Translate

Jumatano, 2 Januari 2019

Dua kabla na baada ya kula na kumuombea aliyekaribshwa

Du'aa kabla ya kula

 Anapotaka kula mmoja wenu chakula basi aseme:  
بِسْمِ الله
Bismillahi
“Kwa jina la Allaah"

Na akisahau mwanzo wake basi aseme:
بِسْمِ اللهِ في أَوَّلِهِ وَآخِـرِهِ
Bismillahi Fiy Awwalihi Wa Aakihirihi

“Kwa jina la Allaah  mwanzo Wake na mwisho Wake”

Yeyote ambae Allaah Amemruzuku chakula aseme:
اللّهُـمَّ بارِكْ لَنا فيهِ وَأَطْـعِمْنا خَـيْراً مِنْـهُ
Allaahumma Baarik Lana Fiyhi Wa Atw'imna Khayran minhu.

“Ee Allaah Tubariki katika chakula hichi na Tulishe bora kuliko hichi "
Na yeyote ambae Amemruzuku maziwa basi aseme:
اللّهُـمَّ بارِكْ لَنا فيهِ وَزِدْنا مِنْهُ
Allaahumma Baarik Lana Fiyhi Wazidna  Minhu
 “Ee Allaah Tubarikie kinywaji hichi na Utuzidishie”

Du'aa ya baada ya kula
الْحَمْـدُ للهِ الَّذي أَطْعَمَنـي هـذا وَرَزَقَنـيهِ مِنْ غَـيْرِ حَوْلٍ مِنِّي وَلاقُوَّةٍ
Alhamduli-Llahi-lladhiy Atw'amaniy Haadhaa Warazaqaniyhi Min Ghayri Hawlim-Minniy Walaa Quwwatin.

“Sifa njema ni za Allaah  Ambaye Amenilisha mimi chakula hichi na Akaniruzuku pasina uwezo wangu wala nguvu zangu”

الْحَمْـدُ للهِ حَمْـداً كَثـيراً طَيِّـباً مُبـارَكاً فيه، ]غَيْرَ مَكْفِيٍّ[ وَلامُوَدَّعٍ وَلا مُسْتَغْـنىً عَنْـهُ رَبُّـنا
AlhamduliLLahi Hamdan Kathiyran Twayyiban Mubaarakan Fiyhi, Ghayra Mukfiyyi  Walaa Muwadda'iw- Walaa Mustaghna 'Anhu Rabbunaa.

“Sifa njema ni za Allaah, sifa nyingi nzuri, zenye  baraka ndani yake, zisizo toshelezwa wala kuagwa, wala kutoshwa nazo mtu.  Ee Mola wetu”


Du'aa ya mgeni kumuombea aliyemkaribisha chakula
اللّهُـمَّ بارِكْ لَهُمْ فيما رَزَقْـتَهُم، وَاغْفِـرْ لَهُـمْ وَارْحَمْهُمْ
Allahumma Baarik Lahum Fiyma Razaq-tahum Waghfir-lahum War-ham-hum.

 “Ee Allaah Wabariki katika Ulichowaruzuku na Uwasemehe na Uwarehemu


Du'aa ya kumuombea aliyekupa kinywaji au anayetaka kukupa
اللّهُـمَّ أَطْعِمْ مَن أَطْعَمَني، وَاسْقِ مَن سَقانِي
Allaahumma Atw'im Man Atw'amaniy Wasqi Man Saqaaniy.
“Ee Allaah Mlishe aliyenilisha na Mnyweshe aliyeninywesha"



Du'aa ya kumuombea uliyefuturu/futari kwake

أَفْطَـرَ عِنْدَكُم الصّـائِمونَ وَأَكَلَ طَعامَـكُمُ الأبْـرار، وَصَلَّـتْ عَلَـيْكُمُالملائِكَـة

Aftwara 'Indakumu-Swaaimuna WaAkala Twa'aamakumul-Abraar, Waswallat 'Alyakumul-Malaaikah.

 “Wafuturu kwenu waliofunga na wale chakula chenu watu wema, na wawaombee rehema malaika”



Du'aa ya aliyealikwa chakula lakini akawa amefunga

Akialikwa mmoja wenu aitike mwito, akiwa amefunga basi awaombee Du'aa na kamahakufunga basi ale

Anachosema aliyetukanwa hali ya kuwa amefunga
إنِّي صَائِمٌ ,  إنِّي صَائِمٌ
Inniy Swaaimun Inniy Swaaimun

“Hakika mimi nimefunga, hakika mimi nimefunga"


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2EZYWZb
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...