Translate

Jumanne, 1 Januari 2019

Nguzo za Swalah

                                                       NGUZO  ZA  SWALAH



Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh

Nguzo ni zile ambazo ukiswali na ukaziacha kwa makusudi Swalah yako inabatilika, na ikiwa umeacha kwa kusahau, Swalah yako pia itakuwa haikukamilika hadi urejee kitendo chenyewe au urejee rakaa na kisha mwishoni utoe Sajdatus-Sahw. 

Lakini ukiwa umesahau nguzo ya Takbiyratul-Ihraam, basi itakubidi uiswali Swalah upya tokea mwanzo.

Nguzo za Swalah ni 14.

Nguzo hizo 14 ni hizi zifuatazo:

1. Kusimama katika Swalah za Fardh kwa yule mwenye uwezo. (Wanachuoni wengine wamesema nguzo ya kwanza ni Niyah kabla ya Kusimama). Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema: "Na simameni kwa ajili ya Allaah hali ya kuwa watiifu" (Al-Baqarah: 238). Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swali hali ya kuwa umesimama, usipoweza, basi kwa kukaa na usipoweza basi kwa kulala ubavu" (Al-Bukhaariy na Abu Daawuud).


2. Takbiyrah ya kuhirimia (Takbiyratul-Ihraam) kwa tamko laAllaahu Akbar kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ufunguo wa Swalah ni kujitwaharisha, na kuifunga ni Takbiyrah, na kuifungua ni kutoa Salaam" (Abu Daawuud na At-Tirmidhiy).


3. Kusoma Suratul-Faatihah katika kila rakaa. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: "Hapana Swalah kwa ambaye hakusoma Suratul Faatihah" (Al-Bukhaariy).


4. Kurukuu.


5. Utulivu (Twumaaniynah) katika Rukuu.


6. I'itidaal (hapa inaingia na kunyanyuka kutoka katika Rukuu hadi anaponyooka mtu).


7. Utulivu katika I'Itidaal.


8. Kusujudu.


9. Utulivu katika kusujudu. Kutulia wakati wa kurukuu, kusujudu, kusimama, kukaa baina ya Sijdah mbili kwa msemo wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Kisha rukuu mpaka utulizane hali ya kurukuu, kisha nyanyuka mpaka ulingane sawa hali ya kusimama, kisha sujudu mpaka utulizane na hali umesujudu, kisha nyanyuka mpaka utulizane hali ya kuwa umekaa" (Al-Bukhaariy).


10. Kikao baina ya Sijdah mbili.


11. Utulivu katika kikao baina ya Sijdah mbili.


12. Tashahhud ya mwisho.


13. Kikao katika Tashahhud ya mwisho.


14. Salaam (Kutoa Salaam) ya kwanza.
Utahakikisha unafuatanisha yote hayo kama utaratibu ulivyopangika.


Na  Allaah  anajua  zaidi


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2TrNGZJ
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...