Translate

Ijumaa, 24 Aprili 2020

Mwenendo wa virusi vya corona dunia nzima

Mwenendo wa virusi vya corona dunia nzima

Corona Virus Daily Updates

  • Idadi ya waliopimwa na kuthibitika na virusi vya corona (cases)
  • Idadi ya waliokufa (Deaths)
  • Idadi ya waliopona dunia nzima (Recovered)
  • Wenye hali mbaya zaidi (Critical)

Takwimu za mwisho za kila siku kidunia na Tanzania

Global Total
Last update on:
Cases Today

Deaths Today

Affected Countries

Total in Tanzania
Last update on:
Cases Today

Deaths Today

Cases Per Million

Tafuta jina la nchi yako na upate takwimu zake pia zipo takwimu kwa nchi zingine zote dunia nzima

Sort by confirmed numbers.

Country or Region Cases Deaths Recovered

Soma hii pia > Dawa ya asili inayoongeza kinga ya mwili

Mjulishe rafiki yako kwenye Twitter asome taarifa hizi kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Mwenendo wa virusi vya corona dunia nzima Click To Tweet

Data source

SHARE post hii na wengine uwapendao

Imesomwa mara 22

Let's block ads! (Why?)

Jumatano, 22 Aprili 2020

Madhara 9 ya vidonda vya tumbo mwilini

Madhara 9 ya Vidonda vya tumbo mwilini

Vidonda vya tumbo ni majeraha au vidonda ndani ya kuta za tumbo.

Majeraha au vidonda hivyo huleta maumivu yanayokera na hutokea mara nyingi tumboni na yanaweza kutibika lakini kama hutachukuwa hatua mapema za kutibu yanaweza kukuletea majanga mengine mengi kiafya.

Tumbo na utumbo mdogo vina kuta maalumu yenye ute ute wa ulinzi ambao hulilinda tumbo lako dhidi ya maadui wanaoleta shida tumboni mwako yaani bakteria wabaya, virusi na vijidudu nyemelezi vingine.

Wakati kuna vitu vingi vinavyoweza kukusababishia vidonda vya tumbo ikiwemo kutumia dawa za kupunguza maumivu kwa muda mrefu bila ushauri wa kitaalamu, kuvuta sana sigara au kunywa pombe kupita kiasi; kuna bakteria ambaye anaweza kulaumiwa kama mhusika mkuu wa vidonda vya tumbo.

Bakteria huyo anajulikana kama helicobacter pylori kwa kifupi H. pylori. Ni bakteria mwenye umbo la duara ambaye hushambulia ute ute wa ulinzi wa tumbo na sehemu ya juu ya utumbo mdogo.

Matokeo ya mashambulizi hayo ya huyu bakteria ni kutokea kwa vidonda kwenye kuta za tumbo na kuweka uwazi (vidonda) ambavyo hutumika kama njia ya kupitia bakteria wengine wabaya na kuongeza gesi tumboni.

Wakati hakuna uelewa wa moja kwa moja ni jinsi gani huyu bakteria anaingia tumboni, bado ni bakteria wa kawaida anayepatikana tumboni mwa watu wengi na anaweza kukuingia kupitia chakula na maji ya kunywa.

Tatizo la vidonda vya tumbo linalosababishwa na huyu bakteria ni kuwa anachelewa sana kukuonyesha dalili kwamba una vidonda vya tumbo.

Wakati unaweza kuishi na vidonda vya tumbo kwa muda fulani bila kukuletea shida kubwa, kuviacha kwa muda mrefu bila kupata matibabu kunaweza kukuletea madhara yafuatayo;

Madhara 9 ya Vidonda vya tumbo mwilini

  1. Kuvuja damu ndani ya mwili (Internal bleeding and serious blood loss)
  2. Upungufu wa damu (Anemia)
  3. Kutapika damu
  4. Kupata kinyesi cheusi kama cha mbuzi
  5. Kuvurugika kwa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula (Obstructed digestion)
  6. Shida katika kupumua
  7. Saratani ya tumbo (Stomach cancer)
  8. Msongo wa mawazo (stress)
  9. Kupungua kwa nguvu za kiume

Ni mhimu kupata vipimo na uchunguzi zaidi wa daktari mapema tu unapohisi unaweza kuwa na vidonda vya tumbo ili kuzuia usipatwe na madhara haya yatokanayo na vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo huwa ni rahisi kutibika unapowahi kuanza matibabu kuliko ukisubiri mpaka viwe sugu.

Soma hii pia > Uhusiano wa vidonda vya tumbo na saratani ya tumbo

Madhara 9 ya Vidonda vya tumbo mwilini

Madhara ya vidonda vya tumbo

.

Vyakula hivi usile kama unaumwa vidonda vya tumbo

Kuna maelezo mengi juu ya vyakula kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Kuna wanaosema hiki hakifai wengine hiki kinafaa lakini kwa ujumla vyakula vifuatavyo vinakubalika na wengi kwamba havifai kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo, navyo ni;

  • PiliPili Manga nyeusi na nyeupe
  • PiliPili kichaa
  • Vinywaji vyenye Kaffeine
  • Kahawa
  • Pombe
  • Chai ya rangi
  • Chokoleti na cocoa
  • Soda zote
  • Sukari na viongeza utamu vingine vya kutengenezwa
  • Wali na ugali wa sembe
  • Vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi kama vile maandazi nk (Fried foods)
  • Nyanya
  • Mnanaa (Peppermint)
  • Mbegu mbegu zenye Omega – 6
  • Maziwa fresh na bidhaa nyingine zinazotokana na maziwa

Kuepuka vyakula hivi ni hatua moja kuelekea kwenye uponyaji wako hata hivyo unahitaji kubadili tabia zako zingine ikiwemo kuachana na msongo wa mawazo (stress) kwa gharama yoyote.

Iwe ni mtu ambaye una kawaida ya kuugua vidonda vya tumbo mara kwa mara au huumwi vidonda vya tumbo kwa sasa, kuviepuka vidonda hivi ni pamoja na kuhakikisha mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula unafanya kazi vizuri kwa kiwango chake cha juu kabisa.

Pia unaweza kuimarisha afya ya mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kwa kufanya yafuatayo:

  1. Kunywa maji glasi 2 (nusu lita) mara tu uamkapo kutoka kitandani kila siku. Kunywa tena kiasi hiki cha maji kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na cha jioni kila siku.
  2. Kula chakula kichache milo mingi. Kula hata mara 5 kwa siku lakini chakula kidogo kidogo siyo kingi kwa wakati mmoja.
  3. Kula pole pole ulapo chakula
  4. Hakikisha unapokula chakula huna mawazo mawazo (stress) yoyote.
  5. Kula zaidi vyakula vyenye nyuzi nyuzi
  6. Kula vyakula vyenye bakteria wazuri (probiotics) kama vile mtindi na uji wa unga wa ndizi

Hata kama utampata huyu bakteria (H. pylori) kama unao bakteria wengine wazuri tumboni ni rahisi kwako kumdhibiti huy anayeleta vidonda vya tumbo.

Kuimarisha afya ya mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula ni jambo zuri kiafya siyo kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo tu bali kwa mtu yoyote asiyependa kuugua mara kwa mara kwani tumboni ndiko kuliko na injini ya mwili wote kwa ujumla.

H. pylori ni bakteria anayesababisha vidonda vya tumbo kwa karibu ya zaidi ya nusu ya watu wote duniani hivyo uwezekano wa kumpata au kuugua ugonjwa huu ni mkubwa sana kwa mtu yoyote.

Kama unahitaji dawa ya asili inayotibu kabisa vidonda vya tumbo niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.

Kama unapenda kujifunza mengi kuhusu vidonda vya tumbo bonyeza HAPA.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Mjulishe rafiki yako kwenye Twitter naye asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Madhara 9 ya vidonda vya tumbo mwilini Click To Tweet

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine

Imesomwa mara 1

Let's block ads! (Why?)

Fahamu kuhusu kirusi cha korona

Fahamu kuhusu kirusi cha korona

Kirusi cha Korona

Fahamu kuhusu kirusi cha korona

Kirusi cha korona (Coronavirus), ni kimelea chenye gamba na kutunza vinasaba vyake katika malighafi za RNA.

Corona virus nikisababishi cha magonjwa mbalimbali na vimelea hivyo vina makabila mbalimbali.

COVID-19 Corona Virus Disease 2019 yaani; Ugonjwa utokanao na virusi vya korona vilivyogunduliwa mwaka 2019

Historia•

Kirusi cha korona (coronavirus) kimechukua jina lake ‘corona’ kutoka lugha ya kilatini kikimaanisha taji (crown) hii ni kutokana na muonekano wakirusi hicho katika hadubini hufanana na taji ya mfalme.

•Kirusi hicho hutoka katika kundi la vimelea vingi viletavyo homa za mfumo wa hewa mfano mafua.

Kundi hilo la kirusi cha korona lina makabila (strains) mengi ambayo mpaka sasa hayajagunduliwayote.

•Moja ya kabila limegunduliwa mnamo mwezi wa kumi na mbili mwaka 2019 mjini Wuhan, China nalo hujulikana kama 2019–nCoV (Novelcoronavirus).–

Hili ni kabila hatarishi sana kati ya makabila yote ya korona yaliyogunduliwa. – Husababisha kifo.

Ugonjwa wa Korona

•Kirusi cha korona husafilishwa kutoka kwa wanyama kwenda kwabinadamu (zoonoticdisease).

•Baadhi ya wanyama ambao hutunza virusi vya korona na kuleta maradhi ni;–Popo–Ngamia–N.k.

Nani hupatwa na korona?

•Watu wote (wa kike kwa kiume) waweza kudhurika na korona

•Wenye maradhi yanayoshusha kinga mwili huwa na hatari kubwa Zaidi.

•Wazee pia wapo katika hatari kubwa kupata korona kwani wana kinga mwili hafifu.

Ukubwa wa tatizo mpaka sasa

•Hili ni tatizo linalotishia kusambaa dunia nzima likianzia mjini Wuhan, China

Dalili za mgonjwa wa korona

Dalili zionekanazo mara kwa mara

•Homa •Kikohozi kibichi
•Uhemaji wa tabu
•Maumivu ya mwili
•Kuuma kwa koo mfano wa matonses (tonsillitis)
•Kukosa hamu ya kula

Dalili za mara chache

•Kuhara
•Kutapika
•Kichwa kuuma
•Kukohoa damu
•Maumivu ya kifua

Kirusicha korona katika mwili wa binadamu

•Huchukua siku 2 mpaka 14 (wastani siku 5) kwa binadamu kuanza kuonesha dalili baada ya kuambukizwa na virusi vya korona (incubation period)

•Huambukizwa kwa njia ya matone yatokanayo kwa kukohoa au kugusana moja kwa moja.

•Epuka kusalimiana kwa mikono

Wakati gani waweza kudhani ni COVID 19

•Mgonjwa mwenye dalili za homa ya mfumo wa hewa wa chini (LRTI) – tazama kipengele cha dalili na sio homa ya mfumo wa hewa wa juu (mfano: Kukohoa , pua kuwasha, chafya, koo kuuma) na endapo mgonjwa huyo ana historia za Kusafiri kutokea nchi zenye uwezekano mkubwa wa maambukizi ndani ya siku 14

Matibabu

•Dawa za kufifisha makali ya virusi huenda zinaweza kusaidia, lakini bado haijathibitishwa.

–Lopinavir
–Ritonavir
–Ganciclovir
–Oseltamivir
–Remdesivir
–Interferon alpha

Dalili hatari za ugonjwa wa korona

•Homa kali ya mapafu (severe pneumonia)
•Utindio wa ubongo
•Kuhema kwa shida na kutoa mlio wa kifilimbi mithili ya mgonjwa wa pumu.

Je, mgonjwa wa nje anaweza kupata tiba ya dawa za kufifisha virusi?

•Haishauliwi
•Mgonjwa aliyelazwa ndiye anaweza kupata dawa hizo.

Je, dawa za kuongeza kinga mwili (Ig) zinaweza kutibu?

•Hakuna shuhuda za dawa hizo kutibu.
•Dawa hizo zinaweza kusaidia tuu kwa kiasi fulani (immunomodulator) kwenye hali ya homa kali ya mafua (severe pneumonia)

Je, dawa ya Chloroquine hutibu korona?

•Chloroquine husaidia kutibu homa kali ya mapafu(SARS–Co-2)
•Kwa sasa, chloroquine haisaidii katika kutokomeza ugonjwa wa korona.

Je, siruhusiwi kuwapa tiba hewa(nebulization) wagonjwa?

•Ndiyo, ikiwa kuna visa vya korona vilivyothibitishwa katika eneo husika haishauriwi kumpa mgonjwa tibahewa.

•Tibahewa huongeza hatari ya usambaaji wa matone yenye maambukizi kwenda mbali Zaidi.

•Dawa za kuvuta (inhaler) huweza kutumika kama m’badala wa tibahewa.

Kipi ni bora Zaidi katika kumpa mgonjwa hewa ikiwa kuna ugonjwa wa korona?

•Mirijahewa (Oxygenprongs) ni salama Zaidi ukilinganisha na vifunika mdomo na uso (facemasks)

Mtu niliyesafiri naye kwenye ndege amegundulika kuwa ana virusi vya Korona!!!!!!

• Usihofu!

– Ikiwa ulikaa naye umbali wa Zaidi ya viti viwili nusu kipenyo kutoka kwake, hatari ya maambukizo kwako ni ndogo mno.

Je, kuwatenga washukiwa wa korona huongeza hatari ya kuambukizana?

• Ikiwa nafasi kati ya vitanda viwili katika eneo la kuwatenga ni chini ya futi 6, hatari ya kuambukizana ni kubwa!

Kinga

• Kuosha mikono vizuri kwa maji safi na sabuni

• Tumia vikinga pua na mdomo (masks) ikiwa unahudumia washukiwa wa korona.

• Epuka kugusa na kurekebisha kikinga mdomo na pua (mask) na uso.

• Zingatia walau umbali wa futi 6 kutoka kwa mgonjwa mwenye korona

• Hakuna chanjo mpaka sasa

1. Lini kuvaa mask

• Kwa watu mwenye afya vaa mask endapo unamuhudumia mshukiwa wa COVID – 19

• Vaa mask kama unakohoa au kupiga chafya

• Mask husaidia tuu endapo utazingatia usafi wa mikono kwa kutumia kitakasi (alcohol-based hand rub) cha kileo au sabuni na maji.

• Uvaapo mask unatakiwa kufahamu namna ya kuitumia na kuitupa pia.

2. Je, nCOV-2019 huambukiza kwa wakubwa au wadogo

• Watu wa umri wote huweza kuambukizwa nCOV-2019

• Wazee na watu wenye maradhi (mfano: Pumu, kisukari, maradhi ya moyo) wana hatari kubwa ya kupata COVID-2019 na pengine kupoteza uhai.

• WHO inashauri watu wote kufuata kanuni za ufya na usafi wa njia ya hewa.

3. Je, mifugo ya nyumbani inaweza kusambaza Ncov-2019?

• Kwa sasa hakuna shuhuda zinazoonesha kuwa wanyama wa nyumbani (pets) mfano mbwa au paka huweza kupata kupata maambukizo ya nCOV-2019.

– Hata hivyo, inashauriwa kuosha mikono kwa maji na sabuni mara baada ya kugusana na mbwa/paka.

4. Je, chanjo ya homa ya mapafu husaidia kukinga nCOV-2019?

• HAPANA! Chanjo za homa ya mapafu, kama pneumococcal vaccine na Haemophilus influenza type B (Hib) vaccine, haziwezi kukukinga dhidi ya nCOV-2019.

– Japo chanjo hizi hazisaidii kukinga Ncov-2019, chanjo hizi ni za muhimu na zinashauriwa ili kulinda afya yako.

5. Je, dawa za kuua vimelea (antibiotics) husaidia kukinga nCOV-2019?

• HAPANA! Viua vimelea haziuwi virusi, huua bakteria tuu.

• nCOV-2019 ni kirusi pia, hivyo viua vimelea (antibiotics) zisitumike katika kutibu au kukinga.

• Japo, kwa mgonjwa aliyelazwa kwa COVID-2019, mgonjwa anaweza kupewa dawa hizo kwani bakteria pia wanaweza kushambulia mwili.

6. Je, kusuuza pua kwa maji ya chumvi husaidia kukinga maradhi ya COVID-2019?

• HAPANA! Hakuna shuhuda zioneshazo kuwa kusuuza pua mara kwa mara kwa maji ya chumvi hukinga maambukizi ya nCOV-2019.

• kuna baadhi ya shuhuda zioneshazo kuwa kusuuza pua mara kwa mara kwa maji ya chumvi husaidia mtu kupona mafua ya kawaida tuu.

• Lakini tiba hii haiwezi kutibu maradhi ya mfumo wa hewa.

7. Je, vipimajoto husaidia kwa kiasi gani katika kutambua maambukizi ya nCOV-2019?

• Vipima joto husaidia kugundua kuongezeka kwa joto mwilini kwa watu wenye homa kutokana na maambukizi ya nCOV-2019.

• Vifaa hivi haviwezi kutambua maambukizi kwa mtu ambaye ameambukizwa virusi na hajaanza kupata dalili.

– Hii ni kwasababu huchukua siku 2 hadi 10 mpaka mtu aliyeambukizwa apate homa.

8. Je, kula vitunguu saumu husaidia kukinga maradhi ya nCOV-2019?

• Vitunguu saumu ni vyakula vya afya ambavyo huenda zina baadhi ya nguvu za kuua bakteria.

• Hata hivyo, hakuna shuhuda mpaka sasa zioneshazo kuwa kutafuna kitunguu saumu hukinga maradhi ya COVID-2019.

Soma hii pia > Vyakula 16 vinavyoongeza kinga ya mwili

9. Je, miale ya mwanga wa taa za ultraviolet huweza kuua nCOV-2019?

• Miale ya taa za ultraviolet (UV) isitumike kutakasa mikono au sehemu zingine za ngozi, kwani miale hiyo huweza kuleta madhara katika ngozi.

10. Je, vikausha mikono (hand dryers) husaidia kuua nCOV-2019?

• HAPANA! Vikausha mikono vya umeme haviwezi kuua nCOV-2019.

• Kujikinga na maambukizi unatakiwa usafishe mikono yako kwa kileo (alcohol-based hand rub) au osha mikono kwa maji safi na sabuni. Ukishaosha mikono yako ikaushe kwa kitambaa safi au vikausha mikono vya umeme.

11. Hali ya hewa baridi na barafu HAYAWEZI kuua nCOV-2019.

• Hakuna sababu ya kuamini kuwa hali ya hewa baridi huweza kuua mashambulio haya.

• Joto la kawaida la binadamu hubaki kati ya 36.50 na 370, hii haijalishi hali ya hewa ya nje ya mwili iko kwa kiasi gani.

• Njia ya kuaminika kuweza kujikinga na vimelea hivi ni kusafisha mikono yako mara kwa mara kwa kileo (alcohol-based handrubs) au maji na sabuni.

12. nCOV-2019 haiwezi kuambukizwa kwa njia ya kung’atwa na mbu.

• Mpaka sasa haijathibitika kuwa mbu huweza kusafirisha nCOV-2019 kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
• COVID-2019 ni kirusi kipya kinachovamia njia ya hewa ambavyo husafirishwa kwa njia ya matone

(droplets) yazalishwayo pindi mgonjwa anpokohoa au kupiga chafya, au mate au makamasi.

• Unashauriwa ufuate kanuni za afya za kunawa mikono pia kuepuka kugusana na mtu anayekohoa au kupiga chafya.

13. Kuoga maji ya moto hakuwezi kukukinga kupata nCOV-2019

• Joto la mwili huwa ni 36.50C na 370C, haijalishi umezungukwa kwa joto la kiasi gani. Kuoga maji ya moto kupita kiasi kutakusababishia kuunguza ngozi yako tuu.

• Kujikinga na maambukizi fuata kanuni za usafi wa mikono. Hii husaidia kuua virusi ambavyo vinaweza kuwa katika mikono yako.

• Epuka maambukizi yanayoweza kukupata kwa kugusagusa pua zako, mdomo na pua.

14. Virusi vya korona haviwezi kuambukizwa kutoka bidhaa zinazozalishwa China au nchi yoyote iliyothibitika kuwa na mashambulio ya nCOV-2019.

• Hata kama kirusi cha korona huweza kukaa kwa masaa au siku kadhaa (hutegemea na aina ya uso wa kitu), hakuna uwezekano kuwa kirusi cha korona kuendelea kuwepo katika uso wa kitu baada ya kuondoshwa, kusafirishwa na kupitia katika hali za hewa tofauti na joto tofauti.

• Kama unadhani uso wa kifaawaweza kuwa na vimelea, basi safisha uso huo kwa kutumia kiua wadudu.

• Baada ya kukigusa kifaa hicho safisha mikono yako.

15. Je, kujipulizia kileo (alcohol) au kemikali za klorini mwili mzima kwaweza kuua Ncov-2019?

• HAPANA! Kujipulizia kileo au kiua wadaudu hakuwezi kuua virusi vilivyo kushambulia.

• Kujipulizia vitu hivyo huweza kuwa hatari kwa nguo au sehemu laini za ngozi (macho, mdomo).

• Kuwa mwangalifu, kileo na kiua wadudu cha klorini huweza kuua wadudu walio katika nyuso za juu, lakini zinatakiwa kutumika kwa maagizo sahihi.

1.

• Kirusi cha korona ni kikubwa, kina ukubwa wa kipenyo cha maikro 400 – 500. Kwa sababu hii, mask yoyote ile huweza kuzuia kirusi hicho kisipenye.

2.

• Kirusi cha korona kikianguka katika uso wa chuma, huweza kuishi kwa masaa 12, hivyo ni lazima kusafisha mikono kwa sabuni na maji safi.

3.

• Ikiwa kirusi cha korona kikianguka katika uso wa pamba au nguo (fabric surface) hubaki hapo hai kwa masaa 9, hivyo yakupasa kusafisha nguo safi au anika juani kwa masaa mawili ili uweze kuviua au kuviondosha.

4.

• Ikiwa kirusi kitakutana na joto kati ya 226 – 270C, hufa, kwani kirusi hicho hakiwezi kuishi katika mazingira ya joto.

• Hivyo kuepuka vyakula vya baridi na ice-cream au kuishi mazingira ya joto husaidia kupunguza kasi ya maambukizi ya korona.

5.

• Kirusi cha korona huishi kwenye mikono kwa takribani dakika 10, hivyo kuwa na kitakasishi cha kileo (alcohol sterilizer) mfukoni husaidia kukinga maambukizi ya korona.

6.

• Kirusi cha korona hakibaki hewani, kirusi hiki hutua chini, hivyo ni vigumu kuambukizwa kwa njia ya hewa.

Soma hii pia > Dawa ya asili inayoongeza kinga ya mwili

ASANTENI

VIRUSI VYA KORONA IMEANDALIWA NA Eusebius Joseph Mikongoti, M.D.Medical Officer The Aga Khan Polyclinic IRINGA

Mjulishe rafiki yako kwenye Twitter naye asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo:

Fahamu kuhusu kirusi cha korona Click To Tweet

Share post hii kwa ajili ya wengine uwapendao

Imesomwa mara 1

Let's block ads! (Why?)

Kama una stress ni vigumu kupata ujauzito

Kama una stress ni vigumu kupata ujauzito

Kama una stress ni vigumu kupata ujauzito

Ni ukweli usiopingika kuwa ndoa nyingi zimepoteza furaha kutokana na watoto kukosekana miongoni mwa wanandoa.

Wanawake na wanaume wamejikuta wakiangukia katika mikono ya matapeli wanaojiita waganga na kufanyiwa mambo mengi ya ajabu, ikiwa ni pamoja na kufanya mapenzi na mizimu au na watu ambao hawakuwatarajia ili tu waweze kupata watoto.

Hakuna ubaya wa kutafuta tiba ya ugonjwa endapo upo, lakini kutafuta tiba ya ugonjwa ambao haupo ni kuchosha mwili na matokeo yake huwa ni mabaya zaidi.

Uchunguzi uliohusisha matatibu kutoka hospitali na vituo vingi vya afya unaonesha kuwa wagumba wengi wanaosaka tiba hospitalini wamebainika kutokuwa na matatizo ya kibaiolojia.

Ninaposema kibaiolojia nina maana kwamba wanandoa wengi wagumba wamekutwa wakiwa na uhai katika viungo vyao vya uzazi.

Katika ulimwengu wa leo idadi ya watu wanaokosa watoto bila kuwa na sababu ya msingi inatajwa kuwa ni kubwa na kila siku wasichana na wavulana wanaingia katika chumba hiki cha huzuni isiyojulikana chanzo chake.

Soma hii pia > Dawa ya asili ya kupata mimba haraka

Kukosa uzazi bila sababu ni tatizo ambalo limekuwa likizisumbua akili za wahitaji watoto wengi na mwisho kuwagotesha katika mawazo ya kurogwa na sababu kubwa ikiwa ni kutojulikana kwa chanzo cha wazi cha kutokuzaa kwao.

Ukweli pekee ambao nimekusudia kuuzungumza leo kuhusiana na wasiokuwa na matatizo ya uzazi kutokuzaa ni ule ambao umeshawekewa misingi na watafiti walioandika taarifa yao katika jarida la Mineriva jinecolojika la nchini Italia kwamba uchovu unaoletwa na mawazo ndiyo unaochangia kwa kiasi kikubwa watu wasipate watoto licha ya kwamba kibaiolojia hawana matatizo.

Tafiti za hivi karibuni zimebaini kuwa, wanawake wengi wenye viungo salama lakini hawazai, wana kiasi kikubwa cha homoni ya Cortisol inayoletwa na uchovu.

Kwa mujibu wa utafiti huo aina hii ya homoni ndiyo inayosimamisha mchakato wa uzalishaji mayai kwa wanawake wakimbia riadha.

Hivyo basi uwiano huu wa kasoro za ukuzaji mayai kati ya wakimbia riadha na wanawake wagumba unaweka usawa baina ya uchovu mkubwa wa mazoezi ya viungo na ule uchovu unaotokana na msongo wa mawazo ya ugumba.

Uchovu wa kihisia huweza kumfanya mwanaume au mwanake asiweze kuzaa kabisa katika maisha yake.

Hii ina maana kuwa watu wanaotingwa zaidi na mawazo ya kukosa fedha, migogoro katika ndoa zao na kujaribu mara kadhaa kupata watoto bila mafanikio wana uwezekano mkubwa wa kutokuzaa hata kama maumbile yao yataonekana kitabibu hayana kasoro.

Imebainika kuwa watu wengi hujisogeza wenyewe katika nguvu ya kukosa mtoto kutokana na ukubwa wa kiu yao ya kupata mtoto, huku wakilazimisha kimawazo mchakato wa kubeba au kubebesha mimba kwa wakati uliopangwa na malengo yao.

Mkazo huu wa mawazo huwakumba hasa wanandoa na wapenzi ambao wanatamaa ya kupita kiasi ya kupata mtoto katika uhusiano wao.

Hawa hujiweka katika uzalishaji mkubwa wa homoni ya Cortisol ambayo huchipuka kwa kasi kutokana na msukumo wa kiu kubwa na ya haraka ya kukumbatia mwana.

Kutokana na ukubwa wa tatizo hili la msongo wa mawazo, imebainika kuwa wagumba wengi wasiokuwa na kasoro katika viungo vya uzazi wanaweza kupona au kupata watoto bila hata kupewa tiba ya miti shamba au vidonge.

Tiba yake kubwa iliyobainishwa ni kupatiwa nasaha zitakazowaondolea mawazo hasi, wasiwasi na kutojiamini.

Ukweli wa tiba hii ya ushauri imethibitishwa hivi karibuni na kituo kimoja nchini Marekani kinachojishughulisha na utafiti wa kuzalisha watoto, ambapo majibu yake yalichapishwa katika majarida na mitandao mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa ya kituo hicho asilimia 75 ya wanawake waliokosa watoto ambao walifika kituoni hapo na kupewa ushauri walifanikiwa kuzaa baada tu ya kuhudhuria kliniki na kupewa ushauri uliowatoa katika msongo wa mawazo.

Nasaha ambazo zimekuwa zikitolewa na wataalamu hao si ngumu, bali ni zile zilizojaa maneno yenye kugeuza fikra hasi zenye kuondoa kiu kali ya kupata watoto kwa utashi na nyakati zilizopangwa na wahusika.

Pia wagumba hufundishwa namna ya kuepuka migogoro ya kimapenzi na kutoumizwa kupita kiasi na kejeli za watu kuhusiana na kutozaa kwao, huku wakijengewa imani kuwa kuzaa ni suala linalowezekana kwao, hivyo kuwafanya watupilie mbali hofu na mawazo kuwa wao ni wagumba.

Lakini pamoja na nchi zilizoendelea kuwa na vituo vya kutolea nasaha kwa waathirika, bado wanasaikolojia wanakiri kwamba mtu mwenyewe anaweza kujiepusha na uchovu unaoletwa na mawazo kwa kurahisisha tatizo lake kutoka kutowezekana na kuwa linalowezekana kutatuliwa.

Akili ya mtu ndiyo inayopima na kuongoza utambubuzi wa ukubwa wa tatizo na si kwamba kuna matatizo makubwa na madogo kama watu wanavyofikiria.

Kwa maana hiyo ili mtu ambaye amejiwekea ukuta wa kutozaa kwa msongo wa mawazo yake kama nilivyosema aweze kuzaa lazima aondoe mawazo ya kwamba yeye ni mtu asiye zaa, kwani hakuna mtu wala vipimo vilivyompa majibu ya kwamba ni mgumba.

Jambo jingine la kufanya ni kupuuza maneno ya kukatisha tamaa toka kwa watu wengine.

Hii ina maana kuwa lawama zozote toka kwa mume au mke au wanafamilia zinazohukumu kosa la mtu kutokuzaa lazima zipuuzwe na zisipewe nafasi ya kutia simanzi moyoni.

Sambamba na hilo kuna suala la wanawake kuzingatia kalenda zao kwa kujichunguza na kubaini muda muafaka wa kukutana kimwili na mwanaume ili kupata matokeo mazuri ya utungishaji mimba.

Kwa mantiki hii kuna wanandoa wengi wameshindwa kupata mtoto kwa kutozingatia siku zenye uwezekano wa kupata mimba ambazo ni siku ya 11 hadi ya 16 tangu siku ya kumaliza hedhi.

Lakini kwa kuwa kuna suala la utumiaji wa dawa za uzazi wa mpango ni budi wahusiaka kusimamisha matumizi yake pindi mtoto anapohitajika ndani ya ndoa.

Hata hivyo kuna umuhimu wa kutumia mitindo ya kuvuta kizazi nyakati za kufanya mapenzi, ili kuzipa msukumo wa haraka mbegu kunasa kwenye mfuko wa uzazi.

Sambamba na hilo wanaume wanatakiwa kuepuka ufanyaji holela wa mapenzi ili kuzifanya mbegu zikomae na wakati wa tendo kuvuta hisia kali ili kuongeza msukumo wa manii kutoka kwenye uume kwenda kwenye uke.

Na jambo la mwisho katika mchakato wa kupata mtoto ni lishe bora miongoni mwa wanandoa.

Lazima miili iwe na nguvu za kutosha kusimamia uzalishaji wa mbegu bora.

Inashauriwa wanaume waepukane na uvaaji wa nguo za ndani za kubana ambazo zinatajwa kuongeza joto kwenye kiwanda cha kuzalisha mbengu na hivyo kuzidhoofisha.

Mjulishe rafiki yako kwenye Twiiter asome post hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo:

Kama una stress ni vigumu kupata ujauzito Click To Tweet

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine

Imesomwa mara 2

Let's block ads! (Why?)

Jumanne, 21 Aprili 2020

Tabia 7 zinazokuchelewesha kupona bawasiri

Tabia 7 zinazokuchelewesha kupona bawasiri

Tabia 7 zinazokuchelewesha kupona bawasiri

1. Kutokunywa maji ya kutosha kila siku

Tafiti zinasema kutokunywa maji ya kutosha kila siku kunaweza kukuletea ugonjwa wa bawasiri.

Kama haunywi maji mengi ya kutosha kila siku ni rahisi sana wewe kupatwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara na mwisho wake ni bawasiri.

Maji ni maji. Juisi, chai, soda au pombe haviwezi kuwa mbadala wa maji na tena vinywaji hivi vinaweza kukausha zaidi hata yale maji machache uliyonayo tayari mwilini.

Haijalishi uwe unaishi sehemu zenye joto au sehemu za baridi jizoeshe tabia ya kupenda kunywa maji mengi ya kutosha kila siku kwa mjibu wa uzito wako.

2. Kukaa tu chini au kwenye kiti masaa mengi

Kwenye dunia hii ya sasa ya kidigitali unaweza kupata vitu vingi ukiwa umekaa tu kwenye computer, simu au runinga (TV).

Wakati maisha yanaweza kuonekana rahisi kuishi kwa namna hii bado aina hii ya maisha inaweza kudhoofisha misuli ya mwili wako na kukuletea Zaidi bawasiri.

Unapokaa tu masaa mengi ni rahisi kuongezeka uzito na unene ni moja ya sababu kuu inayosababisha ugonjwa wa bawasiri.

Mazoezi ya viungo mara nyingi ni dawa ya uhakika kwa magonjwa mengi yatokanayo na tabia.

Kukaa mua mrefu kwenye kiti au chini kunavuruga na kuharibu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kukuletea magonjwa kama bawasiri, vidonda vya tumbo, gesi kujaa tumboni na mengine mengi yanayohusiana na tumbo.

Tazama TV kwa vipindi vile mhimu tu hasa taarifa ya habari, tofauti na hapo usitumie zaidi ya saa moja ukiwa umekaa tu ili kuepuka kuongeza zaidi tatizo la bawasiri.

3. Kula Zaidi vyakula feki

Kama unaishi mjini basi ni ukweli usiopingika kwamba unakula Zaidi vyakula feki (junk foods) na tena vingine vyenye kusisimua (spiced).

Vyakula hivi huongeza msukumo au presha sehemu ya eneo la misuli ya haja kubwa. Jambo hili linaweza kukuletea bawasiri au kuchelewesha uponyaji wa bawasiri uliyonayo tayari.

Vyakula feki ni vyakula vya madukani, vya kwenye makopo au vya kwenye migahawa (fast foods restaurants).

Pendelea kula vyakula vya asili zaidi na vinywaji vya asili zaidi kama unataka kupona haraka ugonjwa huu mbaya wa bawasiri.

4. Kushiriki tendo la ndoa kinyume na maumbile

Hii dunia sijuwi inaelekea wapi.

Kuna tabia mpya imeibuka kwenye kizazi cha sasa watu wanapenda kufanya tendo la ndoa kinyume na maumbile na wengine wanaimba mpaka nyimbo za muziki kabisa kujaribu kuhamasisha na kuwaonyesha wengine kwamba hilo ni jambo la kawaida.

Mapenzi kinyume na maumbile ni sababu nyingine inayokukwamisha usipone bawasiri yako kwa haraka na isijirudie tena.

Kwahiyo kama unataka kupona bawasiri amua kuachana na tabia hii mbaya haraka iwezekanavyo.

5. Kukaa muda mrefu chooni

Kama wewe ni mmoja wa wale ambao ukiwa chooni unaendelea kutumia simu na kuangalia picha facebook basi ujuwe unachelewesha uponyaji wa bawasiri yako bila kufahamu.

Kukaa muda mrefu chooni kunailazimisha damu kujaa na kusukumwa kwenye mishipa ya tundu la haja kubwa kitendo kinachoweza kuongeza uwezekano wa wewe kupatwa zaidi na bawasiri.

Ukienda chooni usiende na simu na usikae huko zaidi ya muda unaotakiwa kuwa huko na ukimaliza haja yako basi mara moja utoke.

6. Unapochelewa kwenda chooni

Kuna wakati inaweza kukutokea upo mbali kidogo na nyumbani na ukapatwa na hitaji la kutaka kupata choo lakini kwa sababu upo mbali na nyumbani unaweza kuamua kujizuia usiingie choo cha kulipia mpaka utakaporudi nyumbani.

Au wakati mwingine tu hata kama upo nyumbani unaweza kuwa upo bize na kazi au jambo fulani kiasi kwamba unapatwa na hitaji la kwenda chooni na bado hukimbii haraka kwenda chooni.

Kama utaendelea na tabia hii mbaya kwa kipindi kirefu inaweza kukuletea au kukuongezea zaidi uvimbe wa bawasiri na kama tabia hii haitadhibitiwa inaweza kukuletea dalili zenye maumivu za bawasiri.

7. Kutokula vyakula vya kutosha vyenye nyuzinyuzi kila siku

Vyakula vyenye nyuzi nyuzi ni mhimu na vya lazima hasa kwa mtu unayesumbuliwa na bawasiri.

Vyakula vyenye nyuzi nyuzi ni mhimu kwa ajili ya mwenendo wa kawaida wa tumbo.

Ukiona unapatwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara ni ishara hauli vyakula vyenye nyuz nyuzi vya kutosha kila siku.

Unapopata choo kigumu kinaweza kukuletea maumivu sehemu ya haja kubwa na kukuletea dalili za bawasiri.

Kama unahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kutibu bawasiri niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Kama unapenda kujifunza mengi zaidi kuhusu ugonjwa wa bawasiri bonyeza HAPA.

Mjulishe rafiki yako kwenye Twitter asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo:

Tabia 7 zinazokuchelewesha kupona bawasiri Click To Tweet

SHARE post hii kwa ajili ya wengine.

Imesomwa mara 9

Let's block ads! (Why?)

Jumanne, 7 Aprili 2020

Namna mfumo wa kinga unavyopambana na virusi vya Corona

Virusi vya corona

CoronaVirus: Wanasayansi nchini Australia wanaonyesha namna mfumo wa kinga unavyopambana na virusi.

Wanasayansi nchini Australia wamesema kuwa wamegundua namna gani mfumo wa kinga mwilini unavyoweza kupambana na virusi vya Covid-19.

Utafiti wao, uliochapishwa kwenye jarida la Nature siku ya Jumanne, unaonesha kuwa watu wanapona maambukizi ya virusi, kama ambavyo wanavyopona mafua.

Duniani kote, mamlaka zimethibitisha maambukizi kwa zaidi ya watu 160,000 ya virusi vya corona na vifo karibu 6,500.

”Ugunduzi huu ni muhimu kwa sababu ni mara ya kwanza ambapo tunafahamishwa namna ambavyo kinga zetu zinavyopambana na virusi vya corona,” amesema mwandishi mwenza Profesa Katherine Kedzierska.

Taasisi ya utafiti ya magonjwa ya maambukizi na kinga ya Peter Doherty wa Melbourne imesifiwa na wataalamu wengine, mmoja akieleza kuwa ni ”mafanikio mapya”.

Soma hii pia > Dawa ya asili inayoongeza kinga ya mwili

Kilichobainika:

Watu wengi wamepona virusi vya Covid-19, ikimaanisha kuwa tayari ilijulikana kuwa mfumo wa kinga unaweza kupambana na virusi.

Lakini kwa mara ya kwanza, utafiti ulibaini aina nne za seli za kinga ambazo zinaweza kupambana na Covid-19.

Zilichunguzwa kwa kumfuatilia mgonjwa ambaye alikuwa na maambukizi ya virusi lakini ambaye hakuwa na matatizo ya kiafya hapo awali.

Mwanamke mmoja mwenye miaka 47 kutoka mjini Wuhan, China aliyewasili hospitali nchini Australia alipona ndani ya siku 14.

Profesa Kedzierska ameiambia BBC kuwa timu yake imechunguza ”uwezo wa kinga kupambana na virusi” kwa mgonjwa huyu.

Siku tatu kabla mwanamke mmoja alianza kujisikia vizuri, seli zilioonekana kwenye mfumo wa damu. Katika wagonjwa wa maradhi ya mfumo wa upumuaji, seli hizi pia zinaonekana kabla ya kupona, Profesa Kedzierska alieleza.

‘Tulifurahia matokeo yetu na ukweli kuwa tunaweza kuona seli za kinga kwa mtu aliyegundulika, kabla ya afya yake kuimarika,” aliiambia BBC.

Wanasayansi walifanya uchunguzi wao kwa wiki nne ili kutathimini hilo, aliongeza.

Hatua hii imesaidia nini?

Kubaini wakati seli za kinga zinaingia zinaweza kusaidia “kutabiri mwenendo wa virusi”, alisema Prof Bruce Thompson, Mkuu wa kitivo cha sayansi ya afya katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Swinburne.

Waziri wa Afya wa Australia Greg Hunt alisema kupatikana kwa ukweli huu pia kunaweza kusaidia “kufuatilia kwa haraka” chanjo na tiba inayowezekana kwa wagonjwa walioambukizwa.

Prof Kedzierska alisema hatua inayofuata kwa wanasayansi ni kutazama kwa nini kinga ni dhaifu kwa wagonjwa walio katika hali mbaya.

“Ni muhimu sana sasa kuelewa ni nini kinachopungua au tofauti kwa wagonjwa ambao wamekufa au ambao wana ugonjwa ulio katika hali mbaya – kwa hivyo tunaweza kuelewa jinsi ya kuwalinda,” alisema.

Mnamo Januari, taasisi hiyo ikawa ya kwanza ulimwenguni kuunda tena virusi nje ya Uchina.

Kituo hicho kimepokea fedha zaidi kutoka kwa serikali ya Australia na pia michango kutoka kwa wafanyabiashara na bilionea wa Kichina Jack Ma.

Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza ujumbe ufuatao:

Namna mfumo wa kinga unavyopambana na virusi vya Corona Click To Tweet

Habari hii ilichapishwa na BBC Tarehe 17 Machi 2020

SOURCE

Imesomwa mara 4

Let's block ads! (Why?)

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...