Translate

Jumapili, 3 Februari 2019

Fadhila za Maiti kuswaliwa na Idadi ya Watu wengi

SWALI

Je, inapokuwa idadi ni kubwa ya wanaomswalia maiti kuna fadhila?


JIBU

Imethibiti katika Hadyth ya Ibn ‘Abbaas kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba amesema:

((مَا مِنْ رَجُلٍ مُسْلِمٍ يَمُوتُ، فَيَقُومُ عَلَى جَنَازَتِهِ أَرْبَعُونَ رَجُلًا، لَا يُشْرِكُونَ بِاَللَّهِ شَيْئًا، إِلَّا شَفَّعَهُمْ اَللَّهُ فِيهِ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Muislamu yeyote anapofariki na wakasimama watu arubaini wasio mshirikisha Allaah na chochote wakamswalia, Allaah Atawakubali wawe waombezi wake.” [Muslim]

Na kwa hivyo, ‘Ulamaa wamependelea kukimbilia Msikiti unaoswaliwa na watu wengi kwa ajili ya kumswalia maiti. Na kila inapokuwa idadi (ya watu) ni kubwa, basi huwa karibu zaidi na khayr na kukithiri du’aa.”


[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy lil-Imaam Ibn Baaz]


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2S6btSI
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...