Translate

Jumanne, 1 Januari 2019

Mambo ya Waajib katika Swalah

                           MAMBO  YA  WAJIIBU (LAZIMA)  KATIKA  SWALAH


 Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh

Ni lile ambalo ni wajibu kulifanya au kusema, inaondoka kwa kusahau na kulazimisha mwenye kuswali kusujudu sijdah mbili za kusahau. Yeyote mwenye kuacha kwa kusudi Swalah yake inabatilika ikiwa anajua uwajibu wake.

Istilahi hii inatumika kwa madhehebu ya Hanafi na Hanbali ila ma-Hanafi hawaoni kuwa mwenye kuacha wajibu kwa kusudi inabatilisha Swalah yake bali yeye amefanya madhambi anayostahiki adhabu. Ama ma-Maaliki na ma-Shaafi'y hawana kigawanyo hichi cha Waajib kwao ila wao wana nguzo na Sunnah kwa ujumla wake.

Ama hapa tutaweka yale yaliyotajwa ambayo yanaelekea kuwa na nguvu zaidi.

Kwanza kabla hatujataja mambo yenyewe, tunapaswa kujua kuwa mambo ya Waajib ni yale ambayo vilevile atakapoacha mtu kwa makusudi hubatilika Swalah yake, na atakapoacha kwa kusahau inamtosheleza yeye kusujudu Sijda mbili za kusahau 'Sujuudus-Sahw'.

Ama mambo ya Waajib ambayo yametajwa katika kitabu cha'Swahiyhu Fiqhus-Sunnah' kwa dalili mbalimbali za Aayah na Hadiyth ni 9 kama yafuatayo:


1. Du'aa ya ufunguzi wa Swalah 'Du'aa al-Istiftaah'.


2. Kusema 'A'udhu biLlaahi Minash-Shaytwaan ar-Rajiym' kabla ya kusoma 'BismiLlaah ar-Ramaanir Rahiym' na 'Suratul-Faatihah'.


3. Kusema 'Aamiyn' baada ya Suratul-Faatihah.


3. Takbiyrah za kuhama baina ya kitendo na kitendo.


4. Kusema 'Sami'a Allaahu liman hamidah'


5. Kusema 'Rabbana Lakal Hamdu' katika I'itidaal.


6. Kusema 'Subhaana Rabbiyal 'Adhwiym' wakati wa kurukuu na kusema 'Subhaana Rabbiyal A'ala' wakati wa kusujudu.


7. Tashahhud ya kwanza.


8. Kikao cha Tashahhud ya kwanza.


Wanachuoni wengine wametaja mambo ya Waajib ni 8 kama yafuatayo:


1. Takbiyrah nyingine zote isiyo ile ya Ihraam.


2. Kusema 'Sami'a Allaahu liman hamidah' kwa Imaam na mwenye kuswali peke.


3. Kusema 'Rabbana Lakal Hamdu'.


4. Kusema 'Subhaana Rabbiyal 'Adhwiym’ mara moja kwenye kurukuu.


5. Kusema 'Subhaana Rabbiyal A'ala' kwenye kusujudu.


6. Kusema 'Rabbi-Ghfir liy' kwenye kikao baina ta Sijda mbili.


7. Tashahhud ya mwanzo.


8. Kikao katika Tashahhud ya mwanzo.


Hizi ndizo maarufu zaidi kwa Wanachuoni wengine.

Na  Allaah  anajua  zaidi


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2SwAQcz
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...