Translate

Jumatano, 11 Novemba 2020

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم

 

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

 

20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

Isti’aadhah maana yake ni kuomba kujikinga kuepukana na shari. Na Isti’aadhah kwa Allaah ni kuomba kujikinga Kwake (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na kuitakidi kuwa unabakia katika hifdhi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na inapasa kujidhalilisha Kwake na kumtegemea Yeye Pekee kuwa Ndiye Atakayekukinga na shari zinazokusudiwa kujikinga nazo. 

 

Ibnul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tambua kwamba tamshi la عاذ na yanayohusiana katika Swarf (sarufi) inamaanisha kujihifadhi na kinga na kuokoka. Na hakika maana yake ni kukimbia kitu unachokiogopa kwa ambaye atakayekuepusha nacho. Na ndio maana ikaitwa Isti’aadhah kwake kama ilivyo maana ya kimbilio.” [Badaa’i Al-Fawaaid (2426)].

 

Isti’aadhah inaweza kuwa kwa kutaja Jina Lake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama Anavyosema:

 

وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٣٦﴾

Na utakapokuchochea uchochezi kutoka kwa shaytwaan, basi omba kinga kwa Allaah. Hakika Yeye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote. [Fusw-Swilat: 36]

 

 

Kujikinga na shaytwaan ni kwa sababu shaytwaan ni adui mkubwa kabisa kwa bin-Aadam, inahitajika kujikinga naye katika kila hali kwa sababu ya ahadi yake ya kuazimia kuwapotosha wanaadamu. Ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaamrisha kujikinga naye pale anapoanza kuchochea.

 

Na katika hali ya kusoma Qur-aan pia inahitajika zaidi kujikinga naye. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameamrisha:

 

فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ﴿٩٨﴾

Unaposoma kusoma Qur-aan basi (kwanza) omba kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa. [An-Nahl: 98]

 

 

Na katika Swalaah inatakiwa kuomba kinga kutokana na shaytwaan kwa pindi anaposhawishi katika Swalaah kwa kusema:

أَعُوذُ بِاللَّه مِنْ شَرِّ خَنْزَبْ

A’uwudhu biLLaahi min sharri khanzab  

 

kama maelezo yalivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

 عن عُثْمَانَ بْن أَبِي الْعَاصِ رضي الله عنه أنه أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ الشَّيْطَانَ قَدْ حَالَ بَيْنِي وَبَيْنَ صَلَاتِي وَقِرَاءَتِي يَلْبِسُهَا عَلَيَّ: فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((ذَاكَ شَيْطَانٌ يُقَالُ لَهُ خَنْزَبٌ، فَإِذَا أَحْسَسْتَهُ فَتَعَوَّذْ بِاللَّهِ مِنْهُ وَاتْفِلْ عَلَى يَسَارِكَ ثَلَاثًا)) قَالَ: فَفَعَلْتُ ذَلِكَ فَأَذْهَبَهُ اللَّهُ عَنِّي .

‘Uthmaan bin Abiy Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba alikwenda kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika shaytwaan kanijia baina yangu na Swalaah yangu na kisomo changu akinivaa. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema ((Huyo ni shaytwaan anayeitwa Khanzab, basi ukimhisi jikinge naye kwa Allaah, na tema mate upande wa kushoto kwako  mara tatu)). Akasema: Nikafanya hivyo basi akaniondoka shaytwaan. [Muslim]

 

Isti’aadhah pia inawezekana kwa kutaja ‘Rabb’ kwa dalili ya Suwrah mbili katika Qur-aan zinajulikana kama ni Al-Mu‘awwidhataan (mbili za kujikinga)  

 

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾

Sema: “Najikinga na Rabb wa mapambazuko. [Al-Falaq: 1] mpaka mwisho wake na

 

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾

Sema: “Najikinga na Rabb wa watu. [An-Naas: 1] mpaka mwisho wake.

 

Na isti’aadhah inafaa pia kwa kutumia Sifa Zake na Utukufu Wake. Ilipoteremka Aayah:

 

قُلْ هُوَ الْقَادِرُ عَلَىٰ أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ

Sema: “Yeye ni Muweza wa kukuleteeni adhabu kutoka juu yenu, au kutoka chini ya miguu yenu,  [Al-An’aam: 65]

 

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliomba kinga akasema:

 

أَعُوذُ بِوَجْهِكُ

Najikinga kwa Wajihi Wako [Hadiyth kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia Al-Bukhaariy]

 

Na pia kwa kuunganisha Jina Lake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) pamoja Sifa Zake kama ilivyothibiti katika kinga ya pale mtu anapopata maumivu akashika sehemu inayopatikana maumivu akasema:

 

أَعُوذُ بِاللَّهِ وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ

A’uwdhu biLLaahi wa-Qudratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhiru

 

Najikinga kwa Allaah na kwa Uwezo Wake kutokana na shari ya ninachokisikia na ninachokiogopa)) [Muslim, Ibn Maajah na wengineo kwa usimulizi tofauti kidogo]

 

Pia Isti’aadhah kwa kutumia Maneno Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa dalili:

 

 أَعُوْذُ بِكَلِماتِ اللَّهِ التَّامَّتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ

A’uwdhu bi-Kalimaati-LLaahit-ttaammati min sharri maa khalaq (mara 3 jioni na asubuhi)

 

Najikinga kwa Maneno ya Allaah yaliyotimia kutokana na shari Aliyoiumba [Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ameisimulia Ahmad (2/290), An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [590], Ibn As-Sunniy [68]. Taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/187), Swahiyh Ibn Maajah (92/266), Tuhfat Al-Akhyaar (Uk. 45)   katika Swahiyh Al-Jaami’ [6427] (Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayesema mara tatu jioni hatodhuriwa na mdudu wa sumu usiku huo”] 

 

Pia; Dalili nyingi zipo katika Sunnah kuhusu kuomba kinga za kila aina;

 

-Kuomba kinga kutokana na adhabu za Allaah za duniani na Aakhirah.

 

-Kuomba kinga kutokana na adhabu za kaburi, fitnah za Masiyh Ad-Dajjaal na fitna za uhai na fitnah za mauti.

 

-Kuomba kinga  kutokana na Moto wa Jahannam.

 

-Kuomba kinga kutokana na shari za mashaytwaan na majini.

 

-Kuomba kinga kutokana na shari za adui.

 

-Kuomba kinga kutokana na maradhi.

 

-Kuomba kinga kutokana na upotofu.

 

-Kuomba kinga kutokana na ufakiri na kufru,.

 

-Kuomba kinga kutokana na shari za viungo vya mwili, na vitu vinginevyo kadhaa.

 

-Pia kuomba kinga  kutokana na hali kadhaa wa kadhaa. [Rejea Du’aa za Sunnah ya Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam]

 

Kujikinga kupitia kwa bin-Aadam inaruhusika pale inapokuwa jambo ambalo analoombwa kukinga ni katika uwezo wake kwa dalili:

 

 

عَنْ جَابِرٍ أَنَّ امْرَأَةً مِنْ بَنِي مَخْزُومٍ سَرَقَتْ فَأُتِيَ بِهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَعَاذَتْ بِأُمِّ سَلَمَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((وَاللَّهِ لَوْ كَانَتْ فَاطِمَةُ لَقَطَعْتُ)) يَدَهَا فَقُطِعَتْ

Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba mwanamke mmoja katika Baniy Makhzuwm aliiba akaletwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akajikinga kwa Ummu Salamah ambaye ni mke wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Wa-Allaahi angekuwa ni Faatwimah (aliyeiba) ningelimkata mkono wake)) Ukakatwa mkono wake. [Muslim]

 

Pia kujikinga katika mahali kadhaa:

 

عَنْ أبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((سَتَكُونُ فِتَنٌ الْقَاعِدُ فِيهَا خَيْرٌ مِنَ الْقَائِمِ، وَالْقَائِمُ خَيْرٌ مِنَ الْمَاشِي، وَالْمَاشِي فِيهَا خَيْرٌ مِنَ السَّاعِي، مَنْ تَشَرَّفَ لَهَا تَسْتَشْرِفْهُ، فَمَنْ وَجَدَ مَلْجَأً أَوْ مَعَاذًا فَلْيَعُذْ بِهِ))‏.‏

Abuu Huraryah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kutatokea fitnah ambayo mtu aliyekaa kitako atakuwa bora kuliko yule aliyesimama, na aliyesimama atakuwa bora kuliko yule anayetembea, na anayetembea humo atakuwa bora kuliko anayekimbia. Atakayajitokeza kuingia katika fitnah hizi basi zitamuangamiza. Kwa hiyo yeyote atakayepata mahali pa kujikinga au kimbilio basi ajikinge kwayo)) [Al-Bukhaariy]

 

Na pia:

 

عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ ابْنِ الْقِبْطِيَّةِ، قَالَ دَخَلَ الْحَارِثُ بْنُ أَبِي رَبِيعَةَ وَعَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَفْوَانَ وَأَنَا مَعَهُمَا، عَلَى أُمِّ سَلَمَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ فَسَأَلاَهَا عَنِ الْجَيْشِ الَّذِي يُخْسَفُ بِهِ وَكَانَ ذَلِكَ فِي أَيَّامِ ابْنِ الزُّبَيْرِ فَقَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((يَعُوذُ عَائِذٌ بِالْبَيْتِ فَيُبْعَثُ إِلَيْهِ بَعْثٌ فَإِذَا كَانُوا بِبَيْدَاءَ مِنَ الأَرْضِ خُسِفَ بِهِمْ))‏ ‏ فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ فَكَيْفَ بِمَنْ كَانَ كَارِهًا؟  قَالَ: ((يُخْسَفُ بِهِ مَعَهُمْ وَلَكِنَّهُ يُبْعَثُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَى نِيَّتِهِ)) ‏ وَقَالَ أَبُو جَعْفَرٍ هِيَ بَيْدَاءُ الْمَدِينَةِ  

‘Ubaydu-Allaah bin Al-Qitwbiyyah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Haarith bin Abiy Rabiy’ah na ‘Abdullaah bin Abiy Swafwaan pamoja nami tulikwenda kwa Mama wa Waumini Ummu Salamah wakamuuliza kuhusu jeshi ambalo litadidimizwa ardhini, na hii ni pale wakati ambapo Ibn Zubayr  (alipokuwa gavana wa Makkah).  Akahadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: ((Atatafuta mtu kinga katika Nyumba Tukufu kisha jeshi litatumwa kwake (ili wamuue) basi litakapoingia ardhi kame iliyohamwa (jangwa) litadidimizwa)) Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je itakuwaje kwa ambaye amelazimishwa hayo? Akasema: ((Atatadimizwa nao lakini atafufuliwa Siku ya Qiyaamah katika hali ya niyyah yake)) Abu Ja’far amesema: Ardhi kame ni Madiynah. [Muslim]  

 

Ama kujikinga kinyume na vile ilivyothibiti katika shariy’ah kwa kuomba kinga kwa mambo ambayo hakuna mwenye uwezo nayo isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) huwa ni shirki, kama vile walivyofanya washirikina walipokuwa wakijikinga kwa majini Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا﴿٦﴾

 “Na kwamba walikuwa wanaume miongoni mwa wana Aadam wanajikinga na wanaume miongoni mwa majini, basi wakawazidishia madhambi, uvukaji mipaka ya kuasi na khofu.” [Al-Jinn: 6]

 

 

Makosa yafanywayo na Waislamu wa sasa katika kujikinga kwa asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kufuata mila mfano;

 

-Baadhi ya watu  wanaojikinga katika kufunga ndoa kwa kumwaga damu ya mbuzi na kuikanyaga.

 

-Kuna wanaojikinga dhidi ya jicho baya au husda kwa kuvunja mayai kwenye hicho kitu alichonunua mtu kama vile gari mpya.

 

-Kuna wanaojikinga kwa mayatima kwa kuwafadhili kwa chakula kuitakidi kuwa du’aa yao inawatosheleza kujikinga.

 

-Kuna wanaojikinga na mashaytwaan wanapohamia nyumba mpya kwa kuchinja mbuzi au mialiko ya watu kusoma kisomo.

 

 

Kinga hizo zote hazijuzu bali mtu Muislamu anapaswa kutumia kinga zilizothibiti katika mafundisho Swahiyh  aliyokuja nayo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Mfano katika kuhamia nyumba mafunzo Swahiyh ni:

 

عن خَوْلَةَ بِنْت الحَكِيمِ قالت: سمعت رَسُولِ الله -صلى الله عليه وسلم -يقَولَ: ((مَنْ نَزَلَ مَنْزِلاً فقَالَ أَعُوذُ بِكلِمَاتِ الله التّامّاتِ مِن شَرّ مَا خَلَقَ لَمْ يَضُرّهُ شيءٌ حَتّى يَرْحَلَ مِنْ مَنْزِلِهِ ذَلِكَ))

Khawlat bint Hakiym amehadithia kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Atakayeteremka katika kituo (au makazi) kisha akasema: “A’uwdhu bi-Kalimaatil-LLaahit-taammati min sharri maa Khalaq - Najilinda kwa Maneno ya Allaah yaliyotimia na shari Alichokiumba” hakuna kitakachomdhuru hadi atakapoondoka katika kituo (au makazi) hicho)) [Muslim]

 

 

 

 



58-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Masiyh Dajjaal Haingii Katika Mji Wake Wa

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) 

 

58-Masiyh Dajjaal Haingii Katika Mji Wake Wa Madiynah 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Pindi atakapotokeza Masiyh Dajjaal kama ni alama mojawapo kubwa za Qiyaamah, ataenea ulimwengu mzima isipokuwa mji wa Madiynah kutokana na utukufu wa mji huu na utukufu wake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Hadiyth kadhaa zimetaja kuhusu Masiyh Dajjaal na fitnah zake miongoni mwazo ni hizi zinazotaja kutokuweza kuingia Madiynah:

 

 

 عن أَنَس بْن مَالِكٍ رضى الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ لَيْسَ مِنْ بَلَدٍ إِلاَّ سَيَطَؤُهُ الدَّجَّالُ، إِلاَّ مَكَّةَ وَالْمَدِينَةَ، لَيْسَ لَهُ مِنْ نِقَابِهَا نَقْبٌ إِلاَّ عَلَيْهِ الْمَلاَئِكَةُ صَافِّينَ، يَحْرُسُونَهَا، ثُمَّ تَرْجُفُ الْمَدِينَةُ بِأَهْلِهَا ثَلاَثَ رَجَفَاتٍ، فَيُخْرِجُ اللَّهُ كُلَّ كَافِرٍ وَمُنَافِقٍ ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه)   kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: “Hakuna mji hata mmoja ambao Dajjaal hatoingia isipokuwa Makkah na Madiynah, na hakutakuwa na njia (za Makkah na Madiynah) ila watasimama kwa safu Malaika wakiilinda dhidi yake. Kisha Madiynah itatetemeka mitetemeko mitatu pamoja na watu wake, hapo Allaah Atawatoa makafiri na wanafiki wote kwayo.”

 

 

Pia,

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم‏.‏ ‏ "‏ عَلَى أَنْقَابِ الْمَدِينَةِ مَلاَئِكَةٌ، لاَ يَدْخُلُهَا الطَّاعُونُ وَلاَ الدَّجَّالُ ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia Abu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Katika milango inayoingia Madiynah kuna Malaika wenye kulinda njia zake. Madiynah haingiwi na tauni wala Dajjaal.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Pia,

 

  عَنْ أَبِي بَكْرَةَ رضى الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ لاَ يَدْخُلُ الْمَدِينَةَ رُعْبُ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ، لَهَا يَوْمَئِذٍ سَبْعَةُ أَبْوَابٍ، عَلَى كُلِّ باب مَلَكَانِ ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia Abu Bakrah (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Madiynah haitafikiwa na khofu itakayoletwa na Al-Masiyh Dajjaal. Na wakati huo Madiynah itakuwa na milango saba, kila mlango utakuwa na Malaika wawili, wanaolinda.”

 

 

Maelezo mafupi kuhusu Masiyh Dajjaal:

 

 

Masiyh Ad-Dajjaal ni mtu miongoni mwa wana wa Aadam.  Atadhihiri duniani akiwa ni alama kubwa mojawapo za Qiyaamah. Sifa zake kadhaa zimetajwa miongoni mwazo ni kwamba atakuwa ni mtu mwenye jicho moja na baina ya macho yake kuna herufi zisizoungana za  ك ف ر  (ka fa ra)  au كافر   (kaafir) kwa herufi za kuungana. Kila Muislamu anayejua kusoma au asiyejua kusoma ataweza kusoma neno hilo.

 

 

Atakuja kuwafitinisha watu na fitnah yake itakuwa ni fitnah kubwa kabisa haijapata kutokea tangu Allaah (‘Azza wa Jalla) kumuumba Aadam kwa sababu Allaah Atamjaalia uwezo wa kufanya miujiza mikubwa ambayo itawashangaza na kuwachanganya watu wasio na iymaan. Ama Waumini hawatapotoshwa na Masiyd Dajjaal. Na ndio maana Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaifanya du’aa ya kujikinga na fitnah za Masiyh Dajjaal katika Swalaah kuwa ni jambo la muhimu mno.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 



02-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake: Mwenye Moyo Laini Si Mkali Wala Si Mjeuri

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake:

 

02-Mwenye Moyo Laini Si Mkali Wala Si Mjeuri

 

Alhidaaya.com

 

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa mpole, mwenye moyo laini wa huruma na hakuwa mkali wala mjeuri kwa Swahaba zake. Amejaaliwa kuwa hivyo kutokana na Rahmah ya Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyosema: 

 

فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ لِنتَ لَهُمْ ۖ وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوكِّلِينَ ﴿١٥٩﴾

Basi ni kwa rahmah kutoka kwa Allaah umekuwa mpole kwao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na lau ungelikuwa mjeuri mwenye moyo mgumu wangelitawanyika mbali nawe. Basi wasamehe na waombee maghfirah na washauri katika mambo. Na unapoazimia basi tawakali kwa Allaah. Hakika Allaah Anapenda wanaotawakali. [Aal-‘Imraan: 159]

 

 

Imaam Ibn Kathiyr amesema kuhusu kauli hiyo: “Yaani ungelikuwa na maneno maovu ya ujeuri, na moyo mgumu kwao basi wangelikutenga na kukukimbia, lakini Allaah (سبحانه وتعالى)  Amewaunganisha kwako na kukufanya uwe mwema na laini kwao ili mioyo yao iunganike nawe.” Na ‘Abdullaah bin ‘Amr amesema kuwa alisoma  sifa za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Vitabu (Vya Mbinguni) vilivyotangulia kwamba:  "Yeye si mjeuri,  si mwenye moyo mgumu, si  mfidhuli sokoni na halipizi maovu kwa maovu bali anasamehe na kupuuza.” 

 

 

Na ndio maana alikuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anawafanyia Swahaba zake wepesi katika mambo yao ya Dini kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

 

 عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ مَا خُيِّرَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بَيْنَ أَمْرَيْنِ أَحَدُهُمَا أَيْسَرُ مِنَ الآخَرِ إِلاَّ اخْتَارَ أَيْسَرَهُمَا مَا لَمْ يَكُنْ إِثْمًا فَإِنْ كَانَ إِثْمًا كَانَ أَبْعَدَ النَّاسِ مِنْهُ ‏.‏

 

‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema:  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakupewa khiyari ya mambo mawili ila alichagua lilokuwa wepesi kati ya hayo mawili madamu si dhambi. Na kama (hilo la wepesi lilikuwa) ni dhambi, basi alikuwa mbali mno na jambo hilo kuliko watu watu. [Muslim]

 

 

Na sifa zake na huruma zake kwa Swahaba Anazitaja Allaah (سبحانه وتعالى)  katika kauli Yake:
 

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١٢٨﴾

Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe, yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni, anakujalini, mwenye huruma kwa Waumini ni mwenye huruma mno, mwenye rahmah. [At-Tawbah: 128]

 

 



034-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Wanawake Wema Wanaotii Waume Zao Kwa Siri

 

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Fadhila Za Wanawake Wema Wanaotii Waume Zao Kwa Siri

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

 الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ ۚ وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا ﴿٣٤﴾

 

Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na pia kwa ambayo wanatoa katika mali zao. Basi wanawake wema ni wale watiifu wenye kujihifadhi katika hali ya kutokuweko waume zao kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajihifadhi. Na wale ambao mnakhofu uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni (kipigo kisichodhuru). Wakikutiini, basi msitafute njia dhidi yao (ya kuwaudhi). Hakika Allaah daima ni Mwenye Uluwa, Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa. [An-Nisaa: 34]

 

Mafunzo:

 

Kuhusu: “na wahameni katika malazi.” Imekusudiwa kutokulala nao na kutokujimai nao, kwa ujumla ni kuwagomea. Ama kuhusu: “na wapigeni.”  Imekusudiwa kipigo kidogo kisichokuwa cha kumdhuru, wala haipasi kupigwa usoni. Hadiyth imethibitisha:

 

Jaabir (رضي الله عنه) amehadithia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema katika Hijja ya kuaga: “Mcheni Allaah kuhusu wanawake kwani wao ni wasaidizi wenu. Mnayo haki juu yao kuwa wasimruhusu mtu msiyempenda kukanyaga zulia lenu (kuingia katika nyumba) Lakini wakifanya hivyo, mnaruhusiwa kuwatia adabu ndogo. Wao wana haki kwenu kwamba muwatimizie matumizi yao na nguo kwa njia ya kuridhisha.” [Muslim]

 

Fadhila za mke mwema: “Mwanamke atakaposwali Swalaah zake tano, akahifadhi sehemu zake za siri (asifanye uzinifu), akamtii mume wake, ataingia Jannah kupitia mlango wowote autakao.” [Swahiyh At-Targhiyb (1932)].

 

 



064-Asbaabun-Nuzuwl: Maryam: Na (Sisi Malaika) Hatuteremki Ila Kwa Amri Ya Rabb Wako...

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

019-Asbaab Nuzuwl Suwrah Maryam Aayah 64

 

 

 

Kauli Ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلَّا بِأَمْرِ رَبِّكَ ۖ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا وَمَا بَيْنَ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا ﴿٦٤﴾

Na (sisi Malaika) hatuteremki ila kwa amri ya Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Ni Yake Yeye yaliyoko mbele yetu, na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyoko baina ya hayo. Na Rabb wako si Mwenye kusahau kamwe. [Maryam: 64]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا خَلاَّدُ بْنُ يَحْيَى، حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ ذَرٍّ، سَمِعْتُ أَبِي يُحَدِّثُ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ـ أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏"‏ يَا جِبْرِيلُ مَا يَمْنَعُكَ أَنْ تَزُورَنَا أَكْثَرَ مِمَّا تَزُورُنَا ‏"‏‏.‏ فَنَزَلَتْ: ((‏وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلاَّ بِأَمْرِ رَبِّكَ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا))‏  إِلَى آخِرِ الآيَةِ‏.‏ قَالَ هَذَا كَانَ الْجَوَابَ لِمُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم‏.‏

Ametuhadhitia Khallaad bin Yahyaa, ametuhadithia ‘Umar bin Dharr, nimemsikia baba yangu akihadithia kutoka kwa Sa’iyd bin Jubayr kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ee Jibriyl! Nini Ni kinakuzuia kutuzuru sisi zaidi kuliko unavyotuzuru (kama kawaida yako)?” Kwa hiyo, ikataremka:

 

وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلَّا بِأَمْرِ رَبِّكَ ۖ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا  

Na (sisi Malaika) hatuteremki ila kwa amri ya Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Ni Yake Yeye yaliyoko mbele yetu, na yaliyoko nyuma yetu…

 

mpaka mwisho wa Aayah.  Akasema: Hili ndilo likawa jibu la Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) .

 

[Al-Bukhaariy - Kitaab At-Tawhiyd, Kitaab At-Tafsiyr, At-Tirmidhiy - Kitaab Tafsiyr Al-Quraan..]

 

 



058-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Ishi Duniani Kama Mgeni Au Mpita Njia

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 58

Ishi Duniani Kama Mgeni Au Mpita Njia

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ (رضي الله عنهما) قَالَ أَخَذَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِمَنْكِبِي فَقَالَ: ((كُنْ فِي الدُّنْيَا كَأَنَّكَ غَرِيبٌ أَوْ عَابِرُ سَبِيلٍ)). وَكَانَ ابْنُ عُمَرَ يَقُولُ: "إِذَا أَمْسَيْتَ فلاَ تَنْتَظِرْ الصَّبَاحَ وَإِذَا أَصْبَحْتَ فلاَ تَنْتَظِرْ الْمَسَاءَ وَخُذْ مِنْ صِحَّتِكَ لِمَرَضِكَ وَمِنْ حَيَاتِكَ لِمَوْتِكَ"  البخاري

 

 Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinikamata mabega yangu akasema: ((Kuwa duniani kama mgeni au mpita njia)). Na Ibn ‘Umar alikuwa akisema: “Utakapofika jioni usingojee asubuhi, na ukipambaukiwa usingojee jioni. Na chukua siha yako kabla ya maradhi yako, na uhai wako kabla ya kufa kwako.” [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

 

1. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kumkamata ‘Abdullaah bin ‘Umar mabegani ni dalili ya mapenzi yake kwa Maswahaba wake na pia inadhihirisha umuhimu wa jambo analotaka kumwarifu.

 

 

2. Kuishi duniani ni kama mgeni apitaye njia, kwani dunia si ya kudumu, bali Aakhirah ndio yenye maisha ya kudumu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمَا هَـٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَهْوٌ وَلَعِبٌ ۚ وَإِنَّ الدَّارَ الْآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٦٤﴾

Na huu uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni pumbao na mchezo; na hakika Nyumba ya Aakhirah bila shaka hiyo ndiyo yenye uhai wa kweli hasa (wa milele), lau wangelikuwa wanajua! [Al-‘Ankabuwt (29: 64)].

 

Na Allaah (سبحانه وتعالى) Amepiga mfano mzuri wa maisha ya dunia Anaposema:

 

 

وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ فَأَصْبَحَ هَشِيمًا تَذْرُوهُ الرِّيَاحُ ۗوَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقْتَدِرًا ﴿٤٥﴾

Na wapigie mfano wa uhai wa dunia kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, yakachanganyika kwayo mimea ya ardhi (ikasitawi), kisha yakawa makavu yaliyovurugika yanapeperushwa na pepo. Na Allaah daima juu ya kila kitu ni Mwenye Uwezo wa juu kabisa. [Al-Kahf (18: 45)]

 

 

3. Mgeni anayepita njia kuelekea aendako bila shaka amejitayarisha kubeba mahitajio yake, hali kadhalika mwana Aadam anahitaji kujibebea masurufu kuelekea safari ya Aakhirah, na masurufu bora kabisa ni taqwa.

 

Rejea: Al-Baqarah (2: 197).

 

 

4. Kukimbilia kufanya ‘amali njema na kutokufanyia usiri kwa kukhofia mauti yamfike mtu kabla ya kudiriki kutena hizo ‘amali. Mfano wa kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) na kutoa sadaka Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿٩﴾

  Enyi walioamini! Zisikupurukusheni mali zenu na wala watoto wenu mkaacha kumdhukuru Allaah. Na yeyote atakayefanya hivyo basi hao ndio waliokhasirika.

 

 

وَأَنفِقُوا مِن مَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوْلَا أَخَّرْتَنِي إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ الصَّالِحِينَ﴿١٠﴾

  Na toeni katika yale Tuliyokuruzukuni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti akasema: “Rabb wangu! Lau Ungeliniakhirisha mpaka muda wa karibu hivi, basi ningetoa swadaqah na ningelikuwa miongoni mwa Swalihina.”

 

وَلَن يُؤَخِّرَ اللَّـهُ نَفْسًا إِذَا جَاءَ أَجَلُهَا ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١١﴾

  Lakini Allaah Haiakhirishi kamwe nafsi yeyote inapokuja ajali yake na Allaah ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika kwa yale myatendayo. Al-Munaafiquwn  (63: 9-11)

 

 

Rejea pia: Ibraahiym (14: 31), Al-Baqarah (2: 254).

 

 

5. Siha na uhai ni neema mbili kwa Muumin apasazo kuzitumia kwa kutenda mema yatakayomfaa Aakhirah.

 

Rejea Hadiyth namba (9).

 

 

6. Hili ni fundisho kuwa tusikae duniani kama kwamba tutaishi milele.

 

 

7. Haifai kwa Muislamu kuifadhilisha dunia juu ya Aakhirah yake.

 

Rejea Hadiyth namba (57), (59), (60), (62).

 

 

8. Umuhimu wa kuutumia muda wako vyema hapa duniani.

 

 

 



Alhamisi, 5 Novemba 2020

19-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Istighaathah Kwa Asiyekuwa Allaah

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم

 

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

 

19 - Istighaathah (Kuomba Uokozi) Kwa Asiyekuwa Allaah

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

Maana Ya Istighaathah na dalili zake:

 

Istighaathah maana yake ni kuomba uokozi kwa ambaye ataweza kuokoa kutokana na hali ya shida, dhiki na kukaribia kudhurika au kuangamia. Na istighaathah kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) inajumuisha kujidhalilisha Kwake na kuitakidi kwamba hakuna mwengine atakayeweza kuokoa isipokuwa Yeye, kama vile hali ilivyokuwa katika vita vya Badr, Ibn Kathiyr amesema:

 

 

"Ilipokuwa siku ya Badr na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaona uchache wa Maswahaba wake na wingi wa adui zake, wakawa katika shida na khofu, akaelekea Qiblah na kuomba uokovu na akaendelea kumuomba Mola wake mpaka joho lake likamuanguka begani mwake, Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Akateremsha:

 

إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ

Na pindi mlipomuomba uokovu Rabb wenu Naye Akakuitikieni  [Al-Anfaal: 9] [mpaka mwisho wa Aayah 13 Suwrat Al-Anfaal]

 

 

Kuomba uokovu kwa bin-Aadam kwa jambo ambalo limo katika uwezo wake inafaa kwa dalili kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu kisa cha Nabiy Muwsaa (‘Alayhis-Salaam):

 

وَدَخَلَ الْمَدِينَةَ عَلَىٰ حِينِ غَفْلَةٍ مِّنْ أَهْلِهَا فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَـٰذَا مِن شِيعَتِهِ وَهَـٰذَا مِنْ عَدُوِّهِ ۖ فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ

Na akaingia mjini wakati watu wake wako katika mighafiliko, akakuta humo watu wawili wanapigana; mmoja ni miongoni mwa kundi lake, na mwengine miongoni mwa adui wake. Akamsaidia kumuokoa yule ambaye katika kundi lake dhidi ya yule ambaye ni katika adui wake… [Al-Qaswasw: 15]

 

Pia, mtu anaweza kuomba uokovu kwa mwenziwe amuokoe kutokana na adui zake katika hali ya vita n.k. Au mfano mtu anapokuwa katika hali ya kukaribia kuzama baharini akaita: “Ee ndugu! Nazama niokoe!”

 

Ama kuomba uokovu kwa jambo ambalo halimo katika uwezo wa bin-Aadam, hapo huwa ni shirki. Mfano mtu kumuomba mwenziwe:

 

“Ee fulani! Nisaidie kuniokoa na Moto wa Jahannam na niingize Jannah!”

 

“Ee Fulani! Nisaidie kuniokoa katika upotofu unijaalie hidaaya!”

 

Au kuomba walio kaburini:

 

“Ee walii wangu, au shekhe wangu!

 

Au sharifu fulani! Nisaidie kuniokoka na adhabu za kaburi! Nisaidie kuniokoa katika maradhi niliyo nayo!”

 

Kadhaalika, kuomba uokovu kwa mizimwi, mashaytwaan n.k. kuitakidi kuwa wao wana uwezo wa kuokoa katika hali ambazo hakuna mwenye uwezo isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). 

 

Vilevile kuomba uokovu kwa kumchanganya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihu wa sallam) kwa mfano: kusema  "Ee Allaah  niokoe mie katika hizi dhiki kwa baraka Zako na baraka za Rasuli Wako."

 

Hivyo ni shirki kubwa na inamtoa mtu nje ya Uislamu.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwamba hao wanaoombwa uokovu n.k. hawawezi wenyewe kujinusuru nafsi zao humo walimo makaburini wala Siku ya Qiyaamah hawatokuwa na uwezo wowote ule!

يَوْمَ لَا يُغْنِي مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ﴿٤١﴾

Siku ambayo jamaa wa karibu hatomfaa jamaa wa karibu chochote, na wala wao hawatonusuriwa. [Ad-Dukhaan: 41]

  

Hata Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa na uwezo wa kumuokoa mtu kwa dalili kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema katika Aayah kadhaa kwamba yule Ambaye Ameshamhukumu kuwa ni mpotofu, basi hakuna wa kumhidi:

 

مَن يَهْدِ اللَّـهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُ وَلِيًّا مُّرْشِدًا ﴿١٧﴾

Ambaye Allaah Amemwongoza, basi yeye ndiye aliyehidika. Na Anayemwacha kupotoka basi hutompatia mlinzi wa kumuongoza. [Al-Kahf: 17]

 

Au ambaye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amemhukumu kuwa ni mtu wa Motoni, basi hakuna wa kumuokoka, Akamwambia Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

أَفَمَنْ حَقَّ عَلَيْهِ كَلِمَةُ الْعَذَابِ أَفَأَنتَ تُنقِذُ مَن فِي النَّارِ ﴿١٩﴾

Je, yule iliyemthibitikia neno la adhabu je, basi wewe utaweza kumuokoa aliyemo katika moto? [Az-Zumar: 19]

 

 

Alikuweko mnafiki mmoja akiwaudhi Waumini ikahadithiwa:

 

عن عُبَادَةَ بْنَ الصَّامِتِ (رضي الله عنه) قال: خَرَجَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ): قُومُوا نَسْتَغِيثُ بِرَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) مِنْ هَذَا الْمُنَافِقِ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ:  ((أنه لاَ يُسْتَغَاث بِي، وَإِنَّمَا يُسْتَغَاثُ باِلله))

Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitujia kisha Abu Bakr akasema: Simameni tutake msaada kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atuokoe na mnafiki huyu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hakika haipasi kuombwa uokovu kwangu, bali inapaswa kuombwa uokovu kwa Allaah)) [At-Twabaraaniy fiy Mu’jamil–Kabiyr]  

 

Pia Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba ilipoteremshwa kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ ﴿٢١٤﴾

Na onya (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) jamaa zako wa karibu. [Ash-Shu’araa: 214]

 

 

دَعَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قُرَيْشًا فَاجْتَمَعُوا فَعَمَّ وَخَصَّ فَقَالَ: ((يَا بَنِي كَعْبِ بْنِ لُؤَيٍّ، أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ، يَا بَنِي مُرَّةَ بنِ كَعْبٍ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ، يَا بَنِي عَبْدِ شَمْسٍ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ،يَا بَنِي عَبْدِ مَنَافٍ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ، يَا بَنِي هَاشِمٍ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ ، يَا بَنِي عَبْدِ الْمُطَّلِبِ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ، يَا فَاطِمَةُ أَنْقِذِي نَفْسَكِ مِنْ النَّارِ، فَإِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ مِنْ اللَّهِ شَيْئًا غَيْرَ أَنَّ لَكُمْ رَحِمًا سَأَبُلُّهَا بِبَلَالِهَا))

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaita Maquraysh akawaonya kwa ujumla kisha makhsusi (kwa kabila fulani) akasema:  ((Ee Baniy Ka’ab bin Luayy, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto!  Ee Baniy Murrah bin Ka’b, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto! Ee Baniy ‘Abdi Shams, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto. Ee Baniy ‘Abdi Manaaf, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto.” Ee Baniy Haashim, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto.” Ee Baniy ‘Abdil-Muttwalib, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto.” Yaa Faatwimah, okoa nafsi yako kutokana na Moto! Kwani hakika mimi similiki uwezo wowote kwenu isipokuwa nitaendelea kuweka uhusiano wetu wa damu.)) [Muslim]

 

Anatahadharisha pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika kauli Zake mbali mbali:

 

وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَكُمْ وَلَا أَنفُسَهُمْ يَنصُرُونَ﴿١٩٧﴾

Na wale mnaowaomba (na kuwaabudu) badala ya Allaah hawawezi kuwanusuru na wala hawawezi kujinusuru nafsi zao. [Al-A’raaf: 197]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 أَمْ لَهُمْ آلِهَةٌ تَمْنَعُهُم مِّن دُونِنَا ۚ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَ أَنفُسِهِمْ وَلَا هُم مِّنَّا يُصْحَبُونَ ﴿٤٣﴾

Je, kwani wana waabudiwa wanaoweza kuwakinga Nasi?  Hawawezi kujinusuru nafsi zao na wala hawatolindwa Nasi. [Al-Anbiyaa: 43]

 

Na pia Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَاتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ آلِهَةً لَّعَلَّهُمْ يُنصَرُونَ ﴿٧٤﴾

Na wamejichukulia badala ya Allaah waabudiwa ili wakitumaini kuwa watawanusuru!

 

لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَهُمْ وَهُمْ لَهُمْ جُندٌ مُّحْضَرُونَ ﴿٧٥﴾

Hawawezi kuwanusuru, na watahudhurishwa (adhabuni) kama askari dhidi ya hao (waliowaabudu). [Yaasiyn: 74-75]

 

 

 



57-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Dini Yake Ndio Itakayoshinda Dini Zote

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

57-Dini Yake Ndio Itakayoshinda Dini Zote

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا﴿٢٨﴾

Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad  (صلى الله عليه وآله وسلم kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote. Na Allaah Anatosha kuwa ni Shahidi. [Al-Fat-h:28]

 

Qiyaamah hakitasimama hadi Dini ya Kiislaam ishinde Dini zote, na hii imeshaanza kudhihirika ulimwenguni kutokana na matukio kadhaa yaliyosababisha watu wengi kuingia katika Uislaam. 

 

Na katika Dalili kumi kubwa za kusimama Qiyaamah zipo Hadiyth kadhaa zinazoelezea hayo mojawapo ifuatayo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَة قَالَ : قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ  ((يَنْزِل عِيسَى اِبْن مَرْيَم فَيَقْتُل الْخِنْزِير وَيَمْحُو الصَّلِيب وَتُجْمَع لَهُ الصَّلَاة وَيُعْطِي الْمَال حَتَّى لَا يُقْبَل وَيَضَع الْخَرَاج وَيَنْزِل الرَّوْحَاء فَيَحُجّ مِنْهَا أَوْ يَعْتَمِر أَوْ يَجْمَعهُمَا))  أحمد

Kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)    amesema: ((‘Iysaa mwana wa Maryam atateremka na kuua nguruwe, atavunja misalaba, ataimamisha watu katika Swalaah ya Jamaa, na kutoa mali hadi hakuna atakayetaka kupokea tena. Ataondosha jizya (kodi) na atakwenda Ar-Rawhaa ambako ataelekea kutekeleza Hajj, ‘Umrah au zote mbili)) [Ahmad]

 

Imaam Atw-Twabariy amesema  kuhusu kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ ۚ

 

Ili Aishindishe juu ya dini zote.

 

“Hivyo ni kubatilisha millah (dini) zote hadi kwamba hakutakuwa na Dini nyingine isipokuwa hiyo, na hivyo ndivyo ilivyokuwa mpaka ‘Iysaa mwana wa Maryam ashuke na kumuua Ad-Dajaal, hapo Dini zote zitabatilishwa isipokuwa Dini ya Allaah aliyomtuma nayo Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)   na Uislaam ushinde juu ya dini zote."

 

 

Na Hadiyth nyenginezo zifuatazo:   

 

 عَنْ تَمِيمٍ الدَّارِيِّ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَيَبْلُغَنَّ هَذَا الْأَمْرُ مَا بَلَغَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَلَا يَتْرُكُ اللَّهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ هَذَا الدِّينَ بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ بِذُلِّ ذَلِيلٍ عِزًّا يُعِزُّ اللَّهُ بِهِ الْإِسْلَامَ وَذُلًّا يُذِلُّ اللَّهُ بِهِ الْكُفْرَ

Tamiym Ad-Daariyy amesimulia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   amesema: “Jambo hili (Uislaam) hakika litafika kila mahali palipoguswa na usiku na mchana. Allaah Hatoacha  nyumba au makazi isipokuwa Allaah Ataingizi Dini hii kwa ‘izza (utukufu) ambao watukufu watajaaliwa taadhima na wadhalili watadhalilika. Allaah Atawapa utukufu watukufu kwa Uislaam na Atawadhalilisha wadhalili kwa Ukafiri. [Ahmad]       

 

Na pia,

 

عَن الْمِقْدَاد بن الْأسود قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: " يَقُولُ لَا يَبْقَى عَلَى ظَهْرِ الْأَرْضِ بَيْتُ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ كلمة الاسلام بعز عَزِيز أَو ذل ذليل إِمَّا يعزهم الله عز وَجل فَيَجْعَلُهُمْ مِنْ أَهْلِهَا أَوْ يُذِلُّهُمْ فَيَدِينُونَ لَهَا  رَوَاهُ أَحْمد

Miqdaad bin Al-Aswad amesimulia: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akisema: “Haitasalia juu ya ardhi (duniani) nyumba ya udongo wala  hema la nywele za ngamia isipokuwa Allaah Ataingiza humo neno la Islaam kwa ‘izza (utukufu) ambao watukufu watajaaliwa taadhima na wadhalili watadhalilika ima Allaah  (‘Azza wa Jalla)  Awape utukufu wakazi na kuwajaalia wawe katika watu Wake, au Awadhalilishe na wawe duni mbele Yake.”  [Ahmad, Swahiyh Ibn Maajah (6701)]

 

 

Na Kauli Zake nyenginezo Allaah (سبحانه وتعالى):

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٩﴾

Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina. [Asw-Swaff: 9]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٣٣﴾

Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina. [At-Tawbah: 33]

 

 

 



01-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake: Hakumtaka Jibriyl Awaangamize Makafiri Waliomfukuza Na Kumtesa

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake:

 

01-Hakumtaka Jibriyl Awaangamize Makafiri Waliomfukuza Na Kumtesa

 

Alhidaaya.com

 

 

Pindi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alporudi kutoka Twaaif ambako wakaazi wake hawakumpokea kwa wema bali walimfukuza na kumtesa; waliwatuma watoto wadogo na wendawazimu na watumwa wao wamfukuze. Wakawa wanamuandama huku wakimtukana na kumpiga mawe mpaka damu ikaanza kumtoka Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na viatu vyake vikarowa damu. Alipokuwa anarudi kuelekea Makkah katika eneo la Qarn Al-Manaazil, Jibriyl pamoja na Malaika wa majabali wakamuuliza iwapo anataka yaangushwe majabali mawili na kuwaangamiza watu wa Makkah, lakini Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikataa kutokana na huruma zake. Maelezo kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

 عن عَائِشَةَ ـ رضى الله عنها ـ زَوْجَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم حَدَّثَتْهُ أَنَّهَا قَالَتْ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم هَلْ أَتَى عَلَيْكَ يَوْمٌ كَانَ أَشَدَّ مِنْ يَوْمِ أُحُدٍ قَالَ ‏ "‏ لَقَدْ لَقِيتُ مِنْ قَوْمِكِ مَا لَقِيتُ، وَكَانَ أَشَدُّ مَا لَقِيتُ مِنْهُمْ يَوْمَ الْعَقَبَةِ، إِذْ عَرَضْتُ نَفْسِي عَلَى ابْنِ عَبْدِ يَالِيلَ بْنِ عَبْدِ كُلاَلٍ، فَلَمْ يُجِبْنِي إِلَى مَا أَرَدْتُ، فَانْطَلَقْتُ وَأَنَا مَهْمُومٌ عَلَى وَجْهِي، فَلَمْ أَسْتَفِقْ إِلاَّ وَأَنَا بِقَرْنِ الثَّعَالِبِ، فَرَفَعْتُ رَأْسِي، فَإِذَا أَنَا بِسَحَابَةٍ قَدْ أَظَلَّتْنِي، فَنَظَرْتُ فَإِذَا فِيهَا جِبْرِيلُ فَنَادَانِي فَقَالَ إِنَّ اللَّهَ قَدْ سَمِعَ قَوْلَ قَوْمِكَ لَكَ وَمَا رَدُّوا عَلَيْكَ، وَقَدْ بَعَثَ إِلَيْكَ مَلَكَ الْجِبَالِ لِتَأْمُرَهُ بِمَا شِئْتَ فِيهِمْ، فَنَادَانِي مَلَكُ الْجِبَالِ، فَسَلَّمَ عَلَىَّ ثُمَّ قَالَ يَا مُحَمَّدُ، فَقَالَ ذَلِكَ فِيمَا شِئْتَ، إِنْ شِئْتَ أَنْ أُطْبِقَ عَلَيْهِمِ الأَخْشَبَيْنِ، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بَلْ أَرْجُو أَنْ يُخْرِجَ اللَّهُ مِنْ أَصْلاَبِهِمْ مَنْ يَعْبُدُ اللَّهَ وَحْدَهُ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia ‘Aaishah   Mke wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):  Hivi imekupitia siku iliyo ngumu zaidi ya siku ya Uhud? Akasema: “Nimepata mateso niliyo yapata kutoka kwa jamaa zako, na mateso zaidi niliyoyapata kwao ni siku ya ‘Aqabah, pale nilipojipeleka mwenyewe kwa Ibn ‘Abd Yaaliyl ibn ‘Abd Kulaal. Hakunikubalia nilicho kitaka. Nikaondoka sielewi niendako, sikuzinduka isipokuwa nilipokaribia Qarnith Ath-Tha‘alib, nikainua kichwa change nikaliona wingu limenifunika, nikaangalia nikamkuta humo Jibriyl, akaniita akasema: ‘Hakika Allaah Ameisikia kauli ya watu wako kwako na jibu walilokupa, na Amekuletea Malaika wa milima ili umuamuru unachotaka katika adhabu kuwafikia jamaa zako’. Akaniita Malaika wa milima, akanisalimia, kisha akasema: ‘Ee Muhammad!’ Akasema: ‘Ikiwa ni katika unachokitaka niwafunike kwa milima miwili’. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Bali nataraji Allaah atawatoa migongoni mwao watakao mwabudu Allaah Peke Yake, hawamshirikishi na chochote.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 



031-Aayah Na Mafunzo: Maana Ya Al-Kabaair (Dhambi Kubwa) Na Mifano Yake

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Maana Ya Al-Kabaair Dhambi Kubwa Na Mifano Yake

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا ﴿٣١﴾

Mkijiepusha na madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu. [An-Nisaa: 31]

 

Mafunzo:

 

Al-Kabaair (dhambi kubwa): ni lile lililotajiwa ndani yake laana, au haddi (adhabu) hapa duniani, au limeahidiwa juu yake ghadhabu za Allaah au moto.

 

Na Nafiy’ bin Al-Haarith Ath-Thaqafiy Abuu Bakr (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Je, nikujulisheni Al-Kabaair?” Tukasema: “Ndio ee Rasuli wa Allaah! Akasema: “Kumshirikisha Allaah, na kuwaasi wazazi wawili.” Alikuwa ameegemea, akakaa kitako akasema: “Tanabahi! Na kusema uongo na kushuhudia uongo!” “Tanabahi! Na kusema uongo na kushuhudia uongo!” Akaendelea kusema hayo mpaka nikadhani hatonyamaza. [Al-Bukhaariy (5976)].

 

Bonyeza kiungo kifuatacho kwa faida zaidi:

 

Madhambi Makubwa Na Madogo

 

 

 

 

 



110-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Israa: Sema; Muiteni Allaah Au Muiteni Ar-Rahmaan, Vyovyote Mtakavyomwita...

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

017-Asbaab Nuzuwl Suwrah al-Israa Aayah 110

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ﴿١١٠﴾

Sema; Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa. Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya, bali shika njia ya wastani baina yake. [Al-Israa: 110]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، عَنْ هُشَيْمٍ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ((‏وَلاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا‏))‏ قَالَ أُنْزِلَتْ وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مُتَوَارٍ بِمَكَّةَ، فَكَانَ إِذَا رَفَعَ صَوْتَهُ سَمِعَ الْمُشْرِكُونَ فَسَبُّوا الْقُرْآنَ وَمَنْ أَنْزَلَهُ وَمَنْ جَاءَ بِهِ‏.‏ وَقَالَ اللَّهُ تَعَالَى: ((‏وَلاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا‏))‏ لاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ حَتَّى يَسْمَعَ الْمُشْرِكُونَ، وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا عَنْ أَصْحَابِكَ فَلاَ تُسْمِعُهُمْ: ((‏وَابْتَغِ بَيْنَ ذَلِكَ سَبِيلاً‏))‏ أَسْمِعْهُمْ وَلاَ تَجْهَرْ حَتَّى يَأْخُذُوا عَنْكَ الْقُرْآنَ‏.‏  البخاري

 

Ametuhadithia Musaddad kutoka kwa Hushaym kutoka kwa Abuu Bishr, kutoka kwa Sa’iyd bin Jubayr kutoka kwa Ibn ‘Abaas (رضي الله عنهما) kuhusu Kauli ya Allaah (عز وجل):

  

وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا

Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya…

 

Amesema: “Aayah hii iliteremshwa ilhali Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amejificha Makkah. Alikuwa akiipandisha sauti yake katika kusoma Qur-aan, walipomsikia washirikina, wakaitukana Qur-aan na wakamtukana Aliyeiteremsha na aliyeileta. Basi Allaah (عز وجل) Akasema:

 

وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا

Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya…

 

 

Yaani: Usiisome kwa sauti kubwa hadi kwamba washirikiana wakusikie (kisha waitukane). 

 

 

وَلَا تُخَافِتْ بِهَا  

na wala usiifiche kimya kimya

 

Yaani: Usiisome kimya kimya hadi kwamba Swahaba zako wasiisikie unapowasomea washindwe kujifunza kwayo,

 

  وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا  

bali shika njia ya wastani baina yake.

 

Yaani: Wasikilizishe (Swahaba) kiasi cha kuisikia kwao.

 

[Al-Bukhaariy Kitaab At-Tawhiyd]  

 

 

Pia,

 

عَنْ عَائِشَةَ ـ رضى الله عنها ـ قَالَتْ نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ ‏‏وَلاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا‏ فِي الدُّعَاءِ‏.‏ 

 

Kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba Iliteremka Aayah hii:

 

وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا  

Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya...

 

Kasema: “Inahusiana na Du’aa.”

 

[Al-Bukhaariy - Kitaab At-Tawhiyd, Kitaab At-Tafsiyr, na Muslim – Kitaab Asw-Swalaah]

 

 

 



20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...