Ninavyoamini ni kwamba Salafiyyah alionayo al-Albaaniy ndio Salafiyyah ileile walionayo wanachuoni wa Saudi Arabia kama mfano wa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz, Ibn ´Uthaymiyn, al-Fawzaan, ´Abdul-´Aziyz Aalush-Shaykh na wengineo. Anaamini yale wanayoamini juu ya majina na sifa za Allaah, Qadar, kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah yaliyoteremshwa na haikuumbwa na I´tiqaad nyenginezo. Kama kuna tofauti ndogo basi ni katika mambo ya Ijtihaad. Ama katika ´Aqiydah, hakuna tofauti kati yake yeye na wao.
from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2FXSu6Y
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni