Translate

Alhamisi, 5 Novemba 2020

19-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Istighaathah Kwa Asiyekuwa Allaah

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم

 

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

 

19 - Istighaathah (Kuomba Uokozi) Kwa Asiyekuwa Allaah

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

Maana Ya Istighaathah na dalili zake:

 

Istighaathah maana yake ni kuomba uokozi kwa ambaye ataweza kuokoa kutokana na hali ya shida, dhiki na kukaribia kudhurika au kuangamia. Na istighaathah kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) inajumuisha kujidhalilisha Kwake na kuitakidi kwamba hakuna mwengine atakayeweza kuokoa isipokuwa Yeye, kama vile hali ilivyokuwa katika vita vya Badr, Ibn Kathiyr amesema:

 

 

"Ilipokuwa siku ya Badr na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaona uchache wa Maswahaba wake na wingi wa adui zake, wakawa katika shida na khofu, akaelekea Qiblah na kuomba uokovu na akaendelea kumuomba Mola wake mpaka joho lake likamuanguka begani mwake, Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Akateremsha:

 

إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ

Na pindi mlipomuomba uokovu Rabb wenu Naye Akakuitikieni  [Al-Anfaal: 9] [mpaka mwisho wa Aayah 13 Suwrat Al-Anfaal]

 

 

Kuomba uokovu kwa bin-Aadam kwa jambo ambalo limo katika uwezo wake inafaa kwa dalili kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu kisa cha Nabiy Muwsaa (‘Alayhis-Salaam):

 

وَدَخَلَ الْمَدِينَةَ عَلَىٰ حِينِ غَفْلَةٍ مِّنْ أَهْلِهَا فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَـٰذَا مِن شِيعَتِهِ وَهَـٰذَا مِنْ عَدُوِّهِ ۖ فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ

Na akaingia mjini wakati watu wake wako katika mighafiliko, akakuta humo watu wawili wanapigana; mmoja ni miongoni mwa kundi lake, na mwengine miongoni mwa adui wake. Akamsaidia kumuokoa yule ambaye katika kundi lake dhidi ya yule ambaye ni katika adui wake… [Al-Qaswasw: 15]

 

Pia, mtu anaweza kuomba uokovu kwa mwenziwe amuokoe kutokana na adui zake katika hali ya vita n.k. Au mfano mtu anapokuwa katika hali ya kukaribia kuzama baharini akaita: “Ee ndugu! Nazama niokoe!”

 

Ama kuomba uokovu kwa jambo ambalo halimo katika uwezo wa bin-Aadam, hapo huwa ni shirki. Mfano mtu kumuomba mwenziwe:

 

“Ee fulani! Nisaidie kuniokoa na Moto wa Jahannam na niingize Jannah!”

 

“Ee Fulani! Nisaidie kuniokoa katika upotofu unijaalie hidaaya!”

 

Au kuomba walio kaburini:

 

“Ee walii wangu, au shekhe wangu!

 

Au sharifu fulani! Nisaidie kuniokoka na adhabu za kaburi! Nisaidie kuniokoa katika maradhi niliyo nayo!”

 

Kadhaalika, kuomba uokovu kwa mizimwi, mashaytwaan n.k. kuitakidi kuwa wao wana uwezo wa kuokoa katika hali ambazo hakuna mwenye uwezo isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). 

 

Vilevile kuomba uokovu kwa kumchanganya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihu wa sallam) kwa mfano: kusema  "Ee Allaah  niokoe mie katika hizi dhiki kwa baraka Zako na baraka za Rasuli Wako."

 

Hivyo ni shirki kubwa na inamtoa mtu nje ya Uislamu.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwamba hao wanaoombwa uokovu n.k. hawawezi wenyewe kujinusuru nafsi zao humo walimo makaburini wala Siku ya Qiyaamah hawatokuwa na uwezo wowote ule!

يَوْمَ لَا يُغْنِي مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ﴿٤١﴾

Siku ambayo jamaa wa karibu hatomfaa jamaa wa karibu chochote, na wala wao hawatonusuriwa. [Ad-Dukhaan: 41]

  

Hata Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa na uwezo wa kumuokoa mtu kwa dalili kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema katika Aayah kadhaa kwamba yule Ambaye Ameshamhukumu kuwa ni mpotofu, basi hakuna wa kumhidi:

 

مَن يَهْدِ اللَّـهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُ وَلِيًّا مُّرْشِدًا ﴿١٧﴾

Ambaye Allaah Amemwongoza, basi yeye ndiye aliyehidika. Na Anayemwacha kupotoka basi hutompatia mlinzi wa kumuongoza. [Al-Kahf: 17]

 

Au ambaye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amemhukumu kuwa ni mtu wa Motoni, basi hakuna wa kumuokoka, Akamwambia Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

أَفَمَنْ حَقَّ عَلَيْهِ كَلِمَةُ الْعَذَابِ أَفَأَنتَ تُنقِذُ مَن فِي النَّارِ ﴿١٩﴾

Je, yule iliyemthibitikia neno la adhabu je, basi wewe utaweza kumuokoa aliyemo katika moto? [Az-Zumar: 19]

 

 

Alikuweko mnafiki mmoja akiwaudhi Waumini ikahadithiwa:

 

عن عُبَادَةَ بْنَ الصَّامِتِ (رضي الله عنه) قال: خَرَجَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ): قُومُوا نَسْتَغِيثُ بِرَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) مِنْ هَذَا الْمُنَافِقِ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ:  ((أنه لاَ يُسْتَغَاث بِي، وَإِنَّمَا يُسْتَغَاثُ باِلله))

Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitujia kisha Abu Bakr akasema: Simameni tutake msaada kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atuokoe na mnafiki huyu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hakika haipasi kuombwa uokovu kwangu, bali inapaswa kuombwa uokovu kwa Allaah)) [At-Twabaraaniy fiy Mu’jamil–Kabiyr]  

 

Pia Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba ilipoteremshwa kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ ﴿٢١٤﴾

Na onya (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) jamaa zako wa karibu. [Ash-Shu’araa: 214]

 

 

دَعَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قُرَيْشًا فَاجْتَمَعُوا فَعَمَّ وَخَصَّ فَقَالَ: ((يَا بَنِي كَعْبِ بْنِ لُؤَيٍّ، أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ، يَا بَنِي مُرَّةَ بنِ كَعْبٍ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ، يَا بَنِي عَبْدِ شَمْسٍ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ،يَا بَنِي عَبْدِ مَنَافٍ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ، يَا بَنِي هَاشِمٍ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ ، يَا بَنِي عَبْدِ الْمُطَّلِبِ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ، يَا فَاطِمَةُ أَنْقِذِي نَفْسَكِ مِنْ النَّارِ، فَإِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ مِنْ اللَّهِ شَيْئًا غَيْرَ أَنَّ لَكُمْ رَحِمًا سَأَبُلُّهَا بِبَلَالِهَا))

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaita Maquraysh akawaonya kwa ujumla kisha makhsusi (kwa kabila fulani) akasema:  ((Ee Baniy Ka’ab bin Luayy, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto!  Ee Baniy Murrah bin Ka’b, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto! Ee Baniy ‘Abdi Shams, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto. Ee Baniy ‘Abdi Manaaf, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto.” Ee Baniy Haashim, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto.” Ee Baniy ‘Abdil-Muttwalib, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto.” Yaa Faatwimah, okoa nafsi yako kutokana na Moto! Kwani hakika mimi similiki uwezo wowote kwenu isipokuwa nitaendelea kuweka uhusiano wetu wa damu.)) [Muslim]

 

Anatahadharisha pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika kauli Zake mbali mbali:

 

وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَكُمْ وَلَا أَنفُسَهُمْ يَنصُرُونَ﴿١٩٧﴾

Na wale mnaowaomba (na kuwaabudu) badala ya Allaah hawawezi kuwanusuru na wala hawawezi kujinusuru nafsi zao. [Al-A’raaf: 197]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 أَمْ لَهُمْ آلِهَةٌ تَمْنَعُهُم مِّن دُونِنَا ۚ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَ أَنفُسِهِمْ وَلَا هُم مِّنَّا يُصْحَبُونَ ﴿٤٣﴾

Je, kwani wana waabudiwa wanaoweza kuwakinga Nasi?  Hawawezi kujinusuru nafsi zao na wala hawatolindwa Nasi. [Al-Anbiyaa: 43]

 

Na pia Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَاتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ آلِهَةً لَّعَلَّهُمْ يُنصَرُونَ ﴿٧٤﴾

Na wamejichukulia badala ya Allaah waabudiwa ili wakitumaini kuwa watawanusuru!

 

لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَهُمْ وَهُمْ لَهُمْ جُندٌ مُّحْضَرُونَ ﴿٧٥﴾

Hawawezi kuwanusuru, na watahudhurishwa (adhabuni) kama askari dhidi ya hao (waliowaabudu). [Yaasiyn: 74-75]

 

 

 



57-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Dini Yake Ndio Itakayoshinda Dini Zote

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

57-Dini Yake Ndio Itakayoshinda Dini Zote

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا﴿٢٨﴾

Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad  (صلى الله عليه وآله وسلم kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote. Na Allaah Anatosha kuwa ni Shahidi. [Al-Fat-h:28]

 

Qiyaamah hakitasimama hadi Dini ya Kiislaam ishinde Dini zote, na hii imeshaanza kudhihirika ulimwenguni kutokana na matukio kadhaa yaliyosababisha watu wengi kuingia katika Uislaam. 

 

Na katika Dalili kumi kubwa za kusimama Qiyaamah zipo Hadiyth kadhaa zinazoelezea hayo mojawapo ifuatayo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَة قَالَ : قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ  ((يَنْزِل عِيسَى اِبْن مَرْيَم فَيَقْتُل الْخِنْزِير وَيَمْحُو الصَّلِيب وَتُجْمَع لَهُ الصَّلَاة وَيُعْطِي الْمَال حَتَّى لَا يُقْبَل وَيَضَع الْخَرَاج وَيَنْزِل الرَّوْحَاء فَيَحُجّ مِنْهَا أَوْ يَعْتَمِر أَوْ يَجْمَعهُمَا))  أحمد

Kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)    amesema: ((‘Iysaa mwana wa Maryam atateremka na kuua nguruwe, atavunja misalaba, ataimamisha watu katika Swalaah ya Jamaa, na kutoa mali hadi hakuna atakayetaka kupokea tena. Ataondosha jizya (kodi) na atakwenda Ar-Rawhaa ambako ataelekea kutekeleza Hajj, ‘Umrah au zote mbili)) [Ahmad]

 

Imaam Atw-Twabariy amesema  kuhusu kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ ۚ

 

Ili Aishindishe juu ya dini zote.

 

“Hivyo ni kubatilisha millah (dini) zote hadi kwamba hakutakuwa na Dini nyingine isipokuwa hiyo, na hivyo ndivyo ilivyokuwa mpaka ‘Iysaa mwana wa Maryam ashuke na kumuua Ad-Dajaal, hapo Dini zote zitabatilishwa isipokuwa Dini ya Allaah aliyomtuma nayo Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)   na Uislaam ushinde juu ya dini zote."

 

 

Na Hadiyth nyenginezo zifuatazo:   

 

 عَنْ تَمِيمٍ الدَّارِيِّ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَيَبْلُغَنَّ هَذَا الْأَمْرُ مَا بَلَغَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَلَا يَتْرُكُ اللَّهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ هَذَا الدِّينَ بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ بِذُلِّ ذَلِيلٍ عِزًّا يُعِزُّ اللَّهُ بِهِ الْإِسْلَامَ وَذُلًّا يُذِلُّ اللَّهُ بِهِ الْكُفْرَ

Tamiym Ad-Daariyy amesimulia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   amesema: “Jambo hili (Uislaam) hakika litafika kila mahali palipoguswa na usiku na mchana. Allaah Hatoacha  nyumba au makazi isipokuwa Allaah Ataingizi Dini hii kwa ‘izza (utukufu) ambao watukufu watajaaliwa taadhima na wadhalili watadhalilika. Allaah Atawapa utukufu watukufu kwa Uislaam na Atawadhalilisha wadhalili kwa Ukafiri. [Ahmad]       

 

Na pia,

 

عَن الْمِقْدَاد بن الْأسود قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: " يَقُولُ لَا يَبْقَى عَلَى ظَهْرِ الْأَرْضِ بَيْتُ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ كلمة الاسلام بعز عَزِيز أَو ذل ذليل إِمَّا يعزهم الله عز وَجل فَيَجْعَلُهُمْ مِنْ أَهْلِهَا أَوْ يُذِلُّهُمْ فَيَدِينُونَ لَهَا  رَوَاهُ أَحْمد

Miqdaad bin Al-Aswad amesimulia: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akisema: “Haitasalia juu ya ardhi (duniani) nyumba ya udongo wala  hema la nywele za ngamia isipokuwa Allaah Ataingiza humo neno la Islaam kwa ‘izza (utukufu) ambao watukufu watajaaliwa taadhima na wadhalili watadhalilika ima Allaah  (‘Azza wa Jalla)  Awape utukufu wakazi na kuwajaalia wawe katika watu Wake, au Awadhalilishe na wawe duni mbele Yake.”  [Ahmad, Swahiyh Ibn Maajah (6701)]

 

 

Na Kauli Zake nyenginezo Allaah (سبحانه وتعالى):

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٩﴾

Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina. [Asw-Swaff: 9]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٣٣﴾

Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina. [At-Tawbah: 33]

 

 

 



01-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake: Hakumtaka Jibriyl Awaangamize Makafiri Waliomfukuza Na Kumtesa

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake:

 

01-Hakumtaka Jibriyl Awaangamize Makafiri Waliomfukuza Na Kumtesa

 

Alhidaaya.com

 

 

Pindi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alporudi kutoka Twaaif ambako wakaazi wake hawakumpokea kwa wema bali walimfukuza na kumtesa; waliwatuma watoto wadogo na wendawazimu na watumwa wao wamfukuze. Wakawa wanamuandama huku wakimtukana na kumpiga mawe mpaka damu ikaanza kumtoka Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na viatu vyake vikarowa damu. Alipokuwa anarudi kuelekea Makkah katika eneo la Qarn Al-Manaazil, Jibriyl pamoja na Malaika wa majabali wakamuuliza iwapo anataka yaangushwe majabali mawili na kuwaangamiza watu wa Makkah, lakini Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikataa kutokana na huruma zake. Maelezo kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

 عن عَائِشَةَ ـ رضى الله عنها ـ زَوْجَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم حَدَّثَتْهُ أَنَّهَا قَالَتْ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم هَلْ أَتَى عَلَيْكَ يَوْمٌ كَانَ أَشَدَّ مِنْ يَوْمِ أُحُدٍ قَالَ ‏ "‏ لَقَدْ لَقِيتُ مِنْ قَوْمِكِ مَا لَقِيتُ، وَكَانَ أَشَدُّ مَا لَقِيتُ مِنْهُمْ يَوْمَ الْعَقَبَةِ، إِذْ عَرَضْتُ نَفْسِي عَلَى ابْنِ عَبْدِ يَالِيلَ بْنِ عَبْدِ كُلاَلٍ، فَلَمْ يُجِبْنِي إِلَى مَا أَرَدْتُ، فَانْطَلَقْتُ وَأَنَا مَهْمُومٌ عَلَى وَجْهِي، فَلَمْ أَسْتَفِقْ إِلاَّ وَأَنَا بِقَرْنِ الثَّعَالِبِ، فَرَفَعْتُ رَأْسِي، فَإِذَا أَنَا بِسَحَابَةٍ قَدْ أَظَلَّتْنِي، فَنَظَرْتُ فَإِذَا فِيهَا جِبْرِيلُ فَنَادَانِي فَقَالَ إِنَّ اللَّهَ قَدْ سَمِعَ قَوْلَ قَوْمِكَ لَكَ وَمَا رَدُّوا عَلَيْكَ، وَقَدْ بَعَثَ إِلَيْكَ مَلَكَ الْجِبَالِ لِتَأْمُرَهُ بِمَا شِئْتَ فِيهِمْ، فَنَادَانِي مَلَكُ الْجِبَالِ، فَسَلَّمَ عَلَىَّ ثُمَّ قَالَ يَا مُحَمَّدُ، فَقَالَ ذَلِكَ فِيمَا شِئْتَ، إِنْ شِئْتَ أَنْ أُطْبِقَ عَلَيْهِمِ الأَخْشَبَيْنِ، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بَلْ أَرْجُو أَنْ يُخْرِجَ اللَّهُ مِنْ أَصْلاَبِهِمْ مَنْ يَعْبُدُ اللَّهَ وَحْدَهُ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia ‘Aaishah   Mke wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):  Hivi imekupitia siku iliyo ngumu zaidi ya siku ya Uhud? Akasema: “Nimepata mateso niliyo yapata kutoka kwa jamaa zako, na mateso zaidi niliyoyapata kwao ni siku ya ‘Aqabah, pale nilipojipeleka mwenyewe kwa Ibn ‘Abd Yaaliyl ibn ‘Abd Kulaal. Hakunikubalia nilicho kitaka. Nikaondoka sielewi niendako, sikuzinduka isipokuwa nilipokaribia Qarnith Ath-Tha‘alib, nikainua kichwa change nikaliona wingu limenifunika, nikaangalia nikamkuta humo Jibriyl, akaniita akasema: ‘Hakika Allaah Ameisikia kauli ya watu wako kwako na jibu walilokupa, na Amekuletea Malaika wa milima ili umuamuru unachotaka katika adhabu kuwafikia jamaa zako’. Akaniita Malaika wa milima, akanisalimia, kisha akasema: ‘Ee Muhammad!’ Akasema: ‘Ikiwa ni katika unachokitaka niwafunike kwa milima miwili’. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Bali nataraji Allaah atawatoa migongoni mwao watakao mwabudu Allaah Peke Yake, hawamshirikishi na chochote.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 



031-Aayah Na Mafunzo: Maana Ya Al-Kabaair (Dhambi Kubwa) Na Mifano Yake

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Maana Ya Al-Kabaair Dhambi Kubwa Na Mifano Yake

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا ﴿٣١﴾

Mkijiepusha na madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu. [An-Nisaa: 31]

 

Mafunzo:

 

Al-Kabaair (dhambi kubwa): ni lile lililotajiwa ndani yake laana, au haddi (adhabu) hapa duniani, au limeahidiwa juu yake ghadhabu za Allaah au moto.

 

Na Nafiy’ bin Al-Haarith Ath-Thaqafiy Abuu Bakr (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Je, nikujulisheni Al-Kabaair?” Tukasema: “Ndio ee Rasuli wa Allaah! Akasema: “Kumshirikisha Allaah, na kuwaasi wazazi wawili.” Alikuwa ameegemea, akakaa kitako akasema: “Tanabahi! Na kusema uongo na kushuhudia uongo!” “Tanabahi! Na kusema uongo na kushuhudia uongo!” Akaendelea kusema hayo mpaka nikadhani hatonyamaza. [Al-Bukhaariy (5976)].

 

Bonyeza kiungo kifuatacho kwa faida zaidi:

 

Madhambi Makubwa Na Madogo

 

 

 

 

 



110-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Israa: Sema; Muiteni Allaah Au Muiteni Ar-Rahmaan, Vyovyote Mtakavyomwita...

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

017-Asbaab Nuzuwl Suwrah al-Israa Aayah 110

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ﴿١١٠﴾

Sema; Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa. Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya, bali shika njia ya wastani baina yake. [Al-Israa: 110]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، عَنْ هُشَيْمٍ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ((‏وَلاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا‏))‏ قَالَ أُنْزِلَتْ وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مُتَوَارٍ بِمَكَّةَ، فَكَانَ إِذَا رَفَعَ صَوْتَهُ سَمِعَ الْمُشْرِكُونَ فَسَبُّوا الْقُرْآنَ وَمَنْ أَنْزَلَهُ وَمَنْ جَاءَ بِهِ‏.‏ وَقَالَ اللَّهُ تَعَالَى: ((‏وَلاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا‏))‏ لاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ حَتَّى يَسْمَعَ الْمُشْرِكُونَ، وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا عَنْ أَصْحَابِكَ فَلاَ تُسْمِعُهُمْ: ((‏وَابْتَغِ بَيْنَ ذَلِكَ سَبِيلاً‏))‏ أَسْمِعْهُمْ وَلاَ تَجْهَرْ حَتَّى يَأْخُذُوا عَنْكَ الْقُرْآنَ‏.‏  البخاري

 

Ametuhadithia Musaddad kutoka kwa Hushaym kutoka kwa Abuu Bishr, kutoka kwa Sa’iyd bin Jubayr kutoka kwa Ibn ‘Abaas (رضي الله عنهما) kuhusu Kauli ya Allaah (عز وجل):

  

وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا

Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya…

 

Amesema: “Aayah hii iliteremshwa ilhali Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amejificha Makkah. Alikuwa akiipandisha sauti yake katika kusoma Qur-aan, walipomsikia washirikina, wakaitukana Qur-aan na wakamtukana Aliyeiteremsha na aliyeileta. Basi Allaah (عز وجل) Akasema:

 

وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا

Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya…

 

 

Yaani: Usiisome kwa sauti kubwa hadi kwamba washirikiana wakusikie (kisha waitukane). 

 

 

وَلَا تُخَافِتْ بِهَا  

na wala usiifiche kimya kimya

 

Yaani: Usiisome kimya kimya hadi kwamba Swahaba zako wasiisikie unapowasomea washindwe kujifunza kwayo,

 

  وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا  

bali shika njia ya wastani baina yake.

 

Yaani: Wasikilizishe (Swahaba) kiasi cha kuisikia kwao.

 

[Al-Bukhaariy Kitaab At-Tawhiyd]  

 

 

Pia,

 

عَنْ عَائِشَةَ ـ رضى الله عنها ـ قَالَتْ نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ ‏‏وَلاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا‏‏ فِي الدُّعَاءِ‏.‏ 

 

Kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba Iliteremka Aayah hii:

 

وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا  

Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya...

 

Kasema: “Inahusiana na Du’aa.”

 

[Al-Bukhaariy - Kitaab At-Tawhiyd, Kitaab At-Tafsiyr, na Muslim – Kitaab Asw-Swalaah]

 

 

 



057-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Dunia Ni Jela Kwa Muumin, Kafikiri Kwake Ni Kama Jannah

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 57

Dunia Ni Jela Kwa Muumin, Kwa Kafiri Kwake Ni Kama Jannah  

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((الدُّنْيَا سِجْنُ الْمُؤْمِنِ وَجَنَّةُ الْكَافِرِ)) مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Dunia ni jela ya Muumin, na ni Pepo Ya Kafiri)) [Muslim]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Muumin ameharamishwa asivuke mipaka kwa ajili ya matamanio yasiyo ya halali ya kidunia, bali astarehe kwa mazuri aliyohalalishiwa, hivyo huwa kama yuko jela. Ama kafiri, yeye yuko huru kufanya lolote linalomshawishi katika matamanio yake kwa vile anapendelea zaidi maisha ya dunia.

 

 

[Al-A’raaf: 32, Huwd: 15-16, Ar-Ra’d: 26, An-Nahl: 107-109].

 

 

2. Muumin huko Jannah atakuwa huru kutembea atakako. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 وَسِيقَ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ إِلَى الْجَنَّةِ زُمَرًا ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوهَا وَفُتِحَتْ أَبْوَابُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا سَلَامٌ عَلَيْكُمْ طِبْتُمْ فَادْخُلُوهَا خَالِدِينَ﴿٧٣﴾

Na wataendeshwa wale waliomcha Rabb wao kuelekea Jannah makundi-makundi, mpaka watakapoifikia na ikafunguliwa milango yake, na watasema walinzi wake: “Salaamun ‘Alaykum! Amani iwe juu yenu furahini na iingieni ni wenye kudumu.”

 

 

وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي صَدَقَنَا وَعْدَهُ وَأَوْرَثَنَا الْأَرْضَ نَتَبَوَّأُ مِنَ الْجَنَّةِ حَيْثُ نَشَاءُ ۖ فَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ﴿٧٤﴾

Watasema: “AlhamduliLLaahi, Himidi Anastahiki Allaah Ambaye Ametuhakikishia kweli ahadi Yake, na Ameturithisha ardhi tunakaa popote katika Jannah tutakapo”. Basi uzuri ulioje ujira wa watendao. [Az-Zumar: 73-74]

 

 Rejea pia: Al-Kahf (18: 107-108).

 

Ama kafiri, yeye atakuwa jela yaani motoni, na hatoweza kutoka wala kubadilisha hali yake ya adhabu.

 

Rejea: Ghaafir (40: 47-50), Az-Zukhruf 43: 74-78), Al-Muuminuwn (23: 103-108), Ash-Shuwraa (42: 44).

 

 

 3. Dunia ni jela kwa Muumin kulingana na Jannah ya neema za kudumu Aliyoahidi Allaah (سبحانه وتعالى).

 

وَأَمَّا الَّذِينَ سُعِدُوا فَفِي الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۖ عَطَاءً غَيْرَ مَجْذُوذٍ﴿١٠٨﴾

Na ama wale walio furahani, basi watakuwa katika Jannah, ni wenye kudumu humo zitakavyodumu mbingu na ardhi isipokuwa Atakavyo Rabb wako. Ni hiba isiyokatizwa. [Huwd (11: 108)]

 

Rejea pia: Aal-‘Imraan (3: 14-15), At-Tawbah (9: 20-22) (72), Az-Zukhruf (43: (33-35), Al-Bayyinah (98: 7-8).

 

Lakini dunia ni Jannah kwa kafiri kulingana na adhabu ya kudumu Aliyoahidi Allaah (سبحانه وتعالى) Aakhirah. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَا يَغُرَّنَّكَ تَقَلُّبُ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي الْبِلَادِ ﴿١٩٦﴾

Isikudanganye kabisa kutangatanga kwa wale waliokufuru katika nchi.

 

مَتَاعٌ قَلِيلٌ ثُمَّ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۚ وَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿١٩٧﴾ 

Ni starehe ndogo, kisha makazi yao ni Jahannam. Na ni mahala pabaya mno pa kupumzikia. [Aal-‘Imraan (3196-197)]

 

 

Rejea pia: An-Nahl (16: 117), Luqmaan: (31:23-24).

 

 

4. Muumin anatakiwa asiwe mwenye mapenzi makubwa ya dunia na starehe zake, bali awe na shauku ya kupenda nyumba ya kudumu ya Aakhirah. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمَا أُوتِيتُم مِّن شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَزِينَتُهَا ۚ وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٠﴾

Na chochote mlichopewa katika vitu, basi ni starehe za uhai wa dunia na mapambo yake. Na yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi na yakubakia. Je, basi hamtii akilini? [Al-Qaswasw (28: 60)]

 

 

Rejea: Aal-‘Imraan (3: 14), Al-An’aam (6: 32), Al-Hadiyd (57: 20), Al-‘Ankabuwt (29: 64), Al-Kahf (18: 46), Ash-Shuwraa (42: 36), Ghaafir (40: 39), Az-Zukhruf (43: 33-35). 

 

 



Jumatatu, 2 Novemba 2020

Dawa mbadala 14 zinazotibu maumivu ya gauti

Dawa mbadala 14 zinazotibu maumivu ya gauti
Gout au maumivu ya jongo kwa Kiswahili ni aina mojawapo ya maumivu ya mishipa na yanaweza kuleta maumivu makubwa katika maungio hasa katika kidole gumba cha mguu.
Ishara kubwa za maumivu ya jongo ni maumivu ya uvimbe nyakati za usiku, kupatwa na hasira, na maumivu katika kidole kikubwa cha mguu.
Unaweza pia kujisikia maumivu katika kifundo cha mguu, magotini au katika maungio mengine ya mwili.
Kitu kikubwa kinachosababisha maumivu ya jongo au gout ni kiasi kingi cha asidi katika mzunguko wa damu.
Ikiwa unasikia maumivu kila mara katika mikono, vidole, magoti, katika maungio mbalimbali mwilini unashauriwa ukapate vipimo dhidi ya jongo.
Ukiacha maji ya kunywa ambayo ni mhimu sana katika kupunguza kiasi cha asidi mwilini, Hapa nimekuandikia mimea na matunda mhimu ambavyo vimejaribiwa na kuonyesha uwezo mkubwa katika kupunguza maumivu yatokanayo na gout.
1. Juisi ya limau
Juisi ya Limau ina viinilishe vya asili ambavyo vinaweza kusaidia kutibu maumivu ya jongo au gout kama tulivyozoea wengi wetu.
Tafiti zinaonyesha kuwa matunda jamii ya chungwa kama vile machungwa yenyewe, machenza, na limau au ndimu husaidia kuyeyusha asidi iliyogandamana katika damu na hivyo kukupatia nafuu ya haraka itokanayo na maumivu ya gout.
Tengeneza juisi hii ya limau ukichanganya na maji na unywe mara tatu kwa siku kwa majuma kadhaa.
2. Siki ya tufaha
Kwakuwa tunda la tufaha ni zuri katika kudhibiti gout hakuna shaka kwamba siki yake isiweze kudhibiti gout.
Na kwa kawaida siki ya tufaha inafanya vizuri kutibu gout kuliko hata tunda lake.
Siki ya tufaha ina asidi nzuri iitwayo acetic acid ambayo huongeza kiasi cha alkalini ndani ya mwili na kuunda usawa na mazingira mazuri ya pH (Potential Hydrogen) na hivyo moja kwa moja kuwa msaada mkubwa katika kupunguza na hata kutibu maumivu ya gout.
Kumbuka pia hakuna utafiti ambao umefanywa kuthibitisha madai haya ya siki ya tufaha kuwa na uwezo huu.
Unaweza kuchanganya siki ya tufaha katika chakula unachokula au kuongeza kijiko kikubwa kimoja katika glasi ya maji na unywe mara moja kila siku.
3. Baking Soda
Baking soda ina faida nyingi na matumizi mengi sana ikiwemo kukusaidia katika tatizo lako la gout.
Sodium bicarbonate iliyomo kwenye baking soda huifanya damu kuwa na alkalini zaidi kitu ambacho ni mhimu katika kudhibiti gout.
Chota kijiko kimoja kidogo cha baking soda na uiweke katika maji robo lita na unywe kutwa mara mbili kwa majuma kadhaa.
Kama unasumbuliwa na shinikizo la juu la damu usiitumie hii baking soda kujitibu gout.
4. Nanasi
Nanasi lina kimeng’enya mhimu kiitwacho ‘bromelain’ ambacho kina sifa ya kuzuia muwako wa ndani ya mwili (inflammation).
Kwahiyo kuwa na mazoea ya kula nanasi kila siku kunaweza kuzuia usipatwe au hata kupunguza maumivu yatokanayo na gout.
5. Zabibu
Zabibu zina kiasi kingi cha kiuaji sumu na zinaweza kupunguza maumivu ya gout kwa haraka zaidi.
Mbegu za tunda la zabibu zina kitu mhimu kiitwacho pycnogenols ambacho ni kiuaji sumu kingine kinachosaidia kupigana na aina zote za maumivu ya mishipa ikiwemo gout.
Kula kila siku zabibu na utaona matokeo mazuri dhidi ya maumivu yako ya gout.
6. Tangawizi
Tangawizi ina matumizi mengi na imekuwa kwenye orodha ya dawa za asili au mbadala kwa ajili ya kutibu maradhi mengi kwa miaka mingi ikiwemo gout.
Chemsha maji kama unachemsha maji ya chai, chukua tangawizi mbichi yaani ile ambayo siyo ya unga, kwangua (grate) kipande kimoja au viwili vya tangawizi ndani ya maji hayo yanayochemka, acha ichemke kama dakika 10, ipuwa na unywe kama chai kutwa mara tatu kwa wiki 3.
Unaweza kuongeza asali au hata sukari kwenye huo mchanganyiko wa maji na tangawizi.
7. Ndizi
Ndizi zina kiasi kingi cha Potassiamu na Vitamini C na zinao uwezo pia wa kupunguza maumivu yatokanayo na gout kwa kuyeyusha asidi iliyoganda kwenye mkojo kuwa katika umajimaji ambao mwili wako unaweza kuutoa nje kirahisi.
Kula ndizi kila mara kama unasumbuliwa na gout.
8. Mcheri
Tunda la mcheri lina kiasi kingi cha Vitamini C ambayo ni msaada mkubwa katika kupunguza asidi katika damu.
Matunda 20 ya mcheri yakiliwa katika vipindi tofauti tofauti katika siku yanaweza kufanya maajabu dhidi ya maumivu yako ya gout.
Ukinywa juisi ya mcheri pia ina matokeo yaliyo sawa na ukila matunda yake.
9. Unga wa mkaa
Pengine tayari unajuwa kuwa mkaa unao uwezo wa kuondoa harufu mbaya na hata sumu mwilini.
Lakini lile ulikuwa hujuwi hadi sasa ni kuwa unga wa mkaa ambao unapatikana kwa kuusaga tu mkaa, unaweza pia kupunguza maumivu yatokanayo na gout.
Changanya unga huu wa mkaa katika maji, chukua kitambaa kilichotengenezwa kwa pamba na ukiloweke kwenye hayo maji kisha funika katika eneo lenye maumivu ukiacha hapo kwa dakika kadhaa mara kwa mara kwa siku kwa majuma kadhaa kutasaidia kama siyo kuondoa kabisa maumivu ya gout.
10. Maji ya Kunywa
Maji ni mhimu sana katika kushusha maumivu ya kwenye maungio ikiwemo gout.
Maji ndicho kilainishi mhimu katika viungo vyote vya mwili.
Kunywa kila siku glasi 8 mpaka 10 za maji, maji yaliyo katika joto la kawaida na siyo ya baridi, ukifanya hivi kila siku baada ya wiki 2 au 3 utakuwa huru kabisa na maumivu ya gout.
11. Juisi ya maharage machanga (French Beans)
Kunywa Juisi hii ya maharage machanga kwa muda wa mwezi mmoja ili kupata matokeo mazuri.
Shida itakuwa namna ya kuyapata haya maharage hasa kwa wale walio nje ya D’salaam lakini ukihitaji nijulishe.
12. Mharadali
Mharadali (Mustard) ni nzuri sana katika kupunguza maumivu ya gout.
Chukuwa mharadali ya unga na uweke kwenye eneo lenye maumivu na uuache ufyonzwe na ngozi yako kwa usiku mzima na utakapoamka asubuhi utajisikia vizuri kabisa.
13. Mchanganyiko wa juisi ya matunda na mboga mboga
Mchanganyiko wa juisi ya tango, magimbi na karoti unawea kutumika kutuliza maumivu yatokanayo na gout haraka sana.
14. Mafuta ya nyonyo
Pasha kidogo mafuta ya nyonyo katika moto kisha pakaa eneo lenye maumivu taratibu kama vile unafanya masaji kwa dakika kadhaa mara mbili mpaka tatu kwa siku, fanya hivi kila siku mpaka utakapopona kabisa.
Ikiwa utahitaji mojawapo ya hizi dawa wasiliana na mimi kwenye WhatsApp +255714800175
Ikiwa huhitaji dawa unahitaji ushauri tu wa bure niulize hapa hapa chini kwenye comment nitakujibu tena hapa hapa BURE.
Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 23

Let's block ads! (Why?)

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...