Translate

Ijumaa, 14 Agosti 2020

Kifua Kikuu (Tuberculosis-TB) Ni Ugonjwa Gani?

 

mgonjwa wa TB

 

Kifua Kikuu (Tuberculosis) ni ugonjwa wa kuambukiza ambao mara nyingi hushambulia mapafu. Ugonjwa huu unachukua nafasi ya pili duniani ya vifo vinavyotokana na maambukizi yanayotokana na kitu kimoja. Ugonjwa wa kifua kikuu huenezwa na bakteria na  kifua kikuu (TB) huenea kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia matone madogo yanayotolewa na mtu akikohoa au kupiga chafya. Awali, ugonjwa huu ulikuwa nadra katika nchi zilizoendelea, lakini maambukizi yalianza kuongezeka mwaka 1985, kwa namna fulani yakichangiwa na kuibuka kwa HIV, virusi waletao UKIMWI.

Vizazi vingi vya bakteria wa tuberculosis vimekuwa sugu kwa dawa ambazo zilikuwa zikitumika kuuponya ugonjwa huo. Watu wenye ugonjwa huo wanawajibika kutumia dawa za aina nyingi kwa muda mrefu ili waweze kupona.

Katika miaka ya katikati ya karne za 18 na 19, kulitokea milipuko ya ugonjwa huu huko Ulaya na Marekani Ya Kaskazini, kabla ya mwanasayansi kutoka Ujerumani, Robert Koch, kumgundua bakteria anayesababisha kifua kikuu mwaka 1882.

Kufuatia ugunduzi wa Robert Koch, ugunduzi na utumiaji wa chanjo na dawa za kuponya kifua kikuu ulileta imani kuwa ugonjwa huu ungetokomezwa. Mara moja Shirika la Umoja Wa Mataifa lilibashiri kuwa ugonjwa huu utakuwa umetokomezwa kufikia 2025.

Lakini katika miaka ya kati ya 1980 na 1990, TB iliongezeka kwa kasi duniani, hivi kwamba mwaka 1993 Shirika La Afya Duniani (WHO) lilitangaza hali ya hatari, kwa mara ya kwanza kabisa ugonjwa kutangazwa kwa namna hiyo.

Kwa bahati nzuri, kwa kufuata tiba kikamilifu, watu wengi waliopata TB hupona. Bila kupewa tiba nzuri, katika idadi ya wagonjwa wote wa TB, wagonjwa wafikiao hadi theluthi mbili watafariki dunia.

 

Tuberculosis Ni Nini?

 

Madakatari hutofautisha kati ya aina mbili za maambukizi ya kifua kikuu: latent na active.

 

TB aina za TB

 

Latent TB – bakteria hubaki ndani ya mwili bila kuleta madhara. Hawatoi dalili zo zote, na hawaambukizi, lakini wanaweza kuja kuanza kuleta madhara.

Active TB – bakteria wanaleta madhara na wanaweza kuambukiza kwa wengine.

Inaaminika kuwa karibu theluthi moja ya watu duniani wana latent TB. Kuna asilimia 10 ya uwezekano wa watu hawa kupata active TB, uwezekano huo ukichagizwa na upungufu wa kinga za mwili au kukosa mlo wa kutosha au kuvuta sigara.

TB ni ugonjwa unaoshambulia watu wa rika zote na watu wa pande zote za dunia. Lakini ugonjwa huu hushambulia zaidi vijana na watu wanaoishi kwenye nchi zinazoendelea. Takwimu za 2012 zilionyesha kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wa TB walitoka katika nchi 22 tu.

 

Kifua Kikuu Husambazwa Na Nini?

 

TB husambazwa na bakteria aitwaye Mycobacterium tuberculosis. Bakteria huyu husambaa kwenye hewa wakati mtu mwenye TB (ambaye mapafu yake yameshambuliwa) akikohoa, akipiga chafya, akitema mate, akicheka , au akizungumza.

TB huambukiza lakini siyo rahisi kuipata. Uwezekano wa kupata TB kutoka kwa mtu unayeishi au kufanya naye kazi ni mkubwa kuliko kutoka kwa mgeni. Watu wengi ambao tayari wamaeanza tiba sahihi angalau kwa wiki 2 hawaambukizi.

Toka antibiotics zilipoanza kutumika kutibu TB, baadhi ya aina ya bakteria hao wamegeuka sugu kwa dawa. Multidrug-resistant TB (MDR-TB) ni hali ambapo dawa haziwezi tena kuwaua bakteria wote, bakteria wanaosalia wakijijengea usugu wa dawa hiyo na dawa nyingine pia kwa wakati mmoja.

Multidrug-resistant TB (MDR-TB) inatibika kwa kutumia dawa za kipekee (very specific anti-TB drugs) ambazo ni chache na hazipatikani kirahisi. Katika mwaka 2012, karibu watu 450,000 walipata MDR-TB.

Watu wenye upungufu wa kinga za mwili huwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata active TB. HIV hudhoofisha kinga za mwili, na kuufanya mwili kupata shida ya kudhibiti bakteria wa TB. Watu wenye mchanganyiko wa HIV na TB wana uwezekano wa kupata active TB kwa kiwango cha asilimia 20-30 ukilinganisha na wale ambao hawana HIV.

Matumizi ya tumbaku yamedhihirika kuongeza uwezekano wa kupata active TB. Asilimia 20 ya TB duniani huhusishwa na matumizi ya tumbaku.

 

Dalili Za Kifua Kikuu

 

Wakati latent TB haina dalili zo zote, active TB huwa na dalili zifuatazo:

. Kukohoa, wakati mwingine kukiwa na makohozi au damu
. Kusikia baridi
. Uchovu
. Homa
. Kukonda kwa mwili
. Kukosa hamu ya kula
. Kutoa jasho usiku

 

dalili za kifua kikuu

 

Kifua kikuu huathiri hasa mapafu, lakini kinaweza kuathiri vile vile sehemu nyingine za mwili. Wakati TB imeathiri sehemu tofauti ya mwili, dalili zinaweza kubadilika. Bila kupata tiba, TB huweza kusambaa kwenye sehemu nyingine za mwili kupitia mfumo wa damu.

. Tb ikishambulia mifupa inaweza kuleta maumivu ya uti wa mgongo na kuharibu maungio ya mifupa
. TB ikishambulia ubongo husababisha meningitis
. TB ikishambulia maini na figo huweza kusababisha damu ndani ya mkojo
. TB ikishambulia moyo inaweza kuathiri uwezo wa moyo wa kusukuma damu na kusababisha cardiac tamponade ambayo inaweza kuua.

 

Tiba Ya Kifua Kikuu

 

Wagonjwa wengi wa TB wanaweza kupona kama dawa stahiki itakuwepo na kutolewa inavyopaswa. Aina ya dawa na urefu wa muda wa matumizi vitategemea umri wa mgonjwa, hali yake ya afya kwa ujumla, usugu wa mwili wake kwa dawa, kama TB in latent au active, sehemu yake ya mwili iliyoathirika (i.e mapafu, ubongo, figo)
Watu wenye latent TB wanaweza kuhitaji aina moja tu ya dawa, wakati watu wenye active TB (na hasa MDR-TB) watahitaji mchanganyiko wa dawa.

 

TB tiba ya TB

 

Antibiotics za TB hutakiwa kutumiwa kwa muda mrefu kidogo, muda wa wastani ukiwa ni miezi 6.

Matumizi ya dawa za kifua kikuu huweza kusababisha sumu kwa ini, ingawa ni mara chache hili kutokea, linapotokea, linaweza kuleta matatizo makubwa. Madhara ya dawa hizi yanapojitokeza, ni lazima taarifa itolewe kwa daktari. Madhara hayo ni pamoja na:
.  Mkojo mweusi
.  Homa
.  Homa ya manjano
.  Kukosa hamu ya kula
.  Kichefuchefu na kutapika

Ni muhimu kwa mgonjwa kuhakikisha kuwa anamaliza dawa, hata kama dalili za TB zitakuwa zimeondoka. Bakteria waliosalia na kuvumilia tiba iliyotolewa wanaweza kugeuka sugu kwa tiba hiyo na kupelekea kupata MDR-TB hapo baadaye.

Kataka mada nyingine tatajadili kuhusu ugonjwa wa homa ya ini (hepatitis) .

Ndugu msomaji, usisite kutoa maoni yako au kuuliza maswali kuhusu mada hii. Tutafurahi kuwa nawe na kukujibu.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

 

Ijumaa, 7 Agosti 2020

11-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Kutufu Makaburi Kuwaomba Waliomo Kaburini

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

11- Kutufu Makaburi Kuwaomba Waliomo Kaburini

Alhidaaya.com

 

 

Miongoni mwa shirki kubwa ni kutufu makaburini, kuwaomba au kutawasali kwa walio makaburini. Maiti hawasikii du’aa wala hawaitikii, bali hawana uwezo wa kumnufaisha mtu wala kumdhuru! Dalili ni kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) zifuatazo:  

 

 إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ ۖ فَادْعُوهُمْ فَلْيَسْتَجِيبُوا لَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٩٤﴾

Hakika wale mnaowaomba badala ya Allaah ni waja kama nyinyi. Hebu waiteni wakuitikieni ikiwa nyinyi ni wakweli. [Al-A’raaf: 194] 

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ﴿١٠٦﴾

Na wala usiombe badala ya Allaah visivyokufaa wala visivyokudhuru. Na ukifanya, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu. [Yuwnus: 106] 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَجِيبُونَ لَهُم بِشَيْءٍ إِلَّا كَبَاسِطِ كَفَّيْهِ إِلَى الْمَاءِ لِيَبْلُغَ فَاهُ وَمَا هُوَ بِبَالِغِهِ ۚ وَمَا دُعَاءُ الْكَافِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَالٍ ﴿١٤﴾

Na wale wanaowaomba badala Yake, hawawaitikii kwa chochote isipokuwa kama anayenyosha viganja vyake viwili vya mikono kwenye maji ili yafikie kinywani mwake, na wala hayafikii hata kidogo.  Na du’aa za makafiri hazipo ila katika upotofu.  [Ar-Ra’d: 14] 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 قُلْ مَن رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ قُلِ اللَّـهُ ۚ قُلْ أَفَاتَّخَذْتُم مِّن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ لَا يَمْلِكُونَ لِأَنفُسِهِمْ نَفْعًا وَلَا ضَرًّا ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ أَمْ هَلْ تَسْتَوِي الظُّلُمَاتُ وَالنُّورُ ۗ أَمْ جَعَلُوا لِلَّـهِ شُرَكَاءَ خَلَقُوا كَخَلْقِهِ فَتَشَابَهَ الْخَلْقُ عَلَيْهِمْۚ قُلِ اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿١٦﴾

Sema: “Ni nani Rabb wa mbingu na ardhi?” Sema: “Ni Allaah.” Sema: “Je, mnawafanya wengineo badala Yake kuwa walinzi na hali hawamiliki kwa ajili ya nafsi zao manufaa wala dhara?”  Sema: “Je, kipofu analingana sawa na mwenye kuona, au je, viza vinalingana sawa na nuru?” Au wamemfanyia Allaah washirika walioumba kama uumbaji Wake, kisha yakafanana maumbile kwao?  Sema: “Allaah ni Muumbaji wa kila kitu, Naye ni Mmoja Pekee, Mwenye kudhibiti na kudhalilisha, Mshindi, Asiyepingika.” [Ar-Ra’d: 16] 

 

 

Nukuu kutoka Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (1/206) inasema:

