Wakati wa Kuingia Msikitini
Mwenye kuingia Msikitini anapaswa kuzingatia taratibu (adabu) zifuatazo:
1. Kutanguliza Mguu wa Kulia Kwanza
Swahaba maarufu wa Mtume, Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:
“Ni katika Sunnah, kuwa mtu anapoingia Msikitini basi atangulize mguu wake wa kulia, na (anapotoka), atoke kwa kutanguliza mguu wake wa kushoto.” [Mustadrak Al-Haakim].
Na imenukuliwa pia, kuwa ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa na mtazamo huo huo. [Swahiyh Al-Bukhaariy].
2. Du’aa (Ya Kusoma) Unapoingia Msikitini
Hii inapatikana katika Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Mmoja wenu anapoingia Msikitini, basi aseme: Allaahumma iftah liy ab-waaba rahmatik (Ee Mola! Nifungulie milango ya Rahmah Zako).” [Swahiyh Muslim]
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema pia:
“Atakapoingia mmoja wenu Msikitini, aniswalie mimi, na kisha aseme:Allaahumma iftah liy abwaaba rahmatik (Ee Allaah, nifungulie mimi milango ya Rahmah Zako).” [Sunan Abi Daawuwd].
3. Kuswali Rakaa 2 Kabla Ya Kukaa (Tahiyyatul Masjid)
Uthibitisho wa haya nimaneno ya Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Mmoja wenu atakapoingia Msikitini, aswali rakaa mbili kabla ya kukaa.”[Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim].
4. Kuswali Nyuma ya Sutrah (Kizuizi)
Sutra ni kizuizi kinachomsaidia mtu anayeswali kutomruhusu mtu mwingine kupita mbele yake. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Mmoja wenu anaposwali, basi asimame nyuma ya sutrah na aswali karibu na hiyo sutrah. Hii ni kwa ajili ya kumzuia shaytwaan asimsumbue katika Swalah yake.” [Sunan Abi Daawuwd].
4. Mtu Ajitahidi Kadiri Awezavyo Kupata Nafasi Katika Safu Ya Kwanza[2]
Hii ni kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Lau watu wangelijua malipo makubwa yapatikanayo kwa kuitikia mwito wa Swalah (adhana), na kuswali katika swafu ya kwanza, basi wangeshindania kupata nafasi katika swafu ya kwanza.” [Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim].
Amesema pia:
“Bora ya swafu kwa wanaume ni swafu ya kwanza.” [Swahiyh Muslim].
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipata kuwaona baadhi ya Maswahaba zake wakiwa wamekaa (swafu) ya nyuma ya Msikiti punde tu, kabla ya kuanza kwa Swalah. Alipoona hivyo, alisema:
“Watajivuta na kujichelewesha (kuendea swafu ya kwanza) mpaka Allaah Atawachelewesha (kuingia peponi).”[3][Swahiyh Muslim].
5. Kurudia (Maneno) Baada Ya Muadhini
Hii ni kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Utakapoisikia adhana, sema kama asemavyo Muadhini.” [Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim].
5. Du’aa Baina Ya Adhana (Mwito Wa Swalah) Na Iqaamah
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameujulisha ummah wake nyakati tofauti ambazo du’aa zina uwezekano mkubwa wa kukubaliwa na Allaah. Moja ya nyakati hizo ni baina ya adhana na iqaamah. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Du’aa inayoombwa baina ya adhana na iqaamah haitokataliwa.” [Musnad Imaam Ahmad].
6. Kusoma Qur-aan Na Kumtaja Allaah
Tumeshaonesha awali katika Makala hii, maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa:
“Kwa hakika nyumba za Allaah zimejengwa kwa ajili ya kumtaja Allaah, Swalah, na kusomwa Qur-aan (ndani yake).”[Swahiyh Muslim].
7. Kujitahidi Kuhudhuria Mikusanyiko Ya Kielimu (Duruus Za Misikitini)
Haya ni kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:
“Hakikusanyiki kikundi cha watu katika nyumba ya Allaah, wakisoma Kitabu Chake na kufundishana wenyewe kwa wenyewe isipokuwa utulivu hushuka juu yao, Malaika huwazunguka, Rahmah huwateremkia, na Allaah Huwataja katika mjumuiko Wake (mbele ya Malaika).”[Swahiyh Muslim].
Pia maelezo ya ujumla ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kuwa:
“Yeyote mwenye kuifuata njia (kwa ajili ya) kutafuta elimu, Allaah Atamfanyia wepesi njia yake kuelekea peponi.” [Swahiyh Muslim].
Kutokana na Hadiyth hiyo hapo juu, ni sawa kusema kuwa, ikiwa mtu ataondoka nyumbani kwake akiwa na niyyah ya kuswali (Swalah kwa) Jamaa’ah na pia akiwa na niyyah ya kutafuta elimu Msikitini, kwa kupenda Kwake Allaah, atapata malipo makubwa sana kutokana na ukweli kuwa amekusanya mambo (matendo) mawili makubwa Ayapendayo Allaah (Azza wa Jalla).
8. Ni Wajibu Kwa Misikiti Kuwa Misafi, Na Muumini Anatakiwa Ajitahidi Kadiri Awezavyo Kusaidia Hili
Hii ni kutokana na maneno ya ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) aliyesema kuwa, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliagiza kuwa Misikiti inapaswa kusafishwa na kufukizwa (manukato mazuri). [Musnad Imaam Ahmad].
Na Allaah anajua zaidi
Na Allaah anajua zaidi
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2Qggi5W
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni