Translate

Jumanne, 1 Januari 2019

Mmabo ya Sunnah katika Swalah

MAMBO  YA  SUNNAH  KATIKA  SWALAH



Sunnah za Swalah

Hizi ni kauli na vitendo zinazopendeza kuletwa katika Swalah. Mwenye kufanya hayo hupata thawabu wala Swalah haibatiliki kwa kuachwa hata kwa kusudi. Wala sijdah ya kusahau hailetwi. Hapa tuna vigawanyo viwili vya Sunnah katika Swalah; Sunnah za kauli na Sunnah za vitendo.  


Sunnah Za Kauli

1. Kisomo baada ya al-Faatihah.


2. Dhikr nyinginezo katika Rukuu.


3. Dhikr baada ya kusimama kutoka katika Rukuu na baada ya kusema ‘Rabbana Lakal Hamd’.


4. Dhikr nyinginezo katika Sujuud.


5. Du’aa baina ya Sijdah mbili.


6. Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Tashahhud ya kwanza na ya pili.


7. Du’aa baada ya Tashahhud ya kwanza na ya pili.


8. Salaam ya pili.


9. Dhikr na du’aa mbalimbali baada ya Swalah.


Sunnah Za Vitendo


1. Kuweka Sutrah (kizuizi mbele ya sehemu unayoswalia) katika Swalah.


2. Kunyanyua mikono wakati waTakbiyratul Ihraam, na wakati wa kurukuu na na wakayi wa kunyanyuka kwayo na wakati wa kuinuka kutoka katika Tashahhud ya kwanza. Na kadhalika wakati unapoinama na kuinuka.


3. Kuweka mkono wa kuume juu ya mkono wa kushoto juu ya kifua unaposimama kuswali.


4. Kutazama mahali pa kusujudu.


5. Kulingana sawa mgongo unaporukuu na kutonyanyua kichwa au kukiinamisha sana, na kuweka viganja kwenye magoti mawili na huku umeviachanisha vidole vya mikono na kuachanisha viwiko visiguse mbavu au tumbo lako.


6. Kuteremka katika Sijdah kwa mikono miwili kabla ya magoti (Wengine huona kushuka kwa magoti kabla ya mikono).


7. Kuimakinisha paji la uso, pua na mikono (viganja viwili) kwenye ardhi pamoja na kupanua mikono isiguse mbavu zako; kuwe na uwazi wa kuweza kupita kinyama kidogo. Na viganja vyako viwe usawa wa mabega au masikio wakati uko katika kusujudu na viwiko vikiwa vimenyanyuliwa juu na vidole vya mikono vikiwa vinaelekea Qiblah. Matumbo ya vidole vya miguu yakiwa ardhini visigino vikielekea juu na hali vidole vya miguu vikielekea Qiblah.


8. Kulilalisha guu la kushoto na kulisimamisha la kulia wakati wa kikao baina Sijdah mbili.


9. Kurefusha kikao baina ya Sijdah mbili.


10. Kikao cha mapumziko baada ya kukamilisha rakaa ya kwanza na ya tatu.


11. Kutegemea ardhi kwa mikono wakati mtu anaponyanyuka kutoka kusujudu na kwenda kwenye rakaa nyingine.


12. Kukaa kikao cha Iftiraash(Kusimamisha mguu wa kulia na kukalia mguu wa kushoto) katika Tashahhud ya mwanzo. Na kukaa kikao cha Tawarruk (kusimamisha mguu wa kulia na kuipitisha mguu wa kushoto chini ya muundi wa mguu wa kulia na huku kikalio chako kimekaa juu ya ardhi).


13. Kuashiria kwa kidole cha shahada katika Tashahhud kuanzia mwanzo hadi mwisho bila kukishusha na huku unasoma na ukikitazama.
(Abu Maalik Kamaal Saalim, Swahiyh Fiqhus Sunnah, Mj. 1).


Ingawa kuna ikhtiliaaf baina ya Wanachuoni katika mas-alah hayo, tunapenda kuwakumbushia Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliyesema: "Swalini kama mlivyoniona nikiswali" (Al-Bukhaariy).

Kwa hivyo, ni juu yetu kufanya juhudi kufuata yote aliyofanya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ili Swalah zetu zitimize daraja zote za ujra na ili tuchume thawabu nyingi zaidi.  

Na  Allaah  anajua  zaidi


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2ApBuBj
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...