SUMU ni kitu chochote ambacho kinaweza kuingia mwilini na kusababisha mifumo ya mwili ishindwe kufanya kazi ipasavyo.
Unafikiria kuwa una afya njema, lakini haujisikii vyema. Unapuuza, unaona ni vitu vidogo vidogo.
Hivyo, haushughuliki kwenda hospitali au kwa wataalamu wa afya kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
Hatimaye tatizo linakuwa kubwa. Unafika hospitali unaambiwa una saratani, unapata mshtuko mkubwa! Unaambiwa chanzo cha ugonjwa hakifahamiki, ila unaelezwa chakula na mtindo wa maisha kwa ujumla ni sababu kubwa.
Hii ina maana kuna uwezekano umeingiza sumu nyingi mwilini. Kinga ni bora kuliko tiba. Kama ungeelewa mapema, ungejikinga na saratani.
Sizungumzii sumu za kung’atwa na nyoka, wala sizungumzii sumu zinazohitaji matibabu ya dharura.
Nazungumzia sumu ambazo zinatuua polepole na kimya kimya bila ya sisi kujua wala kutambua chochote. Nazungumzia sumu ambazo kila kuchapo tuko kwenye mlango wa daktari.
Kila kuchapo afya zetu hizidi kuzorota zaidi. Hizi ni sumu ambazo ziko kwenye vyakula vyetu.
Ni sumu tunazozivuta katika hewa kila siku kutokana na mioshi ya magari, viwanda n.k.
Sumu ambazo zinaweza kutokana na madawa mbalimbali tunayojitibia afya zetu, sumu zinazotokana na vipodozi mbalimbali tunavyotumia kila siku kwa ajili ya urembo na kupendeza.
Tunapata sumu mwilini kwa sababu lazima tuvute hewa, hata kwa sekunde kadhaa tusipopata hewa ya oksijeni tunakufa.
Lakini tunavuta hewa iliyochafuliwa na mioshi ya viwanda na magari ambayo imetamalaki kila kona.
Hivyo lazima tufe polepole na kimya kimya!
Tunapata sumu mwilini kwa sababu lazima tule na tunywe. Lakini kwa bahati mbaya, vyakula vingi tunavyokula siyo salama, vimesheheni kemikali.
Tunapata sumu kwa sababu lazima tujipodoe, lazima tujipambe tupambike, na lazima tung’are tupendeze.
Kwa bahati mbaya sana, vipodozi vingi vimekuwa siyo vipodozi, ni vipopozi. Vimejaa kemikali ambazo huleta madhara mengi ya kiafya.
Tunapongeza mamlaka ya chakula na dawa, TFDA, kwa kuviteketeza baadhi ya vipodozi na kutoa orodha ya vipodozi visivyofaa, lakini hata hivyo juhudi kubwa lazima ifanyike.
Ishara zitakazokuonyesha mwili wako una sumu nyingi:
-Uchovu sugu
-Maumivu ya maungio
-Msongamano puani
-Kuumwa kichwa kila mara
-Tumbo kujaa gesi
-Kufunga choo au kupata choo kigumu
-Kukosa utulivu
-Matatizo mbalimbali ya ngozi ikiwemo chunusi
-Pumzi mbaya
-Mzunguko wa hedhi usio sawa
-Kuishiwa nguvu
-Kushindwa kupungua uzito
-Kupenda kula kula kila mara
Kinachosababisha mwili kuwa na sumu au taka taka
Mwili unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na mwili kwa namna mbili, ama kupitia mazingira tunayoishi (viwanda, migodi nk) au kupitia vyakula na vinywaji ambavyo tunatumia kila siku.
Sumu au taka pia zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali hasa za kizungu tunazotumia kujitibia magonjwa mbalimbali.
Mwili huzalisha hizi sumu au takataka (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng’enyo wa chakula mwilini mwako.
1. Kutokula matunda na mboga za majani
Matunda na mboga za majani ni vitu viwili mhimu sana ili kusafisha mwili wako na kukukinga dhidi ya sumu na taka taka mbalimbali.
Kama huna tabia ya kula matunda na mboga za majani kila siku ni wazi mwili wako utatengeneza sumu za kutosha.
2. Kula vyakula vya viwandani
Kama unataka kuepuka sumu au takataka nyingine kirahisi kuingia katika mwili wako basi pendelea zaidi kula vyakula vya asili vinavyopikwa nyumbani kuliko kula vya kwenye makopo au vya dukani au vya kwenye migahawa (fast foods).
