Translate

Jumamosi, 1 Desemba 2018

Hukumu ya Qaswida na An-Nashiyd


SWALI:

Ni ipi hukumu ya anashidi pia naomba kujua tofauti katika anashidi na qaswaida


JAWABU

الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء وإمام المرسلين
وبعد.

Katika mambo ambayo tunamshukuru ALLAAH kwa uwazi wa hukumu yake katika Shari’ah yetu ya Kiislamu na fatawa za Wanazuoni wetu waliosoma wakabobea katika ‘Ulamaa wa Ahlus-Sunnah wal-jamaa (ALLAAH Awarehemu waliotangulia na kuwahifadhi waliobakia) Ni hili suala ambalo fitna yake imekithiri sana katika jamii ya Kiislam. Wakazeeka juu yake vijana, na kukongorojoka juu yake wazee, Ila wachache katika waliorehemewa na ALLAAH.

Ila -walillaah al-hamd- Wanazuoni wamelitolea kauli nyingi zinazokurubia kuwa ni Ijmaa kama hazijakuwa ni ijmaa.

Ntataja hapa baadhi ya kauli za baadhi yao, Na kukhitimisha kwa kauli nzito ya Baqiyyatus-Salaf (Al-Imaam Swaaleh Al-Fawzaan -ALLAAH Amhifadhi).

1. Al-Imaam Al-Albaaniy (Allaah Amraham!):

Yeye hakulikubali jambo hilo la anaashiid bali amelipiga vita na kutoa tamko la kutofaa kwake.

Na miongoni mwa hoja zake juu ya hilo alisema:

“Ni vyema kujenga hoja juu ya hilo kwa mambo mawili:

1. Kwamba hizi anaashiid hazikuwa katika uongofu wa Wema wetu waliotutangulia (Radhi za ALLAAH ziwe juu yao!).

2. Hali halisi inayoshuhudiwa na kujulikana ni ya khatari pia.

Na hilo ni kwasababu tumeanza kuona kwa baadhi ya vijana wa Kiislam wanapumbazika kwa hizi anaashiidi za kidini. Na huwa wanazighanni daima. Jambo ambalo limepelekea wengi wao waache kujishughulisha na kisomo cha Qur’an na kumdhukuru ALLAAH na kumswalia Mtume (swalla LLAAHU ‘alayhi wasallam) na kusikiliza mawaidha…” .

البيان المفيد عن حكم التمثيل والأناشيد”.

2.Al-Imaam Al-‘Uthaymiin (ALLAAH Amrehem) Anasema:

“Anaashiid ziitwazo za Kiislamu ni Anaashiid za Kizushi (za kibidaa), zinafanana na zilizozuliwa na Masufi. Na kwa hali hiyo inapasa watu waachane nazo na waelekeze jitihada zao kwenye mawaidha ya Kitabu na Sunnah.

Ama ikiwa ni tungo ambazo zitatumika kwenye vita kusaidia kupandisha mori katika Jihadi ni jambo zuri”.

3.Imaam Ahmad shaakir katika kitabu chake ummda tafsir: aliulizwa ni ipi hukmu ya anaashiid za kidini?

Akajibu: Hizi zote ni katika mambo ya bidaa yenye kuchukiza, hayamzidishii mfanyaji ispokuwa anakuwa mbali (yanamuweka mbali muimbaji na msikilizaji na kheri),

Muulizaji akasema: laakin Allah anasema "nikumbukeni nami nitakukumbeni" na hawa wanaoimba wanamtaja Allah hasa hasa katika wakat wa mwisho wa usiku (wale waimbaji wa usiku).

Shekh akasema: jee mimi nimeipinga hiyo aya? Wao wanamtaja Allah kwa maasia naye Allah anawakumbuka kwa kuwachukia,

Wao pia wanamtaja Allah kwa njia ya bidaa nayeye Allah anawakumbuka kwakuwachukia".

4.Imaam Ahmad aliulizwa: Unawazungumziaje watu wanaoimbaimba?

Akasema: Wanachokifanya ni bidaa na haifai kukaa nawatu wanamna hiyo".

5.Imaam Shaafiy anasema: "nimeacha katika mji wa baghadaad (iraqi) kitu ambacho azanaadiqa (kundi miongon mwa wanaafiq) wameanzisha (wamekizusha) wanakiita anashid wanataka kuwazuia watu na quraan".

Anaashid zinawazuia watu na kusikiliza quran kupata uhuzin na majonzi, wangap katika waislam  wanaposikiliza baadhi ya anaashiid wanatokwa na machozi na wanakaribia kulia?

Wangap katika wapenz wa anashid kwenye sim zao wamedownload ma anashiid kuliko quran na mawaidha? Wangap?

Angalia watoto, wanawake na wanaume ambao majumba yao mara kwa mara wamezoea kuweka maanaashiid na maqaswida, angalia walivyohifadh kichwani mwao, ni manyimbo tu

Imefikia mtu huyo ukimuwekea quran anakwambia zima, zima, anajiskia vibaya

Mtu akisikiliza quran ahisi km ina mchoma choma nakuwatia kizungu zungu, laakin akisiliza anaashid moyo wake unaburudiika na anajisikia raaha kabisa. Subhaana Allah. Jee hizi sio athari za anaashidi

6. Al-‘Allaamah Al-Fawzaan (ALLAAH Amhifadhi) Anasema:

“Na miongoni mwa yanayohitaji uzinduzi juu yake ni yale mambo yaliyoenea kwa wengi miongoni mwa vijana wa Dini kuhusu kanda ambazo zina sauti za watu waimbao kwa pamoja Wanaziita kanda za anaashiid za Kiislamu, na kwa uhakika ni miongoni mwa nyimbo tu. Na huenda zikawa na sauti za kufitini (kabisa). Na huuzwa kwenye maduka ya studio pamoja na kanda za Qur’aan na mihadhara ya Kidini.

Na kuziita hizi nashidi kuwa ni anaashiid Islaamiyyah ni jina la kimakosa (kabisa!), Kwa sababu Uislamu haujatuwekea anaashiid, bali umetuwekea Dhikrillaah na Kisomo cha Qur’aaan na Ilmu yenye manufaa. Ama anaashiid (ziitwazo) Islaamiyyah, hizo ni katika Dini za Masufi wazushi. Ambao wameijaalia Dini yao kuwa ni mambo ya kipuuzi puuzi na mchezo mchezo. Na kuzifanya anaashiid kuwa ni sehemu ya Dini, ni kujishabihisha na manaswara WAKRISTO….”

AL-KHUTWAB AL-MIMBARIYYAH 3/-184-185

Ama qaswiidah:

Ni mkusanyiko wa beti za kishairi ambazo zimeafikiana kwa wizani na vina.

Na tofauti ambayo ipo ni kuwa qaswidah inaweza kusomwa na mtu mmoja tu kwa lengo la kufikisha ujumbe fulani bila ya kujikalifisha kuiremba na kuipamba na kujitutumua. Ama anaashiid ni mkusanyiko wa sauti za watu wanaozipamba sauti zao na kuziremba wakiwa na naghma huku wakiimba anaashiid zao.

Na zote hizi hazifai ni mambo ya kizushi yapumbao

Na Allaah anajua zaidi



from fisabilillaah.com https://ift.tt/2Q3Bd0Z
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...