Translate

Jumatano, 2 Januari 2019

Du'aa ya Qunuut ya Witr


Du'aa ya Qunuut ya Witr

اللّهُـمَّ اهْـدِنـي فـيمَنْ هَـدَيْـت، وَعـافِنـي فـيمَنْ عافَـيْت، وَتَوَلَّـني فـيمَنْ تَوَلَّـيْت ، وَبارِكْ لـي فـيما أَعْطَـيْت، وَقِـني شَرَّ ما قَضَـيْت،فَإِنَّـكَ تَقْـضي وَلا يُقْـضى عَلَـيْك ، إِنَّـهُ لا يَـذِلُّ مَنْ والَـيْت، وَلا يَعِـزُّ مَن عـادَيْت ]، تَبـارَكْـتَ رَبَّـنا وَتَعـالَـيْت.
Allaahummah-diniy fiyman Hadayta , Wa 'Aafiniy fiyman 'Aafayta, Watawallaniy fiyman Tawallayta, Wabaarik liy fiymaa A'atwayta, Waqiniy Sharra Maa Qadhwayta, Fainnaka Taqdhwiy Walaa Yuq-dhwa 'Alayka, Innahu Laa yadhillu  mawwaalayta, Walaa Ya'izzu man 'Aadayta, Tabaarakta Rabbana Wa Ta'aalayta.

“Ee Allaah  Niongoze pamoja na Uliowaongoza, na Unipe afya njema pamoja na Uliowapa afaya njema, na Nifanye kuwa ni mpenzi Wako pamoja na Uliowafanya  wapenzi na Nibariki katika Ulichonipa na Nikinge na shari ya Ulilolihukumu kwani Wewe Unahukumu wala Huhukumiwi.  Hakika hadhaliliki Uliyemfanya mpenzi (wala hatukuki Uliyemfanya adui) Umetakasika Ee Mola wetu na Umetukuka
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِرِضـاكَ مِنْ  سَخَطِـك، وَبِمُعـافاتِـكَ مِنْ عُقوبَـتِك، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْـك، لا أُحْصـي ثَنـاءً عَلَـيْك، أَنْـتَ كَمـا أَثْنَـيْتَ عَلـى نَفْسـِك
Allaahumma Inniy A'udhu Biridhwaaka Min Sakhatwika, Wabimu'aafaatika min 'UquubatikaWa A'udhu Bika Minka, Laa Uhswiy Thanaan 'Alayka, Anta Kamaa Ath-nayta 'Alaa Nafsika.

“Ee Allaah  hakika mimi najilinda kwa radhi Zako kutokana na hasira Zako na kwa msamaha Wako kutokana na adhabu Yako, na najilinda  Kwako kutokana na Wewe, mimi siwezi kuzidhibiti sifa Zako, Wewe ni kama Ulivyojisifu Mwenyewe”
اللّهُـمَّ إِيّـاكَ نعْـبُدْ، وَلَـكَ نُصَلّـي وَنَسْـجُد، وَإِلَـيْكَ نَسْـعى وَنَحْـفِد،نَـرْجو رَحْمَـتَك، وَنَخْشـى عَـذابَك، إِنَّ عَـذابَكَ بالكـافرين ملْحَـق.اللّهُـمَّ إِنّا نَسْتَعـينُكَ وَنَسْتَـغْفِرُك، وَنُثْـنـي عَلَـيْك الخَـيْرَ، وَلا نَكْـفُرُك، وَنُـؤْمِنُ بِك، وَنَخْـضَعُ لَكَ وَنَخْـلَعُ مَنْ يَكْـفرُك
Allaahumma Iyyaaka Na'abud WalakaNuswalliy WanasjuduWa-Ilayka Nas'aa Wanahfidu, Narju Rahmataka, Wanakhsha 'Adhaabaka, Inna 'Adhaabaka Bil-Kaafiriyna Mulhaqq.  Allaahumma  Innaa Nasta'iynuka Wanastaghfiruka, Wanuthniy 'Alaykal-khayra, Walaa Nakfuruka, Wanu-uminu Bika, Wanakhdhwa'u Laka, Wanakhla'u Man Yakfuruka.

“Ee Allaah, Wewe tu Ndiye tunaekuabudu, na Kwako tunaswali na tunasujudu, na Kwako tunakimbilia na tunakutumikia, tunataraji rehema Yako na tunaogopa adhabu Yako, kwani adhabu Yako hakuna shaka kuwa makafiri itawifikia.  Ee Allaah  hakika sisi tunakutaka msaada na tunakutaka msamaha na tunakusifu kwa kheri na wala hatukukufurishi na tunakuamini Wewe, na tunakunyenyekea na tunamuepuka anaekukufuru”


Du'aa baada ya salamu katika swala ya Witri (Mwisho kabisa baada ya kumaliza Swalah yote na si kila baada ya Rakaa mbili au nne)

سُـبْحانَ المَلِكِ القُدّوس
Subhaanal-Malikul-Qudduus

“Ametakasika Allaah  Mfalme, Mtakatifu"
(mara tatu)
(Kisha unavuta kwa sauti )
 ربِّ الملائكةِ والرّوح
Rabbul-Malaaikati War-Ruuh

“Ee Mola wa Malaika na wa Jibriyl”



Na  Allaah  anajua  zaidi


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2RrCBKC
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...