Aayah Na Mafunzo
Aal-‘Imraan
Fadhila Za Ummah Wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)
Anasema Allaah ('Azza wa Jalla):
كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾
110. Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Ahlul-Kitaabi ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wanaoamini na wengi wao ni mafasiki.
Mafunzo:
Hadiyth kadhaa zimetajwa fadhila za Ummah huu wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi yake ni:
Mu’aawiyah bin Haydah Al-Qash-riyy (رضي الله عنه) amehadithia kutoka kwa baba yake kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nyinyi mnakamilisha Ummah sabini. Nyinyi ndio mbora wao na ndio watukufu zaidi mbele ya Allaah (عزّ وجلّ).” [Ahmad, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Al-Haakim, na wengineo kwa riwaayah tofauti kidogo taz. Swahiyh Al-Jaami’ (2301), Swahiyh At-Tirmidhiy (3001)].
Pia rejea tanbihi (2: 213).
Na pia, Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Sisi (Waislamu) ni wa mwisho (kuja) na (tutakuwa) wa mwisho Siku ya Qiyaamah na wa mwanzo kuingia Jannah…” [Al-Bukhaariy na Muslim].
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni