Translate

Jumanne, 23 Juni 2020

Vitu 6 nilivyojifunza kuhusu vidonda vya tumbo

VITU 6 NILIVYOJIFUNZA KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO

Vitu 6 nilivyojifunza kuhusu vidonda vya tumbo 1

1. Vinaweza kumpata mtu yeyote.

Mwanzoni  mwa miaka ya 1980 wakati madaktari na watu wengine wote walipokuwa wakiwaambia watu kwamba vidonda vya tumbo vilikuwa vinasababishwa na msongo wa mawazo (stress) na vyakula vyenye kusisimua (vyenye pilipili – spiced foods), wanasayansi wawili kutoka Australia wakagundua kwamba pamoja na hayo kisababishi kikuu kingine cha vidonda vya tumbo ni bakteria ajulikanaye kama ‘Helicobacter pylori’.

Ugunduzi huo wa hawa wanasayansi wawili ndiyo ukawawezesha kupata tuzo ya Nobel ya mwaka 2005 na kukaanza zama za kutibu vidonda vya tumbo kwa kutumia antibiotiki.

Pamoja na hayo yote bado jinamizi la vidonda vya tumbo limeendelea kusumbuwa mamilioni ya watu kote duniani mwaka hadi mwaka.

Inakadiriwa katika kila watu watatu mtu mmoja ana vidonda vya tumbo na wengi wa hawa wagonjwa tayari wamekata tamaa kwamba kuna kupona vidonda vya tumbo na wameamua na wamekubali kuishi na vidonda vya tumbo kama sehemu ya maisha yao.

Pia matumizi ya muda mrefu mrefu au ya mara kwa mara ya baadhi ya dawa za hospitali kama vile ibuprofen au aspirin nayo huchangia kutokea kwa vidonda vya tumbo.

2. Inachukuwa muda kufahamu ni nini hasa unatakiwa kula

Inachukuwa muda kufahamu ni chakula gani hasa unatakiwa kula na ni vyakula vipi hutakiwi kula.

Vyakula vikuu unavyopaswa kupenda kula ni vile vinavyokupeleka kupunguza asidi, gesi na sumu mwilini.

Kumekuwa na mkanganyiko na marumbano ya hapa na pale juu ya nini mgonjwa wa vidonda vya tumbo unaweza kula au usile.

Kwa hapa mimi nilipata somo kuu moja tu nalo ni kuhakikisha asilimia 80 ya chakula chako kwa siku iwe ni matunda na mboga za majani.

Hii ina maana kwamba kama kwa siku unakula chakula cha uzito wa kg 2 kwa mfano basi kg 1 na gram 80 ziwe ni matunda na mboga za majani na gram 20 tu ndiyo viwe vyakula vingine ambavyo bado ni vyakula rafiki kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo.

Watu wengi tunaposema ule kwa wingi matunda na mboga za majani huwa hawaelewi.

Wanafikiri ni kitendo cha wewe kula wali sahani imejaa halafu umalizie na chungwa au parachichi moja eti ndiyo umekula matunda.

Siyo hivyo.

Inafaa hiyo sahani iliyojaa ugali ndiyo ijae mboga za majani au matunda na ugali uwe ndiyo matonge 10 au 15 tu.

Ili kupata faida hasa kwa upande huu amua na utenge mlo mmoja katika milo yako mitatu kwa siku mlo mmoja uwe ni matunda au mboga za majani pekee.

Ningekushauri mlo wa asubuhi uwe ni matunda tu au juisi ya matunda yenye asali ndani yake na siyo sukari au mlo wako wa usiku uwe ni matunda na mboga mboga za majani tu.

Kama utaweza kupata mboga ya majani unayoweza kuila ikiwa mbichi bila kupikwa katika moto hiyo ndiyo nzuri zaidi kwako.

Wazungu wana mboga nyingi za namna hii ambazo huliwa mbichi hivyo hivyo bila kupikwa.

Nakushauri upande mti wa mlonge nyumbani kwako, majani yake yanaweza kuliwa mabichi na yana vitamini C mara 7 zaidi ya ile ya kwenye chungwa. Ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako kwa siku inakutosha kwenye kachumbali au hata katika juisi ya matunda.

Pia pendelea kula kabeji mbichi mara kwa mara.

Ukifeli hapa kwenye vyakula kupona kwako vidonda vya tumbo itakuwa ni mtihani na utakata tamaa na utaamini vidonda vya tumbo havitibiki jambo ambalo si kweli.

Ukweli ni kwamba hata madaktari wenyewe bado hawafahamu ni kwa vipi baadhi ya vyakula vinasababisha gesi na matatizo ya mmeng’enyo wa chakula.

Ukiacha vyakula au vinywaji, tumbo lenyewe kwa asili huitengeneza hii asidi ili kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi yake ya kumeng’enya chakula.

Kwa ujumla kama una vidonda vya tumbo utalazimika kuacha kabisa vitu kama pombe, sigara, sukari, soda, kahawa, chai ya rangi, vyakula vinavyosindikwa viwandani na vyakula vyenye mafuta mengi.

3. Kufunga kula au kuacha kula ni hatari kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo

Kufunga kula au kuacha kula hakuwezi kukusaidia na pengine kunaweza kukuongezea vidonda zaidi.

Kwa sababu unapoumwa vidonda vya tumbo mawazo yako mengi yanakuwa kwenye kuwaza ule nini na usile nini ili kuhofia madhara yanayoweza kukutokea kuna wakati unaweza kuamua bora usile kabisa chochote.

Huo ni uamuzi mbaya kuliko wote unaweza kuuchukuwa unapoumwa vidonda vya tumbo.

Bila kula chochote au kukaa masaa mengi bila kula tumbo lako linakuwa limebaki kwa sehemu kubwa na asidi tu ambayo inaweza kupelekea kuongezeka zaidi kwa vidonda vya tumbo.

Kula milo midogo midogo mingi na usikae muda mrefu bila kula na wala huhitaji kufunga kula.

Kanuni ni ile ile, matunda na mboga za majani.

4. Usile chakula na kulala wakati huo huo

Usile wakati wa kulala.

Kuna nyumba zingine zina mambo ya ajabu huwezi hata kuamini. Eti mama anaingia jikoni kupika chakula cha usiku saa tatu usiku!

Ukila saa tatu au saa nne usiku utalala saa ngapi?

Kuna mtu akimaliza tu kula anajitupa kitandani kulala.

Kama kweli unaumwa vidonda vya tumbo na umeamua kupona au kuzuia usipatwe na vidonda vya tumbo huwezi kuishi hivyo.

Kama unataka maumivu ukiwa usingizini au maumivu ya vidonda vya tumbo nyakati za usiku basi wewe maliza tu kula na ujitupe kitandani, utaniambia habari yake.

Tangu umekula chakula na unapoenda kulala kuwe na tofauti ya kati ya lisaa limoja hata masaa mawili.

Hivyo kama wewe huwa unaingia kitandani kulala saa tatu usiku basi jitahidi kwenye saa moja kamili au saa moja na nusu jioni uwe tayari umekula.

Na ukishakula usikae chini. Ukimaliza kula tembea tembea kwa miguu hata nusu saa ndiyo utulie.

Kitendo cha kumaliza kula na ukaamua kutembea tembea huusaidia mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi yake kwa kiwango chake cha juu kabisa na kwa ufanisi mkubwa.

Unapomaliza kula na kujitupa kitandani unauzuia mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi yake vizui na utaambulia maumivu zaidi ya vidonda.

Kwa kipande hiki napenda kuongeza pia kama utaweza kuwa unakula chakula chako huku umesimama na ukimaliza hukai chini unatembea tembea kama nusu saa hivi wewe unaweza kupona haraka zaidi vidonda vya tumbo.

Unapokuwa umekaa mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula unakuwa unafanya kazi chini ya kiwango na pengine gesi na asidi vinaweza kujitengeneza kirahisi kwa njia hiyo ya kukaa kwenye kiti au chini muda mwingi.

5. Usiwaze sana kuhusu vyakula vyenye asidi

Mara nyingi sana nakutana na comment zinazouliza je mwenye vidonda vya tumbo anaweza kutumia limau? Ndimu? Tangawizi? Kitunguu swaumu? Machungwa ? na mengine mengi ya namna hiyo.

Na wengine wanaweza hadi kukujaji na kukuona hujuwi lolote kwa sababu umemwambia ale chakula fulani ambacho daktari wake alimwambia asile.

Kwa sehemu kubwa tumbo lenyewe huitengeneza hii asidi hata kama utakula vizuri kiasi gani.

Matokeo ya mwisho kabisa ya asidi ni saratani.

Ndiyo maana unakutana na mtu hajawahi kuvuta sigara wala kunywa pombe na anaugua saratani fulani!

Nimekutana na wachungaji wanaumwa saratani, wachungaji hata mashehe wanaumwa bawasiri na kadharika na watu hawa ni wale wapo makini sana juu ya nini wale na nini wasile au kunywa.

Wanawake wengi sana wanaumwa saratani ya matiti na wengi wao hawajawahi kutumia kilevi chochote.

Kwahiyo unakutana na mtu hapa anauliza eti mwenye vidonda vya tumbo anaruhusiwa kutumia limau? Ukimjibu ndiyo anakuona wewe hujuwi kitu kutokana na alivyoaminishwa na daktari wake.

Ni msitu mkubwa. Hivyo mpendwa kuwa mpole.

Limau kwa mfano lina vitamini C ambayo ni mhimu sana kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Limau linapokuwa nje ya mwili ni asidi lakini kile wewe hufahamu ni kuwa limau linapofika chini tumboni hubadilika na kuwa alkalini tena alkalini ile nzuri kuliko hata ya kwenye mboga za majani au matunda mengine.

Kwahiyo usiwe bize sana kukariri hiki ni asidi na hiki siyo asidi kwa sababu tumbo lenyewe kwa asili lazima liizalishe hii asidi ili mfumo wake wa mmeng’enyo wa chakula uweze kufanya kazi yake.

Uwe ni mtu uliye tayari kujifunza > open minded.

Endelea kupenda kula zaidi matunda na mboga za majani huku ukiepuka kukaa chini au kwenye kiti masaa mengi

Usiwaze sana kuhusu vyakula vyenye asidi.

6. Usiidharau stress (msongo wa mawazo)

Kuna uhusiano kati ya msongo wa mawazo na vidonda vya tumbo na kila kimoja kinaweza kumleta mwenzake.

Msongo wa mawazo (stress) unaweza kuleta vidonda vya tumbo na vidonda vya tumbo vinaweza kuleta msongo wa mawazo.

Jambo baya na la kipuuzi kabisa unaweza kufanya unapoumwa vidonda vya tumbo ni kuwa na stress.

Kwahiyo jikaguwe na ujipeleleze ni kitu gani hasa ndiyo sababu ya wewe kuwa na msongo wa mawazo na ukiondowe hicho kwenye maisha yako bila kujali ni nini au ni nani.

Usiiuguze stress wala usikubali kuishi nayo.

Haijalishi itakugharimu nini, uamuzi mzuri kabisa unaweza kuufanya kwenye maisha yako ni kuamua kuishi maisha ya amani na utulivu bila msongo wowote wa mawazo usio na kichwa wala miguu.

Kumbuka maisha ni mafupi na maisha ni yako na hii dunia ni kubwa sana ina mahitaji ya kumtosha kila mtu ni wewe tu kuamua kubadilika na kufungua akili zako.

Usijifungie kwenye boksi.

Lolote linalokusibu lina suluhisho lake.

Ongea na watu, kaa na watu.

Kwa kawaida hata kama hupendi au hutaki mwili wenyewe utaelekeza nguvu kushughurika na stress kwa sababu ni jambo linalohitaji kutokuwepo.

Sasa hizi nguvu ambazo mwili wako unazielekeza kushughulika na stress ndiyo hizo hizo zingetumika kuutibu mwili dhidi ya vidonda vya tumbo.

Uamuzi unabaki kuwa kwako.

Kwamba wewe ushughulike na stress na mwili ushughulike na uponyaji au wewe ushughulike na uponyaji jambo ambalo huliwezi na mwili ushughulike na stress.

Upe mwili uwezo wake wa asili wa kujitibu kwa kuamua kujitenga mbali na msongo wa mawazo.

Kumbuka duniani tunapita na tuna muda mchache sana wa kuwa hapa.

Ishi vizuri kwa amani, furaha na upendo.

Jiunge na Group langu la Afya Kila Siku kwenye WhatsApp kwa ada ya sh 5000 tu kwa mwezi, nitafute WhatsApp +255714800175 na utakuwa karibu na mimi masaa 24

Kama unapenda kujifunza mambo mengine zaidi kuhusu vidonda vya tumbo bonyeza hapa

Kama unahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kutibu kabisa vidonda vya tumbo nipigie simu au niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Mjulishe rafiki yako kwenye Twitter naye asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Vitu 6 nilivyojifunza kuhusu vidonda vya tumbo Click To Tweet

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao

Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 9

Imehaririwa mwisho

Let's block ads! (Why?)

Jumatatu, 22 Juni 2020

Namna saratani inavyojitokeza mwilini

Namna saratani inavyojitokeza mwilini

Kama wewe ni mvivu kusoma pita hivi kwanza nenda ka-like mapicha ya rafiki zako wengine huko kwenye facebook.

Siku hizi tunaambiwa mtu mmoja kati ya watu watatu atakuwa na mojawapo ya aina za saratani, miaka 65 iliyopita ilikuwa mtu mmoja kati ya watu elfu kumi.

Namna saratani inavyojitokeza mwilini 1

Saratani ni nini?

Saratani ni mgawanyiko usio sawa na usiodhibitika wa seli na kuunda uvimbe unaovamia na kuzidhuru tishu.

Seli za Saratani husambaa kupitia mikondo ya damu au kupitia vungu (cavities) mbalimbali za mwili na kuunda uvimbe wa pili katika sehemu nyingine za mwili.

Saratani inaweza kushambulia karibu katika kila tishu yeyote ya mwili.

Bado hakuna uhakika wa moja kwa moja wa nini kinachosababisha kansa ingawa inajulikana wazi kuwa, kuwa karibu na baadhi ya vitu (kemikali) kunaweza pelekea saratani.

Tuna seli za ngozi, seli za Ini, seli za ubongo, seli za mapafu, seli za misuli, seli za mifupa na kadharika.

Seli hizi tofauti zinatujia toka kwa kinasaba (DNA) chetu ambacho kinamiliki maagizo (blue print) juu ya aina gani ya seli itengenezwe.

Wakati baadhi ya vitu (kemikali) vimechukuliwa ndani ya mwili kupitia ngozi au hewa tunayopumua au kwa njia ya chakula, miili yetu inaweza kuvihimili vingi ya hivyo vitu kabla ya safari ya mwisho kuingia kwenye vinasaba vyetu na kusababisha seli zisizo za kawaida kutengenezwa na kupelekea kile tunachokiita SARATANI.

Miili yetu lazima iachwe katika hali ya ualikalini kidogo na siyo katika asidi kabisa isipokuwa kwa kipindi cha muda mfupi, kinyume chake madhara lazima yatatokea kwenye tishu, ogani, seli na mwisho kwenye kinasaba ambako seli hutengenezwa.

Kuna namna tatu ambazo zimebuniwa ili kuishughurikia asidi: mfumo wa mkojo, mapafu na tumbo.

Mfumo wetu wa mkojo hupitisha asidi nje ya mwili.

Mapafu yetu huchukua ndani oksijeni na kutoa nje gesi ya kabonidayoksaidi (co2) ambayo ni asidi.

Hii ndiyo njia namba moja miili yetu iwezavyo kuitoa asidi ambayo ni taka za seli.

Tumboni mwetu ndimo haidrokloriki asidi hutengenezwa na kuhifadhiwa ikisubiri kutumika wakati chakula kinaliwa.

Haidrokloriki asidi hii inahitajika na mwili ili kuuwezesha mwili kuyatumia madini yanayopatikana kwenye vyakula tulavyo.

Baada ya hii haidrokloriki asidi kuwa imeandaliwa (opened up the food), valvu ya chini ya tumbo itajifungua na chakula huenda ndani mwanzoni mwa utumbo mdogo ambako asidi hupunguzwa makali (neutralized) na bikaboneti toka katika kongosho.

Ikiwa asidi hii haikurekebishwa vya kutosha na baadhi ya asidi inaingia katika utumbo mdogo, asidi hiyo itaziathiri seli za tishu na kwa kipindi cha muda mrefu itaathiri kinasaba na unapata kuzarisha seli zisizo za kawaida na kupelekea kansa ya utumbo mdogo (intestinal cancer).

Wakati asidi hii inaingia kwenye mkondo wa damu ikitokea kwenye utumbo mdogo hupelekwa kwenye ini ambako damu husafishwa na asidi hurekebishwa.

Ini letu haliwezi kuhimili kiasi kingi cha asidi inapotokea tunakunywa kiasi kingi cha vinywaji vyenye kabonidayoksaidi (the carbonation), ni kiasi kidogo kinachopatikana katika soda, bia na shampanye (champagne).

Ubongo wetu unatambua damu hiyo yenye asidi nyingi lazima irekebishwe kwa haraka, hivyo utaamuru kalsiamu itolewe toka katika mifupa yetu ili kuirekebisha damu hiyo.

Ukopaji huu wa kalsiamu kutoka katika mifupa kama hautalipwa kwa wakati, utapelekea matatizo mengine ya kiafya kama vile ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).

Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati   7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH (potential hydrogen). Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini.

Unaweza kukinunua kipimo cha PH na kupima Ph ya mate na mkojo, hii itakupa mwelekeo wa namna gani unafanya kuitunza 7.2 mpaka 7.4 kwenye seli ndani ya mwili wako.

Ikiwa mate yanasoma 6.0 au 6.5 ni kiashiria kuwa una asidi iliyozidi kwenye seli zako.

Haidrojeni ina chaji chanya (+), wakati alkalini ina chaji hasi (-)
.

Kila mtu anapaswa kula zaidi vyakula vyenye alkalini (matunda na mboga za majani) na kunywa vinywaji vyenye asidi chache, alkalini nyingi kama juisi ya limau, ya chungwa, ya zabibu na maji halisi.

Maeneo ndani ya mwili ambayo hayana mtiririko wa moja kwa moja wa damu yanaweza kupatwa na asidi kwa urahisi zaidi.

Tishu zitaisajiri asidi hiyo na kihisio maalumu (special sensor) ambacho kitapeleka ujumbe kwenye ubongo kama MAUMIVU.

Kunakokuwa na damu chache au hakuna mtiririko wa moja kwa moja wa damu kama vile kwenye maungio, katileji na uti wa mgongo, maeneo haya yanaweza kupungukiwa kwa urahisi madini, chumvi, maji na elektrolaiti na kusababisha misuli iliyo karibu nayo kufanya kazi zaidi ya uwezo wake na kusababisha uwezekano wa kukakamaa kwa mishipa, madhara kwenye misuli na kwenye mafundo (ligaments).

Maumivu ambayo hayakusababishwa na jeraha au ajari, ni kiashiria kuwa tishu, ogani, maungio na seli vina asidi iliyozidi ambayo inahitaji kufanywa alkalini.

Kwa kunywa glasi moja (ml 250) ya maji halisi na kuchukua kipande cha chumvi ya baharini, kutapunguza kama siyo kuondoa kabisa maumivu.

Jaribu hii kwa kunywa glasi moja ya maji na kisha kuiweka chumvi mwishoni mwa ulimi wako na kuiacha iyeyuke kwa dakika na kisha isafishe kwenda chini na glasi ya pili ya maji.

Kitendo hiki kitabadili PH ya damu, tishu, ogani na seli ndani ya mwili.

Asilimia 94 ya damu ni maji, ubongo wetu una zaidi ya asilimia 85 za maji, na tishu zetu laini zina asilimia 75 ya maji.

Tunatumia maji kupumua nje, kila masaa 24 tunapoteza glasi 4 za maji kwa kupumua tu nje.

Chukua kioo, hemea juu ya kioo, utaona ukungu (maji).

Kumbuka kuwa hali hiyo ya uasidi wa tishu, ogani, na seli, mwisho itaingia kwenye kinasaba (DNA) chetu na kubadili mpangilio (codes) na kusababisha seli mbovu kutengenezwa ambazo tunaziita ‘SARATANI’.

Saratani inaweza kuishi katika mazingira ya uasidi na uanaerobiki, yaani katika upungufu wa oksijeni pekee.

Ikiwa kinga yako ya mwili inafanya kazi vizuri, itakuwa na seli nyeupe za damu ambazo zinaweza kutengeneza oksijeni na kuitoa ‘haidrojeni peroksaidi’ kama inavyohitajiwa kuzuia kutengenezwa kwa seli za kansa.

Wakati mtu anapokuwa katika upungufu wa maji na chumvi (out of balance in cells), mwili utajifunguwa na kuizarisha histamini ili kujiwezesha kuiweka upya seli katika usawa wake, kupiga chafya ni angalizo kuwa histamini imeamushwa.

Moja kati ya madhara ya histamini ni kuisimamisha seli nyeupe ambayo hutengeneza haidrojeni peroksaidi kwenye mfumo wetu wa kinga ya mwili.

Kwa sababu ya biashara kuunda vyakula vyetu vyote maalumu na vinywaji vyenye radha mpya, radha nzuri na nguvu ya kutosha kwa kutumia kafeina toka katika mimea na mitishamba kama vile ginseng kuisisimua tezi ya adreno, kunasababisha Ini kutoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa.

Hakuna nguvu iliyomo kwenye kafeina au ginseng.

Kuna majina mengine mengi ya visisimuaji hivi kama vile, kokwa za guru, kokwa za cola na mfalme wa yote ni guarana.

Mbegu za guarana zina kiasi cha kafeina mara tatu zaidi ya zile za kahawa, na hawatakiwi kuliorodhesha neno kafeina kwenye vifungashio (packages) au kontena.

Ungaunga wa guarana hutumika kutengeneza vidonge vya kupunguza uzito kwa sababu kafeina itazisambaratisha hisia za njaa, lakini hakuna mahala neno kafeina linaonekana kwenye kifungashio.

Kuna mimea, kokwa na kemikali nyingi ambazo zitaisisimua tezi ya adreno na kusababisha ini kuitoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa au hata kuitengeneza toka tishu za mwili wenyewe.

Kafeina kama kikojoshi, huyalazimisha maji kukimbia nje ya mwili kwa haraka na kuziacha seli bila muda wa kutosha kuyatumia maji hayo, maji yanapokimbia kwa haraka nje ya mwili huyakimbiza pia madini mhimu nje ya miili yetu.

Nguvu safi katika mwili wa binadamu huja kutoka katika maji/chumvi na potasiamu ambavyo huwasha pampu za majenereta machache yaitwayo kwa kitaalamu ‘cation pumps’, umeme wake huifadhiwa katika beteri ziitwazo “Adenosine Triphosphate”(ATP) na “Guanosine Triphosphate”(GTP).

Aina nyingine ya nguvu kwa mwili inatokana na sukari.

Inahitajika sukari zaidi kuzarisha kiasi sawa cha nguvu izarishwayo kwa maji/chumvi na potasiamu, ni kama vile umeme wa maji (haidroelectric power) dhidi ya umeme uzarishwao kwa makaa ya mawe.

Wakati sukari inapochomwa kuzarisha nguvu, huzarisha taka nyingi zaidi (oxidation) zinazohitaji vidhibiti zaidi vya taka hizo (anti-oxidants) ili kuirekebisha hali hiyo ya taka za sumu.

Ikiwa huna tabia ya kupenda kula matunda na mboga za majani vya kutosha, basi Ini lazima lizitumie asidi amino zenye umhimu sana kama vidhibiti vya taka hizo.

Tunapokula vyakula vya asidi vilivyoongezwa utamu kama kemikali na kemikali vihifadhio, jumlisha vinywaji ambavyo ni asidi na vimeongezwa utamu kama kemikali; vitakuwa vikiuandaa mwili kupata ‘Saratani’.

Moja ya sababu kuu kwanini unatakiwa kula matunda na mboga za majani kwa wingi ni kuwa vyakula hivi ni alkalini, wakati nyama, kuku, samaki, nyama ya nguruwe, pasta (tambi) mayai na vyakula vingine karibu vyote ni asidi.

Watu wetu siku hizi tunakula vyakula ambavyo vimekwisha andaliwa (fast food) na hatutumii vyakula vyenye alkalini ya kutosha.

Kumbuka kuwa kabonidayoksaidi ni asidi pia kama ilivyo kwa kahawa, chai na pombe ambavyo huathiri PH ya damu na tishu.

Madawa na wewe, kwa mjibu wa dr.Earl mindell, mwandishi wa kitabu; ‘Earl mindell’s new vitamin bible’ (zaidi ya nakala milioni 10), anasema katika ukurasa wa 414 wa kitabu hicho kuwa ‘kafeina ni dawa yenye nguvu kubwa, uwezekano ni kuwa, hauifurahii tu kahawa au cola yako ya kila siku, bali umekuwa mtegemezi (addicted) kwavyo’.

Kafeina inafanya kazi moja kwa moja kwenye mfumo mkuu wa fahamu (central nervous system).

Inakupa hisia safi kwa haraka na kupunguza uchovu.

Inasisimuwa pia kutolewa kwa sukari iliyokuwa imehifadhiwa kwenye Ini ambayo inatumika kama kiinuzi (lift) kwa kahawa, cola na chokoleti (The caffeine big three), lakini faida hizi zinaweza kuzidiwa uzito na hasara zake.

Utolewaji wa sukari iliyokuwa imehifadhiwa, kunapelekea mfadhaiko mkubwa kwenye mfumo wa dharura wa mwili.

Unaposhitushwa kidogo tu, unakuwa na nguvu za haraka kushughurika na tatizo (hamaki).

Hali hii hatimaye inaweza pelekea kukauka kwa tezi ya adreno kutakakosababisha damu chache yenye sukari (hypoglycemia), udhaifu, na kuumwa sana iwapo sukari haitachukuliwa mapema kupandisha juu damu sukari.

Pia dalili za uchovu sugu zinaweza kujitokeza kwa sababu mwili utakuwa umelazimishwa kutengeneza sukari toka katika tishu, mishipa na umbile lake wenyewe.

Kitendo hiki huitwa kwa kitaalamu kama ‘Gluco-neogenesis’, yaani kutengenezwa upya kwa sukari toka katika hifadhi ya mwili na kisha toka katika tishu, mishipa na umbile lake wenyewe (mwili).

Imethibitika pia kuwa kafeina imekuwa ikiingilia na kuathiri unakilishaji wa kinasaba (DNA), namna ambavyo seli mpya hutengenezwa.

Kafeina inaweza kusababisha upotevu toka mwilini wa vitamini nyingi za kundi B, kundi C, zinki, potasiamu na madini mengine.

Kahawa huongeza hali ya uasidi kwenye utumbo mdogo.

Kafeina inaweza kusababisha msukosuko ndani ya mwili.

Kafeina siyo kwamba tu huimaliza nguvu iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ubongo, bali pia huzuia mfumo vimeng’enya katika kutengeneza kumbukumbu kwenye ubongo.

Jarida moja la afya la Uingereza, ‘The British Medical Journal Lancet’, limeripoti uhusiano mkubwa uliopo baina ya utumiaji wa kahawa na kansa ya kibofu cha mkojo na kupungua kwa uzarishaji wa mkojo.

Kituo cha sayansi kwa masirahi ya umma (Center for science in public interest) kimewashauri kinamama wajawazito kukaa mbali na kafeina kwa kuwa tafiti zimeonesha kwamba kiasi cha kafeina kilichomo kwenye vikombe 4 vya kahawa kwa siku kinaweza kusababisha matatizo wakati wa kujifungua kama yalivyoonwa katika majaribio kwa wanyama.

Kunywa maji kunahitaji kiasi cha chumvi kuchukuliwa pia ili kuzirekebisha taka (haidrojeni) kutokana na maji kutotumika kwenye seli.

Haidrojeni ni asidi.

Damu yetu ina chumvi na kongosho letu lazima liwe na chumvi ili kuitumia kutengeneza bikaboneti inayotumika kurekebisha asidi ndani ya tumbo.

Siku hizi vyakula vyetu vingi vinazarishwa kwa kutumia mbolea kemikali na kupuliziwa tena kemikali ili kudhibiti wadudu waharibifu.

Tunatumia kemikali kali kwenye vyakula vyetu ili kuvihifadhi kwa matumizi ya baadaye.

Miili yetu lazima ishughurike na kemikali hizi kila siku.

Siku hizi, kemikali zinazotumika kuongeza utamu kwenye vyakula zinasababisha matatizo makubwa kwenye miili yetu kwa sababu zina radha ya utamu lakini hazina sukari.

Sukari ni asidi, lakini kemikali zinazotumika badala ya sukari zinasababisha madhara zaidi ya sukari halisi.

Baadhi ya kemikali hizi kali zipatikanazo kwenye vyakula vyetu nyakati hizi zinabaki na kujishikiza kwenye utumbo mdogo na kuendelea kurundikana na hivyo kuufanya utumbo usifanye kazi zake vema.

Ini letu pia litazishikilia baadhi ya kemikali hizi kali ambazo zinaingia kwenye damu na kujaribu kuzirekebisha kadiri liwezavyo.

Ini litaendelea kuzihifadhi kemikali nyingi kadiri liwezavyo mpaka litakaposhindwa na kuamua kuzitupa tena kwenye mkondo wa damu na kwenda kwenye kila seli mwilini.

Kwa sababu hii, ndiyo maana watu wengi siku hizi wanatumia dawa rafiki na vifaa maalumu kusafisha utumbo mdogo na Ini kila mara ili kuziondoa taka hizi na uzito zinazoongezeka tumboni.

Kisha mtu analazimika kuwa mwangarifu sana kuepuka vyakula ambavyo vina kemikali kali nyingi.

Damu yote hupita kwenye Ini na amino asidi zinatumika kuzirekebisha sumu ambazo huliingia Ini.

Wakati Ini linapokuwa katika upungufu wa amino asidi hizi, litalazimika kukopa baadhi toka katika ogani zingine kama vile Kongosho.

Kitendo cha kongosho kukopwa amino asidi zake kutapelekea matatizo mengine kwenye kongosho kama vile kisukari, na uwezekano wa kutokea kwa saratani ya kongosho (pancreatic cancer) ikiwa amino asidi zilizokopwa hazikurudishwa kwa wakati ili kuliwezesha kongosho kuendelea na kazi zake vizuri.

Miili yetu ilisanifiwa kula vyakula halisi vya asili (fresh natural grown food) au kula nyama iliyouliwa wakati huo huo (fresh live kill).

Kwa njia za kijenetiki, siku hizi tumebadili vyakula vyetu ili kupata mavuno mengi.

Tunawalisha wanyama wetu vitu (kemikali) ili kuwafanya wakue haraka na kuongezeka uzito kwa haraka.

Tumekuwa wafugaji wa samaki pia ili kukidhi mahitaji na kuepukana na bei kubwa zitokanazo na gharama za kutumia meli za uvuvi na matatizo ya hali ya hewa.

Siku hizi sote tunaharaka katika kila jambo, hatuna muda wa kutosha, kila kitu ni mwendokasi, kitu kinachotusababishia wengi wetu kutokula mlo kamili wenye matunda halisi na mboga za majani.

Masaa 24 kwa siku seli ndani ya mwili zinaunguza kaboni kama mafuta ili kutuacha katika hali joto ya nyuzi joto 37.5.

Unapochoma kitu chochote, kinatoa nje taka moshi.

Taka zote hizo toka katika seli zote za mwili, lazima zirekebishwe kwa muda wa masaa yote 24 kwa msaada wa matunda na mboga za majani.

Asidi amino zina umhimu mkubwa kwa afya bora.

Ubongo wetu lazima upate kusambaziwa asidi amino kila siku ili ufanye kazi.

Ini haliwezi kufanya kazi vizuri bila uwepo wa asidi amino.

Mishipa yetu lazima iwe na amino asidi, kila seli kwenye mwili wa binadamu inazihitaji amino asidi au asidi ambazo zimetengenezwa toka asidi amino ndani ya mwili.

Deoxyribonucleic acid (DNA), Ribonucleic acid (RNA) na Decosahexaenoic acid (DHA), zote ni asidi.

Tunapopumua katika hewa iliyochafuliwa kama vile moshi wa magari au tunapovuta sigara miili yetu lazima izitumie asidi amino hizi kuirekebisha sumu hiyo kadiri iwezekanavyo.

Gari huyaunguza mafuta ya kaboni kwa kutumia oksijeni na kutoa nje taka (moshi) ziitwazo ‘kabonimonoksaidi’.

Moto wa kuni pia huzarisha moshi.

Hata uchomaji wa mafuta safi huzarisha taka ziitwazo kabonimonoksaidi.

Kwa hiyo mtu anapoamua kuvuta sigara, anakuwa ameamua kuvuta ndani kabonimonoksaidi ambayo ni sumu kwa mwili wa binadamu.

Uvutaji wa sigara pia unasababisha upungufu wa oksijeni mwilini, hii inamaanisha kuwa baadhi ya seli ndani ya mwili hazipati oksijeni ya kutosha na zinapatwa na asidi toka katika kabonimonoksaidi.

Kitendo hiki kitapelekea siku moja kutokea kwa SARATANI katika sehemu dhaifu za mwili.

Watu wengine hawajawahi kuvuta sigara tangu wazaliwe lakini wamepatwa na saratani ya matiti pia saratani ya mapafu na saratani nyinginezo.

Kila mwili wa kila mtu lazima ukope asidi amino na hivyo kupunguza usambazwaji mzuri wa oksijeni kwenye baadhi ya sehemu za mwili ili kukutetea uendelee, kwa matumaini kuwa utaupa mwili unachokihitaji siku za mbeleni ili kuyarudishia maeneo yaliyokopwa amino asidi zake.

Unajiuliza kwanini watu wanavuta?

Wote wanajibu kuwa wanaifurahia.

Unaenda kufa kwa sababu fulani kwa namna fulani.

Kuvuta kunawafanya wajisikie vema.

Wakati mtu anajaribu kuvuta sigara kwa mara ya kwanza, mapafu yake hujifunga na atakohoa kwakuwa mapafu yanajaribu kuitoa kwa haraka hewa iliyochafuliwa (moshi).

Lakini atakapojaribu ‘puff’ ya pili, mwili wake utaitoa kemikali iitwayo ‘endorphinsi’ ili kumuwezesha kuhimili (kuvumilia maumivu) moshi huo mpaka atakapopata hewa safi kupumua.

Ni kemikali hii ambayo mwili unaitoa ndiyo inayomfanya mtu kuwa mtegemezi (addicted) wa kuvuta.

Kutolewa huku kwa endorphinsi kunamfanya mtu kujisikia ‘super’.

Endorphinsi hutolewa pia wakati mama anajifungua kwa sababu ya maumivu.

Kwa kawaida ni ngumu sana kwa mwanamke kuacha kuvuta au kuacha kilevi chochote kuliko kwa mwanaume kwa sababu wanawake wana kiasi kingi cha endorphinsi kuliko wanaume.

Endorphinsi ni homoni ambayo huusaidia mwili kuvumilia maumivu.

Unywaji pombe pia unaweza kupelekea baadhi ya miili kuitoa endorphinsi na kumpelekea mtu huyo kuwa mtegemezi wa POMBE.

Moshi unaweza kunukia vizuri, lakini kamwe hauwezi kuwa mzuri kwa afya zetu.

Vinukizi vingi (air fresheners) vinatumia kemikali kali ambazo si nzuri kwetu, baadhi ya mishumaa pia ina kemikali hizo.

Mtu anapaswa kuwa makini na kusoma maelekezo ya kwenye vidandiko vya bidhaa ili kujua ni nini anakula, kunywa, kunusa au anaongeza kwenye ngozi yake.

Inashauriwa pia kuepuka kubaki katika mkao mmoja kwa muda mrefu iwe ni kukaa au kusimama.

Watu wengi kutokana na kazi wanazofanya wanalazimika kubaki wamekaa au kusimama tu kwa masaa mengi kwa siku jambo ambalo ni hatari kwa afya kwa kuwa asidi hujikusanya hivyo kwa urahisi zaidi.

Yapo mazoezi maalumu ya kufanya kila mara kwa watu wa kazi za aina hiyo ili kurudishia damu katika mfumo na hivyo kutoa nje taka za asidi.

Ukiamua kuacha kunywa vinywaji vyenye kafeina na kula chokoleti; na kisha kunywa maji nusu ya uzito wao katika aunsi na kuchukua robotatu gramu za chumvi kwa kila aunsi 16 (ml 500) za maji na kuongeza matunda na mboga za majani zaidi kwenye milo yako na kufanya mazoezi, saratani yako itaisha na mwili wako utajiripea wenyewe.

Je unasumbuliwa na saratani yoyote na unahitaji dawa ya asili kwa ajili hiyo na isiyo na madhara? nipigie simu au niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Jiunge na Group langu la Afya Kila Siku kwenye WhatsApp kwa ada ya sh 5000 tu kwa mwezi, nitafute WhatsApp +255714800175 na utakuwa karibu na mimi masaa 24

Tafadhari SHARE kwa ajili ya wengine

Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 5

Imehaririwa mwisho

Let's block ads! (Why?)

Jumapili, 21 Juni 2020

Njia zingine mpya 8 za kuondoa tatizo la kuwahi kufika kileleni

NJIA ZINGINE MPYA 8 ZA KUONDOA TATIZO LA KUWAHI KUFIKA KILELENI

Kati ya matatizo makubwa kabisa yanayowasumbuwa wanaume katika suala la kujamiiana ni kufika kileleni mapema.

Takwimu zisizo rasmi zinasema kuwa, wanaume 7 kati ya 10 wanapatwa na tatizo hii.

Malalamiko yanayotolewa na baadhi ya wanaume yanathibitisha kwamba, muda wa kumaliza tendo huwa kati ya nusu dakika na dakika mbili kwa tendo la kwanza, huku wengine wakimaliza hamu katika hatua za awali tu wakati wakiandaana na kukosa hamu kabisa ya tendo la ndoa.

Hata hivyo wale wanaoweza kusimama tena mara baada ya tendo la kwanza wanakiri kuchelewa kidogo, ingawa bado suala la kutangulia kufika kileleni kabla ya mwanamke limekuwa likiwahuzunisha wanaume wengi wa rika zote vijana hata wazee.

Ndoa nyingi zimevunjika chanzo kikiwa ni tatizo hili. Karibu kila pembe ya dunia kunasikika vilio toka kwa wanaume wakilalamika kukabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni, ambalo limewafanya waonekane si lolote kwa wenzi wao.

Ni ukweli usio pingika kuwa mwanaume anapowahi kufika kileleni kabla ya mwenzake humwacha mwanamke na huzuni kwani anakuwa hajapata kile anakihitaji katika tendo hilo.

Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.

Njia zingine mpya 8 za kuondoa tatizo la kuwahi kufika kileleni 1

Njia 8 za kujitibu tatizo la kuwahi kufika kileleni:

1. Acha mawazo

Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye uume na kusababisha nguvu kupungua nguvu za kiume na hata uume wenyewe.

Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko au stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote.

Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba kwa Mungu huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.

2. Jitibu magonjwa yafuatayo

Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, vidonda vya tumbo, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza maradhi haya.

Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli.

Kisukari, shinikizo la juu la damu, vidonda vya tumbo na hata uzito kupita kiasi ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.

3. Acha vilevi

Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai.

Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.

4. Fanya mazoezi ya viungo

Zingatia sana umhimu wa mazoezi ya viungo. Bila kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu sana kwako kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Kutengeneza mishipa na kupunguza uzito isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym. Kama unahitaji nguvu za kiume na uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume.

Kama uzito wako upo juu sana na ni mnene fanya mazoezi ya kukimbia (jogging) kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili. Kama uzito wako upo sahihi tu kwa mjibu wa urefu wako fanya sana mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama.

Una chuchumaa na kusimama mara 25 mpaka 30, unaweza kupumzika dakika mbili unaendelea tena kuchuchumaa na kusimama hivyo hivyo unapumzika dakika 2 mpaka mizunguko (rounds) mitano kila siku.

5. Shiriki tendo la ndoa mara nyingi

Kuna stori zinasema twiga hakuzaliwa na shingo ndefu namna hii kama anavyoonekana akiwa mkubwa, bali wanasema ile tabia yake ya kupenda kula majani ya juu ya miti ndiyo ikapelekea shingo yake ikarefuka!. Inawezekana kuna ukweli kidogo wa stori hizi.

Usinielewe vibaya wala usije ukasema huyu jamaa anahamasisha watu kufanya mapenzi! Hapana usiwe na haraka hivyo utanielewa tu ninachotaka kusema.

Wanasayansi wa masuala ya mapenzi wanasema ikiwa mtu mzima hana msongo wowote wa mawazo (stress), ana afya nzuri tu ya kutosha na anakula vizuri basi anaweza kushiriki tendo la tendo kila baada ya masaa 24.

Angalia na umsome pia mwenza wako pia angalia umri wako, sababu kuna wanawake wengine kwa asili hawapendi kushiriki tendo la ndoa kila mara pia hatuwezi kusema mtu mwenye miaka 50 atakuwa na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kila mara kama mtu wa miaka 18 hadi 40 hivi.

Ni vigumu mtu anakaa mwenzi mzima mwingine miezi miwili mwingine anakaa miezi 6 bila kushiriki tendo la ndoa na utegemee utakuwa na uwezo wa kuchelewa kufika kileleni.

Kama hushiriki tendo la ndoa kuna uwezekano mkubwa ukawa unapiga punyeto kitendo ambacho ni kibaya zaidi kwa afya ya uume wako.

Kwahiyo unaweza kushiriki mara 2 hadi 3 kwa wiki na unaposhiriki tuliza akili na upate muda wa kutosha wa kuandaana kabla ya tendo na siyo haraka haraka tu (mambo ya short time).

6. Tumia vumbi la kongo

Vumbi la Kongo ni dawa ya asili yenye uwezo wa kukusaidia kuchelewa kufika kileleni kwa muda mrefu kadri upendavyo.

Ni dawa ya kupakaa kwenye uume muda mchache kabla ya kushiriki tendo la ndoa.

Inafaa itumike kwa mtu ambaye uume unasimama vizuri lakini anawahi sana kufika kileleni.

Pamoja na kuwa ni dawa ya asili bado usiifanye kama ndiyo suluhisho lako la kudumu kwamba unatumia hiyo kila mara au kila siku.

Haimarishi mishipa ya uume au nguvu za kiume au za mwili kwa ujumla bali inaufanya uume uache kuhisi hali ya utamu ya ukeni inayokufanya ukojowe haraka.

7. Tumia mafuta ya karafuu

Mafuta origino ya karafuu ukipakaa kwenye uume matone kadhaa mawili au matatu dakika 15 hivi kabla ya tendo la ndoa yatakusaidia pia kuchelewa kufika kileleni kwa muda mrefu kadri uwezavyo.

Mafuta ya karafuu yanafanya kazi sawa na vumbi la Kongo hapo juu.
Mhimu hapa ni yawe orijino bila kuongezwa chochote ndani yake na ni matone kadhaa tu.

Kama ilivyo kwa vumbi la kongo hii pia isiwe ndiyo suluhisho lako la milele bali utafute njia zingine za kuimarisha nguvu zako za kiume na mwili kwa ujumla.

8. Tumia msamitu

Msamitu ni mchanganyiko wa mimea na mitishamba mbalimbali ya asili. Ni dawa nzuri sana katika kutibu tatizo la nguvu za kiume na pia inasaidia sana kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume hasa lililosababishwa na kujichua au kupiga punyeto kwa muda mrefu kwani inaimarisha sana mishipa ya uume.

Pia unaweza kuitumia hata kama unasumbuliwa na tatizo la kisukari au Shinikizo la juu la damu. Msamitu inao uwezo mkubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume hata wa umri mkubwa.

Ndiyo Msamitu ni dawa bora ya nguvu za kiume ambayo hakuna dawa nyingine ya kuifananisha nayo kwa uwezo wake wa kutibu tatizo la nguvu za kiume na kuwahi kufika kileleni.

Vitu vifuatavyo vinafanya Msamitu kuwa dawa bora zaidi ya nguvu za kiume mpaka sasa:

(a). Msamitu inatibu tatizo la msongo wa mawazo (stress)

Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu mwilini na kusababisha nguvu za mwili kupungua, nguvu za kiume kuwa chini na hata uume wenyewe unaweza kunywea na kuwa mdogo na legelege.

Kama una mfadhaiko wa akili (stress) ni vigumu sana wewe kuwa na nguvu za kiume. Hilo haliwezekani. Ili uwe na nguvu za kiume unatakiwa usiwe na mawazo mawazo yoyote. Uwe mtu uliyetulia kimwili, kiakili na kiroho (cool).

Chanzo namba 1 cha tatizo la nguvu za kiume na kuwahi kufika kileleni kwa wanaume karibu wote ni msongo wa mawazo (stress). Jambo la kushangaza ni kuwa msamitu ni dawa bora ya kuondoa stress nzuri ya asili isiyo na madhara mengine mabaya tofauti na zilivyo dawa zenye kemikali zinazotibu msongo wa mawazo.

Sasa kama una stress hizo nguvu za kiume zitatoka wapi ndugu?

Tafiti nyingi zimekuwa zikionyesha kuwa moja ya kisababishi kikubwa cha msongo wa mawazo (stress) ni kukosekana kwa viinilishe mhimu katika chakula.

Kukosekana huku kwa viinilishe mhimu katika chakula kunasababisha usawa usio sawa wa homoni mwilini (hormonal imbalance) jambo linalopelekea kutokea kwa msongo wa mawazo.

Msongo wa mawazo umeendelea kuwa tatizo kubwa kwa watu miaka ya sasa na wengi wao wakipatwa na tatizo la kukosa pia usingizi.

Hata hivyo, tatizo hilo linaweza kutibika kirahisi kwa kuongeza viinilishe sahihi kwenye mwili wako

Kwa bahati nzuri msamitu ina viinilishe vingi kuliko dawa nyingine yoyote ya asili ya kutibu tatizo la nguvu za kiume uliowahi kuitumia au kuisikia ukiwa na viinilishe zaidi ya 120 ndani yake!

Msamitu ina kiasi cha kutosha cha vitamini A, B, C, E, Potasiamu, Kalsiamu, zinki na viinilishe vingine vingi mhimu kwa afya ya mwanaume.

Kwahiyo kama utatumia Msamitu kujitibu tatizo la nguvu za kiume na kuwahi kufika kileleni itakuwa ni vigumu kwako kupata tatizo la msongo wa mawazo.

Magnesiamu madini yapatikanayo kwenye Msamitu ni dawa maarufu ya kutuliza akili (Tranquillizer) na kutibu matatizo kama msongo wa mawazo, sononeko, huzuni, hamaki na matatizo mengine ya mvurugiko wa akili.

(b). Msamitu inaongeza kinga ya mwili

Sasa kama kinga yako ya mwili haipo sawa je utapata wapi nguvu za kiume?

Kumbuka, ile hali ya kuonekana umezeeka au mwili wako kuonekana umechoka mara zote huwa kuna uhusiano wa moja kwa moja na kushuka kwa kinga yako ya mwili hali ambayo inauacha mwili wako kushambuliwa kirahisi na vijidudu nyemelezi na magonjwa mbalimbali.

Kama unataka kuwa na nguvu za kiume kila siku basi jifunze namna kinga yako ya mwili inavyoweza kuongezwa na kuimarishwa.

Sasa unaweza kuwa unajiuliza ni nini kinachoifanya dawa hii kuwa kitu cha thamani SANA katika kuimarisha kinga yako ya mwili na hivyo kukuongezea nguvu za kiume, kujikinga na vijidudu nyemelezi, homa na magonjwa mbalimbali?

Kwanza kabisa Msamitu una viinilishe vingi ndani yake ukiwa na zaidi ya viinilishe 120, una vitamini nyingi, madini na viondoa sumu mwilini tofauti tofauti zaidi ya 46!

Vitamini C iliyomo kwenye dawa hii ni kitu mhimu katika kurejesha kinga ya mwili kwa sababu ni vitamini inayofanya kazi ya kuripea seli za mwili na kinga ya mwili. Zaidi sana vitamini C huimarisha ngozi ya mwili, nywele, fizi, macho na kuongeza nguvu ya jumla ya mwili kwa kuyataja machache mazuri ya vitamini C

Vitamini A ni moja ya vitamini zilizomo kwa wingi kwenye Msamitu na ni vitamini mhimu sana katika kuimarisha kinga ya mwili. Vitamini A ni mhimu pia kwa watu wanaosumbuliwa na matatizo kama ya kuharisha, upungufu wa kinga mwilini, surua na malaria.

Vileviele kuna madini ya chuma (Iron) kwenye Msamitu na ni kitu mhimu katika mfumo wa kinga ya mwili ambayo hukuwezesha usipatwe na magonjwa na homa mara kwa mara.

Msamitu inaimarisha usawa wa himoglobini katika damu jambo ambalo matokeo yake ni kuimarika kwa kinga yako ya mwili na msukumo wako wa damu kwenda kwenye uume.

Kwa kuongezea Msamitu ina lundo la vitamini kundi B kama vitamini B, B1, B2, B3, B5, B6, B12, D, E, K, folic acid, Kalsiamu, madini ya shaba, potasiamu, magnesia, kromiamu na vitamini, na madini madogo madogo mengine mengi mhimu kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili.

Msamitu inasafisha mwili wako wote, inasafisha ini, figo, moyo, macho, inaimarisha meno, ngozi na nywele.

Wakati unatumia Msamitu itakufanya ujisikie vizuri, ujisikie mpya (fresh) na mwenye nguvu.

Upungufu wa nguvu za kiume ni matokeo ya lishe yenye viinilishe duni au hafifu jambo linalopelekea kuwa na kinga ya mwili isiyo na nguvu kupigana na magonjwa mbalimbali na hivyo mwanaume kuwa na uume mlegevu.

Unaporekebisha usawa huo usio sawa wa kinga yako ya mwili hutakawia kuona matokeo mazuri kwenye uwezo wako wa kushiriki tendo la ndoa kwa ufanisi zaidi.

Uwezo wa Msamitu kuyaweza yote hayo ni kutokana na kuwa na vitamini, madini mbalimbali na viondowaji sumu vingi ndani yake.

(c). Msamitu ina madini na vitamini zote mhimu kwa ajili ya nguvu za kiume

Msamitu ina madini ya Zinki madini ambayo ni mhimu sana linapokuja suala la nguvu za kiume. Pia una protini ya kutosha, protini ni mhimu katika suala zima la nguvu ya mwili

Vitamini nyingine mhimu kwa ajili ya nguvu za kiume zilizomo kwenye Msamitu ni pamoja na vitamini B6, B12, D na E

(d). Msamitu inatoa sumu mwilini

Chanzo kingine cha kupungua nguvu za kiume miaka ya sasa ni sumu nyingi mwilini sababu ya vilevi na vyakula tunavyokula kila siku. Habari njema ni kuwa hakuna sumu inaweza kubaki salama mbele ya Msamitu.

Kwa hiyo ni vigumu mtu utumie Msamitu halafu bado uwe huna nguvu kitandani kama Simba.

(e). Msamitu inaongeza msukumo wa damu mwilini

Msukumo mzuri wa damu usiozuiliwa kusafiri kwa uhuru wote sehemu mbalimbali za mwili ni mhimu katika kutibu tatizo la nguvu za kiume. Kwa ajili hii watu hushauri kunywa maji na kufanya mazoezi ya viungo kila siku. Jambo la ajabu ni kuwa hiyo kazi ya kuongeza msukumo wa damu sehemu zote za mwili ni kazi inayoweza kufanywa vizuri na Msamitu.

Bado sijaona ni namna gani Msamitu itashindwa kukutibu tatizo lako la nguvu za kiume na kuwahi kufika kileleleni.

Jaribu Msamitu na uniletee mrejesho

Kazi inabaki kuwa kwako tu kuanzia sasa …

Kama utahitaji Msamitu nipigie simu au niachie ujumbe WhatsApp 0714800175

Kama una swali au unahitaji ushauri wowote uliza hapo kwenye comment ni faraja kwangu kuona nimekujibu vizuri.

Jiunge na Group langu la Afya Kila Siku kwenye WhatsApp kwa ada ya sh 5000 tu kwa mwezi, nitafute WhatsApp +255714800175 na utakuwa karibu na mimi masaa 24

Tafadhari SHARE kwa ajili ya wengine

Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 1

Imehaririwa mwisho

Let's block ads! (Why?)

Jumamosi, 20 Juni 2020

Chakula cha mama mjamzito

Chakula cha mama mjamzito 1

CHAKULA CHA MAMA MJAMZITO

Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na madini yote kama vitamini na protini.

Mama mjamzito anatakiwa apate gramu 100 za protini kila siku.

Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ujauzito wake kwa afya bora.

Nimeweza kukundalia vyakula 10 bora ambavyo mama mjamzito na mtoto wake wanastahili kula

1. Vyakula Jamii ya Kunde

Mbegu za makundekunde ni sehemu muhimu ya chakula kwa mama mjamzito kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha protini.

Kwa watu wasiokula nyama au wana uwezo mdogo tu kujipatia nyama mbegu za jamii kunde zinatosheleza mahitaji ya protini.

Hivi ni vyakula vya mimea kama Soya, Njegere, Karanga, Mikunde, maharage nk

2. Mayai

Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protini, vitamini A na madini ambayo husaidia kuzuia kupatwa na maradhi mbali mbali.

Kumbuka ni mayai ya kuku wa kienyeji ndiyo mazuri kwako na siyo mayai mengine yoyote

3. Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa

Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na/au vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi na siagi.

Maziwa ni muhimu kwa protini, calcium, vitamini na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa na misuli,

Ni muhimu kwa damu yenye afya, kusaidia usingizi na kusawazisha mapigo ya moyo.

4. Viazi vitamu

Viazi vitamu vina vitamini A ambayo husaidia ukuaji wa macho ya mtoto, ngozi na mifupa

5. Nyama

Nyama ya nguruwe (kama dini yako inakuruhusu), kuku au ng’ombe huwa na protini nyingi sana na husaidia katika ukuaji wa mwili wa mtoto hasa kwa mama mjamzito wa miezi minne

6. Nafaka na vyakula vya wanga

Vyakula hivi huipa mwili nguvu ya kufanya kazi na pia ukuaji wa mtoto tumboni. Vyakula hivi ni kama mahindi, mtama, mihogo, vyakula vya ngano kama mkate n.k.

7. Parachichi

Ni matunda ambayo yana mafuta mengi maarufu kama fatty acid. Parachichi husaidia katika ukuaji wa ubongo, ngozi nyororo na ukuaji wa misuli ya mtoto tumboni.

8. Mboga za majani

Mboga za majani kama spinach, kabeji, mchicha na matembele. Mboga hizi zinafaa ziwe zenye rangi ya kijani iliyokolea kwa sababu hizi ndizo zenye virutubisho vya kutosha.

Mboga hizi zitampa mama na mtoto wake Vitamin A na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kupata protini ya kutosha, ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu.

Kutopata mboga za kutosha kunaweza sababisha mama kupata ugonjwa wa Anemia.

9. Samaki

Mafuta yaliyomo kwenye samaki huwa na Omega fatty acids ambayo inasaidia ukuaji wa ubongo na macho ya mtoto.

10. Maji

Maji ni muhimu kwa mwili kwa sababu inasaidia kwenye mmenyenyo na unyonywaji chakula na pia husaidia kuzia choo ngumu Maji pia huzuia uvimbe wa mwili na maambukizi ya mfumo wa mkojo(UTI)

Kuna chakula kingine mhimu kwa mjamzito sijakiandika? nishirikishe hapo kwenye comment sasa hivi

Ikiwa unatafuta dawa ya asili ili kupata ujauzito nipigie simu au niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Chakula cha mama mjamzito 2

Usisahau juisi au chai ya rosella ina madini mengi mhimu kwa mjamzito na ni multivitamin mhimu kwa mjamzito

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine

Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 2

Imehaririwa mwisho

Let's block ads! (Why?)

Dalili kuu 3 za mwanzo za kisukari kwa wanaume

Dalili kuu 3 za mwanzo za kisukari kwa wanaume 1

Dalili kuu 3 za mwanzo za kisukari kwa wanaume

1. Upungufu wa nguvu za kiume

Upungufu wa nguvu za kiume ni kitendo cha kukosa uwezo wa uume kusimama na kufanya kazi ipasavyo.

Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kuwa ni dalili za matatizo mengine ya kiafya ikiwemo shinikizo la juu la damu, magonjwa ya figo na matatizo mengine kwenye mfumo wa upumuwaji.

Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kuletwa pia na msongo wa mawazo (stress), baadhi ya dawa za hospitali, kuvuta sigara nk

Jifunze mengi zaidi kuhusu nguvu za kiume kwa kubonyeza hapa.

Wanaume wanoumwa kisukari wana hatari zaidi ya kupatwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kuliko wanaume wengine.

Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali, karibu asilimia 50 ya wanaume wote wenye kisukari wanakabiriwa pia na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Wanaume wenye kisukari hupatwa na upungufu wa nguvu za kiume mwanzoni kabisa wakiwa bado vijana au umri wa kati.

Ikiwa upungufu wa nguvu za kiume limekuwa ni tatizo likikunyemelea na kutishia afya yako ya kitandani kuna uwezekano mkubwa ukawa na kisukari.

2. Kushuka kwa homoni ya testosterone

Wanaume wanaosumbuliwa na kisukari hasa kisukari aina ya pili wana uwezekano wa mara mbili zaidi wa kupungukiwa na homoni mhimu sana kwa mwanaume ijulikanayo kama testosterone.

Testosterone ni homoni mhimu sana kwa afya ya mwanaume na inahusika na afya ya mwanaume kwa ujumla kuanzia kwenye afya yake ya kitandani, afya ya uzazi, wingi wa misuli, mgawanyo wa mafuta mwilini, na uzalishaji wa seli nyekundu za damu.

Kwa sababu ya kuwa na kiasi kidogo cha homoni hii wanaume wenye kisukari wanaweza kuwa na dalili zingine mbaya zaidi za kiafya kuliko dalili hizo zinavyojitokeza kwa wanawake.

Kushuka kwa homoni ya testosterone kunaweza kupelekea matatizo kwa wanaume kama

  • Kushuka kwa hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa
  • Msongo wa mawazo (stress)
  • Kushuka kwa nguvu ya jumla ya mwili
  • Kupungua kwa wingi wa misuli
  • Kushindwa kuhimili mkojo
  • U.T.I
  • Kushindwa kutungisha mimba na
  • Matatizo mengine kwenye kibofu cha mkojo

3. Kufika kileleni bila mbegu kutoka

Dalili kuu 3 za mwanzo za kisukari kwa wanaume 2

Lipo tatizo lingine ambalo ni ishara za kuja kwa kisukari kwa mwanaume nalo ni kitendo cha mwanaume kushiriki tendo la ndoa na asitowe mbegu au mbegu zinatoka lakini ni chache sana karibu na hakuna.

Kwa kitaalamu tatizo hili hujulikana kama ‘retrograde ejaculation’.

Hujulikana pia kama kilele kikavu.

Kinachotokea ni kuwa mwanaume anaweza kushiriki tendo la ndoa vizuri na akasikia kabisa ile raha ya kufika kileleni kama kawaida lakini akiangalia haoni mbegu zikitoka.

Hapa mbegu zinakuwa zipo ila badala ya kutoka nje kupitia mrija wa kwenye uume (urethra) zenyewe zinaenda moja kwa moja kwenye kibofu cha mkojo.

Ni matokeo ya madhara ya kisukari kwenye mishipa ya damu inayodhibiti kibofu cha mkojo na mrija wa mkojo.

Tatizo hili lenyewe kwa ujumla halina madhara makubwa bali linaweza kupelekea ugumba au hali ya mwanaume kushindwa kutungisha mimba.

Sababu zingine zinazoweza kuleta tatizo hili ni pamoja na upasuaji wa tezidume au kibofu cha mkojo, baadhi ya dawa za shinikizo la juu la damu na dawa za msongo wa mawazo pia majeraha katika uti wa mgongo.

Soma pia hii > Dawa ya kuongeza mbegu za kiume

Vitu vinavyosababisha kisukari kwa wanaume

  • Uvutaji sigara, tumbaku, bangi
  • Unywaji wa pombe kupita kiasi
  • Uzito kupita kiasi
  • Kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo
  • Kolesto
  • Shinikizo la juu la damu
  • Ukiwa na umri kuanzia miaka 45 na kuendelea

Mjulishe raiki yako kwenye Twitter naye asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Dalili kuu 3 za mwanzo za kisukari kwa wanaume Click To Tweet

Kama unahitaji dawa ya asili inayotibu kabisa kisukari hasa kisukari aina ya pili nipigie simu au niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Tafadhali SHARE post hii na wengine uwapendao

Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 4

Imehaririwa mwisho

Let's block ads! (Why?)

Alhamisi, 18 Juni 2020

161-Aayah Na Mafunzo: Tahadharisho La Kufanya Khiyana

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Tahadharisho La Kufanya Khiyana

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦١﴾

Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini (ngawira). Na yeyote atakayekhini atakuja na kile alichokikhini Siku ya Qiyaamah. Kisha italipwa kamilifu kila nafsi yale iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa. [Aal-'Imraan: 161]

 

 

Mafunzo:

 

Abuu Maalik Al-Ashja’iy amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ghuluwl (khiyaana ya wizi) kubwa mbele ya Allaah ni kipande cha ardhi ambacho utakuta watu wawili majirani katika ardhi au katika nyumba kisha mmoja wapo akakata kipande cha ardhi ya mwenziwe (bila haki), basi akifanya hivyo, atafungwa nacho kutoka ardhi saba mpaka Siku ya Qiyaamah.” [Ahmad].

 

Pia,

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Alisimama mbele yetu Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akataja suala la kuiba ngawira, akalishadidia na kulitilia umuhimu jambo hilo, akasema: “Nisije kumkuta mmoja wenu siku ya Qiyaamah juu ya shingo yake kuna mbuzi anatoa sauti, juu yake kuna farasi anatoa sauti aseme: Ee Rasuli wa Allaah! Niokoe! Nitamwambia: Similiki kwako kitu chochote, hakika nilikubalighishia. Na juu ya shingo yake kuna ngamia anatoa sauti aseme: Ee Rasuli wa Allaah! Niokoe! Nitamwambia: Similiki kwako kitu chochote hakika nilikubalighishia. Na juu ya shingo yake kuna nguo zilizo chanikachanika zinapepea kisha aseme: Ee Rasuli wa Allaah! Niokoe! Nitamwambia: Similiki kwako kitu chochote hakika nilikubalighishia. [Al-Bukhaariy (2891)].

 

Na pia,

 

‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Siku ya vita vya Khaybar, Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) walimwendea na kusema: Fulani na fulani wamekufa shahidi, fulani na fulani wamekufa shahidi. Walipomtaja mmojawapo kuwa kafariki shahidi, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hapana! Nimemuona motoni kwa sababu ya kanzu aliyoiiba (katika ngawira).” [Ahmad na Muslim kwa riwaayah nyingine].

 

 



117-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tawbah: Aayah: 117 - 119

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

Suwrah At-Tawbah Aayah: 117 - 119

 

 

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ مِن بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّهُ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١١٧﴾

Kwa yakini Allaah Amepokea tawbah ya Nabiy na Muhajirina na Answaar ambao wamemfuata (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) katika saa ya dhiki baada ya nyoyo za kundi miongoni mwao zilikaribia kuelemea mbali na haki Akapokea tawbah yao. Hakika Yeye kwao ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.

 

وَعَلَى الثَّلَاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا حَتَّىٰ إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ وَضَاقَتْ عَلَيْهِمْ أَنفُسُهُمْ وَظَنُّوا أَن لَّا مَلْجَأَ مِنَ اللَّـهِ إِلَّا إِلَيْهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴿١١٨﴾

Na (Akapokea tawbah) ya wale watatu waliobaki nyuma (wakajuta mno) mpaka ardhi ikadhikika kwao juu ya kuwa ni pana na zikadhikika nafsi zao, na wakatambua kwamba hakuna pa kumkimbia Allaah isipokuwa kuelekea Kwake; kisha (Allaah) Akapokea tawbah yao, ili watubie. Hakika Allaah Yeye Ndiye Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ﴿١١٩﴾

Enyi walioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli. [At-Tawbah: 117-119]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ عُقَيْلٍ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ كَعْبِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ كَعْبِ بْنِ مَالِكٍ ـ وَكَانَ قَائِدَ كَعْبٍ مِنْ بَنِيهِ حِينَ عَمِيَ ـ قَالَ سَمِعْتُ كَعْبَ بْنَ مَالِكٍ، يُحَدِّثُ حِينَ تَخَلَّفَ عَنْ قِصَّةِ، تَبُوكَ قَالَ كَعْبٌ لَمْ أَتَخَلَّفْ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي غَزْوَةٍ غَزَاهَا إِلاَّ فِي غَزْوَةِ تَبُوكَ، غَيْرَ أَنِّي كُنْتُ تَخَلَّفْتُ فِي غَزْوَةِ بَدْرٍ، وَلَمْ يُعَاتِبْ أَحَدًا تَخَلَّفَ، عَنْهَا إِنَّمَا خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُرِيدُ عِيرَ قُرَيْشٍ، حَتَّى جَمَعَ اللَّهُ بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ عَدُوِّهِمْ عَلَى غَيْرِ مِيعَادٍ وَلَقَدْ شَهِدْتُ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لَيْلَةَ الْعَقَبَةِ حِينَ تَوَاثَقْنَا عَلَى الإِسْلاَمِ، وَمَا أُحِبُّ أَنَّ لِي بِهَا مَشْهَدَ بَدْرٍ، وَإِنْ كَانَتْ بَدْرٌ أَذْكَرَ فِي النَّاسِ مِنْهَا، كَانَ مِنْ خَبَرِي أَنِّي لَمْ أَكُنْ قَطُّ أَقْوَى وَلاَ أَيْسَرَ حِينَ تَخَلَّفْتُ عَنْهُ فِي تِلْكَ الْغَزْوَةِ، وَاللَّهِ مَا اجْتَمَعَتْ عِنْدِي قَبْلَهُ رَاحِلَتَانِ قَطُّ حَتَّى جَمَعْتُهُمَا فِي تِلْكَ الْغَزْوَةِ، وَلَمْ يَكُنْ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُرِيدُ غَزْوَةً إِلاَّ وَرَّى بِغَيْرِهَا، حَتَّى كَانَتْ تِلْكَ الْغَزْوَةُ، غَزَاهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي حَرٍّ شَدِيدٍ، وَاسْتَقْبَلَ سَفَرًا بَعِيدًا وَمَفَازًا وَعَدُوًّا كَثِيرًا، فَجَلَّى لِلْمُسْلِمِينَ أَمْرَهُمْ لِيَتَأَهَّبُوا أُهْبَةَ غَزْوِهِمْ، فَأَخْبَرَهُمْ بِوَجْهِهِ الَّذِي يُرِيدُ، وَالْمُسْلِمُونَ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَثِيرٌ، وَلاَ يَجْمَعُهُمْ كِتَابٌ حَافِظٌ ـ يُرِيدُ الدِّيوَانَ ـ قَالَ كَعْبٌ فَمَا رَجُلٌ يُرِيدُ أَنْ يَتَغَيَّبَ إِلاَّ ظَنَّ أَنْ سَيَخْفَى لَهُ مَا لَمْ يَنْزِلْ فِيهِ وَحْىُ اللَّهِ، وَغَزَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم تِلْكَ الْغَزْوَةَ حِينَ طَابَتِ الثِّمَارُ وَالظِّلاَلُ، وَتَجَهَّزَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَالْمُسْلِمُونَ مَعَهُ، فَطَفِقْتُ أَغْدُو لِكَىْ أَتَجَهَّزَ مَعَهُمْ فَأَرْجِعُ وَلَمْ أَقْضِ شَيْئًا، فَأَقُولُ فِي نَفْسِي أَنَا قَادِرٌ عَلَيْهِ‏.‏ فَلَمْ يَزَلْ يَتَمَادَى بِي حَتَّى اشْتَدَّ بِالنَّاسِ الْجِدُّ، فَأَصْبَحَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَالْمُسْلِمُونَ مَعَهُ وَلَمْ أَقْضِ مِنْ جَهَازِي شَيْئًا، فَقُلْتُ أَتَجَهَّزُ بَعْدَهُ بِيَوْمٍ أَوْ يَوْمَيْنِ ثُمَّ أَلْحَقُهُمْ، فَغَدَوْتُ بَعْدَ أَنْ فَصَلُوا لأَتَجَهَّزَ، فَرَجَعْتُ وَلَمْ أَقْضِ شَيْئًا، ثُمَّ غَدَوْتُ ثُمَّ رَجَعْتُ وَلَمْ أَقْضِ شَيْئًا، فَلَمْ يَزَلْ بِي حَتَّى أَسْرَعُوا وَتَفَارَطَ الْغَزْوُ، وَهَمَمْتُ أَنْ أَرْتَحِلَ فَأُدْرِكَهُمْ، وَلَيْتَنِي فَعَلْتُ، فَلَمْ يُقَدَّرْ لِي ذَلِكَ، فَكُنْتُ إِذَا خَرَجْتُ فِي النَّاسِ بَعْدَ خُرُوجِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَطُفْتُ فِيهِمْ، أَحْزَنَنِي أَنِّي لاَ أَرَى إِلاَّ رَجُلاً مَغْمُوصًا عَلَيْهِ النِّفَاقُ أَوْ رَجُلاً مِمَّنْ عَذَرَ اللَّهُ مِنَ الضُّعَفَاءِ، وَلَمْ يَذْكُرْنِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم حَتَّى بَلَغَ تَبُوكَ، فَقَالَ وَهْوَ جَالِسٌ فِي الْقَوْمِ بِتَبُوكَ ‏"‏ مَا فَعَلَ كَعْبٌ ‏"‏‏.‏ فَقَالَ رَجُلٌ مِنْ بَنِي سَلِمَةَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، حَبَسَهُ بُرْدَاهُ وَنَظَرُهُ فِي عِطْفِهِ‏.‏ فَقَالَ مُعَاذُ بْنُ جَبَلٍ بِئْسَ مَا قُلْتَ، وَاللَّهِ يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَا عَلِمْنَا عَلَيْهِ إِلاَّ خَيْرًا‏.‏ فَسَكَتَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم‏.‏ قَالَ كَعْبُ بْنُ مَالِكٍ فَلَمَّا بَلَغَنِي أَنَّهُ تَوَجَّهَ قَافِلاً حَضَرَنِي هَمِّي، وَطَفِقْتُ أَتَذَكَّرُ الْكَذِبَ وَأَقُولُ بِمَاذَا أَخْرُجُ مِنْ سَخَطِهِ غَدًا وَاسْتَعَنْتُ عَلَى ذَلِكَ بِكُلِّ ذِي رَأْىٍ مِنْ أَهْلِي، فَلَمَّا قِيلَ إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَدْ أَظَلَّ قَادِمًا زَاحَ عَنِّي الْبَاطِلُ، وَعَرَفْتُ أَنِّي لَنْ أَخْرُجَ مِنْهُ أَبَدًا بِشَىْءٍ فِيهِ كَذِبٌ، فَأَجْمَعْتُ صِدْقَهُ، وَأَصْبَحَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَادِمًا، وَكَانَ إِذَا قَدِمَ مِنْ سَفَرٍ بَدَأَ بِالْمَسْجِدِ فَيَرْكَعُ فِيهِ رَكْعَتَيْنِ ثُمَّ جَلَسَ لِلنَّاسِ، فَلَمَّا فَعَلَ ذَلِكَ جَاءَهُ الْمُخَلَّفُونَ، فَطَفِقُوا يَعْتَذِرُونَ إِلَيْهِ، وَيَحْلِفُونَ لَهُ، وَكَانُوا بِضْعَةً وَثَمَانِينَ رَجُلاً فَقَبِلَ مِنْهُمْ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلاَنِيَتَهُمْ، وَبَايَعَهُمْ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمْ، وَوَكَلَ سَرَائِرَهُمْ إِلَى اللَّهِ، فَجِئْتُهُ فَلَمَّا سَلَّمْتُ عَلَيْهِ تَبَسَّمَ تَبَسُّمَ الْمُغْضَبِ، ثُمَّ قَالَ ‏"‏ تَعَالَ ‏"‏‏.‏ فَجِئْتُ أَمْشِي حَتَّى جَلَسْتُ بَيْنَ يَدَيْهِ، فَقَالَ لِي ‏"‏ مَا خَلَّفَكَ أَلَمْ تَكُنْ قَدِ ابْتَعْتَ ظَهْرَكَ ‏"‏‏.‏ فَقُلْتُ بَلَى، إِنِّي وَاللَّهِ لَوْ جَلَسْتُ عِنْدَ غَيْرِكَ مِنْ أَهْلِ الدُّنْيَا، لَرَأَيْتُ أَنْ سَأَخْرُجُ مِنْ سَخَطِهِ بِعُذْرٍ، وَلَقَدْ أُعْطِيتُ جَدَلاً، وَلَكِنِّي وَاللَّهِ لَقَدْ عَلِمْتُ لَئِنْ حَدَّثْتُكَ الْيَوْمَ حَدِيثَ كَذِبٍ تَرْضَى بِهِ عَنِّي لَيُوشِكَنَّ اللَّهُ أَنْ يُسْخِطَكَ عَلَىَّ، وَلَئِنْ حَدَّثْتُكَ حَدِيثَ صِدْقٍ تَجِدُ عَلَىَّ فِيهِ إِنِّي لأَرْجُو فِيهِ عَفْوَ اللَّهِ، لاَ وَاللَّهِ مَا كَانَ لِي مِنْ عُذْرٍ، وَاللَّهِ مَا كُنْتُ قَطُّ أَقْوَى وَلاَ أَيْسَرَ مِنِّي حِينَ تَخَلَّفْتُ عَنْكَ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ أَمَّا هَذَا فَقَدْ صَدَقَ، فَقُمْ حَتَّى يَقْضِيَ اللَّهُ فِيكَ ‏"‏‏.‏ فَقُمْتُ وَثَارَ رِجَالٌ مِنْ بَنِي سَلِمَةَ فَاتَّبَعُونِي، فَقَالُوا لِي وَاللَّهِ مَا عَلِمْنَاكَ كُنْتَ أَذْنَبْتَ ذَنْبًا قَبْلَ هَذَا، وَلَقَدْ عَجَزْتَ أَنْ لاَ تَكُونَ اعْتَذَرْتَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِمَا اعْتَذَرَ إِلَيْهِ الْمُتَخَلِّفُونَ، قَدْ كَانَ كَافِيَكَ ذَنْبَكَ اسْتِغْفَارُ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لَكَ، فَوَاللَّهِ مَا زَالُوا يُؤَنِّبُونِي حَتَّى أَرَدْتُ أَنْ أَرْجِعَ فَأُكَذِّبُ نَفْسِي، ثُمَّ قُلْتُ لَهُمْ هَلْ لَقِيَ هَذَا مَعِي أَحَدٌ قَالُوا نَعَمْ، رَجُلاَنِ قَالاَ مِثْلَ مَا قُلْتَ، فَقِيلَ لَهُمَا مِثْلُ مَا قِيلَ لَكَ‏.‏ فَقُلْتُ مَنْ هُمَا قَالُوا مُرَارَةُ بْنُ الرَّبِيعِ الْعَمْرِيُّ وَهِلاَلُ بْنُ أُمَيَّةَ الْوَاقِفِيُّ‏.‏ فَذَكَرُوا لِي رَجُلَيْنِ صَالِحَيْنِ قَدْ شَهِدَا بَدْرًا فِيهِمَا إِسْوَةٌ، فَمَضَيْتُ حِينَ ذَكَرُوهُمَا لِي، وَنَهَى رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم الْمُسْلِمِينَ عَنْ كَلاَمِنَا أَيُّهَا الثَّلاَثَةُ مِنْ بَيْنِ مَنْ تَخَلَّفَ عَنْهُ، فَاجْتَنَبَنَا النَّاسُ وَتَغَيَّرُوا لَنَا حَتَّى تَنَكَّرَتْ فِي نَفْسِي الأَرْضُ، فَمَا هِيَ الَّتِي أَعْرِفُ، فَلَبِثْنَا عَلَى ذَلِكَ خَمْسِينَ لَيْلَةً، فَأَمَّا صَاحِبَاىَ فَاسْتَكَانَا وَقَعَدَا فِي بُيُوتِهِمَا يَبْكِيَانِ، وَأَمَّا أَنَا فَكُنْتُ أَشَبَّ الْقَوْمِ وَأَجْلَدَهُمْ، فَكُنْتُ أَخْرُجُ فَأَشْهَدُ الصَّلاَةَ مَعَ الْمُسْلِمِينَ وَأَطُوفُ فِي الأَسْوَاقِ، وَلاَ يُكَلِّمُنِي أَحَدٌ، وَآتِي رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَأُسَلِّمُ عَلَيْهِ وَهْوَ فِي مَجْلِسِهِ بَعْدَ الصَّلاَةِ، فَأَقُولُ فِي نَفْسِي هَلْ حَرَّكَ شَفَتَيْهِ بِرَدِّ السَّلاَمِ عَلَىَّ أَمْ لاَ ثُمَّ أُصَلِّي قَرِيبًا مِنْهُ فَأُسَارِقُهُ النَّظَرَ، فَإِذَا أَقْبَلْتُ عَلَى صَلاَتِي أَقْبَلَ إِلَىَّ، وَإِذَا الْتَفَتُّ نَحْوَهُ أَعْرَضَ عَنِّي، حَتَّى إِذَا طَالَ عَلَىَّ ذَلِكَ مِنْ جَفْوَةِ النَّاسِ مَشَيْتُ حَتَّى تَسَوَّرْتُ جِدَارَ حَائِطِ أَبِي قَتَادَةَ وَهْوَ ابْنُ عَمِّي وَأَحَبُّ النَّاسِ إِلَىَّ، فَسَلَّمْتُ عَلَيْهِ، فَوَاللَّهِ مَا رَدَّ عَلَىَّ السَّلاَمَ، فَقُلْتُ يَا أَبَا قَتَادَةَ، أَنْشُدُكَ بِاللَّهِ هَلْ تَعْلَمُنِي أُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَسَكَتَ، فَعُدْتُ لَهُ فَنَشَدْتُهُ فَسَكَتَ، فَعُدْتُ لَهُ فَنَشَدْتُهُ‏.