Translate

Jumapili, 3 Februari 2019

Hukmu ya Unajimu (Kutabiri Kwa Nyota)

SWALI

Assalam alakum 

Nini maana ya unajimu, na upi hukumu yake katika uislam? Jazakallahul khayrun


JIBU

Wa Aleykum Sallaam WarahmatulLaah Wabarakatuh


 Maana ya unajimu ni elimu ya nyota. Unajimu ni elimu ambayo ina manufaa yake  katika Uislamu kwa ajili  elimu hiyo Waislamu waliweza kusafiri na majahazi na meli kuelekea sehemu nyingi baharini na kwa ajili hiyo Waislamu waliweza kueneza Uislamu na kufanya biashara bila ya matatizo yoyote.


Lakini wapo baadhi ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu wanatumia nyota kutabiri mambo yatakayokufika au yatakayotokea. Kuna wanaotabiri kwa njia ya unajimu (kutazamia nyota) kuhusiana na mwezi aliozaliwa mtu inayojulikana kama 'horoscope'.  Unajimu huu hutiwa magazetini na watu husoma kila mara kutabiri bahati zao au shari zitakazowasibu katika siku fulani. 

Wanadai kuwa sayari kama gemini, taurus, aries n.k. zinahusiana na mwezi wa mtu aliozaliwa na hivyo basi waliozaliwa katika sayari hizo siku hiyo kwao huwaathiri nafsi zao na kadhaa wa kadhaa.

Haramisho la kutazamia kwa unajimu ni katika Hadiyth:

Amehadithia ‘Abdullaah bin ‘Abaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayejichumia tawi katika ujuzi wa unajimu, atakuwa amejichumia tawi katika sihri, na itaendelea kuzidi na kuzidi.” [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]

Kusoma elimu hiyo na kuamini ni ushirikina na hivyo dhambi kubwa inayomtoa mtu nje ya Uislamu kwa sababu Mtume Muhammad(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)    ametuhimiza sana tusiwe ni wenye kwenda kwa wapiga bao, ramli au kutizamia kwa kutumia nyota au mkono kwani mwenye kufanya hivyo atakuwa amekufuru kwa aliyokuja nayo Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayemwendea kahini au mpigaji ramli akamuamini asemayo, basi atakuwa ameshakufuru yale aliyoteremshiwa nayo Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).” [Ahmad, na Aswhaabus-Sunan wanne, na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb wat-Tarhiyb (3047)

Na pia:

((Atakayekwenda kwa mtabiri akamuuliza kitu haitokubaliwa Swalaah yake siku arubaini)) [Muslim]


Na Allaah Anajua zaidi



from fisabilillaah.com http://bit.ly/2S3AcHf
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...