 “…wala haijuzu kuomba du’aa kwa Mawalii au wengineo baada ya kufa kwao, bali inajuzu kuwaomba waja wema wakuombee. Wala haijuzu kutufu makaburi, kwani kutufu ni makhsusi kwa Ka’bah tukufu pekee. Atakayetufu makaburini kwa ajili ya kujikurubisha na watu wake humo ni shirki kubwa, japokuwa akiwa anakusudia kujikurubisha kwa Allaah tu! Hivyo ni bid’ah inayochukiza kabisa kwani haipasi kutufu makaburi wala kuswali kuyaelekea hata kama itakuwa ni kwa makusudio ya kutaka radhi za Allaah.” 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa): 

وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ ﴿١٣﴾

Na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende.

 

 

إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ ﴿١٤﴾

 Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, hawatakuitikieni.  Na Siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu, na wala hakuna atakayekujulisha vilivyo kamaMwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Faatwir: 13-14] 

 

 

Bali Siku ya Qiyaamah utadhihirika uadui baina yao na watawakanusha kabisa kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)! 

 

وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّن يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَن لَّا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَهُمْ عَن دُعَائِهِمْ غَافِلُونَ﴿٥﴾

 

“Na nani aliyepotoka zaidi kuliko ambaye anayeomba asiyekuwa Allaah ambaye hamuitikii mpaka Siku ya Qiyaamah; nao wala hawatambui  maombi yao.”

 

 

وَإِذَا حُشِرَ النَّاسُ كَانُوا لَهُمْ أَعْدَاءً وَكَانُوا بِعِبَادَتِهِمْ كَافِرِينَ﴿٦﴾

Na pale watakapokusanywa watu, (miungu ya uongo) watakuwa ni maadui wao, na watakuwa wenye kuzikanusha ‘ibaadah zao. [Al-Ahqaaf: 5- 6] 

 

 

 

Washirikina kabla ya Uislamu walikuwa wakiomba masanamu ya Al-Laata, ‘Al-‘Uzza na wengineo, na hawakuwa wakiitakidi kuwa wana uwezo wa kuumba au kuteremsha mvua bali walidai kuwa yanawakurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kwamba masanamu hayo ni kama viombezi kwao. Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): 

 

وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ فِي مَا هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ كَاذِبٌ كَفَّارٌ ﴿٣﴾

na wale waliojichukulia badala Yake walinzi (wakisema): “Hatuwaabudu isipokuwa ili wapate kutukurubisha kwa Allaah tumkaribie” Hakika Allaah Atahukumu baina yao katika yale waliyokhitilafiana nayo. Hakika Allaah Hamwongoi aliye muongo, kafiri. [Az-Zumar: 3] 

 

Basi hakuna tofauti na wanaoomba wakaazi wa makaburi kwani sanamu, makaburi, matwaghuti… yote yana maana moja ya kuabudu au kuomba asiyekuwa Allaah; ikiwa ni maiti au hai, na sababu za kuomba ni kama hizo. Anakanusha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) hayo Anaposema:

 

قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا ﴿٥٦﴾

Sema: “Iteni wale ambao mnadai (ni waabudiwa) pasi Naye, basi hawamiliki kukuondesheeni dhara na wala kuihamisha (kwa mwengine).” [Al-Israa: 56] 

 

 

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anamwambia Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) awajibu washirikina: 

 

 قُلْ أَفَرَأَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ إِنْ أَرَادَنِيَ اللَّـهُ بِضُرٍّ هَلْ هُنَّ كَاشِفَاتُ ضُرِّهِ أَوْ أَرَادَنِي بِرَحْمَةٍ هَلْ هُنَّ مُمْسِكَاتُ رَحْمَتِهِ ۚ قُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ ۖ عَلَيْهِ يَتَوَكَّلُ الْمُتَوَكِّلُونَ﴿٣٨﴾

Sema: “Je, mnaonaje wale mnaowaomba badala ya Allaah; ikiwa Allaah Atanikusudia dhara; je, wao wataweza kuondosha dhara Yake? Au Akinikusudia rahmah; je wao wataweza kuizuia rahmah Yake?” Sema: “Ananitosheleza Allaah”, Kwake watawakali wenye kutawakali. [Az-Zumar: 38] 

 

Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۚ وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ ۚ إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿١٨٨﴾

Sema: “Siimilikii nafsi yangu manufaa yoyote wala dhara yoyote isipokuwa Apendavyo Allaah. Na lau ningekuwa najua ya ghayb, bila shaka ningelijikithirishia ya kheri, na wala lisingelinigusa ovu. Mimi si chochote isipokuwa ni mwonyaji na mbashiriaji kwa watu wanaoamini.” [Al-A’raaf: 188] 

 

Na pia Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَمَا لَهُمْ فِيهِمَا مِن شِرْكٍ وَمَا لَهُ مِنْهُم مِّن ظَهِيرٍ ﴿٢٢﴾

Sema: “Ombeni wale mnaodai kwa dhana (ni waabudiwa) badala ya Allaah, hawamiliki hata uzito wa sisimizi mbinguni wala ardhini, na wala hawana humo ushirika Naye, na wala Yeye (Allaah) Hana msaidizi miongoni mwao.” [Sabaa: 22] 

  

Tahadhari Muislamu kuingia katika shirki kubwa juu ya kuwa hao wanaoombwa hawawezi kukuitikia du’aa zako bali elekea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ambaye Ndiye Mwenye uwezo wa kukunufaisha au kukuondoshea madhara kama Anavyosema: 

 

أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٦٢﴾

Au nani Anayemuitika mwenye dhiki mno anapomwomba, na Akamuondoshea ouvu na Akakufanyeni makhalifa wa ardhi? Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Ni machache mno mnayokumbuka. [An-Naml: 62] 

 

 

Aayah hiyo aliisoma mtu alipofikwa na balaa la kukaribia kuuliwa, alipoisoma Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alimuokoa. [Tafsiyr Ibn Kathiyr] 

 

Tena Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Yuko karibu mno nawe na Mwenye kuitikia du’aa za kila anayemuomba, Anasema: 

 

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ﴿١٨٦﴾

Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka. [Al-Baqarah: 186] 

 

 

Na fuata mafunzo Swahiyh kama alivyofundisha Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba unapozuru au kupitia makaburi usome du’aa: 

 

السَّلامُ عَلَـيْكُمْ أَهْلَ الدِّيارِ مِنَ المؤْمِنيـنَ وَالْمُسْلِمينَ، وَإِنّا إِنْ شاءَ اللهُ بِكُـمْ لاحِقُـونَ، (وَيَرْحَمُاللَّهُالْمُسْتَقْدِمِينَ مِنَّاوَالْمُسْتَأْخِرِينَ) أَسْـاَلُ اللهَ لَنَـا وَلَكُـمْ العَـافِيَةَ. 

Assalaamu ’Alaykum ahlad-diyaar minal Mu-uminiyna wal Muslimiyn, wainnaa In Shaa Allaahu bikum laahiquwn. (Wa yarhamu-Allaahu al-mustaqdimiyna minnaa wal musta-akhiriyna). As-alu-Allaaha lanaa walakumul-’aafiyah.

 

Amani ishuke juu yenu watu wa nyumba za Waumini na Waislamu, nasi apendapo Allaahtutakutana nanyi (Na Allaah Awarehemu wa mwanzo na wa mwisho). Namuomba Allaah Atupe sisi nanyi afya njema. [Hadiyth ya Buraydah bin Al-Huswayb (Radhwiya Allaahu ‘anhu) - Muslim (2/671) [975], Ibn Maajah na tamshi lake (1/494) [1547] kutoka kwa Buraydah  (Radhwiya Allaahu ‘anhu). Yaliyo katika mabano ni Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) iliyopokelewa na Muslim (2/671) [974].] 

 

 

 



49-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Nabiy Pekee Aliyepewa Kauli Za Kusherehi Kitabu Chake

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

49-Nabiy Pekee Aliyepewa Kauli Za Kusherehi Kitabu Chake

 

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

  وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾

 (Tumewatuma) Kwa hoja bayana na vitabu. Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari. [An-Nahl: 44]

 

 

Maana yake: “Tumekuteremshia Qur-aan ee Rasuli, ili uwabainishie wazi watu yaliyofichikia katika maana zake, hukmu zake na ili wazingatie (Aayaat) na waongoke kwayo.” [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

Hivyo basi anayoyasema katika kusherehi Aayaat za Qur-aan ni Wahyi Aliofunuliwa Na Allaah (سبحانه وتعالى) Ambaye Anasema:

 

 

مَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾

Na wala hatamki kwa hawaa.

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. [An-Najm: 3-4]

 

Akasema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  kuthibitisha hayo katika Hadiyth:

 

((أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ مَعَهُ)) صحيح رواه أبو داود

((Hakika mimi nimepewa Qur-aan na mfano wake)) [Hadiyth Swahiyh, Abuu Daawuwd]

 

 

 



05-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Zuhd Yake: Akibaki Na Njaa Na Chakula Chake Kilikuwa Duni

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

05-Zuhd Yake: Akibaki Na Njaa Na Chakula Chake Kilikuwa Duni  

 Alhidaaya.com

 

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akibaki na njaa yeye pamoja na ahli zake, na aghlabu ya chakula chake kilikuwa ni duni.  Hadiyth kadhaa zimethibiti kuhusu hali hizi, miongoni mwazo ni Hadiyth zifuatazo:

 

Aghlabu ya chakula chao kilikuwa ni mkate wa shayiri:

 

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال :  "كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَبِيتُ اللَّيَالِي الْمُتَتَابِعَةَ طَاوِيًا ، وَأَهْلُهُ لاَ يَجِدُونَ عَشَاءً ، وَكَانَ أَكْثَرُ خُبْزِهِمْ خُبْزَ الشَّعِيرِ" رواه الترمذي (2360) وحسنه الألباني في صحيح الترمذي .

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akipitisha nyusiku kadhaa na ilhali ahli zake hawakupata chakula cha usiku, na aghlabu ya chakula chao kilikuwa ni mkate wa shayiri.” [At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy]  

 

Hakupata kula nyama ya kuoka wala mkate mwembamba:

 

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سِنَانٍ، حَدَّثَنَا هَمَّامٌ، عَنْ قَتَادَةَ، قَالَ: "كُنَّا عِنْدَ أَنَسٍ وَعِنْدَهُ خَبَّازٌ لَهُ فَقَالَ مَا أَكَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم خُبْزًا مُرَقَّقًا وَلاَ شَاةً مَسْمُوطَةً حَتَّى لَقِيَ اللَّهَ"‏.‏  البخاري

Ametuhadithia Muhammad bin Sinaan, ametuhadithia Hammaam, kutoka kwa Qataadah amesema: Tulikuwa kwa Anas na mwokaji mikate alikuwa pamoja naye. Anas akasema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakupata kula mkate mwembamba wala mbuzi wa kuokwa mpaka kukutana kwake na Allaah (kufariki kwake).”  [Al-Bukhaariy]

 

Hakupata kula supu ya nyama ya kuwashibisha siku tatu mfululizo:

 

عَنْ عَائِشَةَ رضى الله عنها قَالَتْ: "مَا فَعَلَهُ إِلاَّ فِي عَامٍ جَاعَ النَّاسُ، أَرَادَ أَنْ يُطْعِمَ الْغَنِيُّ الْفَقِيرَ، وَإِنْ كُنَّا لَنَرْفَعُ الْكُرَاعَ بَعْدَ خَمْسَ عَشْرَةَ، وَمَا شَبِعَ آلُ مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم مَنْ خُبْزِ بُرٍّ مَأْدُومٍ ثَلاَثًا"‏.‏

‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema:  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakufanya hivyo (yaani: kukataza uhifadhi wa nyama ya Udhwhiya kwa siku tatu) isipokuwa (aliruhusu kuhifadhi nyama) ili tajiri awalishe masikini. Lakini baadaye tulikuwa tunaweka makongoro (ya mbuzi) zaidi ya siku kumi na tano. Familia ya Muhammad haikupata kula mkate wa ngano kwa nyama au supu ya kuwashibisha kwa siku tatu mfululizo.”   [Al-Bukhaariy]

 

Faida:

 

‘Aaishah (رضي الله عنها) aliulizwa katika Hadithi hii kuhusu ukatazaji wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kula nyama ya Udhwhiyah baada ya siku tatu. Akasema kuwa Nabiy aliamrisha  hivyo yaani kuhifadhi nyama ya Udhwhiyah. (Kuchinjwa mnyama siku ‘Iydul-Adhwhaa) kwa siku tatu katika mwaka uliokuwa ni mwaka wa njaa ili tajiri waweze kulisha maskini nyama ya Udhwhiyah.

 

 



190-Aayah Na Mafunzo: Unapoamka Tahajjud Sunnah Kusoma Aayah Za Mwisho Suwratul-‘Imraan

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Unapoamka Tahajjud Sunnah Kusoma Aayah Za Mwisho Suwratul-‘Imraan

Alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾ 

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana; bila shaka ni Aayaat (ishara, zingatio n.k.) kwa wenye akili. [Aal-'Imraan:]

 

Mafunzo:

 

 

Ni Sunnah kuzisoma Aayah kuanzia hiyo mpaka mwisho wa Suwrah anapoamka mtu usiku kuswali (tahajjud). Pia Mama wa Waumini ‘Aaishah  (رضي الله عنها)aliulizwa kuhusu jambo la ajabu alilolishuhudia kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ‘Aaishah akalia kwanza kisha akasema: Mambo yake yote yalikuwa ya ajabu! Usiku mmoja alikuja karibu na mimi mpaka ngozi yake ikagusa ngozi yangu na akasema: “Huniachi nimuabudu Rabb wangu?” Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Wa-Allaahi hakika mimi napenda ukaribu wako kwangu na pia napenda mahaba yako, na kwamba napenda usiwe mbali na mimi, na napenda yale yanayokufurahisha. Akasema ('Aaishah): Akainuka na kutumia kiroba cha maji na akafanya wudhuu wala hakutumia maji mengi., kisha akasimama akaswali 'Tahajjud' akalia mpaka ndevu zake zikawa zimerowa. Kisha akasujudu na kulia mpaka akaifanya ardhi irowe. Kisha akalala kwa upande wa kulia mpaka akaja Bilaal kumjulisha Adhaan ya Alfajiri, akamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Jambo gani linakuliza na hali Allaah (سبحانه وتعالى) Amekwishakufutia madhambi yako yaliyotangulia na yanayokuja? Nabiy(صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema: “Ee Bilaal! Nini kinizuie mimi kulia wakati usiku huu Allaah (سبحانه وتعالى) Ameniteremshia Aayah hizi? – “Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano ya usiku na mchana; bila shaka ni Aayaat… (mpaka mwisho wa Suwrah hii ya Aal-‘Imraan). Kisha akasema: “Ole wake, yule anayezisoma lakini hatafakari kwayo.” [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo].

 

 



014-Asbaabun-Nuzuwl: Ibraahiym: Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah...

