Translate
Jumatano, 18 Desemba 2019
Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili
CHAKULA CHA MGONJWA MWENYE KISUKARI AINA YA PILI Chakula bora kabisa kwa mgonjwa wa kisukari ni kile ambacho ni chakula cha asili na si kile ambacho kimetengenezwa kiwandani. Unahitaji chakula ambacho hakijakobolewa, unahitaji zaidi matunda na mboga za majani. Kutumia vyakula hivi naenda kukueleza kwenye hii makala kutakusaidia kupata mahitaji […]
Msikiti Mtakatifu wa al-Aqswa wavamiwa tena
Walowezi wa Kizayuni leo wameuvamia tena Msikiti wa al-Aqswa huko Palestina wakisaidiwa na askari wa jeshi la utawala haramu wa Israel na kuuvunjia heshima msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.
Walowezi hao wa Kizayuni baada ya kuingia katika eneo la ndani la msikiti huo mtakatifu walisikika wakipiga nara dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti kwamba, hujuma na uvamizi huo umefanyika kwa msaada na uungaji mkono wa wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel.
Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za kukabiliana na vitendo hivyo.
Kwa mujibu wa duru za Kipalestina, karibu kila siku walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakifanya uvamizi katika msikiti huo lengo likiwa ni kutekeleza njama za kutokomeza utambulisho wa Kiislamu na Kikristo wa Msikiti wa al-Aqswa na badala yake kuweka nembo za Kizayuni.
aqswa
Bakwata wampongeza Rais Wa Tanzania kwa kwasamehe wafungwa 5,000
Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limeadhimisha miaka 51 tangu kuanzishwa kwake kwa mafanikio kadhaa, huku likimpongeza Rais John Pombe Magufuli wa nchi hiyo kwa namna anavyowatumikia wanyonge ikiwamo kuwapatia msamaha zaidi ya wafungwa 5,000 hivi karibuni
Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limetoa wito kwa wafungwa walioachiliwa, kutumia fursa ya maisha yao kutenda mema na kutumikia nchi yao kama nguvu kazi muhimu katika jamii na wasirejee tena katika vitendo vya uhalifu na uovu.
Akihutubia hapo jana jijjini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) Nuhu Mruma alisema kuwa, taasisi hiyo inampongeza sana Rais Magufuli kwa kuwasamehe wafungwa hao ambao bado walikuwa hawajamaliza muda wao wa kukaa gerezani.
Katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika mkoani Mwanza Disemba 9 mwaka huu, Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliandika historia mpya kwa mara ya kwanza tangu nchi ipate uhuru kwa kutangaza msamaha kwa wafungwa 5,533.
Wakati Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) likimpongeza Rais Magufuli kwa msamaha wake kwa wafungwa, baadhi ya wafungwa walioachiliwa huru hivi karibuni kwa msamaha wa Rais wameripotiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu na hata mauaji. Inaarifiwa kuwa, mtu mmoja ambaye aliachiwa huru kwa msamaha wa Rais Dkt. John hivi karibuni aliwavamia na kuwachoma visu watu 6 huku mmoja wao akifariki dunia hapo hapo. Tukio lilitokea katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera. Baada ya mtuhumiwa kutekeleza tukio hilo, wananchi wenye hasira kali walimvamia na kuanza kumshambulia hadi kumuua.
Jumanne, 17 Desemba 2019
Aliyekamilika Iymaan Kwa Tabia Na Kumfanyia Wema Mke
Lu-ulu-un-Manthuwrun
(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)
Hadiyth Ya 29
Aliyekamilika Iymaan Kwa Tabia Na Kumfanyia Wema Mke
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا وَخِيَارُكُمْ خِيَارُكُمْ لِنِسَائِهِمْ خُلُقًا)) الترمذي وقال: حديث حسن صحيح
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muumin aliyekamilika iymaan ni aliye na tabia njema kabisa, na wabora wenu ni walio bora kwa wake zao kwa tabia)) [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Swahiyh Hasan]
Mafunzo na Mwongozo:
1. Uislamu unasisitiza kuwa na tabia njema kwa kila mtu.
2. Mume anasisitizwa kumfanyia wema mkewe katika maisha ya ndoa, si kumfanyia uovu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَا تَنسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ
Na wala msisahau fadhila baina yenu. [Al-Baqarah (2: 237)]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ
Na kaeni nao kwa wema. [An-Nisaa (4: 19)]
Pia rejea kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): [Ar-Ruwm 30: 21]
3. Inapasa kuweko subira baina ya mume na mke katika mitihani inayowakabili ya maisha baina yao. [((Na mkisubiri ni kheri kwenu)) [An-Nisaa (4: 25)].
4. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kigezo bora kabisa katika kuamiliana na wake [Al-Ahzaab (33: 21)].
Pia Hadiyth zifuatazo:
((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa mke wake, na mimi ni mbora kwa watu wangu wa nyumbani [ahli])) [Ibn Maajah na Ad-Daarimiy].
((Mwanamke ameumbwa kwa ubavu, na sehemu iliyopinda ya ubavu ni juu yake, ukijaribu kuunyoosha utauvunja, na lau utauacha utaendelea kupinda, nakuusieni [kuwafanyia wema]) wake zenu)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
((Allaah, Allaah, kwa wanawake, hao ni wasaidizi wenu walio kwenye mikono yenu, mmewachukuwa kama ni amana kutoka kwa Allaah, na imekuwa halali tupu zao kwenu kwa neno lake Allaah [iyjaab na qubuwl])) [Muslim, Abu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad]
Rejea pia Hadiyth namba (28), (35), (40).
Kuvumiliana Tabia Mbaya Katika Maisha Ya Ndoa Kwa Kukumbuka Tabia Zilizo Nzuri
Lu-ulu-un-Manthuwrun
(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)
Hadiyth Ya 28
Kuvumiliana Tabia Mbaya Katika Maisha Ya Ndoa Kwa Kukumbuka Tabia Zilizo Nzuri
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لاَ يَفْرَكْ مُؤْمِنٌ مُؤْمِنَةً إِنْ كَرِهَ مِنْهَا خُلُقًا رَضِيَ مِنْهَا آخَرَ)) مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muumin [mume] asimchukie Muumin [mke]. Asipompendelea kwa tabia fulani ataridhika naye kwa tabia nyingine)) [Muslim]
Mafunzo Na Mwongozo:
1. Hakuna binaadamu aliyekamilika kwa tabia njema. Kila mmoja ana kasoro zake; huenda zikawa ni tabia zinazolingana; nzuri au mbaya.
2. Kuishi pamoja kunadhihirisha tabia baina ya watu.
3. Inapasa kuvumiliana katika maisha ya ndoa, kwani kila mmoja ni mtihani kwa mwenziwe. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَجَعَلْنَا بَعْضَكُمْ لِبَعْضٍ فِتْنَةً أَتَصْبِرُونَ ۗ وَكَانَ رَبُّكَ بَصِيرًا ﴿٢٠﴾
Na Tumejaalia baadhi yenu nyinyi kwa nyinyi kuwa ni majaribio je mtasubiri? Na Rabb wako ni Mwenye kuona daima. [Al-Furqaan: 20]
4. Uislamu unamsisitiza mume kumfanyia wema mke.
Rejea: An-Nisaa (4: 19).
Rejea pia Hadiyth namba (29).
5. Hadiyth hii ni suluhisho mojawapo la kutatua matatizo baina ya mume na mkewe.
Rejea An-Nisaa (4: 128).
6. Inasisitizwa Muislamu kuchagua mke mwema, kwani ndio sababu ya furaha yake duniani na Aakhirah.
Rejea Hadiyth namba (35), (40).
7. Hii Hadiyth inamtaka mume awe makini wala asichukue hatua za haraka kama talaka ambayo huenda ikamletea majuto.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Fadhila Za Nabiy ( صلى الله عليه وآله وسلم ) 58-Masiyh Dajjaal Haingii Katika Mji Wake Wa Madiynah Alhidaaya.com Pi...







