Translate

Ijumaa, 1 Februari 2019

´Ibaadah ya du´aa 02



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2D0CQmx
via IFTTT

01. Lulu kuhusu Ibn-ul-Mundhir

1- Ibn-ul-Mundhir (kfrk. 318) tabaka 11

adh-Dhahabiy ameelezea wasifu wake katika ”Tadhkirat-ul-Huffaadhw” na akasema:

”Haafidhw wa kipekee, ´Allaamah na Faqiyh Abu Bakr Muhammad bin Ibraahiym bin al-Mundhir an-Naysaabuuriy. Alikuwa ni Shaykh wa Haram na mwandishi wa vitabu visivokuwa na mfano kukiwemo:

1 – al-Mabsuutw fiyl-Fiqh

2 – al-Ishraaf fiy Ikhtilaaf-il-´Ulamaa’

3 – al-Ijmaa´

Alikuwa na elimu iliopindukia katika kutambua tofauti za wanachuoni na dalili. Alikuwa ni Mujtahid asiyemfuata kipofu yeyote.

Shaykh Abu Ishaaq ash-Shiyraaziy alimtaja kuwa miongoni mwa wanachuoni wa Shaafi´iyyah.

Ametukhabarisha ´Umar bin ´Abdil-Mun´im: Ametukhabarisha al-Kindiy 608: Ametukhabarisha ´Aliy bin Hibatullaah: Ametukhabarisha Abu Ishaaq:

”Abu Bakr Muhammad bin Ibraahiym bin al-Mundhir an-Naysaabuuriy. Alikufa Makkah mwaka wa 309 au 310. Ametunga vitabu kuhusu tofauti za wanachuoni ambavyo havina mfano wake. Ambaye alikuwa akikubaliana naye na kwenda kinyume naye wote wawili walihitajia vitabu vyake. Sijui alichukua Fiqh kutoka kwa nani.”

Aliyotaja Abu Ishaaq kuhusu mwaka wake wa kufa si sahihi. Ibn ´Ammaar alikutana naye na akasikia kutoka kwake mwaka wa 316. Ibn-ul-Qattwaan al-Faasiy ameandika kwamba amefariki 318. Mwaka wa kwanza uliotajwa ni makosa.



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2t3IShD
via IFTTT

Khatari ya shirki na vigawanyo vyake



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2MIm683
via IFTTT

Kuswali juu ya mkeka Bid´ah?

Swali: Kuswali nyumbani juu ya mkeka/msala kunazingatiwa ni Bid´ah?

Jibu: Hakuhesabiki ni Bid´ah. Imepokelewa kutoka kwa Imaam Maalik ya kwamba amekataza kuswali juu ya mkeka/msala na kwamba amemuadhibu yule mwenye kufanya hivo.



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2sXglKN
via IFTTT

Yote haya ni matendo ya kufuru

Swali: Je, Raafidhwah ni makafiri na khaswakhaswa wale wenye kuwalaani Maswahabah?

Jibu: Ikiwa wanawakufurisha Maswahabah, wanawatia kwenye ufuska, wanawaabudu watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au wanasema kuwa Qur-aan haikuhifadhiwa na kwamba kumebaki tu theluthi, hii ni kufuru na kuritadi. Mwenye kuwatukana Maswahabah, akawatia kwenye ufuska au akawatukana amemkadhibisha Allaah.  Kwa sababu Allaah amewatakasa na amewafanya kuwa ni waadilifu. Kumkadhibisha Allaah ni kufuru. Kadhalika kuwaabudu watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kuritadi. Tunamuomba Allaah usalama na afya. Mfano wake ni kusema kwamba Qur-aan haikuhifadhiwa na kwamba hakukubaki isipokuwa tu theluthi. Huku pia ni kumkadhibisha Allaah. Kwani amesema:

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ

“Hakika Sisi ndio tulioteremsha Ukumbusho na hakika Sisi ndio tutaolinda.” (15:09)

Haya yote ni matendo ya kufuru.



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2HH6l2x
via IFTTT

Kitaab-ul-Buyu´ 03



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2t0A6RB
via IFTTT

Kitaab-ul-Buyu´ 02



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2HLOEyI
via IFTTT

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...