Swali 28: Ni hali zipi ambapo mtu anasujudu Sujuud ya kusahau kabla ya Tasliym na baada ya Tasliym?
Jibu: Sujuud ya kusahau inasujudiwa kabla ya Tasliym isipokuwa tu katika hali mbili:
1- Pale atapotoa Tasliym mapema kwa kupunguza Rak´ah moja au zaidi. Katika hali hii bora ni kuileta baada ya Tasliym. Dalili ya hilo ni Hadiyth ya Dhuul-Yadayn (Radhiya Allaahu ´anh).
2- Pale ambapo mtu atakuwa na dhana yenye nguvu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Atapokuwa na mashaka mmoja wenu juu ya swalah yake, basi ajibidishe juu ya lile la sawa, akamilishe kitendo chake, kisha alete Tasliym na kusujudu Sujudu mbili.”[1]
Ameifanya Sujuud kuwa baada ya Tasliym. Hili ndio bora. Vinginevo Sujuud ya kusahau mtu anaileta kabla ya Tasliym.
[1] al-Bukhaariy (401) na Muslim (572).
from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2JyGxmo
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni