Translate

Alhamisi, 24 Oktoba 2019

009-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tawbah: Aayah 19

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

009-Suwrah At-Tawbah: Aayah Na Namba 19

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ الْحَاجِّ وَعِمَارَةَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ كَمَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَجَاهَدَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ لَا يَسْتَوُونَ عِندَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿١٩﴾

Je, mmefanya kunywesha maji Hujaji na kuamirisha Al-Masjid Al-Haraam kama sawasawa na (‘amali za) anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na akafanya jihaad katika njia ya Allaah? (Hapana!) Hawawi sawa mbele ya Allaah. Na Allaah Haongoi watu madhalimu. [At-Tawbah: 9]

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

 

دَّثَنِي حَسَنُ بْنُ عَلِيٍّ الْحُلْوَانِيُّ، حَدَّثَنَا أَبُو تَوْبَةَ، حَدَّثَنَا مُعَاوِيَةُ بْنُ سَلاَّمٍ، عَنْ زَيْدِ بْنِ سَلاَّمٍ، أَنَّهُ سَمِعَ أَبَا سَلاَّمٍ، قَالَ حَدَّثَنِي النُّعْمَانُ بْنُ بَشِيرٍ، قَالَ كُنْتُ عِنْدَ مِنْبَرِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ رَجُلٌ مَا أُبَالِي أَنْ لاَ أَعْمَلَ عَمَلاً بَعْدَ الإِسْلاَمِ إِلاَّ أَنْ أُسْقِيَ الْحَاجَّ ‏.‏ وَقَالَ آخَرُ مَا أُبَالِي أَنْ لاَ أَعْمَلَ عَمَلاً بَعْدَ الإِسْلاَمِ إِلاَّ أَنْ أَعْمُرَ الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ ‏.‏ وَقَالَ آخَرُ الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَفْضَلُ مِمَّا قُلْتُمْ ‏.‏ فَزَجَرَهُمْ عُمَرُ وَقَالَ لاَ تَرْفَعُوا أَصْوَاتَكُمْ عِنْدَ مِنْبَرِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يَوْمُ الْجُمُعَةِ وَلَكِنْ إِذَا صَلَّيْتُ الْجُمُعَةَ دَخَلْتُ فَاسْتَفْتَيْتُهُ فِيمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ ‏.‏ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: ((أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ الْحَاجِّ وَعِمَارَةَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ كَمَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الآخِر))‏ الآيَةَ إِلَى آخِرِهَا ‏.

Amenihadithia Hasan bin Áliy Al-Hulwaaniy, ametuhadithia Abuu Tawbah, ametuhadithia Mu’aawiyah bin Sallaam, toka kwa Zayd bin Sallaam kwamba amemsikia Abuu Sallaam, amesema: Amenihadithia An-Nu’maan bin Bashiyr, amesema: Nilikuwa karibu na mimbari ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  na mtu mmoja akasema: “Mimi sijali nisifanye amali yoyote baada ya Uislamu zaidi ya kuwanywesha maji Hujjaaj.” Mwingine akasema: “Mimi sijali nisifanye amali yoyote baada ya Uislamu zaidi ya kuamirisha Al-Masjid Al-Haraam”. Mwingine akasema: “Jihaad katika Njia ya Allaah ni bora zaidi kuliko mliyoyasema”. ‘Umar akawakataza na kuwaambia: “Msipaze sauti zenu katika mimbari ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  nayo ni Siku ya Ijumaa, nami nikishaswali Ijumaa nitaingia nimuulize mliyobishania.” Hapo Allaah (عزّ وجلّ)  Akateremsha:

 

 أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ الْحَاجِّ وَعِمَارَةَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ كَمَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَجَاهَدَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ لَا يَسْتَوُونَ عِندَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿١٩﴾

19. Je, mmefanya kunywesha maji Hujaji na kuamirisha Al-Masjid Al-Haraam kama sawasawa na (‘amali za) anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na akafanya jihaad katika njia ya Allaah? (Hapana!) Hawawi sawa mbele ya Allaah. Na Allaah Haongoi watu madhalimu.

[Muslim Kitaab Al-Imaarah]

 

 



037-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Mwenye Iymaan Kweli Amkirimu Mgeni, Na Aseme Ya Kheri Au Anyamaze

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 37

 

Mwenye Iymaan Kweli Amkirimu Mgeni, Na Aseme Ya Kheri Au Anyamaze

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ أَبِي شُرَيْحٍ الْخُزَاعِيِّ (رضي الله عنه) أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الأَخِرِ فَلْيُحْسِنْ إِلَى جَارِهِ،  وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الأَخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ،  وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الأَخِرِ فَلْيَقُلْ خَيْرًا أَوْ لِيَسْكُتْ)) مسلم وروي البخاري بعضه

Imepokelewa kutoka kwa Abu Shurayh Al-Khuzaa’iyy( (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, basi amfanyie wema jirani yake, na anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho,  basi amkirimu mgeni wake, na anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, basi azungumze kheri au anyamaze)) [Muslim na amepokea Al-Bukhaariy baadhi yake]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Kumkirimu mgeni na kutokusema maovu ni mojawapo wa uthibitisho wa kumwamini Allaah (سبحانه وتعالى)  na Siku ya Mwisho. Rejea Hadiyth namba (36).

 

 

2. Ukarimu ni miongoni mwa tabia njema za Muumin na sababu ya kuingia Jannah.

 

3. Umuhimu wa kuchunga na kuzuia ulimi usiseme maneno ya upuuzi, kwani kila linalotamkwa linaandikwa na litaulizwa. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ﴿١٧﴾

Pale wanapopokea wapokeaji wawili (Malaika) wanaokaa kuliani na kushotoni. 

 

 

مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴿١٨﴾

Hatamki kauli yeyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha (kurekodi). [Qaaf: 17-18]

 

Hadiyth: ((Kwa hakika mja atazungumza neno ambalo halizingatii [kuwa ni la kheri au la shari] ateleze nalo motoni umbali zaidi ya umbali ulioko baina ya Mashariki na Magharibi)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Rejea Hadiyth namba (86), (87), (93), (94),

 

4. Ulimi unaonena maovu unasababisha kila aina ya shari, kwa mgeni, jirani na jamii nzima kwa ujumla. Na Allaah (سبحانه وتعالى)  Anaamrisha kusema na watu yaliyo mema:

 

  وَقُولُوا لِلنَّاسِ حُسْنًا

Na semeni na watu kwa uzuri  [Al-Baqarah: (2: 83)]

 

 

5. Inapendekeza kukaa kimya panapokuwa hakuna faida ya kusema jambo na hiyo ni sifa mojawapo miongoni mwa sifa zitakazompatia Muislamu Jannah ya Al-Firdaws kwani hivyo ni kujiepusha na porojo na upuuzi. [Al-Muuminuwn: (23: 3]

 

Rejea pia Al-Furqaan (25: 72)

 



118-Aayah Na Mafunzo: Kila Nabiy Au Khaliyfah Alikuwa Na Rafiki Mwandani Wawili

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Kila Nabiy Au Khaliyfah Alikuwa Na Rafiki Mwandani Wawili 

Alhidaaya.com

 

 

 Anasema Allaah ('Azza wa Jalla):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١١٨﴾

118. Enyi walioamini! Msifanye rafiki mwandani na msiri (wenu) wasiokuwa nyinyi. Hawatoacha kukuharibieni. Wanatamani kama mngetaabika. Imekwishajitokeza bughudha kutoka midomoni mwao. Na yale yanayoficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Aayaat, (ishara, hoja, dalili) mkiwa mtatia akilini.

 

Mafunzo:

 

Abuu Sa’iyd (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah Hakutuma Nabiy yeyote wala hakumweka Khaliyfah yeyote isipokuwa alikuwa na rafiki mwandani wawili; mmoja anayeamrisha ya kheri na kumsisitiza nayo, na mwengine akiamrisha maovu na kumchochea nayo. Na Al-Ma’swuwm (aliyehifahdiwa asikosee) ni ambaye ma’swuwm (amehifadhiwa asisokee) na Allaah.” [Al-Bukhaariy na An-Nasaaiy].



37-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake: Akimpandisha Kwanza Swahaba Wake Kabla Yake Katika Kipando

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

37-Unyenyekevu Wake Akimpandisha Kwanza Swahaba Wake Kabla Yake Katika Kipando

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

 عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ جَعْفَرٍ قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَدِمَ مِنْ سَفَرٍ تُلُقِّيَ بِصِبْيَانِ أَهْلِ بَيْتِهِ قَالَ: وَإِنَّهُ قَدِمَ مِنْ سَفَرٍ فَسُبِقَ بِي إِلَيْهِ فَحَمَلَنِي بَيْنَ يَدَيْهِ ثُمَّ جِيءَ بِأَحَدِ ابْنَيْ فَاطِمَةَ فَأَرْدَفَهُ خَلْفَهُ قَالَ: فَأُدْخِلْنَا الْمَدِينَةَ ثَلَاثَةً عَلَى دَابَّةٍ  

 ‘Abdullaah bin Ja’far (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa pindi anaporudi safarini, watoto katika ahli yake walikuwa wakija kumpokea na kumkaribisha. Safari moja  ikawa katika hali kama hii, pindi aliporudi safarini ikawa nimemwendea mimi kwanza kabla ya mtu mwengine. Akanipandisha (katika mnyama) mimi kabla yake. Kisha akaja mmojawapo wa watoto wawili wa Faatwimah akampandisha nyuma yake ikawa hivi ndivyo sisi watatu tulivyoingia Madiynah huku tumepanda mnayma.”  [Muslim]

 

 



37-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amefutiwa Madhambi Yake Yote Yaliyotangulia Na Ya Yaliyo Mbele Yake

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

37-Amefutiwa Madhambi Yake Yote Yaliyotangulia Na Ya Yaliyo Mbele Yake

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (عزّ وجلّ):

 

 إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا ﴿١﴾ لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَيَهْدِيَكَ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا ﴿٢﴾

Hakika Tumekupa ushindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم ambao ni) ushindi wa dhahiri. Ili Allaah Akughufurie yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayokuja; na Akutimizie neema Yake juu yako na Akuongoze njia iliyonyooka. [Al-Fat-h: 1-2]

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akafurahi mno kuteremshiwa kwake Aayah hiyo kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

 

عَنْ أَنَسٍ، رضى الله عنه قَالَ أُنْزِلَتْ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلمَ ‏:‏ ‏((ليغْفِرَ لَكَ اللَّهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّر))َ  مَرْجِعَهُ مِنَ الْحُدَيْبِيَةِ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ لَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَىَّ آيَةٌ أَحَبُّ إِلَىَّ مِمَّا عَلَى الأَرْضِ ثُمَّ قَرَأَهَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَيْهِمْ فَقَالُوا هَنِيئًا مَرِيئًا يَا نَبِيَّ اللَّهِ قَدْ بَيَّنَ اللَّهُ لَكَ مَاذَا يُفْعَلُ بِكَ فَمَاذَا يُفْعَلُ بِنَا فَنَزَلَتْ عَلَيْهِ: ((ليُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الأَنْهَارُ))  حَتَّى بَلَغَ ‏:‏ ‏((‏فوزًا عَظِيمًا ))‏  قَالَ هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ  ‏.‏

 

Anas bin Maalik amehadithia kwamba: Tulipokuwa tunarudi kutoka Hudaybiyyah, iliteremshwa kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

 

لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَيَهْدِيَكَ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا﴿٢﴾

Ili Allaah Akughufurie yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayofuatia; na Akutimizie neema Yake juu yako na Akuongoze njia iliyonyooka.

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika nimeteremshiwa Aayah ambayo ni kipenzi mno kuliko chochote kilichoko duniani.” Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawasomea Aayah hiyo, wakasema: Hongera kwako ee Nabiy wa Allaah, hakika Allaah Amekubainishia Atakalokufanyia, lakini je Atatufanyia nini sisi? Hapo ikateremshwa: 

 

لِّيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عِندَ اللَّـهِ فَوْزًا عَظِيمًا﴿٥﴾

Ili Awaingize Waumini wa kiume na Waumini wa kike Jannaat zipitazao chini yake mito, ni wenye kudumu humo, na Awafutie maovu yao; na kukawa huko mbele ya Allaah, ni kufuzu adhimu. [Al-Fat-h: 5]

 

 [At-Tirmidhiy Amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]

 



Ijumaa, 18 Oktoba 2019

36-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Hakuwaadhibu Au Kuwaangamiza Makafari Kwa Sababu Ya Uwepo Wakee

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

36-Allaah Hakuwaadhibu Au Kuwaangamiza Makafari Kwa Sababu Ya Kuweko Kwake

 

www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

  وَإِذْ قَالُوا اللَّـهُمَّ إِن كَانَ هَـٰذَا هُوَ الْحَقَّ مِنْ عِندِكَ فَأَمْطِرْ عَلَيْنَا حِجَارَةً مِّنَ السَّمَاءِ أَوِ ائْتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٢﴾

Na pindi waliposema: “Ee Allaah! Kama haya ni haki kutoka Kwako; basi Tunyeshee mvua ya mawe kutoka mbinguni, au Tuletee adhabu iumizayo.”

 

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنتَ فِيهِمْ ۚ وَمَا كَانَ اللَّـهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ﴿٣٣﴾

Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu na hali wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uko nao. Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu hali wao wanaomba maghfirah. [Al-Anfaal: 32- 33]

 

Imaam As-Sa’diy  (رحمه الله)  amesema:  “Kutokana na kauli yao hiyo (ya Aayah 32 ya kuomba adhabu) ni dhahiri kuwa wao ni wajinga wapumbavu, madhalimu. Lau kama Allaah Angewaharakazia adhabu basi wasingebakia kuishi. Lakini Allaah Amewakinga na adhabu kwa sababu ya uwepo wa Rasuli miongoni mwao. Basi uwepo wa Rasuli ni amani kwao kutona na adhabu.”

 



36-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):Unyenyekevu Wake: Akila Na Kuketi Kama Wanavyokula Na Kuketi Maswahaba

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

36-Unyenyekevu Wake  Akila Na Kuketi Kama Wanavyokula Na Kuketi Maswahaba

 

www.alhidaaya.com

 

 

عَنْ يَحْيَى بْنِ أَبِي كَثِيرٍ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ آكُلُ كَمَا يَأْكُلُ الْعَبْدُ وَأَجْلِسُ كَمَا يَجْلِسُ الْعَبْدُ فَإِنَّمَا أَنَا عَبْدٌ

Kutoka kwa Yahya bin Abi Kathiyr kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mimi nakula kama anavyokula mja na nakaa kitako kama anavyokaa mja, kwani hakika mim ni mja.”  [Al-Bayhaqiy na ameisahihisha Al-Albaaniy As-Silsilah Asw-Swahiyhah (544)]

 

Katika Riwaayah nyengine:

 

حَدَّثَنَا جَرِيرُ بْنُ حَازِمٍ، قَالَ: سَمِعْتُ الْحَسَنَ، يَقُولُ: إِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يُؤْتَى بِطَعَامٍ، فَيَأْمُرُ بِهِ فَيُوضَعُ عَلَى الْأَرْضِ، ثُمَّ يَقُولُ: "إِنِّي إِنَّمَا أَنَا عَبْدٌ، آكُلُ كَمَا يَأْكُلُ الْعَبْدُ" ، وَأَحْسَبُهُ قَالَ: وَأَجْلِسُ كَمَا يَجْلِسُ الْعَبْدُز" رواه البيهقي

Jariyr ibn Haazim amehadithia kwamba: Nilimsikia Al-Hasan akisema:  Hakika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa analetewa chakula huamrisha kiwekwe huwekwa chini kisha husema: “Hakika mimi ni mja, nakula kama mnavyokula.” Na nadhani pia amesema: “Na nakaa kitako kama mnavyokaa kitako.”

[Al-Bayhaqiy, As-Silsilah Asw-Swahiyhah (544)]



110-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Ummah Wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

 Fadhila Za Ummah Wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah ('Azza wa Jalla):

 

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾

110. Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Ahlul-Kitaabi ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wanaoamini na wengi wao ni mafasiki.

 

Mafunzo:

 

Hadiyth kadhaa zimetajwa fadhila za Ummah huu wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi yake ni:

Mu’aawiyah bin Haydah Al-Qash-riyy  (رضي الله عنه) amehadithia kutoka kwa baba yake kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nyinyi mnakamilisha Ummah sabini. Nyinyi ndio mbora wao na ndio watukufu zaidi mbele ya Allaah (عزّ وجلّ).” [Ahmad, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Al-Haakim, na wengineo kwa riwaayah tofauti kidogo taz. Swahiyh Al-Jaami’ (2301), Swahiyh At-Tirmidhiy (3001)].

Pia rejea tanbihi (2: 213).

 

Na pia, Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Sisi (Waislamu) ni wa mwisho (kuja) na (tutakuwa) wa mwisho Siku ya Qiyaamah na wa mwanzo kuingia Jannah…” [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 



048-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Fat-h: Aayah 5

 

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

048-Al-Fat-h Aayah 5

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

  لِّيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عِندَ اللَّـهِ فَوْزًا عَظِيمًا﴿٥﴾

Ili Awaingize Waumini wa kiume na Waumini wa kike Jannaat zipitazao chini yake mito, ni wenye kudumu humo, na Awafutie maovu yao; na kukawa huko mbele ya Allaah, ni kufuzu adhimu. [Al-Fat-h: 5]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

عَنْ أَنَسٍ، رضى الله عنه قَالَ أُنْزِلَتْ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلمَ ‏:‏ ‏((ليغْفِرَ لَكَ اللَّهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّر))َ  مَرْجِعَهُ مِنَ الْحُدَيْبِيَةِ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ لَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَىَّ آيَةٌ أَحَبُّ إِلَىَّ مِمَّا عَلَى الأَرْضِ ثُمَّ قَرَأَهَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَيْهِمْ فَقَالُوا هَنِيئًا مَرِيئًا يَا نَبِيَّ اللَّهِ قَدْ بَيَّنَ اللَّهُ لَكَ مَاذَا يُفْعَلُ بِكَ فَمَاذَا يُفْعَلُ بِنَا فَنَزَلَتْ عَلَيْهِ: ((ليُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الأَنْهَارُ))  حَتَّى بَلَغَ ‏:‏ ‏((‏فوزًا عَظِيمًا ))‏  قَالَ هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ  ‏.‏

 

Anas bin Maalik amehadithia kwamba: Tulipokuwa tunarudi kutoka Hudaybiyyah, iliteremshwa kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَيَهْدِيَكَ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا﴿٢﴾

Ili Allaah Akughufurie yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayofuatia; na Akutimizie neema Yake juu yako na Akuongoze njia iliyonyooka.

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika nimeteremshiwa Aayah ambayo ni kipenzi mno kuliko chochote kilichoko duniani.” Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawasomea Aayah hiyo, wakasema: Hongera kwako ee Nabiy wa Allaah, hakika Allaah Amekubainisha Atakalokufanyia, lakini je Atatufanyia nini sisi? Hapo ikateremshwa: 

 

لِّيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عِندَ اللَّـهِ فَوْزًا عَظِيمًا﴿٥﴾

Ili Awaingize Waumini wa kiume na Waumini wa kike Jannaat zipitazao chini yake mito, ni wenye kudumu humo, na Awafutie maovu yao; na kukawa huko mbele ya Allaah, ni kufuzu adhimu. [Al-Fat-h: 5]

 [At-Tirmidhiy Amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]

 



036-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Hana Iymaan Na Hatoingia Jannah Mwenye Kumtendea Jirani Shar

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 36

 

Hana Iymaan Na Hatoingia Jannah Mwenye Kumtendea Jirani Shari

 

Alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ، وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ،  وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ!))  قِيلَ: مَنْ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟  قَالَ: الَّذِي لاَ يَأْمَنُ جَارُهُ بَوَائقَهُ)) متفق عليه

 وَفِي رِوَايَة: ((لاَ يَدْخُلُ الْجَنَّةَ مَنْ لاَ يَأْمَنُ جَارُهُ بَوَائِقَهُ)) مسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Wa-Allaahi hakuamini (hana Iymaan). Wa-Allaahi hakuamini, Wa-Allaahi hakuamini!)) Akaulizwa: Nani ee Rasuli wa Allaah?  Akasema: ((Ambaye jirani yake hasalimiki na shari zake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Na katika riwaayah nyengine: ((Hatoingia Jannah ambaye jirani yake hasalimiki na shari zake)) [Muslim]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Uislamu unasisitiza kumtendea wema jirani. Umuhimu wake hadi kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameapa kwa Allaah! Na katika Hadiyth nyengine:

 

عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَا زَالَ جِبْرِيلُ يُوصِينِي بِالْجَارِ حَتَّى ظَنَنْتُ أَنَّهُ سَيُوَرِّثُهُ)). متفق عليه

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Jibriyl hakuacha kuniusia jirani mpaka nikadhani kuwa atamrithisha [mali yangu])). [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

2. Mojawapo ya uthibitisho wa Iymaan ya Muumin ni kutomuudhi jirani.

 

 

3.Kumfanyia wema jirani ni sababu mojawapo ya kuingia Jannah, na kinyume chake ni kuingia motoni.

 

4. Muislamu anatakiwa ajiepushe na sifa mbaya ya kuudhi mtu na awe mwenye tabia njema na mwenye kulinda haki za watu.

 

 

5. Jirani ni aliye ubavuni, mtaani au hata aliye mbali. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

 وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا ﴿٣٦﴾

Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na jirani mwenye ujamaa na jirani asiye na ujamaa na rafiki wa karibu, na msafiri aliyeishiwa masurufu, na wale iliyowamiliki mikonoyenu ya kulia. Hakika Allaah Hapendi mwenye majivuno mwenye kujifakharisha.  [An-Nisaa (4: 36)]

 

 

6. Uislamu haukubagua kufanya wema hata kwa jirani asiye Muislamu anapaswa kutendewa wema.

Rejea: Al-Mumtahinah (60: 8-9).

 

 

7. Kumfanyia wema jirani na kutomuudhi ni katika uthibitisho wa Iymaan. Na Hadiyth: ((Mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho, basi asimuudhi jirani yake))[Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na at-Tirmidhiy]

 

 

Na pia Hadiyth: ((Mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho, amfanyie wema jirani yake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 



Ijumaa, 11 Oktoba 2019

35-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Amemtunza Na Kumuongoza Na Kumtimizia Mahitaji Yake

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

35-Allaah Amemtunza Na Kumuongoza Na Kumtimizia Mahitaji Yake

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَىٰ ﴿٦﴾

Je, kwani Hakukukuta yatima, Akakupa makazi?

 

 

وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَىٰ ﴿٧﴾

Na Akakukuta mpotevu Akakuongoza?

 

 

وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَىٰ ﴿٨﴾

Na Akakukuta mhitaji, Akakutosheleza? [Adhw-Dhwuhaa: 6-8]



35-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake: Akinyenyekea Kwa Ahli Zake

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

35-Unyenyekevu Wake Akinyenyekea Kwa Ahli Zake

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنِ النَّبِيِّ ـ صلى الله عليه وسلم ـ قَالَ ‏ "‏ خَيْرُكُمْ خَيْرُكُمْ لأَهْلِهِ وَأَنَا خَيْرُكُمْ لأَهْلِي ‏"‏ ‏ رواه الترمذي

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:  ((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa mke wake, na mimi ni mbora kwa watu wangu wa nyumbani [ahli])) [Ibn Maajah na Ad-Daarimiy].



105-Aayah Na Mafunzo: Makundi Sabini Na Tatu Yataingia Motoni Isipokuwa Moja Tu.

 

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

 

Makundi Sabini Na Tatu Yataingia Motoni Isipokuwa Moja Tu

 

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٠٥﴾

Na wala msiwe kama wale waliofarikiana na wakakhitilafiana baada ya kuwajia hoja bayana. Na hao watapata adhabu kuu. [Aal-'Imraan: 105]

 

Mafunzo:

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wamegawanyika Mayahudi katika mapote sabini na moja na wakagawanyika Manaswara katika mapote sabini na mbili na Ummah wangu utagawanyika mapote sabini na tatu. Yote hayo yataingia motoni ila moja tu.” Maswahaba waliuliza: Ni lipi hilo ee Rasuli wa Allaah?  Akasema: “Ni lile nililokuwemo mimi na Maswahaba zangu.” [Ahmad, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ad-Daarimiy].

 



048-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Fat-h: Aayah 1 - 5

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

048-Al-Fat-h: Aayah 1 - 5

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا﴿١﴾

Hakika Tumekupa ushindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), ushindi bayana.

 

لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَيَهْدِيَكَ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا﴿٢﴾

Ili Allaah Akughufurie yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayofuatia; na Akutimizie neema Yake juu yako na Akuongoze njia iliyonyooka.

 

وَيَنصُرَكَ اللَّـهُ نَصْرًا عَزِيزًا﴿٣﴾

Na Akunusuru Allaah nusura yenye nguvu kabisa.

 

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ السَّكِينَةَ فِي قُلُوبِ الْمُؤْمِنِينَ لِيَزْدَادُوا إِيمَانًا مَّعَ إِيمَانِهِمْ ۗ وَلِلَّـهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا﴿٤﴾

Yeye Ndiye Aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili Awazidishie iymaan pamoja na iymaan zao. Na ni ya Allaah Pekee majeshi ya mbinguni na ardhini, na Allaah ni daima Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

لِّيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عِندَ اللَّـهِ فَوْزًا عَظِيمًا﴿٥﴾

Ili Awaingize Waumini wa kiume na Waumini wa kike Jannaat zipitazao chini yake mito, ni wenye kudumu humo, na Awafutie maovu yao; na kukawa huko mbele ya Allaah, ni kufuzu adhimu.

 [[Al-Fat-h: 1 – 5]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 

عَنْ أَنَسٍ ابن مالك رضى الله عنه  قَالَ لَمَّا نَزَلَتْ: ((إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا * لِيَغْفِرَ لَكَ اللَّهُ‏))  إِلَى قَوْلِهِ: ((‏فَوْزًا عَظِيمًا‏))‏ مَرْجِعَهُ مِنَ الْحُدَيْبِيَةِ وَهُمْ يُخَالِطُهُمُ الْحُزْنُ وَالْكَآبَةُ وَقَدْ نَحَرَ الْهَدْىَ بِالْحُدَيْبِيَةِ فَقَالَ ‏"‏ لَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَىَّ آيَةٌ هِيَ أَحَبُّ إِلَىَّ مِنَ الدُّنْيَا جَمِيعًا ‏"‏ ‏.‏

 Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema:  Ilipoteremka:

 

إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا﴿١﴾

Mpaka kauli Yake:

فَوْزًا عَظِيمًا

Alipokuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba  wanarudi kutoka Hudaybiyyah wakiwa katika hali ya kuzidiwa na  ghadhabu, huzuni na dhiki (kwa kuzuiliwa na Makafiri Quryash kuingia Makkah) Wakawa wamechinja Hady (mnyana wa Hajj) wao. (Hapo zikateremshwa Aayah hizo) na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika nimeteremshiwa Aayah ambazo ni vipenzi zaidi kuliko dunia nzima.”  [Muslim Kitaab Al-Jihaad Was Sayr]    

 

 

Pia,

 

عَنْ أَنَسٍ ابن مالك رضى الله عنه:  ((إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا))  قالَ الْحُدَيْبِيَةُ‏.‏ قَالَ أَصْحَابُهُ هَنِيئًا مَرِيئًا فَمَا لَنَا?  فَأَنْزَلَ اللَّهُ : ‏ ‏((لِيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ‏))  قَالَ شُعْبَةُ فَقَدِمْتُ الْكُوفَةَ فَحَدَّثْتُ بِهَذَا كُلِّهِ عَنْ قَتَادَةَ ثُمَّ رَجَعْتُ فَذَكَرْتُ لَهُ فَقَالَ أَمَّا:  ‏((‏إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ‏))‏ فَعَنْ أَنَسٍ، وَأَمَّا هَنِيئًا مَرِيئًا فَعَنْ عِكْرِمَةَ‏.

Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema kuhusu:

إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا

Inahusiana na (Bay’ah) ya Hudaybiyyah.  Maswahaba wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) wakasema kumwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Hongera na furaha kwako, lakini je sisi tunapata nini?” Hapo Allaah Akateremsha:

 

لِّيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عِندَ اللَّـهِ فَوْزًا عَظِيمًا﴿٥﴾

Ili Awaingize Waumini wa kiume na Waumini wa kike Jannaat zipitazao chini yake mito, ni wenye kudumu humo, na Awafutie maovu yao; na kukawa huko mbele ya Allaah, ni kufuzu adhimu. [Al-Bukhaariy]

 

Pia,

 

عن أَنَسٍ ابن مالك رضى الله عنه  عن زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ سَمِعْتُ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ، رضى الله عنه يَقُولُ كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي بَعْضِ أَسْفَارِهِ فَكَلَّمْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَسَكَتَ ثُمَّ كَلَّمْتُهُ فَسَكَتَ ثُمَّ كَلَّمْتُهُ فَسَكَتَ فَحَرَّكْتُ رَاحِلَتِي فَتَنَحَّيْتُ وَقُلْتُ ثَكِلَتْكَ أُمُّكَ يَا ابْنَ الْخَطَّابِ نَزَرْتَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ثَلاَثَ مَرَّاتٍ كُلُّ ذَلِكَ لاَ يُكَلِّمُكَ مَا أَخْلَقَكَ أَنْ يَنْزِلَ فِيكَ قُرْآنٌ قَالَ فَمَا نَشِبْتُ أَنْ سَمِعْتُ صَارِخًا يَصْرُخُ بِي قَالَ فَجِئْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: "يَا ابْنَ الْخَطَّابِ لَقَدْ أُنْزِلَ عَلَىَّ هَذِهِ اللَّيْلَةَ سُورَةٌ مَا أُحِبُّ أَنَّ لِي بِهَا مَا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ" ‏:‏ ‏((‏إنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا )) ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ غَرِيبٌ

 

Kutoka kwa Anas bin Maalik kutoka Zayd bin Aslam kutoka kwa baba yake amesema: Nilimsikia  'Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه)  akisema: Tulikuwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  wakati mmoja wa safari zake, nikamwambia jambo lakini alikuwa kimya. Kisha nikamwambia tena lakini alikuwa kimya. Nikaharakiza kasi yangu ya kipando changu kwenda mbele. Nikasema (kujiambia mwenyewe): “Mama yako akupoteze ee ibn Al-Khattwaab! Umemchagiza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  mara tatu na kila mara hakukujibu! Unastahili kwamba uteremshiwe jambo  juu yako katika Qur-aan.” (‘Umar) Akasema:  Haikuchukua muda mrefu kabla kusikia sauti ikiniita.   Nikamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema: “Ee ibn Al-Khatwaab! Imeteremshwa Suwrah kwangu jana usiku ambayo ni kipendzi zaidi kwangu kulikoni chochote kile  kinachochomezewa na jua.”

 

إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا

 

[At-Tirmidhiy amesema Hadiyth Hasan Swahiyh Ghariyb]

 

Na katika Riwaayah nyenginezo kama hizo:

 

عَنْ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَسِيرُ فِي بَعْضِ أَسْفَارِهِ، وَعُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ يَسِيرُ مَعَهُ لَيْلاً، فَسَأَلَهُ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ عَنْ شَىْءٍ فَلَمْ يُجِبْهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ سَأَلَهُ فَلَمْ يُجِبْهُ، ثُمَّ سَأَلَهُ فَلَمْ يُجِبْهُ وَقَالَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ ثَكِلَتْكَ أُمُّكَ يَا عُمَرُ، نَزَرْتَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ثَلاَثَ مَرَّاتٍ، كُلُّ ذَلِكَ لاَ يُجِيبُكَ‏.‏ قَالَ عُمَرُ فَحَرَّكْتُ بَعِيرِي ثُمَّ تَقَدَّمْتُ أَمَامَ الْمُسْلِمِينَ، وَخَشِيتُ أَنْ يَنْزِلَ فِيَّ قُرْآنٌ، فَمَا نَشِبْتُ أَنْ سَمِعْتُ صَارِخًا يَصْرُخُ بِي ـ قَالَ ـ فَقُلْتُ لَقَدْ خَشِيتُ أَنْ يَكُونَ نَزَلَ فِيَّ قُرْآنٌ‏.‏ وَجِئْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَسَلَّمْتُ عَلَيْهِ فَقَالَ ‏"‏ لَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَىَّ اللَّيْلَةَ سُورَةٌ لَهِيَ أَحَبُّ إِلَىَّ مِمَّا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ، ثُمَّ قَرَأَ: ((إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا‏))

 

Kutoka kwa Zayd bin Aslam kutoka kwa baba yake kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  alikuwa katika safari usiku mmoja na ‘Umar bin Al-Khatwaab alikwa pamoja naye. ‘Umar  ibn Al-Khatwaab akamuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) jambo lakini hakumjibu. Kisha akamuuliza tena lakini hakumjibu. Akamuuliza tena lakini hakumjibu.  ‘Umar akasema:  (kujiambia mwenyewe): “Ee ibn Al-Khatwaab! Mama yako akupoteze, kwani umemchagiza (صلى الله عليه وآله وسلم) mara tatu, lakini hakukujibu.”  ‘Umar Akasema Nikamwendesha mnyama wangu kwa kasi kuwatangulia  Waislamu mbele na nikawa nakhofu kuwa iteremshwa jambo katika Qur-aan.  Sikusubiri hata dakika nikasikia mtu ananiita. Nikasema: Nilikuwa nakhofu kwamba nimeteremshiwa Qur-aan. Nikafika kwa Rasuli wa Alaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nikamsalimia akasema:  “Hakika nimeteremshiwa  usiku Suwrah ambayo hakika ni kipenzi kwangu kuliko chochote kile kilichochomezewa na jua.” Kisha akasoma:

إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا

[Al-Bukhaariy  Kitaab Al-Maghaaziy; Baab Ghazwat Al-Hudaybiyyah, pia Riwaaya kama hizo katika Kitaab Fadhwaail Al-Qur-aan, Kitaab At-Tafsiyr]



035-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Starehe Bora Kabisa Ya Dunia Ni Mke Mwema

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 35

Starehe Bora Kabisa Ya Dunia Ni Mke Mwema

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو بْنِ الْعَاص (رضي الله عنهما)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  ((الدُّنْيَا مَتَاعٌ وَخَيْرُ مَتَاعِ الدُّنْيَا الْمَرْأَةُ الصَّالِحَة)) مسلم

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رضي الله عنهما) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Dunia ni starehe, na bora ya starehe zake ni mke mwema)) [Muslim]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo :

 

 

1. Umuhimu wa kuchagua mke mwema, mwenye taqwa.

 

Rejea: Hadiyth namba (40).

 

 

2. Sababu mojawapo ya furaha ya dunia na Aakhirah ni kuwa na mke mwema, mwenye taqwa.

 

 

3. Fadhila za mwanamke mwema mwenye taqwa kufananishwa na starehe na pambo la dunia. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

 زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ   ﴿ ١٤﴾

Watu wamepambiwa huba ya matamanio miongoni mwa wanawake, na watoto, na mirundi ya mali iliyorundikwa ya dhahabu na fedha na farasi wenye chapa ya aina bora na wanyama wa mifugo na mashamba. Hayo ni starehe za uhai wa dunia, na Allaah Kwake kuna marejeo mazuri.  [Aal-‘Imraan (3: 14)]

 

 

4. Wema na taqwa ni miongoni mwa sifa njema anazopasa mwanamke wa Kiislamu kumiliki.

 

Rejea At-Tahriym (66: 11-12)

 

 

5. Mume anayeruzukiwa mke mwema ni neema kwake. Inampasa ailinde neema kwa kuishi naye vyema na kuwa na huruma naye na mapenzi ili apate kudiriki starehe za dunia na Aakhirah.

 

Rejea: Ar-Ruwm (30: 21), An-Nuwr (24: 26).

 

Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameusia waume kuwatendea wema wanawake zao katika Hadiyth kadhaa miongoni mwazo ni:

 

Kauli yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

((Nakuusieni kuwafanyia wema wanawake))  [Al-Bukhaariy na Muslim

 

Na pia:

 

((واتَّقُوا اللهَ في النِّساءِ، فإنهن عندكم عَوَانٌ))

  ((Mcheni Allaah kuhusu wanawake kwani wao ni wasaidizi wenu…)   

 

Na pia amesema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa familia yake na mimi ni mbora kabisa kwa familia yangu))  [At-Twabaraaniy]

 

Na amesema pia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

أن تطعمها إذا طعمت  وتكسوها إذا اكتسيت ولا تضرب الوجه ولا تقبّح   ولا تهجر إلاّ في البيت

((Kumlisha unapokula, na kumvisha unapovaa, wala usimpige usoni na kumharibu na usimtusi (kwa matendo yake na maneno yake) wala usimhame kwenda nyumba nyingine (umhame kitanda tu)) [Abuu Daawuwd, Ibn Maajah na Ahmad]

 

 Na amesema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

ارفق بالقوارير

((Wafanyieni wema vyombo vyenu (qawaariyra).” [Al-Bukhaariy]

 

Rejea pia Hadiyth namba (28), (29), (40).

 

 

 



Alhamisi, 3 Oktoba 2019

104-Aayah Na Mafunzo: Umuhimu Wa Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovu

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Umuhimu Wa Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovu

Alhidaaya.com

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفلِحُونَ ﴿١٠٤﴾

Na watokeze kutoka kwenu umati wa watu unaolingania kheri na unaoamrisha mema na unaokataza munkari. Na hao ndio waliofaulu. [Aal-'Imraan: 104]

 

Mafunzo:

 

Umuhimu wa kuamrisha mema na kukataza maovu umesisitizwa katika Qur-aan Aayah kadhaa na pia katika Sunnah, miongoni mwazo ni: Hudhayfah bin Al-Yamaani (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake! Mtaamrisha mema na mtakataza maovu au sivyo Allaah Atakuleteeni adhabu kutoka Kwake, kisha mtamuomba wala Hatokuitikieni.” [Ahmad na At-Tirmidhy - Swahiyh At-Tirmdhiy (2169), Swahiyh Al-Jaami’ (7070)].

 

Pia: Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Atakayeona munkari (uovu) basi aubadilishe kwa mkono wake, na asipoweza basi kwa ulimi wake, na asipoweza basi kwa moyo wake (achukizwe) na huo ni udhaifu wa Iymaan.”  [Muslim].

 



049-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Hujuraat: 11

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

049-Al-Hujuraat  11

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَىٰ أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَىٰ أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ ۖ وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ ۖ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ ۚ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿١١﴾

Enyi walioamini! Wanaume wasiwafanyie dhihaka na kudharau wanaume wengineo asaa wakawa bora kuliko wao, wala wanawake kwa wanawake wengineo, asaa wakawa bora kuliko wao. Na wala msifedheheshane kwa kutukanana na wala msiitane majina (mabaya) ya utani. Ubaya ulioje kuita jina la ufasiki baada ya iymaan. Na yeyote asiyetubu, basi hao ndio madhalimu. [Al-Hujuraat: 11]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ إِسْمَاعِيلَ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، عَنْ دَاوُدَ، عَنْ عَامِرٍ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبُو جُبَيْرَةَ بْنُ الضَّحَّاكِ،  قَالَ فِينَا نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ فِي بَنِي سَلِمَةَ: ((وَلاَ تَنَابَزُوا بِالأَلْقَابِ بِئْسَ الاِسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الإِيمَانِ)) قَالَ قَدِمَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَلَيْسَ مِنَّا رَجُلٌ إِلاَّ وَلَهُ اسْمَانِ أَوْ ثَلاَثَةٌ فَجَعَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏"‏ يَا فُلاَنُ ‏"‏ ‏.‏ فَيَقُولُونَ مَهْ يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهُ يَغْضَبُ مِنْ هَذَا الاِسْمِ فَأُنْزِلَتْ هَذِهِ الآيَةُ: ((وَلاَ تَنَابَزُوا بِالأَلْقَابِ))

 

Ametuhadithia Muwsaa ibn Ismaa’iyl, ametuhadithia Wuhayb, kutoka kwa Daawuwd, kutoka kwa ‘Aamir amesema: ametuhadithia Jubayrah ibn Adhw-Dhwahaak ambaye amesema:  Aayah hii imeteremshwa kwa ajili yetu Bani Salimah:

 

وَلاَ تَنَابَزُوا بِالأَلْقَابِ بِئْسَ الاِسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الإِيمَان

Na wala msiitane majina (mabaya) ya utani. Ubaya ulioje kuita jina la ufasiki baada ya iymaan.

 

Akasema: Pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipotufikia, kila mmoja wetu alikuwa ana majina mawili au matatu.  Basi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa Anasema:  “Ee fulani!” Lakini wao husema: Ee Rasuli wa Allaah (Usimwite kwa jina hilo), hakika yeye hughadhibika kuitwa kwa jina hilo!  Basi hapo ikateremshwa Aayah hii:

وَلاَ تَنَابَزُوا بِالأَلْقَابِ  

Na wala msiitane majina (mabaya) ya utani. 

 

[Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, At-Tirmidhiy, ameisahihisha Al-Albaaniy: Swahiyh Abiy Daawuwd (4962), Swahiyh Ibn Maajah (3030), Swahiyh At-Tirmidhiy (3268),Swahiyh Adab Al-Mufrad (251)]

 



034-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Kuswali Wakati Wake, Kuwafanyia Wema Wazazi, na Kufanya Jihaad

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 34

Kuswali Wakati Wake, Kuwafanyia Wema Wazazi, na Kufanya Jihaad

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بن مَسْعُودٍ (رضي الله عنه) قَالَ: سَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَيُّ الْعَمَلِ أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ؟ قَالَ: ((الصَّلاَةُ عَلَى وَقْتِهَا)) قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: ((ثُمَّ بِرُّ الْوَالِدَيْنِ)) قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟  قَالَ: ((الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه)  ambaye amesema: Nilimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):  ‘amali gani inayopendeza zaidi kwa Allaah? Akasema: ((Swalaah kwa wakati wake)). Akasema: Kisha ipi? Akasema: ((Kisha kuwafanyia wema wazazi wawili)). Akasema: Kisha ipi? Akasema: ((Kufanya Jihaad katika Njia ya Allaah)).  [Al-Bukhaariy na Muslim.]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. ‘Amali zinatofuatiana kwa daraja, kwa maana kuwa nyinginezo zina thawabu zaidi ya nyingine.

 

 

2. Hima kubwa ya Maswahaba kupenda kujifunza mambo ya Dini yao, kwani walikuwa wakimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kila jambo wasilolijua.

 

 

3. Tabia njema ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na upole wake wa kuvumilia maswali kadhaa ya Maswahaba zake akiwajibu bila ya kuchoka.

 

 

4. Kuswali kwa wakati ni ‘amali bora kabisa kwa Allaah na ni amrisho katika Qur-aan.  Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا ﴿١٠٣﴾

Hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu. An-Nisaa (4: 103).

 

Rejea pia Hadiyth namba (49), (79).

 

 

5. Uislamu unahimiza kuwafanyia wema wazazi wawili. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا ﴿٢٣﴾

 

Na Rabb wako Amehukumu kwamba: “Msiabudu isipokuwa Yeye Pekee na (Ameamrisha) kuwafanyia ihsaan wazazi wawili. Kama mmoja wao akifikia uzee naye yuko pamoja nawe, au wote wawili basi usiwaambie, Uff! Na wala usiwakemee; na waambie maneno ya heshima.

 

 وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا

﴿٢٤﴾

Na wainamishie bawa la unyenyekevu kwa huruma, na useme: “Rabb wangu! Warehemu kama walivyonilea udogoni.” [Al-Israa (17: 22-23)]

 

 

Rejea pia: Al-Baqarah (2: 83), An-Nisaa (4: 36), Al-An’aam (6: 151), Al-‘Ankabuwt (29: 8), Luqmaan (31: 14)].

 

Rejea pia Hadiyth namba (125).

 

 

6. Kuwafanyia wema wazazi ina thawabu zaidi kuliko kufanya Jihaad katika njia ya Allaah kwa dalili ya Hadiyth: Abdullaah bin ‘Amr Al-‘Aasw (رضي الله عنهما) alisimulia: Mtu mmoja alimkabili Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: Nitakubai juu ya Hijrah na kupigana jihaad katika njia ya Allaah nikitafuta ujira kutoka kwa Allaah. Akamuuliza: ((Je katika wazazi wako yuko aliye hai?)) Akajibu: Ndio, wote wako hai. Akamuuliza: ((Unatafuta ujira kutoka kwa Allaah?)) Akajibu: Ndio. Akamwamiba: ((Rudi kwa wazazi wako na uwafanyie wema)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

7. Kufanya jihaad katika njia ya Allaah ni mojawapo wa ‘amali kipenzi kwa Allaah (سبحانه وتعالى) na Allaah (سبحانه وتعالى) Amewaahidi wafanyao jihaad kuwakinga na adhabu na kupata mema ya Jannah   Anasema:

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَارَةٍ تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ﴿١٠﴾

Enyi walioamini! Nikujulisheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo?

 

 

 

تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿١١﴾

Mumuamini Allaah na Rasuli Wake, na mfanye jihaad katika njia ya Allaah kwa mali zenu, na nafsi zenu. Hivyo ndiyo bora kwenu mkiwa mnajua.

 

 

يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١٢﴾

 (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito na masikani mazuri katika Jannaat za kudumu milele. Huko ndiko kufuzu adhimu.

 

وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا ۖ نَصْرٌ مِّنَ اللَّـهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٣﴾

Na jengine mlipendalo; nusura kutoka kwa Allaah na ushindi wa karibu. Na wabashirie Waumini. [Asw-Swaff 61: 10-13]

 

Fadhia nyenginezo mbali mbali zimetajwa za kufanya jihaad. Rejea: Al-Maaidah (5: 35), Al-Anfaal (8: 74), Al-Baqarah (2: 218), An-Nisaa (4: 95), Al-‘Ankabuwt (29: 69), Al-Hujuraat (49: 15).

 

 

 

8. Mwanafunzi anatakiwa amuulize maswali mwalimu wake ambayo yatamsaidia katika dunia na Aakhirah yake.

 

 

9. Mwanafunzi anapaswa awe na adabu nzuri kwa mwalimu wake wala asitoke katika nidhamu hiyo ya adabu na haki za mwalimu na mwanafunzi kwa Mwalimu.

 

 

 



20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...