Wengi wanaaminu kuna nyoka mmoja tu aitwaye cobra, lakini ukweli ni kwamba kuna aina takriban 270 za viumbe za cobra. Hata hivyo, wataalamu wa elimu ya viumbe wanasema kuna wanaowaita kobra wa kweli 28 (true cobra), miongoni mwao ni huyo Indian cobra, Binosolate cobra, Cape cobra, Spitting cobra bila kumsahau mkubwa wao King cobra nk.
Indian cobra hapatikani katika maeneo yetu ya ukanda huu wa Afrika, bali wapo kwa wingi Asia ya Kusini katika nchi za l India, Pakistan, Bangladesh, Nepal na katika kisiwa cha Srilanka. Naye hutukuzwa sana katika imani na mila za kihindu na pia kule Srilanka katika dini ya Mabudha kiasi kwamba ni haramu kumuua katika sheria zao.
Sifa kubwa ya Indian cobra ni kutanuka shingoni na inatajwa kuwa ndiye nyoka pekee anayetanuka eneo hilo lakini kichwa kikabaki vilevile. Wengi wana urefu wa kati ya mita 1-mita 1.5 lakini wale wa Srilanka wapo mpaka kuanzia mita 2.1 hadi mita 2.2. Indian Cobra anaweza kuwa na rangi ya njano, kijivu, kahawia, nyekundu au nyeusi.
Uzazi
Indian cobra ni ‘oviparus’ yaani anataga mayai nje. Kipindi chao cha kutaga mayai ni mwezi wa Aprili hadi Julai. Nyoka hawa hutaga mayai kuanzia 10 hadi 30 katika mashimo ya panya au sungu sungu na baada ya siku 48 au 60 mayai yanaanguliwa.
Kama ilivyo kwa nyoka wengine, nyoka hawa pia hawana kawaida wala muda wa kulinda mayai yao. Ni King cobra pekee ndiye hulinda mayai yake. Pia, muda mfupi tu baada ya Indian cobra kutotoa mayai, vitoto vinavyozaliwa huanza kujitegemea.
Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Indian cobra
- Sumu ya Indian cobra ni kali sana na inaweza kuua.
- Katika kundi la cobra, inazidiwa na ile ya King cobra na Cape cobra tu. Sumu ya Indian cobra inaua kwa njia mbili. Kwanza inalemaza (paralayse) mishipa ya fahamu (neuro toxin) na pili inadhuru moyo (cadio toxin).
- Wengi wanadhani cobra wanasikia lakini ukweli ni kuwa hawasikii bali wanapata hisia kwa mitetemo ya ardhi (vibration) kupitia tumbo lake.
- Katika maeneo niliyoyataja ambayo wanapatikana Indian cobra, basi tarajia kumkuta chinibya mti, juu ya mti, kwenye mawe na hata katika mashimo.
- Sumu ya Indian cobra inaanza kufanya kazi kuanzia dakika 15 hadi masaa mawili, ingawa hali ni hiyohiyo pia kwa nyoka wote. Madaktari wamethibitisha kuwa, licha ya ukali wa sumu yake, Indian cobra lakini anaweza kumuuma mtu na asife iwapo tu atawahishwa hospitali kwa kuwa sasa dawa za kupambana na sumu za nyoka zipo.
- Indian cobra hutumia ulimi kuwasaidia kutambua harufu ya kitu.
- Umri wao wa kuishi ni miaka tisa ila cobra wengine wanaishi zaidi ya hapo.
- Pamoja na hatari aliyokuwa nayo kwa viumbe wengi, akikutana na kiumbe kama njegere na ndege aina ya tai; Indian cobra huwa hana ujanja. Anakamatwa na kuliwa kirahisi tu.
- Indian cobra huwa hapendi sana kumuuma binadamu labda umkanyage au uoneshe kutaka kumdhuru. Na akimgonga binadamu huwa haachii sumu yake yote bali kiasi kidogo tu tofauti anavyogonga viumbe wale ambao anawala.
- Hata hivyo, hali ni kwa nyoka wote, si Indian cobra pekee. Ni kwa sababu hii ndio maana vifo vinavyosababishwa na nyoka sio vingi sana ukilinganisha na vifo mfano, vifo vinavyosababishwa na ajali.
from TIF https://ift.tt/2AEtiOr
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni