzuwl: Walikuwa Waarabu zama za Jaahiliyyah pindi anapokufa mwanaume na akaacha mke, basi wale ndugu wa mume wake wanakuwa na haki zaidi kwa mwanamke, na   baadhi yao wakitaka wanamuoa, na wakitaka wanamuozesha, na wakitaka hawamuozeshi, na wao wanakuwa wana haki naye zaidi kuliko hata ndugu zake mwanamke na wazazi wake. Ndipo Allaah (عزّ وجلّ) Akateremsha Aayah hii. [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ameipokea Al-Bukhaary]. 

 

 

 

 

 



057-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Israa: Hao Wanaowaomba (Wao Wenyewe) Wanatafuta Kwa Rabb Wao...

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

017-Asbaab Nuzuwl Suwrah Al-Israa Aayah 56-57

 

 

 

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا ﴿٥٦﴾

Sema: Iteni wale ambao mnadai (ni waabudiwa) pasi Naye, basi hawamiliki kukuondesheeni dhara na wala kuihamisha (kwa mwengine).

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ ۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا ﴿٥٧﴾

Hao wanaowaomba (wao wenyewe) wanatafuta kwa Rabb wao njia ya kujikurubisha, yupi miongoni mwao awe karibu zaidi na wanataraji rahmah Yake, na wanakhofu adhabu Yake. Hakika adhabu ya Rabb wako ni ya kutahadhariwa daima. [Al-Israa: 56- 57]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ إِدْرِيسَ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ أَبِي مَعْمَرٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، فِي قَوْلِهِ عَزَّ وَجَلَّ ‏: ((أُولَئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَى رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ‏))‏ قَالَ كَانَ نَفَرٌ مِنَ الْجِنِّ أَسْلَمُوا وَكَانُوا يُعْبَدُونَ فَبَقِيَ الَّذِينَ كَانُوا يَعْبُدُونَ عَلَى عِبَادَتِهِمْ وَقَدْ أَسْلَمَ النَّفَرُ مِنَ الْجِنِّ ‏.‏

 

Ametuhadithia Abuu Bakkr bin Abiy Shaybah, ametuhadithia ‘Abdullaah bin Idriys, kutoka kwa Al-A’mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa Abuu Ma’mar, kutoka kwa ‘Abdullaah kuhusu kauli Yake Allaah (عز وجل):

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ  

Hao wanaowaomba (wao wenyewe) wanatafuta kwa Rabb wao njia ya kujikurubisha, yupi miongoni mwao awe karibu zaidi na wanataraji rahmah Yake, 

 

Amesema:  Kulikuwa na kundi la majini walisilimu lakini walikuwa wakiabudiwa, na wale waliowaabudu wakaendeea kuwaabudu ilhali majini hao walioabudiwa walisilimu.   

 

 

Na katika Riwaayah nyengine,

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ، مَسْعُودٍ ‏((‏أُولَئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَى رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ))‏ قَالَ: نَزَلَتْ فِي نَفَرٍ مِنَ الْعَرَبِ كَانُوا يَعْبُدُونَ نَفَرًا مِنَ الْجِنِّ فَأَسْلَمَ الْجِنِّيُّونَ وَالإِنْسُ الَّذِينَ كَانُوا يَعْبُدُونَهُمْ لاَ يَشْعُرُونَ فَنَزَلَتْ: ((أُولَئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَى رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ‏)) مسلم‏

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd kuhusu Aayah:

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ

Hao wanaowaomba (wao wenyewe) wanatafuta kwa Rabb wao njia ya kujikurubisha...

 

Kasema: Imeteremka kuhusu kundi la Waarabu walikuwa wakiabudu kundi katika majini. Majini hao walisilimu lakini watu waliendelea kuwaabudu bila ya wao kuhisi. Ikateremka:

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ

Hao wanaowaomba (wao wenyewe) wanatafuta kwa Rabb wao njia ya kujikurubisha…  [Muslim]

 

Na Riwaayah katika Al-Bukhaariy

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ رضى الله عنه فِي هَذِهِ الآيَةِ: ((‏الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَى رَبِّهِمِ الْوَسِيلَةَ‏))‏ قَالَ نَاسٌ مِنَ الْجِنِّ كَانُوا‏‏ يُعْبَدُونَ فَأَسْلَمُوا‏.‏

البخاري

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd amesema kuhusu Aayah hii:

 

الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ

Wale wanaowaomba (wao wenyewe) wanatafuta kwa Rabb wao njia ya kujikurubisha…

 

Imeteremshwa kuhusu baadhi ya majini waliokuwa wakiabudiwa na binaadamu. Kisha (majini hao) wakasilimu (lakini watu wakaendelea kuwaabudu). [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]

 

 



054-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Maiti Anafuatiliwa Na Matatu: Ahli Zake, Mali Na Amali, Zinabaki Amali

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

Hadiyth Ya 54

Maiti Anafuatiliwa Na Matatu: Ahli Zake, Mali Na ‘Amali Zinabaki Naye Amali Zake

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ أَنَسِ (رضي الله عنه) قَال: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((يَتْبَعُ الْمَيِّتَ ثَلاَثَةٌ: أَهْلُهُ وَمَالُهُ وَعَمَلُهُ. فَيَرْجِعُ اثْنَانِ وَيَبْقَى واحِدٌ: يَرِجِعُ أَهْلُهُ وَمَالُهُ وَيَبْقَى عَمَلُهُ)) متفق عليه

 

 Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Maiti hufuatwa na mambo matatu: ahli zake, mali yake, na ‘amali zake. Hurejea mawili na likabakia moja. Ahli zake na mali yake hurejea, na zikabakia ‘amali zake)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. ‘Amali njema anazozitanguliza mtu ni kheri yake kuliko anayoyaacha nyuma, na ‘amali hizi ndizo zitakazodumu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

 مَا عِندَكُمْ يَنفَدُ ۖ وَمَا عِندَ اللَّـهِ بَاقٍ ۗ وَلَنَجْزِيَنَّ الَّذِينَ صَبَرُوا أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٦﴾

Mlivyo navyo nyinyi vinatoweka, na vilioko kwa Allaah ni vya kubakia. Na kwa yakini Tutawalipa wale waliosubiri ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda. [An-Nahl 16: 96)]

 

 

2. Kila mmoja ataingia kaburini peke yake, ataacha kila kitu nyuma yake ila ‘amali zake ndizo zitakazomfaa zikiwa ni njema. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَادَىٰ كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَاكُمْ وَرَاءَ ظُهُورِكُمْ ۖ  

  Na kwa yakini mmetujia mmoja mmoja kama Tulivyokuumbeni mara ya kwanza; na mmeyaacha nyuma yenu yote Tuliyokuruzukuni.  [Al-An’aam (6: 94]

 

 

Rejea pia: Maryam (19: 95).

 

Na Rejea: Hadiyth namba (1).

 

 

3. Muumin anapasa akimbilie kutenda ‘amali njema nyingi zimfae Aakhirah. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ ﴿٣٩﴾

Na kwamba insani hatopata (jazaa) isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi.

 

وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ يُرَىٰ ﴿٤٠﴾

Na kwamba juhudi yake itakuja kuonekana

 

ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاءَ الْأَوْفَىٰ ﴿٤١﴾

Kisha atalipwa jazaa kamilifu. [An-Najm (53: 39-41)]

 

 

Rejea pia: Aal-‘Imraan (3: 133), Al-Hadiyd (57: 21), Al-Hashr 59: 18), Al-Baqarah (2: 110), Al-Muddath-thir (74: 74).

 

 

4. Wanaobaki nyuma ya maiti iwe ni funzo kwao watambue kwamba nao bila shaka siku moja watapelekwa kaburini.

 

 

5. Rejea Hadiyth namba (8) (63) (72), (78). 

 

 

 



20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...