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

014-Suwrah Ibraahiym Aayah: 27

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَيُضِلُّ اللَّـهُ الظَّالِمِينَ ۚ وَيَفْعَلُ اللَّـهُ مَا يَشَاءُ﴿٢٧﴾

Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah. Na Allaah Huwaacha kupotoka madhalimu. Na Allaah Anafanya Atakavyo. [Ibraahiym: 27]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

عَنِ الْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ‏)) قَالَ: ‏ نَزَلَتْ فِي عَذَابِ الْقَبْرِ فَيُقَالُ لَهُ: مَنْ رَبُّكَ فَيَقُولُ رَبِّيَ اللَّهُ وَنَبِيِّيَ مُحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم ‏.‏ فَذَلِكَ قَوْلُهُ عَزَّ وَجَلَّ: ((يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ))

 

Al-Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema (kuhusu kauli ya Allaah):

 

يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ  

Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti…

 

Amesema: “Imeteremka kuhusiana na adhabu ya kaburini. Huulizwa mtu humo: “Nani Rabb wako?” Husema: “Rabb wangu ni Allaah, na Nabiy wangu ni Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)”, basi hiyo ndio kauli Yake Allaah (عز وجل):

 

يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ  

Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah.

 

[Muslim - Kitabu Cha Jannah, Sifa Zake, Neema Zake na Wakazi Wake]

 

 

Riwaayah ya Muslim na Sunan An-Nasaaiy imesema:

 

يُقَالُ لَهُ مَنْ رَبُّكَ فَيَقُولُ رَبِّيَ اللَّهُ وَدِينِي دِينُ مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم

“Huulizwa mtu kaburini: Nani Rabb wako? Hujibu: Rabb wangu ni Allaah, na Dini yangu ni Dini ya Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)…”

 

Na pia,

 

عنِ الْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ‏"‏الْمُسْلِمُ إِذَا سُئِلَ فِي الْقَبْرِ يَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ، فَذَلِكَ قَوْلُهُ: ((‏يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ‏))

 

Imehadithiwa na Al-Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Muislamu atakapoulizwa kaburini ashuhudie kwamba:

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ

Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah

 

Basi hiyo ndio maana ya Kauli Yake (Allaah):

 

يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ  

Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah.

 

[Al-Bukhaariy – Kitaab Cha Tafsiyr]

 

 

 



049-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Swalaah Husafisha Madhambi Kama Anavyojisafisha Mtu Anapooga

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya  49

Swalaah Husafisha Madhambi Kama Anavyojisafisha Mtu Anapooga

Alhidaaya.com

 

 

 

 

عَنْ جَابِرٍ (رضي الله عنه) قَالَ:  قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((مَثَلُ الصَّلَوَاتِ الْخَمْسِ كَمَثَلِ نَهْرٍ جَارٍ غَمْرٍ عَلَى بَابِ أَحَدِكُمْ يَغْتَسِلُ مِنْهُ كُلَّ يَوْمٍ خَمْسَ مَرَّاتٍ)) مسلم  

 

 Kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mfano wa Swalaah tano ni kama mfano wa mto uliojaa maji mengi upitao mbele ya mlango wa mmoja wenu, anaoga mara tano kwa siku)). [Muslim]

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

 

1. Bainisho la umuhimu wa Swalaah za fardhi, na Aayah nyingi zimetaja maamrisho ya Swalaah.

 

 

 [Rejea: An-Nisaa (4: 103), Al-Baqarah (2: 43), An-Nuwr (24: 56), Ar-Ruwm (30: 31)].

 

 

2. Swalaah husafisha madhambi madogo madogo kama maji yanavyoondosha uchafu mwilini.

 

وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ﴿١١٤﴾

Na simamisha Swalaah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku; hakika mema yanaondosha maovu. Hivyo ni ukumbusho kwa wanaokumbuka. [Huwd (11: 114)]

 

 

 3. Muumin anahifadhika kutenda maasi, kwani siku nzima kuna vipindi vya Swalaah vinavyomsubiri asimamishe Swalaah, kwa hiyo Swalaah ni kinga ya maasi. [Al-‘Ankabuwt (29: 45)].

 

 

4. Hadiyth inatoa mfano miongoni mwa  mifano ya kulingana, kubainisha, na kufahamisha jambo fulani.

 

 

5. Hikma ya maneno ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika kufunza Maswahaba zake kwa kupiga mifano mizuri iliyo sahali kufahamika kwao na kwetu sisi tunaposoma Hadiyth kama hizi. 

 

 

 



20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...