Translate

Ijumaa, 10 Januari 2020

Vyakula 14 vinavyoongeza nguvu katika ubongo

Kuongeza akili

Vyakula 14 vinavyoongeza nguvu katika ubongo

Kuna wakati unaona wazi ubongo wako umechoka au ufanisi wake umepungua tofauti na zamani. Au sababu tu ya kazi na misongamano mingi unajikuta kichwa kimechoka kufanya kazi.

Hakuna dawa yoyote hospitalini inayoweza kukurudishia nguvu zako za ubongo. Dawa nyingi za kizungu za kuongeza nguvu za ubongo zina madhara makubwa baadaye katika mwili.

Kila mmoja wetu anapatwa na tatizo hili la kuhisi kushuka kwa nguvu za ubongo wake. Takwimu zinaonyesha baada ya miaka 85 uwezekano wako wa kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu huongezeka kwa asilimia 50.

Hivyo ni wazi tunahitaji kujiwekea mazoea na tabia ya kula vyakula na kuishi namna ambazo zitakuwa zikiendelea kuupa nguvu ubongo kila siku.

Hapa nimekuandalia orodha ya haraka haraka ya vyakula hivyo, pia uhakikishe unapata usingizi wa kutosha kila siku:

1. Mafuta ya zeituni
2. Mafuta ya nazi
3. Samaki
4. Binzari
5. Mayai
6. Korosho
7. Mazoezi ya viungo
8. Broccoli
9. Parachichi
10. Mvinyo mwekundu
11. Spinachi
12. Lozi (Almonds)
13. Unga wa mbegu za maboga
14. Kitunguu swaumu

Kama una swali lolote kuhusu post hii niulize hapo chini kwenye comment nitakujibu hapa hapa.

SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao

Imesomwa mara 1

Imehaririwa

Let's block ads! (Why?)

Jumanne, 7 Januari 2020

Vyakula 16 vinavyoongeza kinga ya mwili

VYAKULA 16 VINAVYOONGEZA KINGA YA MWILI Watu wengi tumekuwa tukijiuliza kinga ya mwili ni kitu gani na je ni nini tufanye ili kuiongeza hiyo kinga ndani ya miili yetu. Suala la kuimarisha na kuiongeza kinga ya mwili linapaswa kuwa ni jambo endelevu la kila siku. Hakuna dawa au chakula cha […]

Jumatano, 18 Desemba 2019

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili

CHAKULA CHA MGONJWA MWENYE KISUKARI AINA YA PILI Chakula bora kabisa kwa mgonjwa wa kisukari ni kile ambacho ni chakula cha asili na si kile ambacho kimetengenezwa kiwandani. Unahitaji chakula ambacho hakijakobolewa, unahitaji zaidi matunda na mboga za majani. Kutumia vyakula hivi naenda kukueleza kwenye hii makala kutakusaidia kupata mahitaji […]

Msikiti Mtakatifu wa al-Aqswa wavamiwa tena

Walowezi wa Kizayuni leo wameuvamia tena Msikiti wa al-Aqswa huko Palestina wakisaidiwa na askari wa jeshi la utawala haramu wa Israel na kuuvunjia heshima msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.
Walowezi hao  wa Kizayuni baada ya kuingia katika eneo la ndani la msikiti huo mtakatifu walisikika wakipiga nara dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti kwamba, hujuma na uvamizi huo umefanyika kwa msaada na uungaji mkono wa wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel.
Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za kukabiliana na vitendo hivyo.
Kwa mujibu wa duru za Kipalestina, karibu kila siku walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakifanya uvamizi katika msikiti huo lengo likiwa ni kutekeleza njama za kutokomeza utambulisho wa Kiislamu na Kikristo wa Msikiti wa al-Aqswa na badala yake kuweka nembo za Kizayuni.
aqswa
Walowezi wa Kizayuni wakipiga nara dhidi ya Uislamu baada ya kuvamia Msikiti wa al-Aqswa
Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.
Hata hivyo kusimama kidete wananchi wa Palestina hadi sasa kumekwamisha njama na mipango yote ya Wazayuni, zikiwemo njama zake za kubadilisha muundo wa kijamii na kijiografia wa Baytul Muqaddas.
Uvamizi huo unakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi ya Palestina. 




Bakwata wampongeza Rais Wa Tanzania kwa kwasamehe wafungwa 5,000

Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limeadhimisha miaka 51 tangu kuanzishwa kwake kwa mafanikio kadhaa, huku likimpongeza Rais John Pombe Magufuli wa nchi hiyo kwa namna anavyowatumikia wanyonge ikiwamo kuwapatia msamaha zaidi ya wafungwa 5,000 hivi karibuni
Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limetoa wito kwa wafungwa walioachiliwa, kutumia fursa ya maisha yao kutenda mema na kutumikia nchi yao kama nguvu kazi muhimu katika jamii na wasirejee tena katika vitendo vya uhalifu na uovu.
Akihutubia hapo jana jijjini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) Nuhu Mruma alisema kuwa, taasisi hiyo inampongeza sana Rais Magufuli kwa kuwasamehe wafungwa hao ambao bado walikuwa hawajamaliza muda wao wa kukaa gerezani.
Katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika mkoani Mwanza Disemba 9 mwaka huu, Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliandika historia mpya kwa mara ya kwanza tangu nchi ipate uhuru kwa kutangaza msamaha kwa wafungwa 5,533.

Wakati Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) likimpongeza Rais Magufuli kwa msamaha wake kwa wafungwa, baadhi ya wafungwa walioachiliwa huru hivi karibuni kwa msamaha wa Rais wameripotiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu na hata mauaji. Inaarifiwa kuwa, mtu mmoja ambaye aliachiwa huru kwa msamaha wa Rais Dkt. John hivi karibuni aliwavamia na kuwachoma visu watu 6 huku mmoja wao akifariki dunia hapo hapo. Tukio lilitokea katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera. Baada ya mtuhumiwa kutekeleza tukio hilo, wananchi wenye hasira kali walimvamia na kuanza kumshambulia hadi kumuua.


Jumanne, 17 Desemba 2019

Mawaidha : Othman maalim - Hekma ya Mtume swalallahu aleihi wasalaam [Listen/Download]





Aliyekamilika Iymaan Kwa Tabia Na Kumfanyia Wema Mke

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

Hadiyth Ya 29

Aliyekamilika Iymaan Kwa Tabia Na Kumfanyia Wema Mke





عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا  وَخِيَارُكُمْ خِيَارُكُمْ لِنِسَائِهِمْ خُلُقًا)) الترمذي وقال: حديث حسن صحيح
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muumin aliyekamilika iymaan ni aliye na tabia njema kabisa, na wabora wenu ni walio bora kwa wake zao kwa tabia))  [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Swahiyh Hasan]



Mafunzo na Mwongozo:


1. Uislamu unasisitiza kuwa na tabia njema kwa kila mtu.



2. Mume anasisitizwa kumfanyia wema mkewe katika maisha ya ndoa, si kumfanyia uovu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):


وَلَا تَنسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ   
  Na wala msisahau fadhila baina yenu.  [Al-Baqarah (2: 237)]

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):


  وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ  
Na kaeni nao kwa wema. [An-Nisaa (4: 19)]


Pia rejea kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): [Ar-Ruwm 30: 21]


3. Inapasa kuweko subira baina ya mume na mke katika mitihani inayowakabili ya maisha baina yao. [((Na mkisubiri ni kheri kwenu)) [An-Nisaa (4: 25)].



4. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kigezo bora kabisa katika kuamiliana na wake [Al-Ahzaab (33: 21)].

Pia Hadiyth zifuatazo:


 ((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa mke wake, na mimi ni mbora kwa watu wangu wa nyumbani [ahli])) [Ibn Maajah na Ad-Daarimiy].


((Mwanamke ameumbwa kwa ubavu, na sehemu iliyopinda ya ubavu ni juu yake, ukijaribu kuunyoosha utauvunja, na lau utauacha utaendelea kupinda, nakuusieni [kuwafanyia wema]) wake zenu)) [Al-Bukhaariy, Muslim]


((Allaah, Allaah, kwa wanawake,  hao ni wasaidizi wenu walio kwenye mikono yenu, mmewachukuwa kama ni amana kutoka kwa Allaah, na imekuwa halali tupu zao kwenu kwa neno lake Allaah  [iyjaab na qubuwl])) [Muslim, Abu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad]

Rejea pia Hadiyth namba (28), (35), (40).


20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...