Translate

Jumatano, 31 Oktoba 2018

Video -





from FB-RSS feed for Islamkingdom - Swahili https://ift.tt/2Pwwdkl
via IFTTT

Sharh ´Aqiydat-il-Waasitwiyyah 06



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2SyRVTk
via IFTTT

Uharamu wa kuitakidi juu ya mikosi 03



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2AGMRFP
via IFTTT

Uharamu wa kuitakidi juu ya mikosi 02



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2SARoAu
via IFTTT

Kalima ya ‘Aqiyqah



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2Rn2ZSi
via IFTTT

Sharh ´Aqiydat-il-Waasitwiyyah 05



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2AFSOTv
via IFTTT

New video by GROUP FAIDIKA NA MAWAIDHA on YouTube

*Tafsir Ya Qur-an* *📖 Surat Luqman 20-30* *👤👤Sh. Mishari Al Afasiy.* *Sh. Mahammad Sulayman.*
*Tafsir Ya Qur-an* *📖 Surat Luqman 20-30* *👤👤Sh. Mishari Al Afasiy.* *Sh. Mahammad Sulayman.*


View on YouTube

Indian cobra: Hatari ukimchokoza, lakini hana ujanja kwa tai

Utukufu ni wake Allah, Mbora wa waumbaji, Muumba wa kila kilichopo ulimwengu kwa sifa tofauti. Juma hili tukauone ukubwa wa Allah Aliyetukuka kwa kumsoma nyoka aitwaye Indian Cobra, miongoni mwa aina ya nyoka hatari katika kundi la epidae.

Wengi wanaaminu kuna nyoka mmoja tu aitwaye cobra, lakini ukweli ni kwamba kuna aina takriban 270 za viumbe za cobra. Hata hivyo, wataalamu wa elimu ya viumbe wanasema kuna wanaowaita kobra wa kweli 28 (true cobra), miongoni mwao ni huyo Indian cobra, Binosolate cobra, Cape cobra, Spitting cobra bila kumsahau mkubwa wao King cobra nk.

Indian cobra hapatikani katika maeneo yetu ya ukanda huu wa Afrika, bali wapo kwa wingi Asia ya Kusini katika nchi za l India, Pakistan, Bangladesh, Nepal na katika kisiwa cha Srilanka. Naye hutukuzwa sana katika imani na mila za kihindu na pia kule Srilanka katika dini ya Mabudha kiasi kwamba ni haramu kumuua katika sheria zao.

Sifa kubwa ya Indian cobra ni kutanuka shingoni na inatajwa kuwa ndiye nyoka pekee anayetanuka eneo hilo lakini kichwa kikabaki vilevile. Wengi wana urefu wa kati ya mita 1-mita 1.5 lakini wale wa Srilanka wapo mpaka kuanzia mita 2.1 hadi mita 2.2. Indian Cobra anaweza kuwa na rangi ya njano, kijivu, kahawia, nyekundu au nyeusi.

Uzazi

Indian cobra ni ‘oviparus’ yaani anataga mayai nje. Kipindi chao cha kutaga mayai ni mwezi wa Aprili hadi Julai. Nyoka hawa hutaga mayai kuanzia 10 hadi 30 katika mashimo ya panya au sungu sungu na baada ya siku 48 au 60 mayai yanaanguliwa.

Kama ilivyo kwa nyoka wengine, nyoka hawa pia hawana kawaida wala muda wa kulinda mayai yao. Ni King cobra pekee ndiye hulinda mayai yake. Pia, muda mfupi tu baada ya Indian cobra kutotoa mayai, vitoto vinavyozaliwa huanza kujitegemea.

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Indian cobra

  • Sumu ya Indian cobra ni kali sana na inaweza kuua.
  • Katika kundi la cobra, inazidiwa na ile ya King cobra na Cape cobra tu. Sumu ya Indian cobra inaua kwa njia mbili. Kwanza inalemaza (paralayse) mishipa ya fahamu (neuro toxin) na pili inadhuru moyo (cadio toxin).
  • Wengi wanadhani cobra wanasikia lakini ukweli ni kuwa hawasikii bali wanapata hisia kwa mitetemo ya ardhi (vibration) kupitia tumbo lake.
  • Katika maeneo niliyoyataja ambayo wanapatikana Indian cobra, basi tarajia kumkuta chinibya mti, juu ya mti, kwenye mawe na hata katika mashimo.
  • Sumu ya Indian cobra inaanza kufanya kazi kuanzia dakika 15 hadi masaa mawili, ingawa hali ni hiyohiyo pia kwa nyoka wote. Madaktari wamethibitisha kuwa, licha ya ukali wa sumu yake, Indian cobra lakini anaweza kumuuma mtu na asife iwapo tu atawahishwa hospitali kwa kuwa sasa dawa za kupambana na sumu za nyoka zipo.
  • Indian cobra hutumia ulimi kuwasaidia kutambua harufu ya kitu.
  • Umri wao wa kuishi ni miaka tisa ila cobra wengine wanaishi zaidi ya hapo.
  • Pamoja na hatari aliyokuwa nayo kwa viumbe wengi, akikutana na kiumbe kama njegere na ndege aina ya tai; Indian cobra huwa hana ujanja. Anakamatwa na kuliwa kirahisi tu.
  • Indian cobra huwa hapendi sana kumuuma binadamu labda umkanyage au uoneshe kutaka kumdhuru. Na akimgonga binadamu huwa haachii sumu yake yote bali kiasi kidogo tu tofauti anavyogonga viumbe wale ambao anawala.
  • Hata hivyo, hali ni kwa nyoka wote, si Indian cobra pekee. Ni kwa sababu hii ndio maana vifo vinavyosababishwa na nyoka sio vingi sana ukilinganisha na vifo mfano, vifo vinavyosababishwa na ajali.


from TIF https://ift.tt/2AEtiOr
via IFTTT

MAWAIDHA : Sheikh Nassor Bachu : Mauti na Maandilizi ya Siku ya Kiyama [Listen/Download]

Ulimwengu Wa Wamasoni (1)

Imetafsiriwa na Naaswir Haamid



Namna Gani Dunia Inaendeshwa Kitaalamu?
Mnamo Ogasti ya 2, 1990 majeshi ya Saddam Hussayn yalikwaruzana na vikosi vya ulinzi vya Kuwaiti iliyo tajiri kwa mafuta kwa khofu ya Iraqi kuivamia Saudi Arabia. Marekani na majeshi yake ya ushirika yalijimwaga ndani ya eneo la Arabuni kutengeneza himaya itakayojulikana kwa jina la Ngome ya Jangwani. Hayo yalipelekea kwenye meza ya mazungumzo ya kisiasa, maelewano na majibu yake ambayo mara moja yaliporomoka na kutotarajia lolote. Mnamo Ogasti ya 17, 1991 Ngome ya Jangwani ikawa ni Jangwa la Makombora.


Migongano hiyo ilishuhudiwa na mamilioni ya watu kupitia IF, CNN na BBC zikionesha propaganda za mtindo wa kuondosha majeshi ya Saddam kwa ushirikiano wa mataifa yaliyo juu kwenye teknolojia, kisiasa na nguvu za kiuchumi. Hata hivyo, kisichoeleweka ni kwamba kuanzia muono wake wa nje, vita hivyo vilitengenezwa, kuendeshwa na kufanyiwa hila na kundi lililo werevu. Kundi ambalo limejitengeneza kiudanganyifu kama mwanaadamu aliye na nguvu juu ya mamilioni ya majeshi yaliyo na nguvu kwa hila za nuclear. Mtu ambaye amepata kushikilia 1/5 ya mafuta yote duniani kwa usiku mmoja; hata hivyo, ukweli ni kwamba hakuwa chochote isipokuwa alikuwa na duru yake kama walivyo wengine. Ni kama mfano wa kijibwa ndani ya mpango mkuu wa Vita vya Ughaibuni na pia kama ni mpigaji filimbi. Wapigaji filimbi hao wa Vita hiyo sio kwamba hawaeleweki katika kuendesha matokeo makuu Duniani. Ukweli ni kwamba wamefanya hivyo kwa kipindi kirefu, sasa ni karne.

Kuanzia kujificha kwao katika kila vita vikuu wanavyoviongoza wao, mapinduzi na mgawanyo. Wana mikono yao katika kila kitu unachosoma, kila kitu unachosikia na kila kitu unachoona. Wamefanikiwa kuingiza ndani ya kila ubongo wa mtu aina za fikra zao na kutumbukiza watu wao kwenye mamlaka za nchi zilizo muhimu na ni kutokana na kivuli hichi wamekitumilia kuanzisha mfumo mpya wa kisiasa, mfumo mpya wa kiuchumi na bila ya shaka mfumo wa dini ulio sheheni dhambi. Lengo lao la moja kwa moja ni kuhodhi mamlaka ya ulimwengu mzima na watafanya kila waliwezalo kuzuia chochote kitakachokuwa ni kikwazo kufikia malengo yao. Shabaha ambayo imewekwa wazi ndani ya risala iliyotolewa na Raisi mstaafu wa Marekani, George Bush: "Kilicho mbele yenu ni zaidi ya nchi moja ndogo, ni fikra mpya na Mfumo Mpya Wa Ulimwengu".

Hata hivyo, asili ya mpango wa ulimwengu mzima haukuanzishwa ndani ya ofisi zaWhite House. Ukweli ni kwamba, mizizi yake imeanzia kwenye vita vyengine, huko mwaka 1095 sehemu za Claremont – Ufaransa. Karne ya 11 ya Ulaya ilitawaliwa na kanisa ambalo liliwakamata barabara watu, kuanzia mioyo yao hadi fikra zao. Nguvu hii ilimuwezesha Papa Erwin II kuanza vita alivyoviita takatifu (crusade) dhidi ya Kiongozi wa Kiislamu kwa jina la Vita Vya Msalaba kuikomboa ardhi ya Jerusalem. Ardhi ambayo ilikuwa chini ya himaya ya Waislamu tokea mwaka 637, lakini mwaka 1099 himaya hii ilikhitimishwa kwa umwagaji damu na ghafla moja ikafikia tamati.Kwa jina la Msalaba, wanawake walibakwa na kuuawa, watoto walikatwa mapanga na inasemekana kwamba damu iliogelea kwenye mitaa hadi kufikia urefu wa goti la farasi. Nje ya ardhi hii ya umwagaji damu kulikuwa na kundi linalotisha (terror) ambalo litafanya lolote kupata wanalotaka hata kwa gharama yoyote. Miaka ishirini baada ya kuchukuliwa Jerusalem, Baytul-Maqdis ilitekwa nyara na kundi la wapiganaji waliookoka wanaojiita wenyewe Wapiganaji Wa Hekalu La Sulaymaan au kiufupi Wapiganaji Wa Hekalu.

Huko Jerusalem, Wapiganaji Wa Hekalu walianza kuachana na mafunzo ya Ukristo mbali zaidi na zaidi. Walijifunza siri za usanii wa Kabala na mitindo ya kale ya uchawi wa Kiyahudi pamoja na miiko yake isiyoeleweka. Mayahudi hao walijifunza usanifu wa kale wa kipagani kutoka Misri kwenye kipindi cha utumwa chini ya Firauni na kuziendeleza ndani ya Babylon katika kipindi cha utawala wa Navakanazar. Mnamo mwaka 1307, Mfalme Philip wa Ufaransa aliwatia hatiani kwa mashitaka ya kumkataa Kristo, liwati na ibada za mizimu pamoja na uchawi. Mnamo mwaka 1314, Papa Claymont V alitangaza kwamba Mahekalu yote ni ya urithi wa Ukristo na kuamrisha kwa nguvu zote majengo hayo kushikiliwa. Kiongozi wao aitwae Chekthemolay alitekwa nyara na kuchomwa.

Hekalu hilo lilizungushiwa pembe zote na karibu ya kumaliza kazi hiyo itakayodumu milele, matumaini yaliibuka lakini walihitajika kutafuta mshirika wa usalama wao lakini sio kwa Ufaransa. Walihitaji nchi ambayo ipo kwenye shauku kubwa ya kupigania uhuru dhidi ya Waingereza, nchi ya Scotland ilifaa kwa hili. Nchi ambayo matumaini yake ya uhuru yalififia kutokana na kifo cha William Wallace. Hata hivyo, kwa Mfalme wa Scotland, Robert Bruce, kuwasili kwa Wapiganaji Wa Hekalu kulimpa zana ya siri mpya. Uzoefu wao ulipatikana kwa zaidi ya miaka mia mbili ya kupigana dhidi ya majeshi makubwa ya Uislamu, mapigano ambayo yaliwafanya kuwa wataalamu katika kujihami na upiganaji kuliko mapigano yoyote ambayo yanaweza kuletwa mbele yao.
Mnamo mwaka 1314, Wapiganaji Wa Hekalu waliungana na Robert Bruce na jeshi lake lilichukuwa sehemu za Ballack Burn, wakiwa tayari kusubiri mapigano pamoja na Waingereza. Uoni wa Robert Bruce kwenye pembe zote nne ulimuwezesha kulipiga vibaya mno jeshi lenye wapiganaji 25,000 lililo na nguvu la Muingereza dhidi ya wapiganaji 6,500 tu. Ndoto ya Scotland iliyo huru hatimaye ilifikiwa. Wapiganaji Wa Hekalu sasa wamerudi na hawatakuwa tayari tena kujikubalisha kushindwa.
Wakati huu, wataiendesha nchi hiyo kwa kuwadhibiti Wafalme wake na ili kuficha siri yao moja kati ya mawili lazima
yatendeke;ama wafe Wapiganaji Wa Hekalu wote au jina lao life. Wapiganaji Wa Hekalu ambao walitoroka Ulaya, hatimaye walizikwa huko Rovelin Chapel – Scotland (kama inavyoonekana kwenye picha hapo kushoto) jengo ambalo hadi leo linasimama kama ni alama ya kuwepo kwao nchini Uingereza. Vizazi vyao vilikuja kuwa na nguvu sahihi ya Scotland. Kifo cha Malkia Elizabeth I mnamo mwaka 1603, kiliiacha Uingereza bila ya mrithi wa kiti cha ufalme. Kwa mnasaba wa kizazi cha Mfalme James V wa Scotland ndiye atakayekuwa Mfalme wa Uingereza, na kwa kufanya hivyo, Scotland na Uingereza walilazimika kujiunga pamoja kuunda utawala mpya. Na nguvu ambayo ilikuwa nayo Wapiganaji Wa Hekalu juu ya Scotland iliwaenea kuwapa himaya thabiti ya Uingereza yote. Kwa zaidi ya miaka mia moja, Wapiganaji Wa Hekalu walizificha shughuli zao chinichini hadi walipojulikana kwa uchache na kukumbukwa kidogo. Hata hivyo, hawakusimama kukamata himaya thabiti ya Uingereza.
Kipindi chote hicho walikuwa wakipanga na kujipangua na kujiingiza ndani ya uongozi katika pembe zote za utawala. Mwaka 1717, Wapiganaji Wa Hekalu walijitokeza tena Uingereza wakiwa wengi na nguvu zaidi, na sasa wakiwa tayari kujibadilisha utambulisho wao utakaokuwa mbali na sifa yao ya hapo nyuma. Hawakupata hadhi isipokuwa kwa wakuu na watawala wa Uingereza na jina walilolijichagulia lilikuwa ni jina litakalojulikana na wengi lakini litakaloeleweka na wachache. [Sikubaliani na jina la "freemasons" linalotokana na Kifaransa "frerés masons" yaani ndugu wa Kimasoni. Ni Waingereza wasioelewa ndio waliolibadilisha kuwa Freemasons].

Utambulisho huo mpya kwa wajumbe wenye mamlaka za kuamrisha mambo uliwawezesha Wamasoni kuwa na sifa na heshima. Mwanachama wa mwanzo wa Kimasoni kimataifa alikuwa ni Frederick, Mtoto wa Mfalme wa Wales.Mwanachama wa hivi karibuni ni Phillip, Mtoto wa Mfalme wa Duke wa Edinburgh na mwandani wa karibu wa Malkia wa leo wa Uingereza Bibi Elizabeth II ambaye yeye mwenyewe ni mlezi wa zamani wa Wamasoni. Hata hivyo, nyuma ya milango iliyofungwa, Wamasoni walikuwa huru kujihusisha na maadili na kanuni za siri zilizokabidhiwa kwao na wazee wao, na hizi zikaja kuwa ni msingi wa kiwango cha uwanachama kiitwacho Degree. Wamasoni hawakujihusisha tu na mfumo wa Uingereza peke yake, mawazo yao yalikuwa mbali ya hapo. Miaka inayokuja badaye, wakati ambao Dunia na Marekani zitatumbukizwa kwenye vita na mapinduzi zaidi na zaidi, mmoja kumshinda mwenziwe. Hata hivyo, hayakuwa haya ni malengo makuu yaliyokuwa yakiaminika kuwa na athari kwa wenye kuonewa. Lakini ukweli ni kwamba mipango ilibuniwa na watu wachache maalumu, waliokuwa na njaa ya uongozi katika kila kitu. Yote haya yatatokea ndani ya nchi zao walizozikimbia kwa karne zilizopita na nchi hizi zitakuwa ni msingi wa Kuutawala Ulimwengu Mzima.

Katika karne ya 18, idadi kubwa ya Wafaransa walikuwa ni masikini wakati koo za kifalme na zile zinazojiweza zikiishi kwa starehe na ubadhirifu, kukaibuka tofauti kubwa baina ya matabaka haya mawili. Wamasoni watatumia hili kushurutisha madaraka juu yao na hivyo kusababisha mgongano mkubwa katika historia ya Ufaransa. Wamasoni wakachukua nafasi hiyo ya hali mbaya iliyojaa ghadhabu miongoni mwa Wafaransa na wakatumia hilo kufanikisha malengo yao kwa kupanga vizuri vita vya propaganda. Walivihodhi vyombo vyote vya habari kisawasawa na walivitumia kuyapinda maoni ya walio wengi. Magazeti yalitezwa nguvu kutangaza mwisho wa utawala wa kifalme na kuanzisha jamii inayofuata uhuru, usawa na ushurutishwaji.

Mamilioni ya fedha yalitumika kuweka chini ya uangalizi hali ya kisiasa ya Ufaransa. Wanasiasa wanaofadhiliwa na Wamasoni walihamasisha dhana ya Kimasoni, siri zilizojikita za Wamasoni zilifunguliwa kwa wajumbe wa jeshi la Ufaransa, maofisa wa juu na makamanda waliendeshwa kwa kutumia mawazo ya Wamasoni. Wamasoni walifanya kila jitihada kuwatawala wanasiasa na majeshi ya Ufaransa chini ya Umasoni. Ilipofika tarehe 14 Julai 1789, kundi la watu lilivamia jela ya Basteel, Paris. Alama za upinzani uliojikita dhidi ya watawala wa Ufaransa hapo zilidhihirika kwa watu wengi kujitokeza sehemu tofauti nchini Ufaransa.

Huko vijijini na mijini, watu walitoa mawazo yao yaliyojaa chuki dhidi ya utawala wa kifalme. Lakini chuki hizo za Wafaransa hazikuweza kuzimwa moto hadi kufikia mwaka 1793. Mnamo tarehe 21 Januari ya mwaka huo huo, Mfalme Louis XVI alikatwa kichwa mbele ya umati wa watu na kuwa ni sababu ya kufikia kikomo utawala wa Kifalme wa Kifaransa na kusafisha njia ya taifa jengine la Kimasoni barani Ulaya. Kutokana na ufalme huo kuondoka, ilionekana kana kwamba hakuna kitakachowazuia Wamasoni kuitawala Ufaransa kisawasawa. Hata hivyo, kilichotokezea badaye kitawaacha Wamasoni katika kilema kibaya na kitakachotokezea badaye hakika hakikuwa ni kwa mujibu wa mipango ya Kimasoni.

Kijana mmoja kwa jina la Napoleon Bonarparte alikuwa ni askari. Yeye alikosea kidogo kuipeleka Ufaransa kwenye vita vibaya kabisa pamoja na Ulaya pale alipoacha kuufuata muziki wa Kimasoni. Napoleon alijitangaza mwenyewe kwamba yeye ndie Mtawala wa milele wa Ufaransa. Napoleon alilazimishwa kuachana na ufalme huo mnamo mwaka 1814 na alihamishwa kisiwani Corsica. Hata hivyo, mwaka 1815 Napoleon alitokeza kwa mara nyengine tena Paris akihamasisha jeshi jipya likiwa tayari na vita vipya huko Ulaya. Hapo Wamasoni walikuwa na tatizo kubwa mikononi mwao. Uingereza na washirika wake wa Kimasoni hawakuweza kufadhili vita virefu dhidi ya Napoleon bila ya kukaribia kufilisika.

Msaada ulikuja kutoka kwa mtu asiye marufu kabisa. Nathan Rothschild alikuwa ni mkuu akiongoza benki ya kifamilia, lakini kwasababu ya hadhi yao ya Uyahudi, walilazimishwa kufanya kazi kwa kutumia kivuli cha watu wengine. Rothschild alihakikisha kutumia nafasi ya kuwakomboa watu wake na mara nyingi mwenyewe peke yake akidai kurudishwa utambulisho wa Wayahudi kama ni watu walio sawa ndani ya Ulaya, wakiwa nao wana haki ya kufanya biashara wazi wazi. Na kama Wamasoni watazikataa fedha zao mara zote zitaenda kwa Napoleon.

Wamasoni hawakuwa na khiyari isipokuwa kukubali, na biashara ya mkopo ikakamilishwa. Mnamo mwaka 1815 askari wa Kiingereza, Kidachi na Kirusi walikanyaga ardhi ya Waterloo nchini Ubelgiji ambapo walikutana na vikosi vya Napoleon na kuwashinda. Napoleon mara hii alikamatwa na kutorudi tena Ufaransa ambayo hatimaye sasa ilikuwa chini ya muongozo wa Wamasoni. Ingawa wanahistoira wametaja machache katika mahusiano ya Wamasoni ndani ya mapinduzi, Wamasoni wenyewe walilazimika kudhihirisha utambulisho wao wakati wa kipindi hichi muhimu katika historia. Mnamo mwaka 1904 Marc Vadourasamboakiwa ni Mmasoni alitangaza waraka wa makubaliano: "Wamasoni wamefanya (mapinduzi) kwa kujificha lakini kwa namna madhubuti ya kutayarisha mapinduzi, hivyo tupo na makubaliano ya moja kwa moja, Wamasoni wakiwa ndio waanzilishi wa mapinduzi na sifa nilizozipata kutoka kushoto na ambazo nimeridhika nazo zinaonesha kwamba nyinyi waungwana mnakubaliana na mimi kwamba walikuwa ni Wamasoni waliofanya Mapinduzi ya Ufaransa."

Wavumbuzi wa taifa la Marekani walipokanyaga mguu katika jabali la Plymouth, sio tu kwamba walileta watu wasio na haki ya uraia bali pia walileta fikra za Kimasoni za Ulaya. Yale madhila yaliyokimbiwa Ulaya na hao wavumbuzi wa Marekani pia yaliweza kuonekana ndani ya ardhi mpya kwenye mfumo wa utawala wa kibabe wa Kiingereza. Ili kudhibiti na kuendesha katika hali zote taifa hilo jipya la Marekani, Wamasoni walitumia njia zile zile walizotumia kuiteka Ufaransa.

Ingawa ufalme wa Uingereza ulikuwa ukiongozwa na Wamasoni, vita vya Marekani vya kudai uhuru wa Marekani vilihitajika. Na watu walioshiriki ndani ya vita hivyo waligharamika kutimiza ndoto za Wamasoni. Hisia za watu ziliharibiwa katika hamaki na kama zilivyo ghadhabu za Ufaransa zilisababisha vita. Hata hivyo, wakati huu makosa yaliyofanywa huko nyuma hayatarudiwa. Ushindani waliokutana nao Wamasoni dhidi ya Napoleon na jeshi lake huko Ulaya uliwafunza adabu Wamasoni. Kiongozi yeyote wa upinzani anayefuatia ni lazima atekeleze matakwa ya Kimasoni na njia bora ya kufanya hilo ni kuhakikisha kiongozi mwenyewe ni Mmasoni. Na kiongozi aliyepigana dhidi ya Waingereza hakuwa mwengine isipokuwa ni George Washington.

Mnamo tarehe 4 ya Julai mwaka 1776, tamko la uhuru lilitangazwa.
Tarehe 17 Oktoba 1781, hatimaye Waingereza walishindwa na kuyasalimisha makoloni kwa Wamarekani na Taifa la mwanzo la Kimasoni likazaliwa, taifa litakalowakilisha Umasoni katika kila njia. Alama ya kuwepo Umasoni ndani ya Marekani inaonekana wazi kwenye sarafu ya dola ambayo inabeba picha ya raisi wa mwanzo wa Kimasoni George Washington ndani ya ulimwengu, na picha ya alama ya Kimasoni iitwayo "Jicho Moja Linaloona Kila Kitu."
Kumbukumbu zinaonesha kwamba udhibiti na uharibifu wa maoni ya kisiasa ni zana kuu inayotumiwa na Wamasoni katika kushikilia nchi na mataifa. Pale tu watawala na wanasiasa wa nchi wanapodhibitiwa, basi sheria na mfumo wa siasa unaweza mara moja kubadilishwa kwa mujibu wa matakwa yao. Hata hivyo, kuutawala mwili haina maana kwamba umeitawala akili.
Wamasoni wanaelewa kwamba mipango yao ya Serikali Moja inafungamana moja kwa moja na
kuwalainisha watu katika matakwa yao  na hivyo kudhibiti upinzani kutokana na yale wanayoyafanya na tishio kubwa dhidi ya mipango yao ni akili iliyo na fikra huru. Hili kwao ni tishio kubwa kuliko hata jeshi au sheria. Ili kudhibiti tishio hili na kufanikisha malengo yao, Wamasoni wametengeneza mpango wa hatari usiowahi kutengenezwa hapo kabla. Mpango ambao utatawala kila nyanja ya mwanadamu, maisha yako na zana wanazotumia dhidi yako zipo ndani ya nyumba yako mwenyewe, zikikuburudisha wewe pamoja na watoto wako na kidogo kidogo zikikutawala bila ya wewe mwenyewe kulitambua hilo. Ndani ya jamii ya leo, watu wanatumia muda zaidi na zaidi katika vyombo vya kisasa. Luninga, Sinema, Michezo ya Kompyuta, Tovuti, Michezo na vipindi vya ulaghai na Miziki iliyoenea imeganda ndani ya maisha yao.

Na kweli vitu hivi vinasababisha upanuzi wa haraka wa habari ambazo wewe unachukua ndani ya akili yako aidha kwa kutambua ama bila ya kutambua. Habari ndani ya jamii zinaoneshwa katika maadili na tamaduni, tofauti ya zuri na baya hadi namna ya jamii na uchumi unavyotakiwa kutengenezwa. Haya yote yapo mbele ya macho yako katika kila siku ya maisha yako.

Vyombo hivi vya habari, kwa nafasi kubwa vinatumika katika kuweka msingi wa kuamua uoni wa mtu kwa Ulimwengu na kila kitu kilicho mbele yake. Hivyo, kila mtu anapodhibitiwa na vyombo vya habari kama hivi bila ya shaka ataathirika na nguvu za kutawaliwa, na kwa kweli idadi kubwa ya watu duniani inaathirika na fikra zao, na hili hakika ndilo Wamasoni wanaloendelea kuvumbua.

Hakika Wamasoni wanatumia vyombo vya starehe kushurutisha watu katika namna zao za fikra ima wazi wazi au kwa kujificha. Taratibu wanazotumia zinatofautiana lakini lengo lao ni hilo hilo kuingiza imani zao, fikra zao na madhumuni yao kwako wewe katika namna ambayo unaanza kuwafikiria kama ni watu wako. Ushahidi wa kuwepo kwao ndani ya starehe marufu umeenea kila pahala. Ushirikishwaji wa Wamasoni ndani ya uzalishaji huu sio jambo geni. Hail ni miongoni mwa watunzi wa zamani, Wolf Gang Amadeus, Mozart ambaye yeye mwenyewe ni Mmasoni ametengeneza muziki ambao ulikuwa na uonekano wa wazi wa Umasoni. Muziki huo umetungwa kutokana na hadithi iliyochukuliwa kutoka kwa Wamisri wa kale Avysus na Cyrus. Haki za wapagani katika hadithi za kutungwa za kale za Misri za Kabala ni miongoni mwa sifa kuu za Kimasoni. Ni kutokana na asili ya upagani huu wa Kimisri ndio ikapatikana alama ya Shina La Jicho Moja.
Ushahidi wa kuwepo kwa Wamasoni pia unapatikana sana ndani ya miziki marufu ya sasa. Kwa mfano Michael Jackson ambaye anatambulika kama ni mfalme wa pop na anasifika kuwa ni mburudishaji wa wakati huu (wakati huo ilipoandikwa makala hii). Pia anazalisha na kuuza albamu nyingi tu duniani kote, lakini pia anaweza kuunganishwa na Umasoni. Gamba la albamu lake la "Dangerous" lina sifa ya kushangaza kwa kuwa na alama ya Jicho Moja, na pia kuna picha ya mfano wa maji ya mto yanayowaka kwa moto. Inaonesha wazi kwamba yeyote anayeingia ndani ya maji hakika atatumbukia ndani ya moto. Gamba pia lina fumbo ya picha ya mtu mwenye kipara kama ni Alistair Crowley. Yeye mwenyewe alikuwa ni Mmasoni na badaye akawa Mlokole na kuandika kitabu cha "Sheria Mpya Ya Mwanadamu" ambacho kimeeleza ndani yake kwamba siku moja kitachukua nafasi ya Qur-aan kama ni sheria ya mwanadamu.

Ulinganisho huo baina ya Umasoni na fumbo hauishii hapo. Uzalishaji wa miziki inayodhibitiwa na Wamasoni inaingizwa vitendawili vyenye ujumbe wa kishetani. Uchezeshwaji wa kuanza mwisho kuja mwanzo (back tracking) ni njama zinazotumiwa katika kuhifadhi ujumbe ili kuufanya kuwa ni sauti ya muziki katika namna ambayo zinatambuliwa pale tu zinapochezeshwa kwa mtindo wa mwisho kuja mwanzo. Pale inapochezeshwa kwenda mbele, msikilizaji hataelewa hata kidogo ujumbe unaochezeshwa.

Ingawa msikilizaji hatakuwa makini kwamba akili yake inakamata ujumbe asiouelewa, lakini katika siku za mbele ujumbe kama huu unaweza kuhifadhiwa ndani ya akili ya mtu na unaweza kuathiri tabia za mtu ama maamuzi yake. Katika namna nyingi, uchezeshwaji wa muziki wa kuanza mwisho kuja mwanzo ni mfumo wa kumfanya mtu atende mambo bila ya kujitambua na ni mfumo wenye kuharibu mara moja. Mfano wa mwanzo wa uchezeshwaji huu ni kutoka kwa msanii wa kike aitwaye Madonna. Unapatikana katika albamu yake marufu kwenye nyimbo ya "Like a Prayer." Hata hivyo, kama utakavyosikia sio mungu anayeonekana kuombwa katika nyimbo hiyo bali ni shetani. Inapochezeshwa kwa mtindo wa mwisho kuja mwanzo maneno ya "Ah shetani tuitikie" yanasikika wazi wazi. Pia alama ya Jicho Moja imetumika miongoni mwa video za nyimbo zake Madonna. Ambapo jicho moja linaonekana likitoka katika kichwa chake. Pia anaonekana ndani ya video ambapo amesimama katika maandishi, uchunguzi wa karibu unaonesha kwamba maandishi haya ni ya Kiarabu katika lugha ya Qur-aan.

Mfano mwengine wa uchezeshwaji huu unapatikana katika kundi la "The Eagles" na nyimbo yao inayoitwa "Hotel California". Maneno haya yanapochezeshwa kwa mtindo wa mwisho kuja mwanzo yanasikika maneno haya kwa uwazi "Ndio shetani". Na pia hadithi yake wenyewe ni ya kishetani. California ya hapo sio hoteli bali ni mtaa ndani ya Marekani unaoitwa California. Ni katika mtaa huu ambapo makao makuu ya kanisa yalipatikana, lakini sio aina ya kanisa ambalo mtu anaweza kufikiria, bali ni kanisa ambalo baadhi wameliita "Kanisa la shetani." Lililo ongozwa na kuanzishwa na Anthony Sans Delivy, muandishi wa Biblia ya Kishetani. Inaonesha mafundisho ya kanisa hili yamekuwa ndio imani ya watu marufu katika uzalishaji wa bidhaa za starehe kwa waimbaji wote, kuanzia rock hadi main streams, wengine wamefikia hatua ya kushajiisha imani za kanisa hili. Miongoni mwa mjumbe anayetuhumiwa kuhusika na kanisa hili ni mwimbaji wa Rolling Stones anayeitwa Mick Jagger aliyeandika nyimbo ya "Sympathy for the Devil". Inaonesha kwamba kile kilichoanza kama ni Jumuiya ya Wakristo badaye ikabadilika na kuwa ni dini iliyorithiwa hata kwa Wakristo na sasa ina sifa za kishetani zilizochanganywa ndani yake. Ulimwengu wote wa burudani umegandana na ushahidi wa kuwepo kwa Wamasoni wazi wazi au kuzitangaza imani zao kwa fahari kabisa.
(Tanbihi: Mwandishi wa makala hii kutoa mifano ya hiyo miziki, haina maana kuwa miziki inakubalika katika Uislamu, bali ni njia ya kuonyesha upotofu na ushetani wa mielekeo hiyo na inayoambatana nayo. Muziki ni haramu katika Uislamu, na zaidi msomaji asome na asikilize humu:


Hili linadhihirishwa zaidi ndani ya filamu marufu katika big screen au small screen, kwa gharama kubwa za filamu za Hollywood hadi cartoons za kawaida. Wamasoni hawakuacha kuingiza hamasa zao katika kitu chochote ili kushajihisha ujumbe wao wa serikali moja. Matt Growning ambaye ni mtengenezaji wa kipindi cha cartoonmarufu katika historia ya luninga. "The Simpsons" ni cartoon inayotaka uhuru wa madaraka. Matt Growming mwenyewe kwa uwazi kabisa ametangaza kwamba anataka kuziweka fikra zake za kisiasa ndani ya kazi zake. Lakini anataka kufanya hivi katika namna ambayo watu watakubaliana kwa urahisi na mawazo yake. Na njia aliyotumia kulifanya hili ni cartoon ya kitalamu inayoitwa "The Simpsons". Sasa nini haswa hakika Simpsons inatufunza sisi na watoto wetu? Kuna mafunzo mengi (mabaya) yanayofundishwa kwetu, haya yanahusu kutotii utawala aidha ikiwa ni wa mzazi au wa serikali. Tabia mbaya na kutofuata amri ni njia ambazo zinatumika kupata hadhi miongoni mwa watu na kwamba ujahili ni sifa nzuri wakati elimu ni kitu kilichopitwa na wakati. Hata hivyo, kitu kinachotisha haswa ni mambo yaliyojificha chini ndani ya miongoni mwa vipindi vyake.

Kipindi ambacho baba mtu wa familia anayeitwa Homer Simpson anawahamakia kundi linaloitwa stone cutters. Alipojiunga na kundi hilo, wafuasi wenziwe wanatambua alama ya kuzaliwa inayofanya kundi lote kumtangaza kuwa ni aliyechaguliwa lakini kwa hadhi yake na tabia zake yeye Homer Simpson anajidanganya mwenyewe kwa kujidhania kwamba yeye ni mungu. Mtu anaweza kulidharau hilo na kuelewa kwamba jambo hilo ni la cartoon ya kitoto, burudani na kitu kisicho na dhara. Lakini nguvu iliyokuwa nayo kwa watazamaji inafanya kuwa ni njia ya kuathiri watu kwa kuwabadilisha bila ya wenyewe kujitambua. Watengenezaji wake wanakiri kwamba wanaingiza propaganda zao za fikra za kisiasa kwa watazamaji katika njia iliyojificha. Fikra zinazoenezwa kupitia luninga ya nyumbani zinasambaa mbali sana kuliko michezo inayooneshwa sinema. Na ni kupitia vyombo hivi kwamba dhana mpya inawasilishwa. Nayo ni dhana ya kiongozi mmoja kwa ulimwengu mzima.


Inaendelea in  Shaa Allaah…


from Muislamu https://ift.tt/2ETpWLt
via IFTTT

40. Anayepinga kitu katika majina na sifa za Allaah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Kauli ya Allaah (Ta´ala):

                                                        وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِالرَّحْمَنِ

“… ilihali wao wanamkanusha Mwingi wa rehema.” (ar-Ra´d 13:30)

2- al-Bukhaariy amepokea katika “as-Swahiyh” yake kwamba ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Waelezeni watu kwa wanayoyajua. Je, mnataka akadhibishwe Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?”[1]

3- ´Abdur-Razzaaq amepokea kutoka kwa Ma´mar, kutoka kwa Ibn Twaawuus, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye alimuona mtu akisisimka wakati aliposikia Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) iliotaja sifa za Allaah akiwa ni mwenye kulipinga hilo ambapo akasema:

“Ni kitu gani kinachowatia woga watu hawa? Wanafanya woga kwa Aayah zilizo wazi ilihali wanaegemea Aayah sizizokuwa waz.”[2]

Pindi Quraysh walipomsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitaja Mwingi wa rehema wakapinga hilo. Ndipo Allaah akateremsha juu yao:

وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِالرَّحْمَنِ

“… ilihali wao wanamkanusha Mwingi wa rehema.”

MAELEZO

Mlango huu mwandishi ameutunga kwa ajili ya kubainisha uwajibu wa kuthibitisha majina na sifa za Allaah kwa njia inayolingana Naye (Subhaanahu wa Ta´ala) pasi na kupotosha, kukanusha, kuzifanyia namna, kuzifananisha wala kuzigeuza. Mtu hatakiwi kudhanganyika na maoni ya Mu´tazilah na watu wa batili wengine. Ni wajibu kwake kuchukua yale yaliyosemwa na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika Maswahabah na wale waliofuata mwenendo wao. Hii ndio ´Aqiydah iliofikishwa na Mitume. Wote walikuwa ni wenye kuthibitisha majina na sifa za Allaah kwa njia inayolingana Naye. Maswahabah na wale wote waliowafuata kwa wema walizipitisha Aayah na Hadiyth zinazozungumzia sifa kama zilivyokuja na wakathibitisha zile dalili za majina na sifa. Yote hayo kwa ajili ya kutendea kazi maneno Yake Allaah:

قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ اللَّهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

“Sema: “Yeye ni Allaah – Mmoja pekee, Allaah aliyekamilika, mkusudiwa wa haja zote. Hakuzaa na wala hakuzaliwa, na wala hakuna yeyote anayefanana na kulingana Naye.” (al-Ikhlaasw 112:01-04)

فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

”Basi msimpigie Allaah mifano! Hakika Allaah anajua nanyi hamjui.” (al-Israa´ 16:74)

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (ash-Shuuraa 42:11)

هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا

“Je, unamjua yeyote mwenye jina kama Lake?” (Maryam 19:65)

 Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hana Mwenye jina kama Lake wala anayelingana Naye.

Kuhusu Jahmiyyah wao wamekanusha majina na sifa za Allaah na wakayapindisha majina. Maoni yao yanapelekea kukanusha kabisa kabisa uwepo wa Allaah. Kwa ajili hiyo ndio maana Ahl-us-Sunnah wamewakufurisha. Ni wajibu kuwaua ikiwa hawakutubia. Wanatakiwa kuambiwa kutubia kwa sababu ya kupinga kwao yale yaliyotajwa katika Qur-aan na Sunnah na maafikiano. Mwandishi ametaja kichwa cha khabari kwa kutokufungamanisha pasi na kumhukumu yule mwenye kukanusha majina na sifa za Allaah. Hata hivyo hukumu yake ni kwamba ni kafiri.

 1- Kauli ya Allaah (Ta´ala):

                                                        وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِالرَّحْمَنِ

“… ilihali wao wanamkanusha Mwingi wa rehema.”

Allaah (Ta´ala) amebainisha kwamba Mwingi wa rehema ndio Mola na Mungu wetu na kwamba yule mwenye kumkufuru Mwingi wa rehema basi amemkufuru Allaah. Kwa hivyo ni wajibu kwa muumini kutahadhari na sifa za wapotevu hawa na afuate mwenendo wa wanachuoni na waumini. Allaah ameonelea kule kukanusha kwao sifa hii ni kumkufuru Mwingi wa huruma na ni dalili inayofahamisha kwamba mwenye kukanusha sifa amekufuru.

2- al-Bukhaariy amepokea katika “as-Swahiyh” yake kwamba ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Waelezeni watu kwa wanayoyajua. Je, mnataka akadhibishwe Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?”

Mtu ambaye anawawaidhi na kuwakumbusha wengine basi anatakiwa kutumia matamshi na usulubu wanaoutambua ili waweze kustafidi na kufaidika. Kila watu wana usulubu wao. Ukiwazungumzisha watu kwa njia wasiyoitambua basi kuna khatari wakaja kukufahamu vibaya. Haijalishi kitu maudhui yanahusiana na majina, sifa au hukumu za Allaah. Haijalishi kitu lugha unayozungumza ni kiarabu, kingereza, urdu au lugha nyingine. Hata waarabu wenyewe wanaelewa tofauti. Zungumza na watu wote kwa njia waliyozowea ili waweze kukifahamu kile unachokisema na ili wasije kumkadhibisha Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Wale wanaomkadhibisha Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika sifa za Allaah wako katika khatari kubwa. Kwa sababu wamezipindisha sifa za Allaah kinyume na tafsiri zake na wamezizungumzia kwa njia isiyostahiki mpaka mwishowe wakazikanusha. Wengi wao kuna uwezekano wakawa wamezifahamu kimakosa kwa sababu sio waarabu. Baadhi ya Salaf wamesema kuwa ´Amr bin ´Ubayd amesema kuwa watenda madhambi watadumishwa Motoni milele kwa sababu Allaah kawaahidi hilo. Ndipo Salaf wakamwambia kwamba Allaah anaweza kuvunja ahadi ya adhabu na hawezi kuvunja ahadi ya thawabu. Kuvunja ahadi ya adhabu ni utukufu na kuvunja ahadi ya thawabu ni kusemwa vibaya. Ndipo wakamwambia:

“Umetumbukia katika hayo kwa sababu sio mwarabu.”

Bi maana unadhani kuwa ni jambo baya kuvunja ahadi ya adhabu. Si kweli. Mshairi amesema:

Mimi nikiahidi kumuadhibu au kumlipa

nitaivunja ahadi yangu ya kumuadhibu na kutimiza ahadi yangu ya kumlipa

Hii ni sifa.

3- ´Abdur-Razzaaq amepokea kutoka kwa Ma´mar, kutoka kwa Ibn Twaawuus, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye alimuona mtu akisisimka wakati aliposikia Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) iliotaja sifa za Allaah akiwa ni mwenye kulipinga hilo ambapo akasema:

“Ni kitu gani kinachowatia woga watu hawa? Wanafanya woga kwa Aayah zilizo wazi ilihali wanaegemea Aayah sizizokuwa waz.”

Pindi Quraysh walipomsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitaja Mwingi wa rehema wakapinga hilo. Ndipo Allaah akawateremshia juu yao:

وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِالرَّحْمَنِ

“… ilihali wao wanamkanusha Mwingi wa rehema.”

Wakati wanaposikia Aayah za wazi na Hadiyth wanasikia woga na wanakuwa na unyenyekevu. Wanaposikia Aayah kuhusu sifa za Allaah zinawatatiza na wanaangamia kwa sababu ya kutatizika na kukanusha. Hii ni dalili inayoonyesha kuwa jambo hili ni la tokea hapo kale na kwamba kitu kama hicho kilikuwepo tokea hapo wakati wa Maswahabah. Wanaangamia kwa sababu ya Aayah za Qur-aan na Hadiyth ambazo wanaona kuwa haziko wazi na wanazitilia mashaka. Ni dalili inayofahamisha kwamba kupinga na kutilia mashaka yale Allaah aliyowabainishia waja Wake ni maangamivu.

Haki ni kuamini yale yote yaliyokhabarishwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ukifahamu kilichosemwa, ni jambo zuri na himdi zote ni za Allaah, na kama bado hujafahamu, basi unachotakiwa kusema ni kwamba Allaah ndiye mjuzi zaidi na uwaulize wanachuoni. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaamini yale yote yaliyotajwa katika Qur-aan na Sunnah. Wameridhishwa nayo na wanayatendea kazi. Pindi wanapokutana na kitu ambacho kimewatatiza basi wanakirudisha katika zile Aayah ambazo ziko wazi na bainifu na kwa njia hiyo wanakifahamu. Hawaifanyi Qur-aan wala Sunnah kuwa ni vyenye kugongana. Hawatilii mashaka. Wanatambua kuwa yale maandiko ambayo hayako wazi hayapingani na yale yaliyo wazi. Bali uhakika wa mambo yale maandiko yasiyokuwa wazi ni sehemu ya yale yaliyo wazi. Yale yote ambayo hawakuyafahamu wanamwacha Yeye ambaye anayajua yaliyofichikana ayashughulikie ambaye ni Allaah (Subhaanah). Kuhusu maana yake ni yenye kufahamika katika lugha ya kiarabu ambayo Allaah amewazungumzisha watu kwayo. Kwa ajili hiyo Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema wakati alipoulizwa swali kuhusu kulingana kwa Allaah:

“Kulingana kunatambulika. Namna haijulikani. Kuuliza juu ya hilo ni Bid´ah.”

Bi maana ni Bid´ah kuuliza kuhusu namna. Amebainisha (Rahimahu Allaah) kwamba kulingana kunatambulika na kwamba namna haitambuliki.

Faida:

Mwenye kusema kwamba Pepo na Moto vitatokomea/vitakwisha ni kafiri. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

وَأَمَّا الَّذِينَ سُعِدُوا فَفِي الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۖ عَطَاءً غَيْرَ مَجْذُوذٍ

“Ama wale walio furahani, basi watakuwa katika mabustani, ni wenye kudumu ndani yake zitakavyodumu mbingu na ardhi isipokuwa atakavyo Mola wako – ni hiba isiyokatizwa.” (Huud 11:108)

لَا يَمَسُّهُمْ فِيهَا نَصَبٌ وَمَا هُم مِّنْهَا بِمُخْرَجِينَ

“Hautowapata ndani yake uchovu nao humo hawatotolewa.” (al-Hijr 15:48)

Kadhalika ni kosa kusema kwamba Moto utakwisha. Maoni sahihi walionayo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kwamba Moto hautakwisha.

Faida:

Waislamu wamekubaliana juu ya kwamba ardhi imetulizana na jua ndio linalozunguka. Wale wanaosema kwamba ardhi ndio inayolizunguka jua wanachomaanisha ni kwamba ardhi ndio iliyotulizana, jambo ambalo ni kufuru:

وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ۚذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ

“Na jua linatembea hadi matulio yake, hayo ni matengenezo ya Mwenye nguvu kabisa, mjuzi.” (Yaa Siyn 36:38)

[1] al-Bukhaariy (129).

[2] al-Muswannaf (20895). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (485).



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2zkMxKH
via IFTTT

39. Mlango maneno Yake (Ta´ala) “Je, huoni wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka wahukumiane kwa Twaaghuut na hali wameamrishwa wakanushe hiyo, na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali kabisa”

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُواْ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُواْ أَن يَكْفُرُواْ بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلاَلاً بَعِيدًا

”Je, huoni wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka wahukumiane kwa Twaaghuut na hali wameamrishwa wakanushe hiyo, na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali kabisa.” (an-Nisaa´ 04:60)

2-

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لاَ تُفْسِدُواْ فِي الأَرْضِ قَالُواْ إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ

”Na wanapoambiwa: “Msifanye uharibifu katika ardhi.” Husema: “Hakika sisi ni watengenezaji.” (al-Baqarah 02:11)

3-

وَلاَ تُفْسِدُواْ فِي الأَرْضِ بَعْدَ إِصْلاَحِهَا

”Na wala msifanye ufisadi katika ardhi baada ya kutengenea kwake.” (al-A´raaf 07:56)

4-

أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ

”Je, wanataka [uwahukumu kwa] hukumu ya kipindi cha makafiri?” (al-Maaidah 05:50)

5- ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hatoamini mmoja wenu mpaka matamanio yake yawe ni yenye kufuata yale niliyokuja nayo.”[1]

an-Nawawiy amesema:

“Hadiyth ni Swahiyh. Nimeipokea katika “Kitaab-ul-Hujjah” kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

6- ash-Sha´biy amesema:

“Kulikuwa ugomvi baina ya mtu mmoja mnafiki na mwingine myahudi. Yule myahudi akasema: “Twende kwa Muhammad atuhukumu.” Mnafiki yule alijua kuwa hachukui rushwa. Mnafiki yule akasema: “Twende kwa mayahudi watuhukumu.” Kwa kujua kwake kuwa wao wanachukua rushwa. Hivyo wote wawili wakakubaliana kumwendea kuhani Juhaynah ili awahukumu. Ndipo kukateremka:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُواْ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُواْ أَن يَكْفُرُواْ بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلاَلاً بَعِيدًا

”Je, huoni wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka wahukumiane kwa Twaaghuut na hali wameamrishwa wakanushe hiyo, na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali kabisa.” (an-Nisaa´ 04:60)

Kuna maoni mengine yanayosema kwamba iliteremka juu ya watu wawili waliogombana ambapo mmoja wao akasema:

“Hebu tumpelekee kesi yetu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aihukumu.” Yule mwengine akasema: “Wacha tumpelekee Ka´b bin al-Ashraf.” Mwishowe wakampelekea nayo ´Umar mmoja wao akamueleza kisa kilivyokuwa. Akamuuliza yule ambaye hakuridhia ipelekwe kesi kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Mambo ni hivyo?” Mtu yule akasema: “Ndio.” ´Umar akampiga kwa upanga na akamuua.”

MAELEZO

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُواْ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُواْ أَن يَكْفُرُواْ بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلاَلاً بَعِيدًا

”Je, huoni wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka wahukumiane kwa Twaaghuut na hali wameamrishwa wakanushe hiyo, na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali kabisa.”

Anachotaka mwandishi ni kuwatahadharisha watu kuhukumiana kinyume na Shari´ah ya Allaah. Lililo la wajibu ni kuhukumian na Shari´ah ya Allaah katika mambo yote. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Naapa kwa Mola wako! Hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana kati yao kisha wasipate katika nyoyo zao uzito katika yale uliyohukumu na wajisalimishe kwa kujisalimisha” (an-Nisaa´ 04:65)

وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ

“Wahukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Allaah.” (al-Maaidah 05:49)

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ

“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.” (al-Maaidah 05:44)

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ

“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu.” (al-Maaidah 05:45)

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ

“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki.” (al-Maaidah 05:47)

Haya yote yanafahamisha juu ya uwajibu wa kuhukumiana na Shari´ah ya Allaah na kwamba haijuzu kuhukumiana na kitu kingine. Huu ni msingi ambao kuna maafikiano juu yake.

Aayah inabainisha vilevile kwamba wapo watu wanaodai imani na Uislamu ilihali ukweli wa mambo sivo hivyo;  bali ni wanafiki. Kunapotokea kitu basi wanataka wahukumiwe kinyume na Shari´ah ya Allaah na Twaaghuut. Twaaghuut ni kila chenye kuabudiwa badala ya Allaah na mwenye kuhukumu kinyume na Shari´ah ya Allaah kwa kukusudia na kwa matamanio. Wanafiki wanataka wahukumiwe na yule ambaye anaafikiana na matamanio yao na ambaye anapokea rushwa ili aweze kuwapatia haki wao. Hii ni dalili juu ya unafiki wao. Wanafiki kazi yao ni kuipa mgongo haki. Allaah (Ta´ala) amesema:

ذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا

“Wanapoambiwa: “Njooni kwenye yale aliyoyateremsha Allaah na kwa Mtume”, basi utawaona wanafiki wanakugeukilia mbali kwa mkengeuko.” (an-Nisaa´ 04:61)

Kwa hivyo ni wajibu kwa mtu kutahadhari nao na tabia zao mbaya.

2-

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لاَ تُفْسِدُواْ فِي الأَرْضِ قَالُواْ إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ

”Na wanapoambiwa: “Msifanye uharibifu katika ardhi.” Husema: “Hakika sisi ni watengenezaji.”

Wanadai kwamba ni wenye kutengeneza, lakini uhakika wa mambo ni wenye kuharibu kwa sababu ya ujinga wao, upotevu wao na unafiki wao. Akili zao zimepinduliwa chini juu na ndio maana wakachukulia ufisadi kuwa ni matengenezo. Kwa ajili hii Allaah (Ta´ala) akasema:

أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَـٰكِن لَّا يَشْعُرُونَ

“Tanabahi! Hakika wao ndio mafisadi lakini hawahisi.” (al-Baqarah 02:12)

3-

وَلاَ تُفْسِدُواْ فِي الأَرْضِ بَعْدَ إِصْلاَحِهَا

”Na wala msifanye ufisadi katika ardhi baada ya kutengenea kwake.”

Kutengenea kwa ardhi kunakuwa kwa kufuata na kuhukumiana kwa Shari´ah. Inaharibiwa kwa kwenda kinyume na amri ya Allaah na kuhukumiana na sheria zengine.

4-

أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ

”Je, wanataka [uwahukumu kwa] hukumu ya kipindi cha makafiri?”

Watu hawa wanataka kuhukumiwa na mayahudi na Twaaghuut sampuli zengine kwa hukumu za kipindi cha kikafiri. Hivi kuna hukumu ilio bora kuliko hukumu ya Allaah? Yeye ndiye anajua bora manufaa ya waja Wake. Anajua namna mambo yatavyomalizika. Yeye ndiye mjuzi wa kila kitu.

5- ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hatoamini mmoja wenu mpaka matamanio yake yawe ni yenye kufuata yale niliyokuja nayo.”

Bi maana hatoamini imani kamilifu na ya wajibu mpaka matamanio yake, utashi wake, makusudio yake na matakwa yake yawe ni yenye kufuata yale aliyokuja nayo yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni wajibu makusudio ya muumini yawe ni yenye kujisalimisha na hukumu ya Allaah. Baadhi ya wanachuoni wamesema kuwa Hadiyth hii ni dhaifu, lakini hata hivyo maana yake ni sahihi.

6- ash-Sha´biy amesema:

“Kulikuwa ugomvi baina ya mtu mmoja mnafiki na mwingine myahudi. Yule myahudi akasema: “Twende kwa Muhammad atuhukumu.” Mnafiki yule alijua kuwa hachukui rushwa. Mnafiki yule akasema: “Twende kwa mayahudi watuhukumu.” Kwa kujua kwake kuwa wao wanachukua rushwa. Hivyo wote wawili wakakubaliana kumwendea kuhani Juhaynah ili awahukumu. Ndipo kukateremka:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُواْ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُواْ أَن يَكْفُرُواْ بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلاَلاً بَعِيدًا

”Je, huoni wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka wahukumiane kwa Twaaghuut na hali wameamrishwa wakanushe hiyo, na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali kabisa.”

Hii ni dalili inayoonyesha kuwa mnafiki ana shari zaidi kuliko myahudi. Kwa sababu wanawababaisha watu na kusababisha upotevu. Kwa ajili hio ndio maana wakawa katika tabala ya chini kabisa Motoni.

Ni wajibu kuhukumiana na Shari´ah ya Allaah na kutoridhia nyengine. Kisa cha ´Umar kinathibitisha kwamba kuhukumu kinyume na Shari´ah ni kufuru na kuritadi. Vilevile yule mwenye kuchukia hukumu ya Allaah ni kafiri. Usahihi wa visa vyote viwili unahitajia kutazamwa vizuri, lakini maana zake ni sahihi.

ash-Sha´biy ni ´Aamir bin Sharaahil.

Faida:

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amemuumba Aadam kwa sura Yake.”[2]

Ina maana kwamba Allaah alimuumba Aadam kwa usikizi, uoni, akizungumza, uso, mikono, nyayo na mengineyo. Allaah anasikia na Aadam pia alikuwa akisikia. Allaah anazungumza na Aadam pia alikuwa akizungumza na kadhalika. Lakini hafanani na Allaah inapokuja katika dhati na sifa za Allaah:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (ash-Shuuraa 42:11)

Kuhusiana na ambaye amesema kuwa dhamiri inarudi kwa Aadam, ni kosa. Aliyesema hivo lengo lake ilikuwa kukimbia kufananisha.

[1] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (15)na ”Mishkaat-ul-Maswaabîh” (167).

[2] al-Bukhaariy (6227) na Muslim (2841).



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2Q5oOpb
via IFTTT

New video by GROUP FAIDIKA NA MAWAIDHA on YouTube

❇TUJUWE KULEA WAZAZI WENZANGU❇ Kutoka group 👉ELIMIKA UELIMISHE. ❇By Rashid Al-Shukeriy🎧
❇TUJUWE KULEA WAZAZI WENZANGU❇ Kutoka group 👉ELIMIKA UELIMISHE. ❇By Rashid Al-Shukeriy🎧


View on YouTube

Dhambi kubwa kutohajiri katika mji wa Kiislamu

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mimi nimejiweka mbali na kila muislamu anayeishi kati ya washirikina.”[1]

Je, ni dalili yenye kuthibitisha kwamba dhambi hii ni kubwa?

Jibu: Ndio. Kuishi kati ya washirikina, kutulizana kati yao na mtu akaacha kuhajiri katika miji ya waislamu anaguswa na matishio haya.

[1] Abu Daawuud (2647) na at-Tirmidhiy (1604) som sade att al-Bukhârî menade att hadîthens berättarkedja saknar en följeslagare. Detsamma sade Abû Hâtim ar-Râzî och ad-Dâraqutnî. Se ”al-Badr al-Munîr” (9/163). Autentisk enligt al-Albânî i ”Sahîh Sunan Abî Dâwûd” (2420).



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2P16nFO
via IFTTT

Ni ipi hukumu ya kikao cha mapumziko?

Swali 24: Ni ipi hukumu ya kikao cha mapumziko (جلسة الاستراحة)?

Jibu: Kimependekezwa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikikaa. Baadhi ya wanachuoni wengine wanasema kuwa hakikupendekezwa kwa sababu huenda (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo kwa sababu ya uzito wake au kwa sababu ya kuchoka. Lakini maoni yaliyo na nguvu ni kwamba kimependekezwa.



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2CSxjA4
via IFTTT

Kitaab-ut-Twahaarah 33



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2P2oI5a
via IFTTT

Kitaab-ut-Twahaarah 30



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2CSxag0
via IFTTT

Kitaab-ut-Twahaarah 29



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2OXJVgF
via IFTTT

Kitaab-ut-Twahaarah 32



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2CUnguC
via IFTTT

Kitaab-ut-Twahaarah 31



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2P0qTpL
via IFTTT

New video by GROUP FAIDIKA NA MAWAIDHA on YouTube

*Huna Sababu Ya Kupoteza Furaha Yako. (2) By: Mrisho Othman.
*Huna Sababu Ya Kupoteza Furaha Yako. (2) By: Mrisho Othman.


View on YouTube

New video by GROUP FAIDIKA NA MAWAIDHA on YouTube

Wema kwa wazazi. Sehemu ya ( 10 ) ➡Kumbuka wema na huruma zao ulipokua mdogo. By: Mrisho Othman
Wema kwa wazazi. Sehemu ya ( 10 ) ➡Kumbuka wema na huruma zao ulipokua mdogo. By: Mrisho Othman


View on YouTube

Jumanne, 30 Oktoba 2018

New video by GROUP FAIDIKA NA MAWAIDHA on YouTube

Tafsir Ya Qur-an *📖 Surat Luqman 12-19* *👤👤Sh. Mishari Al Afasiy.* *Sh. Mahammad Sulayman.*
Tafsir Ya Qur-an *📖 Surat Luqman 12-19* *👤👤Sh. Mishari Al Afasiy.* *Sh. Mahammad Sulayman.*


View on YouTube

Hukmu ya Ghiyba ( kusengenya )

 Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh

Maana ya Ghiybah:

Kilugha:  Kila kilichokuwa hakipo mbele yako. Na imeitwa Ghiybah kwa kutokuweko anayetajwa wakati anapotajwa na wengine. 

Kishariy’ah: Kumsengenya mtu asiyekuwepo kwa mambo ambayo atachukia kuyasikia. Na maana yake ametujulisha Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipowauliza Maswahaba:


(( أتدرون ما الغيبة؟))  قالوا: الله ورسوله أعلم؛ قال: (( ذكرك أخاك بما يكره  ...))
((Je mnajua maana ya  Ghiybah?)) Wakasema: Allaah na Rasuli Wake wanajua. Akasema: ((Kumsema ndugu yako anayoyachukia …..))  [Al-Bukhaariy]


Imaam An-Nawawiy amesema kuhusu Ghiybah: "Kumsema mtu nyuma yake kwa yale anayoyachukia."

Akaendelea kusema: "Kumsema mtu kwa anayoyachukia ikiwa yanayohusu mwili wake, au Dini yake, au dunia yake, au nafsi yake, au umbile lake au tabia yake, au mali yake, au wazazi wake, au mtoto wake, au mke wake, au mtumishi wake, au nguo yake, au nyendo (shughuli) zake na mengineyo yote yanayomhusu, ikiwa ni kumsema kwa kauli, au kwa ishara au kukonyeza, hata kama kusema neno la kumkejeli.”
  
Maana nyingine ya Ghiybah ni kama alivyosema Ibn   Taymiyyah (Rahimahu Allaah): "Wengine wanasengenya kwa kauli zao za kustaajabu kama kusema: “Nimeshangazwa na fulani vipi hafanyi kadhaa na kadhaa.” Na wengine wanaosengenya moyoni (kwa niyyah) kwa kunena: “Masikini fulani amenisikitisha anayoyatenda.”

Tofauti Baina ya Ghiybah na Buhtaan:

Buhtaan ni kumzulia mtu jambo lisilokuwa la kweli. Ametubainishia Rasuli wa Allaah   (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tofauti baina ya Ghiybah na Buhtaan katika Hadiyth ifuatayo:


 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَال:   (( أَتَدْرُونَ مَا الْغِيبَةُ ؟ ))  قَالُوا : اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ ، قَالَ  ((ذِكْرُكَ أَخَاكَ بِمَا يَكْرَهُ )) ، قِيلَ : أَفَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ فِي أَخِي مَا أَقُولُ ؟ قَالَ  ((إِنْ كَانَ فِيهِ مَا تَقُولُ فَقَدِ اغْتَبْتَهُ ، وَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِيهِ فَقَدْ بَهَتَّهُ))    أخرجه مسلم  
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba aliuuliza Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Je mnajua maana ya  Ghiybah?))Wakasema: Allaah na Rasuli Wake wanajua. Akasema: ((Ni kumtaja ndugu yako kwa jambo analochukia)). Akaulizwa: Hebu nieleze, iwapo ndugu yangu anayo yale niyasemayo? Akasema: (Ikiwa analo hilo usemalo basi umeshamsengenya, na ikiwa hana hilo usemalo basi umeshamzushia uongo)) [Muslim]

Vile vile Hadiyth ifuatayo inaelezea:


عبد الله بن عمرو أنهم ذكروا عند رسول الله صلى الله عليه وسلم رجلاً فقالوا: لا يأكل حتى يُطعم، ولا يَرحل حتى يُرحل، فقال النبي صلى الله عليه وسلم: ((اغتبتموه)) فقالوا: يا رسول الله: إنما حدثنا بما فيه قال: ((حسبك إذا ذكرت أخاك بما فيه))  المحدثالألباني -  المصدر السلسلة الصحيحة
Kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Amru (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba walimtaja mtu mmoja mbele ya Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakasema: "Hali hadi alishwe, wala haendi hadi apelekwe." Akasema Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Mmemsengenya)).  Wakasema: "Ee Rasuli wa Allaah  wa Allaah, tumehadithia ya kweli aliyonayo." Akasema: ((Inakutosheleza kumsema ndugu yako kwa aliyonayo)) [Al-Albaaniy   katika Silsilatus-Swahiyhah]

 Na kutoka katika Qur-aan Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٨﴾
Na wale wanaowaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike bila ya kuwa wamechuma kosa, basi kwa yakini wamejibebea usingiziaji mkuu wa dhulma na dhambi bayana. [Al-Ahzaab: 58]  

Vile vile katika kisa cha Ifk (kuzuliwa) Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) Anasema Allaah   (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 وَلَوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ قُلْتُم مَّا يَكُونُ لَنَا أَن نَّتَكَلَّمَ بِهَـٰذَا سُبْحَانَكَ هَـٰذَا بُهْتَانٌ عَظِيمٌ ﴿١٦﴾
Na kwa nini mlipoisikia (kashfa ya kusingiziwa) msiseme: “Haitupasi sisi tuzungumze haya; Subhaanak! (Utakasifu ni Wako) huu ni usingiziaji wa dhulma mkubwa mno!”  [An-Nuwr: 16]    

Uzushi unaweza kuwa kwa Ghiybah  (kumsengenya nyuma yake mtu) au mbele yake. 

Hasan Al-Baswriy kasema: "Ghiybah ni tatu; zote zimo katika Qur-aan. Ghiybah (kusengenya) ifk (usingiziaji, udaku, umbeya) na buhtaan (kusingizia yasiyo kweli).

Ghiybah ni kumsengenya ndugu yako aliyonayo. Ama  Ifk ni kusema unayoyasikia (ya usingiziaji, umbeya) na ama buhtaan ni kusingizia yasiyo kweli."

Ghiybah hakika ni hatari mno kwa Muislamu kwani     ghiybah zinamharibia mtu ‘amali zake na hatimaye akute patupu katika miyzaan yake ya ‘amali njema Siku ya Qiyaamah. Hatari hii ni kwa yeyote yule hata kama mtu ni mswalihina au ni mtendaji  wema kwa wingi!    


Kutunza Ulimi


Kila binaadamu ana Malaika wawili; mmoja kuliani mwake, na kushotoni mwake. Na kazi zao ni kuandika mema ya mtu na maovu yake; ikiwa ni makubwa au madogo hata kama chembe cha hardali basi huandikwa na Malaika hao, hata kama binaadam atatamka neno liwe dogo mno vipi basi litaandikwa. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِ نَفْسُهُ ۖ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ﴿١٦﴾
Na kwa yakini Tumemuumba insani na Tunajua yale yanayowaza nafsi yake, na Sisi Tuko karibu naye kuliko mshipa wa koo.

إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ﴿١٧﴾
Pale wanapopokea wapokeaji wawili (Malaika) wanaokaa kuliani na kushotoni. 

مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴿١٨﴾
Hatamki kauli yeyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha (kurekodi). [Qaaf: 16-18]

  Hakuna kitakachokosekana kuandikwa na Malaika hao, wala binaadamu hawezi kuwakwepa kwani wao wamewekwa kwa ajili hiyo: Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ ﴿١٠﴾
Na hakika juu yenu bila shaka kuna wenye kuhifadhi (na kuchunga).  


كِرَامًا كَاتِبِينَ ﴿١١﴾
Watukufu wanaoandika (amali).


يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ ﴿١٢﴾
Wanajua yale myafanyayo. [Al-Infitwaar: 10-12]

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametuumba katika umbo bora kabisa na Amepanga kila kiungo mahali pake panapostahiki. Kwa hikma Yake, Ameviumba viungo viwili muhimu katika mwili wa binaadamu katika sehemu zilizofichika ili vihifadhike visidhihirike nje ya mwili wake. Navyo ni: ulimi na sehemu za siri. Ni viungo ambavyo pindi binaadamu atakapovichunga basi vitampeleka Jannah kama Anavyosema Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ رضي الله عنه ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: (( مَنْ يَضْمَنْ لِي مَا بَيْنَ لَحْيَيْهِ وَمَا بَيْنَ رِجْلَيْهِ ، أَضْمَنْ لَهُ الْجَنَّةَ))    متفق عليه
Sahl bin Sa'd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayenidhaminia kilichomo baina ya taya zake [yaani ulimi] na kilichomo baina ya miguu yake [yaani tupu au sehemu za siri] nami nitamdhamini Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika Hadiyth nyingine:

عن عقبة بن عامر رضي الله عنه قال : قلت : يا رسول الله ما النجاة ؟ قال: ((مْسِكْ عَلَيْكَ لِسَانَكَ ، وَلْيَسَعْكَ بَيْتُكَ ، وَابْكِ عَلَى خَطِيئَتِكَ)) رواه الترمذي   صححه الألباني في صحيح الترغيب 3331    
'Uqbah bin 'Aamir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nilimuuliza Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) "Ee Rasuli wa Allaah, ni kupi kuokoka? Akajibu: ((Uzuie ulimi wako, utosheke na nyumba yako na ulie juu ya dhambi zako)) [At-Tirmidhiy na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb (3331)]

 وعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِي اللَّه عَنْه قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ :  (( مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ، فَلْيَقُلْ خَيْرًا أَوْ لِيَصْمُتْ))   متفق عليه  .
Na kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allahu 'anhu) ambaye amsema: Rasuli wa Allaah  (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kumuamini Allaah na siku ya Mwisho basi aseme mema au anyamaze)) [Al-Bukhaariy na Muslim]  



Ulimi ni Kufaulu kwako au Kuangamia kwako

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameuhifadhi ulimi ndani ya mdomo, ili usiwe wazi kila mara ukanena maneno mengi ambayo huenda yakamuangamiza binaadamu kwa kumuharibia ‘amali zake, au kukosa radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) hata mtu akineno neno moja tu ovu ni hatari kwa sababu  Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameonya:

عن أبي عبد الرحمن بلال بن الْحَارِثِ الْمُزَنِيِّ رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال‏:‏ ((‏ان الرَّجُلَ لَيَتَكَلَّمُ بِالْكَلِمَةِ من رِضْوَانِ الله ما كان يَظُنُّ ان تَبْلُغَ ما بَلَغَتْ يَكْتُبُ الله له بها رِضْوَانَهُ إلى يَوْمِ يَلْقَاهُ وَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَتَكَلَّمُ بِالْكَلَمِةِ من سَخَطِ الله ما كان يَظُنُّ ان تَبْلُغَ ما بَلَغَتْ يَكْتُبُ الله له بها سَخَطَهُ إلى يَوْمِ يَلْقَاهُ))‏.‏ رواه مالك في الموطأ والترمذي وقال حديث حسن صحيح‏.
Abuu 'Abdir-Rahmaan Bilaal bin Al-Haarith Al-Muzniy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kwa hakika mja atazungumza neno linalomridhisha Allaah, wala asidhani kuwa litafikia lilipofikia, Allaah Amuandikie kwa neno hilo Radhi Zake hadi Siku ya Qiyaamah. Na Kwa hakika mja atazungumza neno linalomghadhibisha Allaah, wala asidhani kuwa litafikia lilipofikia, Allaah Amuandikie kwa neno hilo hasira Zake hadi Siku ya Qiyaamah)) [Maalik katika Muwattwa na At-Tirmidhiy ambaye amesema Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]

Kutokana na Hadiyth hii, tunapata funzo kwamba, ulimi unaweza kuwa ni kiungo kizuri kabisa katika mwili wa binaadamu na unaweza kuwa ni kiungo kiovu kabisa vile vile.
Kisa kifuatacho cha Luqmaan kinatuthibitishia funzo hili:

Ibn Jariyr amenukuu kwamba Khaalid Ar-Rabaai alisema: "Luqmaan alikuwa mtumwa wa Kiethiopia aliyekuwa na ujuzi wa useremala. Bwana (Tajiri) wake alimwambia: "Tuchinjie huyu kondoo." Akamchinja, kisha akamwambia: "Niletee viungo viwili vilivyokuwa ni bora kabisa." Akampelekea ulimi na moyo. Baada ya siku kupita, alimtaka tena amchinjie kondoo, akachinja kisha Bwana wake akamwambia tena: "Niletee viungo viwili vilivyokuwa ni viovu kabisa." Akameletea vile vile ulimi na moyo. Bwana wake akamuuliza: "Nilipokutaka uniletee viungo bora kabisa umeniletea ulimi na moyo; na nilipokutaka uniletee viungo viovu kabisa umeniletea hivyo hivyo." Luqmaan akamwambia: "Hakuna vilivyo bora kuliko hivi vinapokuwa vizuri, na hakuna vilivyo viovu kabisa kuliko hivi vinapokuwa vibaya." [At-Twabariy: 20:135]

Mafunzo mengineyo kuhusu ulimi:


  1. Ulimi ni kipande kidogo cha nyama kisichokuwa na mifupa lakini kinaweza kumvunja mtu mifupa yake siku ya Qiyaamah.
  1. Ulimi ni kama nyoka utakaomtia sumu binaadamu, au ni kama mkuki utakaomuangamiza binaadamu siku ya Qiyaamah.
  1. Hivyo hivyo, ulimi huenda ukawa ni sababu ya kumuingiza mtu Peponi japo kama hakuwa na matendo mengi ya wema. 

  1. Ulimi ni kiungo kikuu katika mwili wa binaadamu kinachodhibiti viungo vingine vyote vya mwili wa binaadamu kutokana na Hadiyth ifuatayo ya Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَفَعَهُ قَالَ : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:  (( إِذَا أَصْبَحَ ابْنُ آدَمَ، فَإِنَّ الْأَعْضَاءَ كُلَّهَا تُكَفِّرُ  اللِّسَانَ، فَتَقُولُ : اتَّقِ اللَّهَ فِينَا، فَإِنَّمَا نَحْنُ بِكَ، فَإِنِ اسْتَقَمْتَ اسْتَقَمْنَا، وَإِنِ اعْوَجَجْتَ اعْوَجَجْنَا))  أخرجه الترمذي وأحمد وابن خزيمة والبيهقي بسند حسن. رياض الصالحين
Kutoka kwa Abuu Sa'iydil-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah  (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Anapoamka mwana Aadam viungo vyote vinaulaumu ulimi vikisema: Mche Allaah kwetu, kwani sisi tuko katika hifadhi yako; ukiimarika nasi tutaimarika, ukienda pogo, nasi tutakwenda pogo)) [At-Tirmidhiy, Ahmad, Ibn Khuzaymah, Al-Bayhaqiy ikiwa ni sanad hasan. Riyaadhwus-Swaalihiyn]

Ni vyema kuzuia ulimi usitoke kuzungumza maneno yoyote ila pale unapohitajika kwani kuuachia ulimi utamke tu ya kutamkwa bila ya kutahadhari, utampeleka mtu kutoa porojo na kuzungumza yasiyofaa na kumharibia mja Aakhirah yake.


Kuharamishwa kwake na Adhabu zake katika Quraan


Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا ﴿٣٦﴾
Na wala usifuatilie ambayo usiyokuwa nayo ujuzi. Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo vitakuwa vya kuulizwa (Siku ya Qiyaamah). [Al-Israa: 36]  


Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ﴿١٢﴾
na wala wasisengenyane baadhi yenu wengineo. Je, anapenda mmoja wenu kwamba ale nyama ya nduguye aliyekufa? Basi mmelichukia hilo! Na mcheni Allaah! Hakika Allaah ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu. [Al-Hujuraat: 12]

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameharamisha Muumimi kumsengenya mwenziwe kama Alivyoharamisha nyamafu.

‘Ulamaa wamekubaliana kuwa Ghiybah ni haraam kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) iliyotangulia. Na kuhusu kauli Yake:

فَكَرِهْتُمُوهُ
((Basi mmelichukia hilo))

kwa maana kama mnavyochukia kula nyama ya ndugu yenu aliyekufa basi vile vile mchukie kumtaja mwenzenu kwa ubaya.

Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ ۖ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ ۚ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿١١﴾
Na wala msifedheheshane kwa kutukanana na wala msiitane majina (mabaya) ya utani. Ubaya ulioje kuita jina la ufasiki baada ya iymaan. Na yeyote asiyetubu, basi hao ndio madhalimu. [Al-Hujuraat: 11]

Mwenye kufanya hivyo; mwenye kusengenya na mwenye kumzushia mwenziwe uongo wamelaaniwa na kushutumiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Aayah ifuatayo:
وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ ﴿١﴾

Ole kwa kila mwenye kukebehi na kukashifu watu kwa ishara na vitendo na kwa kila mwenye kufedhehesha kwa ulimi. [Al-Humazah: 1]


Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Humazah ina maana yule anayetukana na kufedhehesha wenziwe." [At-Twabariy 24: 596] 

Al-Hammaaz:   Mwenye kusengenya kwa vitendo kwa mkono au kwa macho kama kukonyeza.  

Al-Lammaaz: Mwenye kusengenya kwa ulimi (kunena).

[Kauli ya Mujaahid katika Tafsiyr ya Ibn Kathiyr]

Yote hayo ni  Ghiybah na adhabu zake ni  kama zilivyotajwa katika Aayah zilizotangulia.
   
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa wanaosengenya kwa kuzulia watu maovu:

إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿١٩﴾
Hakika wale wanaopenda uenee uchafu wa kashfa kwa wale walioamini; watapata adhabu iumizayo duniani na Aakhirah. Na Allaah Anajua nanyi hamjui. [An-Nuwr: 19].



Kuharamisihwa kwake na  Adhabu zake katika Sunnah


Makatazo na uharaam wa Ghiybah na adhabu zake katika Sunnah ni kama ifuatavyo: 


 عن أبي بكرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال في خطبته يوم النحر بمنى في حجة الوداع: ((إنَّ دِمَاءَكُمْ وَأَمْوَالَكُمْ وَأَعْرَاضَكُمْ حَرَامٌ عَلَيْكُمْ كَحُرْمَةِ يَوْمِكُمْ هَذَا فِي شَهْرِكُمْ هَذَا فِي بَلَدِكُمْ، أَلا بَلَّغْتُ؟ )) متفق عليه
Kutoka kwa Abuu Bakrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesimulia  kuwa Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema katika khutba yake ya siku ya An-Nahr [siku ya kuchinja] huko Minaa katika  Hijjah ya kuaga: ((Hakika damu zenu, mali zenu na heshima zenu ni haraam kwenu kama uharamu (wa kutenda dhambi) siku yenu hii katika mji wenu huu. Je nimefikisha?)) [Al-Bukhaariy na Muslim]


Hadiyth hii imedhihirisha uharaam wa ghiybah yakiwemo makatazo na uharaam wa kuvunjiana heshima na kwamba ni sawa na kutenda dhambi mji mtukufu na siku tukufu hiyo ya Yawmun-Nahr (siku ya kuchinja).  


Haifai kumteta mtu hata ikiwa mtu huyo ana sifa mbaya unayoitaja madamu unaitaja nyuma yake basi huwa ni ghiybah kama  alivyosema Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Basi seuze iwe ni kumsengenya mtu kwa aibu asiyokuwa nayo au kumtolea aibu zake, au kumzulia kwa mabaya asiyokuwa nayo? Imeharamishwa katika Hadiyth ifuatayo:  


عن عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قُلْتُ لِلنَّبِي صلى الله عليه وسلم: حَسْبُكَ مِنْ صَفِيَّةَ كَذَا وَكَذَا. فَقَالَ: ((لَقَدْ قُلْتِ كَلِمَةً لَوْ مُزِجَتْ بِمَاءِ الْبَحْرِ لَمَزَجَتْهُ)). قَالَتْ: وَحَكَيْتُ لَهُ إِنْسَانًا، فَقَالَ: ((مَا أُحِبُّ أَنِّى حَكَيْتُ إِنْسَانًا وَأَنَّ لِي كَذَا وَكَذَا))  رواه أبو داود   والترمذي   وقال: حديث حسن صحيح.

Kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesimulia: Nilimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Achana na Swafiyyah; yuko kadhaa na kadhaa."  yaani ni mfupi – Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hakika umetamka neno ambalo lau lingalichanganywa na maji ya bahari yangelibadilika)) (kutokana na uvundo wa neno hilo). 'Aaishah alisema: "Siku moja nilimuigiza mtu mbele yake Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: ((Mimi sipendi kumuiga mtu na ilhali mimi nina kadhaa na kadhaa)) [Abu Daawuud na At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh] 


Dini yetu ya Kiislam imesisitiza sana kutunziana heshima na kuhifadhiana mabaya yetu kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:


 عن عبد اللَّه بن عَمْرو بن الْعاص رضي اللَّه عنهما عن النَّبِيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال  : ((الْمُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ الْمُسْلِمُونَ مِنْ لِسانِهِ ويَدِهِ، والْمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ ما نَهَى اللَّه عَنْهُ)) متفق عليه
Kutoka kwa 'Abdullaahi bin 'Amru bin Al-'Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muislam ni yule wanaosalimika Waislam kwa ulimi wake na mkono wake, na Muhaajir (mwenye kuhama) ni yule anayehama yale Aliyoyakataza Allaah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]


Umuhimu wa kuhifadhi ulimi ili usimuingize mtu motoni:

عن معاذِ بن جبلٍ رضي الله عنه قال: قلت: يا رسول الله، أخْبِرني بِعَمَلٍ يُدْخِلُني الجنَةَ ويُبَاعِدُني عَنِ النارِ. قال: ((لَقَدْ سألْتَ عَنْ عَظيمٍ، وإنَهُ لَيَسيرٌ عَلى من يَسَّرَهُ اللهُ تعالى عَلَيْهِ : تَعْبُدُ اللهَ لا تُشْرِكُ بِهِ شَيئاً، وتُقيمُ الصَّلاةَ  ،وتُؤتي الزكاةَ، وتصومُ رمضانَ، وتَحُجُّ البيتَ)) ثم قال: (( ألا أَدُلُّكَ على أبْوَابِ الخيرِ؟: الصَّومُ جُنَّةٌ، والصَّدقةُ تُطْفِىءُ الخَطِيئةَ كما يُطْفىءُ الماءُ النارَ، وصَلاةَ الرَّجُلِ في جَوْفِ الَّليْلِ، ثم تلا: ((تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنْ الْمَضَاجِعِ)) - حتى بلغ – ((يَعْمَلُونَ))  السجدة: 16-17 .
ثم قال:  ((ألا أُخْبِرُكَ بِرَأسِ الأمْرِ وَعَمودِهِ وَذِرْوَةِ سَنَامِهِ؟)) قلتُ: بَلىَ يا رسول الله. قال:  (( رَأْسُ الأمْرِ الإسلامُ، وعَمُودُهُ الصَّلاةُ، وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الجِهادُ )).ثم قال: ((ألا أخْبِرُكَ بِمِلاكَ ذَلِكَ  كلِّهِ ؟)) فَقُلْتُ بَلَى يا رَسول الله، فأخَذَ بِلِسانِهِ وقال:  ((كُفَّ عَلَيْكَ هذا)) . قلت: يا نبيَّ الله، وإنَّا لمؤاخَذُونَ بِما نَتَكَلَّمُ بِه؟)) فقال: (( ثَكِلَتْكَ أمُّكَ يَا مُعَاذُ،  وَهَلْ يَكُبُّ الناسَ في النارِ على وُجُوهِهِمْ ))  أو قال: ((على مناخِرِهِم - إلاَّ حَصَائدُ  ألسِنَتهم)) رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ   وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ. 
Kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Niambie kitendo ambacho kitanipeleka Jannah na kitaniokoa na moto.  Akasema: ((Umeniuliza jambo kubwa lakini ni rahisi kwa yule ambaye Allaah Ta’aalaa Amemsahilishia.  Muabudu Allaah wala usimshirikishe na chochote, Swali, toa Zakaah, funga Ramadhwaan, nenda kuhiji (Makka). Kisha akasema: ((Je? Nikuonyeshe  milango ya kheri?  Swawm ni ngao, Swadaqah inazima dhambi kama vile maji yanavyozima moto, na kuswali katikati ya usiku: Kisha akasoma  ((Mbavu zao zinatengana na vitanda ….)) hadi ilipomalizikia Aayah ((…waliyokuwa wakiyatenda)) [As-Sajdah: 16 na 17]  

Tena akasema: ((Je, nikwambie kilele cha hilo jambo; nguzo yake na sehemu yake ya juu kabisa?)) Nikasema: Ndio ee Rasuli wa Allaah. Akasema: ((Kilele chake ni Uislaam, nguzo yake ni Swalaah na sehemu yake ya juu kabisa ni jihaad))  Kisha akasema: ((Je, nikwambie muhimili wa yote haya?)) Nikasema: Ndio ee Rasuli wa Allaah. Akaukamata ulimi wake na akasema; ((Uzuie huu)) Nikasema: Ee Nabiy wa Allaah,  yale tunayoyasema tutahukumiwa  kwayo? Akasema:  ((Mama yako akuhurumie ee Mu'aadh!  Kuna kitu zaidi kinachowaangusha watu kifudifudi motoni kama si mavuno ya ndimi zao?)) [Imesimuliwa na At-Tirmidhiy na ni Hadiyth Hasan]


Baadhi ya hizo adhabu za Aakhirah alikwishaziona Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokwenda Israa wal Mi'raaj kama ilivyotajwa  katika Hadiyth ifuatayo:


عن أنس قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((لما عُرِجَ بي مررتُ بقومٍ لهم أظفارٌ من نُحاسٍ يخْمِشون وجوهَهم وصدورَهم، فقلتُ: من هؤلاء يا جبريلُ ؟)) قال: هؤلاء الذين يأكلون لحومِ الناسِ ، ويقعون في أعراضِهم.

Kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Nilipopandishwa mbinguni (Siku ya Israa na Mi’raaj) nilipita kwa watu ambao walikuwa wana kucha za shaba nyeupe wakijichana nyuso zao na vifua vyao. Nikauliza: Nani hawa ewe Jibriyl?)) Akasema: Hawa ni watu ambao wamekula nyama za binaadamu na kuwavunjia heshima zao. [Abuu Daawuwd, Swahiyh Abiy Daawuwd (4878)]



Sababu zinazopeleka katika Ghiybah 


1-Kuambatana na marafiki waovu:  


Moja ya sababu ya Ghiyba ni kuambatana na marafiki waovu wasiomkhofu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwani rafiki muovu humuathiri mwenziwe kwa yale anayoyatenda. Mfano mzuri ametupigia  Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إِنَّمَا مَثلُ الجَلِيسِ الصَّالِحِ وَجَلِيسِ السُّوءِ كَحَامِلِ المِسْكِ وَنَافِخِ الْكِيرِ، فَحَامِلُ الْمِسْكِ إمَّا أنْ يُحْذِيَكَ وَإمَّا أنْ تَبْتَاعَ مِنْهُ وَإمَّا أنْ تَجِدَ مِنْهُ ريحًا طَيِّبَةً، وَنَافِخُ الكِيرِ إمَّا أنْ يُحْرِقَ ثِيَابَكَ وَإمَّا أنْ تَجِدَ مِنْهُ رِيحًا مُنْتِنَةً )) متفق عليه
Abuu Muwsaa Al-Ash'ariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesimulia: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mfano wa rafiki mwema unayeambatana naye rafiki  mbaya ni kama mfano wa mbebaji miski na mfua chuma (anayevuvia kipulizo). Mbebaji miski ima atakupa au utanunua kutoka kwake au utapata harufu nzuri kwake. Na mfua chuma (anayepuliza kipulizo), ima atachoma nguo zako au utapata harufu mbaya kutoka kwake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]


2-Mwenye kusengenya kutokuzingatia aibu zake:    

Ghiybah ni maasi yanayoleta madhara makubwa baina ya ndugu wa Kiislamu kwa kukashifiana na kutangaziana aibu zao. Tutambue kuwa hakuna mwana Aadam aliyekamilika, na kila mtu atakuwa na aibu zake; kama si aibu yake mwenyewe, basi huenda ikawa kuna aibu katika familia yake, na kama si familia yake basi huenda akawa ni mtu wa karibu yake n.k.  Na hata kama hakuna aibu yoyote kwake au kwa watu wake, basi akhofu kuwa huenda ikamfikia yeye aibu hiyo au ndugu zake au watoto wake au yeyote katika jamaa zake, kwa sababu huenda Allaah Akalipizia hapa hapa duniani kwa wenye kusengenya kwa kuwasibu nao yatakayopelekea watu kuwasengenya.


3-Simu ni chanzo kikuu:

Chanzo kikuu kinachofanikisha kutendeke Ghiybah na uzushi kuenea katika jamii kwa siku hizi ni simu, hasa kwa kuweko mawasiliano ya bure kama mitandao ya kijamii.    Lau kama simu zingelikuwa ni za kulipiwa basi bila shaka wangelifilisika wenye kupenda kusengenya na kuzusha.  


4-Kudhani kwamba kusikiliza umbeya, uzushi, hakuhusiani na  ghiybah:


Mara nyingi utamsikia mtu anasema: "Lakini mimi nasikiliza tu sitii langu!” Mwenye kusema hivi atambue kuwa mwenye kusengenya na mwenye kusikia wote wako katika ushirikiano wa maasi haya ya ghiybah. Na kila kiungo cha mwana Aadam kitamchongea mwenye kufanya maasi siku ya Qiyaamah, hivyo masikio yatakuchongea unaposikiliza umbeya au usengenyaji kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا ﴿٣٦﴾
Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo vitakuwa vya kuulizwa (Siku ya Qiyaamah).  [Al-Israa: 36]


5-Kujishughulisha na upuuzi badala ya kutumia muda kwa mambo yenye manufaa ya Dini:


Kuwa na faragha (muda na wasaa) ni neema ambayo inampasa Muislamu ashukuru, kwani kila dakika  ni muhimu kuitumia ipasavyo  kwa kujichumia mema na sio kuipoteza kwa mambo ya upuuzi ambayo yanayoweza kumuamgamiza mtu motoni kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

فَوَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١١﴾
Basi ole Siku hiyo kwa wakadhibishao.

الَّذِينَ هُمْ فِي خَوْضٍ يَلْعَبُونَ ﴿١٢﴾
Ambao wamo katika kushughulika na upuuzi wakicheza.         [At-Twuwr: 11-12]


Amesema Imaam Ibn Kathiyr: "Ni wale ambao duniani wanacheza katika mambo ya batili."  Na kusengenya ni maovu, dhambi na batili inayompasa Muislamu ajiepushe nayo.



Namna ya Kujiokoa na Kuokoa Jamii kutokana na Ghiybah


Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٦٨﴾
Na unapowaona wale wanaoshughulika kupiga porojo katika Aayaat Zetu; basi jitenge nao mpaka watumbukie kwenye mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka, usikae pamoja na watu madhalimu. [Al-An'aam: 68]


Hiyo ni moja ya njia ya kujiokoa na maovu haya ya Ghiybah, nayo ni kujiepusha na wanaopendelea kuzungumza yasiyo na maana na yanayomkosesha mtu radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Njia nyingine nyingi ni kama yafuatayo:


Njia Za Kujiokoa Na Kuwaokoa Wenzako Na Ghiybah:

1.  Kuwa na taqwa na umkhofu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  na kusoma Aayah na Hadiyth zenye maonyo na adhabu za Ghiybah.

2. Kufikiria khasara utakayopata kuporomoka ‘amali zako njema zote na badala yake kujazwa madhambi   kama inavyosema Hadiyth ifuatayo:


‏ ‏عن ‏ ‏أبي هريرة رضي الله عنه  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهم عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((أَتَدْرُونَ مَا الْمُفْلِسُ)) قَالُوا: الْمُفْلِسُ فِينَا مَنْ لا دِرْهَمَ لَهُ وَلا مَتَاعَ، فَقَالَ: ((إِنَّ الْمُفْلِسَ مِنْ أُمَّتِي يَأْتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ بِصَلاةٍ وَصِيَامٍ وَزَكَاةٍ وَيَأْتِي قَدْ شَتَمَ هَذَا وَقَذَفَ هَذَا وَأَكَلَ مَالَ هَذَا وَسَفَكَ دَمَ هَذَا وَضَرَبَ هَذَا فَيُعْطَى هَذَا مِنْ حَسَنَاتِهِ وَهَذَا مِنْ حَسَنَاتِهِ فَإِنْ فَنِيَتْ حَسَنَاتُهُ قَبْلَ أَنْ يُقْضَى مَا عَلَيْهِ أُخِذَ مِنْ خَطَايَاهُمْ فَطُرِحَتْ عَلَيْهِ ثُمَّ طُرِحَ فِي النَّارِ)) مسلم، الترمذي
Imetoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mnamjua nani aliyefilisika?)) Wakasema (Maswahaba): Aliyefilisika ni yule miongoni mwetu asiyekuwa na dirham au mali. Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Aliyefilisika katika Ummah wangu ni yule atakayekuja siku ya Qiyaamah na Swalaah zake, Swawm zake na Zakaah zake, lakini atakuja akiwa amemtukana huyu, amemtuhumu huyu, amekula mali ya huyu, amemwaga damu ya huyu na amempiga huyu, yatachukuliwa mema yake na kulipwa wale aliowadhulumu. Yatakapomalizika mema yake kabla ya kufidia madhambi aliyowakosea wenzake, zitachukuliwa dhambi za wale aliowakosea kisha atajaziwa yeye na mwishowe atakuwa ni wa kutupwa motoni)) [Muslim, At-Tirmidhiy]


3.  Fikiria aibu zako au aibu za ndugu, jamaa zako na uwaze kama utapenda aibu hizo zidhihirike kwa wengine.


4.  Mshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kukuepusha na aibu kama za wenzako na muombe Asikupe mtihani wa aibu kama hizo au nyinginezo.


5.  Jiepushe na watu waovu na vikao viovu na andamana na watu wema ambao watakuwa na mazungumzo ya kukupa faida badala ya kukuangamiza.


6. Atakapokutafuta mwenzio kutaka kusengenya, muelezee wazi kuwa hutaki tena kusikia umbeya kwani unamkhofu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), na umnasihi naye pia aache maouvu hayo kwa kumkumbusha adhabu zake.


7. Jipe adhabu mwenyewe kila unapomsengenya mtu kama walivyokuwa wakifanya Salafus-Swaalih (wema waliotangulia);

-Funga Swawm ya siku moja kila unapomsengenya mtu, hatimaye utashindwa kukaa na njaa kila siku.

-Toa kiasi fulani cha pesa kila unapomsengenya mtu, utakapojiona unafilikisha utaacha kusengenya. 


8. Hifadhi ulimi wako usizungumze ila mema tu, jifunze pole pole hata kwa kujikumbusha, mfano uweke kitu mdomoni kama kijiwe au chembe ngumu isiyotafunika ili ibakie kukukumbusha kuzuia ulimi kusema yasiyo na maana.

9. Jiepushe na moto pindi utakapolinda heshima ya mwenzio, kumbuka Hadiyth ifuatayo:

عن أبي الدرداء رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((مَنْ رَدَّ عَنْ عِرْضِ أَخِيهِ رَدَّ اللهُ عَنْ وَجْهِهِ النَّارَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ)) رواه الترمذي وحسنه

Abuu Ad-Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayetetea heshima ya nduguye (Muislamu), Allaah Atamuepusha uso wake na moto)) [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth hii ni Hasan]


10.           Utakaposikia uzushi, kashfa au mtu atakapomsengenya mwenziwe mbele yako sema kama Anavyotufunza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Aayah zifuatazo kuhusu kisa cha 'ifk' (uzushi wa kusingiziwa Mama wa Waumimi 'Aaishah Radhwiya Allaahu 'anhaa):


Kwanza: Jifikirie nafsi yako kama wewe pia unaweza kufanya maovu hayo yanayozungumzwa? Kwa hiyo uweke dhana nzuri pia kwa Waumini wenzako.


لَّوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ ظَنَّ الْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بِأَنفُسِهِمْ خَيْرًا وَقَالُوا هَـٰذَا إِفْكٌ مُّبِينٌ ﴿١٢﴾
Kwa nini mlipoisikia (kashfa ya kusingiziwa), Waumini wanaume na Waumini wanawake wasiwadhanie wenzao kheri, na wakasema: “Hii ni kashfa ya kusingizwa iliyo dhahiri?”[An-Nuwr: 12]


Pili:  Kanusha kabisa uliyoyasikia na chukulia hayo kuwa ni uzushi na Msabbih Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):   
وَلَوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ قُلْتُم مَّا يَكُونُ لَنَا أَن نَّتَكَلَّمَ بِهَـٰذَا سُبْحَانَكَ هَـٰذَا بُهْتَانٌ عَظِيمٌ ﴿١٦﴾
Na kwa nini mlipoisikia (kashfa ya kusingiziwa) msiseme: “Haitupasi sisi tuzungumze haya; Subhaanak! (Utakasifu ni Wako) huu ni usingiziaji wa dhulma mkubwa mno!” [An-Nuwr: 16]



Kafara (Fidia) Ya Ghiybah


Ghiybah ni madhambi ambayo yanayomharibia mtu ‘amali zake njema na badala yake ni kujazwa dhambi za yule anayemsengenya na hatimaye kumuangamiza motoni. Hivyo inampasa Muislamu mwenye tabia hii ovu ambayo ni hatari kwake, afanye haraka kafara ya maovu hayo kama ifuatavyo:


1-Tawbah (Kutubia)

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا
  Enyi walioamini! Tubieni kwa Allaah tawbah ya nasuha (kwelikweli) [At-Tahriym: 8]


Tawbatun-Naswuwhaa (Tawbah ya kweli) ni ile mtu anayokamilisha shuruti zake nazo ni:


  • Kuacha kitendo kiovu hicho.
  • Kujuta
  • Kuazimia kutokurudia tena maovu
  • Ikiwa inahusu haki ya binaadamu basi lazima kwanza kurudisha haki hiyo.

2-Vipi ujihalalishe na Ghiybah

Kama ilivyo sharti ya nne kuwa kwa vile Ghiybah inahusu haki ya binaadamu basi lazima kwanza urudishe haki ya uliyemsengenya hapa duniani kabla ya kuhesabiwa Aakhirah, kwani Hadiyth ifuatayo inatuelezea,


عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم  قال: ((من كانت عنده مظلمة لأخيه من عرضه أو من شيء، فليتحلله منها اليوم قبل أن لا يكون دينار ولا درهم، إن كان له عمل صالح أخذ منه بقدر مظلمته، وإن لم يكن له حسنات أخذ من سيئات صاحبه فحمل عليه  [رواه البخاري

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesimulia kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kitu cha dhulma cha nduguye kutokana na kumvunjia heshima au kitu chochote, basi amuombe amhalalishie leo kabla haijafika siku ambayo hakutakuwa na dinari wala dirhamu; akiwa ana amali njema itachukuliwa kwa kadiri ya alichodhulumu, na akiwa hana amali njema, zitachukuliwa dhambi za aliyemdhulumu na abebeshwe)) [Al-Bukhaariy]

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم) قَالَ:  ((مَنْ كَانَتْ عِنْدَهُ مَظْلَمَةٌ مِنْ أَخِيهِ مِنْ عِرْضِهِ أَوْ  مِنْ شَيْءٍ  فَلْيَتَحَلَّلْهُ مِنْهُ الْيَوْمَ قَبْلَ أَنْ لاَ يَكُونُ دِينَارٌ وَلاَ دِرْهَمٌ ، وَإِنْ كَانَ لَهُ عَمَلٌ صَالِحٌ أُخِذَ مِنْهُ بِقَدْرِ مَظْلَمَتِهِ. وَإِنْ لَمْ يَكُنْ لَهُ أُخِذَ مِنْ سَيِّئَاتِ صَاحِبِهِ فَحُمِل عَلَيْهِ))  رواه البخاري
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu)  kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Aliyekuwa na kitu cha dhulma cha nduguye kutokana na kumvunjia heshima au kitu chochote, basi amuombe amhalalishie leo kabla haijafika siku ambayo hakutakuwa na dinari wala dirham. Ikiwa ana ‘amali njema, basi zitachukuliwa kwa kadiri ya alichodhulumiwa. Na ikiwa hana, basi zitachukuliwa dhambi za aliyemdhulumu abebeshwe)). [Al-Bukhaariy]


3-Mwenye kusengenywa asiwe na huzuni kwa kufanyiwa maovu haya kwani ni yeye mwenye kufaidika kwa kuchuma mema ambayo hakutia juhudi zake zozote za kuzifanyia kazi.  


Inasemekana kuwa Hasan Al-Baswry alimpelekea zawadi mtu aliyemsengenya na kumshukuru kwa kumchumia amali ambazo hakuzifanyia kazi kabisa.


4-Tutazame kauli zifuatazo za Salaf kuhusu kujihalalisha na Ghiybah:


- Sufyaan bin 'Uyaynah amesema: "Ghiybah ni dhambi kubwa kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuliko zinaa au kunywa pombe kwani hizo ni dhambi baina ya mja na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), utakapotubu Atakughufuria, lakini Ghiybah ni baina ya mja na nduguye hadi amsamehe."

Kama tunavyojua kuwa ni vigumu sana mtu kuwa na moyo wa kumsamehe mwenzake anapomsengenya, ndio maana labda Salaf huyu akaona kuwa kusengenya ni madhambi makubwa zaidi kuliko madhambi mengine makubwa.


- Ibn Taymiyah, Ibnul Qayyim na wengineo, wameona kuwa sharti ya kujihalalisha na Ghiybah inaanguka pindi ukihisi kuwa utaharibu uhusiano wa uliyemsengenya na kuzidisha chuki na uadui baina yenu.


5-Sio wepesi kwa mtu mwenye kusengenya kumfuata mwenziwe na kumuomba msamaha kwa khofu ya kuwa ataharibu uhusiano. 

Hali kadhalika sio wepesi kwa mwenye kusengenywa kusamehe, kwani ni jambo linalomuumiza mtu moyoni khaswa ikiwa aliyekusengenya ni rafiki yako mpenzi au mtu wa karibu yako. 

Pindi hali ikiwa ni hivyo ya kusababisha chuki, uadui na kutoweka mapenzi na masikilizano, ni bora kutokumuomba msamaha bali fanya yafuatayo:


  • Muombee maghfirah kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amghufurie madhambi yake.
  • Muombee du'aa za kumtakia kheri nyingi duniani na Aakhirah.
  • Mfanyie wema kwa wingi.  

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atuepushe na maovu haya tusifike hadi hali zetu zikawa za kujuta na khasara ya kupoteza ‘amali zetu tunazojitahidi kuzifanya duniani kumbe hatuzimiliki Aakhirah.


Hali zinazoruhusu Ghiybah


Tumebainishiwa katika Shariy’ah yetu ya Kiislamu kuwa ziko hali zinazojuzu  Ghiybah kwa sababu ya maslaha yanayopatikana. Nazo ni kama ifuatavyo:



1-Kupinga dhulma ya Qadhi au Kiongozi au kuzuia dhulma isitendeke:

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
 لَّا يُحِبُّ اللَّـهُ الْجَهْرَ بِالسُّوءِ مِنَ الْقَوْلِ إِلَّا مَن ظُلِمَ
Allaah Hapendi uovu utajwe hadharani isipokuwa kwa yule aliyedhulumiwa. [An-Nisaa: 148].  


2-Katika kushitaki anapodhulumiwa mtu haki yake:

Kutoa aibu ya mtu inapohitajika mfano kushtaki kwa mhusika (mkuu atakayeweza kutatua matatizo) mfano kulalamika: “Fulani kanidhulumu kadhaa na kadhaa, au kanifanyia kadhaa na kadhaa, au fulani hanipi haki yangu kadhaa na kadhaa."  Hii ni kutokana na dalili ifuatayo:


عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّ هِنْدَ بِنْتَ عُتْبَةَ، قَالَتْ : يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ أَبَا سُفْيَانَ رَجُلٌ شَحِيحٌ وَلَيْسَ يُعْطِينِي مَا يَكْفِينِي وَوَلَدِي، إِلَّا مَا أَخَذْتُ مِنْهُ وَهُوَ لاَ يَعْلَمُ، فَقَالَ: ((خُذِي مَا يَكْفِيكِ وَوَلَدَكِ ، بِالْمَعْرُوفِ )) متفق عليه
Kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Hind mke wa Abuu Sufyaan alisema: "Ee Rasuli wa Allaah , Hakika Abuu Sufyaan ni mtu bakhili, wala hanipi kinachonitosha mimi na mwanangu ila ninachokichukua ilihali hajui." (ni sawa hivi nifanyavyo?) Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Chukua kwa wema kinachokutosha wewe na mwanao)) [Al-Bukhaariy na Muslim]


3-Katika hali ya kubadilisha maovu:

Huenda Muislamu akaona maovu yanatendeka na hatoweza kuyaondosha ila aulizie sababu, na huenda atakayeulizwa amseme aliyetenda maovu mfano kusema: “Fulani ndiye aliyefanya ovu hili kadhaa na kadhaa."


4-Kujikinga na shari, na kunapotolewa nasiha kwa Waislamu:

عنْ فاطِمَة بِنْت قَيْس رضي الله عنها قالت أتَيْت النبي صلى الله عليه وسلم فَقُلْتُ إنَّ أبا الجهم ومعاوية خطباني فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم ( أَمَّا مُعَاوِيَةُ فَصُعْلُوكٌ لَا مَالَ لَهُ، وَأَمَّا أَبُو جَهْمٍ فَلَا يَضَعُ عَصَاهُ عَنْ عَاتِقِهِ)) )) متفق
وفي رواية لمسلم ((وأما أبو الجهم فضراب للنساء)) وهو تفسير لرواية لا يضع العصا عن عاتقه وقيل معناه كثير الأسفار
Faatwimah binti Qays (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesimulia: "Nilimuendea Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikamuambia: "Abul-Jahmi na Mu'aawiyah wameniposa." Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: ((Ama Mu'aawiyah ni mtu fukara hanamali. Ama Abul-Jahmi haondoi fimbo juu ya shingo yake)) [Al-Bukhaaariy na Muslim]

Katika Riwaayah nyingine ya Muslim imesema: ((Na ama Abul-Jahmi anawapiga mno wanawake))

Riwaayah hii ni tafsiyr ya riwaayah isemayo: ((…haondoi fimbo juu ya shingo yake)) Na pia imesemekana kuwa maana ya kutoondosha fimbo juu ya shingo yake ni kuwa, anasafiri mno.

Ibn Taymiyyah amesema: Huenda anapotajwa kwa ubaya mtu kukawa ni kwa ajili ya nasiha kwa Waislamu kwa usalama au manufaa ya Dini yao na dunia yao.


5-Kuwasengenya mafisadi na watu wenye shaka:

Kama ilivyo katika Hadiyth ifuatayo ambayo Al-Bukhaairy ametoa hoja kuwa Hadiyth hii yafaa kuwasengenya mafisadi na watu wenye shaka.

عن عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا أن رَجُلاً اسْتَأْذَنَ عَلَى النبي صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: ((ائْذَنُوا لَهُ بِئْسَ أَخُو الْعَشِيرَةِ))  متفق

Kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anha) amesimulia kuwa mtu mmoja aliomba idhini ya kuingia kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Mruhusuni, ni mtu mbaya katika kabila lake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

6-Kuihami Dini kutokana na wanafiki:

عن عائشة رضي الله عنها قالت قال رسول الله صلى الله عليه وسلم ((مَا أَظُنُّ فُلاَنًا وَفُلاَنًا يَعْرِفَانِ مِنْ دِينِنَا شَيْئًا))   رواه البخاري
قال الليث بن سعد أحد رواة هذا الحديث كَانَا رَجُلَيْنِ مِنَ المُنَافِقِينَ 
Kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Sidhani fulani na fulani wanajua chochote katika Dini yetu)) [Al-Bukhaariy]

Layth bin Sa'ad ambaye ni mmoja wa wapokezi wa Hadiyth hii amesema: "Watu hawa wawili walikuwa ni katika wanafiki."

NA  ALLAAH ANAJUA  ZAIDI


from fisabilillaah.com https://ift.tt/2PAOgGg
via IFTTT

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...