آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾
Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake na Waumini (pia). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rusuli Wake. (Nao husema): “Hatutofautishi baina ya yeyote kati ya Rusuli Wake.” Na wakasema: “Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu na Kwako nimahali pa kuishia.”
لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٨٦﴾
Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata (thawabu) iliyoyachuma, na ni dhidi yake (kwa maovu) iliyojichumia. “Rabb wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Rabb wetu, Usitubebeshe mzigo kama Ulivyoubebesha juu ya wale waliokuwa kabla yetu. Rabb wetu, Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe ni Mola Mlinzi wetu, basi Tunusuru dhidi ya watu makafiri. Suwratul-Baqarah Ayah ya 285 na 286
Mafunzo ya Ayah hizi
1-Kutokuhesabiwa katika kusahau.
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema:((Ummah wangu umenyanyuliwa makosa na kusahau na wanayo shurutishwa)) [Ibn Maajah, Ibn Hibbaan, Ad-Daraqutwniy, At-Twabaraniy na Al-Haakim, Irwaa Al-Ghaliyl (1027)]
2-Atakayezisoma zitamtosheleza:
عن أَبِي مَسْعُودٍ الأَنْصَارِيِّ، قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((الآيَتَانِ مِنْ آخِرِ سُورَةِ الْبَقَرَةِ مَنْ قَرَأَ بِهِمَا فِي لَيْلَةٍ كَفَتَاهُ))
Abuu Mas‘uwd Al-Answaariyy ‘Uqbah bin ‘Amr bin Tha’labah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayesoma usiku Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah zitamtosheleza.” Yaani: zinamtosheleza kumkinga na kila baya na lenye kumdhuru. [Al-Bukhaariy na Muslim]
3-Hakuna Nabiy aliyepewa isipokuwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ بَيْنَمَا جِبْرِيلُ قَاعِدٌ عِنْدَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم سَمِعَ نَقِيضًا مِنْ فَوْقِهِ فَرَفَعَ رَأْسَهُ فَقَالَ: ((هَذَا بَابٌ مِنَ السَّمَاءِ فُتِحَ الْيَوْمَ لَمْ يُفْتَحْ قَطُّ إِلاَّ الْيَوْمَ، فَنَزَلَ مِنْهُ مَلَكٌ فَقَالَ: هَذَا مَلَكٌ نَزَلَ إِلَى الأَرْضِ لَمْ يَنْزِلْ قَطُّ إِلاَّ الْيَوْمَ، فَسَلَّمَ وَقَالَ أَبْشِرْ بِنُورَيْنِ أُوتِيتَهُمَا لَمْ يُؤْتَهُمَا نَبِيٌّ قَبْلَكَ، فَاتِحَةُ الْكِتَابِ وَخَوَاتِيمُ سُورَةِ الْبَقَرَةِ لَنْ تَقْرَأَ بِحَرْفٍ مِنْهُمَا إِلاَّ أُعْطِيتَهُ)) .
Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amehadithia kwamba: Jibriyl ('Alayhis-Salaam) alipokuwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisikia sauti kutoka juu. Jibriyl ('Alayhis-Salaam) akatazama juu akasema: “Huu mlango wa mbinguni umefunguliwa na haujapatapo kufunguliwa isipokuwa leo.” Malaika akateremka humo akasema: “Huyu Malaika ameteremka ardhini, hajapatapo kuteremka kamwe isipokuwa leo.” Akasalimia kisha akasema: “Pokea bishara ya nuru mbili ulizopewa ambazo hakuna Nabiy aliyepewa kabla yako; Ufunguo wa Kitabu (Al-Faatihah), na Aayah (mbili) za mwisho wa Suwratul-Baqarah. Hutosoma herufi humo ila utapewa barakah zake ziliomo.” [Muslim]
4-Amepewa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa mbingu ya saba.
Imaam Muslim amenukuu katika Swahiyh yake kuwa Aayah hizi mbili alipewa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofika kikomo mbingu ya saba katika Safari ya Al-Israa Wal-Mi’raajpamoja na kupewa Swalaah tano na msamaha kwa mtu asiyemshirkisha Allaah na yeyote au chochote.
NA ALLAAH ANAJUA ZAIDI
https://ift.tt/2uqtLzy i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni