Translate

Jumamosi, 1 Desemba 2018

UJENZI WA MADRASA

                                                 BismilLaahir  Rahmanir Rahiim


                                            UJENZI    WA   MADRASA  VIJIJINI


Asalaam aleykum warahmatullah wabarakatuh 

Husika na Kichwa cha habari hapo juu,

Tunatarajia Kuanza Ujenzi wa Madrasa Mkoani Dodoma Wilaya ya Chemba katika Kijiji cha  Kongogo.


Vijana na akina mama wanasoma chini ya mti na mvua zimeanza. Ustadh alitaka kufunga madrasa lakini tumeweka Niyah ya kujenga Madrasa Kubwa na Vyoo viwiili vyenye Thamani ya Shilingi 5,000,000/=(Milioni Tano) 

Kiwanja tunacho na Mpaka sasa katika Kukusanya Michango yetu Tumepata Shilingi 1,500,000/= (Milioni Moja na Laki Tano) Na AlhamduliLaah  tumepokea Mchango wa Mabati 20 kwa sasa.

Tunaomba Mchango wako wa Hali na Mali pia Tunapokea pesa Na Vifaa vya Ujenzi kama vile  Matofali ,Mabati, Nondo, Mbao, Mchanga, cement na Nakadhalika

Allaah (Subhanahu wa taala) anasema:-

مَن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ وَلَهُ أَجْرٌ كَرِيمٌ

"Ni nani atakayemkopesha ALLAH mkopo mwema, ili Amrudishie maradufu, na apate malipo ya ukarimu" [Al-Hadiyd:11]

Na pia anasema:-

 وَمَا تُنفِقُواْ مِنْ خَيْرٍ فَلأنفُسِكُمْ وَمَا تُنفِقُونَ إِلاَّ ابْتِغَاء وَجْهِ اللّهِ وَمَا تُنفِقُواْ مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لاَ تُظْلَمُونَ

Na kheri yoyote mnayotoa ni kwa nafsi zenu. Wala msitoe ila kwa kutafuta wajihi wa Allah. Na kheri yoyote mtakayotoa mtalipwa kwa ukamilifu, wala hamtadhulumiwa" [Al-Baqarah:272]

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن شَيْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ

سبأ (39) Saba

Na chochote mtakacho kitoa Yeye atakilipa. Naye ni Mbora wa wanao ruzuku.

Unaweza Kutuma mchango wako kwa namba zifuatazo

Tigo Pesa +255714974397

Airtel Money +255685779911

M-Pesa +255756403470

(Majina ni ARABI MANDOTA)


Kwa wale waliokuwa Nje ya Nchi unaweza Kutuma Mchango kwa njia ya Western Union au  MoneyGram  au  ExpressMoney  kwa  ARABI   SAID   MANDOTA  natumia Kitambulisho cha Mpiga Kura



Unaweza Kuleta Mchango wako moja kwa moja Mkoani Dodoma Wilaya ya Chemba Kijiji cha Kongogo,ukifika utapiga simu kwa namba hizo hapo juu.

Tunaomba Mchango Wako kwa Hali na Mali ili tufanikishe Jambo hili.

WabilLaah Tawfiq



from fisabilillaah.com https://ift.tt/2Q75uvW
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...