‏ فَقَالَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ‏.‏ فَفَاضَتْ عَيْنَاىَ وَتَوَلَّيْتُ حَتَّى تَسَوَّرْتُ الْجِدَارَ، قَالَ فَبَيْنَا أَنَا أَمْشِي بِسُوقِ الْمَدِينَةِ إِذَا نَبَطِيٌّ مِنْ أَنْبَاطِ أَهْلِ الشَّأْمِ مِمَّنْ قَدِمَ بِالطَّعَامِ يَبِيعُهُ بِالْمَدِينَةِ يَقُولُ مَنْ يَدُلُّ عَلَى كَعْبِ بْنِ مَالِكٍ فَطَفِقَ النَّاسُ يُشِيرُونَ لَهُ، حَتَّى إِذَا جَاءَنِي دَفَعَ إِلَىَّ كِتَابًا مِنْ مَلِكِ غَسَّانَ، فَإِذَا فِيهِ أَمَّا بَعْدُ فَإِنَّهُ قَدْ بَلَغَنِي أَنَّ صَاحِبَكَ قَدْ جَفَاكَ، وَلَمْ يَجْعَلْكَ اللَّهُ بِدَارِ هَوَانٍ وَلاَ مَضْيَعَةٍ، فَالْحَقْ بِنَا نُوَاسِكَ‏.‏ فَقُلْتُ لَمَّا قَرَأْتُهَا وَهَذَا أَيْضًا مِنَ الْبَلاَءِ‏.‏ فَتَيَمَّمْتُ بِهَا التَّنُّورَ فَسَجَرْتُهُ بِهَا، حَتَّى إِذَا مَضَتْ أَرْبَعُونَ لَيْلَةً مِنَ الْخَمْسِينَ إِذَا رَسُولُ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَأْتِينِي فَقَالَ إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَأْمُرُكَ أَنْ تَعْتَزِلَ امْرَأَتَكَ فَقُلْتُ أُطَلِّقُهَا أَمْ مَاذَا أَفْعَلُ قَالَ لاَ بَلِ اعْتَزِلْهَا وَلاَ تَقْرَبْهَا‏.‏ وَأَرْسَلَ إِلَى صَاحِبَىَّ مِثْلَ ذَلِكَ، فَقُلْتُ لاِمْرَأَتِي الْحَقِي بِأَهْلِكِ فَتَكُونِي عِنْدَهُمْ حَتَّى يَقْضِيَ اللَّهُ فِي هَذَا الأَمْرِ‏.‏ قَالَ كَعْبٌ فَجَاءَتِ امْرَأَةُ هِلاَلِ بْنِ أُمَيَّةَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَتْ يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ هِلاَلَ بْنَ أُمَيَّةَ شَيْخٌ ضَائِعٌ لَيْسَ لَهُ خَادِمٌ فَهَلْ تَكْرَهُ أَنْ أَخْدُمَهُ قَالَ ‏"‏ لاَ وَلَكِنْ لاَ يَقْرَبْكِ ‏"‏‏.‏ قَالَتْ إِنَّهُ وَاللَّهِ مَا بِهِ حَرَكَةٌ إِلَى شَىْءٍ، وَاللَّهِ مَا زَالَ يَبْكِي مُنْذُ كَانَ مِنْ أَمْرِهِ مَا كَانَ إِلَى يَوْمِهِ هَذَا‏.‏ فَقَالَ لِي بَعْضُ أَهْلِي لَوِ اسْتَأْذَنْتَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي امْرَأَتِكَ كَمَا أَذِنَ لاِمْرَأَةِ هِلاَلِ بْنِ أُمَيَّةَ أَنْ تَخْدُمَهُ فَقُلْتُ وَاللَّهِ لاَ أَسْتَأْذِنُ فِيهَا رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَمَا يُدْرِينِي مَا يَقُولُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا اسْتَأْذَنْتُهُ فِيهَا وَأَنَا رَجُلٌ شَابٌّ فَلَبِثْتُ بَعْدَ ذَلِكَ عَشْرَ لَيَالٍ حَتَّى كَمَلَتْ لَنَا خَمْسُونَ لَيْلَةً مِنْ حِينِ نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَنْ كَلاَمِنَا، فَلَمَّا صَلَّيْتُ صَلاَةَ الْفَجْرِ صُبْحَ خَمْسِينَ لَيْلَةً، وَأَنَا عَلَى ظَهْرِ بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِنَا، فَبَيْنَا أَنَا جَالِسٌ عَلَى الْحَالِ الَّتِي ذَكَرَ اللَّهُ، قَدْ ضَاقَتْ عَلَىَّ نَفْسِي، وَضَاقَتْ عَلَىَّ الأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ، سَمِعْتُ صَوْتَ صَارِخٍ أَوْفَى عَلَى جَبَلِ سَلْعٍ بِأَعْلَى صَوْتِهِ يَا كَعْبُ بْنَ مَالِكٍ، أَبْشِرْ‏.‏ قَالَ فَخَرَرْتُ سَاجِدًا، وَعَرَفْتُ أَنْ قَدْ جَاءَ فَرَجٌ، وَآذَنَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِتَوْبَةِ اللَّهِ عَلَيْنَا حِينَ صَلَّى صَلاَةَ الْفَجْرِ، فَذَهَبَ النَّاسُ يُبَشِّرُونَنَا، وَذَهَبَ قِبَلَ صَاحِبَىَّ مُبَشِّرُونَ، وَرَكَضَ إِلَىَّ رَجُلٌ فَرَسًا، وَسَعَى سَاعٍ مِنْ أَسْلَمَ فَأَوْفَى عَلَى الْجَبَلِ وَكَانَ الصَّوْتُ أَسْرَعَ مِنَ الْفَرَسِ، فَلَمَّا جَاءَنِي الَّذِي سَمِعْتُ صَوْتَهُ يُبَشِّرُنِي نَزَعْتُ لَهُ ثَوْبَىَّ، فَكَسَوْتُهُ إِيَّاهُمَا بِبُشْرَاهُ، وَاللَّهِ مَا أَمْلِكُ غَيْرَهُمَا يَوْمَئِذٍ، وَاسْتَعَرْتُ ثَوْبَيْنِ فَلَبِسْتُهُمَا، وَانْطَلَقْتُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَيَتَلَقَّانِي النَّاسُ فَوْجًا فَوْجًا يُهَنُّونِي بِالتَّوْبَةِ، يَقُولُونَ لِتَهْنِكَ تَوْبَةُ اللَّهِ عَلَيْكَ‏.‏ قَالَ كَعْبٌ حَتَّى دَخَلْتُ الْمَسْجِدَ، فَإِذَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم جَالِسٌ حَوْلَهُ النَّاسُ فَقَامَ إِلَىَّ طَلْحَةُ بْنُ عُبَيْدِ اللَّهِ يُهَرْوِلُ حَتَّى صَافَحَنِي وَهَنَّانِي، وَاللَّهِ مَا قَامَ إِلَىَّ رَجُلٌ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ غَيْرُهُ، وَلاَ أَنْسَاهَا لِطَلْحَةَ، قَالَ كَعْبٌ فَلَمَّا سَلَّمْتُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَهْوَ يَبْرُقُ وَجْهُهُ مِنَ السُّرُورِ ‏"‏ أَبْشِرْ بِخَيْرِ يَوْمٍ مَرَّ عَلَيْكَ مُنْذُ وَلَدَتْكَ أُمُّكَ ‏"‏‏.‏ قَالَ قُلْتُ أَمِنْ عِنْدِكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَمْ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ قَالَ ‏"‏ لاَ، بَلْ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ ‏"‏‏.‏ وَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا سُرَّ اسْتَنَارَ وَجْهُهُ حَتَّى كَأَنَّهُ قِطْعَةُ قَمَرٍ، وَكُنَّا نَعْرِفُ ذَلِكَ مِنْهُ، فَلَمَّا جَلَسْتُ بَيْنَ يَدَيْهِ قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ مِنْ تَوْبَتِي أَنْ أَنْخَلِعَ مِنْ مَالِي صَدَقَةً إِلَى اللَّهِ وَإِلَى رَسُولِ اللَّهِ‏.‏ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ أَمْسِكْ عَلَيْكَ بَعْضَ مَالِكَ فَهُوَ خَيْرٌ لَكَ ‏"‏‏.‏ قُلْتُ فَإِنِّي أُمْسِكُ سَهْمِي الَّذِي بِخَيْبَرَ، فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ اللَّهَ إِنَّمَا نَجَّانِي بِالصِّدْقِ، وَإِنَّ مِنْ تَوْبَتِي أَنْ لاَ أُحَدِّثَ إِلاَّ صِدْقًا مَا بَقِيتُ، فَوَاللَّهِ مَا أَعْلَمُ أَحَدًا مِنَ الْمُسْلِمِينَ أَبْلاَهُ اللَّهُ فِي صِدْقِ الْحَدِيثِ مُنْذُ ذَكَرْتُ ذَلِكَ لِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَحْسَنَ مِمَّا أَبْلاَنِي، مَا تَعَمَّدْتُ مُنْذُ ذَكَرْتُ ذَلِكَ لِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِلَى يَوْمِي هَذَا كَذِبًا، وَإِنِّي لأَرْجُو أَنْ يَحْفَظَنِي اللَّهُ فِيمَا بَقِيتُ وَأَنْزَلَ اللَّهُ عَلَى رَسُولِهِ صلى الله عليه وسلم ‏((‏لَقَدْ تَابَ اللَّهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ)) إِلَى قَوْلِهِ ((‏‏وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ‏‏)) فَوَاللَّهِ مَا أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَىَّ مِنْ نِعْمَةٍ قَطُّ بَعْدَ أَنْ هَدَانِي لِلإِسْلاَمِ أَعْظَمَ فِي نَفْسِي مِنْ صِدْقِي لِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنْ لاَ أَكُونَ كَذَبْتُهُ، فَأَهْلِكَ كَمَا هَلَكَ الَّذِينَ كَذَبُوا، فَإِنَّ اللَّهَ قَالَ لِلَّذِينَ كَذَبُوا حِينَ أَنْزَلَ الْوَحْىَ شَرَّ مَا قَالَ لأَحَدٍ، فَقَالَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى ((سَيَحْلِفُونَ بِاللَّهِ لَكُمْ إِذَا انْقَلَبْتُمْ‏‏)) إِلَى قَوْلِهِ ((‏‏فَإِنَّ اللَّهَ لاَ يَرْضَى عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ))‏‏‏.‏ قَالَ كَعْبٌ وَكُنَّا تَخَلَّفْنَا أَيُّهَا الثَّلاَثَةُ عَنْ أَمْرِ أُولَئِكَ الَّذِينَ قَبِلَ مِنْهُمْ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم حِينَ حَلَفُوا لَهُ، فَبَايَعَهُمْ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمْ وَأَرْجَأَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَمْرَنَا حَتَّى قَضَى اللَّهُ فِيهِ، فَبِذَلِكَ قَالَ اللَّهُ((‏وَعَلَى الثَّلاَثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا‏))وَلَيْسَ الَّذِي ذَكَرَ اللَّهُ مِمَّا خُلِّفْنَا عَنِ الْغَزْوِ إِنَّمَا هُوَ تَخْلِيفُهُ إِيَّانَا وَإِرْجَاؤُهُ أَمْرَنَا عَمَّنْ حَلَفَ لَهُ وَاعْتَذَرَ إِلَيْهِ، فَقَبِلَ مِنْهُ‏.‏

 

Ametuhadithia Yahyaa bin Bakiyr amesema, ametuhadithia Al-Layth toka kwa ‘Aqiyl toka kwa Ibn Shihaab toka kwa ‘Abdurrahmaan bin ‘Abdillaah bin Ka’ab bin Maalik kuwa ‘Abdullaah bin Ka’ab bin Maalik ambaye alikuwa miongoni mwa watoto wa Ka’ab aliyekuwa akimwongoza barabara wakati alipopoteza macho amesema: Nimemsikia Ka’ab bin Maalik akihadithia kuhusu kisa cha Tabuk baada ya yeye kubaki nyumbani asende vitani. Ka’ab alisema: “Sikubaki nyuma nikamwacha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  katika vita vyovyote alivyopigana isipokuwa vita vya Tabuk, ingawa vita vya Badr sikushirki na hakuna yeyote ambaye hakushiriki alilaumiwa, kwa kuwa Rasuli alitoka kwa ajili ya msafara wa biashara wa Maqureshi, na Allaah Akawakutanisha wao na maadui zao bila kupanga hilo au kutarajia. Hakika mimi nilishuhudia na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  usiku wa Aqabah wakati tulipopeana na kuchukuliana ahadi na agano juu ya Uislamu. Nami sipendi kulinganisha tukio hilo na Badr ingawa Badr inakumbukwa na kutajwa zaidi na watu kuliko Usiku huo. Na ni maarufu kwa kila mmoja kuwa sijawahi kamwe kuwa mwenye nguvu na uwezo zaidi wa kimali niliposalia nyumbani na kumwacha Rasuli kuliko kwenye vita hivi. Wa-Allaahi, sikuwahi kuwa na wanyama wawili kwa pamoja kabla ya hapo, lakini niliweza kuwakusanya katika vita hiyo. Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)    hakwenda katika vita yoyote ila aliitolea habari kinyume (ili kuwahadaa maadui) mpaka vilipokuja vita hivyo ambavyo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alivikabili katika kipindi cha joto kali mno, safari ndefu, jangwa la masafa marefu na idadi kubwa ya maadui. Rasuli akawaeleza Waislamu ukweli halisi wa mambo yalivyo ili wajiandae maandalizi kamili, na akawaeleza ni wapi hasa anataka kwenda nao. Idadi ya Waislamu pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ilikuwa ni kubwa lakini idadi hii  haikusajiliwa kwenye buku la rekodi za wapiganaji. Ka’ab akasema: Hakuna yeyote katika watu aliyetaka kughibu asende vitani isipokuwa alikuwa ana uhakika kuwa hatojulikana (kutokana na wingi wa watu) isipokuwa tu kama Wahyi toka kwa Allaah utashuka (kumfichua). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   akatoka kwenda kwenye vita hiyo wakati matunda yalipokuwa yamekomaa na kuiva. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa amejiandaa vilivyo yeye pamoja na Waislamu, nami nikaanza kutoka asubuhi ili nipate kujiandaa na kujiweka tayari, nikawa narudi bila kufanya lolote. Nikawa najiambia moyoni kuwa nitaweza tu kufanya, na nikaendelea kujivuta na kusogeza muda mpaka watu wakawa tayari kabisa washajiandaa. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akaondoka asubuhi pamoja na Waislamu nami bado sijajiandaa kwa chochote. Nikasema nitajiandaa baada yake kwa siku moja au mbili kisha nitawawahi. Nikarauka mapema ili nijiandae baada ya wao kuondoka, lakini nilirudi bila kufanya kitu, kisha nikarauka tena, nikarudi na sikufanya chochote. Nikaendelea kufanya hivyo na wao wakaongeza mwendo na kasi ya kufika vitani ikachanganyia zaidi. Nikapanga niondoke ili niwawahi, lakini najuta kwa nini sikufanya hivyo, kwani sikuweza tena kuondoka. Nikawa ninapotoka kwa watu na kuanza kuranda huku na kule baada ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  kuondoka, napatwa na huzuni kwa kuwa nilikuwa sioni isipokuwa mtu mwenye sifa mbaya ya unafiki, au mtu dhaifu katika ambao Allaah Amewapa udhuru. Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  hakunitaja mpaka alipowasili Tabuk. Akiwa amekaa na watu huko Tabuk aliwauliza: Yuko wapi Ka’ab? Mtu mmoja wa Baniy Salamah akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Ameshughulishwa na dunia yake na kujipenda nafsi yake na hali yake. Mu’aadh bin Jabal akasema: Maneno gani hayo mabaya umesema?! Wa-Allaahi ee Rasuli wa Allaah, hatumjui kwa jingine lolote isipokuwa kheri tu. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   akanyamaza bila kusema kitu. Ka’ab bin Maalik anasema: Niliposikia habari kuwa Rasuli anarudi pamoja na msafara (wa Waislamu), ghamu ilinigubika. Nikaanza kufikiria uongo na kujishauri kwa njia gani nitajitetea asinikasirikie akifika. Nikaomba ushauri pia kwa kila jamaa yangu mwenye busara. Na iliposemwa kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) yuko njiani na amekaribia kuwasili, fikra mbovu iliniondoka na nikajua kwa hakika kuwa kamwe sitoweza kujinasua toka kwake kwa sababu yoyote nitakayompa ya uongo, nikaamua kwa moyo mmoja kusema ukweli. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa anakuja, na alikuwa anapokuja toka safari, huanza kuingia Msikitini akaswali rakaa mbili, kisha hukaa na kuzungumza na watu. Alipokaa kuzungumza nao, walimjia wanafiki wakaanza kumtolea nyudhuru zao na kumwapia. Walikuwa ni watu themanini na kuzidi kidogo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   akawakubalia mwonekano wao wa nje, akawapa bay-‘i na akawaombea maghfirah, na waliyoyaficha vifuani mwao alimwachia Allaah. Nami nikamjia, na nilipomsalimia, alitabasamu tabasamu la mtu aliyekasirishwa kisha akaniambia: “Njoo.” Nikatembea mpaka nikakaa mbele yake na akaniuliza: “Nini kilikufanya ubaki nyumbani? Hivi hukuwa umenunua ngamia wako wa kupanda?” Nikasema: Na’sm, hakika mimi wa-Allaahi ee Rasuli wa Allaah, lau ningelikaa mbele ya mtu mwingine asiyekuwa wewe katika watu wa dunia, naona ningeliweza kujinasua na hasira zake kwa udhuru wowote. Wa-Allaahi hakika mimi nimepewa kipawa cha ufasaha wa kuzungumza, lakini mimi wa-Allaah hakika nimejua kuwa ikiwa nitakwambia leo maneno ya uongo ambayo utanikubalia, basi bila shaka Allaah Yuakaribia kukujaza hasira juu yangu, na kama nitakueleza maneno ya kweli, basi utayakuta ninayo. Hakika mimi natarajia kupata Msamaha wa Allaah. Hapana, wa-Allaah, mimi sikuwa na udhuru wowote. Wa-Allaah, sikuwahi kamwe kuwa mwenye nguvu na uwezo zaidi wa kimali niliposalia nyumbani na kukuacha kuliko ilivyo sasa. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   akasema: “Ama huyu, hakika amesema kweli. Basi simama mpaka Allaah Atakapohukumu jambo lako.” Nikasimama, na watu katika ukoo wa Baniy Salamah wakahamaki, wakanifata na kuniambia:  Sisi hatujawahi kusikia umefanya kosa lolote kabla ya hili, nawe umeshindwa hata kuomba udhuru kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  kama walivyomtolea udhuru wengine waliobaki nyuma!! Kosa lako lilikuwa linatosha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  kukuombea maghfirah.  Basi wa-Allaah, waliendelea kunisakama kwa lawama mpaka nikataka kurudi nikajikadhibishe mwenyewe (kwa Rasuli). Kisha nikawaambia: Je, kuna mwingine niko naye pamoja kakumbana na haya? Wakasema: Na’am, wako watu wawili waliosema mfano wa ulivyosema, na wakaambiwa kama ulivyoambiwa. Nikawauliza, ni akina nani? Wakasema ni Muraarah bin Ar-Rabiy Al-‘Amriy na Hilaal bin Umayyah Al-Waaqifiy. Wakanieleza kuwa ni watu wema wa kuwa kiigizo chema kwangu, nami nikaondoka kwenda zangu baada tu ya kuwataja. Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akawakataza Waislamu kuzungumza nasi watatu kati ya ambao hawakwenda naye. Watu wakatupiga pande, wakatususa na wakatubadilikia mpaka ardhi yenyewe ikabadilika ndani ya nafsi yangu nikawa naiona si ile ardhi ambayo ninaijua. Tukakaa katika hali hiyo siku khamisini. Ama wenzangu wawili, wao walinyong’onyea kabisa wakabaki majumbani mwao wakilia, lakini mimi nilikuwa jasiri, mkakamavu na mthubutu zaidi. Nilikuwa nikitoka na kwenda kuswali pamoja na Waislamu na kuzunguka masokoni na hakuna yeyote aliyenisemesha, na ninamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)    nikamsalimia, naye yuko katika majlisi yake baada ya Swalaah, nikawa najiuliza kama ametikisa midomo yake kujibu salaam yangu au hakutikisa. Halafu ninaswali karibu yake na kumwangalia kwa jicho la pembe, nikifunga Swalaah yangu hunielekea, lakini ninapogeuka upande wake, hunipa mgongo. Nikachoshwa na kipindi kirefu cha kupigwa pande na watu. Nikaondoka na kwenda kuukwea uzio wa ukuta wa Abuu Qataadah, naye ni mtoto wa ammi yangu na kipenzi changu zaidi kuliko wote, nikamsalimia, na wa-Allaah hakunijibu salamu yangu. Nikasema: Ee Abuu Qataadah, nakusihi kwa Jina la Allaah, je unajua kwamba mimi nampenda Allaah na Rasuli Wake? Akanyamaza, nikamuuliza tena na kumsihi lakini alinyamaza. Nikamrudia tena na kumsihi akasema: Allaah na Rasuli Wake Wanajua zaidi. Macho yangu yakatiririka machozi, nikaondoka na kuukwea ukuta. Nilipokuwa natembea kwenye soko la Madiynah, ghafla nikamwona mkulima katika wakulima wenyeji wa Sham ambaye alileta chakula kuuza Madiynah akiuliza watu: Nani anaweza kunionyesha alipo Ka’ab bin Maalik. Watu wakaanza kumwelekeza, na alipofika kwangu, alinipa barua toka kwa Mfalme Ghassaan ikiwa imeandikwa: “Ama baada ya maamkizi, nimepata habari kuwa swahibu yako amekususa, na Allaah Hakukufanya kuwa katika nchi ya udhalili wala ya kudhulumiwa haki, basi njoo kwetu tukufariji.” Nilipomaliza kuisoma nilisema hii pia ni katika majaribio, nikaenda nayo kwenye tanuri nikaiwashia moto. Zilipopita siku arubaini, ghafla alinijia mjumbe wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   akaniambia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   anakuamuru ukae mbali na mkeo. Nikamuuliza, nimtaliki au nifanye nini? Akasema hapana, bali kaa nae mbali na wala usimkaribie. Na wenzangu wawili walipelekewa ujumbe huo huo. Nikamwambia mke wangu nenda kwa wazazi wako, utabakia huko mpaka pale Allaah Atakapohukumu katika jambo hili. Ka’ab anasema: Mke wa Hilaal bin Umayyah akamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  na kumwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika Hilaal ni mzee asiyejiweza, na hana wa kumtumikia. Je, utachukia nikimtumikia? Akasema: “Hapana, lakini asikukurubie.” Akasema: Hakika Wa-Allaah hawezi kufanya lolote, wa-Allaah hakuacha kulia tokea jambo lake kuwa hivi mpaka leo. Baadhi ya jamaa zangu wakanishauri nami nimwombe idhini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)    kwa mke wangu kama alivyomruhusu mke wa Hilaal amhudumie. Nikasema: Wa-Allaah, simtaki Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  ruhusa kwa mke wangu, sijui nini ataniambia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  nikimwomba ruhusa kwa mke wangu na mimi ni mtu kijana? Nilikaa baada ya hapo siku kumi mpaka zikatimia siku khamsini tokea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  alipokataza watu kuzungumza nasi. Niliposwali Swalaah ya Alfajiri, zilitimu siku khamsini nami niko juu ya paa la nyumba kati ya nyumba zetu. Na nikiwa nimekaa katika hali Aliyoielezea Allaah ya kuwa nafsi imedhikika na ardhi imekuwa finyu kwangu juu ya kuwa ni pana, nilisikia sauti kali ya mtu yenye kupenya masikio toka juu ya Mlima Sal-‘i. Alipaza sauti yake ya juu kabisa (akinadi): Ee Ka’ab bin Maalik! Furahi kwa bishara njema. Akasema: Niliporomoka nikasujudu, na nikajua kwa uhakika kuwa mambo yamemalizika. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  alikuwa ametangaza Allaah kutusamehe baada ya kuswali Swalaah ya Alfajiri. Watu wakaanza kutupa bishara hiyo njema, wakaenda kwa wenzangu wawili kuwapa habari hiyo. Mtu mmoja akaja kwangu mbio kwa farasi na mwingine akaenda kwa miguu juu ya mlima akanadi kwa sauti kali, na sauti yake ilifika haraka zaidi kuliko farasi. Aliponijia yule niliyeisikia sauti yake akinipa bishara hiyo njema, nilivua nguo zangu mbili nikamvisha yeye kwa (furaha ya) kuniletea  bishara. Wa-Allaahi, sikuwa na nguo nyingine zaidi ya hizo mbili siku hiyo. Nikaazima nguo mbili nikazivaa, nikatoka haraka hadi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  na watu makundi kwa makundi wakawa wananipongeza kwa kusamehewa wakiniambia: Hongera kwa kupata Msamaha wa Allaah. Ka’ab akasema: Mpaka nikaingia Msikitini, nikamkuta Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amekaa na watu wamemzunguka. Twalhah bin ‘Ubaydillaah akasimama na kuja kwangu haraka, akanipa mkono na kunipongeza. Wa-Allaah, hakusimama kuja kwangu mtu yeyote katika Muhaajiriyna isipokuwa yeye, na sitomsahau Twalhah kwa hilo. Nilipomsalimia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniambia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  na huku uso wake uking’aa kwa furaha: “Pokea bishara njema ya siku bora zaidi iliyokupitia tokea alipokuzaa mama yako.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anapofurahi, uso wake hung’aa kwa nuru na kuwa mithili ya kipande cha mwezi, nasi tulikuwa tunalijua hilo. Nilipokaa mbele yake nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika tawbah yangu ni kuachia mali yangu yote na kuitoa swadaqah kwa Allaah na Rasuli Wake. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)    akasema: “Baki na sehemu ya mali yako, ni bora zaidi kwako hilo.” Nikasema: Hakika mimi naishikilia hisa yangu ilioko Khaybar. Ee Rasuli wa Allaah! Hakika Allaah Ameniokoa kwa kusema ukweli, na hakika tawbah yangu ni kuwa sitosema isipokuwa kweli tu umri wangu wote uliosalia. Wa-Allaah, simjui hata mmoja katika Waislamu ambaye Allaah Alimpa mtihani mgumu zaidi katika suala la kusema ukweli tokea kuusema kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  kuliko Alivyonijaribu mimi. Na tokea kulitaja hilo kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  sijakusudia kusema uongo mpaka leo hii, nami nataraji Allaah Anihifadhi katika umri uliobakia. Allaah Akashusha kwa Rasuli Wake

 

 

لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ  

Kwa yakini Allaah Amepokea tawbah ya Nabiy na Muhajirina na Answaar

hadi

وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ

na kuweni pamoja na wakweli.

 

Basi naapa kwa Allaah, Allaah Hakunineemesha kamwe kwa neema yoyote baada ya Kunihidi katika Uislamu iliyo kubwa zaidi katika nafsi yangu kuliko kusema ukweli kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)    (Amenineemesha) nisiwe nimemwambia uongo nikaangamia kama walivyoangamia waliosema uongo. Hakika Allaah Ta’alaa Amesema kuhusu waliosema uongo maneno mabaya mno ambayo Hakumwambia yeyote Alipoteremsha Wahyi. Akasema Allaah (تبارك وتعالى)

 

    سَيَحْلِفُونَ بِاللَّهِ لَكُمْ إِذَا انْقَلَبْتُمْ

Watakuapieni kwa Allaah, mtakaporudi.

 

 

hadi Neno Lake

فَإِنَّ اللَّهَ لا يَرْضَى عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ

basi hakika Allaah Haridhii watu mafasiki. [At-Tawbah: 95-96]

 

Na Aliyoyaeleza Allaah (سبحانه وتعالى)  tulipobaki majumbani tusende vitani hayahusiani na vita, bali Anazungumzia kutukawishia (tawbah) na kuliahirisha jambo letu kinyume na waliomwapia, wakamtaka Rasuli udhuru, naye akawakubalia.

 

(Hii anakusudia Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

   وَعَلَى الثَّلَاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا  

Na (Akapokea tawbah) ya wale watatu waliobaki nyuma

 [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy, Ahmad]

 

 



20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...