3. Kutokunywa maji mengi kila siku
Sababu kubwa ya watu wengi kutengeneza sumu au taka mwilini mwao ni kutokunywa maji mengi kila siku. Maji ni uhai, bila kunywa maji mengi kila siku ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.
Haijalishi upo mazingira gani kama ni ya baridi au ni ya joto ni LAZIMA UNYWE MAJI YA KUTOSHA KILA SIKU IENDAYO KWA MUNGU.
Unahitaji maji glasi 8 mpaka 10 kila siku. Watu wengi wanahangaika namna ya kuondoa sumu kusafisha miili yao bila kujua kuwa maji pekee ya kunywa yanatosha kwa kazi hiyo.
Kumbuka asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 za ubongo wako ni maji, hivyo kama huna mazoea ya kupenda kunywa maji kila siku ni rahisi mwili wako kutengeneza sumu. .
4. Vinywaji vyenye kaffeina
Kama tayari imethibitika una sumu au takataka nyingi mwilini nakushauri uache kunywa chai ya rangi na kahawa.
Badala yake hamia kutumia chai yenye tangawizi au mdalasini au mchaichai.
Chai ya rangi na kahawa vina kaffeina ambayo kwanza huyasukuma maji nje ya mwili kwa haraka na kuuacha mwili bila kuwa na maji ya kutosha kwa ajili ya kazi zake.
Kaffeina pia ni madawa ya kulevya kundi la madawa yanayosisimua mwili (stimulants drugs).
5. Kutopata usingizi wa kutosha kila siku
Moja ya vitu vinaweza kukupelekea kuwa na sumu mwilini au takataka nyingi ni pamoja na kutokulala muda wa kutosha kila siku. Usingizi haukopwi na huwezi kuwa na ufanisi katika kazi zako kama hupati usingizi wa kutosha kila siku.
Usingizi siyo jambo la starehe tu, ni sehemu mhimu sana katika afya yako ya kila siku.
Bila kupata usingizi wa kutosha unaweza kuwa karibu na matatizo kama kuongezeka uzito, kushuka kwa kinga ya mwili na nguvu zako za mwili kwa ujumla zinaweza kushuka.
Unapopata muda wa kutosha wa kulala masaa 7 mpaka 8 kwa siku unaupa mwili wako nafasi ya kutosha ya kupumzika na kujiripea upya na hivyo ndivyo sumu na takataka nyingine zinavyoweza kukutoka kirahisi.
Ingia kulala mapema walau saa tatu usiku ingia kulala siyo unakaa unaangalia tamthiliya au mpira mpaka saa sita za usiku!
6. Mazingira tunayoishi
Kuna mazingira yanajulikana wazi kuwa ni vyanzo vya sumu mwilini. Maeneo ya migodi ya madini, maeneo yenye viwanda vingi, maduka yanayouza dawa za kilimo nk
Maeneo haya yanafaa kukaa mbali na makazi ya binadamu kwa usalama wa afya zetu.
7. Vyakula vilivyokobolewa
Ili kuwa na mwili msafi kabisa epuka kula mkate mweupe, sukari na vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi kama vile chipsi, maandazi na vingine vyote vinavyochomwa katikati ya mafuta mengi.
Mkate upo mkate mweusi (brown bread), sukari ipo asali mbichi, vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi unaweza kuamua kuwa unavioka (bake) au uvichemshe (boiling). Uchaguzi ni wako.
8. Mfadhaiko (stress)
Kile tayari unajuwa ni kuwa mfadhaiko au stress ni jambo baya kwa afya yako. Kile unatakiwa kujua kuanzia sasa ni kuwa ili kubaki na afya bora kabisa yenye TBS basi ukae mbali na stress.
Kama utaruhusu stress kutawala maisha yako basi ujuwe mwili wako hauwezi kufanya kazi zake vizuri ikiwemo ya kuondoa taka au sumu mbalimbali mwilini.
Stress peke yake inaweza kupelekea magonjwa mbalimbali mwilini zaidi ya 50. Unapokuwa na mfadhaiko mwili wako hauwezi kutoa taka nje kirahisi na kinga yako ya mwili inashuka matokeo yake unakuwa karibu na magonjwa mengine mengi.
Watu wengine wenye uelewa mdogo wakiwa na stress hukimbilia kutumia vilevi wakidhani zitapungua kumbe ndiyo wanazidi kuongeza tatizo bila kujua.
9. Dawa za kizungu
Dawa nyingi za hospitali huwa zina matokeo chanya (positive) na matokeo hasi (negative) pia ambayo ndiyo matokeo mabaya.
Kama unalazimika kutumia antibiotic kila mara au unameza dawa za kuondoa maumivu kila mara unaweza kuwa unaongeza sumu na taka mwilini bila kujua na bila sababu yoyote ya lazima.
Kuepuka hilo jaribu kutumia mitishamba au mimea ya asili kwa baadhi ya magonjwa ambayo si lazima uende hospitali. Siyo mafua tu mtu ameenda kuchoma sindano!
10. Vilevi
Moja ya vitu vinavyoweza kuleta sumu au taka mwilini moja kwa moja ni vilevi. Vilevi kama pombe, madawa ya kulevya, sigara, bangi na vinginevyo ni vitu vinavyopelekea mwili kuwa na taka moja kwa moja.
Namna pekee ya kuondoa sumu kutokana na vilevi ni kuviacha hivyo vilevi, ndiyo kuviacha.
Usitegemee asubuhi utumie dawa kuondoa sumu mwilini halafu jioni ukanywe pombe au ukavute sigara utegemee tu ile dawa uliyotumia asubuhi kwamba itafanya kazi, hapana unajidanganya, dawa ni kuacha vilevi moja kwa moja.
Vingine vya kuacha kama tayari imegundulika una sumu nyingi mwilini ni pamoja na vinywaji baridi vyote, juisi zote za dukani, chai ya rangi na kahawa.
Dawa ya kutoa sumu mwilini > Unga wa majani ya Mlonge
Unga wa majani ya mlonge ndiyo dawa pekee ya asili ya uhakika ya kuondoa sumu mwilini.
Hii ni orodha ya viondoa sumu (antioxidants) 46 na zaidi vipatikanavyo katika mlonge:
Antioxidants (9, 11, 12, 13, 14, 15)
- β-carotene
- calcium
- potassium
- quercetin
- chlorogenic acid
- hydroxyanisole (BHA)
- butylated hydroxytoluene (BHT)
- tertiary-butylhydroquinones
- propyl gallate
- vitamin E (tocopherols)
- ascorbic acid (vitamin C)
- glucose oxidase
- reduced glutathione
- citric acid
- polyphospages
- aminopolycarboxylic acids
- vanillin
- moringine
- strophantidin
- 4-(α-l-rhamnosyloxy)
- benzyl isothiocyanate
- 4-(4’-O-acetyl-α-l-rhamnosyloxy)
- benzyl isothioyanate
- catechin
- 4-(β-d-glucopyranosyl-1→4-α-l-rhamnopyranosyloxy)
- benzyl thiocarboxamide
- epicatechin
- 4-O-(α-l-rhamnosyloxy)
- benzyl glucosinolate
- 4-(α-l-rhamnopyranosyloxy)-benzylglucosinolate
- Kaempferol
- Niazimicin
- 4-(α-l-rhamnosyloxy)
- benzyl acetonitrile (niazirin)
- O-ethyl-4-(α-l-rhamnosyloxy)
- benzyl carmate
- Gallic acid
- Glycerol-1-1-(9-octadecanoate)
- p-Coumaric acid
- 3-O-(6’-O-oleoyl-β-d-glucopyranosyl)-β-sitosterol
- Ferulic acid
- β-sitosterol-3-O-β-d-glucopyranoside
- Caffeic acid
- 3-Hydroxy-4-(α-l-rhamnopyranosyloxy)
- benzyl glucosinolate
- Protocatechuic acid
- 4-(2/3/4′-O-acetyl-α-l-rhamnopyranosyloxy)
- benzyl glucosinolate
- cinnamic acid
- glucosinalbin
- ellagic acid
- glucoraphanin
- glucoiber
Mlonge unasafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele.
Mlonge una Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe. Mlonge UNA MADINI YA CHUMA MARA 25 ZAIDI YA ILE ILIYOMO KWENYE SPINACHI
Changanya matunda yote na mboga za majani zote bado viinilishe vyake kwa pamoja haviwezi kuvifikia vile vilivyomo kwenye mlonge!
Ni kusema mtu aliyekula matunda na mboga za majani zote bado hatakuwa na afya bora kama yule atakayetumia mlonge tu.
*Usitumie dawa hii bila uangallizi wa karibu wa Tabibu.
Kama unahitaji unga wa majani ya mlonge kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili niachie ujumbe WhatsApp +255714800175
Unga wangu wa majani ya mlonge ni mzuri na naweza kusema pasipo na hofu kuwa huwezi kupata sehemu nyingine wenye ubora unaokaribia na wangu. Ninauandaa kwa umakini mkubwa ili ubaki na viinilishe vyake na ni wa kijani kweli kweli