Swali: Mtu akianza kupangusa kwenye soksi hali ya kuwa ni mkazi kisha akasafiri atatimiza kupangusa akiwa ni msafiri au mkazi?
Jibu: Msafiri. Haya ndio maoni yenye nguvu.
Swali: Mtu akianza kupangusa kwenye soksi hali ya kuwa ni msafiri kisha akarudi katika mji wake atatimiza kupangusa akiwa ni mkazi au msafiri?
Jibu: Atatimiza kupangusa hali ya kuwa ni mkazi. Muda ukiisha ni lazima kwake kuosha miguu yake.
Swali: Inajuzu kwa mtu ambaye anapangusa juu ya soksi kumwongoza katika swalah asiyepangusa?
Jibu: Ndio, inajuzu. Hili ni kama inavyojuzu kwa imamu ambaye amefanya Tayammum kumwongoza ambaye anaswali kwa wudhuu´.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2R5nh6U
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni